Tuesday, February 28, 2012

AJENDA YA MAREKANI NA FREEMASONS



ALFAJIRI, kuamkia Jumamosi, Desemba 30. mwaka 2006,mtawala wa nchi uliko Mto mkubwa, Frati,Saddam Hussein, akanyongwa kwa kamba hadi kufa.
Mahali walipomnyonga, panaitwa Camp Justice; walimnyonga kwa makosa ya ubinadamu,huko Kaskazini mwa Baghdad.
Saddam alinyongwa mbele ya Wairak wachache, na dunia ilishuhudia tukio hilo katika televisheni; akina Mouwafik al-Rubaie,Mshauri wa Usalama wa Irak, alikuwepo Camp Justice.
 Nataka msomaji atambue jambo muhimu na la msingi sana. Kwamba, Marekani kuivamia Irak na kumpindua Saddam Hussein mwaka 2003, wakang’oa sanamu yake jijini Baghdad, ilikuwa kutimiza unabii muhimu sana.
 Sababu zote walizosema juu yake kwamba alikuwa na silaha za kuangamiza,ulikuwa umbeya mtupu- mengi wanayosema Marekani dhidi ya viongozi wanaohitilafiana nao ni uongo tu; utaona hapa chini.
   Ilikuwa kuashiria kuanguka kwa Dola lenye nguvu huko Mashariki, na kando ya mito miwili ya Tigris na Euphrates.Lilikuwa jambo muhimu katika historia ya dunia.
Kunyongwa kwa Saddam mbele ya kamera za televisheni,ilikuwa kuwaambia magamngwe wachache wasiotii mamlaka za Magharibi,kwamba dawa yao ni kitanzi,risasi na kifo!
 Siko ya mauti yake,Saddam alikabidhi kitabu chake cha Koran alichokumbatia kifuani, akasali, wakamsomea sababu za kifo chake kwamba aliwaua Washia 148 huko Dujail mwaka 1982; akakubali kusalimu amri na kufa kistaarabu!
  Ndivyo zilivyokoma enzi za Saddam ambazo wao waliziita, The Dark Period.
  Gaddafi naye ameuliwa baada ya kusalim amri,akapigwa risasi huku akiomba msamaha,utadhani aliwakosea hao wauaji peke yao!
 Feburuari mwaka jana, ikatangazwa kwamba Osama bin Laden ameuliwa huko Pakistan,juzi tukaona kwenye televisheni nyumba aliyoishi ikabomolewa na matingatinga,ili mahujaji wasifululize kwenda kuhiji mahali hapo!
  Naam. Juzi tukatazama katika televisheni,ya kwamba eti mwaka 1988 huko Lockerbie, Scotland, siyo maofisa Usalama wa Libya, akina Megrahi waliolipua ile ndege ya Marekani ya Pan American Airways!
 Nilimwona Al-Megrahi katika kitanda cha mauti anapougulia maumivu ya Saratani baada ya kuachiwa huru akisema, alifungwa kwa uonevu tu-Hao ndiyo Marekani Bwana!
 Hata Syria watashinda,maana imeandikwa Marekani na washirika wake wataushinda Ulimwengu,kwa kuwa husaidiwa na Freemasons, Illuminanti na Ibilisi mwenyewe,Mfalme wa Dunia hii.
Dola la Kisovieti(USSR) lilishashindwa kusimama kijeshi kama dola kuu la dunia, akina Mikail Gorbachev walishajikabidhi Washington kitambo-Urusi imebaki kwa akina Putin watu dhaifu.
Nataka nikwambie msomaji. Dikteta wa zamani wa Yugoslavia,Slobodan Milosevic aliondoka kitini mwa enzi kwa ‘Nguvu ya Umma’ mwaka 2000, akamwachia kiti Vojislav Costunica huko Serbia ya sasa.
 Marekani na washirika wake walimpeleka Milosevic huko Hague kujibu mashitaka ya uhalifu wa vita na haki za  binadamu.
 Amini usiamini,ndani ya kampeni kali ya Haki za Binadamu, Ibilisi anaongoza harakati dunia nzima=haki za mashoga, haki za akina mama hata kuwachapa makonde akina baba, kampeni za kunyimana unyumba, n.k
 Watawala wan chi za ‘Mrengo wa Kushoto waliopinduliwa na Marekani,ni wengi sana akina Noriega huko Amerika Kusini.
  Korea Kaskazini,haitashambuliwa tena kijeshi. Bada ya kifo cha Kim Jong Il, akaingia mtoto,”Chekechea” Kim Jong Un  katika siasa za     Ulimwengu, bila shaka Korea itaacha kutengeneza Nyuklia kwa kupewa mafuta na fedha taslim,na itaachana na kuabudu miungu yao na kujiunga na ‘Dini Maalum’ basi,hakutakuwa na maneno tena.
  Tatizo ni Iran. Juma lililopita,tuliona kitisho cha vita huko Iran ikizidi kuishupalia Israeli na kukomaza shingo yake kukabiliana na Marekani na Washirika wa Magharibi.
  Tumejifunza katika makala zilizotangulia kwamba Marekani na washirika wake na Israeli, Vatican wanaandaa mfumo mpya wa utawala na ibada(Soma Ufunuo wa Yohana 17:1-17).
  Mataifa yenye nguvu duniani, yatakuwa yanabeba mgongoni mwake madhehebu Fulani ya kidini,ambayo kila mtu analazimika kuyakubali mafundisho yao na falsafa yao ya kumpinga Mungu muumbaji.
   Turejee katika unabii wa Ufunuo wa Yohana 13:1-10.Kuna wasomaji wananiuliza Dini itabadilikaje na kuwa  mamlaka ya siasa?
 Ufalme wa mwisho duniani, baada ya Marekani kuitiisha dunzia nzima kwa kushirikiana na iliyokuwa dola ya Rumi, ni ule unaomkufuru Mungu. Kumkufuru Mungu ni binadamu kujiita Mungu; ni mamlaka ya ibada,kuabudu dini Fulani na mtu Fulani anayesema yeye siyo mwakilishi wa MUNGU tu,bali ni Mungu.
   Shetani mwenyewe ataipa dini hii mamlaka yake(Ufunuo13:2).Freemasons,Illuminanti wataipa nguvu Marekani na washirika wake,Ulaya na Israeli, watampa mfalme wa kidini mamlaka yao yote na viti vyao vya enzi na uwezo mwingi na dunia itashangaa kwa mamalaka na uwezo wake.
 Katika Unabii wa Biblia,mnyama ni ufalme,mamlaka Fulani na siyo mtu binafsi.(Danieli 7:17),mnyama huyu anayezungumzwa na manabii Yohana na Danieli atainuka Ulaya,mahali palipokaliwa na watu wengi tangu zama za Yohana mwaka 96 AD.
  Marekani na washirika wake, wakipewa nguvu na nguvu za giza za Ibilisi, Freemasons,Illuminanti n.k watampa mamlaka yao mfalme ajaye, baada ya Marekani kuitiisha dunia na kuondoa demokrasia kwa Sheria –NEW World Order (Ufunuo 13:13).
 Ajenda ya hawa wote ni kumpinga Mungu muumbajiwa dunia. Tabia ya ufalme huu ujao duniani imezungumzwa vizuri kabisa.
  Ufalme huu wa Ufunuo 13:2 UNASEMWA kwamba ulikuwa mfano wa CHUI, huyu chui alikuwa na miguu ya DUBU, kichwa chake kilikuwa cha SIMBA na aliwabeba madikteta 10 ambazo ni mili 10 za mataifa ya Ulaya leo, katika eneo lile la dola ya Rumi ya kale.
  Turejee katika ndoto ya Mfalme Dikteta Nebuchadnezzar, zama za Nabii Danieli katika sura ya Pili na Saba ya kitabu cha Danieli. Kuna historia ya dunia,zamani hata siku hizi. Nabuchadnezzar alioneshwa njozi kwamba baada yake kungekuja falme nyingine nyingi.
Kwa mhtasari, sura ya saba ya kitabu cha Danieli,tunaambiwa kwamba mnyama SIMBA ni ufalme wa Babeli(603-538 BC).
  Ufalme huu wa Babeli (siku hizi Irak) ulipinduliwa Oktoba 13,mwaka 539 na Cyrus The Great, unaweza kusema Koreshi.
Ufalme wa Pili baada ya Nebuchadnezzar,ulikuwa UMEDI na Uajemi waliunda serikali ya mseto, na wanafananishwa na DUBU aliyejiinua upande mmoja wa mshirika wa utawala huu wa mseto.Wakawashinda wafalme watatu ndizo mbavu tatu mdomoni mwa dubu huyu mkali, ulianza kutawala 538 hadi 331 BC.
 Ufalme unaofananishwa na CHUI ni Ugiriki ya sasa iliyoitwa Uyunani. Siku hizi Ugiriki ni dhaifu inayochangiwa fedha na ukanda wa Euro zone, ili wasifilisike. Ugiriki ilianza kutawala dunia mwaka 331 wakati wa Iskanda Mkuu, wakaja kupinduliwa na Rumi Oktoba 13,mwaka 168 BC.
  Dola ya Rumi inafananishwa na MNYAMA wa ajabu!! Alikula na kuponda kwa mkono wa chuma, na aulianza kutawala dunia Januari 22 mwaka 168 BC hadi kupinduliwa na kugawanyika katika falme ndogo 10 za Ulaya leo, na nitazitaja. Ulikuwa mwaka 476 AD. Dola hii ilitawala kwa karne zaidi ya sita. Soma pia Danieli 2:41.
  Baada ya hapa,tumeona akina Napoleon Bonaparte ,Julius Caesar, Adolf Hitler na wenzao wakijaribu kuiunganisha Ulaya,na dunia nzima wakashindwa vibaya.Tumeona vita vya dunia juma lililopita.
  Sasa, tutazame tabia za falme hizi nne za Nabii Danieli ambazo yule Mfalme wa Ufunuo 13:1-10 ana nasaba nazo.
 Mfalme wa Ufunuo 13 ana fanana na CHUI, ana tabia ya ufalme wa Ugiriki ama Uyunani.
 Tunawajua Wagiriki, sifa yao ni FALSAFA.Wale “Great Thinkers” wametokea Ugiriki. Socrates, Plato, Aristotle(384-322, BC) hawa wametuachia maarifa ya sayansi. Masomo kama Biology, Chemistry, Geology, Zoology, Physics, Psychology, Astronomy n.k yametoka kwao.
 Kwa hiyo, Mfalme huyu wa Ufunuo 13:1-10 ana vaa ‘ngozi’  tabia za CHUI-Ugiriki, sayansi,usomi,falsafa,ujanja ujanja.
 Wagiriki, wanajulikana kwa academy zao na ibada ya masanamu. Eti kulikuwa na miungu 391 iliyoishi katika kilele cha Mlima Olympus. Socrates akaipinga hiyo miungu,akasema kulikuwa na Mungu mmoja Mbinguni, wakampa sumu ainywe baada ya kukataa kutubu. Socrates alikufa kwa kuipinga miungu yam lima Olympus!
 Yako mengi Ugiriki,michezo ya Olimpiki hiyo itakayochezwa London Juni mwaka huu,na mbio za Marathon. Siku nyingine nitaandika juu ya hili,leo niliache.

  Mfalme ajaye atakuwa na mwenendo kama Ugiriki, ataleta maarifa na falsafa na ibada ya miungu nitakayotaja kitambo.
  Atakuwa na miguu(mwendo) kama wa UMEDI na UAJEMI, serikali ya mseto iliyoanzisha duniani SHERIA.Sheria za kwanza zimetungwa na Wamedi na Wajemi na hazikubadilika(Danieli 6:15,17)na pia ibada ya sanamu iliyomtupa Danieli katika tundu la samba wakali wenye njaa.
  Mfalme huyu atakuwa na kinywa kama na kinywa kama SIMBA, atanena kama BABELI, kutengeneza masanamu na kulazimisha kila mtu kuyasujudia. Masanamu ni kinyume cha Amri ya Pili ya Mungu.
  Danieli 3 na 6 KUNA HADITHI ya Ibada ya masanamu.
 Mfalme wa Ufunuo 13:1-10 atakuwa na tabia za Rumi ya kale. Tuujadili kidogo ufalme wa Rumi.
  Ibada ya sanamu na miungu iliyorithiwa kutoka Babeli,Umedi, Misri,Ugiriki n.k. Baadhi ya miungu ya Rumi, Aphrodite ambaye ni VENUS.
Mfumo wa sayari,nyota na mwezi viliabudiwa na Warumi. Mars ndiye Ares kwa Wagiriki, Artemy ndiye Diana,chimbuko la kumwabudu Bikra Maria siku hizi.Athena, Saturn,Pluto,Mercury,Uranus,Zeus ndiye Jupiter kiongozi wa miungu-orodha ni ndefu.
  Kila mungu alipewa siku maalum ya ibada.
 Saturday, ni kwa ajili ya mungu Saturn, Sunday ni siku ya mungu Jua yaani Sun’s day!
 Ibada ya jua ni Mithras, Isis wa Misri,Demeter wa Ugiriki,orodha ya miungu ni ndefu.
   Mfalme huyu wa Ufunuo 13:1-10 atapewa mamlaka na shetani, tapewa kiti chake cha enzi na uwezo mwingi, soma fungu la pili. Sasa, Urusi ama Iran watatawala wapi dunia?
   Tumejifunza kuhusu ‘donda la mauti’kupona Feburuari 10 mwaka 1929 na kwamba utawala huu uliwahi kutiwa jeraha Feburuari 11 mwaka 1798 wakati wa maasi ya Wafaransa.
  Dunia nzima itashangaa kuona mfalme ajaye anasujudiwa kama Mungu kwa lazima na hakuna demokrasia tena na uhuru wa dini-Religious Liberty.
  Ufalme wa kidini utaongoza dunia na kutoa amri(sheria kali) wale wasiosujudu sanamu wauawe ufunuo 13:15,17. Sitafsiri unabii kama nipendavyo,tusome Danieli 7:17 hadi 24.
  Mnyama huyu atamkufuru Mungu-kumkufuru Mungu ni mwnadamu kujiita Mungu Danieli 17:17,18 NI ‘Pembe Ndogo’ ya Danieli ambayo ni mamlaka hii ya ufunuo 13:1-10. Pembe yenye macho(Intelligence) na mdomo wa kumkufuru Mungu yaani utawala wa dini.
  Mataifa ya Ulaya yanayosemwa kuwa ni vichwa saba  yaani falme saba ni Anglo-Saxons(Uingereza),Alemanni(Ujerumani),Visigoths(Hispania),Franks(Ufaransa),Lombards(Italia),Suevi(Ureno) na Heruli, Ostrogoths na Vandali, walipinduliwa na utawala wa 538 hadi 1798 AD, YAANI MIEZI 42, SIKU 1260, Wakati nyakati mbili na nusu wakati.
 Usikose toleo lijalo uone AJENDA YA SIRI ya Ulaya,Marekani kuunda Dola la mseto wa dini na serikali duniani kwa ufadhili wa Freemasons,Illuminanti na Ibilisi.
0786 324 074
congesdaima@yahoo.com



  

Monday, February 13, 2012

VITA VYA TATU VYA DUNIA?

Unabii wa Biblia, Katika Mathayo sura ya 24, Ufunuo wa Yohana 16 na 17 Tunafundishwa mfululizo wa unabii unaotimia haraka sana.
Vita, pepo nne za Dunia zikianza kuvuma kwa nguvu kwa kuwa sasa Mungu ameacha kudhibiti amani ya dunia. Mikataba ya amani iliyowekwa zamani kama ule wa Visiwa vya Falklands vilivyogombaniwa zamani kati ya Ungereza na Argentina, inavunjwa. Kuna matetesi ya vita.
Tangu vita vya kwanza hadi vya     Pili, matetemeko ya ardhi n.k
Ufunuo 16 HUTUAMBIA Juu ya mapigo saba ya mwisho na VITA VTA HARMAGEDDON ambavyo vi vita vya kiroho zaidi.Wakati Ufunuo 17 inahadithia mamlaka za dunia zikiwa zimebeba madhehebu fulani ya kidini yatakayowalevya wakazi wa dunia nzima kwa Injili ya uongo ili kumkufuru Mungu.
Ufunuo 17 unabeba hadithi ya mamlaka za dunia,baada ya kuzipindua nchi za Mashariki,hususan Iran kuingia mkataba na Kanisa la Kikristo, ambalo litashirikiana na Roho Tatu za Vyura kuidanganya Dunia nzima, na kuwanywesha watu kwa 'mvinyo' wa mafundisho ya Uongo kuhusu Mungu Muumbaji.
VITA YA TATU ya Dunia (The World War III) iko mbioni,kufuatia Iran kutaka kufunga Mlango Bahari wa Hormuz, ambao ni muhimu kabisa kwa mataifa mengi Duniani kupitisha shehena ya mafuta Ghafi.
Mlango bahari huu ni mwembamba, ni kama kilomita 54 tu zinazoitenga nchi kavu ya Iran na Oman.
Mafuta yatokayo katika nchi tano zinazouza kwa wingi mafuta Duniani: Saudi Arabia, Kuwait,Iran,Iraq na Umoja wa Falme za Kiarabu(UAE)hutegemea Mlango Bahari huu wa Hormuz kusafirishia mafuta yao kwenda mataifa ya Magharibi.
Mapipa milioni 17 hupita hapa Mlango Bahari wa Hormuz,kila siku, na mafuta yanayopita mahali hapa ni takriban 1/5 ya mafuta yoote ya dunia nzima.
Iran, itakapoufunga Mlango Bahari wa Hormuz,ili  hayo Mataifa ya Magharibi yasipitishe shehena yao ya mafuta mahali hapo, athari zake zitaenea dunia nzima, na siyo kwa Marekani na Washirika wake wa Ulaya tu.
Kwa mfano, Kenya hutumia kiasi cha mapipa 80,000 ya mafuta kila siku; wakati Tanzania hutumia mapipa 40,000 kila siku na Uganda hutumia mapipa 14,000 ya mafuta kutoka eneo hilo.
 Mafuta haya yote hupitia huu Mlango Bahari wa Hormuz.
Na hii ni kusema kwamba, Iran ikiufunga Mlango Bahari huu meli za mafuta zikashindwa kupita, athari za kupanda kwa bei ya mafuta zitaenea hata Kenya,Uganda, Tanzania n.k na wala hali hiyo haitazipata nchi za Magharibi tu.
Kupanda kwa mafuta maana yake ni kwamba gharama za maisha zitakuwa zimepanda maradufu kila kona ya Dunia.
Hail hii ni kuzidisha maisha magumu zaidi hasa kwa raia masikini ambao hawataweza kumudu bei za bidhaa madukani,huduma za usafiri na huduma nyingine.
Ili kuhakikisha Iran isiufunge Mlango Bahari wa Hormuz,Marekani na Washirika wake wanajiandaa kuishambulia Iran, ili isije ikarogwa kuzishambulia meli kubwa za Mafuta za Ulaya na Marekani zinazopita hapo Hormuz.
Marekani,imetangaza kuiwekea vikwazo vya kiuchumi Iran ili isiuze mafuta yake  Umoja wa Ulaya na mataifa mengine ya dunia.
 Umuhimu wa Mlango Bahari huu wa Hormuz, utaonekana zaidi hata hapa Afrika Mashariki, pale Iran itakapotangaza kuufunga, ili mafuta yasiyosafishwa kutoka Iran au hata Irak,Kuwait,Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu, yasifike huku kwetu Afrika ya Mashariki ama mahali pengine.
Tayari  vita vya maneno baina ya Marekani na Iran vimeanza, na Iran imesema ikiwekewa vikwazo vya kiuchumi kutouza mafuta yake duniani, basi nayo itaufunga mlango Bahari wa Hormuzi, ili mafuta ghafi kutoka nchi zinazosafirisha mafuta kwa wingi yasipite mahali hapo.
Jambo hilo maana yake ni kuashiria vita vya Tatu vya Dunia; yaani kuufunga Mlango Bahari huo wa Hormuz ili meli kubwa za mafuta ghafi zisipite, maana yake ni kama kuweka  ‘jisu’ lenye makali katika koo la dunia!
Tayari meli za kivita za Marekani zenye kubeba madege ya kivita kama USS Abraham Lincoln (CVN 72 huelekea eneo hilila Mlango Bahari wa Hormuz kupitia Bahari ya Arabia,ili kukabiliana na kitisho cha Iran kuufunga mlango Bahari huo.
Wakati huo, Urusi na Uchina nao wametuma nyambizi kupeleleza mienendo ya tishio la vita katika eneo hilo.
Uchina na Russia ni wanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wenye kura ya turufu.
 Juzi, walipinga Syria kushambuliwa kwa sababu  majeshi ya nchi hiyo  yanawashambulia raia wanaoandamana kutaka Rais Al Assad aondoke mamlakani.
Kufuatia hali hiyo, Marekani na washirika wake wakiamua kuishambulia Iran, na China na Urusi wakakataa na kuanza kuvishambulia vikosi vya nyambizi na madege ya kivita ya Marekani, kutatokea nini?
Waama,Iran ikiwekewa vikwazo vya uchumi ili isiuze mafuta yake Ulaya na Marekani, na ‘ikajibu mapigo’ kwa kuufunga mlango Bahari huu muhimu sana kwa uchumi wa dunia, kutatokea nini kama siyo vita vya aina yake vitakavyosasambaratisha ‘chumi’ za nchi masikini hususan hapa kwetu Afrika Mashariki?
Gazeti la The East African la Feburuari 6-12,mwaka huu, limeandika katika ukurasa wake wa nyuma kwamba, “Mlango Bahari wa Hormuz” ukifungwa, ama kukitokea vita eneo hilo, basi ni mithili ya kuweka kisu katika koo la Dunia!
 Naam, kitisho cha uhai wa dunia kimefika huko Hormuz; na maisha ya watu masikini yako hatarini,kuliko wakati wowote.
 Iran, kwa miongo mingi imekuwa haina uhusiano mzuri na mataifa ya Magharibi, hasa baada ya kufukuzwa mamlakani, Mfalme Shah, mwaka 1989, akafia uhamishoni.
 Kiongozi wa Kiroho wa Iran, Ayatollah Ruhollah Khomein ndiye aliyehika utawala wa Taifa baada ya Shah, na Khomeini alipofariki dunia, akarithiwa na Ayatollah Ali Khamenei ambaye ni mtawala  wa sasa wa kiroho.
 Iran ni Jamhuri ya Kiislam inayoongozwa na Ayatollah Khamenei ;na Rais Mahmoud Ahmedinejad ni kiongozi wa serikali. Hawa wote hawana mahusiano mazuri na nchi za Magharibi pamoja na Israeli.
Wakati Fulani Iran ilitaka taifa la Israeli lisiwepo duniani-na hii kauli ilileta mtafaruku mkubwa, kwamba Iran ilikuwa ikirutubisha madini ya Uranium ili kutengeneza silaha za Nyuklia,lengo likiwa kuishambulia Israeli.
Utawala wa mjini Washington umetangaza vikwazo vya kiuchumi kwa Iran,kama itashupaza shingo kurutubisha Uranium na kufanya majaribio ya silaha hatari za nyuklia.
 Marekani,kuna Uranium; hususan katika Majimbo ya Montana, Nebraska, Colorado, New Mexico, Texas na hata Washington kuna Uranium kwa kiwango kidogo. Lakini, Maataifa haya ya Magharibi, yanachelea Uranium kuangukia mikononi mwa  “wenye siasa kali” wanaoweza kutengeneza Platonium, kwa ajili ya kuunda bomu la Nyuklia.
Mataifa ya Magharibi, yangali yanakumbuka hawa ‘siasa kali’(Extremists) walivyolipua mfumo wa reli jijini London, Julai mwaka 2005.
Kwa kuwa kuna Uchaguzi Mkuu Marekani  katika juma la kwanza la Mwezi wa Novemba mwaka huu wa 2012, Rais Barack Obama, anachelea kuiingiza Marekani vitani tena dhidi ya Iran.
 Lakini, kama Iran itafunga Mlango Bahari wa Hormuz, lazima kutatokea vita vikali kutoka kila upande.
 Urusi na Uchina wamepiga kura ya turufu kuzuia Syria kushambuliwa kijeshi. Je, safari hii watakaa kimya Iran inaposhambuliwa, au wataingilia kati?
Bila shaka, Iran ikishambuliwa na manowari za kivita za Ulaya na Marekani, bilashaka itajibu mapigo kwa kulipa kisasi kwa Israeli. Israeli, inajua hatari inayoikabili,pale vita katika Mlango Bahari wa Hormuz, vitakapofumuka.
 Mataifa mengine yenye uanachama wa Kudumu katika Baraza la Usamala la Umoja wa Mataifa, ni Marekani yenyewe, Ufaransa,  na Uingereza, ambao tayari manowari zao ziknakwenda Hormuz bega kwa bega.
 Iran imekuwa ikiituhumu Marekani na mataifa mengine ya Magharibi kwa kusababisha fujo ndani ya Iran.
 Uchaguzi wa Juni mwaka 2009 uliorejesha madarakani Rais Mahmoud Ahmadnejad, ulileta vurugu kubwa, wakati wapinzani wa serikali, Mir Hosein Mousavi alidai kushinda urais,lakini akaibiwa kura.
 Mpinzani mwingine wa serikali ya Iran ni Mehdi Karroubi, amabaye kama Mousavi wanahisiwa ni vibaraka wa Magharibi,hivyo Ayatollah Ali Khamenei ameapa hawawezi kushinda kwa kura na kuitawala nchi hiyo, ambayo ni Jamhuri ya Kiislam.
Propaganda za Magharibi zimekuwa zikidai kuwa Iran hakuna demokrasia,na ni mahali haki za binadamu zinakokiuka kwa kiwango kikubwa, na wapinzani wa serikali wanateswa.
 Hayo na mengine ya Iran kurutubisha Uranium ili kutengeneza Nyuklia, kutaka ‘Uzayoni’ za Kiisraeli kusambaratishwa duniani na kutaka kuufunga Mlango Bahari wa Hormuz, sasa ni kama kuongeza mafuta katika miali ya moto  katika Ghuba ya Uajemi.
 Israeli inajua hatua yoyote ya kuishambulia Iran, Wairan watajibu mapigo kwa kuishambulia Israeli.
Yumkini, nchi 27 za NATO zikaunga mkono manowari za kivita za Marekani zinazojongelea Mlango Bahari huu muhimu kwa kusafirishia ‘uhai’ wa dunia nzima kutoka nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi hapa duniani,pindi ukifungwa na Iran.
Hadi sasa, nchi za Kiarabu kama Yemen, Libya, Misri,Syria, Irak,Oman,Mauritania,Jordan na Tunisia, hamkani si shwari tena.
Nchi ambazo migogoro haijaanza ni Qatar,Kuwait, UAE,Lebanon na Bahrain ambako kungali na amani.
 Mataifa ya Magharibi yanadai katika Dunia ya Kiafrika na  Kiarabu kungali hakuna demokrasia,Uhuru wa watu kuabudu, uhuru wa kutoa mawazo yao na hakuna utawala wa sheria na Haki za Binadamu, nah ii ndiyo sababu ya kupeleka vuguvugu la harakati za mfumo wa mageuzi katika nchi hizi.
Iran itakaposhambuliwa na Mataifa makubwa, hasa itakapoaufunga Mlango Bahari wa Hormuz ili meli zenye kubeba shehena ya mafuta kutoka Arabuni kwenda Ulaya na Marekani, hapo ndipo risasi ya kwanza itakayoashiria Vita vya Tatu vya Dunia itakapoanza.
Vita vya Kwanza vya Dunia, vilianza mwaka 1914 na vikaisha 1918.
Sababu hasa za vita hivi ni Mtawala wa Ujerumani, WILHELM  II,alitaka kuleta changamoto kwa maendeleo ya viwanda vya Uingereza.
 Katika Vita hivi vya Kwanza vya Dunia, walikufa jumla ya wanajeshi 8,418,000.
Askari wa Marekani waliouliwa vitani ni 126,000 na kiasi cha raia waliokufa katika vita hivyo ni 1,300,000.
Katika Vita vya Pili vya Dunia(1939-1945), walikufa askari 16,933,000; askari wa Kimarekani waliokufa ni 292,000 wakati raia waliouliwa ni 34,305,000.
 Vita hivi vilikoma wakati Marekani ilipolipua mabomu ya Atomiki katika miji ya Hiroshima na Nagasaki, Agosti 6 na 9 mwaka 1945. Agosti 14, Japan ilitia saini ya kuacha vita na Septemba 2, mwaka huo wa 1945 vita hivi vilikwisha rasmi,vikiacha makovu ambayo hata sasa yangalipo.
Huku ndiko tuendako,tunarejea katika vita, wakati mikataba ya amani inapovunjika,wakati uharibifu mkubwa wa mazingira unaposababisha karibu sana Mapigo saba ya Mwisho.
Kuharibika kwa utando wa Ozone angani,uharibifu wa vyanzo vya maji na ukataji miti ni janga lingine la hatari.

Tuesday, February 7, 2012

VATICAN CITY NI MSHIRIKA WA UZAYONI KUUMIZA UISLAM?



NAANZA kwa Sahihisho: Kwamba, Yesu hakuzaliwa wakati wa Kaisari Tiberio,bali wakati wa Augusto.
Nataka msomaji ajue urafiki uliokuwepo kati ya Wapalestina, Warusi, Venezuela na Cuba ya  Kamaradi, Field Marshal Fidel Alejandro Castro Ruz.
Warusi, zama hizo USSR  walikuwa milioni 250 sawa na ilivyokuwa Marekani, na walikuwa na Jeshi kubwa lenye vifaa vingi, wakati ule wa Kambi  yao iliyoitwa Nchi za Makataba wa Warsaw(Warsaw Pact) iliyokuwa kambi adui wa NATO. Kasome Military Balance during The Cold War.
Illich Ramirez Sanchez, “Carlos” mwaka 1970 alipokuwa bega kwa bega  na Wapigania Uhuru wa Popular Front for Liberation of Palestine(PFLP),Magazeti ya Ungereza,hususan The Guardian, likambatiza jina hili, “The Jackal” kulingana na alivyowindwa sana na wapelelezi wa Magharibi.
Kulikuwa na kundi la kigaidi liitwalo, Black September, la akina Carlos na Wapalestina,kazi yao ilikuwa kulipa kisasi kwa adui zao wa Magharibi, na wakati mwingine walivamia Taasisi za Fedha za Ulaya na Marekani ili kupata nguvu za kutekeleza Operesheni zao na Harakati za Kupinga Ubeberu.
Septemba 5 mwaka 1972 Black Septemba walijipenyeza katika kijiji cha Olimpiki huko Munich,Ujerumani, wakawateka wanariadha wa Israeli waliokuwa bwenini wakati wa michezo ya Olimpiki ya Majira ya Kiangazi huko Munich.
Carlos, ni mzaliwa wa Venezuela katika mwaka 1949, baba yake alikuwa mwanaharakati,mfuasi wa siasa za Karl Marx. Mama yake alikuwa Mkatoliki. Tunaposema Ukatoliki, tunausema mji wa Rome(Italia) ambao ni mji wa kale zaidi Ulaya,uliojengwa miaka 753 kabla ya kuzaliwa Yesu.
 Carlos, kafanya  harakati nyingi kuzitia hasara nchi za Magharibi za Kibepari, hadi mwaka 1991 alipotiwa mbaroni Mjini Khartoum, Sudan.Sudan hii ya Omar Hassan al Bashir, nayo iko matatani,kuwalea magaidi.
 Ni makachero wa Kifaransa waliomnasa  Carlos The Jackal mjini Khartoum, wakamsafirisha ndani ya gunia hadi mjini Paris. Mwaka 1997, wakati akiwa mahakamani, akasema hivi:
“”Sijawahi kumuua mtu yeyote kwa ajili ya kutaka fedha; nimeua kwa sababu ya ukombozi wa Palestina”. Amesema.
Amefanya harakati nyingi kukiwemo kutaka kuwatia mbaroni mawaziri wan chi za OPEC; hata hawakufanya mkutano tena hadi baada ya miaka 25,
Hata hivyo, Carlos alianza kutiliwa shaka na Chama cha PFLP kwa kushindwa kuwakamata hao mawaziri wa Fedha wa  Saudia na Iran(zama za Shah), kabla ya Ayatollah Ruhollah  Khomeini kumpindua kibaraka, Shah.
Amekuwa ‘gaidi’ wa kukodishwa mahali pengi duniani.Wakati mwingine alishirikiana na Shirika la Ujasusi la Urusi(KGB),wakati huo aliwindwa sana na Shirika la Ujasusi la Marekani, Central Intelligence Agence, na polisi wa Kifaransa.
                                                   “ KUKAUSHWA” KWA MTO FRATI  (Ufunuo 16:12) 
Kuangushwa kwa ukuta wa Berlin mwaka 1991 ndiko kunakoashiria mwisho wa Vita baridi duniani.Dola la Urusi(USSR) ,liliposambaratishwa, basi Carlos akakosa pa kujificha, akakosa hifadhi.
Saddam Hussein aliuawa mwaka 2006 mwishoni,”Mto Frati” ukakaushwa ili kupisha njia kwa mataifa ya Mashariki, China,India na Japan kujiunga na Soko la Pamoja la Ulaya  ili kufanya biashara pamoja.
Wakati huu Carlos akabadili sura na majina, akabadili makazi kila mara hadi alipokamatwa. Mwaka 1997 alikutwa na hatia ya kuua na akafungwa jela kifungo cha maisha huko  Clairvax. Kukaushwa Mto Frati ni kuondoa kizuizi kilichotenga mataifa ya Magharibi na Mashariki.
Carlos, aliingia Uislam akamuoa mwanasheria wake Isabelle Coutant-Peyre, mwaka 2001. Ameandika kitabu kiitwacho Revolutionary Islam ambamo anatetea matumizi ya nguvu dhidi ubeberu wa Kimagharibi.
Amechukia sana baada ya tangazo la Rais Obama la kuuawa kwa Osama bin Laden, ambaye alisema angekuwa ‘Mrithi’ wake, baada ya yeye kuwa amefungwa maisha.
Rais wa Venezuela, Hugo Chavez(aliwahi kumtukana Bush Umoja wa Mataifa)mwaka 2009 alisema Carlos hakuwa gaidi,bali ‘Mpigania Uhuru’ wakati wa harakati za kupinga ubeberu.Aliwahi kushirikiana na Saddam,Muammar Gaddafi,Fidel Castro na mashujaa wengine wanamapinduzi wa zama hizo za Vita Baridi,
Wasomaji wakatafute kitabu kiitwacho, Days of the Jackal cha Frederick Forsth,ili kutazama harakati za akina Carlos wakati wa vita baridi. Usiniulize utakipata wapi; maktaba?
Mwisho wa Vita Baridi,Kuanguka kwa Ukuta wa Berlin,Kusambaratika kwa Dola la Urusi(USSR)maana yake ni kwamba Ukomunisti umekwisha; na Ukomunisti unapokwisha,kinachoshika nafasi ni  mfumo wa kidini ambao Vatican City wanakuwa na nguvu,na tutaeleza kwa undani katika makala hizi.
Hakuna atakayewazuia Magharibi na Washirika wao(Allied Forces of The West)  na Freemasons, kuikomesha nchi yoyote kwa kuwekewa vikwazo vya kiuchumi(Ufunuo 13:11-18).
Yemen,Libya,Syria na Irak na Oman, Mauritania,Jordan wanajisalimisha baada ya mbinyo wa kila namna. Qatar,Kuwait,UAE,Lebanon, Bahrain wanajipeleka wenyewe kwenye muungano wa dini, siasa na uchumi wa dunia.
Watakao kataa kutii sheria hiyo ya Ulimwengu-New World Order-inajulikana wazi watafungwa jela,kuuliwa,kuwekewa vikwazo n.k Gaddafi, Osama, Saddam ni mfano mzuri.
 Mwezi huu,tumeona China na Urusi zikipiga kura ya Veto kupinga Syria kushambuliwa kijeshi na Umoja wa Mataifa,kwa madai kuwa inaua raia wanaoandamana. Unatafutwa mkakati mwingine,lazima mtawala wa Syria aachie ngazi.
Zamani, NATO(Northern Atlantic Treaty Organization) walikuwa nchi  chache tu za Ulaya na Marekani, ambazo zilikuwa Kaskazini mwa Bahari ya Atlantic, sasa kuna nchi 27; ambazo zinafuata kila Marekani na Uingereza wanakokwenda kupindua serikali.
Umoja wa Mataifa ulioanzishwa eti kutuliza vita, umegeuka kuwa Umoja wa Mataifa wa Marekani! Waziri wa Ulinzi wa Marekani,Leon Panetta, anasauti kuliko nchi nyingine yoyote.
Tumjadili kidogo Marehemu Muammar al Gaddafi.
 Ati alikuwa dikteta? Ati Wanachama wa Kudumu wa Baraza la Usalama Umoja wa Mataifa,Marekani, Uchina, Urusi,Ufaransa na Uingereza waliunga mkono apinduliwe kisha akauliwa kwa risasi kwa kukiuka haki za Binadamu.
 Angalia: Libya ya Gaddafi, maji yalikuwa ya kutosha kwa raia tena  ya bure, umeme buree kabisa,nyumba ya kuishi bure,mimi huku ninaongezewa kodi na mwenye nyumba ili apate pa kuponea haya maisha magumu! Kwa Gaddafi nyumba ilikuwa kuishi bure.
Kabla ya kupata ajira unapewa posho ya kujikimu bwana! Libya haikuwa na madeni nje. Akiba yao nje ilikuwa dola za Marekani Bilioni 150.Ukiwauliza hata wapinzani wa Rais KIKWETE hapa kwamba kati ya Kikwete na Gaddafi nani zaidi? Gaddafi angepata kura za Ndiyo!!
Hili niliache. Unabii unatimia, waliopinga sera za Magharibi sasa wanang’olewa, watu wote wa ule ‘mlengo wa kushoto’ sasa wanalazimishwa kufuata ‘mlengo wa kulia’.
Uislam, ni dini iliyoanzia Mashariki,siyo Ukomunisti. Muislam ni mtu aliyejitoa kimamilifu kwa Allah,Uislam ni kulinda utu,ukweli na uhuru-Jambo hili ni hatari kwa siasa za Magharibi. Hakuna tofauti kubwa na kusema UJAMAA NI UTU,na ubepari ni unyama.
Kukaushwa mto Frati(The dries up process of the River Euphrates) maana yake ni kuzing’oa dola za Mashariki na sera zake kudai usawa na utu hivi; ndiko kupinga ubeberu na maguvu ya mtu mmoja mmoja au mabwenyenye wachache.
Carlos, alikuwa mfuasi wa PFLP na alipewa jina hili kwa ushabiki wa babaye kwa akina Che Guevara na Carlos Merighela-wajamaa, ali ‘Slim’ na kuwa na Msimamo mkali, “Extremisms”.
Nimetumia neno kuwa na msimamo mkali kwa kuwa ni ushupavu tu wa kidini-shahids, martyr ama ujasiri wa kutetea dini. Carlos alitetea Ukomunisti na dini,kama Osama na wenzake.
Mwaka 2009,Hugo Chavez, rais wa Venezuela asiyependwa na Marekani, alisema Carlos hakuwa gaidi ,bali Mwanamapinduzi.
Nirejee Historia ya Uislam(kwa mujibu wa Historia) umeanzishwa mwaka wa AD 622 Mecca katika Peninsula ya Arabia na Mtume Muhammad(570-632 AD)kukataa jambo hili ni kuikana historia n a unabii.
Ndani ya Uislam kuna nguzo tano hasa kulinda UTU,UKWELI na Haki, na itakavyokuwa NATO, na washirika wao wanajidai kutetea jambo hili hili lakini wataondoa haya yote matatu, wataondoa uhuru na demokrasia duniani. Hapa ‘majambia’ hayawezi kupambana nao maana wanasaidiwa na Shetani.
Watakaokataa kutii mamlaka inayokuja duniani, watafungwa jela na kukumbwa na mauti ama dhiki ya vikwazo vya uchumi(UFUNUO 13:15-18).
Napenda kumjibu George Mbilinyi wa Iringa kama ifuatavyo:
Vatican City(The Holy See) mwaka 2004 ulikuwa na watu 870;wengi Waitaliano na wapo Waswisi. Wanaongea Kiitaliano, Kilatini, na wote ni Wakatoliki-Vatican ni nchi ya dini moja. Fedha wanayotumia ni Lira ya Vatican na ile ya Italia ambazo thamani yake ni sawa.
Lira tatu hivi thamani yake ni sawa na dola moja ya Marekani. Vatican inazungukwa na Italy-eneo lake ni ekari 108.7 na mtawala wake ni Papa.(Papal State).
Katika kitabu kiichwacho THE WORLD ALMANAC toleo la 2002,ukurasa wa 863 kuna maelezo kuhusu Vatican.
Kwamba,Feburuari 11 mwaka 1929 ulitiwa saini mkataba kati ya Kadinari Gasparri na Waziri Mkuu,Benito Mussolini; mkataba wa uhuru wa Vatican na ukatoliki kupewa “Special Status” ndani ya Italia.
Mkataba huu unaitwa,  Lateran Agreement(Article 7). Feburuari 10 mwaka 1798 Papa alitiwa mbaroni na akafungwa jela. Nataka kusema kwamba, ‘donda la mauti’ la Ufunuo 13 lilipona baada ya miaka 131 kamili.
Marekani, hawakuwahi kuitambua mamlaka haya ya VATICAN,SABABU zinafahamika, wakati wa vita kati ya Wakatoliki na wanamatengenezo(Christian Reformation) wa Ulaya walitimkia Marekani ili kukwepa vita vya miaka 1260 yaani kutoka 538 hadi 1798 AD.
Mtu anaweza kusoma vitabu vingi akajua haya, hasa kile kiitwacho, Africa Learns about Europe, The Great Controversy n.k
Marekani ilikuja kutambua mamlaka ya Vatican mwaka 1984,ilikuwa baada ya kuondoa uhusiano wa Kidiplomasia katika mwaka 1867.
Marekani walipata uhuru Julai mwaka 1776,kwa muda wote hawakuitambua Vatican hadi mwaka huo wa 1984.
 Vatican na Israeli walitiliana saini makubaliano ya uhusiano wa kibalozi Desemba 30 mwaka 1993. Msomaji mmoja aliniuliza uhusiano wa Israeli na Vatican, na anapaswa kujua kwamba Israeli maana yake ni dini ya Kiyahudi, ‘Judaism’ na Ukatoliki wa Vatican kuanza kuhusiana, maana yake ni kuondoa kizingiti kati ya Uzayoni na Ukatoliki.Sasa bado Waislam?
Turejee katika unabii wa Ufunuo wa Yohana 13.
Marekani ni mamlaka inayosemwa katika fungu la kuanzia 11 kwamba ina pembe mbili mfano wa kondoo-yaani UHURU WA DINI na Uhuru wa kisiasa, lakini sasa unabii unasema Marekani wataondoa demokrasia duniani, itapindua serikali nyingi kwa kushirikiana na Vatican, Israeli, Ulaya na mataifa ya Kiarabu yaliyojisalimisha na kushirikiana, na watakuwa chini ya maelekezo ya Freemasons na Ibilisi.
Marekani itashirikiana na VATICAN(Donda la mauti lililopona Feburuari 11 mwaka 1929-Ufunuo 13:12) ili kulazimisha dunia nzima kumsujudu,kumwabudu Mfalme,badala ya Mungu wa Mbinguni. Rejea Danieli sura ya 3.
Waislam, walioniandikia SMS kunipinga wanaweza kusoma Danieli sura ya 3. Jeraha la mauti lilipona wakati wa kutiliana saini ule mkataba(Article 7) wa Lateran Agreement.
Mbilinyi kutoka Iringa, alipenda kujua,Vatican kuna jeshi lipi?
 Papa ni miongoni mwa viongozi wanaolindwa sana hapa duniani. Analindwa na askari wa Kiswisi. Baba Mtakatifu ana maadui pia,lazima alindwe. Papa Pius VI alitiwa mbaroni na Jenerali Berthier wa Ufaransa,Feburuari 11 mwaka 1798.
 Papa John Paul II alipigwa risasi. Novemba 27 mwaka 1970 Papa Paulo VI alishambuliwa kwa kisu(hakuumia) katika Uwanja wa Ndege wa Manila, Ufilipino.
 Mwaka 1981 Papa Paulo II na watu wengine wawili waliokuwa jirani naye walipigwa risasi. Ilikuwa Mei 23, mwaka huo wa 1981 Mahmet Ali Agca, akafumua risasi akamjeruhi Papa. Huyu jamaa Mahmet Ali Agca, ni  Mturuki, ambaye alitekeleza tendo hilo la kigaidi wakati Papa akihutubia St. Peter’s Square ,Rome.
Huyu Papa alikufa mwaka 2005 kwa ugonjwa wa kutetemeka.
Mei 12 mwaka 1982  Papa John PauloII ALINYATIWA na muuaji mwenye kisu,walinzi wake wakamnyang’anya kisu huyo jamaa huko Fatima,Ureno.
Papa ni Askofu wa Rome; ni Mwakilishi wa Yesu-THE VICAR OF JESUS CHRIST-NI Mrithi wa Mtume Petro, ni Mkuu wa Mitume wote,ni Mkuu wa Kanisa lote la Kikristo Duniani. Papa ni Mamlaka.
Kasela wa Mbeya, msomaji wa kila siku wa gazeti hili ameniuliza uhalali wa kueneza dini kwa mfumo wa maguvu,vita na majambia?
Ujumbe wa Biblia ni huu(Yohana 18:10-11)Petro alimkata sikio adui yao aitwaye Malko kwa jambia kali.Yesu akaona tukio hilo na kuanza kumkemea, “Rejesha panga  lako Alani mwake!” Hata mimi nasema, “Rudisheni mapanga yenu mahali pake” ndiyo Amri pekee ya kudumisha Amani Duniani.
 Mpigania haki za Weusi Marekani, Martin Luther King Jr. aliwahi kuwakataza Wamarekani Weusi zama za Ubaguzi wa rangi kupinga unyanyasaji bila vita-Non Violence Resistance- ndivyo walivyowahi kufanya wanamapinduzi kama Mahtma Gandhi wa India,uhuru ukapatikana!
0786-324 074