!
Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa,Ban Ki-Moon, ambaye ni raia wa Korea Kusini, hana ubavu wa
kusema ukweli kuhusu chimbuko la kitisho cha magaidi hapa Duniani.
Kama
hajipendi, anaweza kumfuata kuzimu Katibu Mkuu wa Pili wa Umoja wa
Mataifa,Dk.Darg Hjalmar Carl Hammarskjold wa Sweden!
KI-Moon,
anatoka nchi kibaraka wa Mataifa Makubwa ya Magharibi, ambayo yameigawa Dunia
katika mihimili miwili.
Ugaidi, ni
zao la chuki za zama za Vita Baridi,kufuatia Dunia kutengwa mafungu mawili.
Korea mbili
ni adui wakubwa,kufuatia kutengwa katika siasa za Kikomunisti na kibwanyenye.
Inakisiwa
kwamba,Warusi(Wakomunisti) walikuwa wakidhibiti maisha nchini Somalia tangu
mwaka 1968.
Walikusudia
kujitanua hadi nchi zote za Upembe wa Afrika(The Horn of Africa) ambazo ni
pamoja na Eritrea,Ethiopia, na Djibouti.
Kufuatia
hali hiyo,Rais Jimmy Carter wa Marekani alikuwa na wajibu kuzuia Warusi
kusambaza ushawishi wao Somalia,Ethiopia na mataifa ya jirani ya Kiarabu.
Urusi,ilikuwa
na vituo vya kijeshi(Military Bases) katika nchi hizi za Upembe wa Afrika,hadi
katika njia kuelekea Arabuni na Afghanistan na Pakistan.
Kwa
hiyo,Marekani ikawa na kazi ya kuondoa ushawishi na utawala wa Kisovieti(Soviet
Imperialism) katika Upembe wa Afrika.
Wakati huo,
CUBA na raia wake walitoa msaada mkubwa hapa Brani Afrika.Cuba ilikuwa “Mkono
Msaidizi” wa Dola kuu la Kisovieti(USSR).
Msomaji,
unaweza kutambua sasa kwamba nchi zote za Ulaya Masharikizilionekana kuangukia
zaidi siasa za mrengo wa kushoto wa Kambi ya Mashariki,na siasa zao za Ki-Marx
na Lenin.
Kwa sababu
hiyo,mataifa ya Ulaya Magharibi(ikiwemo Marekani) yalihaha kuhakikisha kuzuia
Ukomunisti usisambae mithili ya saratani hadi Upembe wa Afrika, na tuseme
Afrika nzima,na maslahi yao(ya kikoloni) yakawa hatarini!
Dola la
Kisovieti(USSR)linasemwa kuleta silaha nyingi eneo la Upembe wa Afrika,tena
nzito.Vita Baridi vilianza mara baada ya Vita vya Pili vya Dunia
kwisha,mwaka1945.
Baada ya
vita hivi vya Pili vya Dunia,Mataifa ya Mashariki yakiongozwa na Urusi(USSR)
nay a Magharibi yakiongozwa na Mrekani yaliamkakugombea udhibiti wa Mataifa ya
Ulimwengu wa Tatu,hususan Afrika,Asia na Amerika Kusini.
Kwa kuwa
Warusi hawawezi kushindana na Marekani na washirika wake kwa uchumi, wao
walianza kusambaza msaada wa silaha,magari ya deraya na ndege za kivita.
Hata Rais wa
Somalia,Muhammad Siad Barre, alipewa msaada wa zana za kivita na USSR. Somalia
ya sasa inayolaumiwa kuwafuga magaidi wa al-Shabaab,hutokana na mfuo wa
kikoloni wa Kiingereza na Italia,wakijidai kuunganisha taifa mwaka 1960.
Haya ni
mataifa mengine duniani yanayouza silaha nje kuliko nchi nyingine nyingi.
Wasomali ni
wahamaji(nomadic tribesmen) wasiokuwa na makao maalum zama hizo.
Hawakuwa na
rasilimali za kutosha,halafu uchumi wao haukuwa mzuri,kwa sababu ya kutokaa
eneo moja na kuzalisha mali.
Wakati
mwingine walitaka kuungana na Wasomali wenzao wa Ethiopia,Kenya na Djibouti.
Hivyo,ili
kutimiza azma yao walihitaji silaha tena kali.Ikulu ya Marekani(White House)
ilipokawia kuwafadhili bunduki,Ikulu ya Urusi(Kremlin) ikawapa bunduki kali
hawa Wasomali wanaosemwa kuwa ‘Wakali’ wanapoishi kuzunguka Bandari kuanzia
Mogadishu, hadi Ghuba ya Aden na Bahari ya Hindi.
Sasa utaona
Pwani BAHARI YA Hindi kuanzia Mogadishu,Pwani ya Djibouti,Aden,Yemen,Kenya na
Tanzania ni eneo hatari hata leo kwa maharamia wa Kisomali wenye bunduki za
rashasha za Kirusi.
Wamarekani
waliwahi kusema, ingawa Siad Barre alijidai kutumikia Warusi na falsafa za Marx na Lenin, mvuto wake ulielekea kwenye
Uislam.
‘Doctrines’
za Kirusi hazikufua dafu Somalia, ila bunduki zao walizipeda sana,
nazilipatikana kwa wingi;wakazitumia kwa njia yoyote kupatia chakula na
mahitaji mengine.
Inasemwa,Mfalme
Haile Selassie wa Ethiopia aliunga mkono siasa za Magharibi; akapinduliwa kwa
nguvu za jeshi kutoka Urusi,ili kundi la Wakomunisti washike nchi hii muhimu.
Habari hizi,
zikubaliwe au zikataliwe na ubongo wako,lakini tunapata picha halisi kwamba,
vita upembe huu wa Afrika(The Horn of Africa) yaani Somalia,Djibouti,Ethiopia
na Eritrea ni matokeo ya Ikulu mbili-Kremlin na White House-kunyukana eneo hili
tete hata leo,na matokeo yake wamezaliwa al-Shabaab wanaoua watu Kenya,Uganda
labda watakuja Tanzania siku si nyingi!
Mungu
apishilie mbali!!
Nani
adhibiti ushawishi wa eneo hilo,ndiyo shida inayoleta changamoto za visasi vya
magaidi hapa kwetu Afrika Mashariki.
Utawala wa
Mengistu Haile Mariam(Mkomunisti) baada ya Haile Selassie,ukasemwa na Magharibi
kwamba ulileta, “Terror” hofu kuu Ethiopia!
Neno hili,
“Terror” hofu.ukiliongezea “ism” unapata ‘TERRORISM’ maana yake Ugaidi.
Kwa hiyo
Kambi ya Magharibi inasema aliyeleta ugaidi eneo hilo ni Urusi. Na tukumbuke
Propaganda za Kimagharibi.Bila nguvu nyingine ya Magharibi kutaka kujitanua
huko,Urusi wasinge sogea.
Ni kwa
sababu hii, twapata picha kwamba chimbuko la ugaidi eneo hilo lote ni Madola
makubwa ya Marekani na Urusi kujitanua huko.
Wakati Urusi
inatawala mataifa haya kwa ‘remote’ White House hawakuchoka,wakawasaidia
wafuasi wao ndani ya nchi hizi fedha na bunduki,ili kukamata Ikulu ambayo
ingetawala Bandari za tangu Mogadishu,Djibouti,Aden, na Mlango Bahari wa
Shamu,YEMEN,kuelekea Pakistan na Afghanistan.
Sasa unaona
umuhimu wa kudhibiti eneo hilo la Bahari ya Hindi na Bandari hizo?
Bahari ya
Shamu, ambayo Waisraeli wa zama za Musa waliivuka kwa miguu bila boti,ni muhimu
sana kuunganisha Bahari za Hindi na Mediterranean.
MFEREJI WA
SUEZ,uliochimbwa na Wafaransa na Uingereza huko Misri ni muhimu eneo hilo ili
kuunganisha safari za meli kati ya Bahari za Mediterranean ,Shamu(Red Sea) na
Hindi.
Mto
Nile,unaoanzia Ziwa Nyanza na kutiririka umbali wa kilomita 6,900 unapita eneo
hilo pia.Huu ni mto ambao ni damu itiayo uhai nchini Misri(the life blood to
Egyptians), ni muhimu kusafirisha mafuta,bidhaa muhimu kwa uchumi wa
Ulaya,Mashariki ya Kati,ya Mbali na Amerika na Afrika.
Hili ni eneo
muhimu sana kiuchumi,ndiyo maana madola makubwa hupigana vikumbo kulikamata kwa
usalama wa nchi zao, au usalama wa uchumi wao.
Haya madola
makubwa-Urusi na Marekani- ndiyo waliochochea vita kati ya Somalia na
Ethiopia,kupigania Jimbo la Ogaden, eneo ambalo ni moja ya tano ya Ethiopia.
Ethiopia,Somalia
na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Yemen,hukodolewa macho na udenda na madola haya
makubwa ili kuweka ‘interests’ zao.
Mpango
mkubwa(master plan) wa mataifa makubwa ni kukamata eneo la Kusini mwa Afrika,
na Mataifa tajiri ya Mafuta katika Ghuba ya Arabia.
Chuki za Magharibi dhidi ya Fidel Alejandro
Castro Ruz, ni kufika Afrika kusaidiana na washirika wao Urusi,kukomesha
ukoloni wa Ulaya Magharibi huku Afrika Kusini.
Walikuja
hata kushawishi Somalia kugeukia siasa za Ki-Marx.Utaona hata Shirika la
Ujasusi la Marekani(CIA)likahaha kushawishi Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
jijini Dar es salaam mwaka 1964,ili Zanzibar sisjekuangukia Ukomunisti!
Rais Jimmy
Carter alitoa amri kwa Waziri wa Mambo ya Nje,Cyrus Vance,na Mshauri wake wa
Usalama wa Taifa,Zbignew Brzezinski,kuhakikisha(to move to every possible way)
yaani hata kwa ugaidi ama mabomu, alisema “to get Somalia to be our friend”.
Hii ni kauli
ya Jimmy Carter,ili SOMALIA iwe ‘rafiki’ yao tena kwa gharama yoyote!
Tazama kilichofanyika! Marekani chini ya
Shirika lake la Ujasusi,CIA wakaanza kuipa Somalia msaada wa silaha! Huo ni
mwaka 1977.
Ilisemwa eti ili ‘kujilinda’ ila wasitumie
silaha dhidi ya Djibouti na Kenya!
WAPI MAGAIDI
WANAPATA SILAHA ZA HATARI?
Sasa silaha
za West Gate zimetoka wapi?
‘Msaada’huo
wa silaha kutoka MAREKANI kwenda Mogadishu ,ulikuwa na masharti kwamba Marekani
isiwasaidie wanamgambo wa KISOMALI(Somali Liberation Front) huko Ogaden.
Msomaji
anapofikiri vizuri, aone kwamba Marekani inapotoa msaada hata kwa Waasi,huwa na
kwa sababu ya maslahi,vyama vya ukombozi navyo hunyimwa au kupewa msaada kwa
sababu ya maslahi.
Hawa
Wasomali wameishi Ogaden zaidi ya miaka 500
.Sasa
MAREKANI wanaibembeleza Somalia iwakate URUSI ili wao wasaidie Mradi wa
kukomboa Ogaden.
Unaanza kuona
Somalia inapigana na Ethiopia,Marekani wakiwa nyuma ya Somalia!
Urusi
inaleta MiG-21 Jets, vifaru vipya vya kisasa 400,Mi-8 ambazo ni helkopta za
kivita 30 na maelfu ya silaha kuizuia Marekani kulitawala eneo hilo.
Huku
nyuma,BBC,VoA,SKY NEWS.CNN n.k wanatangaza kwamba,Somalia na Ethiopia
wanapigana kwa sababu ya Ogaden!
Mbumbumbu wa
Tanzania wanasema,”Afrika Bara la Vita! Bara la Giza ,Magonjwa,na Machafuko!!”
Mabwana wa
Vita wa Afrika(war lords) wanabebwa na mataifa haya ya Ulaya,na huwezi kuyaona
mpaka uwe na macho matatu.
‘Satellites’
na ‘radar’ za Marekani za upelelezi zinategwa tangu Misri hadi
Pakistan,zinaletwa upambe huu wa Afrika ili kukoleza vita,ili Urusi wapigwe
waondoke!
Antonov-22
na Ilyushin-76 za Kirusi nazo zinajongea Upembe huo ili kubyesha mabomu makali
kupambana na Marekani aliyekificha nyuma ya pazia,mgongoni mwa Msomali,katika
vita baina ya Somalia na Ethiopia.
Yemen
inatumika kama ‘depots’ za silaha za Mrusi.
Cuba nao
wanaleta askari 15,000 toka Angola(Angola ilisaidiwa ikawa huru 1975) sasa CUBA
anajitoa mhanga kupambana bega kwa bega na Mrusi ili kumzuia Marekani kutwaa
Ogaden, mgongoni mwa Msomali!
General
Vasily Petrov wa Urusi anaongoza mapambano huku, akina Vance nao wanachochea
upande huu, basi Afrika inanuka riha ya baruti na risasi,kwa maslahi ya madola
ya Ulaya!
Somalia
inazidiwa,inaomba silaha Magharibi,vita ngumu Ogaden.
Shah wa
Iran(alikuwa Kibaraka wa Marekani) anaonywa asije akapeleka silaha yoyote
aliyopewa na Marekani katika nchi za Dunia ya Tatu,zisije zikatumika kumsaidia
Ethiopia na Warusi,vita ngumu hii bwana!
White House,
inatoa amri-hakuna kuuza silaha mEthiopia ili Ogaden itekwe na Msomali!
Ili Urafiki
wa Marekani na Msomali upatikane! Naam, maslahi ya mataifa makubwa hupatikana
kwa damu mbichi ya Mwafrika,Mwarabu,Mhindi ama Mhindi Mwekundu wa Bara la
Kusini mwa Marekani.
Viongozi wa
Kiarabu,tangu Sudan hadi Saudi Arabia wanaamrishwa na White House,kuisaidia
Somalia, msaada MUHIMU wa silaha(a significant military aid).
Lengo,ni ili
Ukomunisti ushindwe Afrika. Hawa akina Brzezinski walishatengeneza Ukimwi mwaka
huo wa 1975 ili kuwaua Waafrika,kuwapunguza ili wao wachukue mali kwa gharama
yoyote, sasa wako Somalia.
Wanapoona
Warusi na Wacuba wameingia wenyewe vitani,na vita vinamwelemea Msomali,wanaanza
kutangaza mikataba ya kusimamisha utengenezaji wa silaha!
Wanaita kwa
Kingereza, “Arms-limitation talks” ama Arms Limitation Treaty!
Sasa
wanasema Mrusi akiendelea kuwasaidia Wahabeshi, basi mazungumzo hayo ya
kupunguza silaha duniani yatakuwa hatarini kuvunjika!
Msomaji,sijui
unaona unafiki huu wa Marekani! Kumbuka hii siyo hadithi ya Paukwa Pakawa! Ni
ukweli kutokana na Historia.
Urafiki wa
Marekani na Somalia unakuja kwa njia ya kuchochea vita Ogaden,Cuba nao wanaleta
‘artillery’ na MiGs zinanyesha mabomu tani nyingi,Wasomali wanapigwa wanakimbia
nyuma milimani huko JIJIGA!
Damu ya
Wasomali inabubujika kama mto,mvua ya mabomu inaendelea,wanakatwa vipande
vipande kwa mabomu-maguruneti kwa uchochezi wa Kimarekani inayotaka kuikamata
Somalia kwa gharama yoyote.
Majeruhi
walikuwa maelfu.
Nataka ujue
ugaidi wa Somalia ulianza lini?
Kwa nini na kwa sababu gani?
Kumbuka,vita
baina ya Somalia na Ethiopia vimechochewa na Rais Jimmy Carter ili ajifanye
rafiki wa Somalia,kumzuia Mrusi kujitanua Upembe wa Afrika.
Hii kampeni iliitwa, ‘THE SOMALIA’S OGADEN CAMPAIGN’ unaweza
kufuatilia ujue ninachoandika hapa.Wajinga wanaposema,Wasomali wapenda vita!
Jiulizeni nani yuko nyuma yao?
Nani huwapa pesa na silaha? Ni Mwarabu?
Mchina? Mzungu!!
Wamarekani
wanapoona Msomali kachakazwa vikali,damu inavuja puani, wanaandika barua ya
rangi ya njano na nyeusi kusema!
“Serikali ya
Somalia itoe tamko, sisi(Marekani) tumeona katika vita hivyo vya Ogaden,kuna
mkono wa Mrusi”,Barua ilisema.
Sasa eti
ndiyo MAREKANI wanaona kwamba kuna Mrusi ameleta MiG-21 zipatazo 48, na kuna
marubani wa Cuba wako mstari wa mbele kuisaidia Ethiopia, vifaru 150 vimetoka
Msumbiji nchi nyingine ya siasa za Ki-Marx,sawa na Zimbabwe ya Robert Mugabe
ambaye wanamchukia sana.
Hadi Iran
kule ambako kuna mafuta ushawishi unaendelea wametoka akina Ahmadnejad,sasa
utawala unajipendekeza Marekani. Ni Urusi,Marekani!
Wacuba
wanafundisha Wayemen kutumia bunduki za Mrusi,akina Carlos The JACKAL
walifunzwa ugaidi na wa Cuba,Warusi ili kupambana na ubeberu wa
Kimarekani.Akina Osama walifundishwa ugaidi na Marekani ili kupambana na
Ukomunisti walipovamia Afghanistan mwaka 1979!
Muktadha wa
makala hii,ni ili msomaji ajue kwamba,Marekani na washirika wake huwa hawana ‘Clear Policy’ kuhusu BARA LA
AFRIKA.
White House
na Kremlin huchochea vita hapa Barani;hufunza wanamgambo eneo hili lote kuanzia
Somali,Urabuni,Bara Hindi hadi Pakistan na Afghanistan.
Hata Osama
Bin Laden, alitokana na makambi ya kigaidi yalifofadhiliwa na Marekani,lengo
likiwa kupambana na Urusi waliotaka kusimika Ukomunisti pindi walipovamia Kabul
mwaka 1979.
Wanamwaga
silaha na mabomu,wanachochea chuki;vita vinapouma wanaitana mkutanoni Ulaya ili
kuitisha “ARMS-LIMITATION TALKS”
Waziri kama
John Kerry anakwenda Moscow,inadaiwa wanajadili kumaliza vita,ama kuepusha vita
Syria,Misri,Libya,IRAK nk.
“Negotiations”
zinazofanywa na kutangazwa na vyombo vya habari vya Kimagharibi, si kitu bali
uongo na Propaganda.
Wanataka
kujitakasa dhidi ya lawama kwa kuwa vitanga vya mikono yao huchuruzika damu
mbichi za Waafrika,Waarabu,Wahindi ama raia wa Ulimwengu wa Tatu! Kila mahali
penye maslahi ya kisiasa na kiuchumi.
Vita ya
Madola Makubwa ni “To conquer The Third World” ama kuutawala Ulimwengu wa Tatu,wa
nchi changa,hasa zenye utajiri wa almasi,dhahabu,mafuta,gesi n.k
Wakiona
Waafrika mnapukutika kwa vita,damu inamwagika,Putin na Obama wanaitana Moscow
ama popote,wanakaa wanaambizana kupeana zabuni.
Wanaunda
ushirika wa kiuchumi, “economic co-operation’ mambo yanatulia!
Wanapigana
kwasababu ya maslahi ya uchumi na siasazao za kibabe.Watu mwingine Marekani
wakiona Putin ni kichwa –ngumu kuhusu maslahi yake,labda ya Syria ama Iran,
wanamwacha na kuungana na ‘Western Powers’ zingine ili kupambana dhidi ya
maslahi ya Urusi na washirika wake.
Dunia
ilikuwa imegawanyika katika kambi mbili za Mkataba wa Wasaw(Poland) na zile za
Mkataba wa Northern Atlantic Treaty Organization(NATO).
Syria haitengenezi
silaha za sumu;kuna super power hupeleka
silaha hizo Syria,lakini lawama haziendi kwa wenye viwanda,huangukia mtumiaji
wa silaha hizo za sumu-Biological and chemical weapons!
Usishangae,
Uingereza au Marekani wakawauzia Syria silaha hizo za maangamizi ili
wamalizane,iwe rahisi kuwakamata kama ilivyo Iraq,Misri na sasa Syria
watakapokuwa wamechoka kabisa.
Kuna kitu
kinaitwa, “Counter force against Soviet-bloc Intervention”.Wamarekani wanaweza
ku-train rebels- kuwapa mafuzo waasi mahali popote ili wakakamate Jimbo lenye
utajiri wa madini!
Sasa,vita
vikizuka watu wanaona wanaohasimiana ni wajinga sana! Kumbe ni biashara
inafanywa.
.Zaire ya
zamani kuna jambo hilo,siku hizi huitwa Congo,DRC.
Taarifa za
hivi karibuni husema,Katibu Mkuu wa Pili wa Umoja wa Mataifa,Dk.Dag
Hammarskjold wa Sweden,ndege yake iliangushwa kwa kombora wakati ikitua mjini
Ndola,Zambia. Huu ni ugaidi wa wazi dhidi ya Katibu Mkuu wa UN.
Ripoti za hivi
karibuni, husema Katibu Mkuu wa Pili wa Umoja wa Mataifa,Dk. Hammarskojold
aliyeshika wadhifa huo Mkuu wa UN mwaka 1953-61 alikuwa katika kinachoitwa,Peace
Mission huko Kongo, wakati DC-6 iliposhushwa kwa kombora kali, usiku wa Desemba
17 kuamkia 18,mwaka 1961 kilomita chache tu njiani kutoka Ndola Zambia.
Eneo
hilo,wakati huo lilitawaliwa Wazungu wa Rhodesia(Zimbabwe), hawakutaka Katibu
Mkuu huyo kukomesha vita vilivyowaletea faida ya madini ya Congo,zama hizo za
Patrice Lumumba.
Ripoti
husema,kilichofanya ndege ile kuanguka ni bomu.
Sababu kubwa
ni Wazungu:
Weupe wa
Rhodesia,Wabelgiji na Waingereza waliokuwa na migodi katika Jimbo lenye utajiri
wa Madini,Katanga, waliokuwa katika hali ya kutoelewana na Umoja wa Mataifa na
wanaharakati wa Kiafrika, wenye itikadi za kimapinduzi, African Nationalism.
M-23 ni
wanamgambo wa kuleta utajiri kutoka majimbo tajiri Kongo kwenda hata Ulaya na
Marekani.
Tawala zitaangukia kwa akina Kagame na
wenzake,wakati anayefaidika mno amejibanza nyuma ya pazia la unyama na
machafuko ya vita!
Wacuba,Walifundisha
Waasi,wakakamata Jimbo la Shaba lenye utajiri.Zaire iakaomba msaada
Ufaransa,Cuba wakaondoka.
Ukiuliza
Waasi au Magaidi hapa Afrika,unaambiwa kwa Kiingereza,
“We have the
men , just to give us the tools to fight!”
Wanasema
wana rafiki zao Ughaibuni(huwa hawawataji,ni siri sirini) wanawapa zana za vita
ili kupigana na serikali za Afrika,Asia ama
popote palipo na utajiri wa rasiliali.
Sasa,utauliza
al-Shabaab aa al-Qaeda wanapata wapi pesa za kununua silaha? Wanapata wapi pesa
za kulipa mishahara na gharama za vita?
Somalia,kuna
kiwanda cha kutengeneza SMG,AK-47 au maguruneti?
Akina Andrew
Young, wakati huo Balozi wa Marekani Umoja wa Mataifa,walishashindwa kuzuia
Urusi na Marekani kuivamia Afrika.
Kila mara “US
Troops” huja Afrika na meli na manowari za vita,huja na drones n.k nia yao ni
kujenga ‘military base’ za kuizuia Urusi na zana zake na ushawishi wake
kuitawala Afrika.
Marekani
ilianzisha al-Qaeda chini ya Osama ili kuwazuia Warusi Afghanistan mwaka 1979,
hupandikiza chuki, huleta silaha halafu tunaanza kudhani wabaya ni Waafrika?
Wasomali!Waarabu?Waislam?
Kabla ya
kuanza kulaumu Waafrika/Waarabu/Waislam na ugaidi WestgatE, Nairobi,tutafakari.
· Nani anamwaga silaha Afrika? Bila shaka
jibu ni Super Powers
· Nani anafunza wanamgambo mafunzo ya
kivita kama hawa al Shabaab walioleta majanga Nairobi,kasha kutokomea?
· Nani analeta chuki?Nani analipa
gharama za ugaidi?
Jawabu ni SUPER POWERS!
Tufanjeje?
Jibu ni Afrika itakapoamka na kukataa kutumiwa mithili ya
vinyangarika,ili nayo iwe SUPER POWER!
0786 324 074
No comments:
Post a Comment