Friday, July 20, 2012

AJALI ZA MAJINI ZA KUTAKA?

                               
JANGA la Ajali ya Meli,  ya Mv. Skagit, huko Mwambao wa Zanzibar, ni matokeo ya serikali, wamiliki wa meli na boti na jamii nzima ya Watanzania kutothamini maisha yao.
 Naam, ni miaka 16 kamili tangu janga la Mv. Bukoba.
  Tanzania ilikuwa tayari imepitisha  miaka 15  ya kuzama kwa Meli ya Mv.Bukoba pale Mv. Spice Islanders ya Zanzibar ilipozama Bahari ya Hindi.
 Mv. Spice Islander, ilizama Septemba 10,ikifanya safari zake kati ya Unguja na Pemba na kupoteza maisha ya watu zaidi ya 200.
Watu 260 waliokolewa.
 Hadithi ni zile zile za Mv Bukoba, kwamba meli ilipakia watu wengi na mizigo kupita uwezo wake, kwamba abiria wengine walichelea kuipanda; ndivyo ilivyotokea kwa MV Bukoba huko Kemondo Bay.
   Meli ya  Mv. Bukoba,ilizama alfajiri, Mei 21, mwaka 1996 na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 800.
Ilikuwa ikitokea Bukoba, na ilizama kilomita kama 12 za majini kutoka bandari ya Mwanza, uelekeo wa Bwiru, jijini Mwanza.
     Inakisiwa kwamba, watu waliojeruhiwa katika ajali hiyo ya kihistoria ni 100; wakati mali nyingi zilipotea na thamani yake bado kujulikana.
 Mara baada ya ajali ile, serikali iliunda Tume iliyokuwa chini ya Jaji Robert Kissanga, ili kuchunguza chanzo cha ajali ile mbaya ya majini.
  Kulingana na Ripoti ya Tume hiyo, usiku wa kuamkia siku ya ajali(Mei 20 mwaka 1996),meli hiyo ilikuwa na abiria kati ya 750 na 800 na wafanyakazi 37.
Kati hao, 114 waliokolewa, na maiti 391 ndiyo walioopolewa na kuzikwa katika makaburi ya Igoma,jijini Mwanza, wakati miili mingine ilichukuliwa na ndugu zao kwenda kuzikwa.
   Kila mwaka, serikali na wananchi huwasha mishumaa na kufukiza ubani katika makaburi hayo kama kumbukumbu ya ajali ile.
  Pengine, serikali huongozana na watu wa madhehebu ya dini kwenda eneo la ajali ili kusoma dua na kumwaga mchanga majini kama ishara ya ibada ya wafu na maziko.
 Inakisiwa, jumla ya miili 332 haikupatikana.
Kwahiyo, serikali ilifanya ‘mazishi’ ziwani katika eneo la ajali,umbali wa kama maili za majini nane tu kutoka ilipo Bandari ya Mwanza.
    Mv.Bukoba, ilijengwa na kampuni ya Meli ya Kibelgiji.Wakati wa kuzinduliwa,Julai 27 mwaka 1979 ilibainika ilitaka kumtosa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere.
 Haikuwa na uwiano wa majini.
 Ilisemwa kwamba, serikali ilishaipiga marufuku meli hiyo isifanye huduma Ziwa Victoria ,  sababu haikuwa na 'sea worthness', vinginevyo lilikuwa kaburi lenye kuelea, ambali siku na saa yoyote ingesababisha maada makubwa.
  Hata hivyo, kufuatia uzembe wa serikali ama kutojali, Mv. Bukoba iliendelea kukata mawimbi ya Ziwa kutoka Mwanza hadi Bukoba, kila siku hadi ilipozama.Iliazama miaka 15 baadaye.
   Baada ya Tume ya Jaji Robert Kissanga kuwasilisha Ripoti ya uchunguzi wake, serikali ikafungua kesi Mahakama Kuu na kuwashitaki aliyekuwa Nahodha wa Meli, Jumanne Rume-Mwiru, aliyekuwa Mkaguzi wa Mamlaka ya Bandari(THA),Gilbert Mokiwa, Meneja wa Bandari ya Bukoba, Alphonce Sambo, na aliyekuwa Meneja wa Bandari ya Kemondo, Prosper Lugumila.
    Kesi hiyo nambari 22,ilifunguliwa Mahakama Kuu,Mwanza mwaka 1998, na ilianza kusikilizwa Mei 14 mwaka 2001.
   Upande wa Mashitaka ukiongozwa na mawakili wa serikali, William Magoma na Eliezer Feleshi(sasa DPP) ulidai mahakamani hapo kwamba washitakiwa kwa pamoja walisababisha vifo,kujeruhi na upotevu wa mali nyingi(hazikufahamika), kwa uzembe.
   Kesi hiyo ilitajwa mara nyingi, ikaahirishwa zaidi ya mara sita hivi, baada ya kusikilizwa kwa mwaka mzima,tangu ilipoanza kusikilzwa Mei,2001.
   Ijumaa, Novemba 29, mwaka 2002, majira ya saa sita mchana, aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Juxton ,Mlay, akasoma hukumu ya kesi hiyo.Nilikuwepo mahakani wakati hukumu ikisomwa.
  Aliwaachia huru washitakiwa wote wanne, baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuithibitishia mahakama(pasipo shaka yoyote) kwamba walisababisha ajali ile na vifo vya watu kama nilivyokwisha taja.
   Jaji Malay, alisema mahakamani wakati akisoma hukumu hiyo ya kihistoria, kwamba hoja za upande wa mashitaka kwamba washitakiwa, Jumanne Mwiru, Mokiwa, Sambo,na Prosper Lugumila walisababisha vifo,kujeruhi na upotevu wa mali, hazikuwa na ushahidi.
   Kwamba, kwa kuwa mashahidi waliiambia mahakama kuwa Rume-Mwiru alisikika asubuhi ile ya ajali, akimwamuru rubani kukata kona, maana yake ni kwamba alikuwa na nia thabiti ya kuokoa maisha ya abiria na wafanyakazi wa meli yake, na wala siyo kutaka kuwaua kwa uzembe kama ilivyodaiwa.
    Akisoma hukumu ndefu, iliyokuwa na jumla ya kurasa 118 zilizvyoandikwa kwa mkono, Jaji Mlay alitumia zaidi ya dakika 160 kufafanua vipengele vya kisheria na kuvitolea maamuzi kwa ufasaha.
   Mwishoni mwa hukumu, akasema kwamba hapakuwa na ushahidi kwamba Mv Bukoba ilizama kwa uzembe wa washitakiwa wanne: Sambo, Mwiru, Mokiwa na Lugumila peke yao !
   Madai ya upande wa mashitaka kwamba Mv.Bukoba ilipakia mizigo mingi kushinda uwezo wake yakatupiliwa mbali na mahakama.
 Kwa sababu, haikufahamika kwa yakini, kwamba MV.Bukoba ilikuwa na abiria wangapi siku ya ajali. Na ilibeba mizigo ya uzito wa kiasi gani?
 Mashahidi wa upande wa mashitaka,walikuwa wameiambia mahakama hiyo kwamba, meli ilipakia mikungu mingi ya ndizi: Lakini, kiasi gani yenye uzito gani?
Nani aliipima uzito?
    Mahakama ilihoji bila majibu. Jaji Mlay alisema, MV.Bukoba ilizama Mei 21, mwaka 1996 kwa sababu haikuwa thabiti; na haikuwa na uwiano wa majini. Hata Tume ya Jaji Kissanga ilisema hivyo.
  Kama kawaida,upande wa mashitaka ukiongozwa Eliezer Feleshi, ukaonesha nia ya kuomba rufaa mahakama ya rufaa.
   Nilikuwepo mahakamani, wakati wa kusomwa hukumu ile.
Niliwaona washitakiwa wakiganda kwa butwaa, kama waliomwagiwa barafu; hawakuamini.
 Nilitaka Jumanne Rume-Mwiru aniambie, alijiskiaje? Hakujibu.
   Miezi mingi baadaye, tulipokutana katika mitaa ya jiji la Mwanza, Mwiru aliniambia kwamba mshitakiwa mwenzake ambaye siku hiyo hakuwepo mahakamani, alipoambiwa kuhusu hukumu ile aliugua nakulazwa hospitalini, mjini Bukoba.
  Leo, ni  miaka mingi  tangu hukumu ile isomwe,rufaa haijasikilizwa, na baadhi ya washitakiwa wamefariki dunia, bila kuona hatma ya kesi yao .
  Mawakili wa upande wa utetezi walikuwa Salum Magongo na Gallati Mwantembe wa jijini Mwanza.
 Mv.Bukoba ilizama kwa sababu za uzembe wa serikali na vyombo vyake.
Haikuwa na uwiano wa majini muda mrefu, hata haikuwa na zana za uokozi kama maboya ya kutosha.
   Haikuwa na mawasiliano.
  Niliwahi kufanya mahojiano na aliyekuwa Nahodha, Jumanne Rume-Mwiru, na kumuuliza hatma ya kesi ile huko mahakama ya rufaa, na kama walikuwa na nia ya kudai mafao yao ?
 “Tunamwachia Mungu” alisema Mwiru huku akicheka bila shaka kukumbuka kilichomtokea.
Aliniahakikishia kwamba mwezao mmoja alikuwa amefariki,bila kujua hatma ya kesi ile.
 Rume-Mwiru, tayari ni marehemu, wakati hatma ya kesi yao haijulikani hadi leo.
   Hata baada ya ajali ile, zimetokea ajali nyingi Ziwa Victoria , mitoni na baharini.
 Mv.Nyamageni,iliyokuwa meli ya binafsi, ilizama miaka ya karibuni ikiwa imebeba masanduku ya soda na abiria kwa pamoja, na haikupatikana hata leo.
 Ilikuwa safari ya kwenda kuzimu.
  Naam, safari ya kuzimu!
Meli za Tanzania ni majeneza yanayosafiri kwenda kuzimu.
Uzembe! Hata ajali za magari huletwa na uzembe tu, usalama barabarani wapo, hakuna hatua. Ziwa Victoria ndipo kuna kazi, majahazi hayana hata boya moja,hakuna vifaa vya kuzima moto!
 miaka ya karibuni, Meli nyingine ya Shirika la Meli(Marine Services Company), Mv.Butiama, ilizimika majini, ikaelea kwa zaidi ya saa nne.
 Meli hiyo ati haikuwa na mawasiliano.
Mtu mmoja alikiambia kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa(RCC) Mkoani Mwanza,kuwa ingeweza kupigwa mawimbi hadi Uganda , au ikaparamia mwamba?
   Majibu hayakutolewa, aliyekuwa akiulizwa alikuwa mtaalam kutoka Mamlaka ya Bandari(TPA), kwamba asingeweza kuisemea MSC, ambao hawakualikwa katika mkutano huo.
  Abiria walihaha, Mv.Butiama ilipozima injini zake jirani tu na Bandari ya Mwanza, lakini hakukuwa na mawasiliano. Eti meli za MSC bado hazina maboya na mawasiliano!
 Je, zile za wajasiliamali zinazotia nanga katika bandari zinazomea kama uyoga, zina zana za uokozi?
Zina maboya mangapi na hufuata sheria kwa kiwango gani?
 Bila shaka, zinafanya kazi kwa mazoea kama ilivyokuwa mwaka 47!
Naam, meli za nchi hii, hata leo hii miaka 15 baada ya kuzama kwa Mv.Bukoba ni majeneza yanayosafiri majini
.Hata MV Spice ilikuwa jeneza lililoelea majini, abiria wakapanda,wakasafiri hadi kuzimu!   Mv. Skagit, yale yale!
Nawapa pole walionusurika!Nawapa pole wafiwa.
  SUMATRA na vyombo vingine vya serikali wapo, wanatazama majahazi yakisafiri ama kuelea kwenda kuzimu.
Serikali huishia kufanya matambiko majini kila mwaka, kama ilivyofanya juzi.
Wengine wamekula ubani wa wafiwa, wengine hujitajirisha kwa maadhimisho haya, wapo tu.
   Wanabarizi upepo.Kufaa kufaana, sijui?
Ni yale yale,ya Mv. Bukoba, Spice Highlanders, Skagit, Nyamageni na nyingine nyingi!
 Hakuna anayejali. Mmiliki wa boti moja Mwanza,juzi alinipigia simu kuniuliza, "Wewe kinakuuma nini hata tukiwalipia nauli SUMATRA waje kukagua meli zetu huku Ziwa Victoria? Nyie waandishi mwataka nini wenye meli tuki accommodate SUMATRA""
 Haya!!
 
 
 
  
  
 

Tuesday, July 17, 2012

http://www.emporis.com/images/show/769872-Small.jpg PICHA YA JENGO REFU DUNIANI, HABARI ZAIDI ZAMA NDANI

AJALI ZIWA VICTORIA?

MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri Nchi Kavu na Majini(SUMATRA) inadaiwa kushindwa kusimamia ukaguzi wa vyombo vya majini Ziwa Victoria, hivyo kusababisha hofu ya kuweza kutokea   ajali.
  “Maofisa wa SUMATRA wanapotoka Dar es salaam kuja Ziwa Victoria kuendesha zoezi la ukaguzi,wanawashurutisha wamiliki wa vyombo vya majini kuwalipia gharama za chakula na malazi hotelini”, Gazeti hili limedokezwa.
Nahodha wa Meli moja ya kampuni binafsi, amemwambia mwandishi wa makala haya kwamba,kitendo cha maofisa wa SUMATRA kupewa hisani ya gharama za chakula,malazi na maburudisho wakati wanapofanya ukaguzi wa vyombo vya usafiri majini Ziwa Victoria,huhafifisha ubora wa vyombo husika,na changamoto kwa manahodha na mabaharia.
“SUMATRA, wanapofika Mwanza,toka Dar es salaam, wanakula na kulala kwa gharama za wamiliki wa meli na boti hapa Ziwa Victoria, sasa watakagua nini kama siyo kulipa fadhila kwa yale waliyotendewa na wamiliki wa meli ama boti?” Amehoji Nahodha wa Meli moja kwa masharti ya kutotajwa jina wakati wa mahojiano na gazeti hili.
 Tumemtafuta    Ofisa Uhusiano wa SUMATRA, David Mziray, kwa takriban juma zima,ili kujibu tuhuma hizo, lakini simu yake ya mkononi ama iliita pasipo majibu, ama ilikuwa imefungwa.
 Hata hivyo, Ofisa Mfawidhi wa SUMATRA,Mkoani Mwanza, Alfred Wariana, amesema maofisa wa SUMATRA kutoka Dar es Salaam,hufika Mwanza kufanya ukaguzi wa kila mwaka,na hulipiwa gharama za usafiri,malazi na chakula na Mamlaka, na wala siyo wamiliki wa vyombo vya usafirishaji Ziwa Victoria.
  Jumapili, Mei 27 mwaka huu,mwandishi wa makala haya alisafiri kutoka Jijini Mwanza,kwenda Nansio,Ukerewe kwa Meli ya Mv. Samar II inayomilikiwa na Kampuni na Kampuni ya Samar Filling Station,ya Mwanza.
Hii ni meli iyojengwa mwaka 2009 na Kampuni ya Songoro Marine Transport pia Jijini Mwanza,kama meli ya mizigo. Ilikuwa ikifanya safari zake kati ya Mwanza na Uganda.
 Meli hiyo ilibadilishwa matumizi mwaka huu, ikawekewa viti na kuanza kusafirisha abiria kutoka Mwanza hadi Nansio,Ukerewe. Uwezo wake ni kuchukua abiria 248 na tani kati ya 101 na 138 za mizigo.
 Nilimuuliza Nahodha wa meli hii,Kapteni Adam Andrew Alex, “Meli ina vifaa vya uokozi kwa kiwango gani?”
“Ina maboya(life rings) 60 na life jackets 350.Tuna mashua moja na vifaa 10 vya kuzimia moto”, Kapteni Alex alisema.
Kutoka Jijini Mwanza hadi Nansio, mji mkuu wa wilaya ya Ukerewe yenye visiwa 27 na vingine 11 visivyokaliwa na watu kuna umbali wa mali 29 za majini.
Kapt.Alex anasema alihitimu katika Chuo cha Mabaharia, Dar es salaam Maritime Insitute, na alikuwa na uzoefu wa mwaka mmoja kazini. Akasema meli yake ilikuwa na mabaharia tisa wenye uzoefu wa kati ya miezi sita na mwaka mmoja kazini.
 Akizungumzia mazingira ya kazi, amesema mikataba ya ajira katika vyombo hivi vya binafsi haiendani na kazi, “Hakuna hata malipo ya muda wa ziada wa kazi(over time),wala hakuna usafiri baada ya kazi”, Kapt. Alex amedai.
 Eferi Bulongo(75) ni miongoni mwa abiria waliosafiri na meli hiyo, Samar II kwenda Nansio. Nilimuuliza, “Una maoni gani kuhusu usafiri Ziwa Victoria?”
 “Sipendi kusafiri kwa meli binafsi;zinasumbua, ratiba ya safari haieleweki,ni namna wanavyojisikia wao, na melini hakuna mahitaji ya lazima ya kuaminika kama chakula na vinywaji;kuna chai”, Bulongo amedai.
 Amesema, meli za Mashirika ya Umma,kama Marine Services Company(MSC) ni bora kabisa, ratiba ya safari huzingatiwa.
“Hizi meli za MSC zinahujumiwa na baadhi ya wafanyakazi wake.Labda wanapewa rushwa na wamiliki wa meli za binafsi ili meli za MSC ziache kufanya huduma ili  wafanye biashara, abiria wengi hawazipendi hizi meli binafsi”, Bulongo amesisitiza, huku akihoji, “Kwanini Meli za MSC ndizo ziharibike kila kunapokucha? Mv.Clarias haijafanya kazi kwa zaidi ya miezi minne; sasa wamesikia Bunge la Bajeti karibu kuanza, ndiyo tunasikia itaanza kati ya kesho(Mei 27) na kesho”, anasema Bulongo.
  Nikampigia simu Kaimu Meneja Mkuu wa MSC,Projest Kaija kujibu tuhuma hizo.
“Leo, Jumapili Mei 27, tunaifanyia majaribio Mv.Clarias. Baada ya siku chache itaanza safari zake kwenda Ukerewe”, Kaija anasema.
 Anakanusha kuwepo kwa tuhuma zenye lengo la kuhujumu Kampuni ya umma kwa nia ya kuwanufaisha wenye meli binafsi.
“Wafanyakazi wa MSC wanawezaje kuhujumu kampuni inayowapa mshahara?” Anahoji,huku akisisitiza kuwa tuhuma hizo zitachunguzwa,kwa kuwa uongozi wa kampuni hiyo ya umma umebadilishwa siku chache zilizopita; kampuni inafanya matengenezo(reform) anuwai.
 Nikampigia simu  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Everest Ndikilo,ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa,  kumsaili:
“Kwanini abiria wanapopanda katika vyombo vya majini Ziwa Victoria hawakaguliwi, ili kubaini uwezekano wa kuwepo kwa magaidi kama  Al-Qaeda na Al-Shabaab, wanaotishia maisha ya watu nchi jirani ya Kenya?”
Magaidi waliwahi kuteka nyara ndege ya Air Tanzania(ATC)mwaka 1988 , yenye maandishi ubavuni, ‘Tango Charlie” wakati ikipaa kutoka uwanja wa ndege wa Mwanza,ikalazimishwa kwenda Jijini London ambako hatimaye jumla ya wateka nyara watano raia wa Tanzania walihukumiwa kifungo cha kati ya miaka mitatu na mitano jela,Jijini London.
 “Ulinzi na Usalama ni Ajenda ya  kudumu na siyo majini tu, hata kwenye majengo,mahoteli na makazi ya raia”, Mkuu wa Mkoa Ndikilo anasema.
Kuhusu maofisa wa SUMATRA,kutoka Dar es Salaam kulazimisha kulipiwa gharama za ukaguzi na wamiliki wa vyombo ziwa Victoria, Ndikilo akasema, “Kama jambo hilo lipo,basi ni tatizo kubwa,nitafuatilia ili hili likemewe”, Ndikilo akasema.
 Gazeti moja litolewalo kila siku hapa nchini kwa lugha ya Kiingereza, katika toleo lake la Mei 23 mwaka huu lilisema kwamba,mwaka 1996 Mv.Bukoba ilipozama na kupoteza maisha ya abiria wake takriban 1,000; miongoni mwao alikuwemo Abu Ubaidah al-Banshiri, ambeye alikuwa nambari mbili wa kundi la kigaidi la Al-Qaeda.
Naam, kundi hili la AlQaeda, lilianzishwa na Osama bin Muhammad bin Awad bin Laden,Feburuari mwaka 1998 kwa jina la WORLD ISLAMIC FRONT,ili kuhujumu maslahi ya Marekani na washirika wake mahali popote duniani,hata kama ni Ziwa Victoria,
Osama alikuwa mshirika wa Marekani na shirika lao la Ujasusi(CIA) mwaka 1979 wakati majeshi ya Warusi walipovamia Afghanistan.CIA walimfadhili mabilioni ya Dola za Marekani kuanzisha kambi ya mafunzo ya Makhtab al-Khidamat(MAK).
Lakini,baada ya Urusi kuondoka Kabul mwaka 1989, Osama akageuka kuwa adui wa MAREKANI na washirika wao, akaungana na Taliban na Mullah Muhammad Omar kuendesha ‘Jihad’ dhidi ya Marekani na washirika.
Nataka kusema kwamba,mwaka 1996 wakati Mv.Bukoba inazama ziwa Victoria, al-Qaeda tayari walikuwepo,na wangeweza kufanya madhara hapa nchini kwa mashambulizi yenye kulenga shabaha Wamarekani ama maslahi yao hapa Tanzania.
Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Everest Ndikilo, amesema serikali imeimarisha ulinzi katika Ziwa Victoria,kwa kuwa zipo boti za doria zinazozunguka ziwani, na raia wanapaswa kutoa taarifa pindi wanapoona mienendo yenye mashaka ama kitisho cha magaidi wa al-Qaeda ama al-Shabaab!
0786 324 074
 
 
 
 
 
  
         


anza

al shabaab Mwanz?

Mwangwi wa A-Shabaab Nairobi, unatikisa usafiri Ziwa Victoria?

          *Mabadiliko ya Tabianchi yatishia meli kuparamia miamba na kuzama
        Na Conges Mramba, Mwanza
   MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari(TPA), imewapandisha kizimbani wamiliki wa meli binafsi, kwani wanazuia Mamlaka hiyo kusimamia usalama wa abiria na mizigo, hata wakati huu wa kitisho cha magaidi wa Al-Shabaab,Afrika Mashariki.
 Mkuu wa Bandari(Port Master)Mwanza, John Mutalemwa, katika mahojiano maalum na mwandishi wa makala haya  juzi, alisema wamiliki hao wa Bandari binafsi wanashindana na Sheria Na. 17(Tanzania Port Act) ya mwaka 2004.
Sheria hiyo inaipa TPA  nguvu ya kusimamia bandari zote, zikiwemo za watu binafsi,ili kukagua usalama wa abiria na mizigo,kabla na baada ya safari.
 “Sheria inatupa Mamlaka ya kusimamia bandari zote zikiwemo  bubu, tukague na kujua mizigo kiasi gani inasafirishwa; tunatakiwa kutazama abiria ikiwa wanalingana na uwezo wa meli au boti,kulinganisha na uwezo wa  chombo chenyewe, halafu tunatoa, “Port Clearance” kabla ya meli kuanza safari”, Mutalemwa alisema.
Kwa mujibu wa Mutalemwa, vipo vyombo vya usafiri majini,huchukua abiria na mizigo kuoita uwezo. Hii ni kazi ya TPA kufanya ukaguzi makini,ili kuondokana na Ajali Ziwa Victoria.
 “Bandari ni mpaka wa nchi. Lazima tusimamie hali ya usalama, meli inaweza kuleta Al-Qaeda ama Al-Shabaab, nap engine inaweza kuingiza nchini silaha kutoka nchi za vita na migogoro. Eti wanakataa tusiwasimamie…tumewafungulia kesi mahakamani”,Mutalemwa ameliambia gazeti hili katika mahojiano Maalum ofisini kwake juzi.
 Meli za mizigo za Jijini Mwanza, hufanya safari zake hadi Port Bell, Uganda,na Kisumu nchini Kenya, ambako sasa magaidi wa Al-Shabaab wanasaidia kuzimu kupanua kinywa chake.
 Aidha, Mkuu huyo wa Bandari Mwanza amesema nchi za Maziwa Makuu kama Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, na Burundi hazina amani, na Kenya hamkani si shwari,kufuatia kitisho cha Al-Shabaab, wanaopinga majeshi ya nchi hiyo kuingia Somalia kuwafulusha magaidi hao.
Kufuatia hali tete ya usalama nchi jirani, Mutalemwa amesema lazima Mamlaka yake kuwa macho na usalama wa abiria na mali zao dhidi ya hujuma za magaidi, wanaoweza kupata upenyo wakaingiza silaha nchini kupitia Ziwa Victoria.
  Mamlaka ya Bandari humiliki bandari za Mwanza Kaskazini na Kusini,Nansio Ukerewe,Kemondo Bay    na Musoma.
Vituo vingine vidogo vinavyomilikiwa na TPA ni Maisome,Nkome,Bukondo,Kahunda,Miharaba,Kome,Buchosa,Solima,Karumo,Chato na Nyamirembe(Kagera) na Kinesi mkoani Mara.
 Bandari ya Mwanza ni kiungo muhimu kwa nchi za Maziwa  Makuu,hususan Uganda na Kenya,na huchangia kwa kiwango kikubwa kukua kwa shughuli za uchumi,hata katika nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki(EAC).
 Ripoti ya Malka hii iliyotolewa kwa Kamati ya Bunge ya Miundombinu(nakala tunayo), inasema bandari ya Mwanza ingeweza kusafirisha abiria milioni moja kwa mwaka.
 Ingeweza kusafirisha tani mamilioni za  moja za mizigo,kama Reli ya Kati ingekuwa inafanya kazi kwa ufanisi. Hili ni eneo muhimu kwa ukuaji wa uchumi wan chi,lakini kinyume chake ni hasara kila upande.
 “Huduma hafifu za Reli zimesababisha shehena ya kahawa kutoka Uganda na hata Bukoba,kubadili njia(route) na kupitia Bandari ya Mombasa,Kenya “, Ripoti hii inasema.
 Kufuatia huduma duni za Shirika la Reli, Bandari za Mwanza ziko taaban,kwa sababu ya kupungukiwa mapato, zinaendeshwa bila faida.
 Kulingana na Ripoti hii kwa Kamati ya Bunge ya Miundombinu,katika kipindi cha miaka mitano,kuanzia 2006/2007 hadi 2010/2011, mizigo imepungua katika Bandari za Mwanza kutoka tani 480,568 hadi 248,860 mwaka 2011.
Utendaji mbovu wa lililokuwa Shirika la Reli(TRL) ulisababisha treni iliyokuwa ikisafirisha abiria na mizigo kati ya Mwanza na Bandari ya Dar es salaam kusimamishwa.Hali hii husababishwa abiria na mizigo kubadili njia na kukosesha mapato bandari za Mwanza.
 Wafanyabiashara wa Uganda wanasafirisha bidhaa zao kupitia bandari ya Mombasa,nchini Kenya.Shehena ya kahawa kutoka Uganda iliyokuwa ikipitia bandari za Mwanza, inapitia Mombasa na hivyo kupunguza kiwango cha mizigo kutoka tani 250,000 mwaka 2007 hadi tani 100,000 mwaka 2009/2010.
 Kufuatia madudu ya TRL, hata abiria wamepungua katika bandari za Mwanza kutoka abiria 891,634 mwaka 2007 hadi abiria 593,342.Huu ni upungufu wa asilimia 6.3 unaoikosesha nchi mapato na fursa za ajira kwa watu wake.
 Ripoti hiyo ya TPA, imebaini kwamba, wasafiri wa vyombo vya majini Ziwa Victoria wamepungua kufuatia ushindani uliopo wa barabara,hususan baada ya mtandao wa barabara kukamika ujenzi kwa kiwango cha lami.
 Kati ya Mwanza na Bukoba kuna usafiri wa ndege ambao huchangia pia abiria wasisafiri kwa meli.
Kufuatia hali hiyo,ripoti hiyo imebaini kuwa Kampuni ya Huduma za Meli,Marine Services Company(MSC) iko hatarini kufilisika,kufuatia meli zake kuharibika mara kwa mara,kitu kinachodaiwa na baadhi ya abiria kuwa ni hujuma za baadhi ya wafanyakazo wa MSC ili kuwanufaisha wenye meli binafsi.
  Kaimu Meneja Mkuu wa MSC, Projest Kaija, ameliambia Mwanahalisi kwamba madai hayo hayana ukweli, kwa kuwa kuhujumu kampuni unayofanyia kazi maana yake ni kuhujumu mshahara na mapato yako.
“Je, unahujumu Kampuni namna hiyo ili kampuni ikifa wewe utoe wapi mshahara?’ Kaija alihoji.
 Siku za karibuni MSC imewaondoa viongozi wa Kampuni hiyo na kuwaweka wapya ili kuboresha ufanisi na kupunguza nakisi.
 Kwa kipindi cha miaka mitano, idadi ya meli zilizohudumiwa na Bandari za Mwanza, imepungua kutoka 2,684 hadi meli 1,900 mwaka jana.
Bandari ya Mwanza pia huendeshwa kwa hasara ya mamilioni ya shilingi kila mwaka,nakisi ni takriban shilingi bilioni 4.5
Mabadiliko ya Tabianchi na Ongezeko la Joto Duniani,pia hutishia USALAMA wa usafiri Ziwani Victoria.
Kwa kipindi cha kati ya mwaka 1998 hadi 2006,maji ya Ziwa Victoria yamepungua kutoka mita 1,141.24 juu ya usawa wa bahari hadi mita 1,139.20. Upungufu ni wastani wa mita 2.04.
Kulingana na Ripoti hiyo, meli nyingi zimekuwa zikishindwa kufungwa katika bandari za Mwanza na Nansio,Ukerewe. Kupungua kwa kina cha maji ya Ziwa hili pia huweza kusababisha kuzuka kwa miamba ambayo huhatarisha usalama wa meli na boti na usalama wa abiria,hasa wanaposafiri nyakati za usiku.
Meli zinapoparamia miamba hutoboka na kujaa maji,ama kuwa katika hatari ya kuzama.
 Ziwa Victoria ni chanzo cha Mto Nile, ambao huanzia katika Maporomoko ya Owen,Uganda; maji husafiri umbali wa zaidi ya kilomita 6,900 hadi Misri. Mvua za masika zinaponyesha Afrika ya Mashariki hubeba rutuba mezi ya Aprili na Mei na rutuba hiyo hufika Misri kati ya Agosti na Septemba na kuwawezesha Wamisri kupata rutuba jangwani.
 Mto Nile ni mungu wa Wamisri. Miungu ya Misri ina ‘mama’ yao Ziwa Victoria. Ni kwa sababu hii, mwaka 1929 na 1957 Misri walitiliana saini mkataba na Wakiloni wa Kiingereza kuzuia matumizi ya maji ya Ziwa Victoria kwa shughuli za kilimo na hata vyanzo vya umeme kama kilichopo Jinja.
 Aidha,kupungua kwa kina cha maji ya Ziwa hili hufanya meli kutia nanga katika maji ya kina kirefu,na huku ni kuhatarisha maisha ya abiria,hasa katika maeneo ya visiwa.
 Mkuu wa Bandari ya Mwanza, John Mutalemwa anasema Mamlaka yake imelazimika kuchimba mchanga katika bandari za Mwanza ili kuongeza kina cha futi tatu ili kuwezesha meli kufunga gatini.
 Mradi kama huu unafanyiwa upembuzi yakinifu katika bandari ya Nansio,Ukerewe,lengo likiwa kujenga gati imara na salama.
Mpango wa serikali wa kuunganisha Reli kutoka Tanga hadi Musoma kupitia Arusha, utaweza kurejesha wingi wa abiria na mizigo katika Bandari za Mwanza, au abiria na mizigo ya Uganda,Rwanda,Burundi na Congo wanaweza kutozifikia kabisa bandari za Mwanza,na hivyo kuleta kifo cha mende kwa TPA na Meli za MSC.
Ziwa Victoria ni fursa muhimu kwa Tanzania katika Soko la Pamoja la EAC,lakini fursa hii inaachwa kwa wageni kupitia hujuma na ufisadi unaofanywa na maofisa wa mashirika ya umma kama TRL na MSC.
  www.congesmrambatoday.blogspot.com
    0786 324 074
 
  
 
 


vita, tangu Jerusalem ya kale hadi Jerusalem Mpya


TUIJADILI ISRAEL, nchi ambayo ina jumla ya watu 757 katika maili moja tu ya mraba.
Jirani za taifa hili babe sana  Mashariki ya Kati na mshirika wa Mataifa ya Magharibi ni Lebanon, Syria ambako vita vya kumwondoa Al Assad vinapamba moto,Ukanda wa Magharibi wa Mto Jordan, Jordan yenyewe, Gaza Strip, na kuna Nchi ya Misri, ambako wanajeshi wamekataa kuheshimu mamlaka ya  Rais mpya, Mohammed Mursi.
Israeli, ina ukubwa wa maili za eneo 7,800. Mwaka 1997 mji mkuu wa zamani wa Israeli, Jerusalem(Yeroo-Shalayim)  yaani mji wa Amani, ulikuwa na wakazi 591,400 sawa lilivyokuwa Jiji la Mwanza,wakati huo.
Tel Aviv, una wakazi 2,181,000. Kuna vikosi vya wanajeshi 172,500. Nchi hii hutumia fedha inayoitwa Shekeli, ambayo miaka michache tu iliyopita, Shekeli Tano zilikuwa na thamani sawa na Dola moja ya Marekani.
 Mji huu wa kihistoria ulijengwa mwanzoni zama za Mfalme Daudi(1004-965 BC), umewahi kutekwa na kutawaliwa na Babeli, Wamedi,Waperizi,Wagiriki,Rumi ambao waliubomoa mji kabisa mwaka 70 AD.
Awali, jiji hilo lilitekwa na Mfalme Nebuchadnezzar mwanzoni kabisa mwaka 605 BC huu ni wakati Nabii Danieli alipotekwa pia na kuchukuliwa hadi Babeli.Danieli aliishi huko uhamishoni hadi mwaka wa BC 530 akafariki dunia.
Nebchadnezzar aliuzingira mji huu na kuutekwa kwa mara ya pili mwaka 598 BC huu ulikuwa wakati wa Nabii Ezekieli, ambaye naye alihamishwa hadi Babeli ambayo sasa iko Irak.
Ezekieli, aliishi Babeli mwaka 593 hadi 570 BC. Mara ya tatu Mfalme huyu aliutekwa Jerusalem mwaka wa BC 586 MJI UKABOMOLEWA kabisa, hadi hapo ulipojengwa wakati wa akina Nehemia.
Waarabu walikuja kuliteka  eneo hilo mwaka wa AD 636; na tangu karne ya 11 Waarabu wamelimiliki eneo hili la Israeli. Hawa ni pamoja na Seljuk, Mamluks na Dola ile ya Ottomans ya Uturuki.
 Uingereza ililichukua eneo hili mwaka 1917, hii ni kudhihirisha kwamba watu wa Israeli wamepata misukosuko ya kutawaliwa na mataifa ya kigeni, na vita vimewaua wengi hadi wakakimbilia uhamishoni katika mataifa mengi sana duniani.
Umepata kuona Filamu iitwayo, ESCAPE FROM SOBIBO?Ukitazama filamu hiyo utaona kwamba Waisraeli hawa wamenja shubiri wakati wa Adolf Hitler, ambaye alikusudia kuwafyeka kabisa katika uso wa dunia.
Awali, baada ya kuchukuliwa mateka mwaka wa BC 586-537 BC Jerusalem ulijengwa upya zama za Ezra, Nehemia hadi kufika BC 404 Mji huu ulishakamilika.
Kwanini Waisraeli wameshambuliwa mara nyingi na wakazoea sana vita? Biblia inatupa jibu kwamba, walimwasi Mungu.
Watu wengi sana hudhani Israeli bado ni Taifa pendwa la watu wa Mungu! Huku ni kuibaka historia kwa kiwango cha kutisha.
Tutazame kwamba, watu hawa(Waisraeli) walimkataa Masihi, wakamchongea hadi akauawa. Yesu, alitabiri maangamizi ya taifa hili, hadi kuwa kwao wakimbizi katika nchi nyingi,kama tutakavyooona.
Wamekuja kurejeshewa taifa  lao Mei 14, mwaka 1948 na Umoja wa Mataifa. Hata hivyo,Waarabu wanapinga vikali jambo hili, kwa kuwa huku kulikuwa kuchukua ardhi ya Waarabu waliyoikalia kwa karne nyingi wakati Waisraeli walipokuwa uhamishoni, mataifa mbalimbali.
 Warejea ,na Umoja wa Mataifa ukawapa eneo hilo ili wakae na Waarabu, wameshambuliwa mara nyingi na Misri, Saudi Arabia,Syria,Lebanon na Irak. Imefanywa mikataba ya amani,bila mafanikio vita vinapamba moto hata leo hii.
Nimejadili Mkataba wa Amani wa Camp     David, wakati ule wa Rais Jimmy Carter,nimejadili mkataba baina yake na Misri,Misri ndiyo nchi yenye ushawishi mkubwa Mashariki ya Kati, nayo sasa Hamkani si Shwari tena.
Unabii unatimia,kwamba nchi za Ulaya na Marekani zinapata nguvu nyingi na zitatawala nchi za Kiarabu.
Vita kati ya Israeli na nchi za Kiarabu vimeanza zamani sana,mikataba ya kulinda amani ilishawekwa mingi sana ikaja kuvunjika. Israeli imeshambuliwa hata wakati wa Siku kuu kama Yom Kippur.
Tumeona katika makala zilizotangulia kwamba Julai 3,mwaka 1976 ndipo waliposhambulia Enttebe,na kuchukua mateka wao.Nimesimulia sana kisa hiki, wengine wananiuliza Entebbe ni mdudu gani?! Poleni sana!
Mwaka 1977 Israeli na Misri walitiliana saini Mkataba wa kuacha vita baina yao kwa miaka 30.
 Hata hivyo, kungali na vita na jiradi zao; kuna “Intifada” naam ni Intifada hadi kiama. Sasa kukosekana kwa siasa tulivi Misri hivi sasa,kunatishia sana amani ya Israeli na Mashariki ya Kati.
Tumemwona Hillary Rodham Clinton akifika Cairo chini ya ulinzi mkali sana kwenda kupoza joto ili vita visizuke, baada ya jaribio la kumpindua Hosni Mubarak(87) na kumtia korokoroni,kuonekana siyo suluhu,baada ya maandamano ya Taharir Square.
 Jerusalem kuna msikiti mkubwa unaoitwa, Al-Aqsa,vita huingia hadi misikitini na katika masinagogi watu hupigwa mabomu na kuuawa.
Israeli, inagombana sana na Chama cha Ukombozi cha Palestina, PLO.Marekani wamejitia kupatanisha mara nyingi sana, bado vita vinapamba moto kila siku, misikitini na mahekaluni watu huuliwa kwa mabomu ya kujitoa mhanga,risasi n.k
Naam, ni vita baina ya Wayahudi na Waislam mjini Jerusalem,kila siku akina Waziri Mkuu, Benyamin Netanyahu na Hayati YasIr Arafat walishakaa vikao, hakuna amani.Hillary Clinton amefika pia Yerusalem lakini hakuna amani na utangamano,ni mtutu wa bunduki tu.
 Sasa inasadikiwa, Kiongozi wa Wapalestina, Yassir Arafat aliuliwa kwa sumu mjini Paris, wanataka maiti yake ifukuliwe na kufanyiwa uchunguzi upya ili kubaini chanzo cha kifo chake-ni vita kila siku.
Mara vita Ukanda wa Magharibi mwa Mto Jordan, Dead Sea ama Gaza Strip huko Peninsula ya Sinai hadi Bahari ya Mediterranean.
Yesu, alitabiri maafa ya Jerusalem ama Yerusalem.Wayahudi walimwasi Mungu karne nyingi wakaungana na mataifa mengine kuabudu miungu na sanamu. Unajua Mungu ni mwenye wivu!
Ibilisi ndiye hasa kiongozi wa hawa taifa la Israeli,kama alivyotabiri Carlos The Jackal, Hugo Chaves, Robert Gabriel Mugabe, na hata Fidel Alejandro Castro Ruz aliwahi kumwita Rais Mstaafu,Bush kwamba ni Shetani!
 Kwa nini? Tazama Luka 21:2-24 na usome pia vitabu vya Isaya,Yeremia na Hosea. Kwa kifupi,unaweza kusoma vitabu hivi Prophets and Kings na Christ’s Object Lessons, katika sura iitwayo, The Vineyard of the Lord, uone Mungu alivyowazira Wayahudi,kwa tabia zao.
Yesu alitabiri Wayahudi kuukimbia mji wao wa Yerusalem, walikimbia uhamishoni wakaangamizwa huko. Tazama Filamu ya ESCAPE FROM SOBIBO uone mateso waliyopata huko, na utaona laana waliyovuna baada ya ukaidi wao; Isaya 27:6
Katika Mathayo 24:15-20 Yesu aliwaonya kutambua kwamba mwaka 70 AD Majeshi ya Warumi yangeubomoa mji, waliambiwa kukimbia wakati huo wakaleta kiburi-waliuliwa wengi hekaluni hadi damu ikavuja kama mto.
Nabii Danieli alishatabiri maafa juu ya Yerusalem,karne sita kabla ya Yesu. Tazama Danieli 9:27 walishupaza shingo zao ngumu wakajidai Mungu angejipendekeza kwao hata wanaposhirikiana na Ibilisi kufanya ukaidi(Yeremia 7:4).
Wayahudi hawa walishakataliwa na Mungu kama taifa lake teule, waliwaua mitume,walimchongea Yesu, waliua wafuasi wengi wa Yesu, Tazama Matendo ya Mitume 6:8-15 na Matendo 7:51-60.
 Ni wakati huu wafuasi waaminifu wa Yesu waliuliwa,wakafukuzwa Yerusalem. Sura ya nane ya kitabu cha Matendo ya Mitume hueleza Wakristo walivoteswa, wakatimkia Ulaya.Wayahudi walimkataa Yesu(Masihi) wakamchagua Jambazi moja aitwaye Baraba(Luka 23:18, Mathayo 27:22).
Kuongozwa na Yesu, walisema afadhali huyo jambazi Baraba kuliko Yesu, na heri wangeendelea kuwa chini ya utawala wa Kaisari wa Rumi kuliko Yesu.
Nataka kusema, Israeli siyo taifa teule la Mungu,na nimetumia Biblia kuonesha ushahidi wa jambo hili.
Tangu mwaka 34 AD walipomuua Stefano na wakawatesa Wakristo(wafuasi wa YESU) Basi wakatawaka Shetani(akina Kaisari Nero)wawatawale(Mathayo 27:24-25) wakajiweka chini ya utawala wa Shetani kama akina Carlos wanavyosema.
 Mungu alishautupa mji huu kitovu cha vita,na Shetani na mawakala wake Freemasonry wanautawala.
Hata hivyo Shetani hawezi kutawala dunia kutokea Jerusalem, atatawala kutokea Babeli ya Kiroho, ambayo ni Jijini Rome,baada ya Washington kukabidhi madaraka yake baadaye siku za usoni.
 Jerusalem ya sasa itaangamizwa kama Babeli,maana hekalu lao na dhabihu zao ni ibada ya sanamu na mizimu,isiyo na maana tena.
Katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana 21:1-8 Nabii Yohana alioneshwa Jerusalem Mpya wenye Amani.Yerusalem wa kale ulishanajisiwa na majeshi na watawala waovu wa dunia.
Katika   Ufunuo 20:7-10 tunaelezwa Jaribio la Shetani na Majemadari wa vita wa kale wakijaribu kuuteka Mji huo wa Jerusalem Mpya.Wamo akina Hitler, Napoleon Bonaparte n.k
Mji huo wa Yerusalem Mpya,huitwa Kambi ya watakatifu Ufunuo 20:9 na Biblia inasema hao majemadari watashindwa,watauliwa kwa nguvu za Mungu.
Tuijadili kidogo, “City Profile”  ya Jiji hili jipya la Jerusalem lililofichwa mahali kusipojulikana. Tusome Ufunuo wa Yohana 21:10 hadi 27. Biblia inasema ni mji halisi, na wala siyo kisasiri ama hadithi za kufikirika(Myth).
Ufunuo 21:16 hutwambia kwamba jiji hili ni mraba,kila upande una urefu wa maili 344.6 hivi. Mji huu unalingana ukubwa na Jimbo la Oregon,huko Marekani,ni kama Colorado hivi.
Katika Afrika Mashariki,ni kama Rwanda na Burundi kwa pamoja. Una ukubwa wa Poland huko Ulaya.
Kimo cha magorofa ya mji ni sawa na urefu wa mji na upana! Hapa ndipo makao ya watakatifu wa Mungu(Yohana 14:2).Kila mkazi wa dunia ana nafasi yake katika majumba yale marefu. Wakazi Bilioni saba,kila mtu anayo sehemu yake katika jiji hilo, isipokuwa mtu akatae mwenyewe,kwa kuhalifu SHERIA ZA MUNGU,Amri 10.
Watu wengine watajenga humo nyumba zao na kuishi(Isaya 65:21-22) wengine watalima mashamba yatakayostawi vizuri.
 Yerusalem Mpya utakuwa na eneo la kilomita za mraba takriban 189,998.7 hivi ni kama Rwanda na Burundi kwa pamoja,kama Cote d’ Ivoire. Mji huu ukubwa wake unazidi Ugiriki, Guinea Bissau, Israeli yote,Italia n.k
Tanzania ina ukubwa wa kilomita za mraba 945,000. Msomaji anaweza kubaini kwamba eneo la Yerusalem Mpya ni kama 1/5 ya Tanzania nzima.
Tujadili kidogo magorofa ya Jerusalem Mpya. Magorofa marefu(SKYCRAPERS) ambayo hakuna hata moja hapa duniani kwa sasa.
Jengo refu kuliko yote hapa Afrika, ni ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika,mjini Addis Ababa, Ethiopia.
 Jengo hilo limejengwa kwa hisani na Wachina,na wamelikabidhi tayari kwa Umoja wa Afrika AU, ambao sasa Mkuu wa Kamisheni yake ni mtaraka wa Jacob Zuma, Bibi Dlamini Zuma. Jengo hilo limejengwa kwa Dola za Marekani milioni 200.
Jengo hilo nalo haliwezi kulingana urefu na magorofa ya Jerusalem utakaoshushwa na Mungu duniani,baada ya Jerusalem wa kale kubomolewa kwa vita kali sana.
Tumeona kwamba magorofa ya jiji hilo yatakuwa na kimo cha maili 344.6 kwenda angani. Kwa mahesabu ya haraka ni kama kilomita 189,998.7 kwenda juu angani.
Kulingana na tovuti za www.worldstallest.com na www.skycraper.com hata jengo pacha la WTC wanalosema lilibomolewa na Osama Septemba 11,mwaka 2001,lilikuwa na kimo cha futi 1,368 tu.
Majengo yote marefu duniani sasa,hakuna lenye urefu wa zaidi ya futi 2000. Kulingana na tovuti hizo,majengo 10 marefu duniani ni pamoja na jengo la Indosat   Telcom huko Jakarta,Indonesia lenye kimo cha futi 1,831. Lilijengwa mwaka 2001.
CN tower la Toronto huko Canada, lina urefu wa futi 1,815 na lilijengwa mwaka 1974. Jerusalem Mpya una majengo yenye urefu wa futi mabilioni.
Majengo mengine marefu yako Moscow,Urusi, Shanghai,China, Iran,Kuala Lumpur huko Malaya,Beijing, Uzbekistan na Kazakhstan haya yalijengwa mashine.
 Huko Giza,Misri yale Mapiramidi anayosema Gideon M.yalijengwa na mikono ya wanadamu,bila mashine wala mitambo. Yalijengwa zamani na yamedumu kwa jumla ya karne 43 sasa, Piramid moja lina urefu wa futi 481.
Kwa kifupi, hakuna jengo hapa duniani litakalolingana na magorofa ya Yerusalem Mpya,yamejengwa na Mungu mwenyewe.
 Ukitaka kujua sura ya Mji huo soma mwenyewe Ufunuo wa Yohana sura nzima ya 21.Biblia inasema hakutakuwa na majambazi, wezi,wachawi,magaidi,majambazi,machangudoa na wasagaji. Hakuna bia wala gongo!
http://t2.gstatic.com/images?q=tbn:ANd9GcSyID4IligvMKiKtwfcp-1KGTaF1NauOjY6EJROwAK-YCjYTHwL picha ya majengo marefu duniani
 Hii ndiyo sababu watu hawapendi kwenda huko maana hakuna sigara, wala madada poa! Hakuna kiti moto huko. Hakuna majuto Tazama Ufunuo 21:4,8 Mji umejengwa kwa madini safi,barabara ni dhahabu angavu kama kioo(Ufunuo 21:18-21)
Hakuna TANESCO huko, maana ni mchana siku zote(Ufunuo 21:23, 22:5) Hakuna udhaifu,hakuna mbumbumbu na watu dhaifu,hakuna hospitali maana watu hawaugui.
Masharti ya kuingia jiji hili ni kuepuka sifa hizi: Ushoga, uchawi,ibada ya sanamu,utapeli,uongo,ufisadi na uchafu wa tabia(Ufunuo 22:15) Hakuna rushwa na chuki kwa watu na kulipa visasi. Hakuna kuteka nyara na “Kuulimboka” ama ‘kukolimba’ watu huko!!
Hakuna utapeli na uongo,rushwa,kila mtu anatiwa moyo kuchukua uraia wa jiji hilo.Neema ya Yesu iwe nanyi wote,Amina,Ufunuo 22:21.
TAMATI
0786 324 074







Thursday, July 12, 2012

Euphrates... RIVER EUFRATES

vita hadi Jerusalem Mpya-4



Katika Biblia, Ufunuo wa Yohana 17:13 husema kwamba, Wafalme wa Dunia sasa hufanya majadiliano, ili kumrithisha mamlaka yao Mfalme mmoja tu Duniani.
Ufalme ujao Duniani, huoneshwa kwa mifano ya “Mwanamke” aliyebebwa na Mnyama, ambaye katika makala zilizotangulia,tukaona mwanamke huyu aitwaye, Goddess Roma, akiwa nje za ofisi za Bunge la Umoja wa Ulaya,huko mjini Brussels.
Makao Makuu ya serikali hii mpya, Gideon M. anasema yatakuwa Jerusalem, lakini mimi nasema yatakuwa mahali kilipokuwa kiti cha enzi cha utawala wa Rumi ya kale.
Hata hivyo,tujadili namna Umoja wa Kujihami wa Ulaya Magharibi(NATO) walivyoanza kuuvuka Mto Frati na Tigris ili wajielekeze Mashariki,ilikokuwa iliyokuwa Dola ya Kisovieti,USSR.
Naam, tujadili namna “Mto Frati” ulivyoanza kukauka,ili kutengeneza njia kwa madola ya Magharibi kuzitwaa milki za Mashariki, ili kuzilazimisha kujiunga nao aidha NATO, ama Umoja wa Ulaya(EU),na Soko lao la Pamoja, European Common Market.
Mhariri wa Jarida la Executive Intelligence Review la Marekani, Edward Spannus, amesema vita vinavyochochewa sasa na Marekani na Uingereza huko Syria,hatimaye vitakuwa VITA VYA TATU VYA DUNIA!
 Uingereza,Marekani na washirika wao wanawaunga mkono waasi wa Syria,na Urusi na China wanamuunga mkono kiongozi wa nchi hiyo, Bashir al-Assad.Sasa, inasemwa,mwisho wa siku Marekani na washirika wake wataingia vitani dhidi ya Urusi na Uchina,na hivi ni vita vya tatu vya Dunia?
Biblia, katika Ufunuo 16 inasema vita vya TATU VYA DUNIA ni Har Mageddon, ambamo Mungu atapingwa kwa nguvu za mashetani na mawakala wao,Freemasons,na malaika toka mbinguni watakuja kusimamia mabambano ili kulinda HAKI NA UKWELI Duniani.
 VITA BARIDI vilikwisha mwaka 1991 Desemba, baada ya Russia,Kazakhstan na Belarus kuwa mataifa huru. Baadhi ya nchi kama Georgia na nyingine tayari zimekuwa washirika wa NATO.
Tunaona JAPAN na mataifa mengine ya Mashariki wakiungana na M arekani na washirika wao. Kile kimbembe kilichowapata Marekani zama za vita Baridi,kinapungua sana siku hizi,na mataifa yanayoitishia NATO yanashambuliwa,na mengine yalishapinduliwa na viongozi wake kuuliwa kama tulivyoona katika makala zilizotangulia.
George Herbert Walker Bush ambaye tumuite “Bush Baba(sasa ana umri wa miaka 88) na mwanaye George Walker Bush(65) wamepigana vita vya Ghuba  vya kwanza na vya pili na kufanikiwa kumpindua Saddam Hussein na kumuulia mbali,huko kandoni mwa   Mto Frati.
Jambo hili la vita vya kwanza vya Ghuba na vya pili na mapinduzi kisha kuhukumiwa kifo Mtawala wa Irak yenye Mito Frati na Tigris, ni utimilifu wa Unabii wa “Kukaushwa” kwa Mto Frati, ili njia itengenezwe kwa Wafalme wa Mashariki kuungana na Magharibi,ili kufanya shauri la kumrithisha Kiongozi      Mmoja wa Dunia nzima!
 Tumeona kwamba Muammar al-Qaddafi aliyetaka kuwapinga naye amepinduliwa na kuuawa, kisha Carlos The Jackal na “Magaidi” wengine wamefungwa jela na wengine wameuliwa.
Hao wanaoitwa magaidi,ni wapinzani wa ubeberu wa Magharibi, kwa staili ya kulipua mabomu!
Mataifa ‘bishi na tukutu’ yaliyosalia sasa ni Iran na Korea Kaskazini,iliyoanza kufanya majaribio ya ya silaha za Nyuklia Oktoba 9,mwaka 2007.
 Hata sasa, ingalipo “Homa ya Dunia” mara hii siyo VITA BARIDI vya Ubepari dhidi ya Ukomunisti, bali ubepari dhidi ya NYUKLIA inayomilikiwa na Madola machache ya Mashariki kama Iran na Korea.
Syria inashughulikiwa, sasa na kama lisemavyo Executive Intelligence Review,ni VITA vya aina yake vya kuwatiisha wenye msimamo tofauti na Marekani, Israeli,Ulaya namfumo wa dini moja unaoandaliwa kushita mamlaka ya Dunia nzima.
 Hakika, sasa tunajua,baada ya Saddam kuuawa, alifuata Gaddafi na Osama bin Laden na atafuata huyo Bashir al-Assad wa Syria na wenzake, kama watazidisha upinzani.
Walianza kuambiwa wasaini mikataba ya kupunguza silaha. Mikataba hii ilianza tangu Agosti 5, mwaka 1963,Russia, Marekani na Uingereza walipotiliana saini mkataba wa kuacha majaribio ya Nyuklia baharini,ardhini na angani.Huu ni Mkataba wa mjini Moscow,Urusi.
Urusi na Marekani walitiliana saini tena kuacha Nyuklia Januari 27,mwaka 1967, tena Uingereza na Russia wakatiliana saini Julai Mosi mwaka 1968 na Mei 26 mwaka 1972 Marekani na Urusi wakaingia mkataba mkubwa uitwao, Strategic Arms Limitation Treaty(SALT- 1), NI HUKO Moscow,kwamba baada ya miaka mitano waache kutengeneza Misaili zenye kuweza kulenga shabaha kutoka Bara moja hadi linguine.
 Haya mamisaili yanaitwa, Intercontinental Ballistic Missiles(ICBM)wakaifanyia marekebisho mikataba hii 1974 hadi Septemba 1997.
Mwaka 1978 iliyokuwa kambi ya Northern  Atlantic  Treaty Organization(NATO) ikiongozwa na Marekani ilikuwa na hayo makombora ya masafa marefu ya ICMBs 1,054 wakati ile Kambi ya Mashariki ya Warsaw Pact( Poland) ilikuwa ikiongozwa na Urusi ,ilikuwa na makombora hayo 1527.
Ukitazama Military Balance wakati huo utaona NATO walipokuwa na manowari za kivita(SLBM) 656,Warsaw Pact walikuwa nazo 845. NATO walikuwa na ndege za kivita 387,Warsaw Pact wao walikuwa na ndege 135.
Nataka kusema kwamba,  Kambi ya Urusi ya Mkataba wa Warsaw ilikuwa na nguvu kuzidi NATO ndiyo maana kulifuatwa mikataba mingine kama SALT-2 uliotiwa saini Vienna, Austria  Juni 18,mwaka 1979.
Kila upande ulikubali kusitisha kutengeneza makombora hayo na mabomu zaidi ya 2,400,na makombora ya ICBM 1,320 yasivukwe kwa kila upande.
Mkata huu wa SALT 2 uliingia doa wakati Urusi ilipoivamia Afghanistan Desemba, mwaka 1979 Rais Jimmy Carter akaacha kuamini Mkataba huo. Osama Bin Laden alianza kulelewa na Marekani wakati huu ili awapinge Warusi huko Afghanistan.
Baadaye aliwageuka,kama       Gaddafi naye alivyowageuka.
NATO pia walikuwa na magari ya  kubeba silaha za nyuklia zenye kulenga shabaha tofauti, Multiple Independently Targetable Re-entry Vehicle(MIRV) kama 1,046 wakati Mashariki walikuwa na 140.
Desemba 8,1987 makombora ya masafa ya Kati nayo yakawewa Mkataba wa INF huko Washington baina ya Urusi ya Mikhail Gorbachev na Ronald Reagan wa Marekani.
Ipo mikataba mingine kama START 1 na START 2 ya Januari 3, 1993 iliyosainiwa Moscow,na ipo marufuku ya majaribio ya Nyuklia ya Septemba 24 mwaka 1996(CTBT) pia kati ya Russia na Marekani ili kukataa milipuko ya Nyuklia.
Huu mkataba mwaka 2000 ulitia saini na nchi 160,na baadaye Oktoba 15 mwaka huu 2000 mkataba huu ulipata nguvu.
Kuna madhara mengi ya kuvuja kwa nyuklia kama yale ya  kinu cha Chernobyl, huko Ukraine siku hizi  Aprili 26 mwaka 1986 karibu na Kiev.
Watu 31 walikufa,lakini hata sasa Japan vinu vimelipuka na Ulaya vimelipuka na kuleta madhara makubwa kwa afya za watu sababu ya mionzi ya sumu inayoleta saratani kwa watu.
Septemba 30  1999 ajali nyingine ilitokea Tokoimura,Japan wakati wanarutubisha madini ya Uranium. Hata Tanzania tukianza kurutubisha Uranium na tukaenda kinyume na Marekani na Ulaya,utaona watakavyotuijia.
Marekani iliwahi kupiga mabomu ya Atomik B-26 katika Hiroshima,Japan Agosti 6,mwaka 1945 kisha siku tatu baadaye wakapiga NAGASAKI.Haya ni mabomu yaliyohitimisha vita vya Pili vya Dunia.
Baada ya hivi vita,Kambi ya Mashariki ilikuwa na majeshi 1,303,000 dhidi ya 1,175,000 ya NATO. Nato walikuwa na vifaru 11,000 dhidi ya 26,000 ya vile vya Warsaw Pact. Madege ya vita NATO walizidiwa kwa takriban ndege 2000. Ndiyo maana ililia mikataba.
Sasa, kiama cha SEPTEMBER 11,2001 pale WTC kilicholeta kifusi kilichojaza ekari 16,na kifusi chenyewe cha WTC kilikuwa na uzito wa tani milioni 1.2 hapo walipoita, ‘Ground Zero’ ndicho chimbuko la visingizio vingi vya kuyakomesha mataifa korofi, hasa ya Kiarabu ambayo ni adui wa Israeli.
Marekani inaendesha kinachoitwa VITA DHIDI YA UGAIDI kwa ushirika na Ulaya na Israeli,ili kuwakomesha Waaarabu wenye msimamo mkali ili wasalimu amri. Hivi ni vita vitakavyoendelea hadi Yesu anapokuja mara ya pili duniani.
 Itaendelea
0786 324 074

KUTOKA JERUSALEM YA KALE HADI JERUSALEM MPYA-5


      
     *Vifo vya Saddam,Osama na Gaddafi ni kutimia kwa Unabii wa Ufunuo 16:12
    *Unabii wa Carlos The Jackal,kuhusu Marekani,Libya na Syria unatimia sasa
Turejee nyuma, wakati wa vita vya kumpindua Mtawala wa Nchi ya Mito miwili ya Tigris na Eufrates,Saddam Hussein.
Marekani, aslani haikusubiri ruhusa ya Umoja wa Mataifa(UN);Saddam alipinduliwa,Sanamu lake likang’olewa kuonesha enzi yake ilikwishakoma, baada ya miaka mitatu gerezani, akanyongwa huko Camp Justice,mjini Baghdad.
George Herbert Walker Bush(88),Agosti mwaka 1990 alijaribu kumng’oa Saddam Hussein huko Irak,kipindi alipoivamia Kuwait. Unajua sababu za Saddam kuivamia Kuwait? Waliiba mafuta.Bush huyu (Baba) alipata ushindi mwembamba katika medani ya vita.
Bush baba alisaidiwa sana na vikosi vya Umoja wa Mataifa(UN),vikosi vya Umoja wa Kujihami Ulaya Magharibi(NATO) na Muungano wa Kiarabu, Arab League.
Kuwait ilikombolewa toka mikononi mwa Saddam, Bush baba akapata hadhi katika historia ya nchi hiyo babe sana duniani siku hizi. Uchumi ulikwenda vibaya mno,ukaja kurekebishwa na Bill Clinton baada ya kushinda Uchaguzi mkuu mwaka 1992.
 Bush Baba, aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi la Marekani(CIA)na alisaidia sana kuparaganyika kwa iliyokuwa Dola ya Kisovieti ya Urusi(USSR) zama za Mikhail Gorbachev.
Kuparaganyika kwa USSR,ilikuwa kupisha njia kwa Mataifa ya Magharibi na Umoja wa Kujihami wa Ulaya Magharibi(NATO) kupanua himaya yake hadi Mashariki, na ilikuwa ishara ya kumalizika kwa VITA BARIDI,kasha UKUTA WA BERLIN ukavunjwa,mwaka 1994.
Kitendo cha George Bush(mtoto)kumnyonga Saddam,ilikuwa kurejesha heshima ya nyumba yao katika Taifa hilo babe sana duniani. Marekani ilivumbuliwa na Christopher Columbus,OKTOBA 12, MWAKA 1492, na ikaja kutangaza uhuru wake Julai 4,mwaka 1776. Juzi walisherehekea miaka 236 ya uhuru.
Sasa, tuchambue Ufunuo 18:11-18. Marekani ilipata uhuru na ikawa nchi kimbilio kwa waliosetwa na tawala katili sana.
Lakini, ilikuja kuwa nchi katili; na ikaanza kufanya mapenzi ya JOKA ambaye ni Ibilisi mwenyewe,pale ilipopindua marais wa mataifa mengine kwa jeuri. Hawa ni pamoja na Jenerali Manuel Noriega wa Panama na Salvador Allende wa Chile, wakamweka kibaraka wao Dikteta, Pinochet.
 Licha ya kupindua serikali za Panama na Chile kama nilivyokwishaandika katika makala zilizotangulia, Shirika lao la CIA lilishirikiana sana na manyang’au kama Dikteta Mobutu  wa Zaire kuua wanamapinduzi wa Afrika, akina Patrice Emely Lumumba.
CIA ilishirikiana na Makaburu wa Afrika ya Kusini kuwawinda wanamapinduzi wa Afrika ya Kusini,ili Botswana, Namibia,,Angola,Msumbiji na hata Afrika ya Kusini waafrika wasijitawale wenyewe.
 Ndani ya Angola,Chama cha MPLA na FNLA vilipambana wakati FNLA wakipewa msaada na CIA hadi uhuru ulipopatikana kutoka Ureno mwaka 1975. Jonas Malheiro Savimbi alikuwa kibaraka wa Marekani,ili kuvuruga maendeleo ya nchi, hadi walipomumwaga juzi juzi  akaachwa kupigwa risasi na majeshi ya serikali. Jambo hili alishalisema Kamara Kusupa.
MMarekani iwe chini ya Barack Obama ama Mgombea wa Republican,Mitt Romney, ina akili ile ile, ya kunena kama Shetani(Ufunuo 13: 11) yaani ubabe wake na kulazimisha watu kile wanachotaka wao.
Angalia, kwamba CIA waliwasaidia Makaburu wa Afrika ya Kusini kuwaua wanafunzi 250 katika kitongoji cha SOWETO(South West Township) mwaka 1976,mjini Pretoria.
Turejee Irak, ambayo baada ya Saddam hamkani si shwari. Nchi imegawanyika sasa ni baina ya dini na dini;msikiti kwa msikiti,ukoo baina ya ukoo wanapambana.
Watu wa Madhehebu ya SUNNI mwaka 2007 walikuwa milioni 3.8 baada ya Saddam ambaye pia alikuwa Sunni kunyongwa. Hawa wako Magharibi.
Wakurdi, ambao Saddam alidaiwa kuua walikuwa milioni 4.4 nao wanaishi Kaskazini  Mashariki mwa Ninawi,ule mji mkubwa aliokwenda kuhubiri Nabii Yona akamezwa na Nyangumi!
 Washia, nao ni milioni 8.4 wanaishi Babeli hadi Kusini Mashariki mwa nchi. Mjini Baghdad na Kati kati mwa nchi kuna watu wa dini mchanganyiko wapatao milioni 9.2.
Najaf na maeneo ya utajiri wa mafuta ni maeneo ya Washia ambao wamewekewa chuki na SUNNI,huku Bush,Obama na hata Mitt Romney(Mgombea wa Republican) wanaweza kuhangaika kurejesha amani,bila mafanikio…ni vita hadi kiama!
Dola lenye nguvu kandoni mwa Mto Frati,lilikuwa limevunjika ili kutoa nafasi kwa madola ya Mashariki kuungana na NATO na European Common Market, ama EU ili kuungana na Marekani kuandaa serikali moja ya Dunia.Huku ndiko kukauka kwa Mto Frati.
 Angalia nchi zilizo Mashariki mwa Mto Frati:Pamoja na nchi zilizokuwa katika Muungano wa Kisovieti(USSR), na Afghanistan,Pakistan,China,India,Korea Kaskazini na Kusini na Japan leo zinalazimishwa ama zinaungana na Marekani kwa hiari katika biashara na katika mambo mengi.
Kabla ya VITA BARIDI kwisha, hali ilikuwa tofauti. Jumatatu, Januari Mosi mwaka 2007, Romania na Burgaria zilijiunga na NATO(Northern Atlantic Treaty Organization); ilikuwa SIKU MOJA tu,baada ya Saddam  kuzikwa. Unabii unatimia bila kukosa.
 Bado Iran na Korea Kaskazini, na Syria itavurugwa kama nitakavyoonesha punde.
Kwa mujibu wa mwqandishi wa Iran anayeishi jijini Paris, Amir Taheri, Yule gaidi wa kale, Carlos The Jackal, alisema Marekani ni “Shaytan” yaani Shetani ama Joka(rejea Ufunuo 13:11) yaani Shetani amejivika mwili wa Marekani ili kuuhadaa Ulimwengu.
 Imesemwa kwamba waumini wa dini ya Kiislam wanapaswa kuichukia Marekani kama Shetani anavyochukiwa pasipo kuulizwa!
 Nirejee kidogo katika Historia ya Carlos ingawa nimeijadili kwa utulivu mwingi katika makala zilizotangulia.
Alizaliwa Oktoba 12,mwaka 1949. Katika kitabu kiitwacho Revolutionary Islam Editions Du Rocher,2003 yeye anadai ni Muislam huko gerezani,Ufaransa.
Babaye alikuwa mwanasheria milionea wa Venezuela,nchi ya Hugo Chavez. Carlos alimkubali sana Osama bin  Laden, na alisoma Patrice Lumumba University,huko Moscow. Hiki ni Chuo Kikuu kilichoanzishwa na Shirika la Ujasusi la Urusi,KGB,ili kuwafundisha wanaharakati wan chi za Dunia ya Tatu,
 Amefanya harakati nyingi mahali pengi kwa miaka 20 hivi, Urusi ilipoparaganyika, akaanza kujificha-ficha, hadi Makachero wa Ufaransa wakaja kumkamata mjini Khartoum, Agosti 14,mwaka 1994.
Alisafirishwa chini ya ulinzi mkali hadi Paris ambako amefungwa maisha. Nataka ujue kwamba 1994 Ukuta wa Berlin uliangushwa na kuondoa Kambi mbili za watu kuashiria kwisha kwa VITA BARIDI,na Marekani kuanza kutawala Dunia,huku Carlos akakamatwa, ambaye pia alipinga mno maslahi ya Magharibi. Umeona?
 Carlos aliwahi kutabiri mambo ambayo yametokea kwa usahihi kabisa. Ametabiri Irak kujengwa upya na Marekani, ametabiri SYRIA kuvunjika vipande vipande, na sasa tunaona vita vikali baina ya majeshi ya kigeni yanayounga mkono waasi na serikali inayoungwa mkono na Urusi na China.
 Ametabiri Lebanon kuanguka na kikundi cha HEZBOLLAH kuharibiwa.Ametabiri Kossovo kuwa huru na kwamba SUDAN(sasa Kusini na Kaskazini) itafanyiwa usanii ili kusukwa upya,hili limetimia,Sudan ni mbili siku hizi.
Ametabiri Ufaransa nayo kusambaratika na kuwa vinchi vidogo-vidogo.Mwisho wa siku Carlos anadhani ni Iran na Korea Kaskazini tu zitakazompinga Marekani.Anasema vita vya kumpinga Marekani vitakuwa virefu sana, na Marekani watashinda sana, anawataka Waislam kufanya JIHAD dhidi ya Marekani kuwa Nguzo Kuu ya Uislam,swala,kufunga,Hija huko Mecca N.K
Alimpenda Sana Rais wa Algeria, Azizi Bouteflika na kumwita,”Kaka yangu mpenzi” na Osama alimwita, “Sheikh” na anaogopa Algeria nayo kumezwa na ubeberu wa Magharibi
Hata hivyo, Carlos hakujua Algeria ilishaungana na Marekani na NATO pamoja na mataifa mengine ya Kiarabu,na Israeli katika urafiki unaoitwa, Partnership for Peace.
Leo, wapo wanaharakati wanaoitwa magaidi walioanzisha JIHAD dhidi ya Marekani na washirika wake.
 Hata hivyo, unabii wa Biblia na hata Carlos tumemwona akitabiri ushindi kwa Marekani,kwani unabii wa Biblia aslani hausemi uongo.
 Tijadili kidogo dhana ya kujitoa mhanga kupambana na Marekani na mabeberu wenzake.
Ni kweli Marekani wanafanya uchafu na unyama duniani. Hata hivyo kwa Wakristo,kupambana na adui kwa kumuua ni dhambi,maana Yesu alikataa chuki na uadui,sembuse kujitoa mhanga?
 Tazama Mathayo 5:43-48 na hata ule ujumbe wa Yesu kwa Petro kurejesha kisu halani mwake.
http://t1.gstatic.com/images?q=tbn:ANd9GcQ4ReGUJS-eIQo4btbH93_4esyBSMHz2WBcOkoPyledUnQMccWUCarlos The Jackal akiwa na pingu
 Itaendelea
0786 324 074