JUZI, mashoga na wasagaji wa Afrika ya Kusini, walifanya tamasha la kukata na shoka ili kusherehekea haki zao; naam Haki za Binadamu !!
Wanawake kwa wanawake na wanaume kwa wanaume waliooana Afrika ya Kusini, walikuwa wakisherehekea kwa kupigana mabusu ya tashtiti,kulembua macho na kulegezeana macho mabarabarani mchana kweupe!
Naam, wao wanaita ilikuwa, ‘Gays Pride Festival’ na huu ndiyo uhuru ambao Marekani,Uingereza na washirika wao wa Ulaya wanataka tubadili katiba zetu na kuufuata,la sivyo hatupati msaada!
Afrika ya Kusini,iliruhusu ndoa za mashoga mwaka 2006.
Kituko kingine kinachodhihirisha uhai wa Freemasons na Ibilisi kuua watu kwa ajali za ndege,meli,milipuko ya maghala ya silaha kama ya Mbagala na Congo-Brazaville, ni kile cha yule ‘shushushu’ wa Libya, Basset Ali al-Meghri,kuhukumiwa kifo Januari 31 mwaka 2001,kwamba alilipua ndege ya Pan American World Airways(Pan Am), halafu juzi wakaja kusema alionewa!
Ilisemwa kwamba, ile ndege ya Marekani Flight 103 ya Pan Am mwaka 1988 huko Lockerbie, Scotland, haikulipuliwa na akina Basset al-Meghri, walisingiziwa tu.
Ulikuwa uongo,bila shaka wa Marekani na ‘Mkono wake msaidizi’ Freemasons, kutungua ndege ile na kuua mamia ya watu,kasha kutafuta ‘mbuzi wa kafara’ aitwaye kwa Kiingereza, Scapegoat, ili kumtwisha dhambi ile,kwa lengo la kutaka kuishambulia Libya,kwamba iliwatuma hao magaidi!
Ukitaka kujikomba kwa Ulaya na Marekani, utawala wa Marehemu Saddam Hussein ulitaka ‘kufunika kombe mwanaharamu apite’ kwa kumkabidhi al-Meghri katika mahakama ya Uholanzi,ili akashitakiwe kwa sheria za uholanzi kwa kosa la kulipua ndege, kosa ambalo leo tumeambiwa hawakulifanya hata chembe!
Ilikuwa Aprili 5 mwaka 1999 utawala wa Gaddafi ulipomkabidhi al-Meghri,ili kuepuka kipigo cha mbwa mwizi kutoka Marekani na washirika wake.
Utaona,kumbe Freemason wanapoua watu kwa ajali za ndege,boti,moto na meli, halafu anasingiziwa mtu Fulani, anafungwa jela ama anauliwa-hatujasahau uongo kwamba Irak kulikuwa na silaha za maangamizi,kumbe umbeya tu.
Al-Meghri ameachwa huru na yuko Libya ambako anagugumia maumivu ya saratani, katika kitanda cha mauti akisubiri mauti yanayomkodolea jicho la bashasha.
Ndivyo dunia inayotawaliwa na Ibilisi ilivyo-Libya yenye utajiri wa mafuta, taifa la kale la Waberiberi, iliwahi kutawaliwa na Kathago, Rumi, Wavandali na Utawala wa Ottomans.
Italia, iliitawala Libya tangu mwaka 1912. Uingereza na Ufaransa waliitawala Libya baada ya Vita vya Pili vya Dunia; ikapata uhuru wa bendera Januari Pili mwaka 1952,kisha Muammar Gaddafi akaja kupindua mwaka 1969.
FREEMASONS NA UTAJIRI WA MAFUTA
Nataka kusema kwamba,Ulaya wameitawala Libya,wanajua utamu wa utajiri wake wa mafuta. Ulaya na Marekani ndiyo wenye makampuni makubwa, “Supermajors” ya mafuta hapa duniani.
Utawala wa Gaddafi ukitaka kubinafsisha mafuta yote yawe kwa maslahi ya Walibya, ooh…wakamkosea Mzungu. Freemasons wanatafuta kumiliki chumi za dunia nzima na mafuta ni ‘damu’ inayobeba uhai wa dunia na mataifa yao.
Siku nyingine nitajadili jambo hili kwa kina.
Sasa, twajua kwa nini Freemasons waliingiza Libya katika Mhimili wa Uovu(The Axis of Evil) wapate kuishambulia na kumuulia mbali Gaddafi na wapinzani wa sera zao.
Na kwa misingi hii hii tujue kwa nini Iran itashambuliwa baada ya Marekani kukamilisha Uchaguzi Mkuu,Novemba mwaka huu.
Uingereza, Ujerumani, Hispania, Ufaransa, Italia, Ureno, Uswisi hawa ni vichwa saba katika mnyama wa Ufunuo 13, ufunuo 17, Danieli 7.
Marekani, ni mwanakondoo wa Ufunuo 13:11-18 na hawa wote wanahaha kuhakikisha wanafanya kampeni kali na propaganda kupitia mashirika yao ya habari yenye nguvu duniani, kuwapaka matope watu wasiopendwa,ili wapinduliwe kijeshi na AJENDA YAO YA SIRI itekelezwe.
Katika unabii wa Biblia, katika kitabu cha Danieli 2:43 mataifa haya ya Ulaya yameoneshwa yakiwa yanabebwa na historia ya iliyokuwa Dola ya RUMI.
Mataifa haya hufananishwa na vidole vya sanamu ya Nebuchadnezzar, katika sura ya Pili ya Danieli. Ni sawa na pembe 10 za mnyama wa ajabu ambaye ni Rumi katika Danieli 7:7.
Hizi dola 10 za Ulaya, zilizoinuka baada ya dola ya Rumi, zina tabia ile ya Rumi ya Washenzi wa kale(Danieli 7:24).
Pembe ndogo(Danieli 7:24,25) ni nguvu isiyo mamlaka ya kisiasa ambayo ilizifukuza Ulaya tawala tatu za Wavandali, Waheruli na Ostrogoths. Nguvu hii ilianza kuitawala Dunia mwaka 538 AD.
Huu ndiyo utawala uliohuishwa baadaye na utaitawala dunia nzima na kulazimisha watu kuuabudu(Danieli 7:24,25).
Utawala huu utapewa mamlaka na shetani na mawakala wake,Freemasons,Illuminati,Marekani na washirika wake wa Magharibi, wataunganisha siasa na dini, watalazimisha Mfalme aabudiwe, watakaokataa watawekewa vikwazo vya kiuchumi, watafungwa jela ama kuuliwa.
Sasa, demokrasia wanayojidai kueneza iko wapi? Kama watu watalazimishwa kuabudu dini moja, wakikataa wanafungwa, mtu kwa kuwa ni mtawala anajiita Mungu(Danieli 7:25 na Ufunuo 13:1-10) ndiyo demokrasia gani hii?
Utawala uliozuka baada ya dola ya Rumi kusambaratishwa na washenzi wa Kaskazini, ukafukuza dola tatu za Wavandali(mwaka 454 AD),Heruli(493 AD) na Ostrogoths(538 AD) na kuanza kutawala dunia kwa jumla ya miaka 1260.
“Pembe Ndogo” yenye macho kama mtu mwanaume, huwakilisha mamlaka itakayoongoza serikali ya Dini na Siasa- Religio-Political Power.
Mtawala huyu anaitwa, ‘Mpinga Kristo’ ama Chukizo la Uharibifu lililonenwa na Nabii Danieli(Mathayo 24:15).
Katika Ufunuo wa Yohana 17: 5 upo mfano wa utawala huu wenye nguvu na wa ina yake unaoandaliwa kuitawala dunia,kidini,kiuchumi,utamaduni na kila nyanja.
Yohana wa Ufunuo wa Yohana 17:5 ,katika mwaka 96 AD alioneshwa utawala huu wa mseto wa dini na siasa.
Akaoneshwa Jiji liitwalo “Babeli ya Siri” likiwa limebebwa na malaka(mnyama) za serikali za Ulaya na Marekani.
Babeli, ni Jiji la kale sana, zama za Dikteta Nebuchadnezzar, mwaka 6060 BC. Siku hizi, Babeli ni moja ya Maajabu saba ya Dunia,kutokana na utajiri wake wa dhahabu ulioporwa katika mahali walikopindua na kuua, bustani zenye kuning’inia katika kuta ndefu zenye futi za mraba 400.
Bustani hizi zilikuwa juu kutani kiasi cha futi 75 kutoka ardhini.
Hii ni nchi ya Wakaldayo wa zamani waliokula nguruwe na kunywa mvinyo kwa wingi. Na kabla ya kula vyakula hivi vya kitajiri, walivitoa sadaka kwa miungi yao mikuu, Bel na Murdoch.
Danieli na vijana wenzake wa Kiebrania waligoma kula chakula hiki na pombe zilizotolewa dhabihu kwa miungu kabla ya kuliwa eti ili kumfanya mlaji awe na nguvu za miungu hii mwilini mwake!
Wakasema, kula nguruwe hizi na kunywa pombe ilikuwa kujitia unajisi na chakula cha Mfalme(Danieli 1:1-8).
Babeli, mabaki yake yangalipo hata leo huko kando ya Mito miwili ya Tigris na Euphrates, mchangani-na unaweza kufika kwa treni, ni eneo la utalii siku hizi, sasa ni makao ya mashetani na ndege wachafu kama popo, bundi n.k
Jiji hili la siri hufananishwa na mwanamke, katika Ufunuo wa Yohana 17:5-9.
Hata jiji la Mwanza, huitwa, “Jiji-Dada” la Wurzburgh, Ujerumani. Kumbe mji hupewa heshima ya mwanamke?
Babeli wa mafumbo katika Ufunuo 17:5-9 ni Jiji la Siri, litakalobebwa na Ulaya siku za karibuni,ili kuua watu watakaokataa kumsujudia shetani na Freemasons-ndiye mtawala atakayefuata baada ya Marekani na washirika kuitiisha dunia.
Mwanamke huyu, “Babeli” ndani yake kuna waabuduo sanamu, wala nguruwe,walevi, waabudu jua na mfumo wa sayari zote, wenye imani za kuongea na mizimu(spiritualism) n.k
Mwanamke huyu, amezaa watoto, anaitwa ‘MAMA WA MAKAHABA’ na machukizo ya nchi.
Katika Biblia, ukahaba ni pale watu wa Mungu wanapo anza kuungana na waabudu sanamu na miungu,ulevi, ibada ya mizimu na uongo na kuacha usafi na kicho kwa Mungu muumbaji(Hosea 1:2)
‘Uzinzi’ ni kumwacha Mungu na kuabudu sanamu na miungu(Hosea 1:2). Mji huu Babeli, katika Ufunuo 17:3-11 unabebwa na Ulaya na Marekani, “SUPER POWERS” zenye nyuklia na uchumi mkubwa na wana sera moja.
Iran watapigwa na Marekani, Israeli na Ulaya kwa sababu wakiachwa, wakawa na Nyuklia,watapinga kuibeba Babeli hii!!
Mji huu Babeli wa siri una ‘Meya’ wake anajiita Mungu duniani na ahera, VICARIUS FILIIDEI na nyumerali hizi za Kirumi huwakilisha nambari 666.
Mji dada wa Babeli umebeba kikombe cha ulevi wa mafundisho,ndiyo propaganda za uongo duniani,ni uchafu katika imani ya kidini,Kiislam,Kiyahudi ama Kikristo.
Mji huu Babeli uliua wapinzani wake,maana ulikuwepo zamani,mwaka 538-1798 AD.Ulikoma Feburuari 10 mwaka 1798 baada ya miaka 1260 ukawa mwisho wa Dark Ages.
Mwanamke huyu ambaye ni ‘Mji Dada’wa Babeli ya kale, wakati wa Nabii Yohana akiandika kitabu cha Ufunuo(mwaka 96 AD) haukuwepo, na ukafufuka toka kuzimu Feburuari 11 mwaka 1929 AD.(Ufunuo 17:8-9)
Mji dada wa Babeli uko juu ya milima saba. Mji ulikoko katika vilima saba Ulaya! Tazama Ufunuo 17:9 UONE SIRI hii, na milima saba pia huwakilisha falme saba za kale, Babeli, Wamedi na Waajemi katika serikali ya mseto, Wagiriki, Rumi ya kipagani, Rumi ya Kikristo, Pembe Ndogo na Serikali Mpya duniani yenye Dinina siasa(Ufunuo 17:9-11)
Naam, Marekani na washirika wanajiandaa kuleta duniani dini mpya ya muungano wa Freemasons,Illuminati n.k
Ni mfumo wa dini(system of religion) ambao ni bandia. Bidhaa bandia(counterfeit) zinaigiza zile bidhaa halisi.Bidhaa feki hufanana na feki, lakini ubora wake ni duni na utazitambua kwa alama yake ya biashara-trade mark- kwa mfano bidhaa feki za Panasonic huitwa,Panasoanic,hukosa ubora wa Panasonic,tujihadhari!
Dini counterfeit ina alama(ALAMA YA MNYAMA) mnyama ni mpinga Kristo yaani utawala bandia wa Kristo Duniani.(2Wathesalonike 2:3-4).
Kwa kawaida utawala wa Mungu siyo wa kidunia, kwa nini dini zianze kuwaandama akina Kikwete na kutaka kuwapindua kwa kampeni kali makanisani?
Utawala bandia wa YESU unapinduaje serikali za dunia wakati utawala wake uko mbinguni?
Utawala wa Mungu utaanzaje kuua watu wanaoupinga hapa duniani? Ufunuo 13 na 17 hutwambia kwamba dini feki itaua watakaoipinga na ulishaua zamani wapinzani zaidi ya milioni 50 yaani zaidi ya waliokufa wakati wa vita kuu ya kwanza nay a Pili.
Mnyama yaani Mpinga Kristo ni mtawala bandia wa dunia hii(2 Thesalonike 2:3-4)
Mpinga Kristo anajifanya Mkristo(1Yohana 2:18,19)Wapinga Kristo hutokea miongoni mwa wakristo, na wana tabia kama za Babeli ya zamani,ulevi, ibada ya sanamu,ulaji wa nguruwe,kiu ya utawala duniani, ibada ya jua nyota na sayari n.k
Wapinga Kristo wameacha Injili na kuhubiri siasa makanisani,ili kuwapindua viongozi waliopo kote duniani-wanajidai kuhamasisha demokrasia, na hujihusisha sana na ushoga,ulawiti na ufisadi wa kiroho,ingawa wao hukazania sana watu waache ufisadi!!
Mpinga Kristo ndiye Pembe Ndogo ya Danieli 7:25 na ni mnyama wa Ufunuo 13:1-10. Mfumo wa Ibada bandia, humbeba Mpinga Kristo wa Ufunuo 13,17 Danieli 7:25 na 2Thesalonike 2:2-4.
Msomaji mmoja akanitumia SMS iliyoandikwa:
“ North Korea na itikadi yao ya Kikomunisti watakubali kwelikuwa Allied(kuungana) na Magharibi? Nina wasiwasi watakuwa upande wa Russia na China ili kuitetea Iran! Pia nilitaka kuweka kumbukumbu sawa katika makala ya Gidion M kuhusu Jewish Revolution ni 1948 na siyo 1848”.
Iran lazima washambuliwe kijeshi,baada ya uchaguzi mkuu wa Mareni Novemba mwaka huu,la sivyo Israeli na Ulaya watachukua jukumu hili wenyewe?
Waziri Mkuu Benyamin Netanyahu hivi niandikapo yuko Washington kuomba kibali ili kuishambulia Tehran. Obama anaogopa kuiingiza Marekani vitani wakati huu wa karibia uchaguzi mkuu.
Hata hivyo, imetangazwa kwamba Korea Kaskazini wamepewa msaada wa chakula ili waachane na mradi wao wa Nyuklia wa Yongbyon.
Nimemwona juzi, Hillary Clinton akiwa Pyongyang kuzungumza na yule rais kijana wa Korea,baada ya kifo cha babaye, Kim Jong Il.
Korea imeshatiwa kabali,haina tena ubavu wa kuipinga Marekani na washirika wake na haina kitu,itaachana na mradi wa nyuklia na kuruhusu wakaguzi wa silaha wa Umoja wa Mataifa ambao ni mawakala wa CIA, Mossad n.k
Maskini Tehran wameachwa kwenye mataa,na watashambuliwa peke yao baada ya mudfa mfupi ujao,ili kuandaa njia kwa Freemasons kuunda mfumo wa dini na siasa duniani.
Itaendelea
0786 324 074
Welcome to brotherhood Illuminati where you can become
ReplyDeleterich famous and popular and your life story we be change
totally my name is Dan Jerry I am here to share my
testimony on how I join the great brotherhood Illuminati
and my life story was change immediately . I was very poor
no job and I has no money to even feed and take care of my
family I was confuse in life I don’t know what to do I try all
my possible best to get money but no one work out for me
each day I share tears, I was just looking out my family no
money to take care of them until one day I decided to join
the great Illuminati , I come across them in the internet I
never believe I said let me try I email them.all what they
said we happen in my life just started it was like a dream to
me they really change my story totally . They give me the
sum of $1,200,000 and many thing. through the Illuminati I
was able to become rich, and have many industry on my
own and become famous and popular in my country , today
me and my family is living happily and I am the most
happiest man here is the opportunity for you to join the
Illuminati and become rich and famous in life and be like
other people and you life we be change totally.If you are
interested in joining the great brotherhood Illuminati.then
contact him +2348106618681 or for more information +1(705)8062021
email:illuminatibrotherpowerful@gmail.com or you need my assistance
email:danjerry04@gmail.com...