JANGA
la Ajali ya Meli, ya Mv. Skagit, huko Mwambao wa Zanzibar, ni matokeo
ya serikali, wamiliki wa meli na boti na jamii nzima ya Watanzania
kutothamini maisha yao.
Naam, ni miaka 16 kamili tangu janga la Mv. Bukoba.
Tanzania ilikuwa tayari imepitisha miaka 15 ya kuzama kwa Meli ya
Mv.Bukoba pale Mv. Spice Islanders ya Zanzibar ilipozama Bahari ya
Hindi.
Mv. Spice Islander, ilizama Septemba 10,ikifanya safari zake kati ya Unguja na Pemba na kupoteza maisha ya watu zaidi ya 200.
Watu 260 waliokolewa.
Hadithi ni zile zile za Mv
Bukoba, kwamba meli ilipakia watu wengi na mizigo kupita uwezo wake,
kwamba abiria wengine walichelea kuipanda; ndivyo ilivyotokea kwa MV
Bukoba huko Kemondo Bay.
Meli ya Mv. Bukoba,ilizama alfajiri, Mei 21, mwaka 1996 na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 800.
Ilikuwa ikitokea Bukoba, na ilizama kilomita kama 12 za majini kutoka bandari ya Mwanza, uelekeo wa Bwiru, jijini Mwanza.
Inakisiwa
kwamba, watu waliojeruhiwa katika ajali hiyo ya kihistoria ni 100;
wakati mali nyingi zilipotea na thamani yake bado kujulikana.
Mara baada ya
ajali ile, serikali iliunda Tume iliyokuwa chini ya Jaji Robert
Kissanga, ili kuchunguza chanzo cha ajali ile mbaya ya majini.
Kulingana na
Ripoti ya Tume hiyo, usiku wa kuamkia siku ya ajali(Mei 20 mwaka
1996),meli hiyo ilikuwa na abiria kati ya 750 na 800 na wafanyakazi 37.
Kati hao, 114 waliokolewa, na
maiti 391 ndiyo walioopolewa na kuzikwa katika makaburi ya Igoma,jijini
Mwanza, wakati miili mingine ilichukuliwa na ndugu zao kwenda kuzikwa.
Kila mwaka, serikali na wananchi huwasha mishumaa na kufukiza ubani katika makaburi hayo kama kumbukumbu ya ajali ile.
Pengine,
serikali huongozana na watu wa madhehebu ya dini kwenda eneo la ajali
ili kusoma dua na kumwaga mchanga majini kama ishara ya ibada ya wafu na
maziko.
Inakisiwa, jumla ya miili 332 haikupatikana.
Kwahiyo, serikali ilifanya
‘mazishi’ ziwani katika eneo la ajali,umbali wa kama maili za majini
nane tu kutoka ilipo Bandari ya Mwanza.
Mv.Bukoba,
ilijengwa na kampuni ya Meli ya Kibelgiji.Wakati wa kuzinduliwa,Julai 27
mwaka 1979 ilibainika ilitaka kumtosa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu
Nyerere.
Haikuwa na uwiano wa majini.
Ilisemwa kwamba,
serikali ilishaipiga marufuku meli hiyo isifanye huduma Ziwa Victoria ,
sababu haikuwa na 'sea worthness', vinginevyo lilikuwa kaburi lenye
kuelea, ambali siku na saa yoyote ingesababisha maada makubwa.
Hata hivyo,
kufuatia uzembe wa serikali ama kutojali, Mv. Bukoba iliendelea kukata
mawimbi ya Ziwa kutoka Mwanza hadi Bukoba, kila siku hadi
ilipozama.Iliazama miaka 15 baadaye.
Baada ya Tume
ya Jaji Robert Kissanga kuwasilisha Ripoti ya uchunguzi wake, serikali
ikafungua kesi Mahakama Kuu na kuwashitaki aliyekuwa Nahodha wa Meli,
Jumanne Rume-Mwiru, aliyekuwa Mkaguzi wa Mamlaka ya Bandari(THA),Gilbert
Mokiwa, Meneja wa Bandari ya Bukoba, Alphonce Sambo, na aliyekuwa
Meneja wa Bandari ya Kemondo, Prosper Lugumila.
Kesi hiyo nambari 22,ilifunguliwa Mahakama Kuu,Mwanza mwaka 1998, na ilianza kusikilizwa Mei 14 mwaka 2001.
Upande wa
Mashitaka ukiongozwa na mawakili wa serikali, William Magoma na Eliezer
Feleshi(sasa DPP) ulidai mahakamani hapo kwamba washitakiwa kwa pamoja
walisababisha vifo,kujeruhi na upotevu wa mali nyingi(hazikufahamika),
kwa uzembe.
Kesi hiyo
ilitajwa mara nyingi, ikaahirishwa zaidi ya mara sita hivi, baada ya
kusikilizwa kwa mwaka mzima,tangu ilipoanza kusikilzwa Mei,2001.
Ijumaa, Novemba
29, mwaka 2002, majira ya saa sita mchana, aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa
Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Juxton ,Mlay, akasoma hukumu ya kesi
hiyo.Nilikuwepo mahakani wakati hukumu ikisomwa.
Aliwaachia huru
washitakiwa wote wanne, baada ya upande wa mashitaka kushindwa
kuithibitishia mahakama(pasipo shaka yoyote) kwamba walisababisha ajali
ile na vifo vya watu kama nilivyokwisha taja.
Jaji Malay,
alisema mahakamani wakati akisoma hukumu hiyo ya kihistoria, kwamba hoja
za upande wa mashitaka kwamba washitakiwa, Jumanne Mwiru, Mokiwa,
Sambo,na Prosper Lugumila walisababisha vifo,kujeruhi na upotevu wa
mali, hazikuwa na ushahidi.
Kwamba, kwa
kuwa mashahidi waliiambia mahakama kuwa Rume-Mwiru alisikika asubuhi ile
ya ajali, akimwamuru rubani kukata kona, maana yake ni kwamba alikuwa
na nia thabiti ya kuokoa maisha ya abiria na wafanyakazi wa meli yake,
na wala siyo kutaka kuwaua kwa uzembe kama ilivyodaiwa.
Akisoma hukumu
ndefu, iliyokuwa na jumla ya kurasa 118 zilizvyoandikwa kwa mkono, Jaji
Mlay alitumia zaidi ya dakika 160 kufafanua vipengele vya kisheria na
kuvitolea maamuzi kwa ufasaha.
Mwishoni mwa
hukumu, akasema kwamba hapakuwa na ushahidi kwamba Mv Bukoba ilizama kwa
uzembe wa washitakiwa wanne: Sambo, Mwiru, Mokiwa na Lugumila peke yao !
Madai ya upande wa mashitaka kwamba Mv.Bukoba ilipakia mizigo mingi kushinda uwezo wake yakatupiliwa mbali na mahakama.
Kwa sababu,
haikufahamika kwa yakini, kwamba MV.Bukoba ilikuwa na abiria wangapi
siku ya ajali. Na ilibeba mizigo ya uzito wa kiasi gani?
Mashahidi wa
upande wa mashitaka,walikuwa wameiambia mahakama hiyo kwamba, meli
ilipakia mikungu mingi ya ndizi: Lakini, kiasi gani yenye uzito gani?
Nani aliipima uzito?
Mahakama
ilihoji bila majibu. Jaji Mlay alisema, MV.Bukoba ilizama Mei 21, mwaka
1996 kwa sababu haikuwa thabiti; na haikuwa na uwiano wa majini. Hata
Tume ya Jaji Kissanga ilisema hivyo.
Kama kawaida,upande wa mashitaka ukiongozwa Eliezer Feleshi, ukaonesha nia ya kuomba rufaa mahakama ya rufaa.
Nilikuwepo mahakamani, wakati wa kusomwa hukumu ile.
Niliwaona washitakiwa wakiganda kwa butwaa, kama waliomwagiwa barafu; hawakuamini.
Nilitaka Jumanne Rume-Mwiru aniambie, alijiskiaje? Hakujibu.
Miezi mingi
baadaye, tulipokutana katika mitaa ya jiji la Mwanza, Mwiru aliniambia
kwamba mshitakiwa mwenzake ambaye siku hiyo hakuwepo mahakamani,
alipoambiwa kuhusu hukumu ile aliugua nakulazwa hospitalini, mjini
Bukoba.
Leo, ni miaka
mingi tangu hukumu ile isomwe,rufaa haijasikilizwa, na baadhi ya
washitakiwa wamefariki dunia, bila kuona hatma ya kesi yao .
Mawakili wa upande wa utetezi walikuwa Salum Magongo na Gallati Mwantembe wa jijini Mwanza.
Mv.Bukoba ilizama kwa sababu za uzembe wa serikali na vyombo vyake.
Haikuwa na uwiano wa majini muda mrefu, hata haikuwa na zana za uokozi kama maboya ya kutosha.
Haikuwa na mawasiliano.
Niliwahi kufanya
mahojiano na aliyekuwa Nahodha, Jumanne Rume-Mwiru, na kumuuliza hatma
ya kesi ile huko mahakama ya rufaa, na kama walikuwa na nia ya kudai
mafao yao ?
“Tunamwachia Mungu” alisema Mwiru huku akicheka bila shaka kukumbuka kilichomtokea.
Aliniahakikishia kwamba mwezao mmoja alikuwa amefariki,bila kujua hatma ya kesi ile.
Rume-Mwiru, tayari ni marehemu, wakati hatma ya kesi yao haijulikani hadi leo.
Hata baada ya ajali ile, zimetokea ajali nyingi Ziwa Victoria , mitoni na baharini.
Mv.Nyamageni,iliyokuwa meli ya
binafsi, ilizama miaka ya karibuni ikiwa imebeba masanduku ya soda na
abiria kwa pamoja, na haikupatikana hata leo.
Ilikuwa safari ya kwenda kuzimu.
Naam, safari ya kuzimu!
Meli za Tanzania ni majeneza yanayosafiri kwenda kuzimu.
Uzembe! Hata ajali za magari
huletwa na uzembe tu, usalama barabarani wapo, hakuna hatua. Ziwa
Victoria ndipo kuna kazi, majahazi hayana hata boya moja,hakuna vifaa
vya kuzima moto!
miaka ya karibuni, Meli nyingine ya Shirika la Meli(Marine Services Company), Mv.Butiama, ilizimika majini, ikaelea kwa zaidi ya saa nne.
Meli hiyo ati haikuwa na mawasiliano.
Mtu mmoja alikiambia kikao cha
Kamati ya Ushauri ya Mkoa(RCC) Mkoani Mwanza,kuwa ingeweza kupigwa
mawimbi hadi Uganda , au ikaparamia mwamba?
Majibu
hayakutolewa, aliyekuwa akiulizwa alikuwa mtaalam kutoka Mamlaka ya
Bandari(TPA), kwamba asingeweza kuisemea MSC, ambao hawakualikwa katika
mkutano huo.
Abiria walihaha,
Mv.Butiama ilipozima injini zake jirani tu na Bandari ya Mwanza, lakini
hakukuwa na mawasiliano. Eti meli za MSC bado hazina maboya na
mawasiliano!
Je, zile za wajasiliamali zinazotia nanga katika bandari zinazomea kama uyoga, zina zana za uokozi?
Zina maboya mangapi na hufuata sheria kwa kiwango gani?
Bila shaka, zinafanya kazi kwa mazoea kama ilivyokuwa mwaka 47!
Naam, meli za nchi hii, hata leo hii miaka 15 baada ya kuzama kwa Mv.Bukoba ni majeneza yanayosafiri majini
.Hata MV Spice ilikuwa jeneza lililoelea majini, abiria wakapanda,wakasafiri hadi kuzimu! Mv. Skagit, yale yale!
Nawapa pole walionusurika!Nawapa pole wafiwa.
SUMATRA na vyombo vingine vya serikali wapo, wanatazama majahazi yakisafiri ama kuelea kwenda kuzimu.
Serikali huishia kufanya matambiko majini kila mwaka, kama ilivyofanya juzi.
Wengine wamekula ubani wa wafiwa, wengine hujitajirisha kwa maadhimisho haya, wapo tu.
Wanabarizi upepo.Kufaa kufaana, sijui?
Ni yale yale,ya Mv. Bukoba, Spice Highlanders, Skagit, Nyamageni na nyingine nyingi!
Hakuna
anayejali. Mmiliki wa boti moja Mwanza,juzi alinipigia simu kuniuliza,
"Wewe kinakuuma nini hata tukiwalipia nauli SUMATRA waje kukagua meli
zetu huku Ziwa Victoria? Nyie waandishi mwataka nini wenye meli tuki
accommodate SUMATRA""
Haya!!
|
Friday, July 20, 2012
AJALI ZA MAJINI ZA KUTAKA?
Tuesday, July 17, 2012
AJALI ZIWA VICTORIA?
MAMLAKA ya
Udhibiti Usafiri Nchi Kavu na Majini(SUMATRA) inadaiwa kushindwa kusimamia
ukaguzi wa vyombo vya majini Ziwa Victoria, hivyo kusababisha hofu ya kuweza
kutokea ajali.
“Maofisa wa SUMATRA wanapotoka Dar es salaam
kuja Ziwa Victoria kuendesha zoezi la ukaguzi,wanawashurutisha wamiliki wa
vyombo vya majini kuwalipia gharama za chakula na malazi hotelini”, Gazeti hili
limedokezwa.
Nahodha wa
Meli moja ya kampuni binafsi, amemwambia mwandishi wa makala haya kwamba,kitendo cha maofisa
wa SUMATRA kupewa hisani ya gharama za chakula,malazi na maburudisho wakati
wanapofanya ukaguzi wa vyombo vya usafiri majini Ziwa Victoria,huhafifisha
ubora wa vyombo husika,na changamoto kwa manahodha na mabaharia.
“SUMATRA,
wanapofika Mwanza,toka Dar es salaam, wanakula na kulala kwa gharama za
wamiliki wa meli na boti hapa Ziwa Victoria, sasa watakagua nini kama siyo
kulipa fadhila kwa yale waliyotendewa na wamiliki wa meli ama boti?” Amehoji
Nahodha wa Meli moja kwa masharti ya kutotajwa jina wakati wa mahojiano na
gazeti hili.
Tumemtafuta
Ofisa Uhusiano wa SUMATRA, David Mziray, kwa takriban juma zima,ili
kujibu tuhuma hizo, lakini simu yake ya mkononi ama iliita pasipo majibu, ama
ilikuwa imefungwa.
Hata hivyo, Ofisa Mfawidhi wa SUMATRA,Mkoani
Mwanza, Alfred Wariana, amesema maofisa wa SUMATRA kutoka Dar es Salaam,hufika
Mwanza kufanya ukaguzi wa kila mwaka,na hulipiwa gharama za usafiri,malazi na
chakula na Mamlaka, na wala siyo wamiliki wa vyombo vya usafirishaji Ziwa
Victoria.
Jumapili, Mei 27 mwaka huu,mwandishi wa
makala haya alisafiri kutoka Jijini Mwanza,kwenda Nansio,Ukerewe kwa Meli ya
Mv. Samar II inayomilikiwa na Kampuni na Kampuni ya Samar Filling Station,ya
Mwanza.
Hii ni meli
iyojengwa mwaka 2009 na Kampuni ya Songoro Marine Transport pia Jijini Mwanza,kama
meli ya mizigo. Ilikuwa ikifanya safari zake kati ya Mwanza na Uganda.
Meli hiyo ilibadilishwa matumizi mwaka huu,
ikawekewa viti na kuanza kusafirisha abiria kutoka Mwanza hadi Nansio,Ukerewe.
Uwezo wake ni kuchukua abiria 248 na tani kati ya 101 na 138 za mizigo.
Nilimuuliza Nahodha wa meli hii,Kapteni Adam
Andrew Alex, “Meli ina vifaa vya uokozi kwa kiwango gani?”
“Ina
maboya(life rings) 60 na life jackets 350.Tuna mashua moja na vifaa 10 vya
kuzimia moto”, Kapteni Alex alisema.
Kutoka Jijini
Mwanza hadi Nansio, mji mkuu wa wilaya ya Ukerewe yenye visiwa 27 na vingine 11
visivyokaliwa na watu kuna umbali wa mali 29 za majini.
Kapt.Alex
anasema alihitimu katika Chuo cha Mabaharia, Dar es salaam Maritime Insitute,
na alikuwa na uzoefu wa mwaka mmoja kazini. Akasema meli yake ilikuwa na
mabaharia tisa wenye uzoefu wa kati ya miezi sita na mwaka mmoja kazini.
Akizungumzia mazingira ya kazi, amesema
mikataba ya ajira katika vyombo hivi vya binafsi haiendani na kazi, “Hakuna
hata malipo ya muda wa ziada wa kazi(over time),wala hakuna usafiri baada ya
kazi”, Kapt. Alex amedai.
Eferi Bulongo(75) ni miongoni mwa abiria
waliosafiri na meli hiyo, Samar II kwenda Nansio. Nilimuuliza, “Una maoni gani
kuhusu usafiri Ziwa Victoria?”
“Sipendi kusafiri kwa meli binafsi;zinasumbua,
ratiba ya safari haieleweki,ni namna wanavyojisikia wao, na melini hakuna
mahitaji ya lazima ya kuaminika kama chakula na vinywaji;kuna chai”, Bulongo
amedai.
Amesema, meli za Mashirika ya Umma,kama Marine
Services Company(MSC) ni bora kabisa, ratiba ya safari huzingatiwa.
“Hizi meli
za MSC zinahujumiwa na baadhi ya wafanyakazi wake.Labda wanapewa rushwa na wamiliki
wa meli za binafsi ili meli za MSC ziache kufanya huduma ili wafanye biashara, abiria wengi hawazipendi
hizi meli binafsi”, Bulongo amesisitiza, huku akihoji, “Kwanini Meli za MSC
ndizo ziharibike kila kunapokucha? Mv.Clarias haijafanya kazi kwa zaidi ya
miezi minne; sasa wamesikia Bunge la Bajeti karibu kuanza, ndiyo tunasikia
itaanza kati ya kesho(Mei 27) na kesho”, anasema Bulongo.
Nikampigia simu Kaimu Meneja Mkuu wa
MSC,Projest Kaija kujibu tuhuma hizo.
“Leo,
Jumapili Mei 27, tunaifanyia majaribio Mv.Clarias. Baada ya siku chache itaanza
safari zake kwenda Ukerewe”, Kaija anasema.
Anakanusha kuwepo kwa tuhuma zenye lengo la
kuhujumu Kampuni ya umma kwa nia ya kuwanufaisha wenye meli binafsi.
“Wafanyakazi
wa MSC wanawezaje kuhujumu kampuni inayowapa mshahara?” Anahoji,huku
akisisitiza kuwa tuhuma hizo zitachunguzwa,kwa kuwa uongozi wa kampuni hiyo ya
umma umebadilishwa siku chache zilizopita; kampuni inafanya matengenezo(reform)
anuwai.
Nikampigia simu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Everest
Ndikilo,ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa, kumsaili:
“Kwanini
abiria wanapopanda katika vyombo vya majini Ziwa Victoria hawakaguliwi, ili
kubaini uwezekano wa kuwepo kwa magaidi kama Al-Qaeda na Al-Shabaab, wanaotishia maisha ya
watu nchi jirani ya Kenya?”
Magaidi
waliwahi kuteka nyara ndege ya Air Tanzania(ATC)mwaka 1988 , yenye maandishi
ubavuni, ‘Tango Charlie” wakati ikipaa kutoka uwanja wa ndege wa
Mwanza,ikalazimishwa kwenda Jijini London ambako hatimaye jumla ya wateka nyara
watano raia wa Tanzania walihukumiwa kifungo cha kati ya miaka mitatu na mitano
jela,Jijini London.
“Ulinzi na Usalama ni Ajenda ya kudumu na siyo majini tu, hata kwenye
majengo,mahoteli na makazi ya raia”, Mkuu wa Mkoa Ndikilo anasema.
Kuhusu
maofisa wa SUMATRA,kutoka Dar es Salaam kulazimisha kulipiwa gharama za ukaguzi
na wamiliki wa vyombo ziwa Victoria, Ndikilo akasema, “Kama jambo hilo
lipo,basi ni tatizo kubwa,nitafuatilia ili hili likemewe”, Ndikilo akasema.
Gazeti moja litolewalo kila siku hapa nchini
kwa lugha ya Kiingereza, katika toleo lake la Mei 23 mwaka huu lilisema
kwamba,mwaka 1996 Mv.Bukoba ilipozama na kupoteza maisha ya abiria wake
takriban 1,000; miongoni mwao alikuwemo Abu Ubaidah al-Banshiri, ambeye alikuwa
nambari mbili wa kundi la kigaidi la Al-Qaeda.
Naam, kundi
hili la AlQaeda, lilianzishwa na Osama bin Muhammad bin Awad bin
Laden,Feburuari mwaka 1998 kwa jina la WORLD ISLAMIC FRONT,ili kuhujumu maslahi
ya Marekani na washirika wake mahali popote duniani,hata kama ni Ziwa Victoria,
Osama
alikuwa mshirika wa Marekani na shirika lao la Ujasusi(CIA) mwaka 1979 wakati
majeshi ya Warusi walipovamia Afghanistan.CIA walimfadhili mabilioni ya Dola za
Marekani kuanzisha kambi ya mafunzo ya Makhtab al-Khidamat(MAK).
Lakini,baada
ya Urusi kuondoka Kabul mwaka 1989, Osama akageuka kuwa adui wa MAREKANI na
washirika wao, akaungana na Taliban na Mullah Muhammad Omar kuendesha ‘Jihad’
dhidi ya Marekani na washirika.
Nataka
kusema kwamba,mwaka 1996 wakati Mv.Bukoba inazama ziwa Victoria, al-Qaeda
tayari walikuwepo,na wangeweza kufanya madhara hapa nchini kwa mashambulizi
yenye kulenga shabaha Wamarekani ama maslahi yao hapa Tanzania.
Hata hivyo,
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Everest Ndikilo, amesema serikali imeimarisha ulinzi
katika Ziwa Victoria,kwa kuwa zipo boti za doria zinazozunguka ziwani, na raia
wanapaswa kutoa taarifa pindi wanapoona mienendo yenye mashaka ama kitisho cha
magaidi wa al-Qaeda ama al-Shabaab!
0786 324 074
anza
al shabaab Mwanz?
Mwangwi wa A-Shabaab Nairobi, unatikisa usafiri Ziwa Victoria?
*Mabadiliko
ya Tabianchi yatishia meli kuparamia miamba na kuzama
Na Conges Mramba, Mwanza
MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari(TPA),
imewapandisha kizimbani wamiliki wa meli binafsi, kwani wanazuia Mamlaka hiyo
kusimamia usalama wa abiria na mizigo, hata wakati huu wa kitisho cha magaidi
wa Al-Shabaab,Afrika Mashariki.
Mkuu wa Bandari(Port Master)Mwanza, John
Mutalemwa, katika mahojiano maalum na mwandishi wa makala haya juzi, alisema wamiliki hao wa
Bandari binafsi wanashindana na Sheria Na. 17(Tanzania Port Act) ya mwaka 2004.
Sheria hiyo
inaipa TPA nguvu ya kusimamia bandari
zote, zikiwemo za watu binafsi,ili kukagua usalama wa abiria na mizigo,kabla na
baada ya safari.
“Sheria inatupa Mamlaka ya kusimamia bandari
zote zikiwemo bubu, tukague na kujua
mizigo kiasi gani inasafirishwa; tunatakiwa kutazama abiria ikiwa wanalingana
na uwezo wa meli au boti,kulinganisha na uwezo wa chombo chenyewe, halafu tunatoa, “Port Clearance”
kabla ya meli kuanza safari”, Mutalemwa alisema.
Kwa mujibu
wa Mutalemwa, vipo vyombo vya usafiri majini,huchukua abiria na mizigo kuoita
uwezo. Hii ni kazi ya TPA kufanya ukaguzi makini,ili kuondokana na Ajali Ziwa
Victoria.
“Bandari ni mpaka wa nchi. Lazima tusimamie
hali ya usalama, meli inaweza kuleta Al-Qaeda ama Al-Shabaab, nap engine inaweza
kuingiza nchini silaha kutoka nchi za vita na migogoro. Eti wanakataa
tusiwasimamie…tumewafungulia kesi mahakamani”,Mutalemwa ameliambia gazeti hili
katika mahojiano Maalum ofisini kwake juzi.
Meli za mizigo za Jijini Mwanza, hufanya
safari zake hadi Port Bell, Uganda,na Kisumu nchini Kenya, ambako sasa magaidi
wa Al-Shabaab wanasaidia kuzimu kupanua kinywa chake.
Aidha, Mkuu huyo wa Bandari Mwanza amesema
nchi za Maziwa Makuu kama Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, na Burundi hazina
amani, na Kenya hamkani si shwari,kufuatia kitisho cha Al-Shabaab, wanaopinga
majeshi ya nchi hiyo kuingia Somalia kuwafulusha magaidi hao.
Kufuatia
hali tete ya usalama nchi jirani, Mutalemwa amesema lazima Mamlaka yake kuwa
macho na usalama wa abiria na mali zao dhidi ya hujuma za magaidi, wanaoweza
kupata upenyo wakaingiza silaha nchini kupitia Ziwa Victoria.
Mamlaka ya Bandari humiliki bandari za Mwanza
Kaskazini na Kusini,Nansio Ukerewe,Kemondo Bay na Musoma.
Vituo
vingine vidogo vinavyomilikiwa na TPA ni Maisome,Nkome,Bukondo,Kahunda,Miharaba,Kome,Buchosa,Solima,Karumo,Chato
na Nyamirembe(Kagera) na Kinesi mkoani Mara.
Bandari ya Mwanza ni kiungo muhimu kwa nchi za
Maziwa Makuu,hususan Uganda na Kenya,na
huchangia kwa kiwango kikubwa kukua kwa shughuli za uchumi,hata katika nchi
wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki(EAC).
Ripoti ya Malka hii iliyotolewa kwa Kamati ya
Bunge ya Miundombinu(nakala tunayo), inasema bandari ya Mwanza ingeweza
kusafirisha abiria milioni moja kwa mwaka.
Ingeweza kusafirisha tani mamilioni za moja za mizigo,kama Reli ya Kati ingekuwa
inafanya kazi kwa ufanisi. Hili ni eneo muhimu kwa ukuaji wa uchumi wan chi,lakini
kinyume chake ni hasara kila upande.
“Huduma hafifu za Reli zimesababisha shehena
ya kahawa kutoka Uganda na hata Bukoba,kubadili njia(route) na kupitia Bandari
ya Mombasa,Kenya “, Ripoti hii inasema.
Kufuatia huduma duni za Shirika la Reli,
Bandari za Mwanza ziko taaban,kwa sababu ya kupungukiwa mapato, zinaendeshwa
bila faida.
Kulingana na Ripoti hii kwa Kamati ya Bunge ya
Miundombinu,katika kipindi cha miaka mitano,kuanzia 2006/2007 hadi 2010/2011,
mizigo imepungua katika Bandari za Mwanza kutoka tani 480,568 hadi 248,860
mwaka 2011.
Utendaji
mbovu wa lililokuwa Shirika la Reli(TRL) ulisababisha treni iliyokuwa
ikisafirisha abiria na mizigo kati ya Mwanza na Bandari ya Dar es salaam
kusimamishwa.Hali hii husababishwa abiria na mizigo kubadili njia na kukosesha
mapato bandari za Mwanza.
Wafanyabiashara wa Uganda wanasafirisha bidhaa
zao kupitia bandari ya Mombasa,nchini Kenya.Shehena ya kahawa kutoka Uganda
iliyokuwa ikipitia bandari za Mwanza, inapitia Mombasa na hivyo kupunguza
kiwango cha mizigo kutoka tani 250,000 mwaka 2007 hadi tani 100,000 mwaka
2009/2010.
Kufuatia madudu ya TRL, hata abiria wamepungua
katika bandari za Mwanza kutoka abiria 891,634 mwaka 2007 hadi abiria
593,342.Huu ni upungufu wa asilimia 6.3 unaoikosesha nchi mapato na fursa za
ajira kwa watu wake.
Ripoti hiyo ya TPA, imebaini kwamba, wasafiri
wa vyombo vya majini Ziwa Victoria wamepungua kufuatia ushindani uliopo wa
barabara,hususan baada ya mtandao wa barabara kukamika ujenzi kwa kiwango cha
lami.
Kati ya Mwanza na Bukoba kuna usafiri wa ndege
ambao huchangia pia abiria wasisafiri kwa meli.
Kufuatia
hali hiyo,ripoti hiyo imebaini kuwa Kampuni ya Huduma za Meli,Marine Services
Company(MSC) iko hatarini kufilisika,kufuatia meli zake kuharibika mara kwa
mara,kitu kinachodaiwa na baadhi ya abiria kuwa ni hujuma za baadhi ya
wafanyakazo wa MSC ili kuwanufaisha wenye meli binafsi.
Kaimu Meneja Mkuu wa MSC, Projest Kaija,
ameliambia Mwanahalisi kwamba madai
hayo hayana ukweli, kwa kuwa kuhujumu kampuni unayofanyia kazi maana yake ni
kuhujumu mshahara na mapato yako.
“Je,
unahujumu Kampuni namna hiyo ili kampuni ikifa wewe utoe wapi mshahara?’ Kaija
alihoji.
Siku za karibuni MSC imewaondoa viongozi wa
Kampuni hiyo na kuwaweka wapya ili kuboresha ufanisi na kupunguza nakisi.
Kwa kipindi cha miaka mitano, idadi ya meli
zilizohudumiwa na Bandari za Mwanza, imepungua kutoka 2,684 hadi meli 1,900
mwaka jana.
Bandari ya
Mwanza pia huendeshwa kwa hasara ya mamilioni ya shilingi kila mwaka,nakisi ni
takriban shilingi bilioni 4.5
Mabadiliko
ya Tabianchi na Ongezeko la Joto Duniani,pia hutishia USALAMA wa usafiri Ziwani
Victoria.
Kwa kipindi
cha kati ya mwaka 1998 hadi 2006,maji ya Ziwa Victoria yamepungua kutoka mita
1,141.24 juu ya usawa wa bahari hadi mita 1,139.20. Upungufu ni wastani wa mita
2.04.
Kulingana na
Ripoti hiyo, meli nyingi zimekuwa zikishindwa kufungwa katika bandari za Mwanza
na Nansio,Ukerewe. Kupungua kwa kina cha maji ya Ziwa hili pia huweza
kusababisha kuzuka kwa miamba ambayo huhatarisha usalama wa meli na boti na
usalama wa abiria,hasa wanaposafiri nyakati za usiku.
Meli
zinapoparamia miamba hutoboka na kujaa maji,ama kuwa katika hatari ya kuzama.
Ziwa Victoria ni chanzo cha Mto Nile, ambao
huanzia katika Maporomoko ya Owen,Uganda; maji husafiri umbali wa zaidi ya
kilomita 6,900 hadi Misri. Mvua za masika zinaponyesha Afrika ya Mashariki
hubeba rutuba mezi ya Aprili na Mei na rutuba hiyo hufika Misri kati ya Agosti
na Septemba na kuwawezesha Wamisri kupata rutuba jangwani.
Mto Nile ni mungu wa Wamisri. Miungu ya Misri
ina ‘mama’ yao Ziwa Victoria. Ni kwa sababu hii, mwaka 1929 na 1957 Misri
walitiliana saini mkataba na Wakiloni wa Kiingereza kuzuia matumizi ya maji ya
Ziwa Victoria kwa shughuli za kilimo na hata vyanzo vya umeme kama kilichopo
Jinja.
Aidha,kupungua kwa kina cha maji ya Ziwa hili
hufanya meli kutia nanga katika maji ya kina kirefu,na huku ni kuhatarisha
maisha ya abiria,hasa katika maeneo ya visiwa.
Mkuu wa Bandari ya Mwanza, John Mutalemwa
anasema Mamlaka yake imelazimika kuchimba mchanga katika bandari za Mwanza ili
kuongeza kina cha futi tatu ili kuwezesha meli kufunga gatini.
Mradi kama huu unafanyiwa upembuzi yakinifu
katika bandari ya Nansio,Ukerewe,lengo likiwa kujenga gati imara na salama.
Mpango wa
serikali wa kuunganisha Reli kutoka Tanga hadi Musoma kupitia Arusha, utaweza
kurejesha wingi wa abiria na mizigo katika Bandari za Mwanza, au abiria na
mizigo ya Uganda,Rwanda,Burundi na Congo wanaweza kutozifikia kabisa bandari za
Mwanza,na hivyo kuleta kifo cha mende kwa TPA na Meli za MSC.
Ziwa Victoria
ni fursa muhimu kwa Tanzania katika Soko la Pamoja la EAC,lakini fursa hii
inaachwa kwa wageni kupitia hujuma na ufisadi unaofanywa na maofisa wa
mashirika ya umma kama TRL na MSC.
www.congesmrambatoday.blogspot.com
0786 324 074
vita, tangu Jerusalem ya kale hadi Jerusalem Mpya
TUIJADILI
ISRAEL, nchi ambayo ina jumla ya watu 757 katika maili moja tu ya mraba.
Jirani za
taifa hili babe sana Mashariki ya Kati
na mshirika wa Mataifa ya Magharibi ni Lebanon, Syria ambako vita vya kumwondoa
Al Assad vinapamba moto,Ukanda wa Magharibi wa Mto Jordan, Jordan yenyewe, Gaza
Strip, na kuna Nchi ya Misri, ambako wanajeshi wamekataa kuheshimu mamlaka
ya Rais mpya, Mohammed Mursi.
Israeli, ina
ukubwa wa maili za eneo 7,800. Mwaka 1997 mji mkuu wa zamani wa Israeli,
Jerusalem(Yeroo-Shalayim) yaani mji wa
Amani, ulikuwa na wakazi 591,400 sawa lilivyokuwa Jiji la Mwanza,wakati huo.
Tel Aviv,
una wakazi 2,181,000. Kuna vikosi vya wanajeshi 172,500. Nchi hii hutumia fedha
inayoitwa Shekeli, ambayo miaka michache tu iliyopita, Shekeli Tano zilikuwa na
thamani sawa na Dola moja ya Marekani.
Mji huu wa kihistoria ulijengwa mwanzoni zama
za Mfalme Daudi(1004-965 BC), umewahi kutekwa na kutawaliwa na Babeli,
Wamedi,Waperizi,Wagiriki,Rumi ambao waliubomoa mji kabisa mwaka 70 AD.
Awali, jiji
hilo lilitekwa na Mfalme Nebuchadnezzar mwanzoni kabisa mwaka 605 BC huu ni
wakati Nabii Danieli alipotekwa pia na kuchukuliwa hadi Babeli.Danieli aliishi
huko uhamishoni hadi mwaka wa BC 530 akafariki dunia.
Nebchadnezzar
aliuzingira mji huu na kuutekwa kwa mara ya pili mwaka 598 BC huu ulikuwa
wakati wa Nabii Ezekieli, ambaye naye alihamishwa hadi Babeli ambayo sasa iko
Irak.
Ezekieli,
aliishi Babeli mwaka 593 hadi 570 BC. Mara ya tatu Mfalme huyu aliutekwa
Jerusalem mwaka wa BC 586 MJI UKABOMOLEWA kabisa, hadi hapo ulipojengwa wakati
wa akina Nehemia.
Waarabu
walikuja kuliteka eneo hilo mwaka wa AD
636; na tangu karne ya 11 Waarabu wamelimiliki eneo hili la Israeli. Hawa ni
pamoja na Seljuk, Mamluks na Dola ile ya Ottomans ya Uturuki.
Uingereza ililichukua eneo hili mwaka 1917,
hii ni kudhihirisha kwamba watu wa Israeli wamepata misukosuko ya kutawaliwa na
mataifa ya kigeni, na vita vimewaua wengi hadi wakakimbilia uhamishoni katika
mataifa mengi sana duniani.
Umepata
kuona Filamu iitwayo, ESCAPE FROM SOBIBO?Ukitazama filamu hiyo utaona kwamba
Waisraeli hawa wamenja shubiri wakati wa Adolf Hitler, ambaye alikusudia
kuwafyeka kabisa katika uso wa dunia.
Awali, baada
ya kuchukuliwa mateka mwaka wa BC 586-537 BC Jerusalem ulijengwa upya zama za
Ezra, Nehemia hadi kufika BC 404 Mji huu ulishakamilika.
Kwanini
Waisraeli wameshambuliwa mara nyingi na wakazoea sana vita? Biblia inatupa jibu
kwamba, walimwasi Mungu.
Watu wengi
sana hudhani Israeli bado ni Taifa pendwa la watu wa Mungu! Huku ni kuibaka
historia kwa kiwango cha kutisha.
Tutazame
kwamba, watu hawa(Waisraeli) walimkataa Masihi, wakamchongea hadi akauawa.
Yesu, alitabiri maangamizi ya taifa hili, hadi kuwa kwao wakimbizi katika nchi
nyingi,kama tutakavyooona.
Wamekuja
kurejeshewa taifa lao Mei 14, mwaka 1948
na Umoja wa Mataifa. Hata hivyo,Waarabu wanapinga vikali jambo hili, kwa kuwa
huku kulikuwa kuchukua ardhi ya Waarabu waliyoikalia kwa karne nyingi wakati
Waisraeli walipokuwa uhamishoni, mataifa mbalimbali.
Warejea ,na Umoja wa Mataifa ukawapa eneo hilo
ili wakae na Waarabu, wameshambuliwa mara nyingi na Misri, Saudi
Arabia,Syria,Lebanon na Irak. Imefanywa mikataba ya amani,bila mafanikio vita
vinapamba moto hata leo hii.
Nimejadili
Mkataba wa Amani wa Camp David,
wakati ule wa Rais Jimmy Carter,nimejadili mkataba baina yake na Misri,Misri
ndiyo nchi yenye ushawishi mkubwa Mashariki ya Kati, nayo sasa Hamkani si
Shwari tena.
Unabii
unatimia,kwamba nchi za Ulaya na Marekani zinapata nguvu nyingi na zitatawala
nchi za Kiarabu.
Vita kati ya
Israeli na nchi za Kiarabu vimeanza zamani sana,mikataba ya kulinda amani
ilishawekwa mingi sana ikaja kuvunjika. Israeli imeshambuliwa hata wakati wa
Siku kuu kama Yom Kippur.
Tumeona
katika makala zilizotangulia kwamba Julai 3,mwaka 1976 ndipo waliposhambulia
Enttebe,na kuchukua mateka wao.Nimesimulia sana kisa hiki, wengine wananiuliza
Entebbe ni mdudu gani?! Poleni sana!
Mwaka 1977
Israeli na Misri walitiliana saini Mkataba wa kuacha vita baina yao kwa miaka
30.
Hata hivyo, kungali na vita na jiradi zao;
kuna “Intifada” naam ni Intifada hadi kiama. Sasa kukosekana kwa siasa tulivi
Misri hivi sasa,kunatishia sana amani ya Israeli na Mashariki ya Kati.
Tumemwona
Hillary Rodham Clinton akifika Cairo chini ya ulinzi mkali sana kwenda kupoza
joto ili vita visizuke, baada ya jaribio la kumpindua Hosni Mubarak(87) na
kumtia korokoroni,kuonekana siyo suluhu,baada ya maandamano ya Taharir Square.
Jerusalem kuna msikiti mkubwa unaoitwa,
Al-Aqsa,vita huingia hadi misikitini na katika masinagogi watu hupigwa mabomu
na kuuawa.
Israeli,
inagombana sana na Chama cha Ukombozi cha Palestina, PLO.Marekani wamejitia
kupatanisha mara nyingi sana, bado vita vinapamba moto kila siku, misikitini na
mahekaluni watu huuliwa kwa mabomu ya kujitoa mhanga,risasi n.k
Naam, ni
vita baina ya Wayahudi na Waislam mjini Jerusalem,kila siku akina Waziri Mkuu,
Benyamin Netanyahu na Hayati YasIr Arafat walishakaa vikao, hakuna amani.Hillary
Clinton amefika pia Yerusalem lakini hakuna amani na utangamano,ni mtutu wa
bunduki tu.
Sasa inasadikiwa, Kiongozi wa Wapalestina,
Yassir Arafat aliuliwa kwa sumu mjini Paris, wanataka maiti yake ifukuliwe na
kufanyiwa uchunguzi upya ili kubaini chanzo cha kifo chake-ni vita kila siku.
Mara vita
Ukanda wa Magharibi mwa Mto Jordan, Dead Sea ama Gaza Strip huko Peninsula ya
Sinai hadi Bahari ya Mediterranean.
Yesu,
alitabiri maafa ya Jerusalem ama Yerusalem.Wayahudi walimwasi Mungu karne
nyingi wakaungana na mataifa mengine kuabudu miungu na sanamu. Unajua Mungu ni
mwenye wivu!
Ibilisi
ndiye hasa kiongozi wa hawa taifa la Israeli,kama alivyotabiri Carlos The
Jackal, Hugo Chaves, Robert Gabriel Mugabe, na hata Fidel Alejandro Castro Ruz
aliwahi kumwita Rais Mstaafu,Bush kwamba ni Shetani!
Kwa nini? Tazama Luka 21:2-24 na usome pia
vitabu vya Isaya,Yeremia na Hosea. Kwa kifupi,unaweza kusoma vitabu hivi
Prophets and Kings na Christ’s Object Lessons, katika sura iitwayo, The
Vineyard of the Lord, uone Mungu alivyowazira Wayahudi,kwa tabia zao.
Yesu
alitabiri Wayahudi kuukimbia mji wao wa Yerusalem, walikimbia uhamishoni
wakaangamizwa huko. Tazama Filamu ya ESCAPE FROM SOBIBO uone mateso waliyopata
huko, na utaona laana waliyovuna baada ya ukaidi wao; Isaya 27:6
Katika
Mathayo 24:15-20 Yesu aliwaonya kutambua kwamba mwaka 70 AD Majeshi ya Warumi
yangeubomoa mji, waliambiwa kukimbia wakati huo wakaleta kiburi-waliuliwa wengi
hekaluni hadi damu ikavuja kama mto.
Nabii
Danieli alishatabiri maafa juu ya Yerusalem,karne sita kabla ya Yesu. Tazama
Danieli 9:27 walishupaza shingo zao ngumu wakajidai Mungu angejipendekeza kwao
hata wanaposhirikiana na Ibilisi kufanya ukaidi(Yeremia 7:4).
Wayahudi
hawa walishakataliwa na Mungu kama taifa lake teule, waliwaua
mitume,walimchongea Yesu, waliua wafuasi wengi wa Yesu, Tazama Matendo ya
Mitume 6:8-15 na Matendo 7:51-60.
Ni wakati huu wafuasi waaminifu wa Yesu
waliuliwa,wakafukuzwa Yerusalem. Sura ya nane ya kitabu cha Matendo ya Mitume
hueleza Wakristo walivoteswa, wakatimkia Ulaya.Wayahudi walimkataa Yesu(Masihi)
wakamchagua Jambazi moja aitwaye Baraba(Luka 23:18, Mathayo 27:22).
Kuongozwa na
Yesu, walisema afadhali huyo jambazi Baraba kuliko Yesu, na heri wangeendelea
kuwa chini ya utawala wa Kaisari wa Rumi kuliko Yesu.
Nataka
kusema, Israeli siyo taifa teule la Mungu,na nimetumia Biblia kuonesha ushahidi
wa jambo hili.
Tangu mwaka
34 AD walipomuua Stefano na wakawatesa Wakristo(wafuasi wa YESU) Basi
wakatawaka Shetani(akina Kaisari Nero)wawatawale(Mathayo 27:24-25) wakajiweka
chini ya utawala wa Shetani kama akina Carlos wanavyosema.
Mungu alishautupa mji huu kitovu cha vita,na
Shetani na mawakala wake Freemasonry wanautawala.
Hata hivyo
Shetani hawezi kutawala dunia kutokea Jerusalem, atatawala kutokea Babeli ya
Kiroho, ambayo ni Jijini Rome,baada ya Washington kukabidhi madaraka yake
baadaye siku za usoni.
Jerusalem ya sasa itaangamizwa kama
Babeli,maana hekalu lao na dhabihu zao ni ibada ya sanamu na mizimu,isiyo na
maana tena.
Katika
kitabu cha Ufunuo wa Yohana 21:1-8 Nabii Yohana alioneshwa Jerusalem Mpya wenye
Amani.Yerusalem wa kale ulishanajisiwa na majeshi na watawala waovu wa dunia.
Katika Ufunuo 20:7-10 tunaelezwa Jaribio la Shetani
na Majemadari wa vita wa kale wakijaribu kuuteka Mji huo wa Jerusalem Mpya.Wamo
akina Hitler, Napoleon Bonaparte n.k
Mji huo wa
Yerusalem Mpya,huitwa Kambi ya watakatifu Ufunuo 20:9 na Biblia inasema hao
majemadari watashindwa,watauliwa kwa nguvu za Mungu.
Tuijadili
kidogo, “City Profile” ya Jiji hili
jipya la Jerusalem lililofichwa mahali kusipojulikana. Tusome Ufunuo wa Yohana
21:10 hadi 27. Biblia inasema ni mji halisi, na wala siyo kisasiri ama hadithi
za kufikirika(Myth).
Ufunuo 21:16
hutwambia kwamba jiji hili ni mraba,kila upande una urefu wa maili 344.6 hivi.
Mji huu unalingana ukubwa na Jimbo la Oregon,huko Marekani,ni kama Colorado
hivi.
Katika
Afrika Mashariki,ni kama Rwanda na Burundi kwa pamoja. Una ukubwa wa Poland
huko Ulaya.
Kimo cha
magorofa ya mji ni sawa na urefu wa mji na upana! Hapa ndipo makao ya
watakatifu wa Mungu(Yohana 14:2).Kila mkazi wa dunia ana nafasi yake katika
majumba yale marefu. Wakazi Bilioni saba,kila mtu anayo sehemu yake katika jiji
hilo, isipokuwa mtu akatae mwenyewe,kwa kuhalifu SHERIA ZA MUNGU,Amri 10.
Watu wengine
watajenga humo nyumba zao na kuishi(Isaya 65:21-22) wengine watalima mashamba
yatakayostawi vizuri.
Yerusalem Mpya utakuwa na eneo la kilomita za
mraba takriban 189,998.7 hivi ni kama Rwanda na Burundi kwa pamoja,kama Cote d’
Ivoire. Mji huu ukubwa wake unazidi Ugiriki, Guinea Bissau, Israeli yote,Italia
n.k
Tanzania ina
ukubwa wa kilomita za mraba 945,000. Msomaji anaweza kubaini kwamba eneo la
Yerusalem Mpya ni kama 1/5 ya Tanzania nzima.
Tujadili
kidogo magorofa ya Jerusalem Mpya. Magorofa marefu(SKYCRAPERS) ambayo hakuna
hata moja hapa duniani kwa sasa.
Jengo refu
kuliko yote hapa Afrika, ni ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika,mjini Addis
Ababa, Ethiopia.
Jengo hilo limejengwa kwa hisani na Wachina,na
wamelikabidhi tayari kwa Umoja wa Afrika AU, ambao sasa Mkuu wa Kamisheni yake
ni mtaraka wa Jacob Zuma, Bibi Dlamini Zuma. Jengo hilo limejengwa kwa Dola za
Marekani milioni 200.
Jengo hilo
nalo haliwezi kulingana urefu na magorofa ya Jerusalem utakaoshushwa na Mungu
duniani,baada ya Jerusalem wa kale kubomolewa kwa vita kali sana.
Tumeona
kwamba magorofa ya jiji hilo yatakuwa na kimo cha maili 344.6 kwenda angani.
Kwa mahesabu ya haraka ni kama kilomita 189,998.7 kwenda juu angani.
Kulingana na
tovuti za www.worldstallest.com na www.skycraper.com hata jengo pacha la WTC wanalosema
lilibomolewa na Osama Septemba 11,mwaka 2001,lilikuwa na kimo cha futi 1,368
tu.
Majengo yote
marefu duniani sasa,hakuna lenye urefu wa zaidi ya futi 2000. Kulingana na
tovuti hizo,majengo 10 marefu duniani ni pamoja na jengo la Indosat Telcom huko Jakarta,Indonesia lenye kimo cha
futi 1,831. Lilijengwa mwaka 2001.
CN tower la
Toronto huko Canada, lina urefu wa futi 1,815 na lilijengwa mwaka 1974.
Jerusalem Mpya una majengo yenye urefu wa futi mabilioni.
Majengo
mengine marefu yako Moscow,Urusi, Shanghai,China, Iran,Kuala Lumpur huko
Malaya,Beijing, Uzbekistan na Kazakhstan haya yalijengwa mashine.
Huko Giza,Misri yale Mapiramidi anayosema
Gideon M.yalijengwa na mikono ya wanadamu,bila mashine wala mitambo. Yalijengwa
zamani na yamedumu kwa jumla ya karne 43 sasa, Piramid moja lina urefu wa futi
481.
Kwa kifupi,
hakuna jengo hapa duniani litakalolingana na magorofa ya Yerusalem
Mpya,yamejengwa na Mungu mwenyewe.
Ukitaka kujua sura ya Mji huo soma mwenyewe
Ufunuo wa Yohana sura nzima ya 21.Biblia inasema hakutakuwa na majambazi, wezi,wachawi,magaidi,majambazi,machangudoa
na wasagaji. Hakuna bia wala gongo!

Hii ndiyo sababu watu hawapendi kwenda huko
maana hakuna sigara, wala madada poa! Hakuna kiti moto huko. Hakuna majuto
Tazama Ufunuo 21:4,8 Mji umejengwa kwa madini safi,barabara ni dhahabu angavu
kama kioo(Ufunuo 21:18-21)
Hakuna
TANESCO huko, maana ni mchana siku zote(Ufunuo 21:23, 22:5) Hakuna
udhaifu,hakuna mbumbumbu na watu dhaifu,hakuna hospitali maana watu hawaugui.
Masharti ya
kuingia jiji hili ni kuepuka sifa hizi: Ushoga, uchawi,ibada ya
sanamu,utapeli,uongo,ufisadi na uchafu wa tabia(Ufunuo 22:15) Hakuna rushwa na
chuki kwa watu na kulipa visasi. Hakuna kuteka nyara na “Kuulimboka” ama
‘kukolimba’ watu huko!!
Hakuna
utapeli na uongo,rushwa,kila mtu anatiwa moyo kuchukua uraia wa jiji hilo.Neema
ya Yesu iwe nanyi wote,Amina,Ufunuo 22:21.
TAMATI
0786 324 074
Thursday, July 12, 2012
vita hadi Jerusalem Mpya-4
Katika
Biblia, Ufunuo wa Yohana 17:13 husema kwamba, Wafalme wa Dunia sasa hufanya
majadiliano, ili kumrithisha mamlaka yao Mfalme mmoja tu Duniani.
Ufalme ujao
Duniani, huoneshwa kwa mifano ya “Mwanamke” aliyebebwa na Mnyama, ambaye katika
makala zilizotangulia,tukaona mwanamke huyu aitwaye, Goddess Roma, akiwa nje za
ofisi za Bunge la Umoja wa Ulaya,huko mjini Brussels.
Makao Makuu
ya serikali hii mpya, Gideon M. anasema yatakuwa Jerusalem, lakini mimi nasema
yatakuwa mahali kilipokuwa kiti cha enzi cha utawala wa Rumi ya kale.
Hata
hivyo,tujadili namna Umoja wa Kujihami wa Ulaya Magharibi(NATO) walivyoanza
kuuvuka Mto Frati na Tigris ili wajielekeze Mashariki,ilikokuwa iliyokuwa Dola
ya Kisovieti,USSR.
Naam,
tujadili namna “Mto Frati” ulivyoanza kukauka,ili kutengeneza njia kwa madola
ya Magharibi kuzitwaa milki za Mashariki, ili kuzilazimisha kujiunga nao aidha
NATO, ama Umoja wa Ulaya(EU),na Soko lao la Pamoja, European Common Market.
Mhariri wa
Jarida la Executive Intelligence Review la Marekani, Edward Spannus, amesema
vita vinavyochochewa sasa na Marekani na Uingereza huko Syria,hatimaye vitakuwa
VITA VYA TATU VYA DUNIA!
Uingereza,Marekani na washirika wao wanawaunga
mkono waasi wa Syria,na Urusi na China wanamuunga mkono kiongozi wa nchi hiyo,
Bashir al-Assad.Sasa, inasemwa,mwisho wa siku Marekani na washirika wake
wataingia vitani dhidi ya Urusi na Uchina,na hivi ni vita vya tatu vya Dunia?
Biblia,
katika Ufunuo 16 inasema vita vya TATU VYA DUNIA ni Har Mageddon, ambamo Mungu
atapingwa kwa nguvu za mashetani na mawakala wao,Freemasons,na malaika toka
mbinguni watakuja kusimamia mabambano ili kulinda HAKI NA UKWELI Duniani.
VITA BARIDI vilikwisha mwaka 1991 Desemba,
baada ya Russia,Kazakhstan na Belarus kuwa mataifa huru. Baadhi ya nchi kama
Georgia na nyingine tayari zimekuwa washirika wa NATO.
Tunaona
JAPAN na mataifa mengine ya Mashariki wakiungana na M arekani na washirika wao.
Kile kimbembe kilichowapata Marekani zama za vita Baridi,kinapungua sana siku
hizi,na mataifa yanayoitishia NATO yanashambuliwa,na mengine yalishapinduliwa
na viongozi wake kuuliwa kama tulivyoona katika makala zilizotangulia.
George
Herbert Walker Bush ambaye tumuite “Bush Baba(sasa ana umri wa miaka 88) na
mwanaye George Walker Bush(65) wamepigana vita vya Ghuba vya kwanza na vya pili na kufanikiwa
kumpindua Saddam Hussein na kumuulia mbali,huko kandoni mwa Mto Frati.
Jambo hili
la vita vya kwanza vya Ghuba na vya pili na mapinduzi kisha kuhukumiwa kifo
Mtawala wa Irak yenye Mito Frati na Tigris, ni utimilifu wa Unabii wa “Kukaushwa”
kwa Mto Frati, ili njia itengenezwe kwa Wafalme wa Mashariki kuungana na
Magharibi,ili kufanya shauri la kumrithisha Kiongozi Mmoja wa Dunia nzima!
Tumeona kwamba Muammar al-Qaddafi aliyetaka
kuwapinga naye amepinduliwa na kuuawa, kisha Carlos The Jackal na “Magaidi”
wengine wamefungwa jela na wengine wameuliwa.
Hao
wanaoitwa magaidi,ni wapinzani wa ubeberu wa Magharibi, kwa staili ya kulipua
mabomu!
Mataifa ‘bishi
na tukutu’ yaliyosalia sasa ni Iran na Korea Kaskazini,iliyoanza kufanya
majaribio ya ya silaha za Nyuklia Oktoba 9,mwaka 2007.
Hata sasa, ingalipo “Homa ya Dunia” mara hii
siyo VITA BARIDI vya Ubepari dhidi ya Ukomunisti, bali ubepari dhidi ya NYUKLIA
inayomilikiwa na Madola machache ya Mashariki kama Iran na Korea.
Syria
inashughulikiwa, sasa na kama lisemavyo Executive Intelligence Review,ni VITA
vya aina yake vya kuwatiisha wenye msimamo tofauti na Marekani, Israeli,Ulaya
namfumo wa dini moja unaoandaliwa kushita mamlaka ya Dunia nzima.
Hakika, sasa tunajua,baada ya Saddam kuuawa,
alifuata Gaddafi na Osama bin Laden na atafuata huyo Bashir al-Assad wa Syria
na wenzake, kama watazidisha upinzani.
Walianza
kuambiwa wasaini mikataba ya kupunguza silaha. Mikataba hii ilianza tangu
Agosti 5, mwaka 1963,Russia, Marekani na Uingereza walipotiliana saini mkataba
wa kuacha majaribio ya Nyuklia baharini,ardhini na angani.Huu ni Mkataba wa
mjini Moscow,Urusi.
Urusi na
Marekani walitiliana saini tena kuacha Nyuklia Januari 27,mwaka 1967, tena
Uingereza na Russia wakatiliana saini Julai Mosi mwaka 1968 na Mei 26 mwaka
1972 Marekani na Urusi wakaingia mkataba mkubwa uitwao, Strategic Arms
Limitation Treaty(SALT- 1), NI HUKO Moscow,kwamba baada ya miaka mitano waache
kutengeneza Misaili zenye kuweza kulenga shabaha kutoka Bara moja hadi linguine.
Haya mamisaili yanaitwa, Intercontinental
Ballistic Missiles(ICBM)wakaifanyia marekebisho mikataba hii 1974 hadi Septemba
1997.
Mwaka 1978
iliyokuwa kambi ya Northern Atlantic Treaty Organization(NATO) ikiongozwa na
Marekani ilikuwa na hayo makombora ya masafa marefu ya ICMBs 1,054 wakati ile
Kambi ya Mashariki ya Warsaw Pact( Poland) ilikuwa ikiongozwa na Urusi ,ilikuwa
na makombora hayo 1527.
Ukitazama
Military Balance wakati huo utaona NATO walipokuwa na manowari za kivita(SLBM)
656,Warsaw Pact walikuwa nazo 845. NATO walikuwa na ndege za kivita 387,Warsaw
Pact wao walikuwa na ndege 135.
Nataka
kusema kwamba, Kambi ya Urusi ya Mkataba
wa Warsaw ilikuwa na nguvu kuzidi NATO ndiyo maana kulifuatwa mikataba mingine
kama SALT-2 uliotiwa saini Vienna, Austria
Juni 18,mwaka 1979.
Kila upande
ulikubali kusitisha kutengeneza makombora hayo na mabomu zaidi ya 2,400,na
makombora ya ICBM 1,320 yasivukwe kwa kila upande.
Mkata huu wa
SALT 2 uliingia doa wakati Urusi ilipoivamia Afghanistan Desemba, mwaka 1979
Rais Jimmy Carter akaacha kuamini Mkataba huo. Osama Bin Laden alianza kulelewa
na Marekani wakati huu ili awapinge Warusi huko Afghanistan.
Baadaye
aliwageuka,kama Gaddafi naye
alivyowageuka.
NATO pia
walikuwa na magari ya kubeba silaha za
nyuklia zenye kulenga shabaha tofauti, Multiple Independently Targetable
Re-entry Vehicle(MIRV) kama 1,046 wakati Mashariki walikuwa na 140.
Desemba 8,1987
makombora ya masafa ya Kati nayo yakawewa Mkataba wa INF huko Washington baina
ya Urusi ya Mikhail Gorbachev na Ronald Reagan wa Marekani.
Ipo mikataba
mingine kama START 1 na START 2 ya Januari 3, 1993 iliyosainiwa Moscow,na ipo
marufuku ya majaribio ya Nyuklia ya Septemba 24 mwaka 1996(CTBT) pia kati ya
Russia na Marekani ili kukataa milipuko ya Nyuklia.
Huu mkataba
mwaka 2000 ulitia saini na nchi 160,na baadaye Oktoba 15 mwaka huu 2000 mkataba
huu ulipata nguvu.
Kuna madhara
mengi ya kuvuja kwa nyuklia kama yale ya kinu cha Chernobyl, huko Ukraine siku
hizi Aprili 26 mwaka 1986 karibu na
Kiev.
Watu 31
walikufa,lakini hata sasa Japan vinu vimelipuka na Ulaya vimelipuka na kuleta
madhara makubwa kwa afya za watu sababu ya mionzi ya sumu inayoleta saratani
kwa watu.
Septemba
30 1999 ajali nyingine ilitokea
Tokoimura,Japan wakati wanarutubisha madini ya Uranium. Hata Tanzania tukianza
kurutubisha Uranium na tukaenda kinyume na Marekani na Ulaya,utaona
watakavyotuijia.
Marekani
iliwahi kupiga mabomu ya Atomik B-26 katika Hiroshima,Japan Agosti 6,mwaka 1945
kisha siku tatu baadaye wakapiga NAGASAKI.Haya ni mabomu yaliyohitimisha vita
vya Pili vya Dunia.
Baada ya
hivi vita,Kambi ya Mashariki ilikuwa na majeshi 1,303,000 dhidi ya 1,175,000 ya
NATO. Nato walikuwa na vifaru 11,000 dhidi ya 26,000 ya vile vya Warsaw Pact.
Madege ya vita NATO walizidiwa kwa takriban ndege 2000. Ndiyo maana ililia
mikataba.
Sasa, kiama
cha SEPTEMBER 11,2001 pale WTC kilicholeta kifusi kilichojaza ekari 16,na kifusi
chenyewe cha WTC kilikuwa na uzito wa tani milioni 1.2 hapo walipoita, ‘Ground
Zero’ ndicho chimbuko la visingizio vingi vya kuyakomesha mataifa korofi, hasa
ya Kiarabu ambayo ni adui wa Israeli.
Marekani
inaendesha kinachoitwa VITA DHIDI YA UGAIDI kwa ushirika na Ulaya na
Israeli,ili kuwakomesha Waaarabu wenye msimamo mkali ili wasalimu amri. Hivi ni
vita vitakavyoendelea hadi Yesu anapokuja mara ya pili duniani.
Itaendelea
0786 324 074
KUTOKA JERUSALEM YA KALE HADI JERUSALEM MPYA-5
*Vifo vya Saddam,Osama na Gaddafi ni
kutimia kwa Unabii wa Ufunuo 16:12
*Unabii wa Carlos The Jackal,kuhusu
Marekani,Libya na Syria unatimia sasa
Turejee
nyuma, wakati wa vita vya kumpindua Mtawala wa Nchi ya Mito miwili ya Tigris na
Eufrates,Saddam Hussein.
Marekani,
aslani haikusubiri ruhusa ya Umoja wa Mataifa(UN);Saddam alipinduliwa,Sanamu
lake likang’olewa kuonesha enzi yake ilikwishakoma, baada ya miaka mitatu
gerezani, akanyongwa huko Camp Justice,mjini Baghdad.
George
Herbert Walker Bush(88),Agosti mwaka 1990 alijaribu kumng’oa Saddam Hussein
huko Irak,kipindi alipoivamia Kuwait. Unajua sababu za Saddam kuivamia Kuwait?
Waliiba mafuta.Bush huyu (Baba) alipata ushindi mwembamba katika medani ya
vita.
Bush baba
alisaidiwa sana na vikosi vya Umoja wa Mataifa(UN),vikosi vya Umoja wa Kujihami
Ulaya Magharibi(NATO) na Muungano wa Kiarabu, Arab League.
Kuwait
ilikombolewa toka mikononi mwa Saddam, Bush baba akapata hadhi katika historia
ya nchi hiyo babe sana duniani siku hizi. Uchumi ulikwenda vibaya mno,ukaja
kurekebishwa na Bill Clinton baada ya kushinda Uchaguzi mkuu mwaka 1992.
Bush Baba, aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Shirika
la Ujasusi la Marekani(CIA)na alisaidia sana kuparaganyika kwa iliyokuwa Dola
ya Kisovieti ya Urusi(USSR) zama za Mikhail Gorbachev.
Kuparaganyika
kwa USSR,ilikuwa kupisha njia kwa Mataifa ya Magharibi na Umoja wa Kujihami wa
Ulaya Magharibi(NATO) kupanua himaya yake hadi Mashariki, na ilikuwa ishara ya
kumalizika kwa VITA BARIDI,kasha UKUTA WA BERLIN ukavunjwa,mwaka 1994.
Kitendo cha
George Bush(mtoto)kumnyonga Saddam,ilikuwa kurejesha heshima ya nyumba yao
katika Taifa hilo babe sana duniani. Marekani ilivumbuliwa na Christopher
Columbus,OKTOBA 12, MWAKA 1492, na ikaja kutangaza uhuru wake Julai 4,mwaka
1776. Juzi walisherehekea miaka 236 ya uhuru.
Sasa,
tuchambue Ufunuo 18:11-18. Marekani ilipata uhuru na ikawa nchi kimbilio kwa
waliosetwa na tawala katili sana.
Lakini,
ilikuja kuwa nchi katili; na ikaanza kufanya mapenzi ya JOKA ambaye ni Ibilisi
mwenyewe,pale ilipopindua marais wa mataifa mengine kwa jeuri. Hawa ni pamoja
na Jenerali Manuel Noriega wa Panama na Salvador Allende wa Chile, wakamweka
kibaraka wao Dikteta, Pinochet.
Licha ya kupindua serikali za Panama na Chile
kama nilivyokwishaandika katika makala zilizotangulia, Shirika lao la CIA
lilishirikiana sana na manyang’au kama Dikteta Mobutu wa Zaire kuua wanamapinduzi wa Afrika, akina
Patrice Emely Lumumba.
CIA
ilishirikiana na Makaburu wa Afrika ya Kusini kuwawinda wanamapinduzi wa Afrika
ya Kusini,ili Botswana, Namibia,,Angola,Msumbiji na hata Afrika ya Kusini
waafrika wasijitawale wenyewe.
Ndani ya Angola,Chama cha MPLA na FNLA
vilipambana wakati FNLA wakipewa msaada na CIA hadi uhuru ulipopatikana kutoka
Ureno mwaka 1975. Jonas Malheiro Savimbi alikuwa kibaraka wa Marekani,ili
kuvuruga maendeleo ya nchi, hadi walipomumwaga juzi juzi akaachwa kupigwa risasi na majeshi ya
serikali. Jambo hili alishalisema Kamara Kusupa.
MMarekani
iwe chini ya Barack Obama ama Mgombea wa Republican,Mitt Romney, ina akili ile
ile, ya kunena kama Shetani(Ufunuo 13: 11) yaani ubabe wake na kulazimisha watu
kile wanachotaka wao.
Angalia,
kwamba CIA waliwasaidia Makaburu wa Afrika ya Kusini kuwaua wanafunzi 250
katika kitongoji cha SOWETO(South West Township) mwaka 1976,mjini Pretoria.
Turejee
Irak, ambayo baada ya Saddam hamkani si shwari. Nchi imegawanyika sasa ni baina
ya dini na dini;msikiti kwa msikiti,ukoo baina ya ukoo wanapambana.
Watu wa
Madhehebu ya SUNNI mwaka 2007 walikuwa milioni 3.8 baada ya Saddam ambaye pia
alikuwa Sunni kunyongwa. Hawa wako Magharibi.
Wakurdi,
ambao Saddam alidaiwa kuua walikuwa milioni 4.4 nao wanaishi Kaskazini Mashariki mwa Ninawi,ule mji mkubwa
aliokwenda kuhubiri Nabii Yona akamezwa na Nyangumi!
Washia, nao ni milioni 8.4 wanaishi Babeli
hadi Kusini Mashariki mwa nchi. Mjini Baghdad na Kati kati mwa nchi kuna watu
wa dini mchanganyiko wapatao milioni 9.2.
Najaf na
maeneo ya utajiri wa mafuta ni maeneo ya Washia ambao wamewekewa chuki na
SUNNI,huku Bush,Obama na hata Mitt Romney(Mgombea wa Republican) wanaweza
kuhangaika kurejesha amani,bila mafanikio…ni vita hadi kiama!
Dola lenye
nguvu kandoni mwa Mto Frati,lilikuwa limevunjika ili kutoa nafasi kwa madola ya
Mashariki kuungana na NATO na European Common Market, ama EU ili kuungana na
Marekani kuandaa serikali moja ya Dunia.Huku ndiko kukauka kwa Mto Frati.
Angalia nchi zilizo Mashariki mwa Mto
Frati:Pamoja na nchi zilizokuwa katika Muungano wa Kisovieti(USSR), na
Afghanistan,Pakistan,China,India,Korea Kaskazini na Kusini na Japan leo
zinalazimishwa ama zinaungana na Marekani kwa hiari katika biashara na katika
mambo mengi.
Kabla ya
VITA BARIDI kwisha, hali ilikuwa tofauti. Jumatatu, Januari Mosi mwaka 2007,
Romania na Burgaria zilijiunga na NATO(Northern Atlantic Treaty Organization);
ilikuwa SIKU MOJA tu,baada ya Saddam
kuzikwa. Unabii unatimia bila kukosa.
Bado Iran na Korea Kaskazini, na Syria
itavurugwa kama nitakavyoonesha punde.
Kwa mujibu
wa mwqandishi wa Iran anayeishi jijini Paris, Amir Taheri, Yule gaidi wa kale,
Carlos The Jackal, alisema Marekani ni “Shaytan” yaani Shetani ama Joka(rejea
Ufunuo 13:11) yaani Shetani amejivika mwili wa Marekani ili kuuhadaa Ulimwengu.
Imesemwa kwamba waumini wa dini ya Kiislam
wanapaswa kuichukia Marekani kama Shetani anavyochukiwa pasipo kuulizwa!
Nirejee kidogo katika Historia ya Carlos
ingawa nimeijadili kwa utulivu mwingi katika makala zilizotangulia.
Alizaliwa
Oktoba 12,mwaka 1949. Katika kitabu kiitwacho Revolutionary Islam Editions Du
Rocher,2003 yeye anadai ni Muislam huko gerezani,Ufaransa.
Babaye
alikuwa mwanasheria milionea wa Venezuela,nchi ya Hugo Chavez. Carlos
alimkubali sana Osama bin Laden, na
alisoma Patrice Lumumba University,huko Moscow. Hiki ni Chuo Kikuu
kilichoanzishwa na Shirika la Ujasusi la Urusi,KGB,ili kuwafundisha
wanaharakati wan chi za Dunia ya Tatu,
Amefanya harakati nyingi mahali pengi kwa
miaka 20 hivi, Urusi ilipoparaganyika, akaanza kujificha-ficha, hadi Makachero
wa Ufaransa wakaja kumkamata mjini Khartoum, Agosti 14,mwaka 1994.
Alisafirishwa
chini ya ulinzi mkali hadi Paris ambako amefungwa maisha. Nataka ujue kwamba
1994 Ukuta wa Berlin uliangushwa na kuondoa Kambi mbili za watu kuashiria
kwisha kwa VITA BARIDI,na Marekani kuanza kutawala Dunia,huku Carlos
akakamatwa, ambaye pia alipinga mno maslahi ya Magharibi. Umeona?
Carlos aliwahi kutabiri mambo ambayo yametokea
kwa usahihi kabisa. Ametabiri Irak kujengwa upya na Marekani, ametabiri SYRIA
kuvunjika vipande vipande, na sasa tunaona vita vikali baina ya majeshi ya
kigeni yanayounga mkono waasi na serikali inayoungwa mkono na Urusi na China.
Ametabiri Lebanon kuanguka na kikundi cha
HEZBOLLAH kuharibiwa.Ametabiri Kossovo kuwa huru na kwamba SUDAN(sasa Kusini na
Kaskazini) itafanyiwa usanii ili kusukwa upya,hili limetimia,Sudan ni mbili
siku hizi.
Ametabiri
Ufaransa nayo kusambaratika na kuwa vinchi vidogo-vidogo.Mwisho wa siku Carlos
anadhani ni Iran na Korea Kaskazini tu zitakazompinga Marekani.Anasema vita vya
kumpinga Marekani vitakuwa virefu sana, na Marekani watashinda sana, anawataka
Waislam kufanya JIHAD dhidi ya Marekani kuwa Nguzo Kuu ya
Uislam,swala,kufunga,Hija huko Mecca N.K
Alimpenda Sana
Rais wa Algeria, Azizi Bouteflika na kumwita,”Kaka yangu mpenzi” na Osama
alimwita, “Sheikh” na anaogopa Algeria nayo kumezwa na ubeberu wa Magharibi
Hata hivyo,
Carlos hakujua Algeria ilishaungana na Marekani na NATO pamoja na mataifa
mengine ya Kiarabu,na Israeli katika urafiki unaoitwa, Partnership for Peace.
Leo, wapo
wanaharakati wanaoitwa magaidi walioanzisha JIHAD dhidi ya Marekani na
washirika wake.
Hata hivyo, unabii wa Biblia na hata Carlos
tumemwona akitabiri ushindi kwa Marekani,kwani unabii wa Biblia aslani hausemi
uongo.
Tijadili kidogo dhana ya kujitoa mhanga
kupambana na Marekani na mabeberu wenzake.
Ni kweli
Marekani wanafanya uchafu na unyama duniani. Hata hivyo kwa Wakristo,kupambana
na adui kwa kumuua ni dhambi,maana Yesu alikataa chuki na uadui,sembuse kujitoa
mhanga?
Tazama Mathayo 5:43-48 na hata ule ujumbe wa
Yesu kwa Petro kurejesha kisu halani mwake.

Itaendelea
0786 324 074
Subscribe to:
Posts (Atom)