Wapo watu
wanadhani mtu kushinda uchaguzi ni kupata kura nyingi za umaarufu(Popular
vote); na wengine wanadhani Rais mzuri ndiye aliyependwa saana.
Rais mwema anamjua Mungu.
Mfalme Sauli alipewa kura nyingi na
Waisraeli wa kale kwa sababu tu alikuwa mrefu na ‘handsome’ lakini akaja
kuboronga sana na kukiingiza kizazi katika ushirikina mkubwa… Mungu hafuati
urefu wa Mfalme wala kura nyingi za wapigakura mbumbumbu.
Wala safu hii
haitetei wizi wa kura wa Rais yeyote.
Isipokuwa, ni vigumu Rais wan chi
moja kuanza kumkosoa mwenzake.
Hapa kwetu kuna madai ya wizi wa kura
yaliyotolewa hata kabla ya uchaguzi wa Kenya .
Kibaki alimkosoa Rais Karume au Mkapa?
Mseveni mwenyewe alidaiwa
kuiba kura Uganda na kumsweka rumande Kanali Dk Kizza Besigye.
Kibaki alikosoa udikteta huo wa
kumsweka rupango mpinzani wa Museveni?
Forum for
Democratic Change(FDC) cha Dk. Besigye, kimekuwa kikilalamika kwa kufanyiwa
mchezo mchafu na National Resistance Movement.
Rais gani hapa Afrika aliyekataa
kutambua ushindi wa Museveni; na kutambua ule wa wapinzani?
Wafuasi wa Besigye
jijini Kampala walipata kupigwa mabomu ya machozi na risasi za mipira hata za
moto, walipopinga kukamatwa kwa kiongozi wao.
Rais gani alimkosoa Museveni
hadharani, achilia mbali kutotambua ushindi wake halali toka kwa Tume yake ya
Uhaguzi?
Kuna suala la Dk. Kiza Besigye
kuzuiwa kwenda kazini kwa miguu,maarufu ‘Walk to Work” ambalo limeleta sana
shida mjini Kampala.
Makomandoo wa Rais Museveni, Black Mamba Urban Hit Squad, waliwahi
kutinga Mahakama Kuu ya Kampala na kuzingira, Kanali Besigye alipoomba dhamana.
Ilikuwa kitisho
kwa Majaji.
Wee Black Mamba wamezingira kiti
chako utajidaije kumpa haki mpinzani? Kampala ni undava-undava!
Dikteta Nduli,
Joka Kuuu, Idi Amin Dada, aliwahi kutuma makachero wa Ikulu, The State Research Bureau, wakaingia
mahakama hiyo Kuu ya Uganda , na kumkamata Jaji Mkuu, kisha kumtia ndani ya
buti ya gari yao na kutoweka naye. Hakuonekana hadi Amin anazikwa Saudi Arabia.
Sasa Majaji wangefanyeke
kazi katika mazingira haya?
Ilibidi baadaye wagome tu, halafu
Rais Mseveni akaomba radhi.
Kumpa haki mpinzani siyo rahisi.
Viongozi wetu ni wababe sana ; hata wao kwa wao huogopana. Wee Bush akishindwa
hata kura ya maoni Irak, utasema kashindwa? Thubutu.
Naam, nampenda
Jenerali Kaguta Museveni, ni kiongozi wa wenzake katika Shirikisho letu la EAC.
Tena basi, Museveni ni mzoefu wa siasa kuliko Kibaki, Kikwete labda na Raila
Odinga.
Kushinda na
kushindwa uchaguzi yeye ndiye anayejua zaidi kuliko hawa wengine.Ni na hofu na
mkuu huyu kuongoza Afrika Mashariki(EAC) na kupatanisha migogoro hapa Maziwa
Makuu.
JENERALI MUSEVENI NI
NANI?
Aliwahi kushindwa ubunge, kwao.
Chama chake cha Uganda Patriotic
Movement kiliambulia kiti kimoja tu, ingawa kilisimika wagombea 44.
Akaanzisha mapambano ya msituni dhidi
ya serikali Desemba 1980.
De Mabior, Samora
wamekufa kifo kimoja cha ajari za ndege.
Kabila aliuawa Ikulu ya Kinshasa
mwanzoni mwa 2001 tena na mlinzi wake, ambaye naye alilimwa risasi.
Museveni ni
mwanasiasa kwa kusomea. Ana shahada ya UDSM.Licha ya kujua mapinduzi ya
kijeshi, amekuwa waziri wa Ulinzi tangu 1979 katika serikali ya Yusuf Lule.
Museveni ameingia
madarakani Januari 26, mwaka 1986 akamtoa Marehemu Jenerali Toto Okello.
Ninachotaka kusema ni kwamba,
Jenerali Museveni si mbumbumbu hata atambue ushindi wa siasa hapa Afrika
Mashariki,na anajua si vita vya msituni tu,bali hata fitna,kupindua serikali na
kuwaweka madarakani akina Kagame n.k
Naam, amesoma siasa na
kuhitimu chuo kikuu. Ameshiriki mapambano ya kudai uhuru, ameingia msituni na
kupindua serikali. Sasa amebadili Katiba ili asalie madarakani tangu hiyo
Januari 29,mwaka 1986 alipoapishwa kuwa Rais wa Uganda .
Wenzake akina
Samora, de Mabior na Kabila wamekufa yeye yupo madarakani.
Mtu aliyesoma
sayansi ya siasa(Political Science) na kuhitimu miaka hiyo ya 70 UDSM,
atakuwaje mbumbumbu wa kushindwa kujua mshindi wa uchaguzi hata Marekani,
achilia mbali Nairobi ?
Ndiyo maana Kikwete kamwambia
kumshauri Kagame aache jeuri hapa Afrika Mashariki,yeye ana madaraka
‘chakupewa’ toka mbawani mwa Museveni!
Mtu ambaye majeshi yake
yamewahi kuingia Kongo na kuchapana na majeshi ya mshirika wake wa siku
nyingi, Meja Paul Kagame, Rais wa Rwanda , hukohuko Kongo; hajui nani
mwenye Afrika Mashariki?
JENERALI PAUL KAGAME NAYE NANI AFRIKA MASHARIKI?
Paul Kagame
alikuwa katika Jeshi la Museveni wakati wa mapambano ya msituni.
Kagame alitoka msituni akaenda
Marekani kusomea medani ya kijeshi, kabla ya kuitwa kuwaongoza RPF.
Jenerali Museveni
aliyemsaidia hata Kagame kutawala Rwanda si mwanafunzi wa siasa za Afrika kama
wengine wanavyomfananisha kijiweni.
Anapotaka kuwa Rais wa kwanza wa
Shirikisho la Afrika Mashariki(EAC) anajua na habahatishi.Watu wawe makini na
wajue maslahi ya akina Museveni,Kagame na wenzake hatutawataja hapa.
Anapopeleka majeshi yake Congo,bila
shaka kupora madini na pembe za ndovu huko,inajulikana anachofanya! Hujui pesa
za magendo hufanya nini?
Naam. Jenerali
Museveni anamjua Raila Amolo Odinga. Anajua kuwa naye si haba. Odinga aliwahi
kukimbilia hapa Tanzania akiogopa kutiwa mbaroni kufuatia harakati zake
za siasa. Odinga na Museveni wanajuana.Wameishi hapa-hapa kwetu ni kimbilio la
hapa ambao leo wanajidai kutudhaharu!
Odinga aliwahi kutuhumiwa kwa kesi za
uhaini zama za Rais Moi.
Odinga ni Mhandisi na si
mwanajeshi.
Museveni ni mwanasiasa wa
kusomea Chuo Kikuu na ni mwanajeshi wa cheo cha ‘General’.
Jenerali Museveni(69), amebaki pekee mkongwe
katika siasa za Afrika Mashariki.
Anajuana vilivyo na Bush na Gordon
Brown,Nick Clegg,Obama na
wengine,
. Malkia Elizabeth II katoka
mjini Kampala kuhudhuria mkutano wa Commonwelth. Miaka michache
iliyopita.
Museveni anaijua Afrika
Mashariki kuliko Kagame. Amepigana vita msituni Tanzania,Uganda,Musumbiji dhidi
ya Wareno na ndani ya Congo!
Hata hivyo,Museveni na Kagame
wamefanikiwa sana kufuatia urafiki wao na Marekani.Wasije wakamsahau Charles
Taylor.
.
CHARLES TAYLOR, Rais wa
zamani wa Liberia ambaye sasa anafungwa jela miala 50 baada ya mashitaka
ya uhalifu wa kivita, alikaririwa na gazeti la Africa Now la Mei mwaka juzi
2011, akisema: “Boss wako anapokuwa adui yako, umeangamia!”
Taylor, alikuwa
akizungumza na gazeti hilo kueleza hisia zake jinsi Dunia leo ilivyo katika
hatari kuliko hata kipindi cha Vita baridi.
Hata hivyo, Taylor
anayataja mataifa makubwa kama ‘ Mabwana wakubwa’ wanaoitawala dunia ya
utandawazi kwa kutumia nguvu zao za kiuchumi, kijeshi na hata kwa kutumia
Taasisi za Fedha kama IMF, Benki ya Dunia na Shirika la Biashara WTO,
kuukandamiza Ulimwengu.
Kulingana na Taylor
aliyekariri kauli ya Waziri wake wa Habari, kwamba “Bwana Mkubwa (Boss)
anapokuwa adui yako, umeangamia”, alikuwa akiilenga Marekani inavyouburuza
Ulimwengu, bila kuogopa ,upinzani toka Umoja wa Mataifa (UN) au hata kutoka
nchi za Mashariki, kama ilivyokuwa kabla ya Vita baridi kumalizika miaka ya 90.
Tunatanguliza maneno
haya kwa moyo wa unyenyekevu, kueleza hali halisi ya Ulimwengu tuliomo, ambamo
gazeti kama hili haliwezi kuepuka nguvu zilizotajwa na Charles Taylor.
Msomaji wetu
mmoja, Pierre Kumaro, aliyejitambulisha kama raia wa Rwanda, aishiye Dar es
salaam, amelalamika kama kichwa cha makala hii kilivyosema!
Pierre
Kumaro,alimwandikia mwandishi wa makala hiyo barua pepe ambayo tutaichapa hapa
chini , ili wasomaji wetu wenye mchango wao wasiache kutoa maoni yao kupitia
gazeti hili linalodhihirisha kuwa ni jukwaa halisi la kusemea wanyonge, tangu
Tanzania, Rwanda, Burundi, Nigeria , Congo na hata Iraq!
Jambo moja ambalo lazima
wasomaji wetu na wenye mamlaka za kisiasa na kisheria wanapaswa kuweka maanani,
ni kwamba maoni ya Pierre Kumaro, siyo msimamo wa gazeti hili, kuhusu mgogoro
wa Rwanda wa mwaka 1994, uliopelekea mauaji ya Kimbari.
Kwa upande mwingine,
sheria zinazokataza “kumtukana” rais wa nchi rafiki (kama Rwanda, Kenya,
Burundi, Uganda, Marekani, Uingereza n.k) kwa namna yoyote, zisitafsiri maoni
ya raia wa Rwanda kama kashfa.
“Kwa nini unaandika
mambo ya mbali, ukasahau mtu kama Paul Kagame wakati ndiye wa karibu?
Ninyi Watanzania
mnaogopa kuandika mateso ya Wanyarwanda wanayopata sababu ya ‘ Kibaraka’
Kagame!
Au hamjui, ama mmepewa
kitu kidogo…mnaandika mateso ya Iraq, Liberia, ya Rwanda hamtaki kuwajulisha
Watanzania! Hebu wewe niambie , kama umewahi kusikia maandamano ya chama cha
Upinzani Rwanda; au mkutano?
Jiulize: Rais wa zamani
anawekwa ndani,eti anataka kuunda chama!
Jiulize: Rwanda wanapata
wapi silaha za kupigana hadi kukamata Congo(DRC) nzima. Jiulize, tangu rais
Paul Kagame awekwe madarakani (Meja Paul Kagame aliapishwa rais wa Rwanda
Aprili 22, mwaka 2000)na Marekani ,ukiwa Waziri Mhutu, ukimaliza tu mhula
wako ni jela au ukimbilie nje, la sivyo unakufa!
Nashangaa sana Tanzania…
jinsi wanavyotuonea sisi Wahutu, hamtaki kuweka mambo hadharani! Sasa hivi kuna
mtu, mwezi uliopita alikuwa Arusha kwenye Mahakama ya Umoja wa Mataifa(ICTR),
alikuwa Mlinzi wa (Rais Paul) Kagame,alisema namna Kagame alivyotoa amri ya
kuangusha ndege iliyomuua (Hayati Rais Juvenal) Habyarimana”.
(Marehemu Habyarimana
ambaye alikuwa Mhutu, na Rais wa Burundi, Cyprien Ntaryamira, waliuawa katika
ajali ya ndege ambayo hadi sasa chanzo chake ni siri, Aprili 6, mwaka 1994.
Walikuwa wakitoka Dar es
salaam kwenye mkutano wa usuluhishi wa migogoro ya nchi zao. Walipanda ndege
moja, na ndipo ajali hiyo ilipotokea. Ntaryamira alichaguliwa rais wa Burundi
Januari 1994, akafa Aprili mwaka huo.
Wakati Habyarimana
alikuwa ametoka kutiliana saini mkataba wa Amani na Waasi wa Kitutsi wa Rwandan
Patriotic Front(RPF) Agosti 1993. Baada ya ajali hiyo, yalianza mauaji ya
Kimbari yaliyochukua maisha ya watu 800,000!)
“Yeye (Kagame)
alishiriki mia kwa mia”, Pierre ameendelea kusema “Mtu huyo(Mlinzi wa rais
Kagame) alitoa ushahidi wa kutosha, lakini Mahakama ya Arusha inakataa
kumkamata, kwa sababu Marekani hawataki! Kwa nini vitu kama hivi msiandike?
Wakati vipo hata kwenye internet?
Watutsi, walioua watu
Congo hadi leo, eti wanasema kuna Wanyamurenge! Wanyamuremge wako wangapi
Congo, wakati ni Wanyarwanda watupu! Wewe (mwandishi) nenda Ubalozini, uwaulize
ni wafanyakazi wangapi Wahutu?
Wote, kuanzia Balozi ni
Wahutu hapa Dar es salaam. Walinzi wawili tu (wa Ubalozi) ni Watanzania;
wengine ni Watutsi, wakati Rwanda hawafiki hata milioni moja! Wahutu ni milioni
saba… sasa wapi na wapi?
Sisi (Wahutu) Wacongo
tuliishi nao vizuri; Kagame kawaingiza kwenye vita. Wanaiba madini wakisaidiana
na Marekani…wanawatesa Wacongo hawajui vita, wanajua Ndombolo na kupenda
starehe,hususan wanawake! Muwe na tahadhari na Kagame katika Ushirikiano
wa Afrika Mashariki (EAC); kwani sera yake ni kuleta Tutsiland!
Wamarekani
wamempa(Kagame) Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.(kitendo cha Marekani
kutoingilia kati mgogoro wa Congo hapa kimeitwa kumpa Kagame Congo) Mtutsi
akiuawa ni Genocide(mauaji ya kuamgamiza) kama vile Muisraeli akifa! Mpalestina
akifa, Waisraeli siyo wauaji!
Lakini, Muisraeli
akifa, Wapalestina ni wauaji…Anza kuandika vitu vilivyopo karibu yako. Mambo ya
Iraq baadaye. Sawa?” aliniambia
Baada ya machafuko hayo
ya Rwanda, takriban Wahutu na Watutsi milioni mbili walikimbilia uhamishoni
Congo na mahali pengine, ambako pia walikufa kwa maradhi kama Kipindupindu na
majanga mengine.
Majeshi ya Umoja wa
Mataifa yaliingia Rwanda Juni 23 mwaka 1994 ili kulinda amani( safe zone).
Meja Paul Kagame
aliapishwa kuwa rais wa nchi hiyo Aprili 22, mwaka 2000.Miezi michache
iliyopita waliadhimisha miaka 19 ya mauaji hayo.
Kwa kuwa suala hili la
mauaji ya Hayati Habyarimana na Ntaryamira ni siri, vema maoni ya Pierre
yakachukuliwa kama mawazo binafsi, kwa kuwa hakuna ushahidi kuwa Rais Paul
Kagame aliamurisha vikosi vya waasi wa RPF kuitungua ndege iliyowachukua.
Kwa kusema hivi hatumtetei rais huyo au kumvua
lawama zinazomzunguka.
Hata hivyo, gazeti hili
linatarajia mjadala mkali juu ya maoni ya Pierre Kumaro. Jambo moja ni dhahiri
juu ya ubabe wa Marekani duniani. Hadi sasa Marekani inawasaidia wababe wa
kivita wa Somalia (Warlods) kuvifyeka vikundi vya wanamgambo wa Kisomali, kwa
madai ya kuwa na uhusiano na mtandao wa Al-Qaeda.
Hili ni jukumu la
ulimwengu mzima kupinga tabia hii ya kibabe. Kama Umoja wa Mataifa umeshindwa
kuikemea Marekani, wa kazi gani basi?
Vita hivyo vya aibu
Afrika, leo vimesababisha silaha za hatari kama AK-47 kuuzwa kwa zaidi
kidogo ya Dola moja ya Marekani( sawa na sh. 1300); na hivyo kuhatarisha eneo
zima la Mashariki na Pembe ya Afrika. Kama silaha hizo zitafika mikononi mwa
majambazi, hali itakuwaje?
Au Marekani haioni aibu kuchochea vita Somalia
kwa mara nyingine kwa sababu ya ile hofu ya Ukomunisti wakati wa VITA Baridi ?
Oktoba 4, mwaka 1993
askari 100 wa Marekani waliivamia Somalia kwa helkopta 12, na kukamata
walinzi 19 wa Mbabe wa kivita, Jen. Muhammad Farrah Aydeed mjini
Mogadishu.
Helkopta moja
ilitunguliwa na wanamgambo wa Aydeed.
Askari 12 wa Marekani
waliuawa na wengine 75 wakajeruhiwa vibaya katika mapigano yaliyodumu kwa saa
15.
Hapa, aibu ya kutisha
ikaikumba Marekani, maana maiti ziliburuzwa mitaani kwa shangwe mjini
Mogadishu! Bado tabia hii haijakoma; Marekani imerejea Somalia kwa
kisingizio cha ugaidi!
Kama alivyosema Taylor,
“Boss wako akiwa adui yako, si umeangamia?” Kama Umoja wa Mataifa
umeshindwa kuikemea Marekani juu ya ubabe wake na upendeleo wake kwa baadhi ya
Madikteta, jumuia ya Kimataifa ifanyeje?
Waandishi wa Tanzania
hawajapewa ‘kitu kidogo’ na Rais Paul Kagame, ili kunyamazia mauaji ya kimbari
ya Rwanda.
Kulingana na sheria
(kila nchi inasheria zake) kuandika masuala tete kama mauaji ya hao marais
wawili mwaka 1994 kwamba Marekani inachelea kumkamata Kagame, ni suala
lililoanza kuzungumzwa na Majaji wa Kifaransa mwaka 2006.
Kuhusu mauaji
hayo, jambo moja ni dhahiri:
Kwamba Juvenal
Habyarimana na Cyprien Ntaryamira walikufa pamoja na watu wengine wanane,
katika ajali ya ndege ya Aprili 6, 1994. Ndege hiyo inadaiwa kuangushwa
kwa kombora na watu wasiofahamika, ingawa inahisiwa ilitunguliwa na waasi wa
RPF.
Kagame kama rais wa
nchi, ana staha yake na haki zake katika kujibu madai hayo, yeye mwenyewe,
msemaji wa serikali yake, au Ubalozi wa Rwanda jijini Dar es salaam Kamwe
hakuna wa kumsemea au kumyima uhuru na haki hizo.
Labda mpaka ushahidi
kamili kama unaodaiwa kutolewa na huyo “mlinzi” ICTR utakapopatikana.
Suala la Kagame na lile
la Bush na Blair ni tofauti, kwa kuwa UN wamekiri juu ya uvamizi dhidi ya Iraq;
wakati kilichotungua ndege ya marais hao kimefanywa kuwa siri.
Aidha, Marekani
yenyewe au jumuia ya kimataifa hajapaza sauti kueleza chanzo cha ajali hiyo ya
ndege iliyochukua uhai wa viongozi hao wa nchi jirani, na kusababisha vita na
mauaji makubwa katika Afrika ya Kati.
Pia, kama alivyosema
Taylor, “When your Master is your enemy,
you are doomed!”
(Bosi wako anapokuwa
adui yako, umekwisha!) si vita lelemama inayosubiri Tazama pekee, bali
ulimwengu mzima upaze sauti kukataa dhuluma ya kutisha inayofanywa na Marekani,
namna hii.
Kwa kusema hivi,
hatujivui jukumu la kusema ukweli na kuilinda jamii dhidi ya uovu.Bali
tunatanguliza staha ya kila mtu ,haki zake mbele ya jamii, utu wa mtu yeyote,
tangu kibarua wa ngazi ya chini, hadi kiongozi machachari kama rais
Kagame
. Zaidi ya yote
tunatanguliza uzalendo wa Afrika, ili kutochochea mateso zaidi kama alivyosema
Pierre, ama mauaji ya kuangamiza kama ya mwaka 1994!
RAIS OMAR HASSAN
al-Bashir wa Sudan , yeye akikanyaga nchi yoyote inayoheshimu ‘waranti’ ya
Mahakama ya Kimataifa(ICC) iliyoko Hague, Uholanzi, atakamatwa.
Sheria za
kimataifa hazitoi upenyo kwa Rais aliyeko madarakani kukamatwa. Kwa sababu,rais
anayo kinga ya kidiplomasia iitwayo, ‘diplomatic immunity’.
Lakini, Rais Omar Hassan al-Bashir ambaye amefunguliwa mashitaka ya
kushirikiana na ‘mabedui’ wa Kiarabu wa Janjaweed, ya kuwaumiza raia Weusi wa
Jimbo la Darfur nchini Sudan , akikanyaga nchi yoyote inayoshirikiana na
Mahakama ya The Hague, atatiwa mbaroni kuanzia sasa.
Katika
kipindi kisichozidi miaka miwili, al-Bashir anakuwa Rais wa pili Barani Afrika
kutishiwa kukamatwa na kushitakiwa katika mahakama za uhalifu wa kivita.
Meja Paul Kagame
wa Rwanda , anatishiwa na mpelelezi wa mauaji ya Kimbari ya Rwanda , ya mwaka
1994, Jaji Jean-Louis Bruguiere.
Jaji huyu wa Kifaransa,
anasema Paul Kagame anahusika sana katika mauaji hayo.
Anasema, Kagame aliamurisha Waasi wa Kitutsi, Rwandese Patriotic Front(RPF)
kutungua ndege iliyokuwa imewachukua marais wawili wa Rwanda na Burundi .
Rais
Juvenal Habyarimana na mwenzake wa Burundi , Cyprian Ntyaramirwa, walikuwa
wakitokea Dar es salaam Aprili 6 mwaka huo wa 1994, ndege yao ikapigwa kombora
kali jirani na kasri la Rais, ilipokuwa ikijiandaa kutua mjini Kigali .
Walikuwa
wakitokea mkutanoni Dar es salaam , ambako walikuwa na mazungumzo na Rais Ali
Hassan Mwinyi, wakati huo.
Huo ndiyo ulikuwa
mwanzo wa mauaji ya Kimbari(genocide); mauaji ya siku 100 yaliyochukua roho za
Watutsi na Wahutu wa msimamo wa wastani kati ya 800,000 na 900,000.
Jaji
Bruguiere, alisema Kagame akiwa Kiongozi wa Waasi wa RPF aliamurisha ndege hiyo
iliyowachukua viongozi hao wawili kupigwa kwa makombora mawili makali, hadi
ikadondoka na kuwaua viongozi hao.
Rais Kagame
anakanusha vikali na kusema ni Wafaransa waliohusika kuiangusha ndege hiyo kwa
sababu walikwishamchoka ‘rafiki yao ’ yaani Rais Habyarimana.
Kwa
sababu hiyo, Wafaransa walishatangaza kutaka Kagame aondolewe kinga, ili
akamatwe na kushitakiwa katika Mahakama ya Umoja wa Mataifa ya Mauaji ya
Kimbari ya Rwanda (ICTR), iliyoko Arusha , Tanzania .
Mahakama ya
Umoja wa Mataifa( ICC) ya mjini Hague inashughulikia makosa ya kivita.
Ina mwanachama
mmoja wa kudumu-Uholanzi-ambako mjini The Hague kuna jopo la majaji 15
wanaoshughulikia kesi zinazohatarisha amani na usalama katika mamlaka za
Kimataifa.
Mahakama hii ya
Hague imeshughulikia kesi nzito, hususan zinazowahusu viongozi wa nchi
kama Charles Ghankay Taylor wa Liberia, Slobodan Milosevic wa Serbia na
wahalifu wengine kama Pierre Bemba wa Jamhuri ya Kimdemokrasi ya Congo,
Kiongozi wa Waasi wa Revolutionary United Front(RUF) wa Sierre Leone, Marehemu
Foday Sankoh, Adolh Hitler na wafuasi wake n.k
Kulingana na
Tangazo la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu la Desemba 10, mwaka 1948, watu
wote wanaopora haki za msingi za kuishi, wanastahili kushitakiwa.
Baraza la
Usalama la Umoja wa Mataifa lenye wanachama wa kudumu kama Uchina, Uingereza,
Marekani, Ufaransa na Urusi na nyingine 10 huja na kuondoka, linapaswa
kuwashughulikia wote wanaosababisha vifo ama maangamizi ya raia wa dunia.
Mfano ni huo wa
Sierra Leone ambako Rais Charles Taylor wa Liberia wakati huo, alishirikiana na
‘rafikiye’ Foday “Poppay’ Sankoh, kuendesha vita kali ili kujipatia na kuuza
almasi.Masoko ya Ulaya na Marekani ndiyo yaliyofaidika na almasi za Sierra
Leone mwaka 1999.
Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo, Pierre Bemba alikamatwa kuhusika na vita. Rwanda, mwaka
1994 Paul Kagame na maofisa wake wa kijeshi wanatuhumiwa kuanzisha vita
vilivyoshindwa kuzima maangamizi, na Darfur, Sudan Omar Hassan al-Bashir
anatuhumiwa kuua na kuwasaidia Janjaweed kuumiza raia wa jimbo hilo.
Ni kwa sababu
hii, kuna wanaharakati wanaoona Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza, Tony Blair na
Rais Mstaafu wa Marekani, George Walker Bush, nao wanastahili kukamatwa
kuhusika na vita Irak na Afghanistan kinyume na matakwa ya Umoja wa
Mataifa(UN).
Yaani,
Uingereza, Marekani na washirika wao walipeleka vita na hasara ya mali na
maisha nchini Irak, walipindua serikali ya Saddam Hussein kwa kisingizio cha
kuwepo silaha za maangamizi, Umoja wa Mataifa ukaja kubaini kuwa hakukuwa na
silaha.
Kufuatia
ukweli huo, si Jaji Jean-Louis Bruguiere wa Ufaransa, wala Mwendesha Mashitaka
Mkuu wa Mahakama ya Uhalifu wa kivita, Luis Moreno-Ocampo, ama Fatou
Bensouda,waliokwishatoa ‘waranti’ ya kumkamata Bush ama Blair ili nao wakabili
mashitaka ya umwagaji damu nchini Irak, kama siyo Afghanistan .
Sasa, wanakwenda Syria
akina Obama na Hollande,Umoja wa Mataifa uko kimya,ingawa umekataa kupeleka
maangamizi huko.
Wakati Luis
Moreno-Ocampo anadai kuwa ushahidi mzito wa kumtia hatiani Rais Omar Hassan al-
Bashir wa Sudan , kwa kuamuru majeshi yake kuteketeza watu wa Makabila ya Fur,
Masalit na Zaghawa, na kuathiri wengine wapato milioni 2.5 wa kabila la
Zaidiya.
Bado hajafikiria
kuwapeleleza Tony Blair na Bush angalau kwa kusema uwongo, kwamba Irak kulikuwa
na silaha za maangamizi(mass destruction wepons), kumbe siyo kabisa!
Ni kwa sababu hii
watu wanasema Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lenye wanachama wa kudumu
na nguvu za ‘Veto’ kama Uingereza, Marekani, Ufaransa, Uchina na Urusi, wana
macho yenye ‘makengeza’ kuona makosa ya wahalifu wa Barani Afrika, wakashindwa
kuona yale ya Mabwana wakubwa kama Bush na Blair!
Hawa ndiyo maana
wanatazama Kagame kama hana hatia hadi sasa ila iko siku watabadilika.
Aidha,
mashitaka dhidi ya Slobodan Milosevic, Foday Sankoh, Charles Taylor, Adolf
Hitler na wafuasi wake wa ki-NAZI, nay ale ambayo yangewakabili watu kama
Marehemu Dikteta Pinochet wa Chile , na wengine waliomwaga damu duniani.
Yana tofauti
gani na Bush na Blair kupeleka majeshi Irak na kupindua serikali ya
Saddam Hussein; kisha wakashindwa kukomesha umwagaji damu?
Nchini
Rwanda, tumeona mchakato wa kumtia mbaroni Rais Paul Kagame ulishaanza, baada
ya Mkuu wake wa Itifaki, Bibi Rose Kabuye kukamatwa mjini Frankfurt, Ujerumani
na kupelekwa Paris, Ufaransa ili kukabili mashitaka yale ya kuhusika na
genocide.
Ni kwa
sababu hii Afrika inajiuliza: Je, mahakama hii ya Umoja wa Mataifa, haioni
kwamba Bush na Blair kuiongopea Umoja wa Mataifa na kwenda kupindua serikali,
wakashindwa hadi sasa kuleta utangamano Irak na Afghanistan , siyo kosa kama la
Kagame, al-Bashir, Taylor na wenzao?
Msumeno leo
hausemi hivi ili kuwalinda marais Paul Kagame wa Rwanda na Omar Hassan
al-Bashir wa Sudan , wasikamatwe na kufunguliwa mashitaka kwa uovu waliofanya,
maadam akina Ocampo na Jaji Bruguiere wana ushahidi mzito.
Hapa,
tunahoji tabia ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lenye wajumbe wa kudumu
kama Marekani, Uingereza, Uchina, Ufaransa na Urusi na wenzao 10 wa kuja
na kuondoka, linaona makosa ya viongozi wa Afrika peke yake, na kuwaacha akina
Bush na Blair kula 'good time’ bila kushitakiwa?
Je, Baraza
la Usalama halijasikia kwamba hawa hawakuwa na ushahidi wa kuivamia Irak?
Kwa sababu Mkaguzi wa
silaha wa Umoja wa Mataifa, alishasema hapakuwa na silaha za maangamizi Irak.
Nataka kusema
kwamba, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Makama ya Uhalifu wa
Kivita(ICC) wanakuwaje na ‘makengeza’ kwa makosa ya akina Bush na Blair?
Foday
Sankoh, Milosevic, Taylor, Kagame, al-Bashir, Pierre Bemba wameshupaliwa.
Tunajua hata akina Jonas Malheiro Savimbi walisaidiwa sana Shirika la Ujasusi
la Marekani(CIA) kuihujumu Angola .
Yaani,
Waafrika wanapofanya uhalifu kwa maslahi ya Uingereza na Marekani watakamatwa
baada ya maslahi kutoweka.Wakifanya uhalifu akina Blair na Bush, UN inapata
makengeza na kushindwa kubaini makosa?
Ndiyo Maana Kenya
wameamua kujitoa katika Mahakama hii ambayo hata Marekani na mataifa mengi ya
Ulaya,hawamo.
Akina Bush
na Blair wakipeleka vita Afghanistan , Irak , Iran , Korea Kaskazini na popote
wanapopingwa sana , hawakemewi.
Wanasema, Bush na Blair
au Barack Obama na Gordon Brown wakiipindua nchi kwa maslahi yao , basi siyo
magaidi bali ni ‘liberators’ .Mtu mwingine akiua wananchi kwa maslahi ya milki
yake, basi ndiye mwalifu wa kivita!
Ni kwa sababu hii
naona“double standards” katika maamuzi ya Baraza la Usalama la Umoja wa
Mataifa na utendaji kazi wa Mahakama ya The Hague .
Waafrika kama
Bemba, Jonas Malheiro Savimbi, Charles Taylor, Sankoh na wenzao wakifanya vita,
kisha wakaiba almasi, dhahabu na mafuta na kumuuzia Mzungu, mwisho wa siku
watakamatwa wao na kufungwa jela, na wala aliyewatuma na kuwapa silaha
haulizwi!
Charles Taylor
alishawashangaa sana Marekani kwa sababu aliposhirikiana na Foday Sankoh
kupigana vita na serikali ya mjini Freetown na kuiba almasi mwaka 1999,
aliwauzia wao!
Sasa,
walipoona watabainika, wakatangaza Taylor na Sankoh wakamatwe.
Taylor yuko jela,baada ya kuhukumiwa Hague, wakati
Sankoh alikamatwa lakini akafariki dunia huko mjini Hague.
Je, huu ni
uungwana?
Anayebisha,
akatazame filamu iitwayo, Blood diamond, atawaona Wazungu kuhusika katika vita
hivi vya almasi za damu nchini Sierra Leone.Wakati Taylor na Poppay Sankoh
walibadilishana na Wazungu almasi kwa bunduki, Umoja wa Mataifa haujaona Mzungu
aliyesaidiana nao katika biashara hii ya damu, ila kawaona Taylor na Sankoh tu!
Hizi ndizo
‘double standards’ tunazozungumza. Vita walivyoanzisha Wazungu, Baraza la
Usalama halioni. Maasi ya akina Sir Mark Thatcher kule Guinea ya Ikweta, ili
waibe mafuta, Mahakama ya uhalifu wa kivita haioni!
Ni kwa sababu
gani Jean-Louis Bruguiere wa Ufaransa na Luis Moreno-Ocampo, hawajaona
rasilimali za Afrika zinazoporwa baada ya wao kuanzisha vurugu na vita?
Vita vya Kongo kuna
mkono wao kwa akina Paul Kagame,ndiyo maana wako kimya, angekuwa Mugabe
wangesema akamatwe haraka!
Tumeona
Blair, Bush, Bemba, Poppay Sankoh, Taylor , Milosevic, Hitler, Kagame na Omar
Hassan al-Bashir, wa na kesi moja!
Sasa, kwanini
washitakiwe wengine akina Bush na Blair wabaki?
Marekani,
Uingereza, Urusi, Ufaransa, Uchina hawaoni kwamba hawa jamaa wana kesi ya
kujibu The Hague, sambamba na Kagame, al-Bashir, Taylor na Bemba?
Wanaendekeza ‘double standards’ katika masuala ya msingi ya amani na usalama wa
dunia eeh?!!
Ndugu yangu raia wa
Rwanda, aliniandikia hivi:
“ Kuhusu Bush,
Blair ,Sadam na Tayor kweli napenda sana kuona munajali sana kwandika
mataifa ya mbali na munajitaidi kwelimisha wa Tanzania.
Lakini, unapoandika
Vibaraka kama Sadam na Taylor namuna Marekani waliatumia kuua ndugu zao
ukasahau mtu Kama Kagame wakati ndiye mtu wa hapa karibu! Kwanini
ninyi Watanzania
munaogopa kwandika mateso ya Wanyarwanda wanaopata kwasababu ya Kibaraka
kagame?
Yani ni kwamba
hamujue au mumepata kitu kidogo kwasababu ninyi munandika tu mateso ya wa Iraq
, Liberia mambo ya Rwanda hamutake kuyajurisha watanzania?
Ebu wewe niambie kama
umewayi kusikia maadamano ya chama cha upinzani Rwanda, umewayi kusikia chama
cha upinzani Rwanda kinafanya mkutano wewe jiwulize Rais wa zamani anawekwa
ndani eti kwasababu anataka kuunda chama
abu jiwurize wewe Rwanda
wanapata wapi silaha wapi za kupigana hadi kukakamata Congo nzima wewe juwulize
tangu Kagame awekwe madarakani na Wamerikani?
Ukiwa
wazili(Waziri) Muhutu ikimariza tu ni jera au injee au unakufa wewe jiwurize
mimi nashangaa sana Tanzania jinsi wanatuonea sisi wahutu hamutake kuweka mambo
hazarani sasa ivi kuna mtu yupo ata last month alikuwa Arusha kwenye ire
mahakama(ICTR) yeye arikua Murinzi wa kagame anasema namuna Kagame aritowa
amuri ya kungausha ire ndenge na ndege iyo ndio mwanzo wa mauwaji yeye
arishiriki mia kwa mia anatoa ushahidi wa kutosha lakini iyi mahakama inakataa
kumukamata kwa sababu Marikani hawataki kwanini vitu kama ivyo hamubyandike
wakati vipo ata kwenye Internet
watutsi wariuua watu uko
Congo hadi leo ati wanasema kuna wanyamurenge wanyamurenge wagapi uko congo
wakati ni wanyarwanda watupu wewe nenda uko Ubarozini uwurize
niwafanyakazi wagapi wahutu wote kwanzia Borozi ni watutsi hapa tu Dar es
salaam only warinzi watanzania tu wengine ni watutsi wakati Rwanda hawafike ata
1m wakati wahutu ni 7m sasa wapi na wapi wewe wuriza wacongo mateso wanayopata
kutoka kwa wanyarwanda watusi sisi na wacongo tuliyishi nao vizuli lakini tangu
Kagame amekuja amawaingiza kwenye vita tama tu ya yeye ya madini ya akisaidiana
na usa wanawatesa wa congo unajuwa wacongo mambo ya vita hawajuwe wanajua tu
Ndombolo na kupenda wanawake tu!
lakini Kagame ameamua
kuwatesa
muwe makini na
kumwingize katika EAC kwababu watu wa kagera warsha sema nia ya Kagame ni
kureta Tutsi –Land!
wewe kama unaitaji mengi
zaidi
sema lakini mujuwe kama
Wanyarwanda tumevamia na Kagame na wa wamerikani kwa sababu ya madini ua congo
ni kwamba wamerikani wamuhandi kumpa Madaraka yeye akawapa Congo ndio mana
anauua hawaseme kitu mutsi akifa ni Genocide kama vile Isaiel yani Mparistina
akifa sio mauuaji lakini mwisirael akifa ni mauuaji yani ndungu tuakufa kama
sio binadamu sasa wewe anza kua unadika vitu vipo karibu yako ayo mambo ya Iraq
badaye sawa”, aliniandikia rafiki yangu raia wa Rwanda, ambaye jina
limehifadhiwa.
Hivi ndivyo Wanyarwanda
waliotimkia Ughaibuni,kumhofia Kagame wanavyolaumu vyombo vya Habari vya Afrika,hususan
Tanzania,kushindwa kuandika ukweli kuhusu Paul Kagame na wenzake wanavyofanya!
|
No comments:
Post a Comment