Tuesday, October 16, 2012

DALADALA(4)



                                                 
Watu wanapojua ukweli kupitia vyombo vya habari,nchi itakuwa salama”,
Hii ni kauli ya Rais wa 16 wa Marekani, Abraham Lincoln,katika moja ya hotoba zake, mwaka 1864.
Abraham Lincoln, alikuwa akizungumzia umuhimu wa Demikrasia katika maendeleo ya Taifa.
Ni hoja ya  taifa kuwa na wananchi na viongozi wa kuzungumza ukweli,naam ukweli usio na chembechembe za uongo.
Hata hivyo, kauli hiyo ya Lincoln, “Let the people know the facts, and the country will be safe” ina maana tu pale wananchi wanapopewa habari sahihi za kuaminika na kutegemewa.
Factual and credible information,” ndizo habari zitakazoifanya nchi kama Tanzania iwe na amani.
Serikali kuficha ukweli katika jambo lolote baya au jema, kutaifanya nchi kukosa amani, na pia vyama vya siasa kupotosha habari kwa nia ya kuchochea umma, kutaifanya nchi kuingia katika dhahma.
Vyombo vya habari vinapowapa wananchi habari za uongo,zisizo za kweli, au zenye uongo na ukweli, habari zisizo aminika ,za uchochezi na propaganda za siasa,uchafu,picha mbaya za uchi na mambo ya kilevi-levi na uchafu mwingine,nchi haitakuwa salama.
Watu wanadhani nchi kuwa salama ni kutokuwepo vita-amani na utulivu-kumbe hata taifa la walafi,wabinafsi na walevi kupindukia,mafisadi wa kimwili na kiroho,wanaonyang’anyana wanawake na kuuana, halina amani tena aslani!
Ndicho tunachoshuhudia leo hata hapa Tanzania,nchi haiko salama, kama alivyosema Abraham Lincoln,kwa sababu vyombo vya habari vilishashindwa kuwapa wananchi habari za kuwajengea amani na usalama myoyoni mwao na miilini mwao. Nchi iko vitani,katika siasa,mmomonyoko wa maadili,chuki,uadui,visasi ni vingi n.k
Vyombo vya habari vinapoacha kuegemea upande mmoja, ndipo huwahudumia wananchi,mithili ya mbwa anavyolinda mali ya bwana wake.
 Hili jukumu la ulinzi- ‘WATCHDOG ROLE’ dhidi ya serikali, uovu na waovu,wala rushwa,majambazi,waliolewa gongo na madaraka kwa pamoja,na mmomonyoko wa maadili,kwa maslahi ya taifa.Walevi wa gongo ni afadhali kuliko walevi wa madaraka.
Wakati fulani, Mwandishi wa chombo kimoja nchini Cameron, akaandika habari juu ya mgodi mmoja wa madini ya thamani kubwa kwenda kinyume na taratibu na sheria za uwekezaji.
Mhariri alipoipata ‘stori’ ile mezani kwake, akaupigia simu uongozi wa mgodi ule kuueleza kwamba kulikuwa na stori/habari ya mgodi huo kuharibu maslahi ya nchi mezani kwake! Akadai wakutane waongee,la sivyo ile stori ilikuwa inawa ‘maliza kabisa’. Mwandishi alikuwa ‘kawalima’.
Je, hayo ndiyo maadili?
 Uongozi wa mgodi ukamtumia mhariri tiketi ya ndege kwenda na kurudi,kisha ukampa vijizawadi-Payola- ili hali ya hewa isichafuliwe na ile stori ya ‘waandishi wa mikoani’.
Mhariri, aliporejea katika dawati lake, baada ya safari ya mgodini, ile habari ikatupwa kabisa kapuni-haikutolewa tena! Mwandishi hana ruhusa kuhoji stori yake ilikofia, eti ni kinyume cha maadili.
 Bila shaka, msomaji umepata kuona,kutazama ama kusikia kwamba migodi hutiririsha maji yenye kemikali za sumu zinazosababisha kuharibu vyanzo vya maji na pengine kusababisha vifo vya watu ,wanyama na mimea?
Mnadhani, waandishi wa habari hawajui mambo hayo?
Kwanini uhalifu mkubwa hautangazwi? Hautangazwi kwa sababu aidha mwandishi kajichokea kuandika stori, ‘Boss’ akiipata anavuta mkwanja! Au naye kachukua chake mapema tu!
Mwandishi, kiatu kinaishia upande bure kutafuta stori, ambayo haitoki, Mhariri atavuta Bahasha ya khaki, yeye asalie ‘Fala’ hata hayo malipo yake njiwa bado halipwi hata mwaka mzima upite, au asilipwe kabisa daima dawamu, na bado anaaulizwa na ‘Editor’… “Haloo, huko Mwanza hakuna samaki?”
Ala, umeingizwa mkenge,halafu utume samaki kwa ndege, ili stori itoke! Na akina mama wanaombwa rushwa ya ngono, la sivyo stori haitoki! Mimi sikubali utumwa huu,-ni kichwa maji.Tuungane kupinga unyama huu.
Waaandishi ni sawa na ‘makonda’ au manamba wasiofaidika na chochote katika DALADALA inayoitwa vyombo vya habari. Nimesema ukweli mchungu. Haidhuru nitakuwa mkosaji wa KOSA LA UKWELI-The Crimes of Truth!!
Huu ndiyo ukweli unaotendwa na  baadhi ya wakuu wa tasnia ya habari hata TANZANIA hapa,kuna vyombo vichache vyenye kujiheshimu na TAZAMA ni mfano mzuri wa kutonyanyasa wanahabari.
Pengine, nimedhulumiwa mamilioni ya shilingi na hawa madereva wa ‘Daladala’!!Wao wanakula mimi nakonda.Shime Yehoha.
        SIASA
John Fitzgerald Kennedy, maarufu sana kama   Mr. “J.F” alisema wanasiasa kazi yao ni ‘assumptions’ na mambo ya kukisia tu  kutoka vyombo vya habari,na umbea,ndiyo hufanyia kazi.Siasa za nchi hizi hutegemea kinachoandikwa kwenye vyombo vya habari.
Sasa jisaili. Katika mazingira kama haya ambayo mhariri anapanda ndege kwenda ‘kuvuta mkwanja’ kufuatia stori iliyoletwa mezani kwake na mwandishi wa mikoani,ili isichapwe gazetini au isitolewe redioni au kwenye ‘kioo’, ndiyo uhuru wa habari sampuli gani mheshimiwa?
Hatimaye,ni tasnia hii watu kushindana kugombea vijibahasha na zawadi-Payola-kutoka kwa ‘ma- source of information’ wasomaji wanaishia kulishwa makombo,maana mbwa mlinzi-watchdog-kala fupa,kalala!
Eti uhuru wa habari; Uharo au uhuru!
Samahani mheshimiwa msomaji, siwezi kupaka rangi dhambi hii ya uchafu unaoitwa uhuru,sasa utasikia kelele nyingi mahali ambapo watu walipewa bahasha za khaki, watasingizia maslahi ya taifa kumbe ‘fix’ tu na ‘fiction’. “Fix” au “Fiction”?!
Vyombo vya habari hupiga kelele saa nyingine(Sometimes Yes, some times No!)utadhani wazalendo sana,kumbe wazalemdo wa matumbo yao.  Niko kazini,nisamehe unapojeruhiwa, ukipita karibu na kijiwe cha kazi.
Tuijadili kidogo Daladala ya SIASA.Siasa ni sayansi ya kuongoza nchi.Lakini…
Elizabeth Alexandra Mary, alikwea kiti cha enzi na kuwa Malkia wa Uingereza na mamlaka anuwai duniani,kama vile kuwa Mkuu wa dini ya Anglican,Jumuiya ya Madola, Commonwealth ,Feburuari 6,mwaka 1952.
Alikuwa nchini Kenya aliposikia habari za msiba wa babaye,King George VI.Alizaliwa Aprili 21,1926.            Alitawazwa kuwa Malkia wa Uingereza akiwa na umri wa miaka 26 tu,leo ni mzee sana. Malkia Victoria naye alitawala Uingereza kwa miaka 82.
Malkia huyu, ambaye akija huku tunaziba pumzi hadi apite, ameshuhudia mawaziri wakuu 12 wakija na kuondoka,akina Tony Blair na David Cameron wamezaliwa yeye akitawala huko Buckingham Palace.
Sasa tunaambiwa Demokrasia.Nataka msomaji aelewe mantiki hapa. Hiyo demokrasia wanayojidai kuijenga ni ipi, ikiwa Malkia huyu anawaburuza hao akina Blair na Cameron,tena wote wametokea dini yao ya Anglican(kasoro wachache sana)akitawala ‘RG’Mugabe wanasema ame ‘overstay’ na eti Mfalme wa Wafalme wa Afrika, Muammar al Qaddafi, alitawala mwaka 1969, aka overstay, kwa hiyo wakamuulia mbali ili kupisha demokrasia!
Ninyi mna malkia wenu, akitoka wanaingia wanaye na wajukuu, Gaddafi naye akiwa Mfalme wa Wafalme(King of African Kings) kuna ubaya gani?” Pilipili msiyokula yawawashiani?
Wengine hudhani mi- chizi! Ebu tazama ukweli. Demokrasia gani ipo Uingereza hata wajidai kupindua serikali za Afrika,kwamba watawala wake wame “over stay”?
Malkia aliyetawala mwaka 1952 na alizaliwa 1926 ana mzidi umri Mugabe, Gaddafi,na wenzao walioitwa, “Extra-Ordinary Dictators” wana tofauti gani?
Huyu anatawala hadi Canada, Austria inatetemeka,na nchi 54 za Commonwealth wanamtetemekea. Je huu siyo ukoloni? Udikteta unazidi huu wa kulambana miguu?
Mwaka 2007 huyu Malkia alikuja Kampala, Uganda kuhudhuria mkutano wa  Commonwealth, uitwao CHOGM, akina Mugabe wakasuswa kwamba wame ‘over stay’ wageni 425 walikuja kupiga goti kwa malkia. Hata sasa Uganda inagugumia kwa maumivu ya mkutano huo wa Chogm.
 Ni gavana mkuu wa kanisa la England,tuliona vimbwanga vya maaskofu kuolewa huko Hampshire, ndiye mkuu wa mataifa 54 yaliyowahi kutawaliwa na Uingereza,ni mkuu wa Normandy, Mann na Chifu mkuu wa visiwa vya Fiji.
 Ni mke wa Prince Phillip tangu 1947, wanaye wanne na wajukuu wanne wakifika hapo Dar hampumui mpaka waondoke, halafu  unasema Uingereza kuna demokrasia!
Kwanini  Diana alikufa? Ubaguzi wa rangi.
Nataka msomaji utambue kwamba vyombo vya habari siyo Masihi wa kuikomboa nchi katika lindi la matatizo yaliyopo. Hawa wanahabari wanaweza kulipwa fedha hata na Ibilisi, wakatangaza kwamba ndiye masihi.Sasa utaamini?
Wee angalia hata dawa feki, zikiwemo  Antiretroviral, zinatangazwa kwamba ni Bora na kiboko! Saa,betri feki, simu, na hata dawa duni na feki za kuulia wadudu waharibifu wa mazao ya wakulima,hutangazwa redioni,magazetini na tv kwamba ndiyo bora kabisa!
Wajinga wanadanganywa kwamba demokrasia na siasa za mabwana wakubwa-Uingereza, Marekani na Ufaransa, hakuna wa kuhoji hata matumizi ya Buckingham Palace hulipa nani? Unajua aliyelipa gharama za harusi ya Prince William?
Angalia ‘AMRI 11 za hawa miungu ikiwemo ‘No Fly Zone’ iliyotangazwa na Hillary Clinton huko Tripoli, Jean Peing  wa Gabon,Yule Mkuu wa Kamisheni ya AU kanyamaza kimya!
Juzi walimtoa wakamweka mama Nkosazana Dlamini Zuma huko Addis, alikuwa kibaraka wa Wafaransa,walichosema akaufyata mithili ya kijibwa.
Hapa, masikini akisema katika vyombo vya habari, hasikiki.Mwenye bahasha za khaki, habari zake zitaandikwa popote, tajiri mtu maarufu wanasema ni ‘Prominent’ wanasema  “Big names makes news” ,halafu mkulima wa pamba akiibiwa uzani wa pamba,hii siyo habari ya kuuza gazeti,unaona?
Vyombo vya habari haviwatumikii masikini, unadanganyika,ni mali ya propaganda za matajiri na wenye mamlaka.
Hata bidhaa bandia hutangazwa kwamba ni safi zimetengenezwa mbinguni! Dawa za ukimwi bandia, wanasema ni bora kabisa Afrika na Ulaya!
Ibilisi anapewa ‘coverage’ kubwa kwenye media.Ngono,ulevi,uvunjaji wa sheria,mauaji ya kinyama kama ya ACP Liberatus Barlow n.k
Watu wengi hawatofautishi kati ya Hard News, Feature, Profiles, analyses ,editorials, opinion, barua za wasomaji nk vyote wanasema redio imetangaza! Pole.
Kila wanachosoma, wanaamini na kufanyia kazi. Blahblah na ahadi hewa za siasa,propaganda za Wamarekani na rafiki zao wao husema ni kweli.Wakisema Mungu kaja juzi yuko Kampala, wanaenda kutambikia!
Angalia,vyombo vya habari,huna soda,kebab,bia na bahasha za khaki,utaenda maelezo nani ataandika stori hiyo? Leo ni bahasha ndipo uandikwe-CHECK BOOK JOURNALISM- sasa utasema habari zinawahusu wananchi wakati ni wakubwa,matajiri na wanasiasa hata tapeli?
Wenye pesa ndiyo husikika, watu wazito, Prominence.
Kuna Daladala nyingi zinazowapleka watu upotevuni. Dini,vyombo vya habari,siasa,kote hakuna maadili. Maadili ni ‘Principles of Right conduct, determination of right and wrong’-s asa niambie wewe katika daladala nilizotaja kuna ‘Right Conduct”?
Kuna ukweli gani,haki ipi, code of ethics au code of conduct, ipi kama siyo kuimba mdomoni?
Haya ndiyo yanayoiua nchi yetu.Wanasema Maadili,mnayajua? Mnayafuata kwa kiwango gani? Mungu ndiye maadili, unamjua? Unafuata   amri zake?
 Itaendelea
0713 324 074







No comments:

Post a Comment