Katika
Biblia, Ufunuo wa Yohana 17:13 husema kwamba, Wafalme wa Dunia sasa hufanya
majadiliano, ili kumrithisha mamlaka yao Mfalme mmoja tu Duniani.
Ufalme ujao
Duniani, huoneshwa kwa mifano ya “Mwanamke” aliyebebwa na Mnyama, ambaye katika
makala zilizotangulia,tukaona mwanamke huyu aitwaye, Goddess Roma, akiwa nje za
ofisi za Bunge la Umoja wa Ulaya,huko mjini Brussels.
Makao Makuu
ya serikali hii mpya, Gideon M. anasema yatakuwa Jerusalem, lakini mimi nasema
yatakuwa mahali kilipokuwa kiti cha enzi cha utawala wa Rumi ya kale.
Hata
hivyo,tujadili namna Umoja wa Kujihami wa Ulaya Magharibi(NATO) walivyoanza
kuuvuka Mto Frati na Tigris ili wajielekeze Mashariki,ilikokuwa iliyokuwa Dola
ya Kisovieti,USSR.
Naam,
tujadili namna “Mto Frati” ulivyoanza kukauka,ili kutengeneza njia kwa madola
ya Magharibi kuzitwaa milki za Mashariki, ili kuzilazimisha kujiunga nao aidha
NATO, ama Umoja wa Ulaya(EU),na Soko lao la Pamoja, European Common Market.
Mhariri wa
Jarida la Executive Intelligence Review la Marekani, Edward Spannus, amesema
vita vinavyochochewa sasa na Marekani na Uingereza huko Syria,hatimaye vitakuwa
VITA VYA TATU VYA DUNIA!
Uingereza,Marekani na washirika wao wanawaunga
mkono waasi wa Syria,na Urusi na China wanamuunga mkono kiongozi wa nchi hiyo,
Bashir al-Assad.Sasa, inasemwa,mwisho wa siku Marekani na washirika wake
wataingia vitani dhidi ya Urusi na Uchina,na hivi ni vita vya tatu vya Dunia?
Biblia,
katika Ufunuo 16 inasema vita vya TATU VYA DUNIA ni Har Mageddon, ambamo Mungu
atapingwa kwa nguvu za mashetani na mawakala wao,Freemasons,na malaika toka
mbinguni watakuja kusimamia mabambano ili kulinda HAKI NA UKWELI Duniani.
VITA BARIDI vilikwisha mwaka 1991 Desemba,
baada ya Russia,Kazakhstan na Belarus kuwa mataifa huru. Baadhi ya nchi kama
Georgia na nyingine tayari zimekuwa washirika wa NATO.
Tunaona
JAPAN na mataifa mengine ya Mashariki wakiungana na M arekani na washirika wao.
Kile kimbembe kilichowapata Marekani zama za vita Baridi,kinapungua sana siku
hizi,na mataifa yanayoitishia NATO yanashambuliwa,na mengine yalishapinduliwa
na viongozi wake kuuliwa kama tulivyoona katika makala zilizotangulia.
George
Herbert Walker Bush ambaye tumuite “Bush Baba(sasa ana umri wa miaka 88) na
mwanaye George Walker Bush(65) wamepigana vita vya Ghuba vya kwanza na vya pili na kufanikiwa
kumpindua Saddam Hussein na kumuulia mbali,huko kandoni mwa Mto Frati.
Jambo hili
la vita vya kwanza vya Ghuba na vya pili na mapinduzi kisha kuhukumiwa kifo
Mtawala wa Irak yenye Mito Frati na Tigris, ni utimilifu wa Unabii wa “Kukaushwa”
kwa Mto Frati, ili njia itengenezwe kwa Wafalme wa Mashariki kuungana na
Magharibi,ili kufanya shauri la kumrithisha Kiongozi Mmoja wa Dunia nzima!
Tumeona kwamba Muammar al-Qaddafi aliyetaka
kuwapinga naye amepinduliwa na kuuawa, kisha Carlos The Jackal na “Magaidi”
wengine wamefungwa jela na wengine wameuliwa.
Hao
wanaoitwa magaidi,ni wapinzani wa ubeberu wa Magharibi, kwa staili ya kulipua
mabomu!
Mataifa ‘bishi
na tukutu’ yaliyosalia sasa ni Iran na Korea Kaskazini,iliyoanza kufanya
majaribio ya ya silaha za Nyuklia Oktoba 9,mwaka 2007.
Hata sasa, ingalipo “Homa ya Dunia” mara hii
siyo VITA BARIDI vya Ubepari dhidi ya Ukomunisti, bali ubepari dhidi ya NYUKLIA
inayomilikiwa na Madola machache ya Mashariki kama Iran na Korea.
Syria
inashughulikiwa, sasa na kama lisemavyo Executive Intelligence Review,ni VITA
vya aina yake vya kuwatiisha wenye msimamo tofauti na Marekani, Israeli,Ulaya
namfumo wa dini moja unaoandaliwa kushita mamlaka ya Dunia nzima.
Hakika, sasa tunajua,baada ya Saddam kuuawa,
alifuata Gaddafi na Osama bin Laden na atafuata huyo Bashir al-Assad wa Syria
na wenzake, kama watazidisha upinzani.
Walianza
kuambiwa wasaini mikataba ya kupunguza silaha. Mikataba hii ilianza tangu
Agosti 5, mwaka 1963,Russia, Marekani na Uingereza walipotiliana saini mkataba
wa kuacha majaribio ya Nyuklia baharini,ardhini na angani.Huu ni Mkataba wa
mjini Moscow,Urusi.
Urusi na
Marekani walitiliana saini tena kuacha Nyuklia Januari 27,mwaka 1967, tena
Uingereza na Russia wakatiliana saini Julai Mosi mwaka 1968 na Mei 26 mwaka
1972 Marekani na Urusi wakaingia mkataba mkubwa uitwao, Strategic Arms
Limitation Treaty(SALT- 1), NI HUKO Moscow,kwamba baada ya miaka mitano waache
kutengeneza Misaili zenye kuweza kulenga shabaha kutoka Bara moja hadi linguine.
Haya mamisaili yanaitwa, Intercontinental
Ballistic Missiles(ICBM)wakaifanyia marekebisho mikataba hii 1974 hadi Septemba
1997.
Mwaka 1978
iliyokuwa kambi ya Northern Atlantic Treaty Organization(NATO) ikiongozwa na
Marekani ilikuwa na hayo makombora ya masafa marefu ya ICMBs 1,054 wakati ile
Kambi ya Mashariki ya Warsaw Pact( Poland) ilikuwa ikiongozwa na Urusi ,ilikuwa
na makombora hayo 1527.
Ukitazama
Military Balance wakati huo utaona NATO walipokuwa na manowari za kivita(SLBM)
656,Warsaw Pact walikuwa nazo 845. NATO walikuwa na ndege za kivita 387,Warsaw
Pact wao walikuwa na ndege 135.
Nataka
kusema kwamba, Kambi ya Urusi ya Mkataba
wa Warsaw ilikuwa na nguvu kuzidi NATO ndiyo maana kulifuatwa mikataba mingine
kama SALT-2 uliotiwa saini Vienna, Austria
Juni 18,mwaka 1979.
Kila upande
ulikubali kusitisha kutengeneza makombora hayo na mabomu zaidi ya 2,400,na
makombora ya ICBM 1,320 yasivukwe kwa kila upande.
Mkata huu wa
SALT 2 uliingia doa wakati Urusi ilipoivamia Afghanistan Desemba, mwaka 1979
Rais Jimmy Carter akaacha kuamini Mkataba huo. Osama Bin Laden alianza kulelewa
na Marekani wakati huu ili awapinge Warusi huko Afghanistan.
Baadaye
aliwageuka,kama Gaddafi naye
alivyowageuka.
NATO pia
walikuwa na magari ya kubeba silaha za
nyuklia zenye kulenga shabaha tofauti, Multiple Independently Targetable
Re-entry Vehicle(MIRV) kama 1,046 wakati Mashariki walikuwa na 140.
Desemba 8,1987
makombora ya masafa ya Kati nayo yakawewa Mkataba wa INF huko Washington baina
ya Urusi ya Mikhail Gorbachev na Ronald Reagan wa Marekani.
Ipo mikataba
mingine kama START 1 na START 2 ya Januari 3, 1993 iliyosainiwa Moscow,na ipo
marufuku ya majaribio ya Nyuklia ya Septemba 24 mwaka 1996(CTBT) pia kati ya
Russia na Marekani ili kukataa milipuko ya Nyuklia.
Huu mkataba
mwaka 2000 ulitia saini na nchi 160,na baadaye Oktoba 15 mwaka huu 2000 mkataba
huu ulipata nguvu.
Kuna madhara
mengi ya kuvuja kwa nyuklia kama yale ya kinu cha Chernobyl, huko Ukraine siku
hizi Aprili 26 mwaka 1986 karibu na
Kiev.
Watu 31
walikufa,lakini hata sasa Japan vinu vimelipuka na Ulaya vimelipuka na kuleta
madhara makubwa kwa afya za watu sababu ya mionzi ya sumu inayoleta saratani
kwa watu.
Septemba
30 1999 ajali nyingine ilitokea
Tokoimura,Japan wakati wanarutubisha madini ya Uranium. Hata Tanzania tukianza
kurutubisha Uranium na tukaenda kinyume na Marekani na Ulaya,utaona
watakavyotuijia.
Marekani
iliwahi kupiga mabomu ya Atomik B-26 katika Hiroshima,Japan Agosti 6,mwaka 1945
kisha siku tatu baadaye wakapiga NAGASAKI.Haya ni mabomu yaliyohitimisha vita
vya Pili vya Dunia.
Baada ya
hivi vita,Kambi ya Mashariki ilikuwa na majeshi 1,303,000 dhidi ya 1,175,000 ya
NATO. Nato walikuwa na vifaru 11,000 dhidi ya 26,000 ya vile vya Warsaw Pact.
Madege ya vita NATO walizidiwa kwa takriban ndege 2000. Ndiyo maana ililia
mikataba.
Sasa, kiama
cha SEPTEMBER 11,2001 pale WTC kilicholeta kifusi kilichojaza ekari 16,na kifusi
chenyewe cha WTC kilikuwa na uzito wa tani milioni 1.2 hapo walipoita, ‘Ground
Zero’ ndicho chimbuko la visingizio vingi vya kuyakomesha mataifa korofi, hasa
ya Kiarabu ambayo ni adui wa Israeli.
Marekani
inaendesha kinachoitwa VITA DHIDI YA UGAIDI kwa ushirika na Ulaya na
Israeli,ili kuwakomesha Waaarabu wenye msimamo mkali ili wasalimu amri. Hivi ni
vita vitakavyoendelea hadi Yesu anapokuja mara ya pili duniani.
Itaendelea
0786 324 074
No comments:
Post a Comment