Monday, October 8, 2012

DALA DALA(3)



                              
Marekani, magazeti kama, Wall Street Journal, USA Today, Los Angeles Times, New York Daily Times, New York Times, Washington Post, New York Times, Tribune, Newsday n.k yanaongoza mauzo.
Huku kwetu Tanzania, jamii haipendi kusoma vitabu na magazeti yenye kuelimisha juu ya uchumi,ujasiliamali, elimu ama taaluma Fulani,kama kilimo bora n.k
Watu hupenda tetesi,picha zenye ladha mbaya(Bad taste),habari za kuvunjia watu heshima, zilizokolezwa na kuongezewa chumvi(exaggerated) ,uchochezi na mambo ya hihi-hivi tu,yasiyo na kichwa wala miguu,hushabikiwa sana.
Tovuti, blogs, face book, twitter zenye picha za kingono-ngono(pornography) hutembelewa na watuy wengi. Kamera za simu za mikononi siku hizi humfanya kila mtu kupiga picha bila hata kufuata taaluma, na kuzichapisha kwenye blogs,facebook n.k
Dhima, “Role” ya vyombo vya habari, “Kutaarifu/kuhabarisha,kuelimisha,kurekebisha jamii,kuburudisha,kukemea(to inform, to educate, to reform, to entertain, to incite) ilishatupwa na vyombo hivi siku nyingi.
Juma lililopita,tukagusia kuheshimu haki za watu,faragha zao(privacy),pasipo kisingizio kwamba eti wanahabari wana uhuru na kwamba kila kitu ni habari,hata kama mtu analalia jamvi. Jamii haina haja kujua kwamba mtu Fulani anaringa,lakini hulala penye jamvi!
Pana sheria zinazokataza vyombo vya habari kuchafua heshima za watu. “Libel” ni kosa linaloweza kuwa, ‘civil’ au ‘criminal offense’ .Kosa la madai au Jinai. Wanahabari wanategemewa kutangaza habari za kujenga na ziwe za kweli, sahihi na za kutegemewa na jamii,pasipo kuwa na upendeleo-habari zisiwe biased, ziwe ‘credible’ na ‘accurate’. Wanahabari hushauriwa kuchungulia katika pande zote za habari -checks and balances.
Tunataka jamii ipate habari ili iamue ifanye nini, na jamii ione mantiki na kuamua aidha kukubaliana au kutokubaliana.
Siku zetu hizi, DALADALA ya vyombo vya habari-MEDIA- inatumia haki ya kikatiba ya watu kujieleza- Freedom of expression, kuhukumu watu kwamba ni wezi,mafisadi na majambazi, na wengine kwamba ni miungu na malaika na mitume!
Vyombo vya habari vinalazimisha hata watu wote wafanye nini! Vimekuwa mgambo, mahakama,polisi, waendesha mashitaka,mahakimu na magereza kwa pamoja!!
Nakiri, vyombo vya habari ni muhimu sana katika taifa lolote, vina wajibu mtukufu kuifanya serikali ijitazame,ione makosa yake ili kujirekebisha,na watawaliwa wanapaswa kuhabarishwa ili waamue wao wenyewe nini cha kufanya.
Hata hivyo,vyombo vya habari vina jukumu mahsusi kuikosoa jamii ili ifuate sheria,taratibu siyo kuishia kuikosoa serikali tu na kuiacha jamii kuangamia kwenye majanga anuwai kama uchangudoa,ujinga,ukimwi,ugaidi n.k
Ukosoaji wa wanahari usiilenge tu serikali kutumia vibaya madaraka,’Abuses of power’ bali pia vyombo vyetu vitafute kuona yalipo maslahi ya taifa zima,na maslahi ya walio wengi.
 Tazama kauli hii:
“The Press is too quick to criticize authority, and does not support national interests”
Vyombo vya habari leo huishia kulalama na kuikosoa serikali, wakati vimesahau wajibu wa kuunga mkono maslahi ya taifa.Yako mengi, hata nchi inapoingia vitani, wanahabari hawapaswi kuunga mkono adui n.k
Kila mtu anajua sasa hatuna MAADILI,ndiyo maana maslahi ya taifa yanatupwa,na maslahi binafsi yanakumbatiwa na kila mtu,mimi hata wewe tukiwemo.
Nipewahi kuandika kwamba Maadili ni SHERIA ambayo kwa Kigiriki huitwa, “Nomos”, ama    ‘Torah’ kwa Kiebrania. Mana yake ni ‘Directions” maelekezo,mwongozo, “Guidance” utaratibu wa kufuata, ‘instructions’, ili watu wote waufuate kwa nia ya kuepuka makosa ama jambo Fulani muhali-baya.
Ni kutokana na Sheria, ‘Torah’ ama ‘Nomos’ tunapata uadilifu. Ikiwa watu watatii sheria na kuwa wanyoofu,tutakuwa na uadilifu. Kumbe, uadilifu hujenga unyoofu. Sheria za unyoofu(Moral Laws) ndiyo hasa maadili yanayolalamikiwa siku hizi kwamba yamepotea sana.
Ukweli ni kwamba, ‘Moral Laws’ ni AMRI 10 ZA MUNGU  ambazo ni kiwango bora cha maadili.
God’s legal standard for morality” kiasi hata vyombo vya habari hatuwezi kuzishika hizo amri 10 za Mungu, kwa sababu wengine hawaamini kama kweli yupo, au ana itawala dunia hii. Labda alishakufa n.k!
Waandishi wa habari wengine licha ya kutokubali kwamba Mungu yupo, wengine hawampendi,na hakuna juhudi za kuwahimiza kuzitii sheria zake zinazojenga maadili katika taifa lolote. Kwa sababu hiyo, hata vipindi vya dini havipendwi na vimepuuzwa sana.
Nataka kusema kwamba uhuru wa habari ni mzuri sana. Hata hivyo, uhuru wa kusema chochote na mwandishi yeyote, au kunakilicho chote kutoka kwa mtu yeyote kwamba ndiyo haki  za binadamu kwa mujibu wa katiba ya nchi(Freedom of expression), ndiyo mwanzo hata wa kutangaza habari za Ibilisi, za uchochezi, maneno mabaya,picha mbaya za kutisha(bad taste);tunapotosha hata watoto wadogo na kuwafunza uchafu,kwa kisingizio cha demokrasia.
Tumeona kwamba, Shetani alimtumia Nyoka kama “MEDIUM”Chombo chake cha mawasiliano kupeleka uchochezi kwa Adamu na Hawa ili wachukie SHERIA/MAADILI’TARATIBU/MWONGOZO/KANUNI kwamba ni vitu visivyotekelezeka; na kwamba mambo hayo yote hapo juu ni ukatili,udikteta na ubinafsi wa Mungu! Mwanzo 3:1-5.
Je, sisi vyombo vya habari na wanahabari katika nchi hii,siku hizi tunatumia demokrasia na uhuru  aliodai Ibilisi dhidi ya sheria za Mungu KUFANYA NINI?
Au ndiyo sababu tunapotosha watu makusudi?
Sisi Media, tumeamua kuwa njia ya Ibilisi kufundisha ajenda yake, ili kuwapotosha watoto,kuwafundisha maneno mabaya,ngono, matusi,kuvaa nguo za uchi,nyimbo za uchi,picha za ngono,uchafu mwingi usiosemeka!
Tazama televisheni nyingi uone michezo ya kuigiza ya uchi uchi,muziki wa ovyo wa wabwia unga na wavuta bangi, maneno machafu ya kingono,ulevi, uvuta bangi, umalaya, halafu tunapiga kelele za kijinga:
“Taifa linaangamia kwa kukosa maadili! Mafisadii!”
Nini chimbuko la mafisadi na walevi, wabwia unga, kama si vyombo vya habari kuwahusudu sana wavuta bangi,Malaya,machangudoa na majambazi na wauaji wa Marekani na Ulaya?
Mauaji ya kinyama watoto wameyaona kwenye televisheni,kwenye sinema, uchangudoa watoto wametazama kwenye twitter,facebook,blogs n.k maadamu siku hizi tumewanunuliwa vijisimu vingi vya China, vinawaharibu wawapo hata vitandani vyumbani mwao. Adui namaba moja wa Maadili ni vyombo vya habari!
Kimsingi,vyombo vya habari visipotumika vizuri,ni DALADALA inayopeleka kizazi hiki Jehanum ya moto; vyombo vya habari vinamsaidia SHETANI KUTANGAZA uhalifu kuliko vinavyotumika kuelimisha watu na kuwaondoa kwenye giza.
Kuna vipindi vingapi vya dini? Nani anafuatilia vipindi vya dini kwenye televisheni? Muda wa habari ukifika watu wana tune kwenye michezo,muziki na kwenye comedy!
Matangaza ya pombe,sigara huwavutia hata watoto kupeperusha moshi angani kama treni, na kusema maneno machafu ya mastaa wa Ulaya au wa hapa Bongo! Nguo za nusu uchi,mapenzi,ngono,filamu za mauaji,za ngono,michezo ya kiwenda wazimu,ukatili,uvuta bangi n.k ndiyo vipindi vinavyopendwa sana!
Vyombo vya habari-MEDIA-vinapeleka habari namna hii kwa watazamaji,wasikilizaji na wasomaji, wau wanaita, Mass Audience. Nakwamba vyombo vya habari ni kama kisu,kikitumika vibaya kitakata nyanya,vitunguu na nyama mekoni nawe utakula chakula bora na kitamu sana. Kikitumika vibaya hiki kisu utaua watu!
Shetani, ametumia MEDIA au kimoja MEDIUM tangu Edeni. Nyoka alitumika kama chombo cha habari kuwasilisha uchochezi kwa Hawa.
Sasa, angalia kama vyombo hivi vya habari vinatekeleza hiyo dhima, “Role” ya vyombo vya habari: To inform, to educate, to reform, to entertain, to incite and to set an agenda!
 Kuhabarisha,kufundisha, kurekebisha jamii,kuburudisha,kuonya na kuweka jukwaa la mjadala wa manufaa kwa jamii.
Je, msomaji, wewe redio yako,televisheni yako na magazeti yako yanakusaidia kwa haya na watoto wako wanafaidika?
Sisi wanahabari tujiulize,tunahabarisha nini? Tunawapa watu jukwaa la kusema nini kama siyo utumbo?
 Sikiliza hata vituo vya redio, utasikia Kiswahili cha ovyo sana, “Masaa masita!!” badala ya saa sita, “Hiko” badala ya Hiki kijiko au hichi kijiti!
Eti lisaa limoja! Kuna lisaa  limoja jamani? Kuna saa moja,basi, Uchafu gani huu? Sikiliza nyimbo zao sasa, wasela wanaimba huku wakishika sehemu zao za siri utadhani wanawashwa upupu! Eti ‘hiko kikombe!’
Eti burudani, utasikia mtangazaji anawachochea manazi wa Yanga au Simba kumdunda mwamuzi kwamba hayuko ‘Fair’ kabisa!
Hivi wewe mtangazaji au mchochezi? Unataka manazi wafanye nini kama unasema goli lilikuwa si halali mwamuzi kaiua timu yenu? ‘sisi moja-wao bila!!
Watangazaji hao wa siku hizi.Muziki wa matusi ya nguoni, taarabu za kusimangana na kuoneshana viuno, hata kwa watoto under age. Katika Biblia, katika Amosi 6:5 Mungu anasema, “Niondoleeni nyimbo zenu za upuuzi” wanaimba Nakupenda tangu asubuhi hadi usiku wa manane, hakua kingine!
Siku hizi,nyimbo kama “Kabwe rudi nyumbani ushirikiane nasi kulijenga taifa” hakuna, hakuna uzalendo wowote,ni ngono tu na viroba!
Hakuna vitabu,hakuna maktaba.Kila mtaa kuna baa,saloni na stoo bubu,hakuna maktaba wala watu kujisomea. Vitabu tunavyopenda ni vyenye mapaja manene ya akina mama na uchawi. Hakuna maarifa, magazeti ya ngonongono ndiyo yanayopendwa.
Sasa, tunasema vyombo vya habari Media ni mhimili wa Nne wa Dola.
Mwanahistoria wa Kiingereza,Thomas Babington Macaulay ndiye aliyeita Media kwamba ni “The Fourth Estate” kwa sababu, ni mithili ya mbwa mlinzi kwa jamii. Vyombo vya habari vina jukumu mahsusi kama mbwa mlinzi –Watchdog Role.
Mihimili mingine ya Dola ni Mahakama,Serikali na Bunge.Sasa vyombo vya habari vinafuata,lakini vinaongoza kuchafua maadili ya watu na vinachangia sana kuwaambia watu kutofauata sheria.Wewe unamnunulia mwanao toy  la bunduki, si unataka awe jambazi?
SHERIA hufunua Mungu na tabia njema aliyo nayo na utakatifu na usafi wake.Sheria ni nakala ya upendo wa Mungu,ni kiwango cha maadili bora,maadili yametupwa kwa sababu vyombo vya habari ni Daladala iliyowasomba wengi na kuwatupa shimoni.
Siku hizi kuna ‘Yellow Journalism’ ambamo kuna ‘cooked stories’ mtu ana kaa anatunga story na kuwagutua watu anaongeza chumvi habari, sensationalism, basi vijana wanaamua kubeba rungu na kufanya vurugu,hapo mwandishi anapata Lead story! ‘Kiama chatokea Mwanza,Arusha au Dar!!’
Watazame baadhi ya wahariri wa vyombo hivi, chungulia maisha yao nje ya ofisi,yanatia kinyaa,Siyo waadilifu.Wao na wakuu wao wa vyombo vya habari,wameshiriki sana kupora malipo ya waandshi wao wa mikoani, ambao sasa ni omba omba,wanaoingilia hata harusi za watu-trespassing- na kudai posho!!
Wakuu wa tasnia ya habari baadhi yao ni wa ajabu mno, wanakula mgongoni mwa wanahanari! Kuna maadili wapi na yapi kwenye tasnia ya habari,kama mwandishi anaomba nauli kila siku,ili kujinusuru maana hajalipwa malipo yake miaka mitatuMwandishi wa safu hii(wa kwanza kulia) akiwa na wenzake walipokuwa wakiendesha kipindi katika studio za televisheni ya Barmedas Jijini Mwanza
 Hapa ndiyo mwanzo wa kutegemea vijizawadi-Payola-kutoka kwa vyanzo vya habari zake ili apate kujikimu! Hapo unategemea habari gani,kama siyo watu kilishwa uongo na uchochezi,na blahblah tu.
Amini usiamini,vyombo vya habari ni DALADALA inayopeleka watu SHIMONI -shimo la Tewa, aliloimba Samba Mapangala.
0713 324 074










No comments:

Post a Comment