Wednesday, June 27, 2012

makomandoo wa Israeli walivfosafiri
filamu ya Raid on entebbe

nchi ya mwarabu

----

VITA JERUSALEM YA KALE HADI MPYA


      
KABLA ya kuendelea na tukio la Makomando 100 wa Israeli kuwakomboa mateka wao, Entebbe, Julai 4mwaka 1976, tuangalie tukio la juzi la ugaidi,Mombasa.
Mombasa,juma lililopita, magaidi waliua watu wasiopungua watatu katika Hoteli moja, walipokuwa wakitazama mechi ya Soka,kati ya Italia na England.
Aghalabu, matukio ya kigaidi yamekuwa yakitokea katika Jiji la kitalii la Mombasa,katika Pwani ya Kenya.
 Novemba 28, mwaka 2002,magaidi wa Kipalestina walishambulia Hoteli ya kitalii ya Paradise iliyoko Kikambala,takriban kilomita 25 kutoka mjini Mombasa, wakaua watu.
 Magaidi hao hao walijaribu kuirushia kombora ndege ya Israeli ya Arkia Airlinesiliyokuwa ikiruka kutoka Uwanja wa Ndege wa Moi, hapo Mombasa. Jaribio hilo la kigaidi halikufanikiwa.
Naam, nataka msomaji amaizi kuwa vita baina ya Israeli na Wapalestina, vilishapiganwa maradufu katika ardhi ya Afrika Mashariki.Msukosuko wa Mashariki ya Kati ulishaleta dhama kubwa katika Dunia nzima.
Agosti 7,mwaka 1998,Balozi za Marekani Tanzania na Kenya zilishambuliwa na magaidi wanaohisiwa al-Qaeda, na kupoteza maisha ya watu zaidi ya 200.Hawakuwemo Wazungu wala Mayahudi, bali Waafrika tu.
 Kampala, haikulipuliwa wakati huo,kwa sababu ndiyo kwanza vikosi vya Marekani vilikuwa na program kamambe ya mafunzo ya kijeshi mjini Kampala,kumbe Kampala ilikuwa, “More alert” kuliko Nairobi na Dar.
Naam,vita kati ya al-Qaeda Israeli kwa upande mmoja, na kati ya Waarabu na Marekani na Ulaya  na wajomba zao Israeli,kwa upande wa pili,havina mipaka ya Kijiografia.Vita hivi vitadumu muda mrefu,kama tutakavyoona mbele ya safari.
Uganda, wakati wa Dikteta,Field Marshal Idi Amin Dada,iliwasaidia wateka nyara wa Kipalestina kufuatia urafiki wake na Waarabu, na ni uadui mkali  kwa Israeli na Magharibi.
Turejee kidogo Entebbe,usiku wa kuamkia Julai 4,mwaka 1976.Muda kitambo baada ya makomandoo 100 washirika wa Mossad,kumtia adabu Amin,Marekani walituma ndege Uganda,naam Entebbe, ili kuwasaidia majeruhi wa Operesheni ile kamambe.
 Unajua, maofisa 53 wa Ubalozi wa Marekani walishikiliwa na wanamgambo wa Kiislam mjini Tehran,huko Iran.
Wateka nyara wa Kipalestina waliuliwa katika tukio hilo la Entebbe, na kabla ya kukumbwa na mauti walisikika wakitaka Israeli iwaachie huru Wapalestina 40 walioshikiliwa nchini Israeli.
Hadi sasa akina Mahmoud Abbas na Benyamin Netanyahu, wanazungumza hay ohayo hata baada ya kifo cha Yasser Arafat.
 Naam vita vya kisasi vya miongo mingi.Hadi sasa Israeli napambana na wanamgambo wa Kipalestina, na wakati mwingine ndege zimetekwa ama zimejaribiwa kulipuliwa angani-VITA VYA KISASI.
 Waama, nipende kusema basi kwamba,Mossad ni majasusi hodari duniani kupambana na uadui wa Waarabu wengi duniani. Unajua kuna Waisraeli milioni nane tu huko Israeli?
Kamanda wa Operesheni ya Entebbe, Muki Besta, alikiri kwamba Operesheni ya Entebbe ilifanikiwa kufuatia ukusanyaji wa data nyingi na muhimu wa Mossad.
Msomaji wangu, Nyalapa, aliniuliza Mossad walipataje ramani ya Entebbe hadi kuweza kushambulia ngafla na kuokoa mateka?
 Hata kama Israeli waliujenga uwanja huo wa ndege wa Entebbe,bado wangeweza kuingia Uganda na kupiga picha muhimu na kujiondokea,pasi na kushtukiwa.
Katika nchi za watu wazembe,wasio na uzalendo,wapenda rushwa na wazalendo wa matumbo yao wenyewe,  Mossad, CIA,MI5,MI6,BOSS la Makaburu ama majasusi wengine wangeweza kufanya lolote na kuondoka,kwa nguvu ya pesa,ama kwa kutumia ulegefu wa fikra.
 Ungedhani, hawa ‘NJAA TUPU’ wanaohujumu fedha za umma katika Halmashauri zetu, wangeweza kulinda maslahi ya watu?Na wengine hupiga kelele nyingi  za hasira,kwa kuwa matumbo yao yangali na njaa! Hasira hutuka tumboni mwa wenye njaa!!
 Ulimwengu wa Kiarabu unasalitiana mno siku hizi. Miaka ya 70 Waarabu walishikilia uchumi wa Dunia kwa silaha moja tu-Mafuta.
Mchora katuni wa Kidachi aliwahi kuchora Mwarabu akiwa kawaweka ‘Chini ya Ulinzi’Wakuu wa Mataifa babe sana Ulaya na Marekani kwa kutumia “Pampu” ya mafuta.
Mafuta ni silaha ambayo siku hizi imesalimishwa Magharibi na Mwarabu mwenyewe,wanaobisha wanakiona cha mtemakuni,nao ni Saddam Hussein,Gaddafi na wenzao.
Mwaka 1976, Ujerumani iliongozwa na Kansela Willy Brandt,Ufaransa iliongozwa na Rais Georges Pompidou,Uingereza ilikuwa chini ya Waziri Mkuu,Edward Heath na Marekani ilikuwa chini ya Richard Milhous Nixon,kabla ya kashfa ya ‘Watergate’. Unaifahamu?
 Unatazama nini kuona viongozi hawa kuwekwa chini ya ulinzi kwa pampu ya mafuta ya Mwarabu,mwaka 1973? Bila shaka,utaona baada ya hapa hawa mabepari wakifanya juu chini kumpora Mwarabu mafuta,kwa kutumia kila njama, hapo upo?
 Nilikwishaandika katika safu hii,kwamba makampuni makubwa sana ya mafuta,”SUPERMAJORS” kutoka mataifa haya na mengine rafiki, yalishafanya Mapinduzi hadi kushikilia siasa za mafuta(Oil Politics) za Mashariki ya Kati.
  Lengo ni kuishikilia ‘silaha’ hii iitwayo, Dhahabu Nyeusi. Viongozi wa Saudi Arabia,Irak, Abu Dhabi,Kuwait,Libya na Algeria, ama wamepinduliwa na kufumbwa midomo, ama wamewekwa mfukoni,waachane na misimamo mikali ya Waarabu.
 Unajua sasa,ni kwanini Iran, Syria,Yemen,Misri na wenzao wamefanyiwa ‘ukarabati’kwa kisingizio cha Demokrasia na Haki za Binadamu,wengine watauawa tu.
 Angalia uhusiano wa Paka na Panya kati ya Urusi ya kale(USSR)na Marekani,Venezuela ya kichwa maji Hugo Chavez,Nigeria,Uingereza, Indonesia,China, Mexico ya madawa ya kulevya na Ecuador. Hizi ni nchi za mafuta.
Maskini, Yoweri Kaguta Museveni, nchi yake itakapofika katika kilele cha uzalishaji wa mafuta, na akawagomea wakubwa hawa,utawala wake utakuwa hatarini maradufu,kuliko sasa polisi wanapowatomasa wanawake matiti,wakubwa wamemnyamazia tu.
  Wee washikie wakubwa bango la mafuta,utakiona cha mtema kuni.Marekani na washirika wake wa NATO ni ‘rafiki maslahi’ na aslani, hawana udugu na mtu masikini; hawafiki Somalia wala Syria,kama hakuna almasi,dhahabu,gesi ya kutosha na mafuta.
  Unapokuja mzozo wa Waarabu na Israeli, Marekani na wenzake hujidai hawaoni uvunjaji wa sheria Israeli maana kuna kanchi kadogo ka mchanga mtupu-wanakodolea jicho nchi za Waarabu,kuna mafuta chini ya ardhi.
  Mwezi Feburuari, tarehe 21 mwaka huu,niliandika katika safu hii kwamba hata Vatican City,Makao Makuu ya Kanisa Katoliki walishakubaliana na Israeli uhusiano wa Kibalozi. Ilikuwa Desemba 30 mwaka 1993.
 Gidion M. alikuja na jina la makubaliano hayo kuwa ni ‘FUNDAMENTAL AGREEMENT’lengo ni kufungua mazungumzo zaidi kati ya Mayahudi hawa na Kanisa Katoliki,lengo ni kukomesha ‘kiherehere’ cha Mwarabu.
 Vatican wanapoungana Marekani,Israeli na Ulaya iliyokuwa dola ya Rumi wakiungana pamoja na Israeli,maana yake ni kwamba Ulimwengu wa Kiarabu utasimama peke yao?
Wengine wanasema Urusi na China. Hawa nao ni wafanyabiashara wa mafuta tu-wanapopewa zabuni ya faida kubwa Mwarabu akipigwa kinyama,watakataa? Usiseme Syria,hakuna unono kama Iran bwana!
 Mwarabu yuko hatarini,kutekwa na kubinywa katika dini yake,utamaduni wake na uchumo wake uliomo katika mapipa ya mafuta ghafi.
 Mzungu anapata ushindi mnono katika medani za kijeshi na siasa, ‘bao la kisigino’ linafungwa,wakati Waarabu hawako tena pamoja,wamefungwa OPEC.
 Unabii wa Ufunuo 9 ulishatimia zamani. Kwamba,nguvu za wanamgambo wa Kiarabu zilizoitesa Ulaya miezi mitano ya kiunabii(miaka 150) hazipo tena Tazama Ufunuo 9:1-11.
 Ottoman Empire haipo, Istanbul siyo tena mji wa Waarabu,ni mali ya Mzungu, adui wa Mwarabu,ndiyo maana Uturuki na Syria  ni mahasimu tu.
 Kulingana na Unabii wa kitabu cha Ufunuo 13,Ulaya na Marekani zitapata ushindi dhidi ya dola za Mashariki,na wataunda Umoja na serikali yenye kuwabagua watu wasiowapigia magoti, watawafanya kama Sadaam, Osama ama Gaddafi, watu watafungwa maisha kama Carlos The Jackal, wengine watawekewa vikwazo vya uchumi(Tazama Ufunuo 13:15).
Umoja wa Mataifa(UN) ullishashindwa kutoa maamuzi ya haki uwanjani-Marekani,Israeli na Ulaya wanacheza ‘rafu’ sana lakini hakuna hata mwamuzi wa pembeni kunyanyua kibendera! Hujipendi?!
Hii ni AJENDA YA SIRI.Al-qaeda,al-Shabaab,Black SEPTEMBER na magaidi wa Kiarabu mwisho wa siku watatokomezwa na vikosi hivi vya CIA,FBI,MI5,MI6,MOSSAD na hata KFB la Urusi likijai kuwasaidia Iran,litauza siri Tel Aviv ama Pentagon.
Asilimia 80 ya Waisraeli wanaabudu dini ya Kiyahudi na  asilimia 15 ndiyo Waislam wa madhehebu ya SUNNI.
Israeli ina watu milioni nane na ardhi ni finyu. Ilijitangazia uhuru Mei 14 mwaka 1948 katika uadui mkali dhidi ya jirani zake Misri,Jodan,Syria,Irak na Saudia.
Jerusalem ilishagawanywa Mashariki na Magharibi, na hapa ndiyo kitovu cha uadui na vita. Vita vilivyokuja kupiganwa hadi Rntebbe Julai 3,mwaka 1976 ili kuwakomboa mateka 103 wa Israeli,tumewaona makomandoo 100 walioandaliwa vema na Mossad wakimkomesha Mwarabu na rafiki yao Amin Dada.
Naam, vita vya dakika 90 tu, The 90 minutes at             Entebbe. Kwa Israeli, Waziri Mkuu anayekuliana na Waarabu ili kuleta amani anauliwa kama Yizak Rabin aliyepigwa risasi Novemba 4 mwaka 1995.
Itaendelea
0786 324 074
 

Thursday, June 21, 2012

israeli dhidi ya waarabu




 *Mashariki ya Kati ni “Focal Point” ya Dunia
 
VITA vya karne nzima, baina ya Waarabu na Israeli kwa upande mmoja, na mnyukano baina ya Waarabu na Mataifa Makubwa ya Ulaya na Marekani kwa upande wa pili, hatimaye madhara yake yamefika kila Bara,kila nchi.
  Katika makala nyingi zilizotangulia,nimeandika sana juu ya Misri ya Anwar Sadat alivyofanya shambulizi la kustukiza huko Israeli, Oktoba, mwaka 1973.
  Nimeandika pia mnukano wa makundi ya wanamapinduzi wa Kipalestina kumenyana na Mataifa ya Magharibi kwa staili ya ‘kigaidi’ zama za  Carlos The Jackal.
Nimeandika vita Baridi kufika hatma yake wakati wa Kuanguka kwa Ukuta wa Berlin mwanzoni mwa miaka ya 90,na kusambaratika kwa Dola la Kisovieti la USSR.
 Juma lililopita nimejadili matukio ya kigaidi ya Black September kuwasaka adui zao Waisraeli hadi Munich,Ujerumani, Septemba 5, mwaka 1972 wakati wa michezo ya Olimpiki.
  Kutoka zama za Black September, yaani Septemba ta utusitusi hadi sasa, akiina Carlos The Jackal wameishia kifungoni, akina Saddam Hussein, Muammar Gaddafi, Osama bin Laden na wenzao wamezimwa kwa mapinduzi ya kijeshi na wamelala makaburini,kufuatia jeuri na mtutu wa bunduki za rashasha.
 Tunakoelekea, mazungumzo ya Amani kama yale ya Camp David mwaka 1973 kati ya Israeli na Waarabu kwa upande mmoja, ama kati ya Waarabu na Ulaya na Marekani, hayatakuwa na maana zaidi ya kulazimishwa kusalim amri mithili ya kijibwa mbele ya dubu mwenye kiu ya damu.
  Naam, Waarabu kujisalimisha kwa njia ya kuufyata mkia mithili ya kijibwa mbele ya fisi,mbele ya Dola babe,jeuri na fisadi za Magharibi!!
Nguvu za Mataifa ya Kiarabu zinatindika sana. Nguvu hizi zilikuwa ndani ya pampu za mafuta katika miaka ya 70. Nguvu hizi zilikuwa katika majambia ya wanamgambo wa Kiarabu katika karne ya Sita hadi karne ya 15.
  Siku hizi, makampuni ya mafuta ya Marekani, Ufaransa, Uingereza, Italia,Uholanzi n.k yanahafifisha ‘nguvu’ za mataifa haya yanayozalisha sana ‘dhahabu nyeusi’ hii duniani. Majambia ya Wanamgambo wa Kiarabu yaliyofananishwa na “Mikia ya Nge”(Tazama Ufunuo 9:7-11) yamegeuka kuwa nyasi.
 Kitu kinachoweza kuonekana katika muktadha huu ni kile kiitwacho, “The Modern Middle East Oil Politics”.
   Nataka kusema kwamba, ‘Oval Office’  iliyoko White House chini ya Bwana Barack Obama, lengo lake ni kuhafifisha nguvu za uchumi(mafuta) wa Milki za Waarabu ama mataifa ya Mashariki ya Kati, huku akiibusu na kuikumbatia Israeli, wakati ‘Intifada’ nyinginezo ni maumivu kwa Mwarabu.
Shirika la Atomiki Duniani(IAEA)limearifiwa na maofisa wa Usalama wa Israeli kwamba Iran siku hizi inajidai kuweza kurutubisha zaidi ya kilogramu 630 za Uranium, ili waweze kutengeneza bomu la Nyuklia katika hatua za awali.
  Hata mataifa mengine ya Kiarabu ya Ghuba, kama Saudi Arabia na Bahrain yako tayuari kuwaunga mkono Marekani na Ulaya kuichakaza Iran ili isijitie ‘kidume’ na kughairi Amri Takatifu za Marekani,Ulaya, Israeli na NATO za kuachana na mradi wa Nyuklia.
  Iran itashambuliwa haraka sana isipojisalimisha chini ya mamlaka za Mzungu tapeli, ambaye hata sasa amezikalia Irak, Libya, Afghanistan, Misri,Libya,Syria na Mzungu anavuka Mto Frati na Tigris kuelekea kwingineko Mashariki.
  Leo, tuanze kulijadili Shirika la Ujasusi la Israeli, MOSSAD, ambalo nembo yake ni Vinara Saba vya Taa vilivyoanza kutumiwa na Waisraeli tangu zama za Nabii Musa, mwaka 1500 BC.
Mossad,ni majasusi hatari duniani ambao hujuma zao zimetamalaki hadi Afrika ya Mashariki tangu mapema mwaka 1976.
Tujadili kidogo mapambano baina ya Chama cha Ukombozi cha Palestina, POPULAR FRONT FOR THE LIBERATION OF PALESTINE (PFLP) dhidi ya Israeli na washirika wake wa Magharibi; vita vilivyopanuka hadi kufika Entebbe,Uganda miaka ya 70.
Vita kama hivyo vingalipo leo baina ya Al-Shabaab,al-Qaeda dhidi ya maslahi ya Magharibi hata hapa Afrika ya Mashariki.
   Entebbe,Uganda tuliona mapambano ya PFLP wakati ule Carlos The Jackal akiongoza hujuma tele dhidi ya Magharibi.
 Ndege ya Ufaransa, Air France Air Bus A 300,iliyokuwa na nambari za Usajili BVGG ilijikuta ikitekwa nyara Juni 27 mwaka 1976.
  Sasa, Uganda wanakumuka miaka 36 kamili ya tukio hilo la kihistoria. Ndege hiyo ilitokea Athens, Ugiriki inayofilisika, ikalazimishwa kwenda kutua Entebbe.
 Ilikuwa na jumla ya abiria 248 na wafanyakazi dazeni,ilitekwa na Wapalestina wawili walioshirikiana wa PFLP kitengo cha Operesheni za Nje kiitwacho PFLP-LEO, na walisaidiwa na Wajerumani wawili wa kikundi cha kimapinduzi  cha German Revolutionary Cells.
Wilfred Bose na Brigite Kuhlmann. Ilikuwa saa 6:30 hivi mchana, Juni 26 kama leo mwaka 1976 ndege hiyo ilipotekwa angani ikalazimishwa kwenda kutua mjini Benghazi,Libya.
 Zama za Muammar Gaddafi, ndege hiyo ikatua Benghazi na kujaza mafuta,ikapumzika kwa muda wa saa saba.
 Mwanamama raia wa Uingereza aliyekuwa mjamzito akajidai kuumwa utungu wa kuzaa mtoto, akaachiwa huru hapo Beghazi,kabla ya safari ya Entebbe,kuanza.
  Nataka msomaji atambue kwamba kuachiwa huru mwanamama huyu kulifikisha habari mjini Tel Aviv mapema, wakaanzisha mkakati kamambe wa kuwakomboa mateka wao katika ardhi ya Uganda.
  Saa tisa na robo, siku iliyofuata, yaani Juni 28 mwaka 1976 hiyo Air Bus ilitua Entebbe, wale mateka wengine ambao nao hawakuwa Waisraeli wakaachiwa huru-kosa lingine.
 Maana yake ni kwamba, serikali ya Israeli ilimaizi kuwa raia wake ambao walikuwa mikononi mwa watekaji wa Kipalestina, walikuwa mikononi mwa mauti. Hivyo, Waziri Mkuu wan chi hiyo akalazimishwa kufanya kila njia waokolewe, hata kama kufanya hivyo kulikuwa kukiuka sheria za kimataifa,kama ugaidi ama mashambulizi ya kijeshi dhidi ya nchi nyingine.Wewe ungeanza mazungunzo ya kidiplomasia ya akina Thabo Mbeki au Kofi Annan.
 Makomando wa Israeli walitua Entebbe,Uganda, na kumshikisha adabu Idi Amin Dada aliyejitia Mshindi wa Dola ya Kingereza,Mwanamasumbwi nguli na Field Marshal.
 Rais wa Maisha wa Uganda alikiona cha mtema kuni mbele ya makomando 100 wa Israeli.Wakati huo Uganda ilikuwa rafiki wa Waarabu, na walijifanya adui wa Israeli.Akina Ghaddafi na Palestina walimponza Amin,
Yule mwanamke wa Kiingereza na mateka wengine walipoachwa, wakasema kupitia vyombo vya habari,kwamba huenda mateka wale wa Israeli wangeuliwa kinyama mkononi mwa adui zao Wapalestina.
 Basi,Makomando walifanya mazoezi kwa muda mfupi wakafika Uganda usiku ili kukomesha kiburi cha Dikteta aliyejifanya mbabe katika medani ya vita. Zama za Waziri Mkuu,Menachem Begin, Shirika la kijasusi la MOSSAD likawezesha makomando wenye vinara saba vya taa(Mwangaza Mkamilifu) kutua Entebbe kwa saa moja na nusu tu na kufanikiwa kuwakomboa mateka wake.
 Hii Operesheni ina majina mengi, inaitwa Operation Thunderbolt, wengine huiita kwa jina la Komando aliyeuliwa pale, Jonathan ama  ‘Yonnie’ Huyu Jonathan Netanyahu alikuwa ndugu wa damu wa Waziri Mkuu wa sasa wa Israeli, Benyamin Netanyahu.
  Wengine tumeiona Operesheni hii kwenye Filamu ya RAID ON ENTEBBE na tumepata kusoma kitabu kiitwacho, 90 Minutes at Entebbe. Usinisumbue kuuliza wapi utakipata!!
  Luteni Kanali Jonathan ‘Yonnie’ Netanyahu alikufa Entebbe,lakini walifanikiwa kuondoka na maiti yake na akazikwa kishujaa.Abiria 103 waliokuwa mateka Waisraeli mikononi mwa adui zao Waarabu, walikombolewa hatimaye. Hawa 103 walikuwa miongoni mwa abiria 248 wa ile Air Bus ya Ufaransa.
 Ni usiku wa manane hiyo Operesheni ilipofanyika Entebbe,kilomita kama 27 kutoka Kampala, Amin hakujua aliamkia kupapasa maiti za askari wake 45 asubuhi, wakati makomando walishaondoka mapema kabla ya alfajiri.
 Uwanja wa ndege wa Entebbe uliharibiwa kwa mabomu  wakati watekanyara wote walifyekwa kwa risasi za makomandoo wa Israeli.
 Ngege iliyowaleta Makomandoo hawa iliruka kwa takriban kilomita 4000 hivi ikawaleta makomando 100 waliokata mzizi wa fitina Entebbe.
 Makomando watano walijeruhiwa,mmoja akafa lakini askari wa Amin 45 na wateka nyara wote walipigwa risasi, mateka watatu walikufa pia.
 Ndege ya Kirusi MIG-17 ilisambaratishwa vibaya.
 Itaendelea




0786 324 074