NA CONGES MRAMBA
RAIS MSTAAFU
wa Afrika Kusini,Nelson Rolihlahla Madiba Mandela, aliwahi kumkemea George
Walker Bush wa Marekani kwamba aliivamia Irak mwaka 2003 ili kupora mafuta.
Madiba,
alisema Vita vya Ghuba vya miaka ya 1990 na 2003 vilikuwa vya kupora
mafuta.Mataifa makubwa ya Ulaya Magharibi, siku hizi hutumia silaha vitani ili
kukamata nishati muhimu kama mafuta,gesi,uranium n.k
Hii ni
kufuatia mataifa tajiri ya mafuta na gesi,hususan ya Kiarabu kukaribia kuukata
koo uchumi wa Mataifa hayo miaka ya 70.
Tangu Vita
vya Pili vya Dunia, mafuta yalipatikana tele na kwa bei poa kwa viwanda na ili
kusafirishia bidhaa za mataifa makubwa haya.
Mwaka 1973,
wakati ule wa vita huko Mashariki ya Kati,Waarabu wanaozalisha mafuta kwa
wingi, walipunguza uzalishaji na kuongeza bei ya nishati hiyo maradufu.
Ongezeko la
bei ya mafuta huko Mashariki ya Kati, ni kusababisha chumi za nchi za viwanda
kuanza kutetereka.
Ukitaka vita
mlangoni kwako,basi anzisha sera za kuzuia chumi za ‘Industrialized Nations’
kukua kwa ufanisi. Utasingiziwa ‘Gaidi’ ili upigwe kwa drones!
Nchi za
Kiarabu zilitangaza kuinyima nchi yoyote mafuta kwa kuwa inaisaidia Israeli(Adui
Mkuu wa Waarabu),kwa hali hiyo,Marekani,Ufaransa,Uingereza na washirika wao
wasingeuziwa mafuta na Mwarabu.
Kwa mara ya
kwanza mwaka 1973,Mwarabu alitumia nishati ya mafuta kama “SILAHA MUHIMU”
katika siasa za kimataifa.
Nchi
wazalishaji na wasafirishaji wa mafuta(OPEC) walikubaliana kupunguza uzalishaji
wa mafuta,kasha wakaongeza bei ya nishati hiyo muhimu kwauchumi wa dunia.
OPEC
walikubaliana kulinda na kutunza akiba yao ya mafuta,ili kuwatoa kamasi
Wazungu!
Bei ya
mafuta ikapaa;mgogoro mkubwa wa mafuta,maarufu kama, “THE OIL CRISIS” ukatikisa
viwanda vya mabwanyenye,uzalishaji ukashuka maradufu.
Mfumuko wa
bei(Inflation) ulikita;viwanda vingine vikafungwa na kusababisha ukosefu wa
ajira ulioikumba dunia.
Mwaka 1979
Mfumuko wa Bei ulipanda kwa asilimia 334 kuanzia takwimu za mwaka 1969.
Hii ni
kusema, bidhaa iliyouzwa kwa Pauni moja ya Kiingereza mwaka huo 1969,sasa
ikauzwa kwa Pauni 3.34. Hali hiyo ilifuatia Waarabu kuzuia mafuta yao kuuzwa
Ulaya-ARAB OIL EMBARGO-mwaka 1973,kukaleta kiama cha kutisha kwa
Marekani,Uingereza, Ufaransa na rafiki zao.
Mfumuko wa
bei(Inflation) usiosemeka ulisababisha bei zikapanda kila kulipokucha,fedha
zilikosa thamani mfululizo.
Nataka
nikwambie msomaji.Ikiwa ili upate nishati ya kupikia chakula chako(kuni,mkaa,mafuta,gesi
n.k) ingekugharimu fedha zinazojaa magunia matatu ya noti za elfu kumi-kumi!
Kwa nini
usitumie magunia mawili ya noti zenyewe kama kuni ili kupikia chakula
chako,kuliko kununua mafuta au kuni kwa magunia matatu ya noti?
Kwenye
mfumuko wa bei noti huwa hazina thamani kwa kiwango hiki! Italia,mfumuko wa bei
ulifika asilimia 319,Japan(236%),Ufaransa(234%),Marekani(196%) n.k
Nimesema, chanzo
kilikuwa ‘reduced supply’ kukaja kuzaliwa shida nyingine ya kitu kinaitwa, “recession”,
biashara ikasinyaa,hata bidhaa hazikuzalishwa tena viwandani-sababu ya kiburi
cha Mwarabu!!
Hata Urusi
haikuwa salama;Afrika nayo iligugumia maumivu ya kupanda kwa gharama kufuatia
kupanda bei ya mafuta soko la dunia.Kununua bidhaa soko la dunia kuligharimu
bei mbaya wakati huo wa miaka ya 70.
Hali hii
ilifanya mataifa ya KIARABU kutajirika maradufu,Waarabu wakawa wanakula maisha
sana hata huko Ulaya.Marekani pamoja na kuwa na mafuta yake yenyewe,ikakumbwa
na kilio kikuu cha ukosefu wa mafuta.
Marekani
hutumia mafuta mengi kuliko nchi yoyote hapa Duniani.
Kufuatia
hali hiyo,Marekani ilikaribia kutembelea magoti na kukoma kuwa “economic strong
man”.
Nakumbuka,
Katuni moja iliyochorwa na Wadachi mwaka 1973,Mwarabu akiwa amewaweka CHINI YA
ULINZI viongozi wanne wa Dunia:
Kansela
Willy Brandt wa Ujerumani,Rais Georges Pompidou wa Ufaransa,Rais Richard Nixon
wa Marekani na Waziri Mkuu,Edward Heath wa Uingereza.
Hawa
walionekana kwenye katuni wakiwa wamewekwa chini ya Ulinzi na Mwarabu kwa
kutumia ‘Pampu’tu ya mafuta, siyo bunduki wala guruneti!
Walishikiliwa
hadi Mzungu alipe kikombozi(ransom) ndipo waachiliwe huru.
Zama hizo,
Saudi Arabia,Irak,Iran,KUWAIT,Libya,Abu Dhabi,Algeria n.k zikapata heshima
mbele ya mabeberu.Nchi nyingine kama Nigeria,Guinea ya IKWETA,Venezuela,Indonesia,Ecuador,Angola
n.k zingeweza kuwa na kiburi cha kuyagomea mataifa haya kwa kutumia mafuta kama
silaha.
Norway,Mexico
na Uingereza walihaha kusaka vyanzo vipya vya mafuta.Mwaka 1979 kulikuwa na
uhaba wa mapipa milioni 2.3 kila siku.
Ni hapa
Mwarabu alipotikisa ndevu za Mzungu, hususan Marekani ambayo kwa siku moja
hutumia theluthi ya mafuta yoote yanayotumiwa na dunia nzima.
Huu ndiyo
wakati Mohammed Reza(Shah) wa Iran alipouza mafuta yote Marekani na kuiacha nchi
yake ikiwa kavu kabisa!
Itaendelea
0713 324 074
No comments:
Post a Comment