ASKOFU SENTAMU WA UGANDA
TUKIIDURUSU
Historia, tunawaona wanamapinduzi wengi waliowahi kuteswa,kuumizwa na kuuliwa
kwa sababu ya kuushikilia ukweli.
Naam, Mahatma
Gandhi,Socrates, Nelson Mandela alifungwa miaka 27 akaja kuachwa huru Feburuali
11 mwaka 1990, Martin Luther wa Ujerumani, Martin Luther King Junior wa
Marekani, orodha ni ndefu kupindukia.
Wapo
mashujaa wengi waliojitoa mhanga maisha yao ili kuusema ukweli,wakaishia
kuuliwa mithili ya wasaliti na maadui. Aghalabu, hatuuelewi ukweli kirahisi.
Ukweli umesitirika sirini.
‘Kuelewa’
kwa lugha ya Kigiriki ni “Ginesko” yaani kufahamu,kupata maarifa, yaani kupata
maarifa ya kweli,ili kujua ama kufahamu.
Kufahamu kweli ni kitu kimoja; na kuufahamu
ukweli na kuupenda ili kuutumia katika maisha ya kila siku,kila wakati ni kitu
kingine cha muhimu sana.
Hata hivyo,
mashujaa wengi wa ukweli wameadhibiwa mithili ya wahalifu. Kusema na kuishi
kulingana na ukweli ni kufanya makosa ya ukweli-Crimes of Truth.
Mwaka jana,
nilikuwa nikijaribu kusoma Gazeti la Uganda liitwalo, “KAMUNYE” maana yake,
DALADALA. Hizi Daladala ambazo huku kwetu tunaita Vifodi(Arusha), Mwanza
wanaita Express n.k
Gazeti hilo,
Daladala ama Kamunye,la Ijumaa,Julai 29 mwaka 2011,liliandika habari ya dini
inayobatiza wanawake wakiwa uchi wa mnyama huko Uganda.
Gazeti
hilo,huandika kwa lugha ya Kiganda, kichwa kikubwa cha habari cha kushangaza:
“KIKA!”niliambiwa, “Kika!” ni neon ambalo halina tofauti kubwa na lile la
Wajitta waishio tarafa ya Nyanja,huko Musoma vijijini, “Echika!” yaani kituko
kikubwa mno,maajabu makubwa n.k
Halafu,
liaandika kwa lugha ya Kiganda, “Eddiini eyambula abakazi okubabatiza esonze!”
Vichwa vidogo vya habari hiyo (sub
headings) vilisema,”Abasajja basudde amaka okugyesogga!”
Nikaambiwa na mtu aliyekuwa mhariri wa Jarida
letu la Kanda ya Ziwa, The Lake Zone Today, Mukoche Sando Michael, raia wa
Tanzania mwenye asili ya Uganda,kwamba gazeti hilo Daladala liliandika habari
ya mchungaji mwanaume huko Uganda kuwabatiza wanawake warembo sana wanapokuwa
uchi wa mnyama.
Mchungaji
anayebatiza wanawake hawa wanapokuwa uchi huko mtoni,kichakani ni mwanaume
rijali.Sasa, ukitaka uchukiwe, ama pengine uuawe. Nenda kawaonye wanawake
wanaokwenda kubatizwa mtoni na wanaume wawapo uchi wa mnyama!
Naam, nakusudia kuandika juu ya makosa ya
ukweli- The Crimes of Truth. Nakusudia
kuandika juu ya watu wasiopenda ukweli wasije wakakosa chumo la udhalimu.Hapa
duniani zipo dini nyingi za kihuni. Dini za uchi, ambazo watu husali wakiwa
uchi wa mnyama,nyakati za usiku wa manane,taa zinapokuwa zimezimwa kabisa!!
Hata maskofu
na wachungaji wa dini hizi hudai wanafundisha KWELI ya neon la Mungu, kwamba
dini ni kama DALADALA ya kuwapeleka abiria mahali sahihi waendapo. Kwamba,
duniani hapawezi kuwepo na DALADALA moja, dini moja,mlango mmoja na njia moja
ya kuendea kwa Mungu n.k.
Naam, DALADALA.Demokrasia ina ‘tamu-chungu’
zake,na ndiyo maana kuna CCM.Chadema, CUF, ADC n.k Kuna Mungu,miungu, Ibilisi,
majini,misambwa, ‘tree spirits’ miungu ya voodoo n.k
Biblia,
katika Injili ya Yohana 8:32 husema, KWELI ya NENO LA MUNGU ambayo mtu
akiifahamu basi huwekwa HURU. Kwa Kiingereza, Yohana 8:32 husema hivi:
“The truth
will set you free” ikiwa na maana kuwa KWELI YA NENO LA MUNGU itakufanya uwe
huru.Uhuru ni kinyume cha utumwa,mbinyo,vizuizi ama kitu cha kulemea moyo na
akili,kama vile mazoea mabaya, ‘Addictions’ n.k
Hata hivyo,
kulingana na Kamunye(DALADALA) kuna mungu bandia siku hizi anayewafanya
wachungaji wanaume kuwa HURU kuwabatiza hata mama zao na dada zao wanapokuwa
uchi wa mnyama huko mtoni. Ubatizo huu ni ule wa kuzamisha, “Baptizo”
majini,mtoni,baharini ama ziwani penye maji mengi. Na wanawake hubatizwa wakiwa
uchi wa mnyama.
Yohana 8:32
huleta mjadala mkali sana juu ya ukweli uwawekao watu huru kweli kweli. Uhuru
upi? Wa kubatizwa wewe mwanamama ukiwa uchi wa mnyama na mchungaji au kasisi
mwanaume rijali? Uhuru upi?
Wa kuachana
na tabia mbaya na mazoea ya hatari yanayolemea watu kama ulevi,uvutaji
sigara,uchawi,uadui,uchafu,ufisadi,unyama,uzinzi,uasherati n.k?
Naam,UHURU
katika muktadha tofauti. Uhuru katika miungu tofauti na DALADALA tofauto
tofauti za kusafiria kwenda malengo tofauti huku ukweli unapofichwa kwamba kuna
njia tofauti zenye lengo moja! DALADALA!
Tujadili
kidogo kuhusu manabii,mitume wa siku hizi, wachungaji,masheikh,maimam na
makasisi na maskofu kukosa ufahamu wa neon la kweli la Mungu wa KWELI hadi
wameupindua ukweli kichwa chini-miguu juu,sasa mwanaume anawabatiza akina mama
warembo wakiwa uchi wa mnyama, ili kuwapeleka mbinguni kwa DALADALA aina hiyo!
Maaskofu
wanaolewa na wanaume wenzao.
Rowan Williams(62)
Juzi,
nikisafiri kwa Daladala moja, kutoka Buzuruga hadi Kirumba jijini Mwanza,
Kondakta akaanza kulalamika kufuatia habari iliyokuwa ikitangazwa saa saba
mchana na Radio Sauti ya
Ujerumani(DW)kwamba uchanguzi wa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiingereza, Anglican,
utaweza kulimega kabisa kanisa hilo,kufuatia kuunga mkono ushoga.
Wagombea
katika nafasi hiyo inayoachwa wazi na Rowan Williams kufuatia kupindukia umri
wa miaka 70 ni Richard Chartres(65), Christopher Cocksworth(53) na Mganda John
SENTAMU(63),na JUSTIN WELBY
.Mmoja wao
jina lake Wazirio Mkuu wa Uingereza, David Cameron analiwasilishwa kwa Malkia
Elizabeth ili litangazwe kuwa ni Askofu Mkuu wa Canterbury, Haya yamefanyika Jumatano na
Alhamisi iliyopita.Tuyaache,yana wenyewe.
Askofu wa
Canterbury, Rowan Williams anaachia ngazi, sasa uchaguzi mwingine ulikuwa
ukifanyika wa askofu atakayechukua mikoba yake.Sasa huyu ‘Konda’ alikuwa
akilalamika kusikia kuna askofu Shoga wa kanisa hili, ni mwanaume aliyeolewa na
mwanaume mwingine-hii nayo ni Daladala nyingine!
Askofu
V.Gene Robinson(kulia) akiwa na “Buzi” lake
V.GENE ROBINSON
Mwandishi,Chief
Red Jacket,katika karne ya 19 alisema utata wa kumwabudu mungu aliyemwita, “THE
GREAT SPIRIT” utawachanganya watu wengi. Bahati mbaya sana, Waafrika wengi
tunapenda kuchaguliwa mungu wa kuabudu na hawa Wazungu.
Watu wa
kwanza kumwabudu Mungu wa kweli ni Waisraeli, akina Ibrahim naye alitokea Ur
ambako ni Irak, na siyo Uingereza au Marekani.
Nataka
kusema kwamba Mzungu alishaleta ‘Moto Mgeni’ katika ibada ya kweli kama
walivyofanya Korah,Dathan na Abiram wakamezwa na tetemeko la ardhi sambamba na
wenzao 250 waliowashabikia.
Kwa kifupi, DALADALA ni makala itakayojadili
kilichomo NYUMA YA PAZIA(Behind the scenes) ili tuone uchafu uliomo katika dini
hizi siku hizi,na zote ni DALADALA zinazojidai kuwasafirisha watu hadi kwa
Mungu,labda kwa mungu,miungu au Great spirit.
Tutajadili
faida na hasara za uhuru. Katika Daladala tutajadili uhuru na faida na hasara
za kuchagua jambo lolote kama vile Mike Ezra,raia wa Uganda wakati Fulani
kutaka kuinunua Klabu ya Leeds ya Premiership huko Uingereza kwa Pauni milioni
60 ambazo ni Dola za Marekani milioni 96. Ni uamuzi tu unaofuatia uhuru wa
uchaguzi.
Itaendelea
0713 324 074
No comments:
Post a Comment