Tuesday, September 17, 2013

CARLOS THE JACKAL



 
Nianze kujadili kidogo kuanguka kwa ukuta wa Berlin mwaka 1994,kwamba kuliashiria kumalizika kwa VITA BARIDI,baada ya Vita vikuu vya Pili vya Dunia 1945.
 Kumalizika kwa vita Baridi,vilivyoanza baada ya vita vya pili kwisha, maana yake ni kuufagilia mbali UKOMUNISTI.Dola la Urusi la Kisovieti(USSR) liliparaganyika tangu mwaka 1991.
Ukuta wa Berlin ulioitenga dunia katika Mihimili miwili ya Magharibi na Mashariki ulishavunjwa na kuifanya dunia kuwa kama kijiji kimoja. Kuanguka kwa Ukuta wa Berlin na Kuparaganyika kwa Dola la Kisovieti la Urusi(USSR) ni kuonesha kwamba ubepari ulikuwa umeushinda ujamaa duniani.
 Tunaishi katika zama za MWENYE NGUVU MPISHE.Kuanguka kwa ukuta wa Berlin na UKOMUNISTI maana yake ni kwamba “Mto Frati” uliokuwa ukiitenda dunia ya zama za Waisraeli kati ya Mashariki na Magharibi, ulikuwa umeanza ‘kukaushwa’.
Mchakato wa kukaushwa maji ya Mto Frati(the dries up process of the River Euphrates) ulishaanza,ili njia itengenezwe wafalme watokao nji za Mashariki(UCHINA,INDIA,JAPAN n.k) wapite na kwenda kuungana na madola ya Magharibi. Tumeona mataifa ya Kisovieti yakijiunga NATO na Umoja wa Ulaya EU.
 Tumeona, Uchina,Urusi, Japan,Korea Kusini,Pakistan,India n.k wakishirikiana na Mataifa ya NATO hata kutoa ardhi zao kwa majeshi ya NATO na mashirika ya kijasusi kama CIA na MOSSAD kutekeleza Operesheni anuwai za kijeshi.
Tumeona nchi za Kiarabu zikigeuza ardhi zao kuwa Base za kijeshi za Marekani na washirika wake, tunaona juhudi za mataifa ya Mashariki hata kujiunga umoja wa sarafu moja ya Euro-Euro Zone , tunaona juhudi za Mashariki kushiriki Soko la Pamoja Ulaya European Common Market n.k
 Ufunuo 16:12-16 huonesha wazi kwamba nchi za Kisovieti na zingine za Mashariki na mrengo wa kijamaa, zitaungana na Ulaya na Marekani, na zitaachana na imani zao na ibada zao na kwenda kuungana na roho za  mashetani, za Freemasons na Illuminati,ndiyo ROHO ZA VYURA na manabii wa Uongo(Ufunuo 16:13-16)
 Har-Magedon, ni vita dhidi ya Mungu na Amri 10. Mataifa yote ya Dunia yataungana ili kumpinga Mungu,yataungana na Ibilisi kwa misingi ya kusaka uhuru na demokrasia.Pepo wachafu wataungana na wanadamu ili kukataa mafundisho ya Mungu na maagizo yake,wanaanzia kwenye kanuni za ndoa na imani ya kweli.
 Dunia nzima itaungana kiuchumi,kisiasa, na wale waliokuwa na itikadi za Carl Marx(Marxists) wataondolewa kwa nguvu kubwa.
Hadithi ya Illich Ramirez Sanchez(Carlos The Jackal) inatuonesha namna hawa Wa-Marx walivyoshindwa na ubepari.
Carlos The Jackal(63) alizaliwa Caracas,Venezuela mwaka 1949.
Babaye alikuwa mfuasi wa siasa za Karl Marx akawahusudu mno wanamapinduzi wa Amerika Kusini: Carlos Merighella, Camillo Torres na Che Guevara.
Carlos, ni mfano wa Osama bin Laden wa zama hizo, alipinga ubeberu wa Magharibi kwa njia ya nguvu za kigaidi,Mungu hataki kutumia njia hizo ili kuleta haki duniani.
 Alisoma katika Chuo cha kijeshi cha Mantanzas huko Havana,Cuba na akatokea kuwa Komandoo kutokana na walimu wa medani za kijeshi wa                   Urusi.
 Babaye hakumwamini Mungu na mamaye alikuwa Mkatoliki,wakaachana. Carlos alikwenda London, baadaye akapelekwa kkusoma katika Chuo Kikuu cha wanamapinduzi cha Patrice Lumumba,huko Moscow.
 Carlos, alikuwa ‘troublemarker’ dhidi ya maslahi ya mabeberu wa Magharibi. Akajiunga na Chama cha Popular Front for The Liberation of  Palestine(PFLP) Wakateka nyara watu na ndege za Magharibi ili kudai uhuru wa Palestina.
 Carlos, alijiunga na PFLP mwaka 1970 akapewa jina la Carlos kwa sababu ya asili yake ya Venezuela, Amerika ya Kusini.
 Aliitwa, The Jackal na gazeti la The Guardian la Uingereza kufuatia kisasiri(novel) cha Mwandishi Fredrick Forsyth.

 Nianze kujadili kidogo kuanguka kwa ukuta wa Berlin mwaka 1994,kwamba kuliashiria kumalizika kwa VITA BARIDI,baada ya Vita vikuu vya Pili vya Dunia 1945.
 Kumalizika kwa vita Baridi,vilivyoanza baada ya vita vya pili kwisha, maana yake ni kuufagilia mbali UKOMUNISTI.Dola la Urusi la Kisovieti(USSR) liliparaganyika tangu mwaka 1991.
Ukuta wa Berlin ulioitenga dunia katika Mihimili miwili ya Magharibi na Mashariki ulishavunjwa na kuifanya dunia kuwa kama kijiji kimoja. Kuanguka kwa Ukuta wa Berlin na Kuparaganyika kwa Dola la Kisovieti la Urusi(USSR) ni kuonesha kwamba ubepari ulikuwa umeushinda ujamaa duniani.
 Tunaishi katika zama za MWENYE NGUVU MPISHE.Kuanguka kwa ukuta wa Berlin na UKOMUNISTI maana yake ni kwamba “Mto Frati” uliokuwa ukiitenda dunia ya zama za Waisraeli kati ya Mashariki na Magharibi, ulikuwa umeanza ‘kukaushwa’.
Mchakato wa kukaushwa maji ya Mto Frati(the dries up process of the River Euphrates) ulishaanza,ili njia itengenezwe wafalme watokao nji za Mashariki(UCHINA,INDIA,JAPAN n.k) wapite na kwenda kuungana na madola ya Magharibi. Tumeona mataifa ya Kisovieti yakijiunga NATO na Umoja wa Ulaya EU.
 Tumeona, Uchina,Urusi, Japan,Korea Kusini,Pakistan,India n.k wakishirikiana na Mataifa ya NATO hata kutoa ardhi zao kwa majeshi ya NATO na mashirika ya kijasusi kama CIA na MOSSAD kutekeleza Operesheni anuwai za kijeshi.
Tumeona nchi za Kiarabu zikigeuza ardhi zao kuwa Base za kijeshi za Marekani na washirika wake, tunaona juhudi za mataifa ya Mashariki hata kujiunga umoja wa sarafu moja ya Euro-Euro Zone , tunaona juhudi za Mashariki kushiriki Soko la Pamoja Ulaya European Common Market n.k
 Ufunuo 16:12-16 huonesha wazi kwamba nchi za Kisovieti na zingine za Mashariki na mrengo wa kijamaa, zitaungana na Ulaya na Marekani, na zitaachana na imani zao na ibada zao na kwenda kuungana na roho za  mashetani, za Freemasons na Illuminati,ndiyo ROHO ZA VYURA na manabii wa Uongo(Ufunuo 16:13-16)
 Har-Magedon, ni vita dhidi ya Mungu na Amri 10. Mataifa yote ya Dunia yataungana ili kumpinga Mungu,yataungana na Ibilisi kwa misingi ya kusaka uhuru na demokrasia.Pepo wachafu wataungana na wanadamu ili kukataa mafundisho ya Mungu na maagizo yake,wanaanzia kwenye kanuni za ndoa na imani ya kweli.
 Dunia nzima itaungana kiuchumi,kisiasa, na wale waliokuwa na itikadi za Carl Marx(Marxists) wataondolewa kwa nguvu kubwa.
Hadithi ya Illich Ramirez Sanchez(Carlos The Jackal) inatuonesha namna hawa Wa-Marx walivyoshindwa na ubepari.
Carlos The Jackal(63) alizaliwa Caracas,Venezuela mwaka 1949.
Babaye alikuwa mfuasi wa siasa za Karl Marx akawahusudu mno wanamapinduzi wa Amerika Kusini: Carlos Merighella, Camillo Torres na Che Guevara.
Carlos, ni mfano wa Osama bin Laden wa zama hizo, alipinga ubeberu wa Magharibi kwa njia ya nguvu za kigaidi,Mungu hataki kutumia njia hizo ili kuleta haki duniani.
 Alisoma katika Chuo cha kijeshi cha Mantanzas huko Havana,Cuba na akatokea kuwa Komandoo kutokana na walimu wa medani za kijeshi wa                   Urusi.
 Babaye hakumwamini Mungu na mamaye alikuwa Mkatoliki,wakaachana. Carlos alikwenda London, baadaye akapelekwa kkusoma katika Chuo Kikuu cha wanamapinduzi cha Patrice Lumumba,huko Moscow.
 Carlos, alikuwa ‘troublemarker’ dhidi ya maslahi ya mabeberu wa Magharibi. Akajiunga na Chama cha Popular Front for The Liberation of  Palestine(PFLP) Wakateka nyara watu na ndege za Magharibi ili kudai uhuru wa Palestina.
 Carlos, alijiunga na PFLP mwaka 1970 akapewa jina la Carlos kwa sababu ya asili yake ya Venezuela, Amerika ya Kusini.
 Aliitwa, The Jackal na gazeti la The Guardian la Uingereza kufuatia kisasiri(novel) cha Mwandishi Fredrick Forsyth.


                                     CARLOS THE JACKAL (muendelezo)
Katika mfululizo wa makala hizi,tumemfahamu  Ilich Ramirez Sanchez(Carlos) kwamba alikuwa mwanaharakati wa kupambana dhidi ya maslahi ya Magharibi zama za Vita Baridi.
Aliungana na wanaharakati wa Kipalestina(PFLP) kupambana dhidi ya maslahi ya Magharibi na wajomba zao,Israeli.
Carlos Tha Jackal alisoma katika Chuo Kikuu cha Patrice Lumumba Jijini Moscow,Urusi ambako alikutana na wanafunzi wengi wanamapinduzi kutoka nchi mbalimbali,miongoni mwao Wapalestina.
Wakati mwingi Carlos aliungana na wanafunzi wa Kipalestina; na lipigana na Wapelistina bega kwa bega katika vita vya kuikomboa nchi yao na ubeberu wa Kizayuni wa Kiisraeli.Wapalestina walitafuta uhuru wan chi yao kwa mapambano ya kigaidi dhidi ya Israeli na Madola Makubwa ya Magharibi.
Hivyo,tukio la kushambuliwa wanariadha wa Israeli katika kijiji cha Olimpiki huko Munich,Ujerumani Septemba 5,mwaka 1972 inahisiwa Carlos ndiye aliyesuka mpango huo wa hatari sana ulioacha historia hapa duniani.
 Ni  Septemba 5, mwaka 1972, Michezo ya Olimpiki ilipovamiwa na Magaidi wa Black September,Ilikuwa kama ifuatavyo:
ASUBUHI,Septemba 5 mwaka huo 1972, mashindano ya Olimpiki ya majira ya kiangazi yaliendelea kama kawaida.
Kulikuwa na wanariadha 12,000 wa mataifa anuwai wakiwa na maofisa wao.Israeli nayo ilituma wanariadha na maofisa wake,ingawa ilijua ilikuwa inawindwa sana na magaidi wa Kiarabu kwa nia ya kulipa kisasi.
Israeli iliomba ulinzi mkali sana kwa serikali ya Ujerumani.Wakati huo, Magaidi wa Kiarabu-The Black September- wakihofiwa sana hapa duniani.Walikuwa na wanachama wao miongoni mwa wanafunzi waliokuwa wakisoma katika vyuo anuwai vya Ujerumani Magharibi zama hizo.
Hata hivyo, kulingana na Shirika la Ujasusi la Israeli(Mossad) mafunzo ya Mpango Mkakati wa kuivamia michezo ya Olimpiki hapo Munich,ilifanyika Syria huko ambako sasa akina Obama wanapanga kuvamia,kupindua na kumuua Bashar al –Assad.
Kabla ya juma la Olimpiki kuanza,Makmandoo wa Kipalestina waliwasili mjini Munich,kila mtu kivyake,lakini kwa njia ya treni.
Walifika Ujerumani na bunduki hatari za Kirusi,SMG na Kalashnikov-47 inayoitwa kwa kifupi, AK-47.Bunduki hiyo ilitengenezwa mara ya mwanzo na Kalashnikov katika mwaka 1947 ikaitwa namna hiyo.
Duru za kipelelezi zilizotua katika ukurasa huu zinasema, walipewa vibarua katika kijiji cha Olimpiki, wakidhani ni watu tu wa kawaida.Kulikuwa na wafanya kazi 30,000 hivi katika kijiji cha Olimpiki.
Naam, ilikuwa saa 10 hivi Alfajiri,Waarabu wakafika mahali hapo kutekeleza Mpango wao wa kuwateka nyara wanariadha wa Kiisraeli kwenye mabweni walimolala,ili kulipa kisasi kwa adui zao hawa.
Wafanya kazi wa kijiji hicho cha Olimpiki walikwishaamka alfajiri hii.Walikuwa raia wawili wa Kijerumani waliowaona Waarabu wakija kutekeleza Mpango huo wa kuvamia kijiji cha Olimpiki.
Walivalia jezi za kimichezo na walifanana sana na wanamichezo.Walivuka uzio wa kijiji hicho,tena walibeba zana za kimichezo.
Hakuna aliyewatilia shaka kwa jinsi walivyokuwa; maana ilikuwa kawaida sana kwa     wanamichezo kuandoka usiku na kwenda mjini kufanya mazoezi kasha kurejea baadaye.
Hata hivyo, hawa Makomandoo wa Kiarabu-Black September- walijipaka masizi ama mkaa wakawa Weusi tii,ili wasifahamike.Walibeba silaha haraka sana kuelekea mabweni ya wanariadha wa Israeli.
Wanariadha 22(wanaume) wa Israeli,makocha na viongozi wao walikuwa wakiishi katika mabweni matatu.Hao adui zao wakabisha mlangoni kwa upole utadhani watu wazuri sana!
“Humu ndimo ilimo timu ya Israeli?” wakasaili kwa sauti ya kiungwana hivi.
Moshe Weinberg(32),Kocha wa mieleka akafungua mlango.Hamadi!!
Akakutana na wanaume wa kazi wakiwa na SMG,AK-47 na maguruneti mikononi.Akarudi nyuma mkuku.
Weinberg, alipigwa riasasi ya SMG iliyotokea mlangoni.Gad Sabari, mwanamasumbwi alipoona wameingiliwa na Waarabu,akavunja dirisha, akaamka kitandani na kujaribu kuchupa ili akimbie.Tyari mvua kubwa ya risasi ikampata masikioni.
Mapambano ya Black September yalipamba moto dhidi ya adui zao Waisraeli hapo jijini Munich.
Katika jingo linguine, mnyanyua vizito,Yosef Romano, akiwa kisu mkononi alijaribu kupambana nao hawa ‘Intruders’, alijeruhiwa vibaya, akatabawali.
Yosef Gottfreund,refa wa mieleka alisukuma mlango ili kuwazuia wasiingie ndani,aliwasukuma watano wakaanguka sakafuni, halafua kasema “Hevra tisalku!” Haya kimbienii!
Waliusukuma mlango ule ukawa umejifunga tena.Waisreli wawili kati ya wale 22 hawakuwemo mabwenini wakati vrangati likitokea.Tisa kati yao walitimka mbio,visigino kisogoni,wakafanikiwa kujiokoa.
Mbali na Romano na Weinberg,wenzao hawakupona kabisa.Walitiwa mbaroni,wakafungwa mikono na miguu kwa kamba,watatu-watatu walifungwa wakasukumizwaili walale kitandani!
Polisi wa Munich walistuliwa na mtu aliyewapigia simu wakaja wanahema-hema.Walifika katika kijiji hicho cha Olimpiki saa 11 hivi alfajiri.
Naam,vita kati ya Black September na Waisraeli vilikuwa vimeanza mjini Munich. Polisi wamefika wakakuta tayari Waisraeli wametiwa chini ya ulinzi ndani ya Bweni,polisi wakifanya uzembe magaidi wale wanawalipua haraka na kutokomea!
Sasa polisi wamefika mahali hapo. Kutatokea nini?
Usikose toleo lijalo!




  •  



  •  

Friday, September 13, 2013

HONGERA KENYA KUKATAA UKOLONI WA MZUNGU ICC


                          
Nalazimika kurejea sehemu ya makala yangu iliyokuwa nakichwa cha habari, “AFRIKA KIZIMBANI”,ili kujaribu kuzibua akili zilizoziba za Watanzania ‘Fuata Upepo” kwa kila kinachosemwa mitaani!
Makala hiyo iliyotwaliwa katika Jarida maarufu sana, New African la Julai, 2012 iliyokuwa na kichwa cha habari, “Is Africa on Trial?’
Kulikuwa na kichwa kidogo(sub heading), “The Role of the ICC(International Criminal Court) examined”.
Julai Mosi, mwaka 2012, Mahakama hii ya Kimataifa(ICC)ilikuwa inatimiza umri wa miaka 10;sasa ina miaka 11,wengine wanaota ilikuwepo miaka milioni nyingi,Afrika tu sasa inajifaragua kutaka kujiondoa katika mahakama hiyo!
Nataka wenye akili baridi wasidhani ilikuwepo zamani wakati Adamu na Hawa wanaumbwa Edeni,mwaka 4000 BC.
Ni mahakama iliyoishi kwa muongo mmoja,kufuatia Mkataba wa Rome, wa 2002.Nchi nyingi za Afrika zilijiingiza kichwa-kichwa katika uanachama wa mahakama hii,kufuatia Senegal kuwa mwanachama wa mwanzo.
Kuna akili mgando zinazoweza kusema Afrika haiwezi kuanzisha Mahakama kama hii hapa ikatoa haki,kwa sababu viongozi wetu-Madikteta- hawana Political Will-utashi wa kisiasa wa kuwa na haki na demokrasia!
Wanasema Afrika ndiyo nyumba ya utawala mbaya,rushwa na mauaji.Huu ni umbumbumbu wa kutojua dunia nzima hii hakuna haki wala uhuru na demokrasia,sembuse Afrika?
Kasumba ya Kikoloni(colonial mentality) imewaibia akili Waafrika kudhani hakuna haki na maendeleo kama hakuna Mzungu! Hawa ni watumwa wa hiari.Wanatimiza unabii wa akina Hitler,Botha na Makaburu wengine wabaguzi wa rangi.
Sasa angalia wewe msomaji mwenye akili.Hata sasa  wendesha Mashitaka Mkuu wa ICC,Fatou Bensouda,toka Gambia,Afrika Magharibi,ni Mweusi tena mwanamama.
Waafrika Weusi wanashika ‘Key Positions’ katika Mahakama hiyo ya The Hague,Uholanzi(kumdanganya Mwafrika);kwanini Umoja wa Afrika(AU) isianzishe Mahakama yake,Nairobi,Arusha,Abuja ama popote?
Afrika haiwezi kuwatia kabala Madikteta na wauaji wanaofanya vita hapa Afrika? Najua vita nyingi Mwafrika hutumiwa kama kinyangarika ili kutekeleza maslahi ya Mzungu,halafu lawama hubeba yeye mgongoni.
Kufuatia ujinga wa Mwafrika,hata hao akina Bensouda huko ICC huendesha mashitaka na kutoa hukumu inayolinda maslahi ya Mzungu na aslani siyo Mwafrika!
Mahakama za Umoja wa Mataifa kama ile ya Sierra Leone,ya Mauaji ya Rwanda(ICTR) na ile ya mjini Hague(ICC) ati hushughulikia mauji ya Kimbari-genocide-na matendo yaliyokinzana na haki za binadamu na uhalifu wa kivita.
Sasa tafakarini:Paul Kagame(rafiki wa Marekani) aliua         marais wawili,Juvenal Habyarimana wa Rwanda na Cyprian Ntaryamirwa wa Burundi,Aprili 6 mwaka 1994.
Ana kesi inayomkabili?
Kagame akiongoza Waasi(rebels) wa RPF aliua maelfu ya watu raia wa Rwanda hadi Wahutu wakaanzisha Intarahamwe ili kulipa visasi,kwa kuwa wao  ni wengi.
Kosa la Kagame halikutazamwa kuwa ni kosa,kosa Wahutu kulipa kisasi!
Pili,Kagame hakuingia Kongo na kupigana vita(kuua) ili kuwateketeza Waasi wa Intarahamwe? Kuvuka mpaka na kuingia nchi ya KONGO siyo kosa katika Jumuiya ya Kimataifa? Ama hakuna ushahidi The Hague!
Kuwatafuta waasi wa Kihutu ndani ya Kongo na kuwaua,bila kuwafikisha mahakamani,ndiyo nini?
Kagame Mtu-tsi,anapowasaka Wahutu na kuwaua ni nini kama siyo genocide?
Siyo, crimes against humanity? Siyo, war crimes?
Kagame na rafikiye Museveni wanawasaidia Waasi wa Kongo(M23,Bosco Ntaganda,Jen. NKUNDABATWARE n.k hii nini?
Wewe unawasaka waasi wa  nchi yako ndani ya ardhi ya nchi nyingine, unaona uasi ni unyama unastahili adhabu kali ya kifo,wakati huo huo unawaunga mkono waasi wan chi ya jirani na kuwalea!
Ukiambiwa kuzungumza nao ‘peace talk’ au ceasefire agreement, unakuwa mkali unatukana watu! Hii nini sasa?
Hiyo ndogo, wewe unaingia nchi ya watu na rafiki yako,mnapora madini,mbao,pembe za ndovu n.k mnaanza kupigana ndani ya nchi ya watu,mnabaka akina mama,mnaua watoto kwa risasi,halafu Wakongo wakisema,mnasema mnawatafuta Intarahamwe!
Mbona ICC haijaona kosa la Museveni na Kagame,hata kama Jaji wa Ufaransa,Jean Louis Bruguire ,alisema Kagame akamatwe na kupelekwa Arusha,baadaye wakasema ana Diplomatic Immunity?
Sasa tujiulize, Omar Hassan Ahmad al Bashir wa Sudan,siyo Rais? Hana diplomatic Immune? Mbona anasakwa akamatwe hadi akakimbia Nigeria juzi,kwa kuwa Nigeria ni mwanachama wa Icc?
Hivi makosa ya hawa wote,hayafanani na makosa ya Bush na Blair kwenda kuipiga Irak na Libya na kumuua Saddam na Gaddafi,bila ridhaa ya Umoja wa Mataifa?
Hiyo nini kama siyo Impunity? Yaani mtu anafanya makosa mabaya, anaachwa bila kushitakiwa mahakamani!
Sasa upendeleo mnaosema madikteta wa Afrika wakianzisha ICC, Addis Ababa itakosa shabaha,hamwoni kitu hicho hata sasa? Mna makengeza!
Sasa akina Obama wanakwenda Syria(nitaeleza kisa hicho toleo lijalo) bila ruhusa ya Umoja wa Mataifa,wanajifanya wao polisi,mahakama,mgambo,hakimu na waendesha mashitaka kwa wakati mmoja!
ICC inakazi gani sasa kama bunduki za Marekani,Uingereza,Ufaransa na wapambe wao wana ruhusa ya kukamata,kuua na kuzika bila mtu kukohoa! Guantanamo na Abu Ghraibu huashiria demokrasia na haki za binadamu enhe?
Mahaka ya Hague ina faida gani,kama watuhumiwa wa ugaidi wanafungwa Guantanamo Bay bila mtu kuhoji?
Wanavyo fanya hawa, kwenda Syria na kuua watu ni sawa na anavyofanya Kagame bila kuulizwa-double standards- sasa Hague ina faida gani hapa Afrika?
Inaona makosa ya akina Uhuru Kenyatta,Ruto,Gbagbo na Watu Weusi wasio na maslahi na Magharibi tu?
Wenye masikio na wasikie.Ni uzumbukuku kusema Afrika ina madikteta wakati baadhi yao ni vibaraka wa maslahi ya Marekani,mwingine akikosea anakatwa na kufungwa jela Hague.
Charles Taylor kafungwa Ulaya miaka 50 kwa kufanya unyama Afrika,kwa hiyo Afrika hakuna jela? Uzumbukuku waMwafrika!
Mwafrika,Bensouda na wenzake,kaajiriwa katika mahakama ya Mzungu ili kumfunga Mwafrika mnashangilia! Ndiyo haki na kuondoa Impunity Afrika!!
Makampuni ya mafuta na gesi huleta vurugu Afrika na kuua watu,kampuni za madini hutiririsha kemikali na kuua watu na wanyama Tarime na kwingineko Afrika, hii kesi haina mashiko The Hague wala kokote! Upumbavu gani huu nyie?
Wao wakiua watu Afrika nani awashitaki The Hague? ICC ina wanachama 66 miongoni mwa zaidi ya nchi 200 duniani,hizo nchi 130 hazijalaumiwa kwa makosa?
Wanashitakiwa wapi? Marekani si mwanachama wa ICC, tumshitaki wapi?
Kenya wanapojiondoa ICC akili zilizoganda zinasema ni hatari! Hatari Kenya kuondoka ICC wakati nchi 130 ikiwemo Marekani yenye makampuni ya mafuta yanayochafua mazingira Nigeria n.k mbona hailazimishwi?
Ken Saro-Wiwa aliuawa na nani wewe kama siyo kampuni ya Shell ya Uingereza,Chevron na Royal?
Tusifikiri kwa kutumia tumbo;tutumie kichwa. Fatou Bensouda hawezi kuajiriwa mahakama za Afrika akatoa haki hadi Ulaya tu?
Tuutafute ukweli kwa darubini,Bensouda anaweza kusaini waranti kumkamata Obama kupeleka vita Syria kinyume cha sheria za Umoja wa Mataifa?
Ukoloni mamboleo ulishajaa akilini mwa watu wanadhani Afrika ndiko kwenye makosa na vita. Magharibi wakipeleka silaha Kongo wakawapa akina Kagame maelekezo kufanya vita,utalaumu Afrika?
Charles Taylor akitolewa jela,akapewa assignment kusaidiana na Fodday Sankoh kuua na kupora almasi,utasema Dikteta na Taylor tu anayestahili kufungwa na akina Sankoh kufia ICC?
‘Critical Mind’ inaweza kutambua ninachokitazama hapa,na waafrika mbumbumbu ni sumu ya maendeleo na uhuru wan chi,demokrasia na harakati za kweli.
Tazama vyama vyenu vya siasa vinavyokunja mikia miguuni kwa akina Cameron,Bush n.k wanaamrishwa ushoga n.k halafu mnasema ni NGUVU YA UMMA wa akina nani?
IMF,WB,WTO,ICC nk ni colonial tools za kumkandamiza Mwafrika hadi awe Mtumwa kifikra,ukiambiwa ukweli unakasirika na kusema Mwafrika ni dikteta.Hongera Kenya kukataa ukoloni.
Itaendelea



Tuesday, September 3, 2013

ukweli ni nini?


      
Historia ndiyo Darubini kali iliyomwibua mmoja wa Wanafalsafa wakubwa Ugiriki, ambaye anaweza kutwambia nini maana ya Ukweli?
Aristotle wa Athens aliyeishi kati ya mwaka 384 hadi 322 BC. Alipata kusema:
“Truth is agreement with FACTS and REALITY” ,Tafsiri yangu ni kwamba,Ukweli ni mwafaka baina ya habari ya kilichotukia na usahihi ama uhalisia wa mambo.
Kulingana na Aristotle, ukweli huweza kuongopa ikiwa UKWELI nusu-nusu unapowaongoza watu kwenye UONGO.
Aristotle  alisema hivi:
“To say what is that is not or of what is not that is-is FALSE, while to say what of what is that it is, and what is not that is not-is TRUE!!
Tafsiri yangu isiyo rasmi ni kwamba Aristotle alisema kusema jambo kwa namna isivyokuwa namna kitu kilivyokuwa hakika,ni UONGO;wakati kusema kitu kilivyo hakika na ukasema kwamba hakiko hivyo wakati hakiko hivyo huo ni Ukweli.
Aristotle, hutwambia kuhusu UONGO WA UKWELI(The lie of Truth) ambao mfano wake ni kama kudondosha tone la ukweli katika pipa la Uongo.Ukweli hauchanganywi na uongo ukabaki ukweli.Sumu kidogo ya panya haichanganywi na unga au mkate,kikabaki kuwa chakula bali sumu!
Chakula jumlisha sumu ni sumu,basi.
Naam, ‘a little truth drop in the bucket’ matokeo yake ni jamii kuamini uongo na kuufanyia kazi, ndivyo ilivyo hata hapa Tanzania.Jamii hufanyia kazi umbeya,uongo na upumbavu tu!
Watu wengi hata hapa Tanzania hudanganywa kwa ukweli kidogo ndani ya uongo mwingi,na tayari wameathiriwa na sumu ya uongo na umbeya,mishipa yao ya fahamu imedhoofishwa na majungu na uvumi.
Nilishaandika kwamba, Daktari akisema ‘Unaumwa Ukimwi’ ni FACTS-ni ukweli dhahiri. Lakini mpigadebe akisema kwakuwa una kikohozi na kichomi na umekonda-ni ‘Opinion’ ni maoni tu-maoni siyo ukweli halisi,ni kukisia na umbeya tu.Angalia sasa nchi hii walivyo hawatofautishi Opinion na Facts!
Ukweli haufahamiki kwa kusemwa na watu wengi ama kwa njia ya sanduku la kura!
Mwandishi,Derek J.Morris aliandika katika Jarida la MINISTRY la Juni mwaka huu 2013, kama ifuatavyo:
“TRUTH is not determined by opinion poll or popular vote!”
Ukweli hauamuliwi kwa wingi wa kura za maoni za watu wengi vijiweni! UKWELI huweza kusemwa na mtu mmoja mwenye taaluma kama daktari kusema ‘una ukimwi’ ndugu zako na jamaa wote wakashikilia umerogwa!
Ukweli hauamuliwi kwa sauti kubwa na maandamano ya vibaka na wanasiasa wakasema ndiyo NGUVU YA UMMA!
Aristotle amesema watu wengi huchelea kusema ukweli wasije wakachukiwa na umma mkubwa, ‘PEOPLES POWER’.
Watu wengi siyo wa kuamini,na mawazo yao siyo ya kufanyia kazi mara zote,wapo wafuata mkumbo tu,mashabiki na mabingwa wa kuigiza kila jambo na kuangamiza jambii kama tunavyoona leo madawa ya kulevya,bangi na ndoa za jinsia moja!
Bendera kufuata upepo tu! Kizazi hiki kimepotoka mno,kwa kuiga ya Magharibi ya watu wengi, sasa wachache hawana cha kusema,wataalam kama madaktari, wahandisi,maprofesa n.k ushauri wao ulishakataliwa na public opinion.
Siku hizi ‘wengi wape’ japo wapumbavu sana!
Watu wengi, aghalabu mbumbumbu mzungu wa reli fuata mkumbo, propaganda za siasa huishia kuipotosha jamii na kizazi hiki kwamba ndiyo haki za Binadamu.Haki za Mashoga,haki za wasagaji,haki za watoto kutochapwa viboko n.k
Watu wachache wenye haki aghalabu hawana ubavu wa kutetea ukweli usiochanganywa na uongo,umbeya,hisia tu na majungu.
Wakristo wameonywa sana kuwa waangalifu katika kuamua kati ya UKWELI(Right) na uongo(Wrong) kwa kufuata kura za maoni za wajinga wengi(Opinion poll) ama kura za watu wengi wanaopenda uhalifu na uovu(popular vote).
Kuna watu hawataki hata sheria ziwepo ili waingie mitaani na kupora mali za wenzao kwa kisingizio, Maisha ni Magumu!
Wachache wenye hekima wanajua matokeo ya kukosekana kwa sheria,lakini wapumbavu wengi watalaani kuwepo sheria,mahakama,polisi,mgambo,mahakimu n.k hawa wote ni vibaka akilini.
Ukweli na uongo,sharti kuamuliwa kwa muktadha wa mafundisho sahihi ya Neno la Mungu(Biblia n.k)Kwa mfano Zaburi 119:105 HUSEMA Neno la Mungu ni Taa iongozayo miguu ya wenye haki.
Watu wanasema Mungu alishakufa,hayupo na neon lake ni batili,sasa hawa wanakwenda njia gani halafu uwafuate gizani?
Watu wanapotaka kwenda upande wa kweli wa Historia,wanapaswa kugeukia hekima ya Mungu tu basi. Hekima ya Mungu ni Ukweli,haki,amani,upendo n.k
Biblia,kwa mfano husema njia ni nyembamba sana iendayo kwenye ukweli nao wanaoona ukweli ni wachache tu.Wengi huenda kwenye uongo,maana njia ya uongo ni pana hata mbumbumbu huiona.
Njia ya haki huonwa na wenye hekima,ni nyembamba hutazamwa kwa hadubini kali.
Ni kwa sababu hii,watu shupavu wanaotetea ukweli(rejea tafsiri ya ukweli) hawapendwi na wengi;huishia kutengwa,kusulubiwa.
Kusema kwamba kitu hiki hakiko hivyo wakati kweli hakiko hivyo ni hatari,unafanywa kama Nabii Yeremia,Martin Luther King Jr,Martin Luther wa Ujerumani,Socrates,Yohana Mbatizaji,orodha ndefu.
Katika kitabu cha Luka Mtakatifu 3:11-14 Yohana Mbatizaji anapokemea rushwa,ufisadi miongoni mwa maofisa wa serikali fisadi, anapokataza masikini kuporwa wake na mali zao, anaishiwa kunyongwa kijinga.
Nani atatetea kichwa ili akatwe kichwa?
Marko Mtakatifu 6: 17 na 18 hutwambia kwamba ni mtu labda mmoja tu anayekubali ukweli usemwe potelea mbali apoteze maisha yake,kuliko kuacha wajinga wengi waseme uongo na kuufurahia.
Public Opinion, mara nyingi hukinzana na ukweli na uhalisia wa mambo-husema minyoo huletwa na wachawi,na wala siyo uchafu na kula bila kunawa ama kunywa maji yasiyo chemshwa!
Ukisema ukweli utaitwa msaliti! Kuna mifano tele katika Biblia,niiache wengine wananiambia hataki kusoma biblia.Biblia ni kitabu,hawapendi kusoma ila kucheza na kucheka-cheka tu.
Nimesema kwamba ukweli huonwa na wachache tu na husimamiwa na watu shupavu wawili ama watatu tu-wengine bendera kufuata upepo unakoelekea, watu wengi wanafiki tu.
Wanaosema ukweli huitwa waongo na waongo huitwa wakweli.Mara nyingi waongo huenda kinyume cha Historia-The wrong side of History.
Historia inamsema Socrates(469-400 BC) ALIVYOULIWA na utawala wa Athens kwa kukataa umbeya kwamba kuna miungu 391 inatawala juu ya Mlima Olympus!
Walimpa sumu ainywe kwa kutetea kwamba kuna Mungu mmoja na huishi mbinguni tu. Yesu aligoma kufuata dini ya ukandamizi ya Kiyahudi, Martin Luther aligomea mafundisho ya Kipapa, Martin Luther King Jr. ambaye juzi Ndoto yake( (I have a Dream)ilisherehekewa miaka 50 na akina Obama, aliuliwa Aprili 1968 kwa kusisitiza ukweli kuhusu ubaguzi wa rangi Marekani, aliuliwa na Pentagon kwa kutetea ukweli.
Wapo akina Mandela wamesota rumande miaka 27, wapo wengine walifukuzwa kazi n.k
Katika mfululizo wa makala haya nitatilia shaka kila kinachoitwa UKWELI ili kutufanya kuchunguza mambo kwa akili tunduizi(critical mind) kuacha mikumbo na umbeya wa siasa za kipumbavu zinzoleta ugomvi katika jamii hii.
Tutajadili ‘fuata mkumbo’ iliyoleta shida hapa Tanzania, katika Nyanja tofauti siyo siasa tumhata dini zinazoshadidiwa na watu.
Nitakuwa nikitumia nukuu za wanafalsafa,wasomi,wataalam lengo ni kukiokoa kizazi hiki na kuiga na kufuata mkumbo wa kila kinachosemwa ili tuepuke propaganda,matangazo ya uongo redioni kwenye tv na maamuzi ya wengi katika kura za maoni(Opinion polls)
Nitatilia shaka hata katiba mpya itakayoamuliwa na wengi,lakini vipofu wakaacha maoni ya wachache ama mmoja mwenye hekima,mtu wa haki mnyoofu n.k
0786 324 074