*Mashariki ya Kati ni “Focal Point” ya Dunia
VITA vya karne nzima, baina ya Waarabu na Israeli kwa upande
mmoja, na mnyukano baina ya Waarabu na Mataifa Makubwa ya Ulaya na Marekani kwa
upande wa pili, hatimaye madhara yake yamefika kila Bara,kila nchi.
Katika makala nyingi
zilizotangulia,nimeandika sana
juu ya Misri ya Anwar Sadat alivyofanya shambulizi la kustukiza huko Israeli,
Oktoba, mwaka 1973.
Nimeandika pia
mnukano wa makundi ya wanamapinduzi wa Kipalestina kumenyana na Mataifa ya
Magharibi kwa staili ya ‘kigaidi’ zama za
Carlos The Jackal.
Nimeandika vita Baridi kufika hatma yake wakati wa Kuanguka
kwa Ukuta wa Berlin mwanzoni mwa miaka ya
90,na kusambaratika kwa Dola la Kisovieti la USSR.
Juma lililopita
nimejadili matukio ya kigaidi ya Black September kuwasaka adui zao Waisraeli
hadi Munich,Ujerumani,
Septemba 5, mwaka 1972 wakati wa michezo ya Olimpiki.
Kutoka zama za Black
September, yaani Septemba ta utusitusi hadi sasa, akiina Carlos The Jackal
wameishia kifungoni, akina Saddam Hussein, Muammar Gaddafi, Osama bin Laden na
wenzao wamezimwa kwa mapinduzi ya kijeshi na wamelala makaburini,kufuatia jeuri
na mtutu wa bunduki za rashasha.
Tunakoelekea,
mazungumzo ya Amani kama yale ya Camp David
mwaka 1973 kati ya Israeli na Waarabu kwa upande mmoja, ama kati ya Waarabu na
Ulaya na Marekani, hayatakuwa na maana zaidi ya kulazimishwa kusalim amri
mithili ya kijibwa mbele ya dubu mwenye kiu ya damu.
Naam, Waarabu
kujisalimisha kwa njia ya kuufyata mkia mithili ya kijibwa mbele ya fisi,mbele
ya Dola babe,jeuri na fisadi za Magharibi!!
Nguvu za Mataifa ya Kiarabu zinatindika sana. Nguvu hizi zilikuwa ndani ya pampu za
mafuta katika miaka ya 70. Nguvu hizi zilikuwa katika majambia ya wanamgambo wa
Kiarabu katika karne ya Sita hadi karne ya 15.
Siku hizi, makampuni
ya mafuta ya Marekani, Ufaransa, Uingereza, Italia,Uholanzi n.k yanahafifisha
‘nguvu’ za mataifa haya yanayozalisha sana ‘dhahabu nyeusi’ hii duniani. Majambia
ya Wanamgambo wa Kiarabu yaliyofananishwa na “Mikia ya Nge”(Tazama Ufunuo
9:7-11) yamegeuka kuwa nyasi.
Kitu kinachoweza
kuonekana katika muktadha huu ni kile kiitwacho, “The Modern Middle East Oil
Politics”.
Nataka kusema
kwamba, ‘Oval Office’ iliyoko White
House chini ya Bwana Barack Obama, lengo lake ni
kuhafifisha nguvu za uchumi(mafuta) wa Milki za Waarabu ama mataifa ya
Mashariki ya Kati, huku akiibusu na kuikumbatia Israeli, wakati ‘Intifada’
nyinginezo ni maumivu kwa Mwarabu.
Shirika la Atomiki Duniani(IAEA)limearifiwa na maofisa wa
Usalama wa Israeli kwamba Iran
siku hizi inajidai kuweza kurutubisha zaidi ya kilogramu 630 za Uranium, ili
waweze kutengeneza bomu la Nyuklia katika hatua za awali.
Hata mataifa mengine
ya Kiarabu ya Ghuba, kama Saudi Arabia na Bahrain yako tayuari kuwaunga mkono
Marekani na Ulaya kuichakaza Iran ili isijitie ‘kidume’ na kughairi Amri
Takatifu za Marekani,Ulaya, Israeli na NATO za kuachana na mradi wa Nyuklia.
Iran itashambuliwa
haraka sana isipojisalimisha chini ya mamlaka za Mzungu tapeli, ambaye hata
sasa amezikalia Irak, Libya, Afghanistan, Misri,Libya,Syria na Mzungu anavuka
Mto Frati na Tigris kuelekea kwingineko Mashariki.
Leo, tuanze
kulijadili Shirika la Ujasusi la Israeli, MOSSAD, ambalo nembo yake ni Vinara
Saba vya Taa vilivyoanza kutumiwa na Waisraeli tangu zama za Nabii Musa, mwaka
1500 BC.
Mossad,ni majasusi hatari duniani ambao hujuma zao
zimetamalaki hadi Afrika ya Mashariki tangu mapema mwaka 1976.
Tujadili kidogo
mapambano baina ya Chama cha Ukombozi cha Palestina, POPULAR FRONT FOR THE LIBERATION OF PALESTINE (PFLP)
dhidi ya Israeli na washirika wake wa Magharibi; vita vilivyopanuka hadi kufika
Entebbe,Uganda miaka ya 70.
Vita kama hivyo vingalipo
leo baina ya Al-Shabaab,al-Qaeda dhidi ya maslahi ya Magharibi hata hapa Afrika
ya Mashariki.
Entebbe,Uganda
tuliona mapambano ya PFLP wakati ule Carlos The Jackal akiongoza hujuma tele
dhidi ya Magharibi.
Ndege ya Ufaransa,
Air France
Air Bus A 300,iliyokuwa na nambari za Usajili BVGG ilijikuta ikitekwa nyara
Juni 27 mwaka 1976.
Sasa,
Uganda wanakumuka miaka 36
kamili ya tukio hilo
la kihistoria. Ndege hiyo ilitokea Athens,
Ugiriki inayofilisika, ikalazimishwa kwenda kutua Entebbe.
Ilikuwa na jumla ya
abiria 248 na wafanyakazi dazeni,ilitekwa na Wapalestina wawili walioshirikiana
wa PFLP kitengo cha Operesheni za Nje kiitwacho PFLP-LEO, na walisaidiwa na
Wajerumani wawili wa kikundi cha kimapinduzi cha German Revolutionary Cells.
Wilfred Bose na Brigite Kuhlmann. Ilikuwa saa 6:30 hivi mchana,
Juni 26 kama leo mwaka 1976 ndege hiyo ilipotekwa angani ikalazimishwa kwenda
kutua mjini Benghazi,Libya.
Zama za Muammar
Gaddafi, ndege hiyo ikatua Benghazi
na kujaza mafuta,ikapumzika kwa muda wa saa saba.
Mwanamama raia wa
Uingereza aliyekuwa mjamzito akajidai kuumwa utungu wa kuzaa mtoto, akaachiwa
huru hapo Beghazi,kabla ya safari ya Entebbe,kuanza.
Nataka msomaji
atambue kwamba kuachiwa huru mwanamama huyu kulifikisha habari mjini Tel Aviv
mapema, wakaanzisha mkakati kamambe wa kuwakomboa mateka wao katika ardhi ya Uganda.
Saa tisa na robo,
siku iliyofuata, yaani Juni 28 mwaka 1976 hiyo Air Bus ilitua Entebbe, wale
mateka wengine ambao nao hawakuwa Waisraeli wakaachiwa huru-kosa lingine.
Maana yake ni kwamba,
serikali ya Israeli ilimaizi kuwa raia wake ambao walikuwa mikononi mwa
watekaji wa Kipalestina, walikuwa mikononi mwa mauti. Hivyo, Waziri Mkuu wan
chi hiyo akalazimishwa kufanya kila njia waokolewe, hata kama kufanya hivyo
kulikuwa kukiuka sheria za kimataifa,kama
ugaidi ama mashambulizi ya kijeshi dhidi ya nchi nyingine.Wewe ungeanza
mazungunzo ya kidiplomasia ya akina Thabo Mbeki au Kofi Annan.
Makomando wa Israeli
walitua Entebbe,Uganda, na kumshikisha adabu Idi
Amin Dada aliyejitia Mshindi wa Dola ya Kingereza,Mwanamasumbwi nguli na Field
Marshal.
Rais wa Maisha wa Uganda alikiona cha mtema kuni mbele ya
makomando 100 wa Israeli.Wakati huo Uganda ilikuwa rafiki wa Waarabu,
na walijifanya adui wa Israeli.Akina Ghaddafi na Palestina walimponza Amin,
Yule mwanamke wa Kiingereza na mateka wengine walipoachwa,
wakasema kupitia vyombo vya habari,kwamba huenda mateka wale wa Israeli
wangeuliwa kinyama mkononi mwa adui zao Wapalestina.
Basi,Makomando
walifanya mazoezi kwa muda mfupi wakafika Uganda usiku ili kukomesha kiburi
cha Dikteta aliyejifanya mbabe katika medani ya vita. Zama za Waziri
Mkuu,Menachem Begin, Shirika la kijasusi la MOSSAD likawezesha makomando wenye
vinara saba vya taa(Mwangaza Mkamilifu) kutua Entebbe kwa saa moja na nusu tu
na kufanikiwa kuwakomboa mateka wake.
Hii Operesheni ina
majina mengi, inaitwa Operation Thunderbolt, wengine huiita kwa jina la Komando
aliyeuliwa pale, Jonathan ama ‘Yonnie’
Huyu Jonathan Netanyahu alikuwa ndugu wa damu wa Waziri Mkuu wa sasa wa
Israeli, Benyamin Netanyahu.
Wengine tumeiona Operesheni
hii kwenye Filamu ya RAID ON ENTEBBE na tumepata
kusoma kitabu kiitwacho, 90 Minutes at Entebbe.
Usinisumbue kuuliza wapi utakipata!!
Luteni Kanali
Jonathan ‘Yonnie’ Netanyahu alikufa Entebbe,lakini
walifanikiwa kuondoka na maiti yake na akazikwa kishujaa.Abiria 103 waliokuwa
mateka Waisraeli mikononi mwa adui zao Waarabu, walikombolewa hatimaye. Hawa
103 walikuwa miongoni mwa abiria 248 wa ile Air Bus ya Ufaransa.
Ni usiku wa manane
hiyo Operesheni ilipofanyika Entebbe,kilomita
kama 27 kutoka Kampala,
Amin hakujua aliamkia kupapasa maiti za askari wake 45 asubuhi, wakati
makomando walishaondoka mapema kabla ya alfajiri.
Uwanja wa ndege wa Entebbe uliharibiwa kwa
mabomu wakati watekanyara wote
walifyekwa kwa risasi za makomandoo wa Israeli.
Ngege iliyowaleta
Makomandoo hawa iliruka kwa takriban kilomita 4000 hivi ikawaleta makomando 100
waliokata mzizi wa fitina Entebbe.
Makomando watano
walijeruhiwa,mmoja akafa lakini askari wa Amin 45 na wateka nyara wote
walipigwa risasi, mateka watatu walikufa pia.
Ndege ya Kirusi
MIG-17 ilisambaratishwa vibaya.
Itaendelea
0786 324 074
No comments:
Post a Comment