Nalazimika
kurejea sehemu ya makala yangu iliyokuwa nakichwa cha habari, “AFRIKA KIZIMBANI”,ili
kujaribu kuzibua akili zilizoziba za Watanzania ‘Fuata Upepo” kwa kila
kinachosemwa mitaani!
Makala hiyo
iliyotwaliwa katika Jarida maarufu sana, New African la Julai, 2012 iliyokuwa
na kichwa cha habari, “Is Africa on
Trial?’
Kulikuwa na
kichwa kidogo(sub heading), “The Role of
the ICC(International Criminal Court) examined”.
Julai Mosi,
mwaka 2012, Mahakama hii ya Kimataifa(ICC)ilikuwa inatimiza umri wa miaka
10;sasa ina miaka 11,wengine wanaota ilikuwepo miaka milioni nyingi,Afrika tu
sasa inajifaragua kutaka kujiondoa katika mahakama hiyo!
Nataka wenye
akili baridi wasidhani ilikuwepo zamani wakati Adamu na Hawa wanaumbwa Edeni,mwaka
4000 BC.
Ni mahakama
iliyoishi kwa muongo mmoja,kufuatia Mkataba wa Rome, wa 2002.Nchi nyingi za
Afrika zilijiingiza kichwa-kichwa katika uanachama wa mahakama hii,kufuatia
Senegal kuwa mwanachama wa mwanzo.
Kuna akili
mgando zinazoweza kusema Afrika haiwezi kuanzisha Mahakama kama hii hapa ikatoa
haki,kwa sababu viongozi wetu-Madikteta- hawana Political Will-utashi wa
kisiasa wa kuwa na haki na demokrasia!
Wanasema
Afrika ndiyo nyumba ya utawala mbaya,rushwa na mauaji.Huu ni umbumbumbu wa
kutojua dunia nzima hii hakuna haki wala uhuru na demokrasia,sembuse Afrika?
Kasumba ya
Kikoloni(colonial mentality) imewaibia akili Waafrika kudhani hakuna haki na
maendeleo kama hakuna Mzungu! Hawa ni watumwa wa hiari.Wanatimiza unabii wa
akina Hitler,Botha na Makaburu wengine wabaguzi wa rangi.
Sasa angalia
wewe msomaji mwenye akili.Hata sasa
wendesha Mashitaka Mkuu wa ICC,Fatou Bensouda,toka Gambia,Afrika
Magharibi,ni Mweusi tena mwanamama.
Waafrika
Weusi wanashika ‘Key Positions’ katika Mahakama hiyo ya The
Hague,Uholanzi(kumdanganya Mwafrika);kwanini Umoja wa Afrika(AU) isianzishe
Mahakama yake,Nairobi,Arusha,Abuja ama popote?
Afrika
haiwezi kuwatia kabala Madikteta na wauaji wanaofanya vita hapa Afrika? Najua
vita nyingi Mwafrika hutumiwa kama kinyangarika ili kutekeleza maslahi ya
Mzungu,halafu lawama hubeba yeye mgongoni.
Kufuatia
ujinga wa Mwafrika,hata hao akina Bensouda huko ICC huendesha mashitaka na
kutoa hukumu inayolinda maslahi ya Mzungu na aslani siyo Mwafrika!
Mahakama za
Umoja wa Mataifa kama ile ya Sierra Leone,ya Mauaji ya Rwanda(ICTR) na ile ya
mjini Hague(ICC) ati hushughulikia mauji ya Kimbari-genocide-na matendo
yaliyokinzana na haki za binadamu na uhalifu wa kivita.
Sasa
tafakarini:Paul Kagame(rafiki wa Marekani) aliua marais wawili,Juvenal Habyarimana wa
Rwanda na Cyprian Ntaryamirwa wa Burundi,Aprili 6 mwaka 1994.
Ana kesi
inayomkabili?
Kagame
akiongoza Waasi(rebels) wa RPF aliua maelfu ya watu raia wa Rwanda hadi Wahutu
wakaanzisha Intarahamwe ili kulipa visasi,kwa kuwa wao ni wengi.
Kosa la
Kagame halikutazamwa kuwa ni kosa,kosa Wahutu kulipa kisasi!
Pili,Kagame
hakuingia Kongo na kupigana vita(kuua) ili kuwateketeza Waasi wa Intarahamwe?
Kuvuka mpaka na kuingia nchi ya KONGO siyo kosa katika Jumuiya ya Kimataifa?
Ama hakuna ushahidi The Hague!
Kuwatafuta
waasi wa Kihutu ndani ya Kongo na kuwaua,bila kuwafikisha mahakamani,ndiyo
nini?
Kagame
Mtu-tsi,anapowasaka Wahutu na kuwaua ni nini kama siyo genocide?
Siyo, crimes against humanity? Siyo, war crimes?
Kagame na
rafikiye Museveni wanawasaidia Waasi wa Kongo(M23,Bosco Ntaganda,Jen.
NKUNDABATWARE n.k hii nini?
Wewe
unawasaka waasi wa nchi yako ndani ya
ardhi ya nchi nyingine, unaona uasi ni unyama unastahili adhabu kali ya
kifo,wakati huo huo unawaunga mkono waasi wan chi ya jirani na kuwalea!
Ukiambiwa
kuzungumza nao ‘peace talk’ au ceasefire agreement, unakuwa mkali
unatukana watu! Hii nini sasa?
Hiyo ndogo,
wewe unaingia nchi ya watu na rafiki yako,mnapora madini,mbao,pembe za ndovu
n.k mnaanza kupigana ndani ya nchi ya watu,mnabaka akina mama,mnaua watoto kwa
risasi,halafu Wakongo wakisema,mnasema mnawatafuta Intarahamwe!
Mbona ICC
haijaona kosa la Museveni na Kagame,hata kama Jaji wa Ufaransa,Jean Louis
Bruguire ,alisema Kagame akamatwe na kupelekwa Arusha,baadaye wakasema ana Diplomatic Immunity?
Sasa
tujiulize, Omar Hassan Ahmad al Bashir wa Sudan,siyo Rais? Hana diplomatic
Immune? Mbona anasakwa akamatwe hadi akakimbia Nigeria juzi,kwa kuwa Nigeria ni
mwanachama wa Icc?
Hivi makosa
ya hawa wote,hayafanani na makosa ya Bush na Blair kwenda kuipiga Irak na Libya
na kumuua Saddam na Gaddafi,bila ridhaa ya Umoja wa Mataifa?
Hiyo nini
kama siyo Impunity? Yaani mtu anafanya makosa mabaya, anaachwa bila kushitakiwa
mahakamani!
Sasa
upendeleo mnaosema madikteta wa Afrika wakianzisha ICC, Addis Ababa itakosa
shabaha,hamwoni kitu hicho hata sasa? Mna makengeza!
Sasa akina
Obama wanakwenda Syria(nitaeleza kisa hicho toleo lijalo) bila ruhusa ya Umoja
wa Mataifa,wanajifanya wao polisi,mahakama,mgambo,hakimu na waendesha mashitaka
kwa wakati mmoja!
ICC inakazi
gani sasa kama bunduki za Marekani,Uingereza,Ufaransa na wapambe wao wana
ruhusa ya kukamata,kuua na kuzika bila mtu kukohoa! Guantanamo na Abu Ghraibu
huashiria demokrasia na haki za binadamu enhe?
Mahaka ya
Hague ina faida gani,kama watuhumiwa wa ugaidi wanafungwa Guantanamo Bay bila
mtu kuhoji?
Wanavyo
fanya hawa, kwenda Syria na kuua watu ni sawa na anavyofanya Kagame bila
kuulizwa-double standards- sasa Hague ina faida gani hapa Afrika?
Inaona
makosa ya akina Uhuru Kenyatta,Ruto,Gbagbo na Watu Weusi wasio na maslahi na
Magharibi tu?
Wenye
masikio na wasikie.Ni uzumbukuku kusema Afrika ina madikteta wakati baadhi yao
ni vibaraka wa maslahi ya Marekani,mwingine akikosea anakatwa na kufungwa jela
Hague.
Charles
Taylor kafungwa Ulaya miaka 50 kwa kufanya unyama Afrika,kwa hiyo Afrika hakuna
jela? Uzumbukuku waMwafrika!
Mwafrika,Bensouda
na wenzake,kaajiriwa katika mahakama ya Mzungu ili kumfunga Mwafrika
mnashangilia! Ndiyo haki na kuondoa Impunity Afrika!!
Makampuni ya
mafuta na gesi huleta vurugu Afrika na kuua watu,kampuni za madini hutiririsha
kemikali na kuua watu na wanyama Tarime na kwingineko Afrika, hii kesi haina
mashiko The Hague wala kokote! Upumbavu gani huu nyie?
Wao wakiua
watu Afrika nani awashitaki The Hague? ICC ina wanachama 66 miongoni mwa zaidi
ya nchi 200 duniani,hizo nchi 130 hazijalaumiwa kwa makosa?
Wanashitakiwa
wapi? Marekani si mwanachama wa ICC, tumshitaki wapi?
Kenya
wanapojiondoa ICC akili zilizoganda zinasema ni hatari! Hatari Kenya kuondoka
ICC wakati nchi 130 ikiwemo Marekani yenye makampuni ya mafuta yanayochafua
mazingira Nigeria n.k mbona hailazimishwi?
Ken
Saro-Wiwa aliuawa na nani wewe kama siyo kampuni ya Shell ya Uingereza,Chevron
na Royal?
Tusifikiri
kwa kutumia tumbo;tutumie kichwa. Fatou Bensouda hawezi kuajiriwa mahakama za
Afrika akatoa haki hadi Ulaya tu?
Tuutafute
ukweli kwa darubini,Bensouda anaweza kusaini waranti kumkamata Obama kupeleka
vita Syria kinyume cha sheria za Umoja wa Mataifa?
Ukoloni
mamboleo ulishajaa akilini mwa watu wanadhani Afrika ndiko kwenye makosa na
vita. Magharibi wakipeleka silaha Kongo wakawapa akina Kagame maelekezo kufanya
vita,utalaumu Afrika?
Charles
Taylor akitolewa jela,akapewa assignment kusaidiana na Fodday Sankoh kuua na
kupora almasi,utasema Dikteta na Taylor tu anayestahili kufungwa na akina
Sankoh kufia ICC?
‘Critical Mind’
inaweza kutambua ninachokitazama hapa,na waafrika mbumbumbu ni sumu ya
maendeleo na uhuru wan chi,demokrasia na harakati za kweli.
Tazama vyama
vyenu vya siasa vinavyokunja mikia miguuni kwa akina Cameron,Bush n.k wanaamrishwa
ushoga n.k halafu mnasema ni NGUVU YA UMMA wa akina nani?
IMF,WB,WTO,ICC
nk ni colonial tools za kumkandamiza Mwafrika hadi awe Mtumwa kifikra,ukiambiwa
ukweli unakasirika na kusema Mwafrika ni dikteta.Hongera Kenya kukataa ukoloni.
Itaendelea
No comments:
Post a Comment