Monday, October 1, 2012

DALADALA (2)



ARISTOTLE(384-322 BC) wa Ugiriki, aliwahi kusema hivi:

To say of what is that is not; or of what is not that it is-is FALSE. While, to say what of what is that it is and of what is not that is not, is TRUE!!
 ARISTOTLE
Aristotle, alikuwa akisema hivi: “Kusema namna jambo lisivyokuwa ni Uongo, wakati mtu anaposema jambo lilivyo ama namna kitu kisivyokuwa,wakati kweli hakiko hivyo, huu ni UKWELI.
Ukweli, unaweza kuongopa pindi nusu ukweli unapochanganywa na uongo. Ukweli ni nini basi?
Kulingana na wanafalsafa UKWELI ni mwafaka baina ya mambo halisi au matukio halisi na ule uhalisia wa mambo( Truth is agreement with facts and reality).
Hata hivyo, kulingana na Injili ya Yohana Mtakatifu, Neno la Mungu ndiyo KWELI yenye uwezo wa kuwapa watu UHURU.
UKWELI, ni ulinganifu baina ya kilichotendeka, ama kilichopo na uhalisia wa mambo(agreement with facts and reality).
Nikaeleza katika sehemu ya kwanza ya makala haya,DALADALA, kwamba neno, “KAMUNYE” maana yake ni DALADALA, ambacho ndicho kichwa cha makala yangu hii.
Dada yangu mmoja, raia wa Uganda,Mwalimu wa sekondari Jijini Mwanza, ameniambia, “KAMUNYE” ni ndege TAI ambaye nimepata kuandika wasifu wake katika makala zilizotangulia.
Daladala za jijini Kampala zimepata jina hilo, KAMUNYE kufuatia sifa za ndege huyu tai; kuruka mbali na juu zaidi kuliko ndege mwingine, na uwezo wa kuona mawindo kutokea umbali mrefu
Wakati mwingine tai hufananishwa na uwezo wa Mungu wa kuona na kujua mambo ya kila mahali ulimwenguni, OMNISCIENCE.
Twapaswa kuona mbali kama Kamunye, wakati tunapofanya bidii kutafakari baina ya ukweli na uongo.
Hata hivyo, zipo DALADALA nyingi katika nyanja tofauti za maisha yaliyochanganyika, baina ya raha na karaka,furaha na huzuni,tumaini na kukata tamaa na amani na kinyume chake.
Maishani,kuna mema na mabaya, faida na hasara, kufuatia chaguzi zetu za kuamua kukwea DALADALA tofauti tofauti.
Leo,tujadili kuhusu UHURU wa uchaguzi- FREEDOM OF CHOICE.Dictionary(kamusi0 ya Kiingereza husema neno, Freedom,(Uhuru)kama ifuatavyo:
Freedom is the state of being free; right or privilege of unlimited access”.
Tafsiri yangu: “Uhuru ni hali ya kuwa huria; ni haki au fursa ya kufika popote au kufanya chochote pasipo kizuizi”.
Kwa sababu hiyo, “Unlimited Access” iliyopiganiwa mwanzoni kabisa wa kuumbwa kwa Dunia,ni pale Ibilisi(Shetani) alipomwambia Hawa katika Bustani ya Edeni kwamba, Binadamu akipewa kujua,kufanya mambo yote-basi atakuwa kama Bwana Mungu(Tazama Mwanzo 3:5).
Mungu, ana “Unlimited Access” lakini kwa kuwa yeye ana nguvu zisizo kawaida ya wanadamu(OMNIPOTENT), hawezi kufanya mabaya. Mungu anayajua mabaya.lakini hana cha kumlazimisha kufanya mabaya-binadamu hawezi kujua baya na akaepuka kulifanya!
Tangu zama za Adamu na Hawa,kama mwaka wa 4004 BC) kumekuwa na harakati nyingi za wanadamu kusaka “Accessibility” Haki ya kupata au kuingia popote na kutenda chochote.
Katika sehemu iliyotangulia ya makala haya, DALADALA,tukajadili kidogo, “DALADALA” waliyokwea viongozi wa dini.Tukawaona wachungaji wanaume wakiwabatiza wanawake wakiwa uchi wa mnyama huko Uganda!
Walikuwa wakiwabatiza mahali penye maji mengi huko mtoni, ambamo waliwatosa au kuwazamisha majini, “Baptizo,” Kigiriki maana yake kuzamisha ambamo jina Baptism,lilitoholewa.
Naam, Uganda,ndiko mahali Kibwetere aliwachoma moto waumini wake 530 huko Kanungu; aliwapandisha “Daladala” ya kuendea peponi na kuzimuni kwa pamoja!
Leo, tutupie macho Daladala waliyokwea WANAHABARI.Naam, MEDIA!
Neno, MEDIA linamaanisha wingi wa neno MEDIUM ambamo limetokea neno,MASS M EDIA.
Nitasema ukweli mkali hata kama nitafanya KOSA LA UKWELI(The Crimes of Truth) kama Socrates,kama Martin Luther, Mahatma Gandhi n.k potelea mbali nichukiwe na wapenda kinyume cha ukweli. Naam, ukweli mchungu.
Medium” maana yake ni chombo cha kuzungumzia,kupitia kuwasiliana,hata baina ya waliohai na wafu na mizimu, majini,misambwa n.k
Hata Ibilisi alimtumia Nyoka kama “Medium” ili kuwasiliana na Hawa, kwa nia ya kumpotosha ili aasi maadili ya Mungu(Tazama Mwanzo 3:1-24)
Medium ni chombo cha mawasiliano(vingi huitwa Media) baina ya watu walio hai kwa waliohai au wafu kwa waliohai. Tunaposema wafu kuwasiliana na waliohai tuna maana, umizimu, Spiritualism.
Kwa bahati mbaya sana, watu huamini kila kinachozungumzwa,kuonekana na kusomwa na vyombo vya habari-media.
Hawajui, hata Ibilisi ana “Access” anazungumza kupitia vyombo vya habari pasipo kuzuiliwa na chochote kama tulivyoona mantiki ya 'accessibility”.
Misingi hiyo huitwa, Uhuru,Demokrasia na eti Haki za Binadamu,haki za kusema, Freedom of Expression!
Watu hawa hawajui, Vyombo vya Habari ni DALADALA ya kuendea pazuri au pabaya, na pengine pazuri na pabaya kwa pamoja!
Kuna watu hawatofautishi maoni, habari 'hard news' makala,tahariri n.k. Hawatofautishi maoni ya mtu anapohojiwa na habari iliyothibitishwa, “balanced story”.
Hawajui katika vyombo vya habari kuna 'Facts” mambo halisi yanayozungumzwa na ushahidi upo na “Fiction” hadithi za kutunga ili kuburudisha.Pengine habari hujaa porojo tu,propaganda,uchochezi na umbea.
Wanaokwea Daladala ya vyombo vya habari, wao huitwa, “audience”ambao wengi wao hawana habari kuwa Ibilisi naye ana ruhusa, “access” ya kutoa uchochezi wake, “SEDITION”, badala ya “TRUTH” ukweli wa mambo-tumeona makosa ya ukweli-The Crimes of Truth.
Kulingana na taaluma ya habari, “SEDITION” is a speech or action encouraging rebellion against the government”
Maneno au vitendo vya kuongoza watu kuasi mamlaka ya serikali. Hivi ndivyo isemavyo sheria hata ya Uingereza na Marekani. Kumbuka kuna sheria mbaya(Bad LAWS)na usiniambie kuzivunja wakati zipo bado hazijaondolewa!
Naam, kuna LIBEL-Taarifa zinazotangazwa katika vyombo vya habari kwa nia ya kuharibu/kuchafua heshima ya watu na kuwaharibia utu wao.
Kuna uhuru wa vyombo vya habari 'Medium” kimoja ama Media,vingi.Taaluma ya habari na weledi, Profession and Professionalism,husisitiza nia ya ku 'Ku- balance between freedom of the press with the rights of individuals to privacy and their good names”.
"Professional Attitude” ya mwandishi wa habari mwenye weledi,ni KUJENGA jamii bora. Siyo kubomoa.Siyo kuchochea na kuchafua watoto,hasa wasichana na wavulana.
Siku hizi vyombo vya habari hujenga au hubomoa? Majibu unayo wewe mwenyewe.Uandishi wa kitaaluma na weledi ni kuweka uwiano/ulinganifu/mizania kati ya uhuru wa vyombo vya habari na Haki za kila mtu,pamoja na kutoingilia uhuru wawatu na kuwaharibia majina yao mazuri katika jamii.
Uhuru wa habari huishia mahali haki za Binadamu zinapoanzia. Habari,maneno,picha za atu,vitu n.k lazima vifuate misingi ya usawa na haki.”Fairness” na usahihi,”Accuracy” na habari lazima kutokuegemea upande kwa nia ya kupedelea na ndiyo habari yenye 'Objectivity”.
Sasa tujiulize: Twasoma nini na kusikiliza na kutazama kitu gani? Vyombo vya habari vinajenga jamii au kuibomoa?
Vyombo vingi vinavyopendwa sana hubeba blah blah nyingi,vicheko na maneno ya matusi yasiyo haiba(hasa ya watangazaji wa kike ambao hujidai kuongelea puani) huku wakisimanga wenzao wazi wazi walionyang'anyana mibuzi huko mitaani!
Vyombo vya habari hususan baadhi ya redio, hutumika kuumbua, kutusi,kutukana,kupeleka mivuto ya ovyo na kupiga vijinyimbo dhaifu vya matusi na ngono tu,hakuna messege.
Lugha wanayotumia mbovu saka, “Hiko” badala ya 'hicho' masaa masita, badala ya saa sita n.k mradi ni kichefuchefu,kikwifukwifu,utumbo mtupu!
Vyombo vyenye blah blah hizi hubeba purchasing power kubwa,husikilizwa na wengi na kupigiwa mfano!!
Redio zenye kuelimisha,kuburudisha,kuonya,kukosoa,kuweka ajenda n.k zimeachwa na vijana-vipindi vya elimu havipendwi,ni miziki ya ovyo ya ngono tangu asubuhi hadi asubuhi, hadi wameacha vijana kufanya kazi- idleness,
ili kusikiliza vijiredio na simu za mkononi.
Picha za ngono zinaonyehwa magazetini na televisheni. Picha za ngono- pornography, hupendwa sana siku hizi kunako facebook,twitter,blogs n.k
Katika vyombo hivi kuna matangazo ya biashara,ya POMBE,SIGARA n.k hata inaonekana itakuwa ngumu sana kwa kizazi hiki kumpata mtu ambaye ni “Teetotaler”-havuti wala hanywi pombe!
Itaendelea
0713 324 074




No comments:

Post a Comment