Thursday, March 29, 2012

unataka utajiri?


                                                         
                                                          *Lazima kulamba dole gumba la Freemasons
                                                          *Ziara ya Papa Benedict XVI  imezika Ukomunisti Cuba
SHETANI, akampandisha Yesu katika kilele cha Mlima, akamwonesha MILKI zote za Ulimwengu kwa muda wa dakika moja tu.
Akamwambia: “Nitakupa wewe enzi yote hii na fahari yake,kwa kuwa imo mikononi mwangu; name humpa yeyote kadiri nipendavyo. Basi, wewe(Yesu) ukinisujudia tu, vyote vitakuwa vyako”, alisema Ibilisi, Luka 4:5-6.
Naam, kifungu hiki ambacho ni nukuu kutoka kwa Shetani,hudai kuwa Enzi na Milki zote Ulimwenguni,fahari yake yote,vimwana warembo walioacha sehemu ya miili yao ya tashtiti nje-nje, rasilimali muhimu kama mafuta, madini ya thamani,gesi,miji mikubwa yenye majengo ya fahari,ndege,meli za fahari kupita Titanic n.k viko mikononi mwake.
 Akitaka, humpa yeyote kwa kadiri apendavyo. Isipokuwa, shatri ni moja,dogo,lakini matokeo yake huathiri maisha-KUSUJUDU MBELE ZA SHETANI-kumsujudia Ibilisi na rafiki zake,Freemasons,Illuminati, viongozi wakuu duniani,mawakala wa  waganga na wachawi n.k
Nimetumia kifungu cha Luka 4:5-6 ili kumwonesha msomaji kwamba, enzi,mamlaka,utajiri na fahari zake zote, vimo mikononi mwa Ibilii na hao rafiki zake na mawakala wake. Na humgawia kila ampendaye. Usianze kunisumbua kuniuliza namba ya kiganjani ya Shetani…mimi sina! Wengine hunisumbua kwa SMS kuniomba namba za Freemasons, sina na sijui!!
  Turejee milki ya Rumi ya kale. Mji mkuu wa Dola hii yenye nguvu na utukufu mwingi duniani,ulikuwa Rome. Siku hizi ni mji mkuu wa Italia. Biblia,iliutaja Rome wa kale kama Makao Makuu ya Shetani(Ufunuo 2:13).
  Jiji hili,lilijengwa yapata takriban Milenia tatu zilizopita. Rome ulikuwa Makao Makuu ya UCHUMI wa Dunia ya wakati huo. Kila mkazi wa dunia,alitamani kuwa na uhusiano mzuri na Rome,ili kupata mafanikio.
 Nataka kusema kwamba, kama Rome ulikuwa “centre of economic Life of the ancient World”, maana yake ni kwamba, mmiliki wake na mwenye mamlaka na uchumi-IBILISI-aliishi jijini Rome, amini usiamini.
 Kulikuwa na wakazi lukuki jijini Rome,kwa kuwa kilikuwa kituo kikuu cha biashara duniani.
Dola hii ya Rumi ilipokuwa ikishambulia mataifa mengine na kuteka nyara nyingi na mali za kutosha, vyote vilileta neema kwa wakazi wa Rome, hadi wakaishi maisha saafi sana!
 Inakisiwa, kulikuwa na watumwa 650,000 jijini humo katika mwaka wa BC 5, wakati huu ndio Yesu alizaliwa Bethlehem. SIku hizi sisi raia wa dunia ni watumwa wa makao makuu ya Fuko la Fedha la Kimataifa(IMF) na Benki Kuu ya Dunia(WB).
Tuwajadili kidogo Makaisari wa Dola ya Rumi, ili kufahamu vizuri somo lifuatalo kitambo: Tiberius(AD 14-37);Caligula(AD 37-41);Claudius(AD 41-54);Nero(AD 54-68);Vespasian(AD 69-79);Titus(AD79-81);Domitian(AD 81-96) wakati Mtume wa Mwisho wa Yesu wa Nazareti(siku hizi kuna mitume lukuki wa Yesu  hata wa Michungwani),Yohana anaandika kitabu cha Ufunuo huko Patmo kisiwani. Yohana alifariki wakati huo huo.
 Dola ya Rumi iliutawala ulimwengu wa wakati huo.Watu wote wakalipa kodi zao kwa makaisari hawa jijini Rome.      Rome ulitegemea utajiri wa mataifa mengine yaliyokuwa makoloni yake,ili kupata ustawi. Hata Yesu alilipa kodi kwa Kaisari.
Mji huu ukapata mali nyingi kutoka Misri, wakapata hata dhahabu kutoka Kushi(Ethiopia),la sivyo wangekufa njaa hawa.Siku hizi,Rome ni Makao Makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo(FAO).
 Utajiri na fahari ya raia wa Rome, vilitoka katika makoloni yao. Hawa watumwa 650,000 waliwatumikia Mabwana wakubwa wa mjini Rome,waliokula wakiwa wamelala. Hata siku hizi za mwisho wa wakati,kutakuwa na utumwa kwa jiji ambalo nitalisema punde, ambalo linaanza kuwa kitovu cha uchumi wa dunia(Ufunuo 13:16-17).
Tumetazama katika makala zilizotangulia,namna masanamu ya Makaisari yalivyotapakaa jijini humo na katika mlki yote,na yaliabudiwa kama miungu(Ufunuo13:14).
 Nataka kusema kwamba, MILKI,mamlaka,enzi, fahari na utajiri huandamana na kulazimisha watu kuabudu ama kusujudia wenye vyote hivi. Hata sasa, wenye mamlaka,enzi,fahari na utajiri wataabudiwa kama miungu. Nazungumzia utajiri haramu, kama mihadarati,fedha chafu,bidhaa bandia,magendo, biashara ya viungo vya binadamu kama albino n.k Na watu huwatoa kafara hata wake,waume na watoto.
 Waarabu wanatumia nguvu ya silaha,majambia,makombeo na mabomu kuzuia ibada hii ya miungu watu-lakini Biblia inatushauri kutumia silaha tofauti na hizi,ili kushinda majaribu haya.
Sasa, nataka utambue kwamba Yule Mtume wa Yesu,Petro, alifika jijini Rome ili kupeleka Injili mwaka 42 AD. Ulikuwa wakati wa Kaisari Claudius, siyo? Haya, Petro aliuawa mwaka AD 67 kwa kutundikwa msalabani kichwa chini-miguu juu.
 Wee uwasikie tu Makaisari wa Kirumi, aliuliwa na Kaisari Nero mkatili kuliko Shetani mwenyewe. Hata mwisho wa wakati Watakatifu watauawa(Ufunuo  17:6 na Ufunuo 13:4-7).
 Kosa la Petro lilikuwa kukataa kuwasujudia Makaisari na sanamu zao,na kuwahubiri watu kwamba kuna Ufalme wa Yesu,badala ya ule wa Kaisari-UCHOCHEZI!!
Wafuasi wa akina Petro walishikilia msimaso wa kutokwenda katika mahekalu ya wafalme kuwasujudia na kupigia magoti masanamu yao, wasisitiza ibada ni kwa Mungu tu, Allah,Yahweh, Adonai,Elshadai, Nyasaye,Nyamuwanga , orodha ya majina ni ndefu.
Tulimwona Socrates(BC 490-400) AKIKATAA kusujudia miungu 391 ya Wagiriki juu ya Mlima Olympus, Wakristo wengi waligoma pia kuwasujudia Makaisari, waliuawa,waliraruliwa na wanyama wakali katika viwanja vilivyoitwa, Colloseum. Historia inajirudia, demokrasia itaondoka na uhuru wa kuabudu uko hatarini.
 Nero, alichoma moto sehemu ya jiji la Rome,mwaka AD 64 ili apate fursa kuwasingizia akina Petro,kwamba ndiyo waliochoma mji-Propaganda! Ndiyo akili za Freemasons na Shetani kuwasingizia watu ili wapate kuwaua!
  Unajua sababu? Injili ya unyofu(ya Yesu) ilikuwa hatari kwa utawala wa Rumi,ilizuia ibada na kicho kwa masanamu yao,na unajua matajiri wote wa dunia walikuwa wakiishi jijini Rome,biashara kubwa zilikuwa homo, na watu maarufu, meli kubwa za fahari zilitia nanga bandarini,zilizleta bidhaa nyingi, shangwe na kiburi vilitamalaki, sasa watu hawakutaka kusikia “Upuuzi” unaoitwa UFALME WA MUNGU!
  Basi, baada ya Petro kuuawa mwaka 67 na Kaisari Nero, akazikwa mjini Rome-bila shaka alipozikwa ndipo lilipojengwa kanisa kubwa kabisa St. Peters  hapo Rome. Wao wanasema,lilijengwa katika mgongo wa Petro-‘juu ya mwamba huu,nitalijenga kanisa’.
 Siku hizi, Kanisa Katoliki hutuambia Petro aliyeuliwa jijini Rome, ndiye PAPA WA KWANZA,muasisi wa Kanisa hilo la Rumi.
  Kwamba, Petro,amewatangulia jumla ya mapapa wasiopungua 302 hivi. Papa wa pili eti alikuwa Mtakatifu Linus(67 AD). Yule Papa aliyetiwa mbaroni Feburuali 1798 wakati wa Maasi ya Wafaransa, Papa Pius VI  na aliyerejeshewa heshima na akina Mussolini Feburuali 1929 ni PAPA PIUS XI.
Huyu aliyepo ni Papa Benedict XVI, yaani wamepita ma-Benedict 15. Ukristo mjini Rome umepitia changamoto tele, hadi kujikomba kwa Makaisari ili kukubali yaishe na kupunguza mateso kwa wakristo.
 Ilifika wakati,kanisa likawa na wapagani, watambikia mizimu na waabudu sanamu na waumini waadilifu kwa pamoja. Ukafika muda,vikaanzishwa vyeti vya msamaha-certificates of pardon,ili mtu akitaka kutenda dhambi kwa uhuru,basi anunue vyeti hivi kwa fedha nyingi ili akatende jinai huko-hatahesabiwa dhambi, maadam keshalipa fedha!
 Hizi ni dhana za kibinadamu(human theories) zilizoko makanisani leo ili kumfurahisha ibilisi na wakala wake Freemasons. Ili kupata fedha, vikauzwa vyeti(sale of indulgencies) makanisa yakajengwa ya fahari sana, ndani yake kulikuwa ibada ya sanamu na miungu.
Mbona tunawafahamu akina Tetzel ambao walifanya biashara hiyo ya vyeti vya misamaha ili kupata fedha nyingi. Msamaha wa dhambi ukaenda kwa matajiri na wenye fedha tu.Huu ndiyo mwanzo wa wenye mali wakifa roho zao kwenda Purgatory, lakini fukara akina eti roho inakwenda Jehanum. Kumbe masikini Mungu hampendi? LA HASHA.
 Pamoja na kwamba, ukipinga mambo haya unakuwa mwasi, lakini kumbe BIASHARA YA KIFO ilianza siku nyingi, hata leo wenye enzi na mamlaka wanafanya madhambi hata makanisani lakini wanaoondolewa ni fukara tu.
 Marekani na washirika wao nao wana, “Certificates of Pardon” wakienda kushambulia nchi yoyote na kuua watu, hawachukuliwi hatua, nchi masikini akina Joseph Kony,  Gbagbo ,Pierre Bemba, Taylor, Uhuru Kenyatta na wenzao wakikisiwa tu,ni kuswekwa rumande-THE HAGUE!
Mpaka wakubwa wapigiwe magoti na sanamu zao szisujudiwe(Ufunuo 13:7-8) halafu hizo sanamu zao zinawafanya watajirike kwa utajiri haramu wa Ibilisi(Ufunuo 13:3-10),twazungumzia utajiri wa damu za watu(Ufunuo 17:6).
 Msomaji aitwaye Mary, ameniandikie SMS kuuliza: “Nimesoma makala ya Machi 27;tufanyeje sasa,kama mambo ni hay? Mbona tunazidi kuchanganyikiwa?”
 Katika mwaka wa 490 BC zama za Sokrati, Dario I  akatoka na jeshi kubwa la Wamedi ili akapambane na hao Wagiriki mahali paitwapo,Marathon.
 Jeshi dogo la Ugiriki likawaotea mahali hapo,likawashambulia ghafla Wamedi ambao walikuwa na jeshi kubwa sana na magari ya deraya ya chuma.Wamedi wakapigwa na kuteketezwa kabisa.
 Baada ya ushindi, Jemedari akamtuma askari mmoja shujaa aitwaye Pheidipides  kwenda mjini Athens kutoa HABARI NJEMA kwamba walikuwa wamelishinda jeshi la adui.
 Basi, Pheidipides akatimua mbio kali kwenda Athens kutoka hapo Marathon,umbali ambao ni maili 29. Alipofika sokoni mjini Athens akasema huku akihema kwa nguvu.
“Tumepigan-nna vita,tumemshind-ddaa… add-ddui!!” Akaanguka mchangani na kufa! Ili kumuenzi shujaa huyu, Pheidipides, siku hizi kuna mbio za Marathon zilizoanzishwa ili kukumbuka ushujaa wake wa kumshinda Dario Mmedi-soma kitabu cha Danieli.
Mashindano ya Olimpiki yalianza Ugiriki karne tano hivi kabla ya Yesu, yamekuja kuboreshwa mwaka 1896. Hivyo Juni mwaka huu huko London,mbio za marathon bado zitamkumbuka huyu shujaa Pheidipides aliyejitoa uhai wake ili KUPELEKA HABARI NJEMA za wokovu. Alikuwa mwaminifu hadi kufa.
 Naam, uaminifu hadi kifo,kama Pheidipides shujaa, kuna akina Socrates(490-400 BC) alishikilia msimamo wa kutoabudu sanamu za Olympus,hadi akauliwa kwa sumu-uaminifu kwa kumwabudu Mungu tu, siyo sanamu za Shetani na mawakala zake, Freemasons.
  Mtume Muhammad(570-632 AD) alipozaliwa mjini Mecca, Saudi Arabia, akawakuta Waarabu wakiabudu sanamu hizi hizi. Ibada ya sanamu ilikuwa Ulaya,Arabuni na ziko bado Ulaya hata Marekani,lakini wapumbavu wanadhani waabudu sanamu ni Waafrika tu!
 Basi, Mtume Muhammad akaazimu kuwapa Waarabu dini safi,ya kumwabudu Allah tu. Allah huyu ndiye Yehovah, Yahweh,Nyasaye,Nyamuwanga,Katonda,Nyamujakhuma!!
 Mjini Mecca,kulikuwa na patakatifu palipoitwa, ‘Kaaba’ kwa Kiarabu eneo hili lenye pande sita zenye kulingana,lilijengwa vizuri na kulikuwa na sanamu nyingi.
 Katika kona moja ya jengo hilo, kulikuwa na JIWE JEUSI ambalo eti lilianguka kutoka angani. Mtume Muhammad aliwaona watu wengi wakitoka mahali pengi duniani wakienda hija (pilgrimation)  hapo al Kaaba,ili kulibusu hili jiwe jeusi. Alikusudia kuwapa dini nzuri-naam Dini saafi! Soma The golden book encyclopedia (DELUXE Edition)kilichoandikwa na Bertha Morris Parker. Mimi sikusema haya.
Barack Obama, alikwenda Seoul,Korea Kusini,kupanga mikakati na wenzake wa China,Urusi,Korea Kusini na Japan ili kuidhibiti Korea Kaskazini,iachane na kiburi chake cha makombora ya Nyuklia huko Ghuba ya Korea.
 Korea na Iran ni mataifa ya Kikomunisti, Korea Kaskazini hakuna Mungu kabisa,ila miungu sasa jamaa wanasema huko Korea hakuna demokrasia na uhuru wa dini, wanataka kwenda kupindua. Iran wanasema Ayatollah Ali Khamenei analazimisha watu kutokuwa na uhuru wa dini nyingine.
  Halafu, nikamwona Papa Benedict XVI akienda Santiago de Cuba na Havana,ili kukutana na Rais Raul Castro Ruz na Rais Mstaafu Fidel Alejandro Castro Ruz.
 Ajenda iliyozungumzwa ni ile ile,kitisho cha UKOMUNISTI na kuwazuia watu demokrasia na uhuru wa dini.
 Eti Korea, Iran na Cuba hakuna demokrasia na uhuru wa kuabudu(hata sanamu). Hii ilikuwa ziara ya mwanzo Papa huyo kufika Cuba ya WAKOMUNISTI-wakampokea kwa maelfu -wamenyoosha mikono yao kwa  UKATOLIKI, wataachana na Ukomunisti, ukomunisti na Ukatoliki havipikiki chungu kimoja!
 Yumkini,huu ni mwisho wa ukomunisti duniani, ziara ya Papa ni dalili za kuzikwa kabisa ukomunisti mjini Havana,na katika ulimwengu wa mrengo wa mashariki-kufuatia kuuliwa kwa akina Osama,Gaddafi, Saddam yaani kukaushwa Mto Frati(Ufunuo 16) na kuangushwa kwa Ukuta wa Berlin ulioitenga dunia katika maeneo mawili-dunia iko tayari kuungana sasa! Ziara ya Papa Cuba,ilikuwa ya mafanikio ya kuiunganisha dunia.
  Tuzijadili kidogo dola zenye nguvu nyingi duniani, ambazo sasa zinaanza kuabudiwa pamoja na sanamu zao,tukitaka kupata neema! Siku hizi kuna sanamu mambo leo.
Rais wa Benki ya Dunia(WB) huteuliwa na Rais wa Marekani. George W.Bush alimteua Robert Zoellick miongoni mwa wafanyabiashara, mabwenyenye na wahafidhina, akamrithi Paul  Walfowitz,  baada ya ile kashfa ya kimwana wa Kiarabu, Shaha Ali-Riza.
 Julai 28 mwaka jana, safu hii ikaandika kwa undani sana kisa hicho, sipendi kurejea. Ukikosa TAZAMA unakosa maarifa.
Marekani,ndiyo nchi yenye mamlaka yap eke yake kumteua Rais wa Benki ya Dunia(WB)na Ulaya wana haki ya pekee katika kumteua Mkuu wa Fuko la Fedha la Kimataifa(IMF), wengine walie tu.
 Alipojiuzulu Dominique Strauss-Khan(DSK) kwa kashfa ya ngono dhidi ya mwanamke mwenye asili ya Afrika Magharibi-Diallo, akateuliwa Mfaransa mwenzake, Christine Lagarde.Kashfa ya DSK ingali inafukuta huko Marekani.
Marais wote 11 wa Benki ya Dunia ni Wamarekani,na kadhalika watendaji wote wakuu  11 wa IMF WAMETOKA ULAYA,
 Kuna mambo mawili ya kutazama hapa; wote 11 wa WB wametoka Marekani,na wakuu wote 11  wa IMF , wametoka Ulaya. 11 na 11, hii namba ni ya Freemasons na haina tofauti na majengo pacha ya WTC yaliyosimama kama 11, na yalisambaratishwa Septemba 11,mwaka 2001, hapo upo?
  Nani wa kuwapinga Ulaya na Marekani sasa,juu ya kuiburuza dunia kwa kutumia WB na IMF? Juni 30 mwaka huu, Robert Zoellic anaachia ngazi,tuone kama Obama hatamchagua Mmarekani mwingine. Rais wa Marekani anamchagua Rais wa Benki ya Dunia!!
  Leo, nimesikia kwamba,Brazil,Russia,China,India na Afrika Kusini(BRICS) wanafanya kampeni ya kuipokonya Marekani kuitawala Benki hiyo mawakala wakuu wa ukoloni duniani.
 Nataka kusema kwamba, Washington ndiyo Makao Makuu ya Uchumi wa Dunia baada ya Rome, na wataamua hiki kiti kiende wapi? Kitakwenda BRICS au Vatican?
 Itaendelea
0786 324 074
 

 






Tuesday, March 20, 2012

UNATAKA UTAJIRI? FREEMASONS JIBU LAKO!!


WANATHEOLOJIA wengi hukubaliana kwamba,Ezekieli 28:16 nikauli ya Mungu,aliyoitoa mbinguni kunhusu Ibilisi.
  Kwamba, ni ‘Mfanyabiashara’ wa haliyajuu.Ukitaka kutajirika haraka kupitia njia haramu sana kamamadawayakulevya na fedha chafu,unawafuata mawakalawake, Freemasons(Ufunuo 18:1-3).
Nakariri kifungu hiki katika Biblia ya Kiingereza, iitwayo, Revised Standard Version (RSV)kama ifuatavyo:
“ In the abundance of your ‘trade’ you were filled with ‘violence’ and you sinned”. Nachagua maneno ‘trade’ yaani biashara na ‘violence’ yaani ghasia na machafuko.
 Naam, katika tafsiri isiyo rasmi, Mungu alimwambia Lusifa kwamba katika ‘Biashara’ yake iliyoenea dunia nzima alifanya ghasia na dhambi.
 Aidha, maneno ya Kiingereza, “Widespread trade” hutafsiriwa kwamba ni “slander” maana yake kwamba hata mbinguni Lusifa alianzisha mashitaka dhidi ya serikali ya Mungu, kwamba haikuwa na demokrasia; iliwanyima (malaika) demokrasia na haki.
Shetani ni Mwanaharakati bingwa wa Haki za Binadamu na Malaika pia! ‘Slander’ ni kauli yenye nia ya kumharibia mhusika heshima(reputation); Shetani anaelezwa na Biblia kama Mshitaki; ama mwenye kauli za kuvunjia watu hadhi(Zekaria 3:1,Ufunuo 12:10).
 Hii kauli yenye kashfa, “Slander” humuongoza Shetani na wafuasi wake, Freemasons, na mawakala wake wengine kama serikali zenye nguvu duniani, superpowers, kufanya vita na ghasia kwa madai ya kuleta haki na demokrasia.
 Lakini, badala yake,tumeona huko Irak,Libya,Misri n.k hakuna vyote viwili;kuna machafuko,mauaji ; hakuna amani.
 Leo,nitajadili biashara haramu ya Shetani,Freemasons na mataifa makubwa ya Magharibi,kasha Uchina na Urusi. Najadili fedha chafu, na utajiri unaoletwa kwa watu na mwanamke Yule, Yezebeli, ama Babeli wa siri.
  Ghasia, vita na machafuko, chanzo chake ni mawazo ya ubinafsi na uchoyo, ambao hatimaye hufanywa kuwa tabia ya mhusika. Wazo huja kwanza(hutangulia) vitendo hufuata baadaye, na matokeo yake ni mauaji ya kinyama.
  Muinjilisti,Kamara Kasupa, juzi amegusia biashara haramu ya ALMASI ZA DAMU huko Sierra Leone.
Siku hizi tunamwona Charles Taylor huko The Hague anakojibu mashitaka ya kuwasaidia Revolutionary United Front, walioua watu na kupora almasi chini ya uongozi wa Fodday “Poppay” Sankoh aliyefariki huko gerezani.
  Chanzo siyo Sankoh ama Taylor; ni ubinafsi wa Freemasons hawa na choyo cha utajiri; mwisho wa siku wamekamatwa zana(mapanga na visu) walioshika visu na mapanga, wameachwa huru-na hakuna wa kuhoji!
  Msomaji mmoja amenionya nisitumie vifungu vya Biblia katika makala zangu,kama nataka zisomwe na watu wasomo makini,la sivyo wasomi makini watasusa kuzisoma!!
 Hata hivyo, katika uandishi wa habari, ili habari iwe ‘credible’ ama ‘reliable’ lazima kuwe na ‘checks and balances’.Lazima habari iwe na news worthiness na iwe na chanzo cha habari cha kuaminika sana.
 Kwa kuwa nakusudia kuandika juu ya “Mchuuzi” ama mfanyabiashara kubwa-kubwa wa mwanzo ulimwenguni, Biblia katika Ezekieli 28:16 inaniambia,
“Lucifer was involved in widespread trade”, kwamba tangu mbinguni Lusifa alianzisha ‘biashara’ haramu ya kashfa ili kubomoa ustawi wan a heshima ya Bosi wake-Mungu.
Sasa, niachane na Biblia,ili nitekelezeje jukumu la uandishi na malengo yake mahsusi, ya  ‘To inform, to educate, to reform, to entertain, to incite?’
Nalazimika kusaka vyanzo vingi vya habari(Biblia,Koran,sheria,kauli za wasomi,wanafalsafa,viongozi na Mungu na Shetani wakiwemo) ili niandike makala yenye kufanyiwa utafiti wa kina,yenye kuhabarisha,kuelimisha,kurekebisha umma, kuburudisha na kuonya,ama kuweka   AJENDA miongoni mwa wasomaji wangu.
  Kama msomaji hatajali, asome habari za Mungu na Shetani kama BURUDANI tu!
Naam, chanzo change cha habari,Biblia,kimesema aliyeanza kufanya biashara chafu ulimwenguni,ni Ibilisi. Biashara yake ililenga ‘kuchuuza’ watu ili wadharauliwe,wauawe.
Tumjadili Mtu Mweusi-Mwafrika. Najua Kamara Kasupa anajadili jambo hili kwa kina; nitoe mchango wangu kidogo.
 Ziko kauli dazeni za kumdhalilisha mtu mweusi. Tazama chache hizi:
Homer (700 BC)- “Ethiopia(Africa) is a remote place at extreme of universe where the people worshipped and sacrificed to gods”
Thomas Hobbes(1588-1679) “Africa is a timeless place in which there are no art, letters or social organization, but instead, only fear and violent death”
Jean-Jacques Rousseau(1712-1778) “The Black people are unable to think in any reflective manner.  Their engagement in arts is therefore, a thoughtless activity which is the antithesis of intellect”.
 Uko upuuzi mwingi na kauli za ovyo kuliko hizi za Wazungu,Wachina, Wahindi,Makaburu n.k dhidi yetu.
 Kibaya zaidi, hata Weusi wenzetu wanaamini hivi, na wanatamani laiti wangezaliwa Wahindi ama Wazungu hivi.
 Kauli za akina Dk.Watson,D.W.De Clerk n.k ni kwamba, hapa Afrika, hakuna ‘thesis of intellect’ kwamba sisi ni ‘unable to think in any reflective manner’ Afrika ni Bara ambamo kumejaa violence and death,ni waabudu miungu na tunaojitoa dhabihu kwa miungu na mashetani!
 Mwafrika, hana fikra, hawezi kufanya jambo lolote la maana, nchi yake imejaa hofu na kifo!
 Hata mwanzilishi wa kauli kwamba ‘Binadamu wote huzaliwa wakiwa sawa’ Thomas Jefferson,rais wa tatu wa Marekani,alisema “Ingekuwa vigumu kama nini Mtu Mweusi kujua kanuni za Hesabu katika kitabu maarufu cha Euclid!”
 Loh!! Hii ndiyo biashara ya Shetani. Na kwa bahati mbaya sana hata Mwafrika anaamini hivi,ndiyo maana leo chetu kimekuwa chao-chao siyo chetu.
Dini ya Ukristo haikuanzia Ulaya,imeanzia Mashariki ya Kati.Wazungu(Rumi) waliwafanyia mitume ukatili mwingi na kuwaua, Weusi wameamini dini siku nyingi.
Simoni Mkrene(Sudan) alimsaidia Yesu Msalaba, huu ulikuwa mwaka wa 31 AD. Yesu alitimkia Misri(Afrika) mwaka 4 BC,la sivyo Wayahudi wangemuulia mbali zamani. Sasa Afrika,waabudu sanamu na miungu tangu lini?
 Juma lililopita,tulijifunza ushenzi wa Dola ya Rumi na ibada ya sanamu ya kulazimisha watu. Abraham alitoka Ur(Iraki) siyo Ulaya,ndiye baba wa Isaka na Yakobo aitwaye Israeli.
  Viongozi wetu na wasomi wetu wamesikiliza ‘biashara’ hii haramu ya Shetani na Freemasons,kwamba sisi weusi siyo lolote. Ndiyo mawazo ya akina Adolf Hittler. Unajua katika Oliumpiki ya mwaka 1936 huko Berlin, Mmarekani Mweusi Jesse Owens,aliwatoa kamasi Wazungu, akapata medali nne za dhahabu kwa dakika 45 tu,Mgeni wa Heshima,Hittler akasusua kutoa zawadi?
 Alisema, Jesse Owens alikuwa mnyama-sasa alishangaa Mzungu atashindanishwaje na mnyama?!
Ndizo akili za akina Materazzi dhidi ya Zenedine Zidane,kwenye uwanja huo huo wa Olimpiki wa Berlin mwaka 2006!
 Matokeo yake, uchumi wa Afrika umekuwa siyo huru,tunaamrishwa kila jambo na Benki ya Dunia(WB) na fuko la Fedha la Kimataifa(IMF) na taasisi za kikoloni kama UNCTAD na WTO n.k
 Ndiyo maana tunalazimishwa kuwa mashoga!!
Hawa wameanzisha ukoloni mwingi baada ya vita vya pili,1945 wakafanya mradi wao kupitia Marshall Plan. Kabla walikaa mwaka 1884 wakagawana Afrika kama nyama choma mezani.
 Mwenyekiti wao alikuwa Freemasons na Ibilisi mwenyewe. Malengo yao ni kutusema vibaya na kutushitaki katika macho ya ulimwengu kwamba sisi Weusi ni sifuri,ni hasi. Halafu,tunakubali.
 Wamesababisha mashirika na viwanda vyetu vife kwa sira za ubinafsishaji zilizoletwa na IMF na WB.
 Nimezungumza na msomi na mzee anayefanya kazi zake jijini Mwanza, Charles Masalakulangwa juu ya WB na IMF itatuepushaje na mazao yetu kama pamba,kahawa,korosho,kahawa n.k yasishuke bei ili kuondokana na umasikini?
 “Tunachakata mazao yetu na kuyaongezea thamani,ili tuyauze katika masoko kama Agoa(Marekani) ama Ulaya. Nchi tajiri zimeweka ruzuku kwa bidhaa zao na wakulima wamepewa ruzuku, sasa bidhaa zetu na mazao yetu yatashindana na yake ya Ulaya na Marekani? Kwanza, bidhaa zao zina ubora mkubwa na bei iko chini, sasa bidhaa gani zitashindana na zile za Ulaya kwenye masoko ya dunia?’
 Matokeo yake, tuna sangara, dhahabu,almasi,tanzanite,mazao ya kilimo lakini wao ndiyo wanaopanga bei. Pamba yetu ingali magulioni,haina bei-bei huja mpaka yawepo majanga  Ulaya,Marekani na China.
 Wanaopanga bei ni G-7,G-8,G-20 sijui European Economic Community, Paris Club n.k
 Tunasumbuliwa na mfumuko wa bei, si kwa sababu ni sisi tumetaka, ni wao wamependa hivi. Inflation na Reccession inatokea pasipo sisi kutaka kwa sababu vitu hupanda bei na ‘supply’ hupungua.
 Tujadili bei ya mafuta ambayo ni chanzo cha kupanda kwa gharama za maisha.Mafuta ndiyo huendesha uchumi wa dunia,huendesha viwanda,mitambo,umeme kama wa TANESCO,Daladala n.k
Mwaka 1979 kulitokea ugomvi wa mafuta,Uingereza mfumuko wa bei ukapanda hadi kuwa  asilimia 334. Sisi hapa mfumuko wa bei ni asilimia 20 tunataka kukata roho kwa maisha magumu!
 Nataka kusema kwamba, nchi zenye rasilimali nyingi zina simamiwa na Freemasons hawa-hazina uhuru,na kuna vita na machafuko. Ukiona amani ujue panapohusika hapana mali, hata mahakama ya The Hague haipasogelei!!
  Utajiri uko mikononi mwa mwanamke aliyebebwa ba Mnyama(Ufunuo 17:1-) na wafalme wa dunia nzima lazima kushirikiana naye na hao rafiki zake Freemasons lazima uchumi wote na mabenki yote view mikononi mwao.
 Nani anamiliki mafuta ya dunia? Angalia makampuni makubwa ya mafuta duniani, “SUPERMAJORS”.
Exxon Mobil-Marekani, British Petroleum(BP)la Uingereza, na Uholanzi kwenye mahakama ya Moreno Ocampo wanamiliki kampuni la ,Royal/Dutch Shell kwa ubia na Uingereza.
 Total ni kampuni la Ufaransa na Ubelgiji,kule Makao Makuu ya EU ambako mwanamke Yule amekaa juu ya mnyama(Ufunuo 17:1-).
Chevron Texaco na Conoco Phillips ni makampuni ya Wamarekani,Yule mwanakondoo wa Ufunuo 13:11-).
Russia, kuna makampuni kama Lukoil,Yukos na Sibneft yanayomilikiwa na Ikulu ya nchi hiyo-Kremlin.
Na Uchina kuna  Petrochina. Nchi zote hizi tano ni wanachama wa   kudumu wa Baraza la Usamala la Umoja wa Mataifa, ambao wakiamua kwenda Irak,Libya,Misri ama Iran kuvamia na kupora mafuta,wanakwenda.
 Hata China na Russia,leo wanafanya biashara ya mafuta tu, hawana lolote la kuipinga Marekani,Ulaya na Freemasons. Hata Kremlin tayari kuna mawakala wa CIA na Freemasons.
  Nchi zinazozalisha kwa wingi mafuta na zimeungana (OPEC) ni Algeria, Indonesia,Iran,Irak,Kuwait,Libya,Nigeria,Qatar,Saudia, Falme za Kiarabu na Venezuela kwa Hugo Chavez.
 Urusi,Mexico,Canada,Norway na Marekani huzalisha sana mafuta,lakini hawamo kwenye OPEC.
Sasa angalia,katika nchi za mafuta ambazo zinawakatalia wababe wa NATO zina amani? Hakuna biashara ya kifo huko maana ‘The merchants of Death’ wako karibu na kila kulipo na rasilimali nyingi,hususan mafuta na gesi.
Hii ‘widespread trade’ ya Ibilisi na Freemasons iko kila kuliko na mafuta; ukiwapa  mafuta, poa wanakuacha,ukiwanyima wanachochea vita na unapinduliwa ama unauliwa!
   Itaendelea
0786 324 074

 

Friday, March 16, 2012

FREEMASONS NA IBADA YA SANAMU INAYOKUJA



NIREJEE historia ya Socrates, Yule mwanafalsafa wa Ugiriki. Ndiye mwalimu wa Plato; Plato ndiye mwalimu wa Aristotle.
Encyclopedia Britannica, hutuambia kwamba, Aristotle (384-322 BC)ndiye mwanasayansi wa ukweli katika historia ya ulimwengu.Hawa wanafalsafa wengine,wamufuatisha kile alichofikiri yeye kwanza.
 Socrates, aliuliwa na mamlaka ya Athens,kwa kuwa aliwafundisha wanafunzi wake,akina Plato, kwamba hakukuwa na miungu 391 juu ya kilele cha Mlima Olympus. Alifundisha kwamba, kulikuwa na Mungu mmoja tu,naye aliishi mbinguni.
Kwamba, magalaksi(galaxies) yoote aliyaumba yeye pamoja na nyota na sayari zote ulimwenguni, na kwamba dunia haikutokea kwa bahati kwa njia uibukaji(evolution) kama alivyofundisha Charles Robert Darwin katika karne ya 19.
Sokrati huyu, alipewa alipewa rehema ya juma moja, ili ayakane mafundisho yake ya kuidharau miungu ya taifa lake la Ugiriki; alikataa na mwisho wa siku alihukumiwa hukumu ya kifo.
Alipewa sumu ainywe mbele ya hao wanafunzi wake akina Plato, akianywa sumu hiyo,mwili ulipopatwa ganzi akalala na kufunikwa shuka akiwa tayari amekufa-waliahidi kumlipa posho ya chakula kila siku kama angeyakana mafundisho yake hayo.
Nataka kusema kwamba, Sokrati alishikilia msimamo,mwisho akauawa mbele ya wanafunzi wake. Naam, ukweli huandamana na hukumu ya mauti.
Msomaji,utambue kuwa ibada ya miungu katika ulimwengu ule lilikuwa suala la maisha au la mauti duniani,tangu Ulaya hiyo ya akuna Sokrati,Plato na Aristotle na ndivyo itakavyokuwa tuendako.
Hao wazungu wa Magharibi,hawakuwahi kuijua dini. Walikuwa washenzi na watambikia mizimu na waabudu sanamu.
 Unajua watu wa kwanza kumwabudu Mungu mmoja ni Waisraeli wa kale? Unajua dini ya Ukristo imekuja wakati wa Yesu na mitume?
 Mitume kama Petro, Paulo n.k ndiyo waliopeleka Ukristo Ulaya,hususan jijini Rome, na wakaishia kukataliwa na kuuliwa kinyama?
 Hata Afrika ilitangulia kumjua Mungu kuliko hawa; tazama historia ya nchi kama Ethiopia, Sudan, Misri n.k
Edward A. McDowell, Profesa wa Agano  Jipya katika Seminari ya Baptisti,Nort Carilina,Marekani, ameandika katika kitabu kiitwacho The Meaning and Message of Revalation,kwamba watawala wa Romi ya kale(emperors) walilazimisha raia wawaabudu, ambao walijiona ndiyo miungu!
  Rumi ya kale kulikuwa na dini ya kuwaabudu wafalme waha wa Rumi. Julius Caesar, alitengeneza SANAMU lake lililowekwa miongoni mwa masanamu mengine hekaluni mwake-hekalu la Kaisari!
Kaisari Augusto(27 BC-14 AD) alikubali cheo kiitwacho, “Augustus” kutoka katika Baraza la seneti. Hiki ni cheo cha miungu.
 Caius Caligula( AD 37-41) aliwalazimisha raia wa milki hiyo ya     Rumi dunia nzima waiabudu sanamu yake. Jitihada zake za kuisimika sanamu hiyo katika hekalu la mjini Jerusalemu zikapingwa vikali sana na Wayahudi; kwa kuwa wao walijua ibada ni kwa Mungu tu ambaye huishi mbinguni,na hawakilishwi na masanamu!
  Domitian, alikuja kupunguza mgogoro mkubwa kati ya Wakristo na makaisari wa Kirumi waliotaka kuabudiwa na watu wote,na wale waliopingwa, waliuawa kwa kuraruliwa na wanyama katika viwanja ambavyo siyo tofauti sana na stadium za sasa hivi.
  Kaisari Nero alitaka raia wa makaloni yote chini ya dola hii wawaone wao kama miungu. Hatimaye masanamu yaliingizwa kanisani,wakati Wakristo wakitaka kujikomba kwa hawa makaisari walioanza kujifanya wameongoka na kuwa wakristo.
Aina hii ya madhehebu ya ibada ya wafalme ni maarufu hata Asia; na ilidhaniwa kumwabudu Mfalme ndiyo ‘Patriotism’ yaani uzalendo kwa taifa lako.
Dola ya Waislam wa Ottoman(Uturuki) ambayo sasa imejisalimisha NATO, walijaribu kuzuia uhalifu huu, lakini kama tulivyoona katika makala zilizotangulia, dola hii ya Ottoman ilianguka katika karne ya 16 AD.
 Kwa hiyo, zama za Ukristo,watu waliokataa kuwasujudia ma-emperor wa Rumi walionekana waasi, watukutu na wasio wazalendo-waliuliwa,kufungwa jela na wengine walifukuzwa wakawa wakimbizi huko uhamishoni,wengine ndiyo waliokimbilia Marekani wakiogopa mateso Ulaya.
  Wakristo, walilazimishwa kuwaabudu makaisari,kuwatolea sadaka katika sanamu zao huku wakitamka maneno haya, “Kyrios Kaisar” maana yake, “Bwana Mungu wangu Kaisari”!!
  Lilikuwa zoezi dogo tu; lakini lenye kukudai uaminifu wako wewe mkristo,Muislam,Budha,Hindu n.k kwa Kaisari badala ya Yule Mungu wako unayemwabudu wewe kwa kicho na kutetemeka.
  Wakazi wa Afrika Mashariki wanajua mambo haya ya “Kasinge Mwombeki” kumbe yalianzia Ulaya. Kiongozi wa kidunia alikuwa nawinda heshima ya kimungu,ili mwanadamu apate kumwabudu yeye.
 Nimeleta kisa hiki ili tujue maana hasa ya kukufuru. Mwanadamu anapojiita Mungu,ndiyo kukufuru,anapowalazimisha wanadamu wenzake kumwabudu yeye badala ya Mungu wa mbinguni-ndiyo kukufuru.
  Msomaji mmoja anataka kujua,namna mamlaka(Mnyama) ya Danieli 7:23-25 na Ufunuo 13:1,4-8 na pia Ufunuo 17:3-11 itakavyojigeuza kutoka mamlaka ya siasa na kuwalazimisha watu wa dunia nzima kuiabudu,kama alivyoabudiwa Kaisari wa Rumi na SANAMU yake,sawa sawa na Wakristo ama Waislam wanavyomwabudu Mungu.
 Mamlaka itakayofuata duniani baada ya Marekani na washirika wake kuitiisha dunia nzima,itatengeneza sanamu(Ufunuo 13:14-15).
Sanamu hii itadai kila raia wa dunia nzima(sensa ya dunia nzima ipo,na kila raia wa dunia anajulikana) kutoa heshima yake kwa Mtawala huyu mpya wa dunia, ambaye atarithi enzi zote za tawala za Kaisari. Watu watadaiwa kuonesha kifo kwa huyu mtawala ili kuonesha uzalendo wao kwa kutamka maneno, “Kyrios Kaisar” yaani Bwana Mungu Kaisari badala ya kutamka,”Kurios lesous” yaani Bwana Yesu ama kwa Waislam, ‘Allah Akbar”!!
 Ugomvi wa sasa wa Marekani,Ulaya, Israeli na washirika wao wengine, ni kitu gani kama siyo kutaka dunia iwe na mtawala mmoja, na taifa la Kiislam kama Iran linagoma?
Hivi leo,kuna vitu vya kijesi(Military Base) nyingi za Marekani huko Ghuba ya Uajemi. Na vita vikianza, tayari Iran iko kati kati-mataifa mengi ya Kiarabu kama Kuwait,Qatar, UAE wameruhusu vituo hivi vya kijeshi vya Marekani,ili Waislam wenzao wakileta jeuri,wananyeshewa mvua kali ya mabomu na risasi za rashasha(automatic rifles).
  Huu ndiyo ulikuwa ugomvi wa Wakristo na Makaisari wa Rumi zama zile.Wakristo wengi waliteswa Ulaya kwa kugoma kumsujudia Kaisari na sanamu zake,na ndivyo itakavyokuwa,kwamba tunakwenda kulazimishwa kuiabudu sanamu ya Kaisari mamboleo, ambaye ndiye Marekani na washirika wake wanamwandalia barabara kuelekea ‘Zulia Jekundu’.
  Kati ya Mungu na Kaisari wa Rumi,kulikuwa na ugomvi,mmoja akidai kuabudiwa na mwanadamu. Kuna nguvu mbili duniani zinashindana kutaka kuabudiwa,na kutolewa sadaka, lazima mmoja apewe heshima na kicho. Ukikataa kuiabudu mamlaka,unauawa.
 Juma lililopita,nikamwona Waziri Mkuu wa Israeli, Benyamin Netanyahu,akimwambia Rais Obama wa Marekani huko White House:
“Iran wanatuita sisi Shetani mdogo; na ninyi Marekani wanawaita Shetani mkubwa! Kwa nini wasishambuliwe na vinu vyao vya Nyuklia kuharibiwa,kabla hawajaanza kutushambulia sisi?” Alisema Netanyahu.
 Iran wanaiita Israeli na Marekani kuwa   Shetani. Tabia ya Shetani ni kujiinua mahali alipo Mungu na kudai kuabudiwa-na tabia hii imeonekana wazi katika siasa za dunia. Marekani ni Baba wa dunia, Israeli wanafanya wapendavyo, hawaguswi.
 Ujinga ni watu kudhani Israeli ni taifa teule la watu wa Mungu-tuwasaidie, Israeli walikoma kuwa taifa teule la watu wa Mungu walipomuua Yesu,Mitume na Manabii na mashahidi kama Stephano,wakasema damu zao ziwe juu ya vichwa vyao na vichwa vya watoto wao.
 Unajua Yerusalem ulibomolewa na majeshi ya Kirumi mwaka 70  AD? Unajua W               aisraeli wamekuwa wakimbizi katika nchi yao, Waarabu wakaikalia hadi huo mwaka 1948 waliporejeshwa kwa msaada wa Umoja wa Mataifa? Marcus Mpangala ameandika jambo hili kwa kina.
  Taifa la Israeli lilisha mwasi Mungu; leo wamekaribia kumalizwa na Adolf Hitler, damu ya manabii iko juu ya vichwa vyao, isipokuwa Muisraeli mmoja mmoja akitubu kwa kiburi chao hiki na ukatili dhidi ya mitume na manabii wa Mungu.
Ni kwa sababu hii, Israeli,Ulaya,Marekani na Vatican wamekubaliana kutengeneza mfumo mmoja wa dini,ili “Kaisari” mmoja miongoni mwao aabudiwe na dunia nzima.
 Huku sasa ni kuondoa UHURU WA DINI,Demokrasia na haki za binadamu. Siku hizi haki za binadamu ni ushoga, usagaji na wanawake kutaka kuoa wanaume zaidi ya mmoja! Waliosikia siku ya wanawake duniani wanajua tuendako.
  Haki za Binadamu!! Haki hizi zinaletwa na miungu ya Ulaya na Freemasons na Illuminati.
Mwandishi mashuhuri hapa nchini, William Shao, amepata kuandika katika jarida la Rai juu ya sanamu ya mwanamke aliyeketi juu ya mnyama huko Makao Makuu ya Umoja wa Ulaya(EU) mjini Brussels.
  Shao, aliandika kwamba sanamu hiyo inayofanana sana na kile kinachosemwa katika Ufunuo 17:3-11 iko mbele ya Ofisi za European Union huko Brussels, Ubelgiji. Nimewahi kuongea na Shao siku za karibuni juu ya kitabu chake kuhusu Freemasons.
  Sasa,kama tunabahatisha,kama wengine wanavyodhani, ni suala la kila mmoja kutafiti na kuamua. Tunawaandikia wenye hekima; hatuna shida na wapumbavu!
  Mwanamke aliye sawa na huyu wa mjini Brussels, ni Yule aliyemwona Mtume Yohana katika Ufunuo 17:3-11. Anaitwa jina la siri, “Yezebeli”.
 Naam, nataka tumjadili Yezebeli. Yezebeli anabebwa na Umoja wa Ulaya(EU) na washirika waao,Israeli na Marekani.
Yezebeli huyu alikuwa muumini wa kanisani Thiatira(Ufunuo 2:20-24) na alijiita Nabii,alifundisha waumini watu wa Mungu ili kuwapoteza,ili wazini(kuabudu miungu) na kula vitu vilivyotolewa dhabihu kwa miungu na masanamu ya makaisari wa Rumi.
 Naam, Yezebeli hataki kutubu,ni mzinzi,nusu yuko kwa Mungu,nusu ibada ya sanamu.Uzinzi wa kiroho ni watu wa Mungu kutambikia mizimu na miungu na kusujudia sanamu(Hesabu 25:1-3).Yezebeli anatufundisha sasa kutambikia miungu ya Misri, Babeli,Uyunani na Rumi,na somo hili tumejifunza katika makala tulizotangulia kuona.
  Yezebeli, anavaa nguo za rangi ya zambarau na nyekundu(Ufunuo 17:4).Mwandishi Gidion M. juzi aliandika kwamba nguo hizi za rangi ya zambarau na nyekundu walivaa wafalme wa Babeli na makuhani wa miungu.
 Labda, ndiyo maana mama huyu ana jina linguine la siri-‘BABELI MKUU,MAMA WA MAKAHABA’!!
Huyu Yezebeli anayebebwa na wafalme hukoo Umoja wa Ulaya(EU) anao watoto ambao pia ni makahaba.Watoto wa changudoa nao huwa changudoa kwa sababu ya mivuto mibaya. Sasa mama huyu ni nani? Amewazaa akina nani? Tafakarini.
  Yezebeli, alikuwa Malkia aliyejifanya mlinzi na Mfadhili wa manabii wa Baali na Ashtorethi zama za Nabii Eliya(1Wafalme18:19).Ashtorethi alikuwa mungu mkuu mke wa Wafoeniki na Baali alikuwa mungu mkuu mume.
 Nani mungu mkuu mke-Ashtoreth? Gidion M. AREJEE SOMO HILI, ili wasomaji waelewe. Tunajifunza,Yezebeli alikuwa adui mkuu wa Eliya,Nabii wa Mungu, na alitaka kumuua Eliya. Hapa Yezebeli anafananishwa na mtu ama kikundi cha watu wanaotaka kuwaua watu kwa sababu wamekataa kuabudu Baal na Ashtoreth. Kwani  kuabudu dini ni lazima?Hata Mungu halazimishi.
 Yezebeli wa kanisani(Thiatira) anawaongoza waumini ‘kuzini’ yaani kula vitu vilivyotolewa dhabihu kwa masanamu(Ufunuo 2:20).
 Yezebeli alikuwa mke wa Mfalme Ahabu,aliyehamasisha Waisraeli wa kale kumwacha Mungu(hata sasa wamemwacha Mungu) na kuabudu Baali na Ashtoreth,kitu hiki huitwa uzinzi. Waisraeli wa sasa wanamwabudu Baali,mungu mume wa Ufoeniki na mungu mke ndiye Ashtoreth, na mataifa mengi watalazimishwa kumwabudu huyu,na wanamwabudu Ashtoreth hata katika siku kuu zijazo za Pasaka, Krismasi,MWAKA Mpya  n.k
 Wapendwa    wakristo,someni 1Wakorintho sura 8 MTAONA jambo hilo lililoanza kutokea AD 95. Uzinzi ni kumwabudu Kaisari,ni ibada ya sanamu, ibada ya sanamu ni kinyume na AMRI 10 ZA MUNGU,ni kinyume cha amri ya Pili(Kutoka 20:4-6).
   Tuijadili kidogo miungu hii.
Zeus,
mwaka 29 BC hekalu lilijengwa na Kaisari Augusto,LIKAWEKWA WAKFU kwa ajili ya Kaisari huko Pergamo,na mjini Rome sanamu hilo liliwekwa makau makuu ya Sinodi ya Kanisa.
Tumeona maofisa wa serikali ya Rumi wakilazimisha watu kumwabudu Kaisari has huko Pergamo. Huyu Zeus(Jupiter) sanamu lake lipo Olympia na ni moja ya MAAJABU SABA YA DUNIA.
 Huyu Zeus ni mfalme wa miungu na anaketi katika kiti cha enzi.Sanamu hili limejengwa mwaka 457 BC na linaabudiwa dunia nzima kwa njia anuwai.
 Utaona sasa Yezebeli wa leo akiwa amebebwa na Umoja wa Ulaya huko mjini Brussels,Ubelgiji, tunalazimishwa kumwabudu na kumtolea dhabihu. Yohana anasema Wafalme wa dunia wamezini naye na wafanyabiashara wamepata mali kwa nguvu ya kiburi chake(Ufunuo 18:1-3).
Unataka utajiri? Yezebeli ni jibu lako,utauza maua wakati wa siku kuu zake, utauza pombe kuliko wakati wowote, utauza miti ya Krisimasi n.k
 Nimegusa jiji la Rome lililojengwa miaka 2765 iliyopita, watawala wake maarufu sana ni Julius Caesar, Augusto, Tiberio, Gaius,Claudio,Nero,Galba, Vespasianus,Titus orodha ni ndefu.Hawa walitengeneza masanamu yao ili yaabudiwe. Hata masanamu ya Nyerere yapo mengi-hatujaambiwa kuyasujudia.
Freemasons ni hatari. Ugiriki imeathiri dunia nzima kwa maarifa yake,tamaduni zake, miungu yake na ustaarabu wake. Demokrasia imeanzia Ugiriki,lakini leo ni nchi masikini, wanapewa msaada na Eurozone!
Mataifa ya kiarabu yanazimwa yasiwe Super power. Afrika utajiri wake ullikwenda wapi? Niliwahi kuhoji,kwanini Ashanti isiendelee kuwa dola ya Ghana ya Mwafrika, eti siku hizi ni kampuni ya Mzungu ya kuchimba dhahabu hata hapa Tanzania?
 Unaweza kusema sisi ni mafala! Lakini, Babeli ama Iraki,Misri,       Wamedi na Waperizi na Wagiriki wako wapi?
 Nani alianza kuandika? Nani alianzisha hesabu? Viwanda vya kufua chuma havikuwa Afrika?
 Zbigniew Brzezinski,mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani enzi za Jimmy Carter alisimamia Mradi wa kutengeneza Virsi vya Ukimwi huko kilomita 75 kutoka Washington miaka ya 70.Lengo lilikuwa kupunguza watu duniani kwa sababu rasimali zinazidi kuwa chache.
Ukimwi ni silaha ya kupunguza idadi ya watu,chakula ni kidogo, watu wengi,makazi yanazidi Wazungu wamekwenda hata mwezini,Mars ili kutafuta nishati.
 Sasa,lazima kuwepo na mkakati wa siri kuwapunguza,wanaobaki ni wale watakaosujudu miungu yao-hawa ni mawakala wa shetani. Tutafanyeje? Mtafuteni Mungu wa kweli.
MWISHO.  
0786 324 074
 
 




Tuesday, March 6, 2012

utawala wa Freemasons katika Biblia takatifu


                           

JUZI, mashoga na wasagaji wa Afrika ya Kusini, walifanya tamasha la kukata na shoka ili kusherehekea haki zao; naam Haki za Binadamu !!
   Wanawake kwa wanawake na wanaume kwa wanaume waliooana Afrika ya Kusini, walikuwa wakisherehekea kwa kupigana mabusu ya tashtiti,kulembua macho na kulegezeana macho mabarabarani mchana kweupe!
  Naam, wao wanaita ilikuwa, ‘Gays Pride Festival’ na huu ndiyo uhuru ambao Marekani,Uingereza na washirika wao wa Ulaya wanataka tubadili katiba zetu na kuufuata,la sivyo hatupati msaada!
  Afrika ya Kusini,iliruhusu ndoa za mashoga mwaka 2006.
 Kituko kingine kinachodhihirisha uhai wa Freemasons na Ibilisi kuua watu kwa ajali za ndege,meli,milipuko ya maghala ya silaha kama ya Mbagala na Congo-Brazaville, ni kile cha yule ‘shushushu’ wa Libya, Basset Ali al-Meghri,kuhukumiwa kifo Januari 31 mwaka 2001,kwamba alilipua ndege ya Pan American  World Airways(Pan Am), halafu juzi wakaja kusema alionewa!
   Ilisemwa kwamba, ile ndege ya Marekani Flight 103 ya Pan Am  mwaka 1988 huko Lockerbie, Scotland, haikulipuliwa na akina Basset al-Meghri, walisingiziwa tu.
 Ulikuwa uongo,bila shaka wa Marekani na ‘Mkono wake msaidizi’ Freemasons, kutungua ndege ile na kuua mamia ya watu,kasha kutafuta ‘mbuzi wa kafara’ aitwaye kwa Kiingereza,  Scapegoat, ili kumtwisha dhambi ile,kwa lengo la kutaka kuishambulia Libya,kwamba iliwatuma hao magaidi!
 Ukitaka kujikomba kwa Ulaya na Marekani, utawala wa Marehemu Saddam Hussein ulitaka  ‘kufunika kombe mwanaharamu apite’ kwa kumkabidhi al-Meghri katika mahakama ya Uholanzi,ili akashitakiwe kwa sheria za uholanzi kwa kosa la kulipua ndege, kosa ambalo leo tumeambiwa hawakulifanya hata chembe!
  Ilikuwa Aprili 5 mwaka 1999 utawala wa Gaddafi ulipomkabidhi al-Meghri,ili kuepuka kipigo cha mbwa mwizi kutoka Marekani na washirika wake.
 Utaona,kumbe Freemason wanapoua watu kwa ajali za ndege,boti,moto na meli, halafu anasingiziwa mtu Fulani, anafungwa jela ama anauliwa-hatujasahau uongo kwamba Irak kulikuwa na silaha za maangamizi,kumbe umbeya tu.
  Al-Meghri ameachwa huru na yuko Libya ambako anagugumia maumivu ya saratani, katika kitanda cha mauti akisubiri mauti yanayomkodolea jicho la bashasha.
  Ndivyo dunia inayotawaliwa na Ibilisi ilivyo-Libya yenye utajiri wa mafuta, taifa la kale la Waberiberi, iliwahi kutawaliwa na Kathago, Rumi, Wavandali na Utawala wa Ottomans.
   Italia, iliitawala Libya tangu mwaka 1912. Uingereza na Ufaransa waliitawala Libya baada ya Vita vya Pili vya Dunia; ikapata uhuru wa bendera Januari Pili mwaka 1952,kisha Muammar Gaddafi akaja kupindua mwaka 1969.
  
                                 FREEMASONS NA UTAJIRI WA MAFUTA
Nataka kusema kwamba,Ulaya wameitawala Libya,wanajua utamu wa utajiri wake wa mafuta. Ulaya na Marekani ndiyo wenye makampuni makubwa, “Supermajors” ya mafuta hapa duniani.
 Utawala wa Gaddafi ukitaka kubinafsisha mafuta yote yawe kwa maslahi ya Walibya, ooh…wakamkosea Mzungu. Freemasons wanatafuta kumiliki chumi za dunia nzima na mafuta ni ‘damu’ inayobeba uhai wa dunia na mataifa yao.
  Siku nyingine nitajadili jambo hili kwa kina.
 Sasa, twajua kwa nini Freemasons waliingiza Libya katika Mhimili wa Uovu(The Axis of Evil) wapate kuishambulia na kumuulia mbali Gaddafi na wapinzani wa sera zao.
 Na kwa misingi hii hii tujue kwa nini Iran itashambuliwa baada ya Marekani kukamilisha Uchaguzi Mkuu,Novemba mwaka huu.
  Uingereza, Ujerumani, Hispania, Ufaransa, Italia, Ureno, Uswisi hawa ni vichwa saba katika mnyama wa Ufunuo 13, ufunuo 17, Danieli 7.
   Marekani, ni mwanakondoo wa Ufunuo 13:11-18 na hawa wote wanahaha kuhakikisha wanafanya kampeni kali na propaganda kupitia mashirika yao ya habari yenye nguvu duniani, kuwapaka matope watu wasiopendwa,ili wapinduliwe kijeshi na AJENDA YAO YA SIRI itekelezwe.
  Katika unabii wa Biblia, katika kitabu cha Danieli 2:43 mataifa haya ya Ulaya yameoneshwa yakiwa yanabebwa na historia ya iliyokuwa Dola ya RUMI.
  Mataifa haya hufananishwa na vidole vya sanamu ya Nebuchadnezzar, katika sura ya Pili ya Danieli. Ni sawa na pembe 10 za mnyama wa ajabu ambaye ni Rumi katika Danieli 7:7.
 Hizi dola 10 za Ulaya, zilizoinuka baada ya dola ya Rumi, zina tabia ile ya Rumi ya Washenzi wa kale(Danieli 7:24).
 Pembe ndogo(Danieli 7:24,25) ni nguvu isiyo mamlaka ya kisiasa ambayo ilizifukuza Ulaya tawala tatu za Wavandali, Waheruli na Ostrogoths. Nguvu hii ilianza kuitawala Dunia mwaka 538 AD.
   Huu ndiyo utawala uliohuishwa baadaye na utaitawala dunia nzima na kulazimisha watu kuuabudu(Danieli 7:24,25).
 Utawala huu utapewa mamlaka na shetani na mawakala wake,Freemasons,Illuminati,Marekani na washirika wake wa Magharibi, wataunganisha siasa na dini, watalazimisha Mfalme aabudiwe, watakaokataa watawekewa vikwazo vya kiuchumi, watafungwa jela ama kuuliwa.
 Sasa, demokrasia wanayojidai kueneza iko wapi? Kama watu watalazimishwa kuabudu dini moja, wakikataa wanafungwa, mtu kwa kuwa ni mtawala anajiita Mungu(Danieli 7:25 na Ufunuo 13:1-10) ndiyo demokrasia gani hii?
  Utawala uliozuka baada ya dola ya Rumi kusambaratishwa na washenzi wa Kaskazini, ukafukuza dola tatu za Wavandali(mwaka 454 AD),Heruli(493 AD) na Ostrogoths(538 AD) na kuanza kutawala dunia kwa jumla ya miaka 1260.
  “Pembe Ndogo” yenye macho kama mtu mwanaume, huwakilisha mamlaka itakayoongoza serikali ya Dini na Siasa-  Religio-Political Power.
   Mtawala huyu anaitwa, ‘Mpinga Kristo’ ama Chukizo la Uharibifu lililonenwa na Nabii  Danieli(Mathayo 24:15).
 Katika Ufunuo wa Yohana 17: 5 upo mfano wa utawala huu wenye nguvu na wa ina yake unaoandaliwa kuitawala dunia,kidini,kiuchumi,utamaduni na kila nyanja.
  Yohana wa Ufunuo wa Yohana 17:5 ,katika mwaka 96 AD alioneshwa  utawala huu wa mseto wa dini na siasa.
  Akaoneshwa Jiji liitwalo “Babeli ya Siri” likiwa limebebwa na malaka(mnyama) za serikali za Ulaya na Marekani.
Babeli, ni Jiji la kale sana, zama za Dikteta Nebuchadnezzar, mwaka 6060 BC. Siku hizi, Babeli ni moja ya Maajabu saba ya Dunia,kutokana na utajiri wake wa dhahabu ulioporwa katika mahali walikopindua na kuua, bustani zenye kuning’inia katika kuta ndefu zenye futi za mraba 400.
Bustani hizi zilikuwa juu kutani kiasi cha futi 75 kutoka ardhini.
 Hii ni nchi ya Wakaldayo wa zamani waliokula nguruwe na kunywa mvinyo kwa wingi. Na kabla ya kula vyakula hivi vya kitajiri, walivitoa sadaka kwa miungi yao mikuu, Bel na Murdoch.
 Danieli na vijana wenzake wa Kiebrania waligoma kula chakula hiki na pombe zilizotolewa dhabihu kwa miungu kabla ya kuliwa eti ili kumfanya mlaji awe na nguvu za miungu hii mwilini mwake!
 Wakasema, kula nguruwe hizi na kunywa pombe ilikuwa kujitia unajisi na chakula cha Mfalme(Danieli 1:1-8).
  Babeli, mabaki yake yangalipo hata leo huko kando ya Mito miwili ya Tigris na Euphrates, mchangani-na unaweza kufika kwa treni, ni eneo la utalii siku hizi, sasa ni makao ya mashetani na ndege wachafu kama popo, bundi n.k
   Jiji hili la siri  hufananishwa na mwanamke, katika Ufunuo wa Yohana 17:5-9.
Hata jiji la Mwanza, huitwa, “Jiji-Dada” la Wurzburgh, Ujerumani. Kumbe mji hupewa heshima ya mwanamke?
  Babeli wa mafumbo katika Ufunuo 17:5-9 ni Jiji la Siri, litakalobebwa na Ulaya siku za karibuni,ili kuua watu watakaokataa kumsujudia shetani na Freemasons-ndiye mtawala atakayefuata baada ya Marekani na washirika kuitiisha dunia.
  Mwanamke huyu, “Babeli” ndani yake kuna waabuduo sanamu, wala nguruwe,walevi, waabudu jua na mfumo wa sayari zote, wenye imani za kuongea na mizimu(spiritualism) n.k
 Mwanamke huyu, amezaa watoto, anaitwa ‘MAMA WA MAKAHABA’ na machukizo ya nchi.
 Katika Biblia, ukahaba ni pale watu wa Mungu wanapo anza kuungana na waabudu sanamu na miungu,ulevi, ibada ya mizimu na uongo na kuacha usafi na kicho kwa Mungu muumbaji(Hosea 1:2)
  ‘Uzinzi’ ni kumwacha Mungu na kuabudu sanamu na miungu(Hosea 1:2). Mji huu Babeli, katika Ufunuo 17:3-11 unabebwa na Ulaya na Marekani, “SUPER POWERS” zenye nyuklia na uchumi mkubwa na wana sera moja.
 Iran watapigwa na Marekani, Israeli na Ulaya kwa sababu wakiachwa, wakawa na Nyuklia,watapinga kuibeba Babeli hii!!
 Mji huu Babeli wa siri una ‘Meya’ wake anajiita Mungu duniani na ahera, VICARIUS FILIIDEI na nyumerali hizi za Kirumi huwakilisha nambari 666.
  Mji dada wa Babeli umebeba kikombe cha ulevi wa mafundisho,ndiyo propaganda za uongo duniani,ni uchafu katika imani ya kidini,Kiislam,Kiyahudi ama Kikristo.
  Mji huu Babeli uliua wapinzani wake,maana ulikuwepo zamani,mwaka 538-1798 AD.Ulikoma Feburuari 10 mwaka 1798 baada ya miaka 1260 ukawa mwisho wa Dark Ages.
  Mwanamke huyu ambaye ni ‘Mji Dada’wa Babeli ya kale, wakati wa Nabii Yohana akiandika kitabu cha Ufunuo(mwaka 96 AD) haukuwepo, na ukafufuka toka kuzimu Feburuari 11 mwaka 1929 AD.(Ufunuo 17:8-9)
 Mji dada wa Babeli uko juu ya milima saba. Mji ulikoko katika vilima saba Ulaya! Tazama Ufunuo 17:9 UONE SIRI hii, na milima saba pia huwakilisha falme saba za kale, Babeli, Wamedi na Waajemi katika serikali ya mseto, Wagiriki, Rumi ya kipagani, Rumi ya Kikristo, Pembe Ndogo na Serikali Mpya duniani yenye Dinina siasa(Ufunuo 17:9-11)
 Naam, Marekani na washirika wanajiandaa kuleta duniani dini mpya ya muungano wa Freemasons,Illuminati n.k
Ni mfumo wa dini(system of religion) ambao ni bandia. Bidhaa bandia(counterfeit) zinaigiza zile bidhaa halisi.Bidhaa feki hufanana na feki, lakini ubora wake ni duni na utazitambua kwa alama yake ya biashara-trade mark- kwa mfano bidhaa feki za Panasonic huitwa,Panasoanic,hukosa ubora wa Panasonic,tujihadhari!
  Dini counterfeit ina alama(ALAMA YA MNYAMA) mnyama ni mpinga Kristo yaani utawala bandia wa Kristo Duniani.(2Wathesalonike 2:3-4).
 Kwa kawaida utawala wa Mungu siyo wa kidunia, kwa nini dini zianze kuwaandama akina Kikwete na kutaka kuwapindua kwa kampeni kali makanisani?
   Utawala bandia wa YESU unapinduaje serikali za dunia wakati utawala wake uko mbinguni?
 Utawala wa Mungu utaanzaje kuua watu wanaoupinga hapa duniani? Ufunuo 13 na 17 hutwambia kwamba dini feki itaua watakaoipinga na ulishaua zamani wapinzani zaidi ya milioni 50 yaani zaidi ya waliokufa wakati wa vita kuu ya kwanza nay a Pili.
   Mnyama yaani Mpinga Kristo ni mtawala bandia wa dunia hii(2 Thesalonike 2:3-4)
 Mpinga Kristo anajifanya Mkristo(1Yohana 2:18,19)Wapinga Kristo hutokea miongoni mwa wakristo, na wana tabia kama za Babeli ya zamani,ulevi, ibada ya sanamu,ulaji wa nguruwe,kiu ya utawala duniani, ibada ya jua nyota na sayari n.k
  Wapinga Kristo wameacha Injili na kuhubiri siasa makanisani,ili kuwapindua viongozi waliopo kote duniani-wanajidai kuhamasisha demokrasia, na hujihusisha sana na ushoga,ulawiti na ufisadi wa kiroho,ingawa wao hukazania sana watu waache ufisadi!!
  Mpinga Kristo ndiye Pembe Ndogo ya Danieli 7:25 na ni mnyama wa Ufunuo 13:1-10. Mfumo wa Ibada bandia, humbeba Mpinga Kristo wa Ufunuo 13,17 Danieli 7:25 na 2Thesalonike 2:2-4.
 Msomaji mmoja akanitumia SMS iliyoandikwa:
  “ North Korea na itikadi yao ya Kikomunisti watakubali kwelikuwa Allied(kuungana) na Magharibi? Nina wasiwasi watakuwa upande wa Russia na China ili kuitetea Iran! Pia nilitaka kuweka kumbukumbu sawa katika makala ya Gidion M kuhusu Jewish Revolution ni 1948 na siyo 1848”.
  Iran lazima washambuliwe kijeshi,baada ya uchaguzi mkuu wa Mareni Novemba mwaka huu,la sivyo Israeli na Ulaya watachukua jukumu hili wenyewe?
  Waziri Mkuu Benyamin Netanyahu hivi niandikapo yuko Washington kuomba kibali ili kuishambulia Tehran. Obama anaogopa kuiingiza Marekani vitani wakati huu wa karibia uchaguzi mkuu.
 Hata hivyo, imetangazwa kwamba Korea Kaskazini wamepewa msaada wa chakula ili waachane na mradi wao wa Nyuklia wa Yongbyon.
  Nimemwona juzi, Hillary Clinton akiwa Pyongyang kuzungumza na yule rais kijana wa Korea,baada ya kifo cha babaye, Kim Jong Il.
  Korea imeshatiwa kabali,haina tena ubavu wa kuipinga Marekani na washirika wake na haina kitu,itaachana na mradi wa nyuklia na kuruhusu wakaguzi wa silaha wa Umoja wa Mataifa ambao ni mawakala wa CIA, Mossad n.k
 Maskini Tehran wameachwa kwenye mataa,na watashambuliwa peke yao baada ya mudfa mfupi ujao,ili kuandaa njia kwa Freemasons kuunda mfumo wa dini na siasa duniani.
Itaendelea
 0786 324 074