SHERIA, inapaswa kuwa nakala ya
tabia halisi ya jamii iliyotunga sharia husika.
Sheria hutokana na KATIBA YA
NCHI,ambayo ndiyo sheria mama.Katiba lazima kuakisi tabia na mwenendo wa
wenye sharia hiyo.
Sheria ya walevi,lazima kuakisi
ulevi-ulevi,sharia ama katiba ya machangudoa,mashoga na wasagaji,lazima
izingatie tabia za watu hawa.
Jamii adili na yenye kutaka haki
na usawa, itatengeneza sharia na katiba yenye kuakisi uadilifu,ukweli na
usawa. Haiwezekani walevi,wabwia unga na machangudoa wakawatengenezea
makasisi,maaskofu na masheikh sharia au kanuni za kufuata katika kazi zao
za dini!
Sasa, najiuliza: Sisi Watanzania
ni nani hata tutengeneze Katiba adili na sheria za unyofu?
Sisi hawa waongo-waongo,tapeli, ‘kekundu
na keusi’ na wapenda ‘short-cut’ ati tutengeneze Katiba nyoofu yenye
kuzingatia usawa? Siyo kutengeneza sheria na Katiba yenye mianya ya
rushwa,ufisadi na uonevu kwa masikini na watu wa kawaida,wakulima wa
vijijini?
Sheria ama katiba laima ifanane
na watu wenyewe wenye kuitunga walivyo! Haiwezekani wezi, machangudoa na
wakwapuzi wa wake za watu kutunga sheria yenye kusema:
“Usiibe, usizini,usikwapue mke
wa mtu,usi…”
Watu waliopinda, watataka sheria
za “Usi” ziondoke,ili waendelee kufanya ukiranga wao kwaq uhuru mkubwa!
Ndiyo maana utasikia watu wabwia
unga wakidai demokrasia ya kuvuta hata bangi hadharani,na serikali kama za
Marekani na Uingereza zimekubali,wanasema ndiyo demokrasia na uhuru,haki za
binadamu n.k
Sheria ya Mungu(AMRI 10 ZA
MUNGU) inafanana na Mungu mwenyewe na Malaika zake.Na watu wanaompenda
Mungu hawana budi kufanana naye na kuwa na tabia inayosemwa kwenye Amri
hizo.Wazinzi na wezi,waonezi na wachawi hawawezi kukubaliana na AMRI za
Mungu,watasema ni sheria kandamizi nay a Kiimla!
Sasa jiulize, katiba ya
Mungu(AMRI 10 ZA MUNGU) tukisema ikubaliwe kuwa Katiba ya Tanzania,halafu
zitungwe kanuni za adhabu kwa wale wasiotaka kuitii,itakuwaje?
Watu wengi wataingia mitaani
kulalamika na kuipinga kwamba inawanyima uhuru,siyo? Mungu na malaika zake
na wafuasi wao hawataguswa na adhabu zitakazowakabili
wazinzi,wezi,mafisadi, watambikia mizimu na wakatili,wauaji,
wafiraji,mashoga na wasagaji,siyo?
Wenye kufanana na katiba
inayotungwa na inayozaa sheria na kanuni za adhabu kwa wakosaji na
watukutu,hawana shida.
Haiwezekani kutunga Katiba safi na
ya haki, wakati watu wenyewe wanaoitunga wamepinda,watatafuta upenyo ili
waendelee kuiba,kudhulumu na kuhujumu masikini. Tusidanganyike na katiba
mpya,wakati sisi siyo wapya kimtazamo,tunaishi kwa dhuluma kila wakati.
Angalia vyombo vya habari na
taasisi zao, ambazo Naibu Waziri wa Wizara husika, Juma Nkamia, aliwahi
kusema taasisi hizo ni NGO za watu binafsi,wakabisha!
Kwanza wanahabari,viongozi wao
na taasisi zao hazinafanani kabisa na katiba zao na malengo na kauli mbiu
zao ambazo ni adili,za kweli na za haki tupu.
Sekretari wa ofisi moja inayojidai kuhudumia
wanahabari nchini, aliwaalika nduguze wanne waje kuhudhuria semina ya siku
tano iliyoandamana na posho nono ya shilingi 40,000 kila siku,badala ya
kualika wanahabari stahiki!
Hao jamaa zake hawakuwa
waandishi wa habari; isipokuwa walikuwa “mamluki” ambao lengo lao
lilikuwa kupata pesa, wanunue magari mazuri na nyumba za kuishi.
Semina hiyo, eti iliandaliwa kwa
waandishi wa habari kwa siku tano wapate maarifa ya kuinua kiwango cha
taaluma na weledi katika kazi zao za kila siku!
Kila siku,hizi “NGOs” za
Mheshimiwa Juma Nkamia huandaa warsha na semina kwa wanahabari. Lakini
wanaohudhuria ni wenyeviti,makatibu na nyumbandogo zao!
Wanachama wakihoji haya madudu,
wanaitwa wasaliti na wahujumu wa maendeleo ya taaluma ya habari!
Basi, Yule sekretari akawaita
ndugu zake wanne, akawavika joho la uanahabari,kwamba walitokea
Bukoba,mkoani Kagera, kwa hiyo wakalipwa posho nono ya shilingi 40,000 kila
siku kwa siku tano,kwa masharti kwamba mwisho wa semina wagawane na
Yule sekretari kilichopatikana.
Kwa bahati mbaya, waandishi wa
habari wakawastukia mamluki wale na kuanza kuwasaili huko Bukoba walikuwa
wakiandikia vyombo gani?
Wakatekewa.
Walipodadisiwa sana, wakafichua
siri na kusema hawajawahi kuandika hata barua za maoni gazetini, isipokuwa
waliitwa na Yule jamaa yao sekretari, ili kugawana posho!
Yaani, semina ya
wanahabari wanaalikwa jamaa na ndugu za hawa vigogo wa ofisi zinazojidai
kuhudumia wanahabari,hasa mikoni, ili wagawane posho nono. Hata wauza baa
hupewa mialiko ili mradi tu posho ikipatikana,wagawane na wahusika! Hawa
nao siku hizi eti wanataka Katiba Mpya!
Eti, wanasema tasnia ya habari
imevamiwa na makanjanja; sasa hawa wanaoitwa kuhudhuria hizo semina ni kina
nani?
Na wanaohodhi semina tuwaiteje?
Waulize mapato na matumizi ya vyama vya wanahabari,uone utakavyotukanwa! ‘Unatumiwa,
sijui nani!!
Na je, ‘stori’
zisipoonekana magazetini, ama zisipotangazwa runingani na redioni,
walaumiwe wahariri au waandishi wa habari?
Nataka kusema kwamba, zile
semina zinazoandamana na posho ya siku tano au majuma kadhaa, wajanja hawa
wanaalika ndugu zao ,wakati mwingine hata nyumba ndogo zao, wanajigawia
‘ulaji’ mwingi migongoni mwa wanahabari.
Wapo jamaa tulikuwa tunasugua
nao lamia ma kudandia daladala,siku hizi wana ma- ‘VX’ yaliyopatikana
migongoni mwa wanahabari,tena kwa miaka michache tu! Hata wafagizi lazima
wanunue magari,maana fedha zote za miradi hewa wanatunza wao, na hakuna wa
kuwakagua. Mkutano Mkuu ukifika, wanaoitwa rafiki zao,wabishi wanaachwa
solemba.
Siku hizi, wanaojidai
waratibu wa semina,mikutano ,warsha na mafunzo kwa wanahabari,hasa wa
mikoani, huchukua posho na kuwagawia kipapatio tu.Kila unachopewa,lazima
uwagawie,la sivyo hutapewa mialiko milele.
Badala yake, wanaalikwa
hata wauza vocha za simu, mradi wakubali kugawana posho na waandaaji na
waratibu wa semina zile.
Amini usiamini, kuna semina hewa
zinazoratibiwa mikoani, majina ya wanahabari yanaorodheshwa, lakini
hawaitwi kuhudhuria, isipokuwa baadaye zinatafutwa saini bandia ili
ionekane walihudhuria na wakalipwa kiasi kikubwa cha posho, chakula,nauli
na masurufu ya safari.
Hata sasa tunapoelekea Oktoba
31,siku ya uchaguzi mkuu, wajanja walishaomba mamilioni ya fedha kwa
wafadhili, eti kuendesha mafunzo kwa wanahabari.
Lengo eti ni kuinua
kiwango cha taaluma na weledi!Na katiba zipo, “Code of Conduct” za
Professionalism zipo ukutani mwa ofisi zao,tena wameandika ‘Usimpe rushwa
mwandishi wa habari”, upuuzi mkubwa wa katiba za makaratasi,badala ya
katiba kutangulia myoyoni mwa wahusika.
Ukitaka vita, kawaulize ni
wanahabari kiasi gani, na asilimia ngapi waliopewa mafunzo na semina kuhusu
uandishi wa habari za uchaguzi?
Wafadhili, wanadanganywa kwamba
kulikuwa na semina mikoa Fulani na posho zilizlipwa,kumbe ndiyo yale
niliyosema kwenye utangulizi,kwamba miradi hiyo mingi ‘hewa’ ilishatekwa na
wajanja hawa, wanajilipa kumbi,chakula na kuita jamaa zao ambao hata barua
za wasomaji hawajawahi kuziandika magazetini.
Hawa hawajawahi kuwa na nia ya
kuinua kiwango cha taaluma kwa wanahabari,lengo lao ni kupora zile fedha za
wafadhili.Kama mnabisha, kawachunguzeni.
Hata wawezeshaji wanaoitwa
kufundisha semina zile siyo wale magwiji tunaowajua, bali ni ‘jamaa’ zao
ili kujihalalishia ulaji wenyewe kwa wenyewe.
Nataka kusema kwamba, hawa
wataalamu wa kuomba fedha kwa wafadhili,huomba fedha nyingi na kuzitafuna
migongoni mwa wanahabari,kasha huwarushia fupa hapa na pale ili walambe,
kumbe firigisi na mapaja yalisha tiwa kinywani!
Tasnia hii ya habari inajivika
majukumu mazito ya kuelimisha,kufahamisha wapigakura namna ya kuchagua
viongozi bora, na wala siyo bora viongozi.
Eti, waratibu hawa wa
semina na mafunzo(siyo wote) kwa wanahabari wana makusudi ya kuboresha
utendaji wa kiweledi wa wanahabari na taaluma zao kuelekea 2015.
Taaluma, weledi na utapeli
kama niliokwishabainisha mwanzoni, wapi na wapi?Wengine wakati wa
kampeni huvaa fulana na kofia za wagombea,wakishushwa kwenye magari ya
wagombea,wanakasirika wanahamia chama kingine, eti ni waandishi!!
Kumbe,huko mikoani kuna wajanja
wachache wanaoteka nyara semina na mafunzo ya wanahabari, wanawaalika ndugu
na jamaa zao wale watakaokubali kugawana nao posho za semina.
Fedha za malipo ya kumbi za mikutano na
chakula zinaliwa ama zinapunguzwa.Mikutano inafanywa baa,wanasema walifanya
ukumbi wa hoteli kubwa,ili wapate fedha za kununua magari ya bei kali sana!
Nadhani Juma Nkamia anajua
haya,ndio maana alisema ni NGO za watu binafsi!Hawa siku hizi wana midomo
mikubwa kudai katiba mpya,sijui ni mpya vipi,wakati myoyo yao inakiri
wanamiliki mali za wizi migongoni mwa wanahabari.
Viburudisho na vinywaji
vinaondolewa ili fungu lake wakagawane! Hawa wajanja wanakula migongoni mwa
wanahabari.
Wanaalikana wenyewe kwa
wenyewe-wanapeana ulaji, wanagawana kila kazi, za kutafuta kumbi za
mikutano, wakati mwingine mikutano hufanyika magengeni,ili wajipatie fedha.
Eti fedha za wafadhili zinaletwa
ili kuboresha taaluma ya habari wakati wa chaguzi,kumbe ni kujenga vitambi
vya wachache tu,na ndugu zao ambao hata barua za wasomaji hawajawahi
kuandika. Kaviangalie vilabu vya wanahabari mikoani, havina hata kiti
sembuse kompyuta?
Tunakaribia uchaguzi mkuu wa
2015. Kuna makelele ya kivuvuzela, kwamba wanahabari wote wamepewa semina
na mafunzo eti waweze kutafiti na kuandika habari za uchaguzi wakati huu wa
uchaguzi.Wanajipanga ku ‘piga hela’.
Eti, wanaimba katika redio na
televisheni kwamba wanahabari wamefundishwa maadili na uandishi wa habari
za uchaguzi, wakati huu wa uchaguzi,kumbe ni huu huu ‘uchafuzi’mkuu.
Kwa mtindo huu, wanahabari
hawawezikuwezesha demokrasia na uchaguzi mkuu,bali ‘uchafuzi’mkuu.
Nataka niseme kwamba
katika baadhi ya mikoa hapa nchini, kuna vituko vinavyoitwa mafunzo
na semina za wanahabari kuhusu uchaguzi mkuu.
Wafadhili wakitaka, wakawaulize
wanahabari,ni wangapi wamehudhuria mafunzo hayo na semina hizo wanazojidai
kuombea mabilioni ya fedha, eti ili kuwezesha uchaguzi uwe wa
kidemokrasia,huru na haki, kumbe tupu na bahasha za khaki.
Fedha nyingi za wafadhili
zinazotengwa kwa mafunzo ya wanahabari kuhishia kujenga vitambi vya
wachache, wengine huishia kughushi saini za wanahabari,bila hata mafunzo
kufanyika.
Naam, kumbe wakati wa kura
ni msimu wa kula pia-kura za kula!!
Sisemi kwamba kila semina
zinapoandaliwa ni hujuma. Sijasema kwamba Baraza la Habari(MCT) huandaa
semina bandia na washirika wake kama UNDP.
Nataka kusema kwamba kuna
mmonyoko mkubwa wa kimaadili na utapeli mkubwa katika maeneo Fulani, ambako
wanahabari wamepata kutapeliwa kwamba walihudhuria mafunzo ama semina
wakalipwa fedha,kumbe uongo na Ghiliba- Ghilibu?
Tunasema kwamba,kuna watu
wamehodhi semina,mafunzo na posho ili wafaidike wao.
Nenda kawaulize wanahabari mikoni watakwambia
kwamba wana miaka mingi bila kuhudhuria hayo mafunzo na semina.
Nani huwa wanahudhuria semina
hizo, kama siyo mamluki ili wakagawane na hao wanajidai kuhodhi kila
mamlaka na mialiko ya wanahabari?
Mwisho wa siku hakuna
kiwango cha taaluma kinachoinuliwa,bali ni vitambi vya wachache
vinavyoinuliwa ama kujengwa katika msimu huu wa uchaguzi mkuu unaoandamana
na uchafuzi mkuu.
Kila siku, kila mtu anawaza
uchaguzi mkuu ufike ili wapate kula kupitia kura.
Mwanahistoria wa Kiingereza,
Thomas Babington Macaulay, ndiye aliyevibatiza vyombo vya habari,jina la
MHIMILI WA NNE WA DOLA.
Majukumu mahsusi ya vyombo hivi
vya habari na wanahabari ni kutengenezea umma uwezo wa kuchagua serikali
itakayowapa wananchi wake ulinzi na manufaa yatokanayo na katiba.
Wanahabari waliowezeshwa
mafunzo ya kitaaluma wanaweza kuuelimisha umma ili kupigakura vizuri
na kujipatia viongozi bora, na kamwe si bora viongozi.
Wanahabari waliokolea kitaaluma,
huwahudumia wananchi kwa uaminifu,bila chembe ya tama na ufisadi.
Ni mbwa walinzi(watchdogs)
wabwekao dhidi ya mienendo yenye mashaka na utusitusi.
Sasa, kama taasisi
zinazojidai kuvihudumia vyombo vya habari, masekretari wake na hata vigogo
kazi yao ni kuhodhi semina na mafunzo na kukimbizana kupora posho, maana
yake ndiyo “Watchdog role”?
Hiki ni kiwango gani cha
ubora,kualika waandishi hewa na kujipatia fedha eti kuudanganya umma kwamba
habari za uchaguzi mkuu zitawezesha demokrasia na uchaguzi huru-kumbe
‘uchafuzi’huru.
Kama tasnia ya habari
ndiyo hii ya wajanja kula migongoni mwa wanahabari nakuwatupia mifupa,
naungana na Rais wa zamani wa Marekani, Thomas Jefferson, alivyosema katika
waraka wake kwa Kanali Edward Carington, mnamo Januari 16, mwaka 1787
kwamba heri kungekuwa na serikali bila mhimili sampuli hii wa Dola.
Kama wajanja wataendelea kuomba
fedha kwa wafadhili kwamba watawezesha taaluma na vyombo vya habari,kumbe
fedha wanagawana gizani, ni heri hata uchaguzi uendeshwe kibubu-bubu,kuliko
kuwa na wanahabari waliojipaka madoa ya ulafi na ubadhirifu.
Hawa watakuwaje waadilifu wakati
hata kile walichopaswa kujengeana uwezo wa kitaaluma,wanakipora?.
Hivi hawa wanaokula
migongoni mwa wanahabari hasa wa mikoani, nao ni wanahabari gani kama siyo
wadandiaji na walaji kila msimu wa uchaguzi?
Hivi hawa wanaopeleka
jamaa zao kuhudhuria semina na mafunzo ya uandishi wa habari, wakati ni
wauza vocha, nao wana “balance freedom of press with the rights of
people” wakati wanawaza kuhujumu fedha za wafadhili za posho za mafunzo ya
kitaaluma?
Kwa mtindo huu, huu ‘uchafuzi
mkuu’ hautazaa ‘Fairness’ au ‘Objectivity’ wala ‘Accuracy’ katika habari na
makala za uchaguzi, bali uchakachuaji tu wa kusaka kujaza matumbo.
Kama hatutaangalia,nchi hii kila
kada, na kila mtu atafikiria siku za uchaguzi zifike haraka ili kujipatia
ulaji.
Tunageuza sasa msimu wa uchaguzi
kuwa msimu wa ‘kura za kula’ tu.Msema kweli mpenzi wa Mungu!!
0772 82 40 74
|