Monday, February 13, 2012

VITA VYA TATU VYA DUNIA?

Unabii wa Biblia, Katika Mathayo sura ya 24, Ufunuo wa Yohana 16 na 17 Tunafundishwa mfululizo wa unabii unaotimia haraka sana.
Vita, pepo nne za Dunia zikianza kuvuma kwa nguvu kwa kuwa sasa Mungu ameacha kudhibiti amani ya dunia. Mikataba ya amani iliyowekwa zamani kama ule wa Visiwa vya Falklands vilivyogombaniwa zamani kati ya Ungereza na Argentina, inavunjwa. Kuna matetesi ya vita.
Tangu vita vya kwanza hadi vya     Pili, matetemeko ya ardhi n.k
Ufunuo 16 HUTUAMBIA Juu ya mapigo saba ya mwisho na VITA VTA HARMAGEDDON ambavyo vi vita vya kiroho zaidi.Wakati Ufunuo 17 inahadithia mamlaka za dunia zikiwa zimebeba madhehebu fulani ya kidini yatakayowalevya wakazi wa dunia nzima kwa Injili ya uongo ili kumkufuru Mungu.
Ufunuo 17 unabeba hadithi ya mamlaka za dunia,baada ya kuzipindua nchi za Mashariki,hususan Iran kuingia mkataba na Kanisa la Kikristo, ambalo litashirikiana na Roho Tatu za Vyura kuidanganya Dunia nzima, na kuwanywesha watu kwa 'mvinyo' wa mafundisho ya Uongo kuhusu Mungu Muumbaji.
VITA YA TATU ya Dunia (The World War III) iko mbioni,kufuatia Iran kutaka kufunga Mlango Bahari wa Hormuz, ambao ni muhimu kabisa kwa mataifa mengi Duniani kupitisha shehena ya mafuta Ghafi.
Mlango bahari huu ni mwembamba, ni kama kilomita 54 tu zinazoitenga nchi kavu ya Iran na Oman.
Mafuta yatokayo katika nchi tano zinazouza kwa wingi mafuta Duniani: Saudi Arabia, Kuwait,Iran,Iraq na Umoja wa Falme za Kiarabu(UAE)hutegemea Mlango Bahari huu wa Hormuz kusafirishia mafuta yao kwenda mataifa ya Magharibi.
Mapipa milioni 17 hupita hapa Mlango Bahari wa Hormuz,kila siku, na mafuta yanayopita mahali hapa ni takriban 1/5 ya mafuta yoote ya dunia nzima.
Iran, itakapoufunga Mlango Bahari wa Hormuz,ili  hayo Mataifa ya Magharibi yasipitishe shehena yao ya mafuta mahali hapo, athari zake zitaenea dunia nzima, na siyo kwa Marekani na Washirika wake wa Ulaya tu.
Kwa mfano, Kenya hutumia kiasi cha mapipa 80,000 ya mafuta kila siku; wakati Tanzania hutumia mapipa 40,000 kila siku na Uganda hutumia mapipa 14,000 ya mafuta kutoka eneo hilo.
 Mafuta haya yote hupitia huu Mlango Bahari wa Hormuz.
Na hii ni kusema kwamba, Iran ikiufunga Mlango Bahari huu meli za mafuta zikashindwa kupita, athari za kupanda kwa bei ya mafuta zitaenea hata Kenya,Uganda, Tanzania n.k na wala hali hiyo haitazipata nchi za Magharibi tu.
Kupanda kwa mafuta maana yake ni kwamba gharama za maisha zitakuwa zimepanda maradufu kila kona ya Dunia.
Hail hii ni kuzidisha maisha magumu zaidi hasa kwa raia masikini ambao hawataweza kumudu bei za bidhaa madukani,huduma za usafiri na huduma nyingine.
Ili kuhakikisha Iran isiufunge Mlango Bahari wa Hormuz,Marekani na Washirika wake wanajiandaa kuishambulia Iran, ili isije ikarogwa kuzishambulia meli kubwa za Mafuta za Ulaya na Marekani zinazopita hapo Hormuz.
Marekani,imetangaza kuiwekea vikwazo vya kiuchumi Iran ili isiuze mafuta yake  Umoja wa Ulaya na mataifa mengine ya dunia.
 Umuhimu wa Mlango Bahari huu wa Hormuz, utaonekana zaidi hata hapa Afrika Mashariki, pale Iran itakapotangaza kuufunga, ili mafuta yasiyosafishwa kutoka Iran au hata Irak,Kuwait,Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu, yasifike huku kwetu Afrika ya Mashariki ama mahali pengine.
Tayari  vita vya maneno baina ya Marekani na Iran vimeanza, na Iran imesema ikiwekewa vikwazo vya kiuchumi kutouza mafuta yake duniani, basi nayo itaufunga mlango Bahari wa Hormuzi, ili mafuta ghafi kutoka nchi zinazosafirisha mafuta kwa wingi yasipite mahali hapo.
Jambo hilo maana yake ni kuashiria vita vya Tatu vya Dunia; yaani kuufunga Mlango Bahari huo wa Hormuz ili meli kubwa za mafuta ghafi zisipite, maana yake ni kama kuweka  ‘jisu’ lenye makali katika koo la dunia!
Tayari meli za kivita za Marekani zenye kubeba madege ya kivita kama USS Abraham Lincoln (CVN 72 huelekea eneo hilila Mlango Bahari wa Hormuz kupitia Bahari ya Arabia,ili kukabiliana na kitisho cha Iran kuufunga mlango Bahari huo.
Wakati huo, Urusi na Uchina nao wametuma nyambizi kupeleleza mienendo ya tishio la vita katika eneo hilo.
Uchina na Russia ni wanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wenye kura ya turufu.
 Juzi, walipinga Syria kushambuliwa kwa sababu  majeshi ya nchi hiyo  yanawashambulia raia wanaoandamana kutaka Rais Al Assad aondoke mamlakani.
Kufuatia hali hiyo, Marekani na washirika wake wakiamua kuishambulia Iran, na China na Urusi wakakataa na kuanza kuvishambulia vikosi vya nyambizi na madege ya kivita ya Marekani, kutatokea nini?
Waama,Iran ikiwekewa vikwazo vya uchumi ili isiuze mafuta yake Ulaya na Marekani, na ‘ikajibu mapigo’ kwa kuufunga mlango Bahari huu muhimu sana kwa uchumi wa dunia, kutatokea nini kama siyo vita vya aina yake vitakavyosasambaratisha ‘chumi’ za nchi masikini hususan hapa kwetu Afrika Mashariki?
Gazeti la The East African la Feburuari 6-12,mwaka huu, limeandika katika ukurasa wake wa nyuma kwamba, “Mlango Bahari wa Hormuz” ukifungwa, ama kukitokea vita eneo hilo, basi ni mithili ya kuweka kisu katika koo la Dunia!
 Naam, kitisho cha uhai wa dunia kimefika huko Hormuz; na maisha ya watu masikini yako hatarini,kuliko wakati wowote.
 Iran, kwa miongo mingi imekuwa haina uhusiano mzuri na mataifa ya Magharibi, hasa baada ya kufukuzwa mamlakani, Mfalme Shah, mwaka 1989, akafia uhamishoni.
 Kiongozi wa Kiroho wa Iran, Ayatollah Ruhollah Khomein ndiye aliyehika utawala wa Taifa baada ya Shah, na Khomeini alipofariki dunia, akarithiwa na Ayatollah Ali Khamenei ambaye ni mtawala  wa sasa wa kiroho.
 Iran ni Jamhuri ya Kiislam inayoongozwa na Ayatollah Khamenei ;na Rais Mahmoud Ahmedinejad ni kiongozi wa serikali. Hawa wote hawana mahusiano mazuri na nchi za Magharibi pamoja na Israeli.
Wakati Fulani Iran ilitaka taifa la Israeli lisiwepo duniani-na hii kauli ilileta mtafaruku mkubwa, kwamba Iran ilikuwa ikirutubisha madini ya Uranium ili kutengeneza silaha za Nyuklia,lengo likiwa kuishambulia Israeli.
Utawala wa mjini Washington umetangaza vikwazo vya kiuchumi kwa Iran,kama itashupaza shingo kurutubisha Uranium na kufanya majaribio ya silaha hatari za nyuklia.
 Marekani,kuna Uranium; hususan katika Majimbo ya Montana, Nebraska, Colorado, New Mexico, Texas na hata Washington kuna Uranium kwa kiwango kidogo. Lakini, Maataifa haya ya Magharibi, yanachelea Uranium kuangukia mikononi mwa  “wenye siasa kali” wanaoweza kutengeneza Platonium, kwa ajili ya kuunda bomu la Nyuklia.
Mataifa ya Magharibi, yangali yanakumbuka hawa ‘siasa kali’(Extremists) walivyolipua mfumo wa reli jijini London, Julai mwaka 2005.
Kwa kuwa kuna Uchaguzi Mkuu Marekani  katika juma la kwanza la Mwezi wa Novemba mwaka huu wa 2012, Rais Barack Obama, anachelea kuiingiza Marekani vitani tena dhidi ya Iran.
 Lakini, kama Iran itafunga Mlango Bahari wa Hormuz, lazima kutatokea vita vikali kutoka kila upande.
 Urusi na Uchina wamepiga kura ya turufu kuzuia Syria kushambuliwa kijeshi. Je, safari hii watakaa kimya Iran inaposhambuliwa, au wataingilia kati?
Bila shaka, Iran ikishambuliwa na manowari za kivita za Ulaya na Marekani, bilashaka itajibu mapigo kwa kulipa kisasi kwa Israeli. Israeli, inajua hatari inayoikabili,pale vita katika Mlango Bahari wa Hormuz, vitakapofumuka.
 Mataifa mengine yenye uanachama wa Kudumu katika Baraza la Usamala la Umoja wa Mataifa, ni Marekani yenyewe, Ufaransa,  na Uingereza, ambao tayari manowari zao ziknakwenda Hormuz bega kwa bega.
 Iran imekuwa ikiituhumu Marekani na mataifa mengine ya Magharibi kwa kusababisha fujo ndani ya Iran.
 Uchaguzi wa Juni mwaka 2009 uliorejesha madarakani Rais Mahmoud Ahmadnejad, ulileta vurugu kubwa, wakati wapinzani wa serikali, Mir Hosein Mousavi alidai kushinda urais,lakini akaibiwa kura.
 Mpinzani mwingine wa serikali ya Iran ni Mehdi Karroubi, amabaye kama Mousavi wanahisiwa ni vibaraka wa Magharibi,hivyo Ayatollah Ali Khamenei ameapa hawawezi kushinda kwa kura na kuitawala nchi hiyo, ambayo ni Jamhuri ya Kiislam.
Propaganda za Magharibi zimekuwa zikidai kuwa Iran hakuna demokrasia,na ni mahali haki za binadamu zinakokiuka kwa kiwango kikubwa, na wapinzani wa serikali wanateswa.
 Hayo na mengine ya Iran kurutubisha Uranium ili kutengeneza Nyuklia, kutaka ‘Uzayoni’ za Kiisraeli kusambaratishwa duniani na kutaka kuufunga Mlango Bahari wa Hormuz, sasa ni kama kuongeza mafuta katika miali ya moto  katika Ghuba ya Uajemi.
 Israeli inajua hatua yoyote ya kuishambulia Iran, Wairan watajibu mapigo kwa kuishambulia Israeli.
Yumkini, nchi 27 za NATO zikaunga mkono manowari za kivita za Marekani zinazojongelea Mlango Bahari huu muhimu kwa kusafirishia ‘uhai’ wa dunia nzima kutoka nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi hapa duniani,pindi ukifungwa na Iran.
Hadi sasa, nchi za Kiarabu kama Yemen, Libya, Misri,Syria, Irak,Oman,Mauritania,Jordan na Tunisia, hamkani si shwari tena.
Nchi ambazo migogoro haijaanza ni Qatar,Kuwait, UAE,Lebanon na Bahrain ambako kungali na amani.
 Mataifa ya Magharibi yanadai katika Dunia ya Kiafrika na  Kiarabu kungali hakuna demokrasia,Uhuru wa watu kuabudu, uhuru wa kutoa mawazo yao na hakuna utawala wa sheria na Haki za Binadamu, nah ii ndiyo sababu ya kupeleka vuguvugu la harakati za mfumo wa mageuzi katika nchi hizi.
Iran itakaposhambuliwa na Mataifa makubwa, hasa itakapoaufunga Mlango Bahari wa Hormuz ili meli zenye kubeba shehena ya mafuta kutoka Arabuni kwenda Ulaya na Marekani, hapo ndipo risasi ya kwanza itakayoashiria Vita vya Tatu vya Dunia itakapoanza.
Vita vya Kwanza vya Dunia, vilianza mwaka 1914 na vikaisha 1918.
Sababu hasa za vita hivi ni Mtawala wa Ujerumani, WILHELM  II,alitaka kuleta changamoto kwa maendeleo ya viwanda vya Uingereza.
 Katika Vita hivi vya Kwanza vya Dunia, walikufa jumla ya wanajeshi 8,418,000.
Askari wa Marekani waliouliwa vitani ni 126,000 na kiasi cha raia waliokufa katika vita hivyo ni 1,300,000.
Katika Vita vya Pili vya Dunia(1939-1945), walikufa askari 16,933,000; askari wa Kimarekani waliokufa ni 292,000 wakati raia waliouliwa ni 34,305,000.
 Vita hivi vilikoma wakati Marekani ilipolipua mabomu ya Atomiki katika miji ya Hiroshima na Nagasaki, Agosti 6 na 9 mwaka 1945. Agosti 14, Japan ilitia saini ya kuacha vita na Septemba 2, mwaka huo wa 1945 vita hivi vilikwisha rasmi,vikiacha makovu ambayo hata sasa yangalipo.
Huku ndiko tuendako,tunarejea katika vita, wakati mikataba ya amani inapovunjika,wakati uharibifu mkubwa wa mazingira unaposababisha karibu sana Mapigo saba ya Mwisho.
Kuharibika kwa utando wa Ozone angani,uharibifu wa vyanzo vya maji na ukataji miti ni janga lingine la hatari.

No comments:

Post a Comment