KABLA ya
kuendelea na tukio la Makomando 100 wa Israeli kuwakomboa mateka wao, Entebbe,
Julai 4mwaka 1976, tuangalie tukio la juzi la ugaidi,Mombasa.
Mombasa,juma
lililopita, magaidi waliua watu wasiopungua watatu katika Hoteli moja,
walipokuwa wakitazama mechi ya Soka,kati ya Italia na England.
Aghalabu,
matukio ya kigaidi yamekuwa yakitokea katika Jiji la kitalii la Mombasa,katika
Pwani ya Kenya.
Novemba 28, mwaka 2002,magaidi wa Kipalestina
walishambulia Hoteli ya kitalii ya Paradise iliyoko Kikambala,takriban kilomita
25 kutoka mjini Mombasa, wakaua watu.
Magaidi hao hao walijaribu kuirushia kombora
ndege ya Israeli ya Arkia Airlinesiliyokuwa ikiruka kutoka Uwanja wa Ndege wa
Moi, hapo Mombasa. Jaribio hilo la kigaidi halikufanikiwa.
Naam, nataka
msomaji amaizi kuwa vita baina ya Israeli na Wapalestina, vilishapiganwa
maradufu katika ardhi ya Afrika Mashariki.Msukosuko wa Mashariki ya Kati
ulishaleta dhama kubwa katika Dunia nzima.
Agosti
7,mwaka 1998,Balozi za Marekani Tanzania na Kenya zilishambuliwa na magaidi
wanaohisiwa al-Qaeda, na kupoteza maisha ya watu zaidi ya 200.Hawakuwemo
Wazungu wala Mayahudi, bali Waafrika tu.
Kampala, haikulipuliwa wakati huo,kwa sababu
ndiyo kwanza vikosi vya Marekani vilikuwa na program kamambe ya mafunzo ya
kijeshi mjini Kampala,kumbe Kampala ilikuwa, “More alert” kuliko Nairobi na
Dar.
Naam,vita
kati ya al-Qaeda Israeli kwa upande mmoja, na kati ya Waarabu na Marekani na
Ulaya na wajomba zao Israeli,kwa upande
wa pili,havina mipaka ya Kijiografia.Vita hivi vitadumu muda mrefu,kama
tutakavyoona mbele ya safari.
Uganda,
wakati wa Dikteta,Field Marshal Idi Amin Dada,iliwasaidia wateka nyara wa
Kipalestina kufuatia urafiki wake na Waarabu, na ni uadui mkali kwa Israeli na Magharibi.
Turejee
kidogo Entebbe,usiku wa kuamkia Julai 4,mwaka 1976.Muda kitambo baada ya
makomandoo 100 washirika wa Mossad,kumtia adabu Amin,Marekani walituma ndege
Uganda,naam Entebbe, ili kuwasaidia majeruhi wa Operesheni ile kamambe.
Unajua, maofisa 53 wa Ubalozi wa Marekani
walishikiliwa na wanamgambo wa Kiislam mjini Tehran,huko Iran.
Wateka nyara
wa Kipalestina waliuliwa katika tukio hilo la Entebbe, na kabla ya kukumbwa na
mauti walisikika wakitaka Israeli iwaachie huru Wapalestina 40 walioshikiliwa
nchini Israeli.
Hadi sasa
akina Mahmoud Abbas na Benyamin Netanyahu, wanazungumza hay ohayo hata baada ya
kifo cha Yasser Arafat.
Naam vita vya kisasi vya miongo mingi.Hadi
sasa Israeli napambana na wanamgambo wa Kipalestina, na wakati mwingine ndege
zimetekwa ama zimejaribiwa kulipuliwa angani-VITA VYA KISASI.
Waama, nipende kusema basi kwamba,Mossad ni
majasusi hodari duniani kupambana na uadui wa Waarabu wengi duniani. Unajua
kuna Waisraeli milioni nane tu huko Israeli?
Kamanda wa
Operesheni ya Entebbe, Muki Besta, alikiri kwamba Operesheni ya Entebbe
ilifanikiwa kufuatia ukusanyaji wa data nyingi na muhimu wa Mossad.
Msomaji
wangu, Nyalapa, aliniuliza Mossad walipataje ramani ya Entebbe hadi kuweza
kushambulia ngafla na kuokoa mateka?
Hata kama Israeli waliujenga uwanja huo wa
ndege wa Entebbe,bado wangeweza kuingia Uganda na kupiga picha muhimu na
kujiondokea,pasi na kushtukiwa.
Katika nchi
za watu wazembe,wasio na uzalendo,wapenda rushwa na wazalendo wa matumbo yao
wenyewe, Mossad, CIA,MI5,MI6,BOSS la
Makaburu ama majasusi wengine wangeweza kufanya lolote na kuondoka,kwa nguvu ya
pesa,ama kwa kutumia ulegefu wa fikra.
Ungedhani, hawa ‘NJAA TUPU’ wanaohujumu fedha
za umma katika Halmashauri zetu, wangeweza kulinda maslahi ya watu?Na wengine
hupiga kelele nyingi za hasira,kwa kuwa
matumbo yao yangali na njaa! Hasira hutuka tumboni mwa wenye njaa!!
Ulimwengu wa Kiarabu unasalitiana mno siku
hizi. Miaka ya 70 Waarabu walishikilia uchumi wa Dunia kwa silaha moja
tu-Mafuta.
Mchora
katuni wa Kidachi aliwahi kuchora Mwarabu akiwa kawaweka ‘Chini ya Ulinzi’Wakuu
wa Mataifa babe sana Ulaya na Marekani kwa kutumia “Pampu” ya mafuta.
Mafuta ni
silaha ambayo siku hizi imesalimishwa Magharibi na Mwarabu mwenyewe,wanaobisha
wanakiona cha mtemakuni,nao ni Saddam Hussein,Gaddafi na wenzao.
Mwaka 1976,
Ujerumani iliongozwa na Kansela Willy Brandt,Ufaransa iliongozwa na Rais
Georges Pompidou,Uingereza ilikuwa chini ya Waziri Mkuu,Edward Heath na
Marekani ilikuwa chini ya Richard Milhous Nixon,kabla ya kashfa ya ‘Watergate’.
Unaifahamu?
Unatazama nini kuona viongozi hawa kuwekwa
chini ya ulinzi kwa pampu ya mafuta ya Mwarabu,mwaka 1973? Bila shaka,utaona
baada ya hapa hawa mabepari wakifanya juu chini kumpora Mwarabu mafuta,kwa
kutumia kila njama, hapo upo?
Nilikwishaandika katika safu hii,kwamba
makampuni makubwa sana ya mafuta,”SUPERMAJORS” kutoka mataifa haya na mengine
rafiki, yalishafanya Mapinduzi hadi kushikilia siasa za mafuta(Oil Politics) za
Mashariki ya Kati.
Lengo ni kuishikilia ‘silaha’ hii iitwayo,
Dhahabu Nyeusi. Viongozi wa Saudi Arabia,Irak, Abu Dhabi,Kuwait,Libya na
Algeria, ama wamepinduliwa na kufumbwa midomo, ama wamewekwa mfukoni,waachane
na misimamo mikali ya Waarabu.
Unajua sasa,ni kwanini Iran, Syria,Yemen,Misri
na wenzao wamefanyiwa ‘ukarabati’kwa kisingizio cha Demokrasia na Haki za
Binadamu,wengine watauawa tu.
Angalia uhusiano wa Paka na Panya kati ya
Urusi ya kale(USSR)na Marekani,Venezuela ya kichwa maji Hugo
Chavez,Nigeria,Uingereza, Indonesia,China, Mexico ya madawa ya kulevya na
Ecuador. Hizi ni nchi za mafuta.
Maskini,
Yoweri Kaguta Museveni, nchi yake itakapofika katika kilele cha uzalishaji wa
mafuta, na akawagomea wakubwa hawa,utawala wake utakuwa hatarini
maradufu,kuliko sasa polisi wanapowatomasa wanawake matiti,wakubwa
wamemnyamazia tu.
Wee washikie wakubwa bango la mafuta,utakiona
cha mtema kuni.Marekani na washirika wake wa NATO ni ‘rafiki maslahi’ na
aslani, hawana udugu na mtu masikini; hawafiki Somalia wala Syria,kama hakuna
almasi,dhahabu,gesi ya kutosha na mafuta.
Unapokuja mzozo wa Waarabu na Israeli,
Marekani na wenzake hujidai hawaoni uvunjaji wa sheria Israeli maana kuna
kanchi kadogo ka mchanga mtupu-wanakodolea jicho nchi za Waarabu,kuna mafuta
chini ya ardhi.
Mwezi Feburuari, tarehe 21 mwaka
huu,niliandika katika safu hii kwamba hata Vatican City,Makao Makuu ya Kanisa
Katoliki walishakubaliana na Israeli uhusiano wa Kibalozi. Ilikuwa Desemba 30
mwaka 1993.
Gidion M. alikuja na jina la makubaliano hayo
kuwa ni ‘FUNDAMENTAL AGREEMENT’lengo ni kufungua mazungumzo zaidi kati ya
Mayahudi hawa na Kanisa Katoliki,lengo ni kukomesha ‘kiherehere’ cha Mwarabu.
Vatican wanapoungana Marekani,Israeli na Ulaya
iliyokuwa dola ya Rumi wakiungana pamoja na Israeli,maana yake ni kwamba
Ulimwengu wa Kiarabu utasimama peke yao?
Wengine
wanasema Urusi na China. Hawa nao ni wafanyabiashara wa mafuta tu-wanapopewa
zabuni ya faida kubwa Mwarabu akipigwa kinyama,watakataa? Usiseme Syria,hakuna
unono kama Iran bwana!
Mwarabu yuko hatarini,kutekwa na kubinywa
katika dini yake,utamaduni wake na uchumo wake uliomo katika mapipa ya mafuta
ghafi.
Mzungu anapata ushindi mnono katika medani za
kijeshi na siasa, ‘bao la kisigino’ linafungwa,wakati Waarabu hawako tena
pamoja,wamefungwa OPEC.
Unabii wa Ufunuo 9 ulishatimia zamani.
Kwamba,nguvu za wanamgambo wa Kiarabu zilizoitesa Ulaya miezi mitano ya
kiunabii(miaka 150) hazipo tena Tazama Ufunuo 9:1-11.
Ottoman Empire haipo, Istanbul siyo tena mji
wa Waarabu,ni mali ya Mzungu, adui wa Mwarabu,ndiyo maana Uturuki na Syria ni mahasimu tu.
Kulingana na Unabii wa kitabu cha Ufunuo
13,Ulaya na Marekani zitapata ushindi dhidi ya dola za Mashariki,na wataunda
Umoja na serikali yenye kuwabagua watu wasiowapigia magoti, watawafanya kama
Sadaam, Osama ama Gaddafi, watu watafungwa maisha kama Carlos The Jackal,
wengine watawekewa vikwazo vya uchumi(Tazama Ufunuo 13:15).
Umoja wa
Mataifa(UN) ullishashindwa kutoa maamuzi ya haki uwanjani-Marekani,Israeli na
Ulaya wanacheza ‘rafu’ sana lakini hakuna hata mwamuzi wa pembeni kunyanyua
kibendera! Hujipendi?!
Hii ni
AJENDA YA SIRI.Al-qaeda,al-Shabaab,Black SEPTEMBER na magaidi wa Kiarabu mwisho
wa siku watatokomezwa na vikosi hivi vya CIA,FBI,MI5,MI6,MOSSAD na hata KFB la
Urusi likijai kuwasaidia Iran,litauza siri Tel Aviv ama Pentagon.
Asilimia 80
ya Waisraeli wanaabudu dini ya Kiyahudi na asilimia 15 ndiyo Waislam wa madhehebu ya
SUNNI.
Israeli ina
watu milioni nane na ardhi ni finyu. Ilijitangazia uhuru Mei 14 mwaka 1948
katika uadui mkali dhidi ya jirani zake Misri,Jodan,Syria,Irak na Saudia.
Jerusalem
ilishagawanywa Mashariki na Magharibi, na hapa ndiyo kitovu cha uadui na vita.
Vita vilivyokuja kupiganwa hadi Rntebbe Julai 3,mwaka 1976 ili kuwakomboa
mateka 103 wa Israeli,tumewaona makomandoo 100 walioandaliwa vema na Mossad
wakimkomesha Mwarabu na rafiki yao Amin Dada.
Naam, vita
vya dakika 90 tu, The 90 minutes at
Entebbe. Kwa Israeli, Waziri Mkuu anayekuliana na Waarabu ili kuleta
amani anauliwa kama Yizak Rabin aliyepigwa risasi Novemba 4 mwaka 1995.
Itaendelea
0786 324 074
No comments:
Post a Comment