Wednesday, September 25, 2013

MAKOMANDOO WA NAIROBI NOMA

Soldiers take their position in an attempt to end the four-day siege at the Westgate shopping mall in Nairobi. (© Reuters)

UGAIDI NAIROBI NOMA

Teenager 'played dead' to survive Kenya mall carnage

KAGAME NA MUSEVENI NI NOMA



APRILI 6 mwaka 1994,Rais wa Rwanda, Juvenal Habyariana, na  mwenzake wa BurundI,Ntaryamirwa Cyprian, wakiwa ndani ya ndege aina ya Falcon-50, wakatunguliwa kwa kombora na Waasi wa Kitutsi,RPF.
Huu ndiy mwanzo wa mauaji ya Halaiki ya Rwanda,nakichocheo cha vita Burundi na hata Mashariki mwa Congo,JK Kongo.
Migogoro ya Watu-tsi na Wahutu,inayotiwa mafuta na Mabwana wa Vita(WAR-LORDS)Paul Kagame na Yoweri Kaguta Museveni,sasa cheche zake hutishia hata amani ya Tanzania.
Wakimbizi maelfu wanakimbilia hapa Tanzania,kufuatia vita baina ya Wahutu na Watu-tsi wa Rwanda,Burundi na hata walewaliotimkia Jamhuri ya Kongo,kwa sababu na muda tofauti.
Tuwatazame wanaojiita Waasi wa Congo,M-23,CNDP na FDRL wanaosababisha Jenerali Kagame aanze kututukana huku.
FDRL(Democratic Forces for The Liberation of Rwanda) ni kikundi cha wanamgambo wa Kihutu ambao ni adui wakubwa wa KAGAME na nduguze Watu-tsi.
Kama jina lao lilivyo,baada ya mauaji ya halaiki, wakatimkia Congo ambako hata leo wanaota kumtimua Kagame mamlakani.
Hawa,ni Wahutu(raia wa Rwanda0 wanaompinga Kagame.
Sasa,Rais Jakaya Kikwete akiwa Addis Ababa, akamshauri Kagame ambaye naye alihudhuria moja ya mikutano ya AU kukaa meza ya mazungumzo na hao Waasi wa Kihutu wa FDRL ili kuleta amani na utangamano Maziwa Makuu,likawa kosa kubwa kwa Kagame na kuanza kurushamakombora ya  kama alivyozoea.
Kingalipo kikundi kingine cha wanamgambo wa Majimaj(Mai mai) ambacho pia kimejichimbia misitu ya CONGO ,kinapeleka mauti huko Jamhuri ya Congo,kinaitwa ADC.
Ndani ya Congo kuna jamaa zake Kagame na rafikiye,Museveni yaani M-23.
Jina hili hutokana na tarehehe 23 Machi mwaka 2009,siku ambayo serikali ya Congo ilifikia makubaliano ya Amani na kundi la Waasi wa CNDP,wakajumuishwa katika majeshi ya serikali.
Naam, hawa ndiyo M-23 Movement ambao ni kikundi cha Waasi kama 5,500 hivi waliojichimbia Kivu ya Kaskazini na kuuza kifo kwa raia wa Kongo,na hapa kwetu wamesababisha kilio kwa kupoteza wanaeshi wetu.
Wametokana na misuguano isiyoisha baina ya serikali ya DRC na hawa wanaojiita Waasi kwenye mipaka ya Uganda,Rwanda na Burundi.
Hawa M-23 wametokana na CNDP(Congress for the National Defence) kilichoanzishwa na ‘jamaa’ za akina KAGAME na Museveni,mmoja anaitwa Jenerali Nkundabatware,Desemba 2006 huko Kivu.
Januari,2009 CNDP Kilikosa umuhimu,kikaparaganyika,hadi eti Nkunda akakamatwa na majeshi ya Rwanda,ambayo sote tunajua yalimpa chakula,nguo,fedha,silaha n.k
Sehemu ya kundi hilo Iliongozwa General Bosco Ntaganda, ambacho kiliingia mkataba wa amani na serikali ya Congo Machi 23, mwaka 2009.
Wapiganaji hawa walipounganishwa na jeshi la Congo,CNDP kikawa chama cha siasa,wanachama wao wakaachiwahuru magerezani.Rais wa kundi hilo akiitwa Askofu Jean-Marie RUNIGA Lugerero!
Utaona ‘maaskofu’ wa siku hizi wakiongoza vikundi vya wanamgambo na kuua raia! Jihadhari sana na wanaojiita Maaskofu,Manabii na Mitume wa siku hizi!!
Rais wa kundi la M-23 akiitwa ‘General’Makenga Sultan-wote hawa mabwana wa vita walikuwa CNDP.
Hawa hawakuwahi kuaminiwa na serikali ya mjini Kinshasa,hata baada ya makubaliano,Rais Joseph Kabila wa Kabange aliamuru Jenerali Nkunda akamatwe Aprili 11 mwaka 2012.
Hawa ni Watu-tsi,ambao ni adui wakubwa wa kile kikundi cha Wahutu cha Democratic Forces for the LIBERATION OF Rwanda(FDRL).Hawa wote wanaendesha harakati zao za kigaidi ndani ardhi ya Congo,ndiyo maana kuna shida kila kukicha.
Bila shaka, msomaji unapata picha kwamba, kuna vikundi vya Wahutu(FDRL) waliokimbia Rwanda wakati wa genocide, walitimkia Cogon a huko wanaendesha harakati za kumpinga Kagame.
Hawa Watutsi walimsaidia Papaa Kabila(baba0kumwondosha Mobutu madarakani, na baada ya vita hivyo,walijumuishwa katika majeshi ya serikali.
Hawa Watu-tsi, wanapokea msaada kutoka Rwanda na Uganda, eti sasa mazungumzo ya kuleta amani Congo hufanyika mjini Kampala chini ya usimamizi wa Kaguta Museveni! Kichekesho kikubwa.
Majeshi ya serikali ya mjini Kinshasa(FARDC) yamekuwa hayawezi kuwatimia hawa jamaa za Kagame na Museveni huko Mashariki mwa Kongo,kwa sababu ambazo sasa tayari umeziona kufuatia mfululizo wa makala haya.
Wakati mwingine, majenerali wa FARDC walijidai kujisalimisha kwa Waasi,wakawapa zana za vita na chakula katika kinachoitwa ‘mapigano makali’ ambamo Waasi wanawateka askari wa serikali!
Wanafanya usanii huo huku majeshi ya Umoja wa Mataifa(MONUSCO) yakiangalia hata ujambazi unaofanywa kwa raia wa Congo.
Hawa MONUSCO wakati mwingine kazi yao ni kupora madini na kuuza Ughaibuni,na wala siyo kulinda raia wa Congo kama walivyotumwa na Umoja wa Mataifa,
Baada ya majeshi ya Tanzania kujumuishwa katika jeshi la MONUSCO, sasa kampeni ya kuwaswaga hao M-23 inaleta tija,wanapigwa ilivyo,ndiyo maana wanasisitiza mazungumzo kuendelea Kampala,ili ikiwezekana warejeshwe jeshini Kinshasa,viongozi wao wapewe mishahara na serikali ili wadumu kufanya ujambazi!
Watanzania tunasema kwa uchungu mkubwa kwa sababu tumekwishamwaga damu ya askari wetu huko Kongo, tayari M-23 ni adui yetu wa dhati,ndiyo maana Kagame anachuki ya wazi kwetu.Ingekuwa heri Umoja wa Mataifa ungeongeza jeshi ili hawa waasi watwangwe vilivyo,wanapoingia Rwanda kupewa chakula,nguo na bunduki,Rwanda wapewe kibano!
Kuna njia tele za kuipa kibano serikali ya Kagame ikiwa ni pamoja na Vikwazo vya kiuchumi, ama kunyimwa msaada wa kijeshi na kuuziwa silaha na mafuta.
Kuishinikiza serikali ya Kinshasa kuzungumza na Waasi,wakati kukiwa na wakimbizi 200,000 au zaidi wanaokimbia mapigano huko Goma,kuna leta ukakasi.
Kagame akiambiwa kufanya mazungumzo na FDRL anakasirika;wakati hao M-23 wakitwangwa vikali na maiti zao kubanikwa na majeshi ya serikali, kelele zinapigwa za mazungumzo mjini Kampala!
Mazungumzo hayo yalianza Desemba 9,mwaka 2012.
M-23 ilianzishwa rasmi Aprili 4,mwaka 2012 wakateka Goma kirahisi sana,kabla ya Makomandoo wa Tanzania kuwachakaza vikali hao Waasi na kuwatimua Goma chini ya mwamvuli wa MONUSCO.
Hawa jamaa za Kagame sasa wamejificha Rwanda! Inasemwa wako mpakani,huku makombora yanapodaiwa kutua Rwanda ili kuwasindikiza huko,ama wanafanya mchezo wa kuchongea kwamba MONUSCO wameivamia Rwanda!
Rais Kikwete anapotaka Rwanda inayoongozwa na serikali ya RPF(ya Watu-tsi) kukaa meza moja na Waasi wa Kihutu,FRDL waliokimbilia Kongo ili kuongeza vurugu huko maana yake nini?
·       Kwamba,ni mazungumzo ya amani wanayotaka Kagame na Museveni na jamaa zao wa M-23 waongee na serikali ya mjini Kinshasa.Ni sawa na namna ambavyo Kagame angezungumza na FDRL ili kuleta amani Maziwa Makuu.
·       Hata RPF(Rwandan Patriotic Front) walipokuwa Waasi wa Rwanda walianza kuzunguza na Habyarimana.
·       Mazungumzo ya mani(Peace talk and cease fire agreement)mwisho huweza kuzaa mikataba ya amani(peace accord) na kuleta amani na utangamano kati ya nchi za migogoro.
Sasa tujiulize Kagame anapojidai kutuliza uhasama kati ya Watu-tsi na Wahutumbaada ya genocide mwaka 1994, anaposhauriwa na Kikwete kuzungumza na FDRL anakasirika nini?
Ili kuleta usalama Mashariki mwa Kongo Waasi wa M-23,CNDP,Maimai n.k wanapozungumza na serikali ya Kabila mjini Kampala, si busara pia Kagame kuzungumza na Wahutu wa FDRL mezani sasa ili kualiza vita Ukanda wa Maziwa Makuu?
Mbona hata Waundi wamekuwa wakipatanishwa na akina Nyerere,Mandela,Bill Clinton,Mwinyi n.k
 Hawa walitia saini makubaliano ya amani mjini Arusha mwaka 2000 chini ya Mandela na Clinton.
Ndiyo maana,wanamgambo wa Kitu-tsi walioko Kongo tunasema wametumumiwewa kuangamiza Wahutu waliokimbiliahuko! Wahutu nao ni binadamu,wahurumiwe.
Rais Kikwete anajua mambo haya, alipomwambia Kagame kuzungumza na FDRL ligusa kizinga cha moto wa visasi,moto ukalipuka.
Wapo watu wanasema:
“Kikwete,kama siyo kuropoka,imemhusu nini kuingilia Rwanda dhidi ya Waasi wa FDRL?”
Swali la kijinga kwelikweli!
Hawa waasi ama Wakimbizi wa Rwanda wanapokimbilia Kongo,hususan Wahutu wanapoleta balaa la vita huko, ama wanapokimbilia kwetu,Kagame na Museveni hawatakuja hata huku kwetu kuwasaka Wahutu ili kulipa kisasi?
Tumeeleza kisa cha mauaji ya Kanungu zama za Kibwetere.
Tumezungumza umuhimu wa Amani Maziwa Makuu.
Wanamgambo wa Intarahamwe-adui za Kagame-ni wakimbizi wa vita kama wakimbizi wengine.
Sheria gani inasema wawindwe na kuuliwa tena katika ardhi ya Kongo?
Kwa nini wasizungumze kama Kongo wanavyozungumza?
Mbona tunazuia genocide(1994) ili kufanya genocide nyingine dhidi ya Wahutu wa FDRL?

R




TUNAHESABU MAITI ZA MAGAIDI


 
·    Al-Shabaab! Al-Qaeda?
Tumechoka kuhesabu maiti
                      
        Na Conges Mramba

MATUKIO ya Ugaidi yaliyotokea jijini London ,Uingereza, na kuua zaidi ya watu 50 mwaka 2005, yanaonyesha kuwa Tony Blair na George Bush, wakati huo walikuwa wameshindwa kudhibiti ugaidi kwa matumizi ya nguvu(Aggressive power); badala yake kilichotakiwa sasa ,ni njia za kidiplomasia.
Diplomasia haikutumika wakati huo,wala haikutumika wakati waSeptember 11 huko Marekani.
Dunia,ikiwemo Afrika,hususan Bara la Afrika tenaMashariki huku,tumeumia maradufu kufuatia kipigo cha magaidi!

Tangu matukio ya Septemba 11,2001 yametokea matukio makubwa mengi sana ya ugaidi duniani; na  nchi za Iraq na Afghanistan  ziliposhambuliwa na Majeshi ya Uingereza na Marekani na kisha kupinduliwa, hakuna amani iliyopatikana.

Ulimwengu ulitegemea kwamba, baada ya serikali za Wataleban na Saddam Hussein kupinduliwa Afghanstan na Iraq , sasa ulimwengu ungekuwa mahali salama, lakini badala yake sasa ni kiama cha mabomu ulimwengu mzima.

Siyo ulimwengu ulioendelea kiulinzi, na wala siyo nchi masikini kama hizi zetu, sote twagugumia machungu ya mabomu mtindo mmoja!
Agosti 7,1998 mabomu yalipolipuliwa katika ubalozi wa Marekani Nairobi na Dar es salaam, na kuua watu 224,ilisemwa kuwa ni kwa sababu ya umasikini wetu, rushwa na miundo mbinu dhaifu ya ulinzi dhidi ya magaidi.
Mwaka 2002,Machi 21, bomu lililotegwa garini liliua watu tisa katika ubalozi wa Marekani mjini Lima , Peru .Ikasemwa hivyo, kwamba ni nchi dhaifu.
Oktoba 12,mwaka huo wa 2002, mabomu yalilipuka katika klabu ya usiku mjini Bali , na kuua watu 202.
Wakati wa milipuko ya Septemba 11, wakauawa zaidi ya watu 3,000 .hatua zilianza kuchukuliwa dhidi ya ugaidi. Maana, ilionekana sasa magaidi hawakuwa wakitania.
Huu ni wakati WTC ilipogeuka Ground Zero,na kifusi chake ni mnara wa kumbukumbu za magaidi,kifusi kimejaa ekari moja!
Walishakamatwa magaidi kama akina Riduan Isamadun, au Hambali, waliohisiwa kushiriki kiama hicho cha Septemba 11
. Alikamatwa pia Khalid Sheikh Mohammed na wengine wengi.
Magaidi wengi walishakamatwa Iraq na Afghanistan na kupelekwa Guantanamo Bay , lakini uovu unaendelea tu.Ilichokipata Marekani, ni lawama za kukiuka haki za Binadamu.

Licha ya Osama Bin Laden, Mullah Mohammed Omar na Abu Musab Al Zarqawi kusakwa sana , bado ugaidi ni kitisho kikubwa  kwa maendeleo ya watu Duniani.
Obama ameuawa na Carlos kafungwa maisha,lakini ugaidi ungalipo.
Licha ya Tawala zilizodaiwa kuwafadhili hawa majaili kupinduliwa, bado mabomu yanalipuka mahali popote magaidi wanapoona panafaa yalipuke.
Agosti 19,2003 bomu lilipolipuka katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa, mjini Baghdad , na kuua watu 22, akiwemo mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, De Mello, ulimwengu ulipata  kitisho kikubwa, kwamba ulimwengu mzima uko hatarini.
Hata Umoja wa Mataifa?
Hata hivyo, mabomu ya 2005 ya London , yaliyoua zaidi ya watu 50, na kuharibu miundombinu ya reli katika jiji hilo maarufu sana duniani, ni hatari zaidi!!
Msiseme Nairobi,Dar au Kampala! Mbona New York,Washington na London ni miji iliyolipuliwa?
 Tatizo watu hawana kumbukumbu,wamekalia siasa za kuchoma magogo na matairi barabarani!

London, ni jiji lenye ulinzi wa hali ya juu.Taasisi za ulinzi, upelelezi au ujasusi zilizopo London ni maarufu mno duniani, na huogopwa ulimwengu mzima.
Lakini jinsi mtandao katili wa Al-Qaeda ulivyojipenyeza na kupiga mabomu njia za reli za chini kwa chini(tube) na mabasi, ni kitisho zaidi; na mashambulizi haya yanatosha kutufanya tuamini kuwa mkakati wa Bush na Blair,Cameron na Obama kupambana na ugaidi kwa kutumia nguvu(Aggressive Power) umepitwa na wakati.
Dunia ikae mezani kutazama magaidi(ama wawe wanaharakati,walipa visasi n.k) wanatakaje ili kutuliza mizuka?
.Magaidi wamesakwa sana, wameuawa sana, lakini wamaomgezeka na kuua watu wengi mahali popote bila kuogopa umahiri wa ulinzi, au utajiri!Marekani, Uingereza, Kenya na Tanzania zote zimepigwa na Al-Qaeda!!

Kama majahili hawa wameweza kufanya unyama mkubwa London , New York na Washington, ni wapi wataogopa?
Walipopiga Nairobi, Dar es salaam , Bali na ofisi za Umoja wa Mataifa, Baghdad , ilionekana ni udhaifu wa ulinzi.
Ilipopigwa miji ya Washington na New York (Septemba 11) ilisemwa kuwa watakomeshwa.
Tumeona Osama akisakwa, utawala wa Taleban na Saddam ukiangushwa, na kumfanya Saddam kuwa mateka na mfungwa katika mji wake Mkuu aliotumia kuitawala Iraq , Lakini mabomu yanaendelea.
Saddam,Osama,Gaddafi wameuliwa lakini mabomu na risasi vimerindima duniani,sasa West Gate,NAIROBI!!
Irak,Libya,Misri,SYRIA nk hamkani si shwari tena.

Mtazamo wangu ni kuwa iko haja ya Umoja wa Mataifa kujua kwamba Blair na Bush siyo majemadari tena wa vita dhidi ya ugaidi duniani; wameshindwa vibaya; kwa kuwa miji yao mikuu imepigwa na maelfu ya watu kuuawa.Iko siku nao watapigwa na kuuawa!

Hawa  Cameron,Obama,Bush na Blair, sasa hawana jipya la kuuhadaa ulimwengu kwamba ugaidi utatokomezwa.
Vita dhidi ya ugaidi, War Against Terrorism, ni danganya toto!
 Ni wajibu wa Umoja wa Mataifa kukaa na kutafuta mbinu sahihi za kuondoa kitisho hiki, badala ya kuwategemea hawa akina Bush, Obama,Hollande na Blair, walioshindwa vibaya na kwa aibu.
Hivi ulimwengu ungekuwaje mabomu ya  London yangeelekezwa Gleneagles, walikokuwa wakifanya mkutano wakuu wan chi tajiri zenye viwanda, G-8?
Bush, aliyeongoza vita dhidi ya Afghanistan na Iraq , alikuwepo, na wengine wengi walikuwepo Scotland , mabomu yalipolipuka.
Nataka kusema kuwa, kufuatia mkutano huo mkubwa, na ulioandamwa na waandamanaji, kulikuwa na ulinzi mkali eneo zima la Ufalme wa Uingereza, Lakini mabomu yalilipuka na kuua watu 52.
Hii ni kuonyesha kuwa iko siku magaidi watapiga ikulu zote duniani, na kuleta msiba mkubwa.
Kwanini isitafutwe njia nyingine ya kupambana na ugaidi, badala ya kutumia ubabe wa akina Bush na Blair? Obama,Cameron,Hollande?
Miongo michache iliyopita, Uingereza ilikuwa katika kitisho cha mabomu ya vikundi kama Irish Republican Army(IRA), ambao sasa hawafanyi tena hujuma, kwa sababu Ireland inao uhuru na Haki zilizokuwa zikitafutwa.
Serikali ya Uingereza ilitambua madai ya magaidi hao wa IRA, na amani ikawepo.
Kwa mantiki hii magaidi ni binadamu wanaofanya vitendo vya kinyama, ili kupata haki zao.
Ugaidi siyo ujambazi unaoandamana na tamaa tu
. Bali , ugaidi ni harakati za kutafuta maslahi Fulani.Wakati Fulani wanaharakati kama Martin Luther King, Kanali John Garang, Museveni, Marehemu Samora Machel na wengine, walionekana kama magaidi, lakini leo tuna waona mashujaa wa watu wao.

Hii ni kusema kuwa hawa magaidi wanayomadai yao , ambayo Umoja wa Mataifa lazima uyatazame, na kuyatafutia ufumbuzi.
Kama Kanali Gaddafi, wakati Fulani ikulu yake ilipigwa mabomu na Marekani, hadi mwanaye akauawa, na leo inasemekana nchi yake imekoma kuunga mkono ugaidi, hata Osama angeweza kubadilika, kupitia meza ya mazungumzo!
Gaddafi baadaye aliuliwa kwa sababu eti za kuwaita waasi mende,panya!

Ulimwengu unataka amani, hivyo zitafutwe njia elfu kukomesha ugaidi, kwani Bush na Blair Obama na Cameron wameshindwa sana ; hata miji yao yote mikuu imepigwa hadi maelfu kuuawa
.Magaidi hawana nchi, hawana mipaka, hivyo wamepata ushindi wa kishindo, yapaswa wakabiliwe kidiplomasia, ili kuondoa kitisho.
Tumecoka kusesabu maiti na ndoo za damu inayomwagika!

Hivi leo mtu aweza kusema Bush na Blair,Obama,Cameron na Hollande wataweza kuifanya dunia mahali pa salama?
 La hasha… wameshindwa tangu Iraq , Afghanistan , Afrika, Asia na hata jirani na Ikulu zao.
Shime, Umoja wa Mataifa utafute njia mbadala ya kupambana na ugaidi; la sivyo tutateketea kwa mabomu ya majahili hawa
0713 324 074.


J

AL SHABAAB NAIROBI PIGO KWETU TANZANIA


 
Na Conges Mramba
Jumatano, Agosti 7 mwaka huu tulikumbuka mashambulizi ya magaidi yaliyofanywa katika Balozi za Marekani, Dar es salaam na Nairobi ; mwaka 1998
.Na  juzi tu,tukakumbuka matukio ya Septemba 11,mwaka 2001.Leo tunaomboleza,West Gate Nairobi.Watu takriban sabini wamekufa,wengi wamejeruhiwa vibaya!
    Zaidi ya watu 240 walikufa mwaka 1998; hawa hawakuwa wa  Kenya pekee bali pia wa Tanzania . Hawakuwa wa kabila moja au wa  dini fulani, waliokuwa wakisali msikiti mmoja ama kanisa fulani.
Magaidi ni hatari kwa raia wote wa dunia.
    Tunawaombolezea waathirika wa tukio hilo la Agosti 7 mwaka huo wa 1998, ambalo msingi mkubwa ni uadui kati ya Marekani na Waarabu walioamua kuisaka Marekani popote duniani, ili kulipa kisasi.
    Naam,kuisaka Marekani katika ardhi yetu, kusababisha hasara ya maisha na mali za watu wetu, ni vitu tunavyovipinga leo na kesho hata kama mbingu zishuke; ama jua litue mchana saa saba!
Hata mgogoro wa Somali ni matokeo ya Vita Baridi kati ya Urusi na Marekani na washirika wao,sisi tunapokwenda kupambana na al-shabaab ama al-Qaeda,maana yake twapambana na mabaki ya minyukano ya Mashariki na Magharibi.
    Si lengo la ukurasa huu kusema kwamba magaidi ni Waarabu peke yao, ama watu wa imani fulani. Nitajadili malengo ya ugaidi na chimbuko lake. Nitajadili imani inavyoupa msukumo na nguvu ugaidi duniani.
   Kuna vikundi tele vya kigaidi duniani. Usishangae, hakuna gaidi anayejiita gaidi.
Wote wanajiita, wanaharakati(activists) wa ‘Haki’ za ubinadamu wao. Ugaidi unakula maisha ya watu na mali vinapopotea au kuharibiwa.
  Kila mmoja ana tafsiri yake ya ugaidi. Sitajali kusikia Rais George W. Bush wa Marekani naye ni gaidi kama Osama bin Laden.
Hata hivyo, najua, magaidi kama wale waliolipua Balozi la Marekani Dar es salaam na Nairobi, Agosti 7 miaka 10 iliyopita, wote ni wauaji; wanastahili adhabu kali.
Walioua watu Nairobi nao wanastahili adhabu kali.
   A-Qaeda ni kundi la harakati za kigaidi, bila kujali wanaharakati wake wanatokana na itikadi gani. Japan, kuna kundi moja linaitwa, “Ukweli Mkuu” kwa Kijapani, Aum shinrikyo-hawa nao hata wakifanya mauaji, watasema wameua ili kuueneza huo Ukweli(The supreme Truth). Mauaji hayaenezi haki yoyote.
   Uhispania, kuna kundi linaitwa, ETA(Freedom for The Bosque Homeland), nalo linadai uhuru. Lebanon , kuna kundi maarufu sana kama , Hezbollah(Chama cha Bwana Mungu), wakati Ireland Kaskazini kuna kundi liitwalo, Irish Republican Army(IRA).
    Nchini Israeli, kitovu cha uadui wa mgogoro wa Mashariki ya Kati, kuna kundi liitwalo, Kach and Kahane Chai, Uturuki kuna PKK(Kurdistan Peoples Party), Sri Lanka kuna, Liberation Tigers of Tamil Eelam(LTTE); wakati nchini Iran kuna Mujahedin-E-Khalq.
   Ugiriki kuna kundi linaitwa, November 17 Revolution.
 Juzi tulisikia kundi la FARC(Revolutionary Armed Forces of Columbia) likifanya utekaji nyara; lakini ni ‘Jeshi la Kimapinduzi’.Jeshi la kimapinduzi hupindua raia?
   Hakuna anayemaizi kuwa matendo yake ni kinyume cha sheria za nchi, za kimataifa, ama ubinadamu. Wengine wanajisingizia, wametumwa na Mungu ili kuwaua binadamu wenzao, waabudu sanamu ama wapagani.
  Wapo, Shining Path kule Peru . Columbia pia kuna National           Liberation Army(ELN), na Ufilipino kuna New People’s Army.
    Tumjadili kidogo tu, gaidi la kale, Ilych Ramirez Sanchez, ambaye kwa utani anaitwa, Carlos The Jackal-mzaliwa wa mjini Caracas , Venezuela . Venezuela , ni nchi aliyoongoza Hugo Chavez, ambaye alimtukana rais Bush, wakati anahutubia Mkutano wa Umoja wa Mataija, jijini New York , akapewa saa chache awe ameondoka nchini humo.
Chavez alishakufa akabaki Nicolas Maduro.
   Carlos, gaidi anayetumikia kifungo cha maisha   Ufaransa, ikifika Oktoba 12 mwaka huu, atakuwa anaadhimisha miaka 59 ya kuzaliwa kwake.
  Sasa, huyu jamaa katika mafaili ya uhalifu na Jinai duniani, kuna mambo yake mengi, ambayo yametokana na chuki za siku nyingi kati ya nchi za Amerika ya Kusini(zilifuata siasa za Carl- Marx) na Marekani. Carlos, ambaye baba yake alikuwa mjamaa, alimpeleka Chuo Kikuu cha Patrice Lumbumba, mjini Moscow , kusoma.
   Huko alikutana na Wapalestina, akaiva katika siasa za mrengo tofauti na ubeberu wa Kimarekani.
   Hata jina ‘Ilych’  aliitwa na babaye ili kuwaenzi ‘makomredi’ wa Urusi ya Ujamaa, akina Lenin.
   Sasa Carlos anaipinga Marekani hata huko jela, alishasema alimuunga mkono Osama bin Laden, kwa asilimia 100; na kwamba anawataka watu wasiache kujitoa mhanga ili kufa na Wamarekani, popote walipo!
   Nitajadili kauli hii baadaye kidogo. Hata hivyo, huyu jamaa aliyetiwa mbaroni na mashushushu wa Ufaransa akiwa mjini Khartoum, Sudan alishakaa Urusi tangu 1968, amekaa Ujerumani mwaka 79, amekaa Syria 91-93, na Ufaransa. Vituko vyake unaweza kuvipata katika sinema za akina James Bond.
  Hapa, nitajadili ugaidi, si Carlos.
   Naam, ugaidi wa Agosti 7 mwaka 1998, ulileta hadithi nyingi. Lakini, tuseme kwamba wale magaidi walishambulia Balozi za Marekani Dar es salaam na Nairobi , karibia muda uleule mmoja, kwa sababu nchi hizi hazikuwa zimejiandaa.
   Wengine wanasema hata Kampala ingeshambuliwa. Kilichoiponya ati ujio wa Rais Bill Clinton wakati ule mjini Kampala , ulivifanya vikosi vya usalama vya Uganda kuwa ‘more alert’ kuliko Dar na Nairobi ! Hayo tuyaache.
Kampala ilishambuliwa na al-Shabaab mwaka 2010 wakati wa Kombe la Dunia Afrika Kusini.
     Shambulizi lingine la magaidi Afrika Mashariki lilifika Novemba 28 mwaka 2002.
 Magaidi waliua watu 16 mjini Mombasa, katika hoteli ya Paradise iliyoko Kikambala. Ni kilomita 25 kutoka mjini Mombasa.
   Hii hoteli ni ya Waisraeli; sasa unaweza kukisia hata wewe, kwamba ilishambuliwa na adui zao Wapalestina. Wapalestina walikuja Afrika Mashariki kuwawinda adui zao Waisraeli, katika ardhi ya Kenya. Hawakuua Waisraeli tu, waliua na Wakenya, na raia wa mataifa mengine.
   Sasa tuseme, vita vya kudai uhuru vinavyoendeshwa na Wapalestina dhidi ya Mayahudi, vina leseni ya kuua na kuumiza binadamu wengine wasio na hatia?
   Halafu, hao magaidi wa Kipalestina walifanya jaribio la kuilipua ndege ya Arkia Airlines ya Israeli, iliyokuwa ikiruka kutoka uwanja wa ndege wa Moi, mjini Mombasa. Bahati tu, lile kombora, bila shaka la Kirusi, liliikosa- kosa ndege ile iliyokuwa na abiria 271 hivi.
    Fikiria, kama kombora lile lingeipata ndege ile,wangekufa Waisraeli pekee?
 Hata raia wa mataifa mengine, wasiojua uadui waa Israeli na Wapalestina wangeungua katika miali ya moto wa mlipuko. Sasa ugaidi unasura ya ukombozi  au uokozi na uhuru wa wapi?
   Narejea mada yangu ya madhara ya ugaidi Afrika Mashariki. Matukio yote ya ugaidi yalisababisha watu mamia kufa, inakisiwa kulitokea hasara ya dola mabilioni. Ili kuponya majeraha ya ugaidi, zimetumika dola matrilioni, ambazo pengine zingetumiwa kuleta maendeleo-ugaidi ni adui wa maendeleo ya watu.
   Nimesema magaidi wapo Wazungu kama IRA, na wa mataifa mengine kama akina Carlos The Jackal; lakini ni magaidi. Magaidi hawana rangi, dini ama taifa moja.
   Ugaidi ni mauaji ya kinyama yanayoendana na matakwa ya ulipaji kisasi. Pengine, magaidi kama Black Banners wa Iraki, wakati ule wa vita, waliwateka jamaa watatu wa Kenya, ili kutafuta fedha kutoka kwa makampuni waliyofanyia kazi.
   Sasa nijadili jambo ambalo watu hupenda kunitolea  matusi. Watoa lugha chafu, hawana weledi juu ya lolote. Silaha yao ni matusi na vitisho. Wanadhani, ukweli ni ule unaolingana na wanavyopenda, ama wanyofikiria wao.
    Hata hivyo, ugaidi ni unyama, hata Mungu mahali popote hajawahi kusema watu walipizane visasi. Sera za ‘Jino kwa Jino’ ama ‘TIT FOR TAT’ ni za Ibilisi. Mungu anawataka watu kutong’oana meno, ili kulipa baya kwa baya?
 ungu anawataka watu wawe vibogoyo au chongo?
  Juzi, Papa Benedict XVI ameungama kwamba Kanisa Katoliki nalo lilishafanya ugaidi. Ugaidi hauna rangi, kanisa, msikiti wala watu wa kabila moja.
   Nilipata kutukanwa na hawa jamaa kwa kupinga kauli ya Carlos, kuwataka watu kufuga midevu mingi kama shamba la miwa la Kilombero, halafu  eti wasiache kujilipua ili kuwakomesha Wamarekani, popote watakapowaona!
    Sasa kama Carlos kawaambia, kwa nini wasiende kujilipua New York au Washington ? Kwa nini Mombasa , Nairobi au Dar? Huku Wamarekani hawapo!
 Mkijilipua huku mnatuumiza sisi, wao hawapo. Kama wapo ni mmoja tu au wawili-wafuateni Wamarekani kwenye uwanja wa mapambano! Wenye uwezo walikwenda kulipua New York na Washington, Septemba 11 mwaka 2001; hadi leo historia inaelekea kuwasahau.
   Sipendi kuamini kuwa, mtu mwenye uwezo wa kufikiri anaweza kuwa’Shahidi’ mwaminifu wa imani yake(uwe Ukristo,upagani ama Uislamu)kwa kujilipua, ili afe yeye na kumuua adui!
   Huku ni kushika dini kupita kiasi(fanaticism), kunakogeuza dini kuwa vifo na mauti, kwamba ni ushahidi(martyr). Hii si Jihad halali kuua hata watoto wasio na hatia, kwa sababu tu walikaa meza moja na adui.Kwa nini kuua adui mmoja kati ya ndugu mamia?
    Najua vita kati ya Waisraeli na Waarabu wa Mashariki ya Kati, inaitwa ‘Vita kati ya wema na uovu’. Sasa kama pande mbili zinaua hata wasiohusika, mwema nani na mwovu ana alama gani?
   George Bush na Tony Blair, wakati wanaishambulia Irak, walisema ni vita dhidi ya watu wasiostaarabika. Wakati magaidi waliposhambulia London, wakasema ni vita dhidi ya ustaarabu.Sasa tujiulize pia, kuua watu wasiohusika hata huko Irak ni ustaarabu? Ni kwa sababu hii, safu hii inasisitiza kuwa mauaji ni jinai, na kila muuaji ni Ibilisi mwenye mikia saba.
    Hakuna kitabu kitakatifu kinachotuma watu kuwaua wenzao wasioamini ama waabudu sanamu. Ndiyo maana hapa Tanzania si lazima kwa mujibu wa Katiba mtu kuwa dini fulani.Hata wapagani na waabudu sanamu ni watu; wasiuawe kwa kutokuwa na dini kwao.
   Nasema hivi kwa sababu rafiki yangu aliniambia, Allah kasema kuua hawa walao nguruwe ni kupata thawabu hata akhera!(to be elevated to a higher plane of existence, where life is an eternal bliss).
   Ni kwa sababu hii, msomi na mhadhiri, Imam  mashuhuri anasema kila siku, kwamba Kuran inakataza kabisa kuua au kujitoa mhanga-na kwamba wanaofanya hivyo, hawafanyi kwa jina la Uislam; bali wanasaliti mafundisho ya Mtume Muhammad.
    “Hatutaruhusu imani yetu adhim kutekwa nyara na wahalifu”, alisema.
 Maneno kama haya kayasema Kiongozi wa Upinzani Bungeni juzi, Hamad Rashid Mohamed, alipokuwa akitoa hutuba fupi wakati wa kuaga mwili wa Chacha Zakayo Wangwe, “Rasta” wa Tarime. Buriani Chacha Wangwe.
    Hamad Rashid, alisema alikwaruzana na Marehemu Chacha Wangwe, lakini wakasameheana, kwa sababu, Kuran inasema, ‘kusamehe ni lazima’ ili upate thawabu.
  Biblia inasema kusamehe ‘saba x sabini’ maana yake siku zote za maisha. Saba ni alama ya ukamilifu wa utimilifu; hivyo tusichoke kusamehe.
 Sasa  hata hapa mtanitukana na kutishia kunipiga kwa kuhimiza amani? Mungu gani kawaambia kumpiga mwenye mawazo tofauti nanyi? Dini yenu  ni ya amani, kwa nini Jino kwa Jino?
    Nilishasema katika makala mbili zilizotangulia, kwamba kuna upendeleo na ‘double standards’. Alichofanya Bush au Blair, akikifanya Mugabe au Mpalestina, ataitwa gaidi, wao “Patriots”.
  Hili ni tatizo ambalo haliondolewi kwa watu kujilipua, lawama hizi haziondoki kwa kujifunga mabomu. Hatupambani na ‘metropolitan power’ kwa kulipua Dar, Mombasa na Nairobi.Tunatakiwa kuilipua Washington kisayansi, maana yake kumlipua Bush pekee bila raia wasio na hatia.
   Ukijifunga bomu utamlipua Blair au Bush? La hasha. Utawalipua ndugu zako wa Dar, Mombasa ama Nairobi. Tutafute njia mwafaka ya kuondoa ‘double standards’ duniani. Tusijiite, “Liberators” ama ‘in the service of’ Allah’ kumbe wauaji wa ndugu zetu wenyewe.
  Tusidhani tunakomboa, kumbe tunajiua! Kujiua ni dhambi kubwa na kosa katika sheria za binadamu na Allah. Mashahidi waaminifu wa imani, hawatoki msikiti fulani tu, hata sinagogi au kanisa.
 Je, hamjaona watu wakienda uwanja wa ndege na biblia pasipo nauli,hati za kusafiria wala visa wakadhani Mungu atawapeleka Ulaya kuhubiri? Huku nako kujifunga mabomu! Magaidi hawana dini moja.
   Nimalize, kwa kusema Kuzimu kumepanua kinywa chake. Kuna visasi vingi tangu matukio ya Septemba 11 mwaka 2001. Lakini, tuangalie faida yake nini? Nani kasema ukifa kwa kujilipua kwa bomu na kuangamiza Mzungu mmoja na Waafrika wenzako 200 ni thawabu? Imani zisitugawe;sisi ni wamoja hapa Tanzania ama Afrika.
  Tutafakari msugoano uliopo kati ya Magharibi na Mashariki. Leo, siasa za akina Hugo Chavez, zinashindwa. Akina Carlos The Jackal wanaonekana majambazi tu, hata kama walifanya kazi bega kwa bega na makomredi kama Fidel Castro, katika kuzuia ubeberu.
  Hatuwezi kuupinga ubeberu kwa kuangamizana Paradise Mombasa, au katika usafiri wa ndege kama ile ya Arkia Airline, ama wa treli London.
  Hata katika balozi za Wazungu, kama Dar, Kampala na Nairobi, ukijilipua hukosi kuua Mzungu mmoja na Waafrika wenzako 300. Kuna thawabu gani hapo?
   Tufanyeje sasa? Tufikiri kwa makini; tuepuke kutukana watu, kupandisha mizuka ili kuhuisha roho ya kisasi. Tutaushinda uadui kwa akili na imani,  si imani bila busara. Busara hutoka kwa Mungu.Kwa mungu kuna haki na thawabu. Mungu ni wa utaratibu, si wa machafuko.Palipo na machafuko, hapana Mungu. Na sheria ni msumeno.
   . Ukweli si ule unaomfrahisha mtu; ukweli ni mchungu lakini mtamu. Ukweli ni ubinadamu. Tuimarishe ubinadamu-humanity.
Ndivyo tunavyoikumbuka Septemba 11 mwaka 2001,tunawapa pole Nairobi kwa kipigo cha al-SHABAAB,
  www.congesmrambatoday.blogspot.com
  0754 324 074,0786 324 074