WANATHEOLOJIA wengi hukubaliana kwamba,Ezekieli 28:16 nikauli ya Mungu,aliyoitoa mbinguni kunhusu Ibilisi.
Kwamba, ni ‘Mfanyabiashara’ wa haliyajuu.Ukitaka kutajirika haraka kupitia njia haramu sana kamamadawayakulevya na fedha chafu,unawafuata mawakalawake, Freemasons(Ufunuo 18:1-3).
Nakariri kifungu hiki katika Biblia ya Kiingereza, iitwayo, Revised Standard Version (RSV)kama ifuatavyo:
“ In the abundance of your ‘trade’ you were filled with ‘violence’ and you sinned”. Nachagua maneno ‘trade’ yaani biashara na ‘violence’ yaani ghasia na machafuko.
Naam, katika tafsiri isiyo rasmi, Mungu alimwambia Lusifa kwamba katika ‘Biashara’ yake iliyoenea dunia nzima alifanya ghasia na dhambi.
Aidha, maneno ya Kiingereza, “Widespread trade” hutafsiriwa kwamba ni “slander” maana yake kwamba hata mbinguni Lusifa alianzisha mashitaka dhidi ya serikali ya Mungu, kwamba haikuwa na demokrasia; iliwanyima (malaika) demokrasia na haki.
Shetani ni Mwanaharakati bingwa wa Haki za Binadamu na Malaika pia! ‘Slander’ ni kauli yenye nia ya kumharibia mhusika heshima(reputation); Shetani anaelezwa na Biblia kama Mshitaki; ama mwenye kauli za kuvunjia watu hadhi(Zekaria 3:1,Ufunuo 12:10).
Hii kauli yenye kashfa, “Slander” humuongoza Shetani na wafuasi wake, Freemasons, na mawakala wake wengine kama serikali zenye nguvu duniani, superpowers, kufanya vita na ghasia kwa madai ya kuleta haki na demokrasia.
Lakini, badala yake,tumeona huko Irak,Libya,Misri n.k hakuna vyote viwili;kuna machafuko,mauaji ; hakuna amani.
Leo,nitajadili biashara haramu ya Shetani,Freemasons na mataifa makubwa ya Magharibi,kasha Uchina na Urusi. Najadili fedha chafu, na utajiri unaoletwa kwa watu na mwanamke Yule, Yezebeli, ama Babeli wa siri.
Ghasia, vita na machafuko, chanzo chake ni mawazo ya ubinafsi na uchoyo, ambao hatimaye hufanywa kuwa tabia ya mhusika. Wazo huja kwanza(hutangulia) vitendo hufuata baadaye, na matokeo yake ni mauaji ya kinyama.
Muinjilisti,Kamara Kasupa, juzi amegusia biashara haramu ya ALMASI ZA DAMU huko Sierra Leone.
Siku hizi tunamwona Charles Taylor huko The Hague anakojibu mashitaka ya kuwasaidia Revolutionary United Front, walioua watu na kupora almasi chini ya uongozi wa Fodday “Poppay” Sankoh aliyefariki huko gerezani.
Chanzo siyo Sankoh ama Taylor; ni ubinafsi wa Freemasons hawa na choyo cha utajiri; mwisho wa siku wamekamatwa zana(mapanga na visu) walioshika visu na mapanga, wameachwa huru-na hakuna wa kuhoji!
Msomaji mmoja amenionya nisitumie vifungu vya Biblia katika makala zangu,kama nataka zisomwe na watu wasomo makini,la sivyo wasomi makini watasusa kuzisoma!!
Hata hivyo, katika uandishi wa habari, ili habari iwe ‘credible’ ama ‘reliable’ lazima kuwe na ‘checks and balances’.Lazima habari iwe na news worthiness na iwe na chanzo cha habari cha kuaminika sana.
Kwa kuwa nakusudia kuandika juu ya “Mchuuzi” ama mfanyabiashara kubwa-kubwa wa mwanzo ulimwenguni, Biblia katika Ezekieli 28:16 inaniambia,
“Lucifer was involved in widespread trade”, kwamba tangu mbinguni Lusifa alianzisha ‘biashara’ haramu ya kashfa ili kubomoa ustawi wan a heshima ya Bosi wake-Mungu.
Sasa, niachane na Biblia,ili nitekelezeje jukumu la uandishi na malengo yake mahsusi, ya ‘To inform, to educate, to reform, to entertain, to incite?’
Nalazimika kusaka vyanzo vingi vya habari(Biblia,Koran,sheria,kauli za wasomi,wanafalsafa,viongozi na Mungu na Shetani wakiwemo) ili niandike makala yenye kufanyiwa utafiti wa kina,yenye kuhabarisha,kuelimisha,kurekebisha umma, kuburudisha na kuonya,ama kuweka AJENDA miongoni mwa wasomaji wangu.
Kama msomaji hatajali, asome habari za Mungu na Shetani kama BURUDANI tu!
Naam, chanzo change cha habari,Biblia,kimesema aliyeanza kufanya biashara chafu ulimwenguni,ni Ibilisi. Biashara yake ililenga ‘kuchuuza’ watu ili wadharauliwe,wauawe.
Tumjadili Mtu Mweusi-Mwafrika. Najua Kamara Kasupa anajadili jambo hili kwa kina; nitoe mchango wangu kidogo.
Ziko kauli dazeni za kumdhalilisha mtu mweusi. Tazama chache hizi:
Homer (700 BC)- “Ethiopia(Africa) is a remote place at extreme of universe where the people worshipped and sacrificed to gods”
Thomas Hobbes(1588-1679) “Africa is a timeless place in which there are no art, letters or social organization, but instead, only fear and violent death”
Jean-Jacques Rousseau(1712-1778) “The Black people are unable to think in any reflective manner. Their engagement in arts is therefore, a thoughtless activity which is the antithesis of intellect”.
Uko upuuzi mwingi na kauli za ovyo kuliko hizi za Wazungu,Wachina, Wahindi,Makaburu n.k dhidi yetu.
Kibaya zaidi, hata Weusi wenzetu wanaamini hivi, na wanatamani laiti wangezaliwa Wahindi ama Wazungu hivi.
Kauli za akina Dk.Watson,D.W.De Clerk n.k ni kwamba, hapa Afrika, hakuna ‘thesis of intellect’ kwamba sisi ni ‘unable to think in any reflective manner’ Afrika ni Bara ambamo kumejaa violence and death,ni waabudu miungu na tunaojitoa dhabihu kwa miungu na mashetani!
Mwafrika, hana fikra, hawezi kufanya jambo lolote la maana, nchi yake imejaa hofu na kifo!
Hata mwanzilishi wa kauli kwamba ‘Binadamu wote huzaliwa wakiwa sawa’ Thomas Jefferson,rais wa tatu wa Marekani,alisema “Ingekuwa vigumu kama nini Mtu Mweusi kujua kanuni za Hesabu katika kitabu maarufu cha Euclid!”
Loh!! Hii ndiyo biashara ya Shetani. Na kwa bahati mbaya sana hata Mwafrika anaamini hivi,ndiyo maana leo chetu kimekuwa chao-chao siyo chetu.
Dini ya Ukristo haikuanzia Ulaya,imeanzia Mashariki ya Kati.Wazungu(Rumi) waliwafanyia mitume ukatili mwingi na kuwaua, Weusi wameamini dini siku nyingi.
Simoni Mkrene(Sudan) alimsaidia Yesu Msalaba, huu ulikuwa mwaka wa 31 AD. Yesu alitimkia Misri(Afrika) mwaka 4 BC,la sivyo Wayahudi wangemuulia mbali zamani. Sasa Afrika,waabudu sanamu na miungu tangu lini?
Juma lililopita,tulijifunza ushenzi wa Dola ya Rumi na ibada ya sanamu ya kulazimisha watu. Abraham alitoka Ur(Iraki) siyo Ulaya,ndiye baba wa Isaka na Yakobo aitwaye Israeli.
Viongozi wetu na wasomi wetu wamesikiliza ‘biashara’ hii haramu ya Shetani na Freemasons,kwamba sisi weusi siyo lolote. Ndiyo mawazo ya akina Adolf Hittler. Unajua katika Oliumpiki ya mwaka 1936 huko Berlin, Mmarekani Mweusi Jesse Owens,aliwatoa kamasi Wazungu, akapata medali nne za dhahabu kwa dakika 45 tu,Mgeni wa Heshima,Hittler akasusua kutoa zawadi?
Alisema, Jesse Owens alikuwa mnyama-sasa alishangaa Mzungu atashindanishwaje na mnyama?!
Ndizo akili za akina Materazzi dhidi ya Zenedine Zidane,kwenye uwanja huo huo wa Olimpiki wa Berlin mwaka 2006!
Matokeo yake, uchumi wa Afrika umekuwa siyo huru,tunaamrishwa kila jambo na Benki ya Dunia(WB) na fuko la Fedha la Kimataifa(IMF) na taasisi za kikoloni kama UNCTAD na WTO n.k
Ndiyo maana tunalazimishwa kuwa mashoga!!
Hawa wameanzisha ukoloni mwingi baada ya vita vya pili,1945 wakafanya mradi wao kupitia Marshall Plan. Kabla walikaa mwaka 1884 wakagawana Afrika kama nyama choma mezani.
Mwenyekiti wao alikuwa Freemasons na Ibilisi mwenyewe. Malengo yao ni kutusema vibaya na kutushitaki katika macho ya ulimwengu kwamba sisi Weusi ni sifuri,ni hasi. Halafu,tunakubali.
Wamesababisha mashirika na viwanda vyetu vife kwa sira za ubinafsishaji zilizoletwa na IMF na WB.
Nimezungumza na msomi na mzee anayefanya kazi zake jijini Mwanza, Charles Masalakulangwa juu ya WB na IMF itatuepushaje na mazao yetu kama pamba,kahawa,korosho,kahawa n.k yasishuke bei ili kuondokana na umasikini?
“Tunachakata mazao yetu na kuyaongezea thamani,ili tuyauze katika masoko kama Agoa(Marekani) ama Ulaya. Nchi tajiri zimeweka ruzuku kwa bidhaa zao na wakulima wamepewa ruzuku, sasa bidhaa zetu na mazao yetu yatashindana na yake ya Ulaya na Marekani? Kwanza, bidhaa zao zina ubora mkubwa na bei iko chini, sasa bidhaa gani zitashindana na zile za Ulaya kwenye masoko ya dunia?’
Matokeo yake, tuna sangara, dhahabu,almasi,tanzanite,mazao ya kilimo lakini wao ndiyo wanaopanga bei. Pamba yetu ingali magulioni,haina bei-bei huja mpaka yawepo majanga Ulaya,Marekani na China.
Wanaopanga bei ni G-7,G-8,G-20 sijui European Economic Community, Paris Club n.k
Tunasumbuliwa na mfumuko wa bei, si kwa sababu ni sisi tumetaka, ni wao wamependa hivi. Inflation na Reccession inatokea pasipo sisi kutaka kwa sababu vitu hupanda bei na ‘supply’ hupungua.
Tujadili bei ya mafuta ambayo ni chanzo cha kupanda kwa gharama za maisha.Mafuta ndiyo huendesha uchumi wa dunia,huendesha viwanda,mitambo,umeme kama wa TANESCO,Daladala n.k
Mwaka 1979 kulitokea ugomvi wa mafuta,Uingereza mfumuko wa bei ukapanda hadi kuwa asilimia 334. Sisi hapa mfumuko wa bei ni asilimia 20 tunataka kukata roho kwa maisha magumu!
Nataka kusema kwamba, nchi zenye rasilimali nyingi zina simamiwa na Freemasons hawa-hazina uhuru,na kuna vita na machafuko. Ukiona amani ujue panapohusika hapana mali, hata mahakama ya The Hague haipasogelei!!
Utajiri uko mikononi mwa mwanamke aliyebebwa ba Mnyama(Ufunuo 17:1-) na wafalme wa dunia nzima lazima kushirikiana naye na hao rafiki zake Freemasons lazima uchumi wote na mabenki yote view mikononi mwao.
Nani anamiliki mafuta ya dunia? Angalia makampuni makubwa ya mafuta duniani, “SUPERMAJORS”.
Exxon Mobil-Marekani, British Petroleum(BP)la Uingereza, na Uholanzi kwenye mahakama ya Moreno Ocampo wanamiliki kampuni la ,Royal/Dutch Shell kwa ubia na Uingereza.
Total ni kampuni la Ufaransa na Ubelgiji,kule Makao Makuu ya EU ambako mwanamke Yule amekaa juu ya mnyama(Ufunuo 17:1-).
Chevron Texaco na Conoco Phillips ni makampuni ya Wamarekani,Yule mwanakondoo wa Ufunuo 13:11-).
Russia, kuna makampuni kama Lukoil,Yukos na Sibneft yanayomilikiwa na Ikulu ya nchi hiyo-Kremlin.
Na Uchina kuna Petrochina. Nchi zote hizi tano ni wanachama wa kudumu wa Baraza la Usamala la Umoja wa Mataifa, ambao wakiamua kwenda Irak,Libya,Misri ama Iran kuvamia na kupora mafuta,wanakwenda.
Hata China na Russia,leo wanafanya biashara ya mafuta tu, hawana lolote la kuipinga Marekani,Ulaya na Freemasons. Hata Kremlin tayari kuna mawakala wa CIA na Freemasons.
Nchi zinazozalisha kwa wingi mafuta na zimeungana (OPEC) ni Algeria, Indonesia,Iran,Irak,Kuwait,Libya,Nigeria,Qatar,Saudia, Falme za Kiarabu na Venezuela kwa Hugo Chavez.
Urusi,Mexico,Canada,Norway na Marekani huzalisha sana mafuta,lakini hawamo kwenye OPEC.
Sasa angalia,katika nchi za mafuta ambazo zinawakatalia wababe wa NATO zina amani? Hakuna biashara ya kifo huko maana ‘The merchants of Death’ wako karibu na kila kulipo na rasilimali nyingi,hususan mafuta na gesi.
Hii ‘widespread trade’ ya Ibilisi na Freemasons iko kila kuliko na mafuta; ukiwapa mafuta, poa wanakuacha,ukiwanyima wanachochea vita na unapinduliwa ama unauliwa!
Itaendelea
0786 324 074
No comments:
Post a Comment