Wednesday, October 23, 2013
mwarabu na mwafrika tosha kukataa ukoloni
NA CONGES MRAMBA
RAIS MSTAAFU
wa Afrika Kusini,Nelson Rolihlahla Madiba Mandela, aliwahi kumkemea George
Walker Bush wa Marekani kwamba aliivamia Irak mwaka 2003 ili kupora mafuta.
Madiba,
alisema Vita vya Ghuba vya miaka ya 1990 na 2003 vilikuwa vya kupora
mafuta.Mataifa makubwa ya Ulaya Magharibi, siku hizi hutumia silaha vitani ili
kukamata nishati muhimu kama mafuta,gesi,uranium n.k
Hii ni
kufuatia mataifa tajiri ya mafuta na gesi,hususan ya Kiarabu kukaribia kuukata
koo uchumi wa Mataifa hayo miaka ya 70.
Tangu Vita
vya Pili vya Dunia, mafuta yalipatikana tele na kwa bei poa kwa viwanda na ili
kusafirishia bidhaa za mataifa makubwa haya.
Mwaka 1973,
wakati ule wa vita huko Mashariki ya Kati,Waarabu wanaozalisha mafuta kwa
wingi, walipunguza uzalishaji na kuongeza bei ya nishati hiyo maradufu.
Ongezeko la
bei ya mafuta huko Mashariki ya Kati, ni kusababisha chumi za nchi za viwanda
kuanza kutetereka.
Ukitaka vita
mlangoni kwako,basi anzisha sera za kuzuia chumi za ‘Industrialized Nations’
kukua kwa ufanisi. Utasingiziwa ‘Gaidi’ ili upigwe kwa drones!
Nchi za
Kiarabu zilitangaza kuinyima nchi yoyote mafuta kwa kuwa inaisaidia Israeli(Adui
Mkuu wa Waarabu),kwa hali hiyo,Marekani,Ufaransa,Uingereza na washirika wao
wasingeuziwa mafuta na Mwarabu.
Kwa mara ya
kwanza mwaka 1973,Mwarabu alitumia nishati ya mafuta kama “SILAHA MUHIMU”
katika siasa za kimataifa.
Nchi
wazalishaji na wasafirishaji wa mafuta(OPEC) walikubaliana kupunguza uzalishaji
wa mafuta,kasha wakaongeza bei ya nishati hiyo muhimu kwauchumi wa dunia.
OPEC
walikubaliana kulinda na kutunza akiba yao ya mafuta,ili kuwatoa kamasi
Wazungu!
Bei ya
mafuta ikapaa;mgogoro mkubwa wa mafuta,maarufu kama, “THE OIL CRISIS” ukatikisa
viwanda vya mabwanyenye,uzalishaji ukashuka maradufu.
Mfumuko wa
bei(Inflation) ulikita;viwanda vingine vikafungwa na kusababisha ukosefu wa
ajira ulioikumba dunia.
Mwaka 1979
Mfumuko wa Bei ulipanda kwa asilimia 334 kuanzia takwimu za mwaka 1969.
Hii ni
kusema, bidhaa iliyouzwa kwa Pauni moja ya Kiingereza mwaka huo 1969,sasa
ikauzwa kwa Pauni 3.34. Hali hiyo ilifuatia Waarabu kuzuia mafuta yao kuuzwa
Ulaya-ARAB OIL EMBARGO-mwaka 1973,kukaleta kiama cha kutisha kwa
Marekani,Uingereza, Ufaransa na rafiki zao.
Mfumuko wa
bei(Inflation) usiosemeka ulisababisha bei zikapanda kila kulipokucha,fedha
zilikosa thamani mfululizo.
Nataka
nikwambie msomaji.Ikiwa ili upate nishati ya kupikia chakula chako(kuni,mkaa,mafuta,gesi
n.k) ingekugharimu fedha zinazojaa magunia matatu ya noti za elfu kumi-kumi!
Kwa nini
usitumie magunia mawili ya noti zenyewe kama kuni ili kupikia chakula
chako,kuliko kununua mafuta au kuni kwa magunia matatu ya noti?
Kwenye
mfumuko wa bei noti huwa hazina thamani kwa kiwango hiki! Italia,mfumuko wa bei
ulifika asilimia 319,Japan(236%),Ufaransa(234%),Marekani(196%) n.k
Nimesema, chanzo
kilikuwa ‘reduced supply’ kukaja kuzaliwa shida nyingine ya kitu kinaitwa, “recession”,
biashara ikasinyaa,hata bidhaa hazikuzalishwa tena viwandani-sababu ya kiburi
cha Mwarabu!!
Hata Urusi
haikuwa salama;Afrika nayo iligugumia maumivu ya kupanda kwa gharama kufuatia
kupanda bei ya mafuta soko la dunia.Kununua bidhaa soko la dunia kuligharimu
bei mbaya wakati huo wa miaka ya 70.
Hali hii
ilifanya mataifa ya KIARABU kutajirika maradufu,Waarabu wakawa wanakula maisha
sana hata huko Ulaya.Marekani pamoja na kuwa na mafuta yake yenyewe,ikakumbwa
na kilio kikuu cha ukosefu wa mafuta.
Marekani
hutumia mafuta mengi kuliko nchi yoyote hapa Duniani.
Kufuatia
hali hiyo,Marekani ilikaribia kutembelea magoti na kukoma kuwa “economic strong
man”.
Nakumbuka,
Katuni moja iliyochorwa na Wadachi mwaka 1973,Mwarabu akiwa amewaweka CHINI YA
ULINZI viongozi wanne wa Dunia:
Kansela
Willy Brandt wa Ujerumani,Rais Georges Pompidou wa Ufaransa,Rais Richard Nixon
wa Marekani na Waziri Mkuu,Edward Heath wa Uingereza.
Hawa
walionekana kwenye katuni wakiwa wamewekwa chini ya Ulinzi na Mwarabu kwa
kutumia ‘Pampu’tu ya mafuta, siyo bunduki wala guruneti!
Walishikiliwa
hadi Mzungu alipe kikombozi(ransom) ndipo waachiliwe huru.
Zama hizo,
Saudi Arabia,Irak,Iran,KUWAIT,Libya,Abu Dhabi,Algeria n.k zikapata heshima
mbele ya mabeberu.Nchi nyingine kama Nigeria,Guinea ya IKWETA,Venezuela,Indonesia,Ecuador,Angola
n.k zingeweza kuwa na kiburi cha kuyagomea mataifa haya kwa kutumia mafuta kama
silaha.
Norway,Mexico
na Uingereza walihaha kusaka vyanzo vipya vya mafuta.Mwaka 1979 kulikuwa na
uhaba wa mapipa milioni 2.3 kila siku.
Ni hapa
Mwarabu alipotikisa ndevu za Mzungu, hususan Marekani ambayo kwa siku moja
hutumia theluthi ya mafuta yoote yanayotumiwa na dunia nzima.
Huu ndiyo
wakati Mohammed Reza(Shah) wa Iran alipouza mafuta yote Marekani na kuiacha nchi
yake ikiwa kavu kabisa!
Itaendelea
0713 324 074
MWARABU NA MWAFRIKA WAKIUNGANA TOSHA KUKOMESHA UKOLONI
CONGES MRAMBA,MWANZA
Mapema mwaka juzi,kulitokea
tishio la vita huko HORMUZ STRAIT.
SABABU NI Iran kutishia
kuufunga mlango bahari wa Hormuz endapo ingeshambuliwa ama ikiwekewa vikwazo
isiuze mafuta yake duniani.
Mataifa matano
wanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa,
Marekani,Uingereza, Ufaransa , China na Urusi ndiyo wanaomiliki makampuni
makubwa sana ya mafuta duniani.
Kutoka miaka ya 70 hadi
2011 tayari Mzungu keshanunua hisa katika visima na makampuni ya mafuta,
anatawala siasa za mafuta duniani.
Makampuni haya,
‘SUPERMAJORS’ yanashikilia sasa soko la mafuta kutokana na mitaji yake mikubwa
kabisa.
PETROCHINA, BRITISH
PETROLEUM (BP), Royal/Dutch Shell,Exxon,Texaco,Gulf,Mobil n.k ni makampuni
yenye mitaji mikubwa na maamuzi makubwa katika soko la mafuta duniani.
Sibneft,Lukoil na Yukos nayo ni makampuni ya Kirusi yaliyo chini ya Ikulu ya
nchi hiyo-Kremlin.
Kuna Chevron,Total
na mengine ambayo huunganisha mitaji ili kulikamata soko la mafuta duniani.
Ni mataifa haya
haya yenye makampuni ya mafuta na viwanda ndiyo huchafua mazingira ya dunia na
hugoma kutia saini mikataba ya mazingira kama ule wa Kyoto-Japan,huku visima
vya mafuta ni moja ya vyanzo vya uharibifu mkubwa wa mazingira,na hakuna wa
kusema.
Ni hawa ambao leo
wanaiona Israeli haina kosa hata kama itaua Wapalestina na kuwakandamiza. Mtu
mmoja aliwahi kuniuliza,kwanini Mkristo nawatetea Waislam.
Mimi si msemaji wao,ila
hata wao hunilaumu kusema kwamba watalazimishwa hata kuabudu sanamu ya
Mzungu kwa sababu ya maslahi.
Wazungu wanataka
mafuta, na bahati mbaya wameungana na dunia nzima kutaka hata miungu yao
iabudiwe na wao waabudiwe kama miungu.Tazama UFUNUO 13:18
Unabii wa Biblia
hutuambia hatma ya vita hivi,kwamba mataifa ya Ulaya na Marekani yatakumbatia
madhhebu Fulani na wakuu wake(Ufunuo 17:9-11) ili kuwaburuza watu wa dunia
nzima.
Na wenye hekima na
akili zenye hekima ndiyo wataelewa jambo hili. Mamlaka haya yatafananishwa na
FALME saba zilizowahi kuitawala dunia huko zamani:
Waashuri,Wamisri,Babeli, Medo-Persia,
UGIRIKI,Rumi ya kale na Rumi zama za Upapa .Katika milki hizi Mungu wa kweli
alipingwa na waliomwabudu waliuliwa na kuteswa,ukweli ulikataliwa, historia
inajirudia.
Ufunuo 17:13 husema
wafalme wa dunia watakuwa na AJENDA MOJA YA SIRI,kumrithisha Mfalme mmoja
utawala wao wa dunia nzima,na wanaopinga wauawe au wawekewe vikwazo vya
uchumi,anayebisha apewe kibano,kama tutakavyoadhibiwa kwa meli za Iran ‘kuvaa’
Utanzania!
Mwanamke anayebebwa
mjini Brussels hatimaye atakuwa na sauti duniani, tazameni Goddes Roma.
Huu ni unabii wa Mzungu
kutawala nchi zenye rasilimali hususan Afrika na Asia,hata kama Mwafrika na Mwarabu
wana rasilimali nyingi kama mafuta,gesi,almasi,dhahabu,ardhi safi n.k
Mzungu anatumia kila
njia kuhujumu amani na uchumi wa Mwarabu na Mwafrika!
Kampuni ya
Shell ya Uingereza,iliwalipa fedha wanamgambo kuwaua wanaharakati wakati
walipoandamana huko Niger Delta, kupinga makampuni hayo ya kigeni kuchimba
mafuta eneo hilo wakati wakiharibu mazingira,bila kulipa fidia.
Niger Delta hakukuwa na mafuta na huduma za
kiuchumi hazikuwepo licha ya mapipa mengi kuchimbwa eneo hilo la Kusini
mwa Nigeria.
Kampuni ya Chevron ya
Marekani,iliwalipa mishahara polisi na jeshi kuwaua wanaharakati kama Ken
Saro-Wiwa, kwa sababu walipinga uhalifu wa makampuni haya kwa maandamano
makubwa ya amani.
Watu wajinga wanapoona Afrika polisi
wakikabiliana na waandamanaji,akili inawatuma Ulaya hawakabiliwi.
Kumbe, Ulaya na Marekani walikuwa nyuma ya
vikosi vya Sani Abacha kuwaua wanaharakati waliopinga makampuni ya kigeni
kuharibu mazingira bila kuleta maendeleo kwa raia hata licha ya kuchimba mafuta
katika eneo hilo.
Sasa, kama Gaddafi alishambulia
waandamanaji wa Benghazi,akapinduliwa kisha kuuliwa kwa risasi, Kiongozi wa
Syria, Bashar al Assad naye anawashambulia raia wanaompinga anashughulikiwa na
Ulaya na Marekani,kwanini Shell na Chevron yalishinikiza serikali ya Nigeria
kuwaua waandamanaji?
Huko Burma,(siku hizi ni Myanmar)
kampuni kubwa la Unocal la Marekani, lilitiliana saini mkataba na jeshi
kuilinda,ilipokuwa ikitekeleza ujenzi wa Bomba la gesi asilia kama hiyo ya Mtwara,
kupelekwa nchi nyingine.
Bomba hilo lilikuwa likijengwa
kutoka Yadana,wanakijiji walitumikishwa pasipo ujira,walibakwa,waliuliwa.
Waliteswa na wanajeshi,Marekani
wakiwa pembeni,wakatumikishwa kitumwa.
Wapo wajinga,wataanza kusema,ilikuwa
kampuni siyo serikali ya Marekani,subiri uone!
Wanakijiji walifungua kesi ya madai
dhidi ya kampuni hilo la Unocal,kulitumia jeshi la Yangon kuua vibarua,kubaka
na kuwatumikisha kitumwa,pasipo malipo ili gesi iende nchi nyingine.
Shirika la Habari la Agence France
Presse(AFP) likasema miaka saba iliyopita kwamba, Unocal walipobanwa wakasema
ukweli,wakakubali kuzungumza na wanavijiji wa Burma ili kesi iondolewe
mahakamani,walikubali kuwalipa fidia na kuwasaidia kuimarisha maendeleo.
Nimesema Unocal; ni kampuni la
Kimarekani la kuchimba gesi.Mahakala ilikuwa inakaribia kuwapa ushindi
wanavijiji wa Burma waliofungua kesi Califonia.
Nikusimulie kidogo.Jumanne,Desemba
10, mwaka 2003 kampuni hili katili la Kimarekani lilipandishwa kizimbani huko
California ili kujibu mashitaka ya hao wanavijiji wa Burma, na kuhalifu haki za
Binadamu.
Nchi ya Burma wakati huo ilikuwa
chini ya utawala wa kiimla wa kijeshi ambao Marekani hujidai sana kuupinga hapa
Barani Afrika,kumbe sehemu nyingine wanajali maslahi tu.
Hii ‘Brutal Military Junta’
waliwalazimisha raia kujenga bomba la urefu wa kilomita 62,waliokataa
waliuliwa,akina mama wakabakwa na kuumizwa bila fidia.
Bomba lenyewe lilikuwa la kilomita
62 sawa na maili 39 ili kupeleka gesi kutoka Myanmar kwenda Thailand.
Basi, Unocal walipobanwa wakakubali
kulipa fidia maana kazi waliyofanya wanavijiji hawa wa Myanmar mwaka 1990s
ilikuwa ya thamani ya Dola bilioni 1.2.
Sasa jiulize,wewe shabiki wa hawa
Marekani na Ulaya, Utumwa kwa wananchi wa Burma
ndiyo Haki za Binadamu?
Utumwa huu katika karne ya karibuni?
Unocal walishirikiana na kampuni la
Ufaransa,Total kupeleka gesi Thai.
Tutazame wanavyoharibu mazingira ya
dunia,hasa nchi za dunia ya tatu na kukataa kusaini mikataba ya upunguzaji wa
hewa za sumu angani,ili tupatwe majanga ya asili.Laiti nchi hizi zingeungana
kupinga ubeberu na ukoloni mambo leo,zingeiamrisha Marekani!
MAREKANI CHIMBUKO LA MAJANGA
haya ni majanga ya kiasili ambayo
ukiyachunguza yataletwa na kiburi cha Moabu,Marekani na washirika wake,kwa
kuchafua sana anga la dunia,kukataa kusaini mikataba kama ule wa Kyoto(Kyoto
Protocol) ili maji yachafuke,viumbe wafe kwa Ongezeko la joto na mabadiliko ya
tabianchi, mafuriko kila mahali,
vifo majanga, kansa, ukimwi,vyanzo
vya maji kuwa damu,kutoboka kwa utando wa Ozone n.k
Moabu ya kiroho(Marekani)
iligoma kutia saini Mkataba wa Kyoto mwaka 1997,kwa sababu kufanya hivyo
kungeleta hasara kwa wafanyabiashara wan chi hiyo-Wakaona heri kuongeza madhara
kwa kumwaga hewa chafu angani ili wajipatie UTAJIRI.
Miongoni mwa shughuli za kiuchumi za
binadamu zinazoharibiwa sana na uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabia
ya nchi ni pamoja na kilimo, ufugaji, uvuvi n.k
Mkutano wa New
York ulioanza Septemba 22 mwak 2009, umefanyika takriban miaka 12 kamili tangu
mkutano wa Kyoto, Japan ufanyike Desemba mwaka 1997.
Katika mkutano wa
Kyoto, viongozi wa mataifa zaidi ya 150 duniani walikutana wakaweka
itifaki ambayo ingewezesha kupunguza hewani kiwango kikubwa cha gesi au hewa
chafu ya sumu zinazoletwa na hewa ya ukaa(C02) na gesi nyingine
kama CH4,N20, HFC8, PFC8 na SF6.
Mkataba huo
uliojulikana kama itifaki ya Kyoto(Kyoto Protocol) uliokusudia kupunguza
gesi za sumu duniani kwa silimia 5.2 kabla ya kufika mwaka 2012.
Mataifa yaliyoshurutishwa
kusaini mkataba huo wa Kyoto ni nchi zote 38 zenye viwanda duniani..
Mataifa yote 15 ya Umoja wa
Ulaya(EU) yakakubali kupunguza asilimia nane ya taka hewa zake duniani.
Marekani ilitakiwa kupunguza asilimia saba ya gesi zake inazotupa angani.
Japan, ilitakiwa kupunguza
asilimia sita ya taka sumu inazotupa angani, na nchi zinazoendelea zilitakiwa
kupunguza kiwango chochote kwa uhuru wake.
Marekani ilisaini mkataba huo
Novemba 12, mwaka 1998, lakini kutokana na kitisho kutoka kwa matajiri wenye
viwanda nchini humo, serikali ya Rais Bill Clinton ilichelea kupeleka ajenda
hiyo katika Bunge la seneti.
Kwa sababu, kusaini mkataba wa
Kyoto na kuutekeleza, maana yake ni kwamba viwanda vya Marekani vingelazimika
kupunguza uzalishaji.
Ni kwa sababu hii serikali ya
Clinton iliufyata.
Mkutano mwingine wa kujadili
upunguzaji wa taka za sumu hewani ulifanyika Bonn, Ujerumani Julai 2001.
Utawala wa George .W. Bush
ulitangaza kujitoa katika mkataba wa Kyoto kwa madai kwamba uliweka zigo kubwa
katika nchi zilizoendelea bila kuzingatia usawa.
Marekani, waligeuka wapinzani
wakubwa katika ajenda za kupunguza hewa za sumu duniani, tangu huko mjini Bonn,
Ujerumani na mahali pengine, kwa sababu ya maslahi yake na ya viwanda vyake,
bila kujali madhara makubwa yaliyotokana na wingi wa viwanda vyake kutupa
angani hewa chafui zenye kusababisha majanga makubwa kwa Ulimwengu mzima..
Hizi ndizo haki za binadamu Ulaya na
Marekani?
Kwa shingo upande, walikubali
kupunguza hewa hizo za sumu ili kutekeleza huo mkataba au itifaki ya Kyoto ya
1997.
Katika makubaliano ya mjini Bonn,
mataifa makubwa yenye viwanda yanayomwaga kwa wingi hewa za sumu angani,
yalishauriwa kufuata malengo waliyowekewa ya kupunguza hewa ya ukka katika
anga.
Kulingana na Shirika la
Kudhibiti Uharibifu wa mazingira, hewa ya ukaa(carbon dioxide) imeongezeka sana
angani kutoka mwaka 1990 hadi sasa; na hii ni kutokana na shughuli za binadamu,
ikiwa ni pamoja na viwanda na migodi.
Wakati hewa za sumu
zinapoongezeka sana duniani, misitu ama miti inayopunguza kwa kiwango kikubwa
hewa ya ukaa kwa kutengenezea chakula chake(starch) inatoweka kwa kasi na kwa
kiwango cha kutisha sana.
Tazama nchi zinavyoongeza
sana kiwango cha hewa za sumu angani.
Mashariki ya Mbali pamoja na
Oceania wanachafua anga kwa kiwango cha asilimia 28.9.
Amerika ya Kaskazini huchafua anga
kwa kiwango cha asilimia 28.8.
Marekani pekee inachafua
anga la dunia nzima kwa moshi wa magari na viwanda vyake kwa asilimia 24.7.
Ulaya Magharibi, kwa
pamoja huchafua anga la dunia kwa asilimia 16.5, wakati Amerika Amerika ya
Kusini nzima na Kati huchafua anga la dunia kwa kiwango cha asilimia 4.3.
Ulaya Mashariki, na
iliyokuwa Jamhuri ya Kisovieti(USSR) huchafua anga la dunia nzima kwa kiwango
cha asilimia 12.8. Mashariki ya Kati huchafua anga kwa kiwango cha asilimia
4.7.
Afrika, inachangia katika
uchafuzi wa anga la dunia kwa asilimia 3.9 tu.
Hii ni kwa mujibu wa Ripoti za
Energy Information Administration, kuanzia
mwaka 1999.
Afrika inayochangia kwa
kiwango kidogo sana katika uchafuzi wa hewa angani, ndiyo inayoathiriwa sana na
madhara makubwa ya uchafuzi wa hewa angani unaoleta mabadiliko ya tabia
ya nchi.
Mifugo ya Afrika, hususan
Kenya na hapa kwetu hufa kwa ukame unaoletwa na uchafuzi wa mazingira ya
anga. Uchafuzi wa anga ndiyo chanzo cha ukame huko kwetu Afrika. Ukamwe huu
ndiyo unaochangia jangwa kuongezeka, ukame na njaa na vifo vya watu pia.
Kulingana na uchafuzi huo wa
hewa angani, Benki ya Dunia(WB) ilishasema mwaka 2001 kwamba kila mwaka watoto
wachanga wapataao 500,000 wangepoteza maisha duniani pote kwa sababu ya
uharibifu huu mkubwa wa anga.
Vifo huletwa na viwanda vya Ulaya na
Marekani siyo? Kumnyang’anya mtu uhai siyo haki za binadamu sawa?
Kunatokea mvua za sumu(acid
rains) zitakazosababisha uharibifu mkubwa sana wa misitu hasa ya Afrika, na
wala mvua za sumu hizi za viwanda vya mataifa makubwa haziharibu huko kwao peke
yake.
Nataka kusema kwamba, Marekani
inaongoza duniani kwa uchafuzi wa anga, lakini athari zake tunapata sisi huku;
tunakufa kwa njaa na matokeo ya ukame na hata vimbunga kama Mitch, tsunami na
Katrina ambavyo vikitokea, huua maelfu ya watu bila kujali mipaka ya nchi za
viwanda na zisizokuwa na viwanda.
Ni kwa sababu hii, ubeberu wa
Marekani wa kukataa kutia saini mikataba ya upunguzaji wa hewa na taka za sumu,
kama huo wa Kyoto wa mwaka 1997, ni hatari kwa maisha ya watu, hasa tuishio
nchi masikini.
Ingekuwa heri kama Mkutano wa
New York na Afrika ya Kusini ungeipa kibano kikali Marekani kwa kiburi
chake na kuwelka mbele maslahi binafsi ya viwanda vyao, huku ng’ombe wa
masikini wanapokufa kwa maelfu huku kwetu, pasipo fidia.
Marekani, hukimbilia
kuliburuza Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuzitenga nchi nyingine kaidi
kutekeleza mikata kama ya Nyuklia n.k
Ni Marekani hiyo hiyo inayotaka Iran na
Korea Kaskazini na Iran zitengwe au zishambuliwe kijeshi kwa kukataa kutia
saini mkataba wa kupunguza silaha za nyuklia.
Mbona yenyewe inakataa
kwa ubabe kutekeleza mkataba wa Kyoto, unaotaka hewa za sumu zinazoleta
majanga duniani kudhibitiwa. Ongezeko la joto duniani linaloleta hayo majanga
kama tsunami, huleta madhara hadi huku Bahari ya Hindi na kusababisha vifo hata
Kenya, Tanzania na Somali. Kwa nini Marekani haidhibitiwi ama kupewa kibano au
kushambuliwa kijeshi, kama yenyewe ilivyozishambulia Irak na Afghanistan,
na iko mbioni kuzishambulia Iran na Korea Kaskazini kwa kukataa kutekeleza
mikataba ya upunguzaji silaha za sumu?
Sumu inayoua watu si ndiyo
iliyo,o pia katika silaha za atomiki na ndiyo ile inayorushwa angani na viwanda
vya Marekani na Ulaya, bila kudhibitiwa na mtu, tena kibabe?
Ni kwa sababu hii, viongozi wa
Afrika waliokwenda New York kujadili kitisho cha hewa za sumu angani na
mabadiliko ya tabia ya nchi, wanapaswa kutoa tamko kali la kuikemea
Marekani au ikibidi kuiwekea vikwazo vya kiuchumi na kuitenga na Jumuiya za
Kimataifa, kwa vitendo vyake vya kibabe vya kuleta maafa Ulimwenguni.
Dunia haina ubavu wa kuitenga
Marekani?
Rasilimali za Waarabu na Waafrika
zinatosha kuwa silaha ya kuikomesha Marekani,kama siyo ujinga wetu wenyewe.
Marekani haiwezi kushambuliwa
kijeshi na dunia nzima ili kuishikisha adabu iache kuiangamiza dunia kwa
kumwaga sumu tani mamilioni kwa siku, huku ikikataa kutia saini kila mkataba
unaowataka kupunguza sumu?
Wakuu wa nchi za
Afrika(akiwemo Rais Kikwete) wanaporejea kutoka New York, wanapaswa kuwaambia
wananchi wao, ni namna gani wamembana Barack Obama, kwa sababu nchi yake ina
kiburi cha ubeberu, kuendeleza uzalishaji wa taka sumu, zinazoleta saratani ya
ngozi huku, kuleta jangwa ama ukame na kuua mifugo Afrika, hususan Tanzania na
Kenya.
Shughuli za kilimo na ufugaji,
ambazo hufanywa na masikini huku Afrika Mashariki zinatatizwa sasa na
mabadiliko ya tabia ya nchi na ukame. Chakula cha binadamu hakuna, kwa sababu
Afrika inakuwa jangwa, kwa sababu Jangwa la Sahara lililoko Kaskazini
linakaribia kushikana na lile la Kalahari, lililopo Kusini.
Sasa, mvua itanyesha jangwani?
Ni kwa sababu hii, tunasema,
kiburi cha Marekani kimekwisha kuleta majanga makubwa hapa Kwetu Tanzania tangu
wakate kusaini Mkataba wa Kyoto Desemba 1997 hadi mkutano huo ulipofanyika New
York, Septemba, 2009.
Ni kwa sababu hii, Rais
Kikwete na ujumbe wake, wanapaswa kuwaambia Watanzania, Rais Obama wa Marekani,
ameambiwa kwa kiwango gani kulipa fidia ya mifugo ya Wamasai, Wajitta,
Wasukuma, Wakurya na wafugaji wengine ambao mifugo yao inaangamia kwa sababu ya
ukame ulioletwa na sumu na taka za hewani kutoka viwanda vya Mabwanyenye wa
Marekani?
Vinginevyo, ile kasi ya Mwarabu kumnyima Mzungu mafuta
ilikwenda wapi ili kukomesha kiburi chao?
Tuesday, October 1, 2013
AL-SHABAAB,AL-QAEDA
!
Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa,Ban Ki-Moon, ambaye ni raia wa Korea Kusini, hana ubavu wa
kusema ukweli kuhusu chimbuko la kitisho cha magaidi hapa Duniani.
Kama
hajipendi, anaweza kumfuata kuzimu Katibu Mkuu wa Pili wa Umoja wa
Mataifa,Dk.Darg Hjalmar Carl Hammarskjold wa Sweden!
KI-Moon,
anatoka nchi kibaraka wa Mataifa Makubwa ya Magharibi, ambayo yameigawa Dunia
katika mihimili miwili.
Ugaidi, ni
zao la chuki za zama za Vita Baridi,kufuatia Dunia kutengwa mafungu mawili.
Korea mbili
ni adui wakubwa,kufuatia kutengwa katika siasa za Kikomunisti na kibwanyenye.
Inakisiwa
kwamba,Warusi(Wakomunisti) walikuwa wakidhibiti maisha nchini Somalia tangu
mwaka 1968.
Walikusudia
kujitanua hadi nchi zote za Upembe wa Afrika(The Horn of Africa) ambazo ni
pamoja na Eritrea,Ethiopia, na Djibouti.
Kufuatia
hali hiyo,Rais Jimmy Carter wa Marekani alikuwa na wajibu kuzuia Warusi
kusambaza ushawishi wao Somalia,Ethiopia na mataifa ya jirani ya Kiarabu.
Urusi,ilikuwa
na vituo vya kijeshi(Military Bases) katika nchi hizi za Upembe wa Afrika,hadi
katika njia kuelekea Arabuni na Afghanistan na Pakistan.
Kwa
hiyo,Marekani ikawa na kazi ya kuondoa ushawishi na utawala wa Kisovieti(Soviet
Imperialism) katika Upembe wa Afrika.
Wakati huo,
CUBA na raia wake walitoa msaada mkubwa hapa Brani Afrika.Cuba ilikuwa “Mkono
Msaidizi” wa Dola kuu la Kisovieti(USSR).
Msomaji,
unaweza kutambua sasa kwamba nchi zote za Ulaya Masharikizilionekana kuangukia
zaidi siasa za mrengo wa kushoto wa Kambi ya Mashariki,na siasa zao za Ki-Marx
na Lenin.
Kwa sababu
hiyo,mataifa ya Ulaya Magharibi(ikiwemo Marekani) yalihaha kuhakikisha kuzuia
Ukomunisti usisambae mithili ya saratani hadi Upembe wa Afrika, na tuseme
Afrika nzima,na maslahi yao(ya kikoloni) yakawa hatarini!
Dola la
Kisovieti(USSR)linasemwa kuleta silaha nyingi eneo la Upembe wa Afrika,tena
nzito.Vita Baridi vilianza mara baada ya Vita vya Pili vya Dunia
kwisha,mwaka1945.
Baada ya
vita hivi vya Pili vya Dunia,Mataifa ya Mashariki yakiongozwa na Urusi(USSR)
nay a Magharibi yakiongozwa na Mrekani yaliamkakugombea udhibiti wa Mataifa ya
Ulimwengu wa Tatu,hususan Afrika,Asia na Amerika Kusini.
Kwa kuwa
Warusi hawawezi kushindana na Marekani na washirika wake kwa uchumi, wao
walianza kusambaza msaada wa silaha,magari ya deraya na ndege za kivita.
Hata Rais wa
Somalia,Muhammad Siad Barre, alipewa msaada wa zana za kivita na USSR. Somalia
ya sasa inayolaumiwa kuwafuga magaidi wa al-Shabaab,hutokana na mfuo wa
kikoloni wa Kiingereza na Italia,wakijidai kuunganisha taifa mwaka 1960.
Haya ni
mataifa mengine duniani yanayouza silaha nje kuliko nchi nyingine nyingi.
Wasomali ni
wahamaji(nomadic tribesmen) wasiokuwa na makao maalum zama hizo.
Hawakuwa na
rasilimali za kutosha,halafu uchumi wao haukuwa mzuri,kwa sababu ya kutokaa
eneo moja na kuzalisha mali.
Wakati
mwingine walitaka kuungana na Wasomali wenzao wa Ethiopia,Kenya na Djibouti.
Hivyo,ili
kutimiza azma yao walihitaji silaha tena kali.Ikulu ya Marekani(White House)
ilipokawia kuwafadhili bunduki,Ikulu ya Urusi(Kremlin) ikawapa bunduki kali
hawa Wasomali wanaosemwa kuwa ‘Wakali’ wanapoishi kuzunguka Bandari kuanzia
Mogadishu, hadi Ghuba ya Aden na Bahari ya Hindi.
Sasa utaona
Pwani BAHARI YA Hindi kuanzia Mogadishu,Pwani ya Djibouti,Aden,Yemen,Kenya na
Tanzania ni eneo hatari hata leo kwa maharamia wa Kisomali wenye bunduki za
rashasha za Kirusi.
Wamarekani
waliwahi kusema, ingawa Siad Barre alijidai kutumikia Warusi na falsafa za Marx na Lenin, mvuto wake ulielekea kwenye
Uislam.
‘Doctrines’
za Kirusi hazikufua dafu Somalia, ila bunduki zao walizipeda sana,
nazilipatikana kwa wingi;wakazitumia kwa njia yoyote kupatia chakula na
mahitaji mengine.
Inasemwa,Mfalme
Haile Selassie wa Ethiopia aliunga mkono siasa za Magharibi; akapinduliwa kwa
nguvu za jeshi kutoka Urusi,ili kundi la Wakomunisti washike nchi hii muhimu.
Habari hizi,
zikubaliwe au zikataliwe na ubongo wako,lakini tunapata picha halisi kwamba,
vita upembe huu wa Afrika(The Horn of Africa) yaani Somalia,Djibouti,Ethiopia
na Eritrea ni matokeo ya Ikulu mbili-Kremlin na White House-kunyukana eneo hili
tete hata leo,na matokeo yake wamezaliwa al-Shabaab wanaoua watu Kenya,Uganda
labda watakuja Tanzania siku si nyingi!
Mungu
apishilie mbali!!
Nani
adhibiti ushawishi wa eneo hilo,ndiyo shida inayoleta changamoto za visasi vya
magaidi hapa kwetu Afrika Mashariki.
Utawala wa
Mengistu Haile Mariam(Mkomunisti) baada ya Haile Selassie,ukasemwa na Magharibi
kwamba ulileta, “Terror” hofu kuu Ethiopia!
Neno hili,
“Terror” hofu.ukiliongezea “ism” unapata ‘TERRORISM’ maana yake Ugaidi.
Kwa hiyo
Kambi ya Magharibi inasema aliyeleta ugaidi eneo hilo ni Urusi. Na tukumbuke
Propaganda za Kimagharibi.Bila nguvu nyingine ya Magharibi kutaka kujitanua
huko,Urusi wasinge sogea.
Ni kwa
sababu hii, twapata picha kwamba chimbuko la ugaidi eneo hilo lote ni Madola
makubwa ya Marekani na Urusi kujitanua huko.
Wakati Urusi
inatawala mataifa haya kwa ‘remote’ White House hawakuchoka,wakawasaidia
wafuasi wao ndani ya nchi hizi fedha na bunduki,ili kukamata Ikulu ambayo
ingetawala Bandari za tangu Mogadishu,Djibouti,Aden, na Mlango Bahari wa
Shamu,YEMEN,kuelekea Pakistan na Afghanistan.
Sasa unaona
umuhimu wa kudhibiti eneo hilo la Bahari ya Hindi na Bandari hizo?
Bahari ya
Shamu, ambayo Waisraeli wa zama za Musa waliivuka kwa miguu bila boti,ni muhimu
sana kuunganisha Bahari za Hindi na Mediterranean.
MFEREJI WA
SUEZ,uliochimbwa na Wafaransa na Uingereza huko Misri ni muhimu eneo hilo ili
kuunganisha safari za meli kati ya Bahari za Mediterranean ,Shamu(Red Sea) na
Hindi.
Mto
Nile,unaoanzia Ziwa Nyanza na kutiririka umbali wa kilomita 6,900 unapita eneo
hilo pia.Huu ni mto ambao ni damu itiayo uhai nchini Misri(the life blood to
Egyptians), ni muhimu kusafirisha mafuta,bidhaa muhimu kwa uchumi wa
Ulaya,Mashariki ya Kati,ya Mbali na Amerika na Afrika.
Hili ni eneo
muhimu sana kiuchumi,ndiyo maana madola makubwa hupigana vikumbo kulikamata kwa
usalama wa nchi zao, au usalama wa uchumi wao.
Haya madola
makubwa-Urusi na Marekani- ndiyo waliochochea vita kati ya Somalia na
Ethiopia,kupigania Jimbo la Ogaden, eneo ambalo ni moja ya tano ya Ethiopia.
Ethiopia,Somalia
na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Yemen,hukodolewa macho na udenda na madola haya
makubwa ili kuweka ‘interests’ zao.
Mpango
mkubwa(master plan) wa mataifa makubwa ni kukamata eneo la Kusini mwa Afrika,
na Mataifa tajiri ya Mafuta katika Ghuba ya Arabia.
Chuki za Magharibi dhidi ya Fidel Alejandro
Castro Ruz, ni kufika Afrika kusaidiana na washirika wao Urusi,kukomesha
ukoloni wa Ulaya Magharibi huku Afrika Kusini.
Walikuja
hata kushawishi Somalia kugeukia siasa za Ki-Marx.Utaona hata Shirika la
Ujasusi la Marekani(CIA)likahaha kushawishi Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
jijini Dar es salaam mwaka 1964,ili Zanzibar sisjekuangukia Ukomunisti!
Rais Jimmy
Carter alitoa amri kwa Waziri wa Mambo ya Nje,Cyrus Vance,na Mshauri wake wa
Usalama wa Taifa,Zbignew Brzezinski,kuhakikisha(to move to every possible way)
yaani hata kwa ugaidi ama mabomu, alisema “to get Somalia to be our friend”.
Hii ni kauli
ya Jimmy Carter,ili SOMALIA iwe ‘rafiki’ yao tena kwa gharama yoyote!
Tazama kilichofanyika! Marekani chini ya
Shirika lake la Ujasusi,CIA wakaanza kuipa Somalia msaada wa silaha! Huo ni
mwaka 1977.
Ilisemwa eti ili ‘kujilinda’ ila wasitumie
silaha dhidi ya Djibouti na Kenya!
WAPI MAGAIDI
WANAPATA SILAHA ZA HATARI?
Sasa silaha
za West Gate zimetoka wapi?
‘Msaada’huo
wa silaha kutoka MAREKANI kwenda Mogadishu ,ulikuwa na masharti kwamba Marekani
isiwasaidie wanamgambo wa KISOMALI(Somali Liberation Front) huko Ogaden.
Msomaji
anapofikiri vizuri, aone kwamba Marekani inapotoa msaada hata kwa Waasi,huwa na
kwa sababu ya maslahi,vyama vya ukombozi navyo hunyimwa au kupewa msaada kwa
sababu ya maslahi.
Hawa
Wasomali wameishi Ogaden zaidi ya miaka 500
.Sasa
MAREKANI wanaibembeleza Somalia iwakate URUSI ili wao wasaidie Mradi wa
kukomboa Ogaden.
Unaanza kuona
Somalia inapigana na Ethiopia,Marekani wakiwa nyuma ya Somalia!
Urusi
inaleta MiG-21 Jets, vifaru vipya vya kisasa 400,Mi-8 ambazo ni helkopta za
kivita 30 na maelfu ya silaha kuizuia Marekani kulitawala eneo hilo.
Huku
nyuma,BBC,VoA,SKY NEWS.CNN n.k wanatangaza kwamba,Somalia na Ethiopia
wanapigana kwa sababu ya Ogaden!
Mbumbumbu wa
Tanzania wanasema,”Afrika Bara la Vita! Bara la Giza ,Magonjwa,na Machafuko!!”
Mabwana wa
Vita wa Afrika(war lords) wanabebwa na mataifa haya ya Ulaya,na huwezi kuyaona
mpaka uwe na macho matatu.
‘Satellites’
na ‘radar’ za Marekani za upelelezi zinategwa tangu Misri hadi
Pakistan,zinaletwa upambe huu wa Afrika ili kukoleza vita,ili Urusi wapigwe
waondoke!
Antonov-22
na Ilyushin-76 za Kirusi nazo zinajongea Upembe huo ili kubyesha mabomu makali
kupambana na Marekani aliyekificha nyuma ya pazia,mgongoni mwa Msomali,katika
vita baina ya Somalia na Ethiopia.
Yemen
inatumika kama ‘depots’ za silaha za Mrusi.
Cuba nao
wanaleta askari 15,000 toka Angola(Angola ilisaidiwa ikawa huru 1975) sasa CUBA
anajitoa mhanga kupambana bega kwa bega na Mrusi ili kumzuia Marekani kutwaa
Ogaden, mgongoni mwa Msomali!
General
Vasily Petrov wa Urusi anaongoza mapambano huku, akina Vance nao wanachochea
upande huu, basi Afrika inanuka riha ya baruti na risasi,kwa maslahi ya madola
ya Ulaya!
Somalia
inazidiwa,inaomba silaha Magharibi,vita ngumu Ogaden.
Shah wa
Iran(alikuwa Kibaraka wa Marekani) anaonywa asije akapeleka silaha yoyote
aliyopewa na Marekani katika nchi za Dunia ya Tatu,zisije zikatumika kumsaidia
Ethiopia na Warusi,vita ngumu hii bwana!
White House,
inatoa amri-hakuna kuuza silaha mEthiopia ili Ogaden itekwe na Msomali!
Ili Urafiki
wa Marekani na Msomali upatikane! Naam, maslahi ya mataifa makubwa hupatikana
kwa damu mbichi ya Mwafrika,Mwarabu,Mhindi ama Mhindi Mwekundu wa Bara la
Kusini mwa Marekani.
Viongozi wa
Kiarabu,tangu Sudan hadi Saudi Arabia wanaamrishwa na White House,kuisaidia
Somalia, msaada MUHIMU wa silaha(a significant military aid).
Lengo,ni ili
Ukomunisti ushindwe Afrika. Hawa akina Brzezinski walishatengeneza Ukimwi mwaka
huo wa 1975 ili kuwaua Waafrika,kuwapunguza ili wao wachukue mali kwa gharama
yoyote, sasa wako Somalia.
Wanapoona
Warusi na Wacuba wameingia wenyewe vitani,na vita vinamwelemea Msomali,wanaanza
kutangaza mikataba ya kusimamisha utengenezaji wa silaha!
Wanaita kwa
Kingereza, “Arms-limitation talks” ama Arms Limitation Treaty!
Sasa
wanasema Mrusi akiendelea kuwasaidia Wahabeshi, basi mazungumzo hayo ya
kupunguza silaha duniani yatakuwa hatarini kuvunjika!
Msomaji,sijui
unaona unafiki huu wa Marekani! Kumbuka hii siyo hadithi ya Paukwa Pakawa! Ni
ukweli kutokana na Historia.
Urafiki wa
Marekani na Somalia unakuja kwa njia ya kuchochea vita Ogaden,Cuba nao wanaleta
‘artillery’ na MiGs zinanyesha mabomu tani nyingi,Wasomali wanapigwa wanakimbia
nyuma milimani huko JIJIGA!
Damu ya
Wasomali inabubujika kama mto,mvua ya mabomu inaendelea,wanakatwa vipande
vipande kwa mabomu-maguruneti kwa uchochezi wa Kimarekani inayotaka kuikamata
Somalia kwa gharama yoyote.
Majeruhi
walikuwa maelfu.
Nataka ujue
ugaidi wa Somalia ulianza lini?
Kwa nini na kwa sababu gani?
Kumbuka,vita
baina ya Somalia na Ethiopia vimechochewa na Rais Jimmy Carter ili ajifanye
rafiki wa Somalia,kumzuia Mrusi kujitanua Upembe wa Afrika.
Hii kampeni iliitwa, ‘THE SOMALIA’S OGADEN CAMPAIGN’ unaweza
kufuatilia ujue ninachoandika hapa.Wajinga wanaposema,Wasomali wapenda vita!
Jiulizeni nani yuko nyuma yao?
Nani huwapa pesa na silaha? Ni Mwarabu?
Mchina? Mzungu!!
Wamarekani
wanapoona Msomali kachakazwa vikali,damu inavuja puani, wanaandika barua ya
rangi ya njano na nyeusi kusema!
“Serikali ya
Somalia itoe tamko, sisi(Marekani) tumeona katika vita hivyo vya Ogaden,kuna
mkono wa Mrusi”,Barua ilisema.
Sasa eti
ndiyo MAREKANI wanaona kwamba kuna Mrusi ameleta MiG-21 zipatazo 48, na kuna
marubani wa Cuba wako mstari wa mbele kuisaidia Ethiopia, vifaru 150 vimetoka
Msumbiji nchi nyingine ya siasa za Ki-Marx,sawa na Zimbabwe ya Robert Mugabe
ambaye wanamchukia sana.
Hadi Iran
kule ambako kuna mafuta ushawishi unaendelea wametoka akina Ahmadnejad,sasa
utawala unajipendekeza Marekani. Ni Urusi,Marekani!
Wacuba
wanafundisha Wayemen kutumia bunduki za Mrusi,akina Carlos The JACKAL
walifunzwa ugaidi na wa Cuba,Warusi ili kupambana na ubeberu wa
Kimarekani.Akina Osama walifundishwa ugaidi na Marekani ili kupambana na
Ukomunisti walipovamia Afghanistan mwaka 1979!
Muktadha wa
makala hii,ni ili msomaji ajue kwamba,Marekani na washirika wake huwa hawana ‘Clear Policy’ kuhusu BARA LA
AFRIKA.
White House
na Kremlin huchochea vita hapa Barani;hufunza wanamgambo eneo hili lote kuanzia
Somali,Urabuni,Bara Hindi hadi Pakistan na Afghanistan.
Hata Osama
Bin Laden, alitokana na makambi ya kigaidi yalifofadhiliwa na Marekani,lengo
likiwa kupambana na Urusi waliotaka kusimika Ukomunisti pindi walipovamia Kabul
mwaka 1979.
Wanamwaga
silaha na mabomu,wanachochea chuki;vita vinapouma wanaitana mkutanoni Ulaya ili
kuitisha “ARMS-LIMITATION TALKS”
Waziri kama
John Kerry anakwenda Moscow,inadaiwa wanajadili kumaliza vita,ama kuepusha vita
Syria,Misri,Libya,IRAK nk.
“Negotiations”
zinazofanywa na kutangazwa na vyombo vya habari vya Kimagharibi, si kitu bali
uongo na Propaganda.
Wanataka
kujitakasa dhidi ya lawama kwa kuwa vitanga vya mikono yao huchuruzika damu
mbichi za Waafrika,Waarabu,Wahindi ama raia wa Ulimwengu wa Tatu! Kila mahali
penye maslahi ya kisiasa na kiuchumi.
Vita ya
Madola Makubwa ni “To conquer The Third World” ama kuutawala Ulimwengu wa Tatu,wa
nchi changa,hasa zenye utajiri wa almasi,dhahabu,mafuta,gesi n.k
Wakiona
Waafrika mnapukutika kwa vita,damu inamwagika,Putin na Obama wanaitana Moscow
ama popote,wanakaa wanaambizana kupeana zabuni.
Subscribe to:
Posts (Atom)