Tuesday, June 17, 2014

dawa ya ukimwi?

SAYANSI YA TIBA MBADALA NA UTAFITI ASASI ENDELEVU NA MAENDELEO YA DAWA ZA ASILI TANZANIA.
OFISI BARABARA YA KLERUU—MABATINI MWANZA
SIMU NO: 0756-410218
TANZANIA NATURAL MEDICINE FOR SUSTAINABLE DEVELOPMENT—TANAMEDE, MWANZA TZ.

OFFICE—KLERUU ROAD—MABATINI MWA NZA MOBILE NO: 0688-410218.
CD4 + CELLS NI NINI?
Ni aina ya chembe chembe nyeupe za damu zilizo na receptor protein zinazoitwa CD4, katika ngozi yake ya nje. Cell zenye CD4 receptor zinaitwa CD4 + CELLS au helper lymphocytes.
Nkugutwa— CD4 CELLS ni nini?
Ni dawa mbadala ya unga iliyotengenezwa kwa matunda na virutubisho asilia inayozalisha helper lymphocytes aina ya chembe chembe nyeupe za damu iliyo na receptor protein, inayotengeneza CD4 + endelevu mwilini. Dawa hii huondoa magonjwa nyemelezi na kurudisha vitamin na virutubisho asili na kuzalisha CD4 + mwilini haraka. Dawa hii huleta njaa kila wakati na jasho mwilini.
MATUMIZI:
Kijiko 1 kidogo x 3 kwenye kikombe cha maji ya moto / mchaichai au uji wa lishe.
DOZI:
Dozi ya dawa hii ni miezi minne (4) mgonjwa kabla  ya kuanza dawa hii anatakiwa apime CD4 + na anapotumia dawa hii apime CD4 baada ya miezi 2 akimaliza dozi apime CD4  baada ya miezi 9 apime CD4 na miezi 12 apime CD4 kuona maendeleo yake. CD4 hufikia kiwango cha mtu asiye mgonjwa na kuendelea na shughuli zake kama kawaida.
ONYO:
Mgonjwa asitumie pombe wala madawa ya kulevya.

MAGONJWA MENGINE TUNAYOTIBU:
¨ PRESHA     VIDONDA VYA TUMBO
¨ PUMU         KUZIBA MKOJO
¨ KISUKARI   FIGO
¨ BAWASIRI   UVIMBE
¨ MOYO MPANA         SICKLE CELL
¨ KANSA        KUPOOZA VIUNGO N.K
¨ CHUNUSI SUGU
¨ INI
DAWA ZETU ZIMETENGENEZWA KWA MATUNDA, MIMEA,


Tuesday, February 4, 2014

Mheshimiwa Juma Nkamia, NGOs hizi utaogopa kuzikaba koo?


    
SHERIA, inapaswa kuwa nakala ya tabia halisi ya jamii iliyotunga sharia husika.
Sheria hutokana na KATIBA YA NCHI,ambayo ndiyo sheria mama.Katiba lazima kuakisi tabia na mwenendo wa wenye sharia hiyo.
Sheria ya walevi,lazima kuakisi ulevi-ulevi,sharia ama katiba ya machangudoa,mashoga na wasagaji,lazima izingatie tabia za watu hawa.
Jamii adili na yenye kutaka haki na usawa, itatengeneza sharia na katiba yenye kuakisi uadilifu,ukweli na usawa. Haiwezekani walevi,wabwia unga na machangudoa wakawatengenezea makasisi,maaskofu na masheikh sharia au kanuni za kufuata katika kazi zao za dini!
Sasa, najiuliza: Sisi Watanzania ni nani hata tutengeneze Katiba adili na sheria za unyofu?
Sisi hawa waongo-waongo,tapeli, ‘kekundu na keusi’ na wapenda ‘short-cut’ ati tutengeneze Katiba nyoofu yenye kuzingatia usawa? Siyo kutengeneza sheria na Katiba yenye mianya ya rushwa,ufisadi na uonevu kwa masikini na watu wa kawaida,wakulima wa vijijini?
Sheria ama katiba laima ifanane na watu wenyewe wenye kuitunga walivyo! Haiwezekani wezi, machangudoa na wakwapuzi wa wake za watu kutunga sheria yenye kusema:
“Usiibe, usizini,usikwapue mke wa mtu,usi…”
Watu waliopinda, watataka sheria za “Usi” ziondoke,ili waendelee kufanya ukiranga wao kwaq uhuru mkubwa!
Ndiyo maana utasikia watu wabwia unga wakidai demokrasia ya kuvuta hata bangi hadharani,na serikali kama za Marekani na Uingereza zimekubali,wanasema ndiyo demokrasia na uhuru,haki za binadamu n.k
Sheria ya Mungu(AMRI 10 ZA MUNGU) inafanana na Mungu mwenyewe na Malaika zake.Na watu wanaompenda Mungu hawana budi kufanana naye na kuwa na tabia inayosemwa kwenye Amri hizo.Wazinzi na wezi,waonezi na wachawi hawawezi kukubaliana na AMRI za Mungu,watasema ni sheria kandamizi nay a Kiimla!
Sasa jiulize, katiba ya Mungu(AMRI 10 ZA MUNGU) tukisema ikubaliwe kuwa Katiba ya Tanzania,halafu zitungwe kanuni za adhabu kwa wale wasiotaka kuitii,itakuwaje?
Watu wengi wataingia mitaani kulalamika na kuipinga kwamba inawanyima uhuru,siyo? Mungu na malaika zake na wafuasi wao hawataguswa na adhabu zitakazowakabili wazinzi,wezi,mafisadi, watambikia mizimu na wakatili,wauaji, wafiraji,mashoga na wasagaji,siyo?
Wenye kufanana na katiba inayotungwa na inayozaa sheria na kanuni za adhabu kwa wakosaji na watukutu,hawana shida.
Haiwezekani kutunga Katiba safi na ya haki, wakati watu wenyewe wanaoitunga wamepinda,watatafuta upenyo ili waendelee kuiba,kudhulumu na kuhujumu masikini. Tusidanganyike na katiba mpya,wakati sisi siyo wapya kimtazamo,tunaishi kwa dhuluma kila wakati.
Angalia vyombo vya habari na taasisi zao, ambazo Naibu Waziri wa Wizara husika, Juma Nkamia, aliwahi kusema taasisi hizo ni NGO za watu binafsi,wakabisha!
Kwanza wanahabari,viongozi wao na taasisi zao hazinafanani kabisa na katiba zao na malengo na kauli mbiu zao ambazo ni adili,za kweli na za haki tupu.
Sekretari  wa ofisi moja inayojidai kuhudumia wanahabari nchini, aliwaalika nduguze wanne waje kuhudhuria semina ya siku tano iliyoandamana na posho nono ya shilingi 40,000 kila siku,badala ya kualika wanahabari stahiki!
 Hao jamaa zake hawakuwa waandishi wa habari; isipokuwa  walikuwa “mamluki” ambao lengo lao lilikuwa kupata pesa, wanunue magari mazuri na nyumba za kuishi.
Semina hiyo, eti iliandaliwa kwa waandishi wa habari kwa siku tano wapate maarifa ya kuinua kiwango cha taaluma na weledi katika kazi zao za kila siku!
Kila siku,hizi “NGOs” za Mheshimiwa Juma Nkamia huandaa warsha na semina kwa wanahabari. Lakini wanaohudhuria ni wenyeviti,makatibu na nyumbandogo zao!
Wanachama wakihoji haya madudu, wanaitwa wasaliti na wahujumu wa maendeleo ya taaluma ya habari!

Basi, Yule sekretari akawaita ndugu zake wanne, akawavika joho la uanahabari,kwamba walitokea Bukoba,mkoani Kagera, kwa hiyo wakalipwa posho nono ya shilingi 40,000 kila siku kwa siku tano,kwa masharti kwamba mwisho wa semina wagawane  na Yule sekretari kilichopatikana.
Kwa bahati mbaya, waandishi wa habari wakawastukia mamluki wale na kuanza kuwasaili huko Bukoba walikuwa wakiandikia vyombo gani?
 Wakatekewa.
Walipodadisiwa sana, wakafichua siri na kusema hawajawahi kuandika hata barua za maoni gazetini, isipokuwa waliitwa na Yule jamaa yao sekretari, ili kugawana posho!
 Yaani, semina ya wanahabari wanaalikwa jamaa na ndugu za hawa vigogo wa ofisi zinazojidai kuhudumia wanahabari,hasa mikoni, ili wagawane posho nono. Hata wauza baa hupewa mialiko ili mradi tu posho ikipatikana,wagawane na wahusika! Hawa nao siku hizi eti wanataka Katiba Mpya!
Eti, wanasema tasnia ya habari imevamiwa na makanjanja; sasa hawa wanaoitwa kuhudhuria hizo semina ni kina nani?
Na wanaohodhi semina tuwaiteje? Waulize mapato na matumizi ya vyama vya wanahabari,uone utakavyotukanwa! ‘Unatumiwa, sijui nani!!
 Na je, ‘stori’ zisipoonekana magazetini, ama zisipotangazwa runingani na redioni, walaumiwe wahariri au waandishi wa habari?
Nataka kusema kwamba, zile semina zinazoandamana na posho ya siku tano au majuma kadhaa, wajanja hawa wanaalika ndugu zao ,wakati mwingine hata nyumba ndogo zao, wanajigawia ‘ulaji’ mwingi migongoni mwa wanahabari.
Wapo jamaa tulikuwa tunasugua nao lamia ma kudandia daladala,siku hizi wana ma- ‘VX’ yaliyopatikana migongoni mwa wanahabari,tena kwa miaka michache tu! Hata wafagizi lazima wanunue magari,maana fedha zote za miradi hewa wanatunza wao, na hakuna wa kuwakagua. Mkutano Mkuu ukifika, wanaoitwa rafiki zao,wabishi wanaachwa solemba.
 Siku hizi, wanaojidai waratibu wa semina,mikutano ,warsha na mafunzo kwa wanahabari,hasa wa mikoani, huchukua posho na kuwagawia kipapatio tu.Kila unachopewa,lazima uwagawie,la sivyo hutapewa mialiko milele.
 Badala yake, wanaalikwa hata wauza vocha za simu, mradi wakubali kugawana posho na waandaaji na waratibu wa semina zile.
Amini usiamini, kuna semina hewa zinazoratibiwa mikoani, majina ya wanahabari yanaorodheshwa, lakini hawaitwi kuhudhuria, isipokuwa baadaye zinatafutwa saini bandia ili ionekane walihudhuria na wakalipwa kiasi kikubwa cha posho, chakula,nauli na masurufu ya safari.
Hata sasa tunapoelekea Oktoba 31,siku ya uchaguzi mkuu, wajanja walishaomba mamilioni ya fedha kwa wafadhili, eti kuendesha mafunzo kwa wanahabari.
 Lengo eti ni kuinua kiwango cha taaluma na weledi!Na katiba zipo, “Code of Conduct” za Professionalism zipo ukutani mwa ofisi zao,tena wameandika ‘Usimpe rushwa mwandishi wa habari”, upuuzi mkubwa wa katiba za makaratasi,badala ya katiba kutangulia myoyoni mwa wahusika.
 Ukitaka vita, kawaulize ni wanahabari kiasi gani, na asilimia ngapi waliopewa mafunzo na semina kuhusu uandishi wa habari za uchaguzi?
Wafadhili, wanadanganywa kwamba kulikuwa na semina mikoa Fulani na posho zilizlipwa,kumbe ndiyo yale niliyosema kwenye utangulizi,kwamba miradi hiyo mingi ‘hewa’ ilishatekwa na wajanja hawa, wanajilipa kumbi,chakula na kuita jamaa zao ambao hata barua za wasomaji hawajawahi kuziandika magazetini.
Hawa hawajawahi kuwa na nia ya kuinua kiwango cha taaluma kwa wanahabari,lengo lao ni kupora zile fedha za wafadhili.Kama mnabisha, kawachunguzeni.
 Hata wawezeshaji wanaoitwa kufundisha semina zile siyo wale magwiji tunaowajua, bali ni ‘jamaa’ zao ili kujihalalishia ulaji wenyewe kwa wenyewe.
 Nataka kusema kwamba, hawa wataalamu wa kuomba fedha kwa wafadhili,huomba fedha nyingi na kuzitafuna migongoni mwa wanahabari,kasha huwarushia fupa hapa na pale ili walambe, kumbe  firigisi na mapaja yalisha tiwa kinywani!
Tasnia hii ya habari inajivika majukumu mazito ya kuelimisha,kufahamisha wapigakura namna ya kuchagua viongozi bora, na wala siyo bora viongozi.
 Eti, waratibu hawa wa semina na mafunzo(siyo wote) kwa wanahabari wana makusudi ya kuboresha utendaji wa kiweledi wa wanahabari na taaluma zao kuelekea  2015.
 Taaluma, weledi na utapeli kama niliokwishabainisha mwanzoni,  wapi na wapi?Wengine wakati wa kampeni huvaa fulana na kofia za wagombea,wakishushwa kwenye magari ya wagombea,wanakasirika wanahamia chama kingine, eti ni waandishi!!
Kumbe,huko mikoani kuna wajanja wachache wanaoteka nyara semina na mafunzo ya wanahabari, wanawaalika ndugu na jamaa zao wale watakaokubali kugawana nao posho za semina.
 Fedha za malipo ya kumbi za mikutano na chakula zinaliwa ama zinapunguzwa.Mikutano inafanywa baa,wanasema walifanya ukumbi wa hoteli kubwa,ili wapate fedha za kununua magari ya bei kali sana!
Nadhani Juma Nkamia anajua haya,ndio maana alisema ni NGO za watu binafsi!Hawa siku hizi wana midomo mikubwa kudai katiba mpya,sijui ni mpya vipi,wakati myoyo yao inakiri wanamiliki mali za wizi migongoni mwa wanahabari.
 Viburudisho na vinywaji vinaondolewa ili fungu lake wakagawane! Hawa wajanja wanakula migongoni mwa wanahabari.
 Wanaalikana wenyewe kwa wenyewe-wanapeana ulaji, wanagawana kila kazi, za kutafuta kumbi za mikutano, wakati mwingine mikutano hufanyika magengeni,ili wajipatie fedha.
Eti fedha za wafadhili zinaletwa ili kuboresha taaluma ya habari wakati wa chaguzi,kumbe ni kujenga vitambi vya wachache tu,na ndugu zao ambao hata barua za wasomaji hawajawahi kuandika. Kaviangalie vilabu vya wanahabari mikoani, havina hata kiti sembuse kompyuta?
Tunakaribia uchaguzi mkuu wa 2015. Kuna makelele ya kivuvuzela, kwamba wanahabari wote wamepewa semina na mafunzo eti waweze kutafiti na kuandika habari za uchaguzi wakati huu wa uchaguzi.Wanajipanga ku ‘piga hela’.
Eti, wanaimba katika redio na televisheni kwamba wanahabari wamefundishwa maadili na uandishi wa habari za uchaguzi, wakati huu wa uchaguzi,kumbe ni huu huu ‘uchafuzi’mkuu.
Kwa mtindo huu, wanahabari hawawezikuwezesha demokrasia na uchaguzi  mkuu,bali ‘uchafuzi’mkuu.
 Nataka niseme kwamba katika baadhi ya mikoa hapa nchini, kuna vituko vinavyoitwa mafunzo  na semina za wanahabari kuhusu uchaguzi mkuu.
Wafadhili wakitaka, wakawaulize wanahabari,ni wangapi wamehudhuria mafunzo hayo na semina hizo wanazojidai kuombea mabilioni ya fedha, eti ili kuwezesha uchaguzi uwe wa kidemokrasia,huru na haki, kumbe tupu na bahasha za khaki.
Fedha nyingi za wafadhili zinazotengwa kwa mafunzo ya wanahabari kuhishia kujenga vitambi vya wachache, wengine huishia kughushi saini za wanahabari,bila hata mafunzo kufanyika.
 Naam, kumbe wakati wa kura ni msimu wa kula pia-kura za kula!!
Sisemi kwamba kila semina zinapoandaliwa ni hujuma. Sijasema kwamba Baraza la Habari(MCT) huandaa semina bandia na washirika wake kama UNDP.
Nataka kusema kwamba kuna mmonyoko mkubwa wa kimaadili na utapeli mkubwa katika maeneo Fulani, ambako wanahabari wamepata kutapeliwa kwamba walihudhuria mafunzo ama semina wakalipwa fedha,kumbe uongo na Ghiliba- Ghilibu?
 Tunasema kwamba,kuna watu wamehodhi semina,mafunzo na posho ili wafaidike wao.
 Nenda kawaulize wanahabari mikoni watakwambia kwamba wana miaka mingi bila kuhudhuria hayo mafunzo na semina.
Nani huwa wanahudhuria semina hizo, kama siyo mamluki ili wakagawane na hao wanajidai kuhodhi kila mamlaka na mialiko ya wanahabari?
 Mwisho wa siku hakuna kiwango cha taaluma kinachoinuliwa,bali ni vitambi vya wachache vinavyoinuliwa ama kujengwa katika msimu huu wa uchaguzi mkuu unaoandamana na uchafuzi mkuu.
Kila siku, kila mtu anawaza uchaguzi mkuu ufike ili wapate kula kupitia kura.
Mwanahistoria wa Kiingereza, Thomas Babington Macaulay, ndiye aliyevibatiza vyombo vya habari,jina la MHIMILI WA NNE WA DOLA.
Majukumu mahsusi ya vyombo hivi vya habari na wanahabari ni kutengenezea umma uwezo wa kuchagua serikali itakayowapa wananchi wake ulinzi na manufaa yatokanayo na katiba.
Wanahabari waliowezeshwa mafunzo  ya kitaaluma wanaweza kuuelimisha umma ili kupigakura vizuri na kujipatia viongozi bora, na kamwe si bora viongozi.
Wanahabari waliokolea kitaaluma, huwahudumia wananchi kwa uaminifu,bila chembe ya tama na ufisadi.
 Ni mbwa walinzi(watchdogs) wabwekao dhidi ya mienendo yenye mashaka na utusitusi.
 Sasa, kama taasisi zinazojidai kuvihudumia vyombo vya habari, masekretari wake na hata vigogo kazi yao ni kuhodhi semina na mafunzo na kukimbizana kupora posho, maana yake ndiyo “Watchdog role”?
Hiki ni kiwango gani cha ubora,kualika waandishi hewa na kujipatia fedha eti kuudanganya umma kwamba habari za uchaguzi mkuu zitawezesha demokrasia na uchaguzi huru-kumbe ‘uchafuzi’huru.
 Kama tasnia ya habari ndiyo hii ya wajanja kula migongoni mwa wanahabari nakuwatupia mifupa, naungana na Rais wa zamani wa Marekani, Thomas Jefferson, alivyosema katika waraka wake kwa Kanali Edward Carington, mnamo Januari 16, mwaka 1787 kwamba heri kungekuwa na serikali bila mhimili sampuli hii wa Dola.
Kama wajanja wataendelea kuomba fedha kwa wafadhili kwamba watawezesha taaluma na vyombo vya habari,kumbe fedha wanagawana gizani, ni heri hata uchaguzi uendeshwe kibubu-bubu,kuliko kuwa na wanahabari waliojipaka madoa ya ulafi na ubadhirifu.
Hawa watakuwaje waadilifu wakati hata kile walichopaswa kujengeana uwezo wa kitaaluma,wanakipora?.
 Hivi hawa wanaokula migongoni mwa wanahabari hasa wa mikoani, nao ni wanahabari gani kama siyo wadandiaji na walaji kila msimu wa uchaguzi?
 Hivi hawa wanaopeleka jamaa zao kuhudhuria semina na mafunzo ya uandishi wa habari, wakati ni wauza vocha, nao wana “balance freedom of press with the rights of people” wakati wanawaza kuhujumu fedha za wafadhili za posho za mafunzo ya kitaaluma?
Kwa mtindo huu, huu ‘uchafuzi mkuu’ hautazaa ‘Fairness’ au ‘Objectivity’ wala ‘Accuracy’ katika habari na makala za uchaguzi, bali uchakachuaji tu wa kusaka kujaza matumbo.
Kama hatutaangalia,nchi hii kila kada, na kila mtu atafikiria siku za uchaguzi zifike haraka ili kujipatia ulaji.
Tunageuza sasa msimu wa uchaguzi kuwa msimu wa ‘kura za kula’ tu.Msema kweli mpenzi wa Mungu!!
0772 82 40 74