Thursday, May 31, 2012
Mwanamke wa Ufunuo 17 ni Kanisa la Rumi
TUWEKE
kumbukumbu zetu makini zaidi.
Feburuari 26 mwaka 2009,William Shao aliandika
katika Gazeti la Rai,kwamba mwanamke anayefanana na Yule wa Ufunuo wa Yohana
17:3-11, amejemgewa sanamu mbele ya Jengo la Bunge la Umoja wa Ulaya, huko
Brussels,Ubelgiji.
Shao,
alienda mbali zaidi kusema, hata jingo lenyewe la Bunge la Ulaya(EU) mjini
Brussels, halina tofauti sana taswira yake na Mnara wa Babeli.
Shao, anasema sanamu ya mwanmke aliyeketi juu ya mnyama mbele ya ofisi za Bunge la Ulaya, haikuwekwa kwa bahati mbaya; inatafsiri jambo fulani muhimu wewe kuelewa.
Ulaya, ilikuwa himaya ya Dola ya Rumi; na
Mwanamke huyo wa mjini Brussels anayeitwa, “Europa Goddes” ni mungu mke wa
Ulaya.
Naam, mungu jike wa Ulaya ndiye mtawala wa
Ulaya na makoloni yake duniani, na mji anaoketi huitwa kwa Jina la Siri, “Babeli”
Ufunuo 17:5!!
Umeona picha
ya mnara wa Babeli? Ni kama alivyosema mwandishi William Shao,kwamba inafanana
sana na jingo la Bunge huko la Ulaya huko mjini Brussels, Ubelgiji.
‘Uropa Goddes’-mungu
jike wa Ulaya,hufananishwa na jiji la kale sana Babeli ambayo ni Irak ya siku
hizi.
Kulingana na Biblia, mwanamke katika Unabii ni
kundi la waabuduo-kanisa, waumini. Kuna wanawake wawili katika Ufunuo wa
Yohana, Ufunuo 12 na 17; moja huwakilisha kundi nyoofu katika maadili ya kidini
na, mwanamke wa Ufunuo 17 ni kundi kengeufu linalojichanganya na waabudu
sanamu, anasa za dunia na uchafu wa kiroho.
Katika Hosea
2:10,Yeremia 3:14 na 2Korintho 11:2 uhusiano baina ya Mungu Mwenyezi na Kanisa
lake hufananishwa na uhusiano wa ndoa,kati ya mume na mke.
Katika
Ufunuo 21:2 mji wa Yerusalem umefananishwa na ‘Bibi Harusi’ yaani mwanamke
safi. Kanisa la Mungu linapoungana na dunia na anasa na kuabudu sanamu,
hufananishwa na UZINZI(Tazama Yakobo 4:4).
Naam, Yakobo
anawaita watu wa Mungu waliomwacha na kuungana na Dunia ya dhambi kwamba ni
Wazinzi, waasherati, makahaba!
Ni hapa, tunapomaizi kwamba mwanamke wa Ufunuo
17:3 ambaye ni “mungu-jike wa Ulaya” ni Kanisa la Mungu lililoungana na Dunia
na mivuto yake na anasa zake na kumwacha Mungu.
Anasa,ulevi,falsafa,ibada
ya sanamu na miungu,ushoga,ulawiti hata wa watoto chekechea n.k
Mavazi ya ‘Mwanamke’
huyo ni rangi nyekundu na zambarau, ambayo yalivaliwa na makuhani wa miungu
huko Babeli ya kale.
Hawa ni kundi tajiri wenye madini,vito vya
thamani na urembo ambalo linamvuto mkubwa kwa Wafalme wa Dunia. Kanisa hilo
linasemwa kutawala miongoni mwa wafalme wa dunia(Marais, Mawaziri Wakuu,Wafalme
n.k) yaani hubebwa na watawala wa Umoja wa Ulaya huko mjini Brussels(Tazama
Ufunuo wa Yohana 17:4-6).
Muungano
haramu wa Kanisa la Mungu na viongozi wa dunia(uzinzi) ndiyo kuungana kufanya
yaliyo kinyume na Amri 10 za Mungu. Kuungana na upagani, kuabudu sanamu na
miungu kama jua, sayari,nyota na mwezi.
Mwanamke wa
mjini Brussels anao watoto wake nao ni ‘Makahaba’ yaani wazinzi wa kiroho.
Sasa,
tutazame kwa makini; kama mji wa Brussels mwaka 96 AD wakati Mtume Yohana
anaandika kitabu cha Ufunuo,ulikuwepo? Hasha!!
Nchi nzima ya Ubelgiji ina watu wasiozidi milioni
12. Brussels siku hizi una wakazi milioni 1.5 tu.
Tuutafute
mji wa kale sana Ulaya, ambao Yohana aliuita jina la mafumbo Babeli. Umejengwa
juu ya milima saba(ufunuo 17:9).
Mwaka 753 BC mji uliojengwa Ulaya ni Rome.
Hata London haukuwepo, Uingereza ilikuwa kijiji kidogo mwaka 1000 AD. Hata
mwaka 500 BC Rome lilikuwa jiji tena “SUPER POWER” Duniani, ulijengwa na
Romulus.
Katika mji huu ndiko yaliko mamlaka ya
kidini,Vatican. Unaposema Vatican unasema kanisa la Mungu. Vatican imekuwa nchi
Feburuari 11, mwaka 1929 zama za Benito Mussolini.
Habari zinazovuja(hata
BBC wametangaza Jumatano iliyopita) kwamba kuna njama za mapinduzi baridi na
mchakato wa kumsimika Papa mpya badala ya Benedict XVI.
Rome ni
mahali ambapo wameishi ma-Baba Watakatifu(Popes) wa Katoliki wapatao 302. Mji
huu ulikuwa makao makuu ya dola ya Rumi, hata zama za Yesu,mitume na zama za
Biblia Takatifu yaani kati ya mwaka BC 1500 ZAMA ZA MUSA Hadi 96 AD alipofariki
Yohana wa Patmo.
Nataka msomaji atambue kwamba, waandishi wa
Biblia waliposema Babeli,baada ya kuanguka kwa mji wa Babeli, walimaanisha MJI
WA ROME(Isaya 21:9).
Fahari yake
na ulikuwa mji mkuu wa biashara duniani. Kanisa Katoliki linadai Petro
aliyefika mjini Rome mwaka 42 AD na akauliwa na Kaisari Nero Mkatili, mwaka AD
67,ndiye Papa wa Kwanza kwa Kanisa hilo.
Tuwatazame mapapa. Huchaguliwa na Makadinari
kama 131 hivi. Papa Benedict XVI yeye alichaguliwa na Makadinali 117, ambao
hawakuwa na umri wa miaka 80. Papa ni Mwakilishi wa Yesu,mrithi wa Mtume
Petro,Mkuu wa Mitume wote duniani,Papa ni Mamlaka na nguvu-Tazama Danieli 7:25.
Rome, ni mahali Kanisa la Mt.Petro
lilipojengwa juu ya Kanisa la Petro; linaitwa, St.Peter’s Basilica. Limejengwa KATIKA
ENEO LA EKARI SITA.
Hili kanisa,
St. Peter’s Basilica, lina urefu wa futi 700 na upana ni futi 450 na linaweza
kuchukua watu 80,000 kwa wakati mmoja.
Rome ni jiji
lililopo nyuzi sawa na New York kwa nyuzi za Latitude; ni jiji lenye Coliseum,
ambamo yalifugwa masimba yaliyorarua Wakristo maelfu.
Rome,uko
futi 40 hadi 270 juu ya usawa wa Bahari. Jiji lenye kelele nyingi kuliko mji
wowote duniani,lipo kando ya Bahari ya Mediterranean.
Zama za Papa Pius XII alibebwa kwenye kiti cha
enzi kiitwacho, Sedia Gastatoria ambacho
ni kiti cha enzi cha dhahabu chenye rangi nyekundu.Papa huketi hapa mara
anapochaguliwa na Moshi Mweupe, hutoa
BARAKA Duniani- Urbi et Orbi.
Rome
umejengwa juu ya milima saba: CAPITALINE, PALATINE, AVENTINE, QUIRINAL, VIMINAL,
ESQUILINE, na CAELIAN.
Hapa, ndipo
liketipo kanisa lile la Mungu ambalo sasa linataka kugeuka kuwa kama Yule mama
wa mjini Brussels.
Mwanamke
huyu ni kanisa. Kanisa linapoungana na dunia na kuacha usafi wa kiroho huitwa, ‘BABELI’
ya siri iliyoanguka na Mungu huwaita watu wake watoke humo(Ufunuo 18:2-4).
Kuanguka ni
kuacha usafi wa kiroho,kumwacha Mungu na kuungana na uchafu kama unajisi,siasa
za kugombea tawala za dunia,ufisadi,mapinduzi,ulawiti,ushoga n.k
Jiji lenye
utajiri wa dhahabu na vito vya thamani lenye kuwakosesha watu kwa mafundisho
yenye kuridhia dhambi(uasi wa sheria ya Mungu) kama jambo dogo tu-Uhuru na
demokrasia,haki za binadamu n.k
Wapo
wanaofuata kila jambo na ni ‘watoto’ wa Yule mama wa mjini Brussels.
Tafakarini.
0786 324 074
MASKINI CHARLES TAYLOR
TITANIC,
TUREJEE kidogo katika somo la Kuzama kwa Meli ya Titanic.
Kwamba, ilizama kwa maelekezo ya Freemasons. Nahodha wa Meli
ya Titanic, E.J.Smith, alielekezwa kuizamisha meli ili kuwaulia mbali matajiri
waliokuwemo.
Mhariri wa Makala wa Gazeti hili, Markus Mpangala,Mei 22
mwaka huu akawataja matajiri hawa walioangamia katika ajali hiyo kwamba ni John
Jacob Astor,Archibald W.Butt,Charles M. Hayes,na mkewe na binzi zao,
W.T.Stead,Benjamin Guggenheim, F.D.Millett na G.D.Widher.
Wengine walioangamia ni Isidor Strauss, na mkewe,J.B Thayer,J,Bruce
Ismay,Henry B. Harris na mkewe na Washington A.Roebling.
Sina haja ya kulumbana na mtu kwamba Freemasons ambao
kimsingi ni mawakala wa Ibilisi hawasababishi ama wanasababisha kutokea kwa
majanga. Sote tunajua kuna nguvu mbili zinazoshindana duniani, nguvu ya wema na
ile ya kufanya mabaya. Freemasons ni mawakala wa Ibilisi wenye kazi maalum ya
kuhadaa watu,wakidhani wanafanya mema.
Hata hivyo, Alex
Mayoge wa Moshi,Kilimanjaro aliniandikia SMS kusema kwamba TITANIC ILIZAMA ili
kuwaua matajiri hao ili Freemasons wapore fedha zao kwenda kugharimia VITA VYA
KWANZA VYA DUNIA.
Titanic ilizama Aprili 1912 na ni miaka miwili baadaye,mwaka
1914 vita kuu ya kwanza ya Dunia ikaanza kwaka 1914.
Vita vila lengo Fulani,
na aghalafu vita wanavyoanzisha Freemasons ni vya kupora rasilimali ama kuweka
mamlaka yao mahali wanapopingwa,nguvu za ushawishi zinaposhindikana.
Vita vya Pili vilianza 1939 vikakoma 1954. Tulishajadili
jambo hili kwa kina,na anayetaka aangalie Blog yangu kuhusu vita hivi na
matokeo yake.
Malengo ya maharamia hawa yangalipo duniani,ndiyo maana kuna
vita leo Congo na maeneo mengine kama Sierra Leone, tuliona Revolutionary
United Front wakipewa silaha kuharibu serikali ya mjini Freetown,ili wapore
ALMASI ZA DAMU.
Mwisho wa siku Fodday Sankoh alikamatwa na kupelekwa The
Hague ambako eti alifariki ama kunyamazishwa, leo niandikapo hapa Taylor
anahukumiwa kifungo cha miaka mingi huko jijini London,Uingereza?
Soma tamthilia hii kama kichekesho tu(Satire) cha
Taylor huko Mahakamani Hague, dhidi ya wakubwa.
CHARLES TAYLOR 64 + 80
ASKARI:
Koooortiiiii?
(Mahakama ya Umoja wa
Mataifa,ICC,inaanza kikao chake, ‘session’ mjini The Hague, Uholanzi.
Washitakiwa, maofisa wa
Mahakama wanaingia,na watu wote ndani ya mahakama hiyo wanasimama wakati
wa majaji kuingia kortini, ambamo Taylor anashitakiwa kwa makosa 11 ya uhalifu
wa kivita huko Sierra Leone tangu 1991 hadi 2002, akiwasaidia United
Revolutionary Front).
KARANI:
Charles Ghankay Taylor
dhidi ya Haki za Binadamu?
TAYLOR: Timamu,
Mheshimiwa Jaji, Lussick. Hata hivyo nashangaa,katika kesi hii washitakiwa
wenzangu, akina mabwana George W.Bush na Tony Blair wameachwa. Haidhuru!
Nimamaizi Mheshimiwa Jaji, mahakama hii ya ICC hapa Hague ina makengeza!
JAJI LUSSICK:
Mwendesha Mashitaka una hoja?
MWENDESHA MASHITAKA: Mshitakiwa aliwafadhili
Waasi wa RUF walipoua watu huko Sierra Leone, akawatumikisha watoto maelfu
jeshini kwa muda wa miaka 11; naye ana makosa 11.
JAJI LUSSICK: Mshitakiwa, Charles
Taylor,Rais wa zamani wa Liberia, unapaswa kuieleza mahakama hii tukufu, una
maanisha nini kusema mahakama ina makengeza? Mahakama ina macho?
(kicheko cha kwikwi
toka kwa wasikilizaji)
TAYLOR: Mheshimiwa, sina maana kwamba
mahakama ni kipofu; ila ina makengeza! Haina macho, mahakama ina ‘double
standards’ yaani upendeleo, haiwaoni Wazungu tuliosaidiana nao kuwafadhili
United Revolutionary Front(RUF) ili wapore ALMASI ZA DAMU ili ‘deal’ hii itupe
utajiri? Sasa mheshimiwa, kazi tumefanya wote na akina Bush na Blair, eti ‘zengwe’
nasukumiwa mimi peke yangu. Hiyo noma Mheshimiwa!
JAJI LUSSICK: Okay! Okay! Nimekupata Mr. Taylor,
ohh..samahani, Mr. X-President! Hata hivyo hujakana shitaka lolote kati ya haya
11 unayokabiliwa nayo?
TAYLOR: Nikanushe nini
Mheshimiwa wakati mlikwishaamua kunitosa?
JAJI LUSSICK: Tumuulize Mwendesha Mashitaka
Mkuu,Louis Mareno-Ocampo. Kwanini Taylor? Why Taylor, and why not Wazungu in
this TRIAL?
OCAMPO:
Mheshimiwa Jaji,Lussick,
Rais Mstaafu wa Liberia, Bwana Caharles Taylor alishatakiwa na wenzake kama
Fodday Sankoh,kiongozi wa RUF.
TAYLOR: Mheshimiwa, nataka Ocampo aieleze hii
mahakama ya Fisi ambako mimi Mbuzi leo nasulubiwa kinyama! ‘Poppy’ Sankoh ni
mshitakiwa namba ngapi katika kesi hii?
OCAMPO:
Sankoh hayupo hapa mahakamani. Kama mahakama inakumbuka, alifariki akiwa
rumande hapa mjini Hague.Waasi wengine wakikamatwa upelelezi ukikamilika nao
tutawashitaki, hakuna ‘impunity’ kwa mkosaji yeyote.
TAYLOR: Mheshimiwa, inakuingia kichwani kwamba mimi peke
yangu ningeweza kufadhili RUF kuua watu,kubaka,kukata raia viungo na kupeleka
watoto 200,000 vitani,kama siyo msaada wa Bush,Blair na ‘Wadosi’ wengine wa
huku ‘majuu’ mheshimiwa, kama siyo kunionea?
JAJI:
Swali
jingine?
TAYLOR:
Mimi peke yangu
ningewezaje kumpa Poppy Sankoh ‘shavu’ kwa miaka thenashara, hadi akombe ALMASI
ZA DAMU Sierra Leone? Eti wanasema mjini Johannesburg nilimhonga yule kimwana,
Naomi Campbell bonge la almasi ghafi. Hizo almasi nilizipataje na nilikuwa
namuuzia nani, Mzungu au Mwafrika,Mweupe au mfupi, mnene au kimbaumbau? Ebo!
Noma mheshimiwa!!
(kicheko cha kwikwi
kutoka kwa wasikilizaji mahakamani)
BRENDA HOLLIS: Taylor na Sankoh
walishirikiana kufanya uhalifu Sierra Leone,KWA MTUTU WA BUNDUKI, walipora
almasi za damu na kuziuza kwa wateja wao Ulaya na Marekani
TAYLOR:
Tena huyu Brenda
Hollis,Mwendesha Mashitaka ni mpuuzi kabisa, afadhali Ocampo, tuliua watu kwa
bunduki? Umesikia Liberia kulikuwa na kiwanda cha bunduki kama AK 47?
OCAMPO: (anasimama) Mheshimiwa Jaji, ALMASI ZA
DAMU zilisafirishwa kwa magendo hadi Afrika Kusini hadi Ulaya na Marekani
ambako walibadilishana na Wazungu kwa almasi kwa bunduki yaani Guns for
Diamonds mheshimiwa!
TAYLOR: Basi poa, Mheshimiwa Jaji, sasa
wanataka mimi nikanushe nini kama hata wao wanajua Mzungu alifanya vikao vya
G-8 vya kinafiki huko Antwerp, kukataza biashara ya almasi za damu,kumbe naye
alizimaindi?
JAJI:
kama sijakosea, swali la mshitakiwa ni kwamba, kwa nini upande wa
mashitaka haujawaleta mahakamani walionunua almasi za damu toka Sierra
Leone,badala yake wamewaleta wauzaji peke yao?
TAYLOR: Hewaa! Jaji,kumbe hukusoma mwembeni na kupata
digrii za ‘madensa’ ila umebukua sheria! Umenipata! Huyu Ocampo kwao ni Buenos
Aires, Argentina, sasa ni kibaraka wa Mzungu wa Ulaya hajui EU walipora almasi
za damu licha ya sheria kupiga marufuku biashara hiyo, halafu anatukamata
Waafrika tu! Wapi Wazungu hapa bwana? Hiyo siyo ‘Fair Play’ ni Unfair kabisa,
Noma msikaji!!
(minong’ono na
miguno inasikika mahakamani)
OCAMPO: Waheshimiwa Jopo la Majaji,
mshitakiwa athibitishe kauli yake kama ICC inawashitaki Waafrika tu,na aslani
hakuna Mzungu hata mmoja! Hiki siyo chombo cha Umoja wa Mataifa(UN) na nchi 54
za Afrika hazijaridhia Mahakama hii tukufu?
TAYLOR:
Hawa mabwana wanatutuma kazi,tunatesa raia,tunakwiba
rasilimali na fursa zao nyingi,ili Punda afe Mzigo ufike! Halafu baadaye
wakitosheka wanaanza kutuchonganisha na raia na maandamano kama walivyofanya
Libya,Misri kwa Mubarak,Tunisia kwa Ben Ali n.k Je huu ni uungwana Mheshimiwa?
Tunapora nchi zetu kwa ufisadi na kuleta mzigo halafu kisha wanatusaliti! Huu
siyo uungwana mheshimiwa!
JAJI: Hujaitajia
mahakama Waafrika wangapi wamekamatwa peke yao na kushitakiwa The Hague?
TAYLOR: Mimi
ningali Rais halali wa Liberia, huyo Hellen Johnson Sielief, wamemleta wao ili
atawale kisha mimi waninyonge! Wanasema hakuna ‘Impunity’ wakati Blair,Bush
wanavamia na kuua hakuna mashitaka! Mnataka nife kama Gaddafi na Saddam?
JAJI: Enhe, wewe
na wengine kina nani? Wataje mlioshirikiana kuua raia mkapora utajiri wa Afrika
na kuuficha Ulaya na Marekani.
TAYLOR: Simple,
Fodday Sankoh, Laurent Nkundabatware, Jean-Pierre Bemba, Laurent Gbagbo, hawa
‘Ocampo Six’ mmewaacha mkachagua ‘Ocampo Four’, halafu mnamtaka Omar Hassan Al
Bashir, Tomas Lubanga,Joseph Kony,Paschal Ntaganda.
JAJI:
Umemaliza?
TAYLOR: Mobutu,
Savimbi,mbona hamsemi mliwasaidia hawa kupora utajiri wa Afrika na kuuhamishia
Ulaya na Marekani sasa Afrika ni The Shame of poverty in Plentiful?
OCAMPO:
Mheshimiwa,huyu jamaa sijui hamnazo, au kachapa kilaji! Amesahau Slobodan
Milosevic wa Serbia naye alishakamatwa mwaka 2000? Atasemaje kwamba
tunawakamata Waafrika tu?
TAYLOR: Mimi siyo
mlevi,ninakupa ‘facts’ usianze chuki zenu hapa. Mimi ni Rais halali Liberia
wananchi wananipenda, Marekani wamenitumia nikapora almasi za damu na
kuwapelekea,sasa wanasema mimi
muuaji. Guns for
Diamond ningefanyaje miaka 11 bila kushirikiana nao? Wazungu, acheni kufikiri
Mwafrika zoba, hamnazo?
(kicheko mahakamani,
zinasikika kelele za mashabiki wake nje ya mahakama wakishangilia)
JAJI: Order! Hapa tuko mahakamani,hatupo baa!
Utulivu tafadhali! Enhe, Taylor endelea kuuliza swali kama unalo; lakini wewe
siyo among the wealthiest in the world?
TAYLOR:
Umbeya tu mheshimiwa. Hawa wanatuchonganisha na wananchi wetu halafu wanasanua
deal kwa mitandao yao kama weakleaks, wanachochea maandamano kwa facebook na
twitter
OCAMPO: Kwani Wazungu
hawakamatwi?
TAYLOR: Baada ya Adolf
Hittler baada ya Vita ya Pili ya dunia nani aliyehukumiwa Hague,kama siyo mimi
mnataka kunionea eti nifungwe miaka 80,sasa nina 64, ndiyo nini kama siyo
kuniziba mdomo nisiseme mlivyopora ALMASI ZA DAMU huko Kono, Sierra Leone? Eti
mnataka kunifunga Uingereza!!
JAJI: Hoja
yako ni ipi hapa?
TAYLOR:
Ukiacha wale NAZIS, hawa jamaa ni matapeli hawajamkamata Mzungu,
wanatukamata sisi Waafrika tu, wana ‘double standards’ mheshimiwa Jaji na mambo
haya hapa siyo kesi ni siasa tupu-This massive inequality can be traced back to
cold war politics!!Sikubaliani na ukoloni wa ICC,WALA hakuna human rights wala
transparency international wala nini!!
JAJI: Wakili wa
mshitakiwa una swali?
WAKILI: Taylor, kina
nani wengine wanaonewa na ICC?
Taylor: Hata
mashirika ya wakimbizi na mengine ya Umoja wa Mataifa Congo,Dafur, Sierra Leone
n.k wizi mtupu, dunia haina amani ni utapeli tu,vita wachochee wao,tushitakiwe
sisi akina Taylor, Mobutu Sseseseko,Jonas Savimbi, Bosco Ntaganda,Thomas
Lubanga,Jonas Kony,orodha ni ndefu mheshimiwa! Hawa wote husaidiwa na Wazungu
kuharibu amani,uchumi na usalama wa Afrika,halafu hugeuka chameleon?
(anainamisha kichwa
kuonesha ameridhika, anaketi)
JAJI: Badala
ya kukanusha mashitaka unalalamika sana kwamba umeonewa,kwamba ICC
inawaonea Waafrika tu. Mahakama imeona una hatia ya mashitaka yote thenashara!
Upande wa Mashitaka una hoja?
BREBDA HOLLIS:
Huyu jamaa afungwe miaka 80, ukijumlishe umri wake wa miaka
64 maana yake ni kwamba afie ‘nondo’ ama mangenge ili liwe fundisho kwa
‘masera’ wenzake wanaoua raia!
JAJI:
Hukumu KAMILI Mei 30 mwaka huu 2012.
ASKARI:
Kooooortiii!!
Mei 30, magazeti ya Tanzania yanaandika, “Taylor
anyeshewa mvua ya miaka 80 jela!” mara, ‘Taylor kunyea mtondoo!”
TAMATI
0786 324 074 ama
www.congesmrambatoday.com
UBAGUZI WA RANGI OLIMPICS
Mwaka 1936 Dikteta wa Ujerumani, Adolph Hitler, alikataa kutambua ushindi wa Mtu mweusi, Jesse Owens, aliyeshinda medali nne za dhahabu kwa dakika 45 tu, katika Mashindano ya Olimpiki ya Majira ya Kiangazi mjini Berlin .
Hitler,
alisema Jesse Owens(Mmarekani mweusi) alikuwa mnyama. Kulingana na
Hitler, haikuwa haki mnyama(Owens) kushindana na Binadamu(Mzungu) katika
mashindano yoyote! Binadamu hushindanishwa na binadamu na wanyama na
wanyama wenzao.
Viongozi
wetu wanaweza kujidai kusahau dharau za akina Hitler, wakadhani ubeberu
na unyang’au wa Wazungu umekoma. Wanafikiri ubaguzi wa rangi haupo.
Huku ni kujidanganya sana ...huyo Watson hajakurupuka, kasema
wanavyoamini wao.
Jumapili,
Julai 9, mwaka 2006. Italia ikapambana na Ufaransa katika Fainali ya
Kombe la Dunia, katika uwanja huohuo wa Berlin aliojenga Hitler miaka 70
iliyopita na kusimika hirizi ya unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya mtu
mweusi.
Marco
Materazzi wa Italia akamtukana Zenedine Zidane ‘Zizou’ matusi
yanayokaribiana na ubaguzi wa rangi.
Zizou, akamtwanga Materazzi na kumwangusha chini…kapewa kadi nyekundu
na mwamuzi na kutolewa nje. Alizua mjadala mkali wa kisiasa.
Zizou ni raia wa Ufaransa, mwenye asili ya Algeria , Afrika.
Zizou ni raia wa Ufaransa, mwenye asili ya Algeria , Afrika.
Siyo
Berlin tu ilikozikwa hirizi ya ubaguzi wa rangi; hata Uhispania akiana
Samuel Eto’o Fils hudhaniwa nyani. Hata Seneta wa Italia, Roberto
Calderoli anaamini watu weusi ni mkosi, tena si binadamu wenye akili
kama Mzungu.
Seneta
Calderoli, alisema Timu ya Taifa ya Ufaransa iliyoundwa na weusi wengi,
akina Eric Abidal, Claud Makelele, Thierry Henry, William Gallas, Louis
Saha, Patrick
Vieira, Djibril Cisse , Zizou na wengineo ndio walioitia mkosi Ufaransa
ikashindwa na Italia mwaka 2006.Laiti ingeundwa na binadamu, Wazungu!
Kujaza weusi wengi katika kikosi chake kukasemwa kuwa ni sababu ya
Ufaransa kushindwa mjini Berlin hata miaka 70 baada ya Hitler kuujenga
uwanja huo!
Haya
yalishasemwa na akina Ian Douglas Smith wa Rhodesia ya zamani sasa
Zimbabwe ya Mugabe, Kaburu Balthazar Johannes Voster na P.W. Botha wa
Afrika Kusini. Wanafunzi 250 wa Kiafrika waliouawa na polisi wa Makaburu
mwaka 1976 kwa sababu ya kukataa kuimba Kiafrikana(lugha ya binadamu)
wamesahaulika akilini mwa vigogo wetu?
Naam,
hawa ndio akina James Watson leo wanaosema Mwafrika hana akili; na
huwezi kumfanya daraja moja na Mzungu!
Wazungu wengi wanaamini Mwafrika nyani; hayawani. Tunadhihirisha hili kwa kujikomba na kuwapa rasilimali zetu ili wauze na kutugawia kidogo.
Wazungu wengi wanaamini Mwafrika nyani; hayawani. Tunadhihirisha hili kwa kujikomba na kuwapa rasilimali zetu ili wauze na kutugawia kidogo.
Rasilimali
zetu zinajenga kwao, wanakula minofu sisi mifupa halafu tunampigia
magoti Malkia, akina Gordon Brown na akina Bush. Tunakosa cha kwetu.
Tunajidai kusahau kuwa Wazungu ni walewale jana hata leo. Wao wanaona ni daraja la kwanza sisi mwisho; chetu chao, chao si chetu…kwanini hatung’amui?
Tunajidai kusahau kuwa Wazungu ni walewale jana hata leo. Wao wanaona ni daraja la kwanza sisi mwisho; chetu chao, chao si chetu…kwanini hatung’amui?
Enzi
zile tulisema tumeonewa kiasi cha kutosha, tumedharauliwa sasa tunataka
mapinduzi. Mbona mapinduzi hayaonekani, isipokuwa tunarejea utumwani?
Itaenelea tolea
lijalo.
0786 324 074
Looking for last minute shopping deals? Find them fast with Yahoo! Search.
Kuelekea Olimpic London, 2012
MASHINDANO
ya Olimpiki ya majira ya kiangazi yanayotarajiwa kufanyika London,
mwezi Julai, mwaka huu, yalianza zamani sana, karne tano kabla ya
Kristo.
Yale mashindano ya Olimpiki tunayoshuhudia siku hizi, yalianza Athens huko Ugiriki mwaka 1896
.Hufanyika kila baada ya miaka minne, wakati leo wanariadha wanaoshiriki wameongezeka kutoka nchi 13 mwaka 476 BC hadi zaidi ya 200 hii leo.
.Hufanyika kila baada ya miaka minne, wakati leo wanariadha wanaoshiriki wameongezeka kutoka nchi 13 mwaka 476 BC hadi zaidi ya 200 hii leo.
Alama ya mashindano haya ya Olimpiki ni miduara mitano iliyoungana;
inayowakilisha urafiki na udugu
wa kimichezo wa watu wa mabara yote.
Miduara hii pia huwakilisha mabara natano ya kijiografia, ambayo ni Afrika, Asia, Ulaya, Australia na Amerika.
Miduara hii pia huwakilisha mabara natano ya kijiografia, ambayo ni Afrika, Asia, Ulaya, Australia na Amerika.
Kila
mduara una rangi tofauti kulingana na rangi ya watu wake. Miduara hii
ina rangi nyeusi(Afrika), bluu(Ulaya), njano(Asia),kijani( Australia )
na Amerika wanawakilishwa na rangi nyekundu.
Miduara hii mitano huwa katika bendera nyeupe ya Olimpiki.
Madhumuni
ya ushiriki wa mashindano haya si kushinda medali peke yake, bali ni
kushiriki. Maisha ya kawaida ya mwanadamu si shangwe ya ushindi; ni
kupambana.Yaani, kitu muhimu si kushinda bali ni kupambana
kwa ari kubwa.
Kauli
mbiu ya mashindano ya Olimpiki ni “Citius, Altius, na Fortius” ambayo
ni maneno ya Kilatini, maana yake, ‘Kupaa haraka, Juu na kwa Nguvu’.
Afrika haina budi kushinda mafashisti mamboleo na kupaa juu kwa haraka
na nguvu katika nyanja zote za maendeleo.
Kiapo
cha kila mwanamichezo anayeshiriki kushindana katika mashindano ya
Olimpiki, ni kushindana kwa heshima kulingana na sheria na kanuni
zinazoongoza mashindano; kuwa na uanamichezo na utukufu wa kweli wa
mashindano, bila kusahau kuipa heshima timu ya kila mwanamichezo
anayehusika.
Mwenge wa Olimpiki uliotua Dar es salaam mwaka 2008,
ukishuka kutoka dege kubwa
la rangi ya ‘Pinki’ hivi, ulianza kukimbizwa mwaka 1936. Tayari mwenge huu umewashwa huko Athens.
.Zamani, mwenge huo uliwashwa kwa miali ya jua huko Olimpia(asili ya mashindano yenyewe), huko Ugiriki. Badaye, mwenge ulichukuliwa kupelekwa uwanja wa mashindano kwa meli au ndege.
.Zamani, mwenge huo uliwashwa kwa miali ya jua huko Olimpia(asili ya mashindano yenyewe), huko Ugiriki. Badaye, mwenge ulichukuliwa kupelekwa uwanja wa mashindano kwa meli au ndege.
Dar
es salaam mwenge huo ulikimbizwa kwa amani bila kitisho cha
waandamanaji, ama al-Qaeda. Mashindano ya kisasa ya Olimpiki yalianza
Athens mji mkuu wa Ugiriki mwaka 1896; miaka minne baadaye yalifanyika
jijini Paris.
Mwaka 1904 mashindano haya yalifanyika St. Louis , Marekani. Mwaka 1906 yalifanyika Athens , lakini hayakutambuliwa na Kamati ya Olimpiki ya
Kimataifa(IOC). Mwaka 1908 yalifanyika mjini London kwa mara ya kwanza.
Mwaka
1912 mashindano ya Olimpiki yalifanyika Stockholm nchini Sweden ,
1920(Antwerp-Ubelgiji);
1924(Paris-Ufaransa);1928(Amsterdam-Uholanzi);1932(Los
Angeles-Marekani);1936(Berlin-Ujerumani ya enzi ya Hitler);1948(London-
Uingereza);1952(Helsinki-Finland);mwaka 1956 yalifanyika
Melbourne-Australia, 1960 yalifanyika Rome mji mkuu wa Italia.
Mwaka
1964 mashindano yalifanyika Tokyo , Japan , wakati yale ya 1968
yalifanyika Mexico City nchini
Mexico . Mwaka 1972 mashindano yalifanyika jijini Munich , Ujerumani
Magharibi wakati huo; yaliacha alama ya kitisho cha magaidi, kama ilivyo
zama hizi za al-Qaeda.
Septemba
5, mwaka huo wa 1972 magaidi wanane wa Kipalestina kutoka kundi
liitwalo, Black Septemba, walidhamiria kulipa kisasi dhidi ya adui zao
Waisraeli.
Walijipenyeza katika
mabweni ya wanariadha katika kijiji cha Olimpiki(wakati wa ufunguzi wa
mashindano); wakiwa wamevalia viruwiruwi(mask) nyusoni mwao,
waliwatwanga risasi wanariadha wawili wa Israeli, kabla ya kuwateka
nyara wengine tisa.
Magaidi
hao wa Black September walikuwa wakiwadai Waisraeli kuwaachia huru
mateka wanamgambo 200 wa Kipalestina waliokuwa wamekamatwa
na majeshi ya Israeli wakati huo.
Black
September, wakaitaka serikali ya Ujerumani Magharibi kuwasafirisha kwa
helkopta wao na mateka wao hadi katika uwanja wa ndege ulio nje ya
Munich.
Waliitaka serikali baadaye iwapeleke katika nchi yoyote ya Kiarabu, iliyokuwa ikiunga mkono Wapalestina kujitawala katika ardhi yao .
Waliitaka serikali baadaye iwapeleke katika nchi yoyote ya Kiarabu, iliyokuwa ikiunga mkono Wapalestina kujitawala katika ardhi yao .
Naam.Wapalestina
waliwateka nyara wanariadha wa Uzayuni kama kisasi cha kutaka mateka wa
Kiarabu kuachiliwa huru; wakijua wakati huo wa michezo ya Olimpiki,
suala lao lingetangazwa sana na vyombo vyote vya Habari vya dunia nzima.
Baada ya majadiliano makali Wajerumani waliamua kuwachukua magaidi wale(nisihukumiwe kuwaita hivi hata
kama ni wanaharakati) na mateka wao hadi katika uwanja wa Furstenfeldbruck.
Vikosi
vya usalama vya Ujerumani vilifanya ujanja wa hali ya juu, vikauzingira
uwanja huo na kuwasubiri. Walipotua tu uwanjani, kabla ya kushuka
ndegeni, mapambano ya silaha yakaanza.
Magaidi watano wa Kiarabu waliuliwa, wengine watatu wakatiwa mbaroni.
Hata hivyo, walikwisha waua wale wanariadha wote tisa wa Israeli,
waliotekwa nyara mabwenini, kule Munich katika kijiji cha Olimpiki.
Tukio
hilo liliidhalilisha sana serikali ya Ujerumani Magharibi, baadhi ya
mataifa yakatishia
kususia mashindano. Huu ni wakati gaidi la kale sana la kimataifa,
Carlos The Jackal, linalotumikia kifungo cha maisha Ufaransa,
lilipotuhumiwa kupanga mashambulizi hayo.
Sakata hilo lilipita, mashindano hayo ya Munich yakaendelea kama ilivyopangwa.
Mwaka 1976 mashindano ya Olimpiki yalifanyika Montreal Alberta Canada .
Mwaka 1976 mashindano ya Olimpiki yalifanyika Montreal Alberta Canada .
Mwaka
1980 yalifanyika Moscow Urusi ya zamani, ambako Tanzania iliwakilishwa
na mabalozi wengi wakiwemo akina Luliga Musa, Mwinga Mwanjala n.k
Mwaka
1984 yalifanyika Los Angeles, Marekani. Mwaka 1988(Seoul-Korea Kusini);
1992(Barcelona-Uhispania); mwaka 1996(Atlanta-Marekani);mwaka
2000(Sydney-Australia); mwaka 2004 yalifanyika tena Athens, Ugiriki
yalikozaliwa; lakini chini ya ulinzi mkali sana, kufuatia
kitisho cha magaidi wa al-Qaeda.
Mwaka
huu wa 2008 mashindano haya yalifanyika Beijing nchini Uchina, huku
kukiwa na kitisho cha matetemeko na magaidi wa al-Qaeda na wa Tibet.
Mwaka 2012 mashindano haya yatafanyika mjini London. Hata huko London kitisho cha magaidi kingalipo…Afrika haijawahi kuandaa mashindano haya adhimu duniani. Kwa nini na kwa sababu gani? Kama ni suala la usalama, mbona hata Munich magaidi walitamba? Afrika itaandaa mashindano haya lini?
Mwaka 2012 mashindano haya yatafanyika mjini London. Hata huko London kitisho cha magaidi kingalipo…Afrika haijawahi kuandaa mashindano haya adhimu duniani. Kwa nini na kwa sababu gani? Kama ni suala la usalama, mbona hata Munich magaidi walitamba? Afrika itaandaa mashindano haya lini?
Zamani, mabingwa wa Olimpiki walituzwa taji ya majani ya mizeituni
.Leo, mashindano haya huandamana na tuzo za kitajiri. Mashindano ya sasa yanapoteza maudhui ya Olimpiki, kama tulivyokwishakuona. Uzalendo unapotea, Olimpiki ni mnada tu wa kusaka utajiri.Mabingwa wa Afrika hurubuniwa kwa rushwa na Wazungu!
.Leo, mashindano haya huandamana na tuzo za kitajiri. Mashindano ya sasa yanapoteza maudhui ya Olimpiki, kama tulivyokwishakuona. Uzalendo unapotea, Olimpiki ni mnada tu wa kusaka utajiri.Mabingwa wa Afrika hurubuniwa kwa rushwa na Wazungu!
Mraba huu unawakumbuka mabingwa wa Olimpiki, hususan askari shujaa sana wa Kigiriki aitwaye, Pheidipides.
Huyu, alitimka umbali wa mali kama 29 hivi, kutoka mahali paitwapo Marathon kwenda mjini Athens.
Huyu, alitimka umbali wa mali kama 29 hivi, kutoka mahali paitwapo Marathon kwenda mjini Athens.
Mwaka
490 BC Majeshi ya Waperizi(Iran ya leo) yalikwenda mahali paitwapo
Marathon na kutaka kuivamia Ugiriki. Walikuwa na majeshi makubwa sana,
kwa bahati jeshi dogo la Ugiriki likafanikiwa kuwapiga na kuwafukuza
kabisa.
Jemadari
wa Jeshi la Ugiriki akamtuma Pheidipides kwenda mjini Athene(wakati
huo) kwenda kupeleka Habari njema za ushindi.Ulikuwa wakati wa Mfalme
Dario wa Umedi-Soma kitabu cha Danieli sura 2-3
Basi,
alipofika mjini Athens, sokoni kwenye mkusanyiko wa watu wengi,
alifanikiwa kusema kwa shida sana kwamba jeshi lao lilikuwa limelishinda
jeshi la wavamizi.
Alipomaliza kusema, akaanguka mchangani na kufa!
Mbio za Marathon zikaanzishwa kwa lengo la kumkumbuka shujaa, Pheidipides.Hizo zilikuwa enzi za Mfalme Dario anayesimuliwa Habari zake katika Biblia, katika Danieli.
Mbio za Marathon zikaanzishwa kwa lengo la kumkumbuka shujaa, Pheidipides.Hizo zilikuwa enzi za Mfalme Dario anayesimuliwa Habari zake katika Biblia, katika Danieli.
Utaona kuwa neno Olimpiki limetokana na Olympia, neno
Marathon ni mahali alipoanza kutimka shujaa huyo kwenda Athens.
Mabingwa
wengine wa Marathon ni pamoja na Joan Benuit wa Marekani mwaka
1984,Rosa Mota wa Ureno(1988); Valentina Yegorova(1996), Fatuma Roba wa
Ethiopia(1996) na Naoko Takahashi wa Japan mwaka 2000.
Afrika inang’ara ipasavyo katika bendera nyeupe ya OIlimpiki. Mabingwa wa Marathon wa Afrika ni pamoja na Abebe
Bikila wa Ethiopia(1960,64); Marmo Wolde wa Ehiopia(1968);Josia
Thugwane wa Afrika Kusini(1996); na Gezahgne Abera wa Ethiopia mwaka
2000. Rekodi za 2004 hazikuwekwa.
Waama, mraba huu unamkumbuka sana kaka yetu, Jesse Owens,
Mmarekani mwenye asili ya Afrika
aliyeshinda medali nne za dhahabu katika mashindano ya Olimpiki ya mwaka 1936 mjini Berlin.
Jesse Owens, alitimka kwa dakika 45 akawa na medali hizo nne, pamoja
na kushinda mita 200.Aliyekuwa mgeni wa heshima wa mashindano hayo,
Dikteta Adolf Hitler, aliamua kususa kutazama mtu mweusi akishinda
Aliondoka
uwanjani hapo na kusema kwamba hakuwa tayari kuona ‘mnyama’ Owens,
akiwanyanyasa binadamu(Wazungu).Wangalipo wenye mawazo kama Hitler hata
sasa, wengine wamezaliwa Afrika.
Hitler,
ndiye mjenzi wa uwanja huo wa Berlin ilikokuja kuchezwa fainali ya
Kombe la Dunia mwaka 2006(miaka 70 baadaye) kati ya Ufaransa na
Italia.
Ufaransa iliyokuwa na Weusi wengi katika kikosi chake, ilitukanwa kwamba ilishindwa kwa sababu ya hao Weusi!
Ufaransa iliyokuwa na Weusi wengi katika kikosi chake, ilitukanwa kwamba ilishindwa kwa sababu ya hao Weusi!
Tena,
Michael Materrazi alimtukana Zenedine Zidane “Zizou” kwamba alikuwa
gaidi, kutokana na asili yake ya Algeria.Zidane alimtwanga kichwa
kikali, akatolewa nje kwa kadi nyekundu! Naam, mzimu wa unyanyapaa na ubaguzi wa rangi ungalipo mjini Berlin hata baada ya Dikteta, Fashisti Adolf Hitler kujiua.
Mabingwa
wengine wa Olimpiki kutoka Afrika ni pamoja na Paul Erang wa Kenya
aliyeshinda mita 800 mwaka 1988, William Tanui pia wa Kenya(1992). Mwaka
2000 Noah Kiprono Ngenyi wa Kenya alishinda mita 1,500, Mirutus Yifter
wa Ethiopia alishinda mita 5000 mwaka 1980,
Said Aouita wa Morocco
alishinda 1984 hizo mita 5000, Venuste Niyongabo wa Burundi alishinda
1996 na Milton Wolde wa Ethiopia aliwika katika mashindano hayo mwaka
2000.
Katika
mita 10,000 Naftali Temu wa Kenya alishinda 1968, Miruts Yifter wa
Ethiopia akashinda mwaka 1980. Haile Gebrselassie wa Ethiopia aliwika
mita 10,000 mwaka 1996 na 2000.Nigeria ya akina Nwankwo Kanu ilipata
kushinda kombe la Olimpiki la soka, kwa kuwachapa vigogo kama Brazil na
Argentina. Afrika, ni kichwa si mkia katika ramani ya Olimpiki.
Mabingwa
wengine wa Olimpiki ni Amos Biwott wa Kenya mwaka 1968, Kipchoge Keino
pia wa Kenya mwaka 1972,Julius Korir wa Kenya mwaka 1984,Julius Kariuki
wa Kenya mwaka 1988, Mathew Birir wa Nyayo mwaka 1996, Joseph Kater
pia wa Nyayo mwaka 1996 na Robert
Kosgei mwaka 1996. Maria Mutola wa Musumbiji alishinda mita 800 mwaka
2000. Afrika ni bara la mabingwa wenye ari ya kushinda.
Tanzania imewahi kushiriki mashindano mengi ya kidunia; inajivunia rekodi za mabingwa wake kama Filbert Bayi, Suleiman Mujaya Nyambui, Juma Ikangaa na wengine wengi.
Afrika Kusini iliaandaa Kombe la Dunia mwaka 2010.
Baadaye Afrika itataka kuandaa mashindano makubwa ya kimataifa, licha ya kampeni chafu sana za Wazungu, kwamba Afrika hakuna usalama, hususan zama hizi za magaidi.
Mbona Black September waliteka wanariadha Munich ? Watasema, Afrika kuna miundo mbinu dhalili n.k
Baadaye Afrika itataka kuandaa mashindano makubwa ya kimataifa, licha ya kampeni chafu sana za Wazungu, kwamba Afrika hakuna usalama, hususan zama hizi za magaidi.
Mbona Black September waliteka wanariadha Munich ? Watasema, Afrika kuna miundo mbinu dhalili n.k
Mwisho,
Afrika si mshiriki bali
mshindani wa dhati kama tulivyoona. Mtu mweusi si mtumwa, bali
‘championi’ katika nyanja anuwai kama tulivyoona akina Jesse Owens.
Wapo mabingwa wengine weusi katika nyanja tofauti za maisha-Afrika inastahili nafasi sawa.
Wapo mabingwa wengine weusi katika nyanja tofauti za maisha-Afrika inastahili nafasi sawa.
Shime, Waafrika wenye maradhi ya kutokujiamini ama kujidharau(inferiority complex) waone kuwa mtu Mweusi yuko juu sana .
Akina Hitler wa kizazi hiki wazomewe kwa sababu Afrika inakwea juu sana . Afrika, “Citius, Altius….Afrika Fortius”, ina kwea Haraka, Juu na kwa Nguvu. Afrika kilele cha utukufu.
Mwaka 2008 mashindano ya Olimpiki yalifanyika Uchina, mwaka huu 2012 yatafanyika London,siku chache zijazo kuanzia sasa. Je kutatokea ubaguzi wa rangi wa kuwabagua akina Caster Semenya?
Akina Hitler wa kizazi hiki wazomewe kwa sababu Afrika inakwea juu sana . Afrika, “Citius, Altius….Afrika Fortius”, ina kwea Haraka, Juu na kwa Nguvu. Afrika kilele cha utukufu.
Mwaka 2008 mashindano ya Olimpiki yalifanyika Uchina, mwaka huu 2012 yatafanyika London,siku chache zijazo kuanzia sasa. Je kutatokea ubaguzi wa rangi wa kuwabagua akina Caster Semenya?
0786 324 074
Tuesday, May 29, 2012
SUMATRA DAR NOMA!!
*Abiria wahofia kitisho cha Al
Shabaab
Na Conges
Mramba, Nansio
MAMLAKA ya
Udhibiti Usafiri Nchi Kavu na Majini(SUMATRA) inadaiwa kushindwa kusimamia
ukaguzi wa vyombo vya majini Ziwa Victoria, hivyo kusababisha hofu ya kuweza
kutokea ajali.
“Maofisa wa SUMATRA wanapotoka Dar es salaam
kuja Ziwa Victoria kuendesha zoezi la ukaguzi,wanawashurutisha wamiliki wa
vyombo vya majini kuwalipia gharama za chakula na malazi hotelini”, Gazeti hili
limedokezwa.
Nahodha wa
Meli moja ya kampuni binafsi, ameliambia Gazeti hili kwamba,kitendo cha maofisa
wa SUMATRA kupewa hisani ya gharama za chakula,malazi na maburudisho wakati
wanapofanya ukaguzi wa vyombo vya usafiri majini Ziwa Victoria,huhafifisha
ubora wa vyombo husika,na changamoto kwa manahodha na mabaharia.
“SUMATRA,
wanapofika Mwanza,toka Dar es salaam, wanakula na kulala kwa gharama za
wamiliki wa meli na boti hapa Ziwa Victoria, sasa watakagua nini kama siyo
kulipa fadhila kwa yale waliyotendewa na wamiliki wa meli ama boti?” Amehoji
Nahodha wa Meli moja kwa masharti ya kutotajwa jina wakati wa mahojiano na
gazeti hili.
Tumemtafuta
Ofisa Uhusiano wa SUMATRA, David Mziray, kwa takriban juma zima,ili
kujibu tuhuma hizo, lakini simu yake ya mkononi ama iliita pasipo majibu, ama
ilikuwa imefungwa.
Hata hivyo, Ofisa Mfawidhi wa SUMATRA,Mkoani
Mwanza, Alfred Wariana, amesema maofisa wa SUMATRA kutoka Dar es Salaam,hufika
Mwanza kufanya ukaguzi wa kila mwaka,na hulipiwa gharama za usafiri,malazi na
chakula na Mamlaka, na wala siyo wamiliki wa vyombo vya usafirishaji Ziwa
Victoria.
Jumapili, Mei 27 mwaka huu,mwandishi wa
makala haya alisafiri kutoka Jijini Mwanza,kwenda Nansio,Ukerewe kwa Meli ya
Mv. Samar II inayomilikiwa na Kampuni na Kampuni ya Samar Filling Station,ya
Mwanza.
Hii ni meli
iyojengwa mwaka 2009 na Kampuni ya Songoro Marine Transport pia Jijini Mwanza,kama
meli ya mizigo. Ilikuwa ikifanya safari zake kati ya Mwanza na Uganda.
Meli hiyo ilibadilishwa matumizi mwaka huu,
ikawekewa viti na kuanza kusafirisha abiria kutoka Mwanza hadi Nansio,Ukerewe.
Uwezo wake ni kuchukua abiria 248 na tani kati ya 101 na 138 za mizigo.
Nilimuuliza Nahodha wa meli hii,Kapteni Adam
Andrew Alex, “Meli ina vifaa vya uokozi kwa kiwango gani?”
“Ina
maboya(life rings) 60 na life jackets 350.Tuna mashua moja na vifaa 10 vya
kuzimia moto”, Kapteni Alex alisema.
Kutoka Jijini
Mwanza hadi Nansio, mji mkuu wa wilaya ya Ukerewe yenye visiwa 27 na vingine 11
visivyokaliwa na watu kuna umbali wa mali 29 za majini.
Kapt.Alex
anasema alihitimu katika Chuo cha Mabaharia, Dar es salaam Maritime Insitute,
na alikuwa na uzoefu wa mwaka mmoja kazini. Akasema meli yake ilikuwa na
mabaharia tisa wenye uzoefu wa kati ya miezi sita na mwaka mmoja kazini.
Akizungumzia mazingira ya kazi, amesema
mikataba ya ajira katika vyombo hivi vya binafsi haiendani na kazi, “Hakuna
hata malipo ya muda wa ziada wa kazi(over time),wala hakuna usafiri baada ya
kazi”, Kapt. Alex amedai.
Eferi Bulongo(75) ni miongoni mwa abiria
waliosafiri na meli hiyo, Samar II kwenda Nansio. Nilimuuliza, “Una maoni gani
kuhusu usafiri Ziwa Victoria?”
“Sipendi kusafiri kwa meli binafsi;zinasumbua,
ratiba ya safari haieleweki,ni namna wanavyojisikia wao, na melini hakuna
mahitaji ya lazima ya kuaminika kama chakula na vinywaji;kuna chai”, Bulongo
amedai.
Amesema, meli za Mashirika ya Umma,kama Marine
Services Company(MSC) ni bora kabisa, ratiba ya safari huzingatiwa.
“Hizi meli
za MSC zinahujumiwa na baadhi ya wafanyakazi wake.Labda wanapewa rushwa na wamiliki
wa meli za binafsi ili meli za MSC ziache kufanya huduma ili wafanye biashara, abiria wengi hawazipendi
hizi meli binafsi”, Bulongo amesisitiza, huku akihoji, “Kwanini Meli za MSC
ndizo ziharibike kila kunapokucha? Mv.Clarias haijafanya kazi kwa zaidi ya
miezi minne; sasa wamesikia Bunge la Bajeti karibu kuanza, ndiyo tunasikia
itaanza kati ya kesho(Mei 27) na kesho”, anasema Bulongo.
Nikampigia simu Kaimu Meneja Mkuu wa
MSC,Projest Kaija kujibu tuhuma hizo.
“Leo,
Jumapili Mei 27, tunaifanyia majaribio Mv.Clarias. Baada ya siku chache itaanza
safari zake kwenda Ukerewe”, Kaija anasema.
Anakanusha kuwepo kwa tuhuma zenye lengo la
kuhujumu Kampuni ya umma kwa nia ya kuwanufaisha wenye meli binafsi.
“Wafanyakazi
wa MSC wanawezaje kuhujumu kampuni inayowapa mshahara?” Anahoji,huku
akisisitiza kuwa tuhuma hizo zitachunguzwa,kwa kuwa uongozi wa kampuni hiyo ya
umma umebadilishwa siku chache zilizopita; kampuni inafanya matengenezo(reform)
anuwai.
Nikampigia simu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Everest
Ndikilo,ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa, kumsaili:
“Kwanini
abiria wanapopanda katika vyombo vya majini Ziwa Victoria hawakaguliwi, ili
kubaini uwezekano wa kuwepo kwa magaidi kama Al-Qaeda na Al-Shabaab, wanaotishia maisha ya
watu nchi jirani ya Kenya?”
Magaidi
waliwahi kuteka nyara ndege ya Air Tanzania(ATC)mwaka 1988 , yenye maandishi
ubavuni, ‘Tango Charlie” wakati ikipaa kutoka uwanja wa ndege wa
Mwanza,ikalazimishwa kwenda Jijini London ambako hatimaye jumla ya wateka nyara
watano raia wa Tanzania walihukumiwa kifungo cha kati ya miaka mitatu na mitano
jela,Jijini London.
“Ulinzi na Usalama ni Ajenda ya kudumu na siyo majini tu, hata kwenye
majengo,mahoteli na makazi ya raia”, Mkuu wa Mkoa Ndikilo anasema.
Kuhusu
maofisa wa SUMATRA,kutoka Dar es Salaam kulazimisha kulipiwa gharama za ukaguzi
na wamiliki wa vyombo ziwa Victoria, Ndikilo akasema, “Kama jambo hilo
lipo,basi ni tatizo kubwa,nitafuatilia ili hili likemewe”, Ndikilo akasema.
Gazeti moja litolewalo kila siku hapa nchini
kwa lugha ya Kiingereza, katika toleo lake la Mei 23 mwaka huu lilisema
kwamba,mwaka 1996 Mv.Bukoba ilipozama na kupoteza maisha ya abiria wake
takriban 1,000; miongoni mwao alikuwemo Abu Ubaidah al-Banshiri, ambeye alikuwa
nambari mbili wa kundi la kigaidi la Al-Qaeda.
Naam, kundi
hili la AlQaeda, lilianzishwa na Osama bin Muhammad bin Awad bin
Laden,Feburuari mwaka 1998 kwa jina la WORLD ISLAMIC FRONT,ili kuhujumu maslahi
ya Marekani na washirika wake mahali popote duniani,hata kama ni Ziwa Victoria,
Osama
alikuwa mshirika wa Marekani na shirika lao la Ujasusi(CIA) mwaka 1979 wakati
majeshi ya Warusi walipovamia Afghanistan.CIA walimfadhili mabilioni ya Dola za
Marekani kuanzisha kambi ya mafunzo ya Makhtab al-Khidamat(MAK).
Lakini,baada
ya Urusi kuondoka Kabul mwaka 1989, Osama akageuka kuwa adui wa MAREKANI na
washirika wao, akaungana na Taliban na Mullah Muhammad Omar kuendesha ‘Jihad’
dhidi ya Marekani na washirika.
Nataka
kusema kwamba,mwaka 1996 wakati Mv.Bukoba inazama ziwa Victoria, al-Qaeda
tayari walikuwepo,na wangeweza kufanya madhara hapa nchini kwa mashambulizi
yenye kulenga shabaha Wamarekani ama maslahi yao hapa Tanzania.
Hata hivyo,
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Everest Ndikilo, amesema serikali imeimarisha ulinzi
katika Ziwa Victoria,kwa kuwa zipo boti za doria zinazozunguka ziwani, na raia
wanapaswa kutoa taarifa pindi wanapoona mienendo yenye mashaka ama kitisho cha
magaidi wa al-Qaeda ama al-Shabaab!
0786 324 074
MAGAIDI HATARINI KUVAMIA ZIWA VICTORIA
Mwangwi wa A-Shabaab Nairobi, watikisa wasafiri Ziwa Victoria
*Mabadiliko
ya Tabianchi yatishia meli kuparamia miamba na kuzama
Na Conges Mramba, Mwanza
MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari(TPA),
imewapandisha kizimbani wamiliki wa meli binafsi, kwani wanazuia Mamlaka hiyo
kusimamia usalama wa abiria na mizigo, hata wakati huu wa kitisho cha magaidi
wa Al-Shabaab,Afrika Mashariki.
Mkuu wa Bandari(Port Master)Mwanza, John
Mutalemwa, katika mahojiano maalum na gazeti hili juzi, alisema wamiliki hao wa
Bandari binafsi wanashindana na Sheria Na. 17(Tanzania Port Act) ya mwaka 2004.
Sheria hiyo
inaipa TPA nguvu ya kusimamia bandari
zote, zikiwemo za watu binafsi,ili kukagua usalama wa abiria na mizigo,kabla na
baada ya safari.
“Sheria inatupa Mamlaka ya kusimamia bandari
zote zikiwemo bubu, tukague na kujua
mizigo kiasi gani inasafirishwa; tunatakiwa kutazama abiria ikiwa wanalingana
na uwezo wa meli au boti,kulinganisha na uwezo wa chombo chenyewe, halafu tunatoa, “Port Clearance”
kabla ya meli kuanza safari”, Mutalemwa alisema.
Kwa mujibu
wa Mutalemwa, vipo vyombo vya usafiri majini,huchukua abiria na mizigo kuoita
uwezo. Hii ni kazi ya TPA kufanya ukaguzi makini,ili kuondokana na Ajali Ziwa
Victoria.
“Bandari ni mpaka wa nchi. Lazima tusimamie
hali ya usalama, meli inaweza kuleta Al-Qaeda ama Al-Shabaab, nap engine inaweza
kuingiza nchini silaha kutoka nchi za vita na migogoro. Eti wanakataa
tusiwasimamie…tumewafungulia kesi mahakamani”,Mutalemwa ameliambia gazeti hili
katika mahojiano Maalum ofisini kwake juzi.
Meli za mizigo za Jijini Mwanza, hufanya
safari zake hadi Port Bell, Uganda,na Kisumu nchini Kenya, ambako sasa magaidi
wa Al-Shabaab wanasaidia kuzimu kupanua kinywa chake.
Aidha, Mkuu huyo wa Bandari Mwanza amesema
nchi za Maziwa Makuu kama Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, na Burundi hazina
amani, na Kenya hamkani si shwari,kufuatia kitisho cha Al-Shabaab, wanaopinga
majeshi ya nchi hiyo kuingia Somalia kuwafulusha magaidi hao.
Kufuatia
hali tete ya usalama nchi jirani, Mutalemwa amesema lazima Mamlaka yake kuwa
macho na usalama wa abiria na mali zao dhidi ya hujuma za magaidi, wanaoweza
kupata upenyo wakaingiza silaha nchini kupitia Ziwa Victoria.
Mamlaka ya Bandari humiliki bandari za Mwanza
Kaskazini na Kusini,Nansio Ukerewe,Kemondo Bay na Musoma.
Vituo
vingine vidogo vinavyomilikiwa na TPA ni Maisome,Nkome,Bukondo,Kahunda,Miharaba,Kome,Buchosa,Solima,Karumo,Chato
na Nyamirembe(Kagera) na Kinesi mkoani Mara.
Bandari ya Mwanza ni kiungo muhimu kwa nchi za
Maziwa Makuu,hususan Uganda na Kenya,na
huchangia kwa kiwango kikubwa kukua kwa shughuli za uchumi,hata katika nchi
wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki(EAC).
Ripoti ya Malka hii iliyotolewa kwa Kamati ya
Bunge ya Miundombinu(nakala tunayo), inasema bandari ya Mwanza ingeweza
kusafirisha abiria milioni moja kwa mwaka.
Ingeweza kusafirisha tani mamilioni za moja za mizigo,kama Reli ya Kati ingekuwa
inafanya kazi kwa ufanisi. Hili ni eneo muhimu kwa ukuaji wa uchumi wan chi,lakini
kinyume chake ni hasara kila upande.
“Huduma hafifu za Reli zimesababisha shehena
ya kahawa kutoka Uganda na hata Bukoba,kubadili njia(route) na kupitia Bandari
ya Mombasa,Kenya “, Ripoti hii inasema.
Kufuatia huduma duni za Shirika la Reli,
Bandari za Mwanza ziko taaban,kwa sababu ya kupungukiwa mapato, zinaendeshwa
bila faida.
Kulingana na Ripoti hii kwa Kamati ya Bunge ya
Miundombinu,katika kipindi cha miaka mitano,kuanzia 2006/2007 hadi 2010/2011,
mizigo imepungua katika Bandari za Mwanza kutoka tani 480,568 hadi 248,860
mwaka 2011.
Utendaji
mbovu wa lililokuwa Shirika la Reli(TRL) ulisababisha treni iliyokuwa
ikisafirisha abiria na mizigo kati ya Mwanza na Bandari ya Dar es salaam
kusimamishwa.Hali hii husababishwa abiria na mizigo kubadili njia na kukosesha
mapato bandari za Mwanza.
Wafanyabiashara wa Uganda wanasafirisha bidhaa
zao kupitia bandari ya Mombasa,nchini Kenya.Shehena ya kahawa kutoka Uganda
iliyokuwa ikipitia bandari za Mwanza, inapitia Mombasa na hivyo kupunguza
kiwango cha mizigo kutoka tani 250,000 mwaka 2007 hadi tani 100,000 mwaka
2009/2010.
Kufuatia madudu ya TRL, hata abiria wamepungua
katika bandari za Mwanza kutoka abiria 891,634 mwaka 2007 hadi abiria
593,342.Huu ni upungufu wa asilimia 6.3 unaoikosesha nchi mapato na fursa za
ajira kwa watu wake.
Ripoti hiyo ya TPA, imebaini kwamba, wasafiri
wa vyombo vya majini Ziwa Victoria wamepungua kufuatia ushindani uliopo wa
barabara,hususan baada ya mtandao wa barabara kukamika ujenzi kwa kiwango cha
lami.
Kati ya Mwanza na Bukoba kuna usafiri wa ndege
ambao huchangia pia abiria wasisafiri kwa meli.
Kufuatia
hali hiyo,ripoti hiyo imebaini kuwa Kampuni ya Huduma za Meli,Marine Services
Company(MSC) iko hatarini kufilisika,kufuatia meli zake kuharibika mara kwa
mara,kitu kinachodaiwa na baadhi ya abiria kuwa ni hujuma za baadhi ya
wafanyakazo wa MSC ili kuwanufaisha wenye meli binafsi.
Kaimu Meneja Mkuu wa MSC, Projest Kaija,
ameliambia Mwanahalisi kwamba madai
hayo hayana ukweli, kwa kuwa kuhujumu kampuni unayofanyia kazi maana yake ni
kuhujumu mshahara na mapato yako.
“Je,
unahujumu Kampuni namna hiyo ili kampuni ikifa wewe utoe wapi mshahara?’ Kaija
alihoji.
Siku za karibuni MSC imewaondoa viongozi wa
Kampuni hiyo na kuwaweka wapya ili kuboresha ufanisi na kupunguza nakisi.
Kwa kipindi cha miaka mitano, idadi ya meli
zilizohudumiwa na Bandari za Mwanza, imepungua kutoka 2,684 hadi meli 1,900
mwaka jana.
Bandari ya
Mwanza pia huendeshwa kwa hasara ya mamilioni ya shilingi kila mwaka,nakisi ni
takriban shilingi bilioni 4.5
Mabadiliko
ya Tabianchi na Ongezeko la Joto Duniani,pia hutishia USALAMA wa usafiri Ziwani
Victoria.
Kwa kipindi
cha kati ya mwaka 1998 hadi 2006,maji ya Ziwa Victoria yamepungua kutoka mita
1,141.24 juu ya usawa wa bahari hadi mita 1,139.20. Upungufu ni wastani wa mita
2.04.
Kulingana na
Ripoti hiyo, meli nyingi zimekuwa zikishindwa kufungwa katika bandari za Mwanza
na Nansio,Ukerewe. Kupungua kwa kina cha maji ya Ziwa hili pia huweza
kusababisha kuzuka kwa miamba ambayo huhatarisha usalama wa meli na boti na
usalama wa abiria,hasa wanaposafiri nyakati za usiku.
Meli
zinapoparamia miamba hutoboka na kujaa maji,ama kuwa katika hatari ya kuzama.
Ziwa Victoria ni chanzo cha Mto Nile, ambao
huanzia katika Maporomoko ya Owen,Uganda; maji husafiri umbali wa zaidi ya
kilomita 6,900 hadi Misri. Mvua za masika zinaponyesha Afrika ya Mashariki
hubeba rutuba mezi ya Aprili na Mei na rutuba hiyo hufika Misri kati ya Agosti
na Septemba na kuwawezesha Wamisri kupata rutuba jangwani.
Mto Nile ni mungu wa Wamisri. Miungu ya Misri
ina ‘mama’ yao Ziwa Victoria. Ni kwa sababu hii, mwaka 1929 na 1957 Misri
walitiliana saini mkataba na Wakiloni wa Kiingereza kuzuia matumizi ya maji ya
Ziwa Victoria kwa shughuli za kilimo na hata vyanzo vya umeme kama kilichopo
Jinja.
Aidha,kupungua kwa kina cha maji ya Ziwa hili
hufanya meli kutia nanga katika maji ya kina kirefu,na huku ni kuhatarisha
maisha ya abiria,hasa katika maeneo ya visiwa.
Mkuu wa Bandari ya Mwanza, John Mutalemwa
anasema Mamlaka yake imelazimika kuchimba mchanga katika bandari za Mwanza ili
kuongeza kina cha futi tatu ili kuwezesha meli kufunga gatini.
Mradi kama huu unafanyiwa upembuzi yakinifu
katika bandari ya Nansio,Ukerewe,lengo likiwa kujenga gati imara na salama.
Mpango wa
serikali wa kuunganisha Reli kutoka Tanga hadi Musoma kupitia Arusha, utaweza
kurejesha wingi wa abiria na mizigo katika Bandari za Mwanza, au abiria na
mizigo ya Uganda,Rwanda,Burundi na Congo wanaweza kutozifikia kabisa bandari za
Mwanza,na hivyo kuleta kifo cha mende kwa TPA na Meli za MSC.
Ziwa Victoria
ni fursa muhimu kwa Tanzania katika Soko la Pamoja la EAC,lakini fursa hii
inaachwa kwa wageni kupitia hujuma na ufisadi unaofanywa na maofisa wa
mashirika ya umma kama TRL na MSC.
www.congesmrambatoday.blogspot.com
0786 324 074
Subscribe to:
Posts (Atom)