UHARIBIFU MKUBWA wa Mzingira hapa Duniani, ni moja ya kichocheo ama chanzo cha safari za wanasayansi katika Anga za Juu.
Tangu
mwaka 1969 akina Neil Armstrong walipofanya safari katika mwezi,
wanasayansi wa Mataifa makubwa wamesafiri kwenda anga za juu ili
kutafuta nishati, na hata makazi huko.
Watu wenye fedha wanatafuta viwanja vya kuishi huko Mars, wengine wametafuta sehemu ya kuzika wafu wao huko!
Inakisiwa
hii Dunia imeharibiwa sana kwa sumu,uharibifu wa maji na anga kiasi
kwamba uhai katika dunia hii hautakuwepo miaka 40 tu ijayo!
Uharibifu
wa mazingira hapa duniani, unapoongeza kitisho cha uhai katika sayari
ya Dunia,matajiri wa Ulaya na Marekani, wanapanga kuitoroka Dunia, ili
wakaishi katika anga za Juu,mfano katika sayari ya Mars ambako kuna kila
dalili ya maji na uhai.
Viwanja
vimepimwa huko, watu wenye fedha kutoka nchi mbalimbali zenye
vita,migogoro,uchumi mbaya,misuko-suko yenye kutokana na uharibifu
mkubwa wa kimazingira n.k wanapanga kuitoroka Dunia yenye njaa,vita na
majanga ya kimazingira.
Zaidi
ya watu 200,000 hapa Duniani wametuma maombi kutaka kuhamia
Mars,kufuatia hofu ya majanga ya kimazingira,maradhi mabaya,njaa n.k
Hawa
wanatoka takriban nchi 140 hapa Duniani wamo pia Marais wa Mataifa
makubwa. Hawa wanaona wakitorokea sayari ya Mars wanaweza kuepuka kifo
kinachoinyemelea sayari hii inayochafuliwa kwa mionzi ya sumu, uchafuzi
wa anga,hewa, uchafuzi wa maji ya maziwa,mito na bahari n.k
Kanda
ya Ziwa, haijafahamu kwamba, wakati Marais kama Barack Obama wanahaha
kutafuta makazi katika Anga za Juu kama katika sayari ya Mars, huku
ndiyo kwanza majumba kama mahoteli makubwa hujengwa ndani ya eneo la
mita 60 za Ziwa Victoria,mito inayomwaga maji katika ziwa hili na kilimo
kinafanywa mita chache toka ziwa na mito.
Imeelezwa
kwamba miji ya Bunda,Mwanza, Musoma na Bukoba,kuna viwanda,mahoteli na
wananchi wanajenga ndani ya eneo la mita 60 ambalo haliruhusu shughuli
za binadamu kutoka vyanzo vya maji kama mito,maziwa,bahari n.k
Mahoteli
yamejengwa ziwani na mengine yako mitoni, shughuli za kiuchumi
zinaendeshwa kama kawaida kinyume cha sheria za Mazingira huku Kanda ya
Ziwa.
Hivi
karibuni, Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira(NEMC) limekusudia
kubomoa sehemu ya Hoteli ya Royal Sunset Beach,iliyopo katika fukwe za
Luchelele, Nyegezi jijini Mwanza,kufuatia ujenzi wa hoteli hiyo kukiuka
sheria za kimazingira.
Royal
Sunset Beach, inamilikiwa na Mkurugunzi wa Jiji la Dar es salaam,Wilson
Mbonea Kabwe, imejengwa ndani ya mita 60 kutoka ndani ya maji ya Ziwa
Victoria.
Kabla ya kuhamishiwa Dar es salaam,mmiliki wa Hoteli hiyo, Royal Sunset Beach, alikuwa Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza.
Kulingana
na Mwanasheria wa Baraza la Taifa la Mazingira(NEMC),Manchare Suguta,
kujenga ndani ya eneo la mita 60 kutoka vyanzo vya maji,ni kinyume cha
sheria ya Usimamizi wa Mazingira,kifungu nambari 57.
Licha
ya Mmiliki wa Hoteli hiyo kutozwa faini ya shilingi milioni 10, wadau
wa Mazingira hapa Kanda ya Ziwa Victoria wanasema, Ziwa hilo ambalo ni
chanzo kikuu cha uchumi, maji ya kunywa na chakula, huharibiwa kwa
kiango cha kutisha.
Wakazi
wa Miji ya Musoma,Bunda, Magu,Mwanza na Bukoba, wasio na mfumo wa
kusafisha maji taka na taka ngumu zenyewe, wanamwaga taka zao katika
Ziwa hili ama katika mito inayomwaga maji Ziwa hili.
Kulingana
na Mradi wa Ulinzi wa Mazingira ya Ziwa Victoria, The Lake Victoria
Environmental Management Project(LVEMP) sehemu ya Pili, wanasema watu na
hata viwanda vya miji ya Mwanza,Bukoba,Musoma,Bunda,Magu n.k na wengine
wa Maswa,Bariadi na Simiyu wanalima mazao katika ndani ya eneo la mita
60 kutoka maji ya mito na Ziwa hili.
Kilimo cha kando kando ya ziwa na Mito inayomwaga maji katika ziwa
Victoria,licha ya kusababisha mmomonyoko wa ardhi,husababisha
utiririshwaji wa kemikali zinazotokana na mbolea na dawa za kuulia
wadudu,na kusababisha hatari kwa maisha ya viumbe kama samaki,
wanyama,mimea,ndege na hata binadamu wanaotegemea maji ya ziwa hilo kwa
kunywa na kuoga.
LVEMP
Phase II wanasema, viwanda vya kutengeneza mafuta (ya pamba) ya kula
huko Bunda,mkoani Mara havikuwa na mfumo wa kuhifadhi taka kwa muda
mrefu.
Viwanda
hivyo,vimekuwa vikitiririsha kemikali na mabaki ya mafuta hayo ziwa
Victoria ambalo liko kilomita chache kutoka Bunda, katika kijiji cha
Guta.
Kulingana na wataalam
wa Mazingira, kemikali za viwanda,majumbani na maduka
zisipodhibitiwa,huweza kusombwa na maji ya mvua hadi katika vyanzo vya
maji hata umbali wa kilomita 100.
Kutoka
Bunda hadi Guta.ni umbali wa takriban kilomita 10 tu; na hali hiyo ya
kutiririsha kemikali na mabaki ya mafuta ya pamba huko Bunda,huhatarisha
maisha ya watu,wanyama na viumbe wanaotegemea Ziwa Victoria kwa maisha
ya kila siku.
Kuna
migodi inayotiririsha kemikali za hatari kama zebaki hadi katika Mito
inayomwaga maji yake katika ziwa hili muhimu kwa uhai wa takriban watu
milioni 30 katika Ukanda wa Mziwa Makuu.
Mifugo Mkoani Mara ilisharipotiwa kufa kwa kunywa maji ya kemikali za migodi,walkati wananchi walishaathiriwa na kemikali hizo hadi kulazwa hospitalini na wengine kupoteza maisha.
Athari
hizi za kimazingira ndizo hufanya sasa matajiri mataifa makubwa kuhaha
kutaka kutorokea katika sayari nyingine kama Mars,ili kuepuka madhara ya
kimazingira katika sayari ya Dunia.
Miji
kama Mwanza, wakazi wake huendesha kilimo kandoni mwa Ziwa
Victoria,hulima bustani kama mbogamboga na matunda ambayo huhitaji
mbolea za viwandani na viuwatilifu vyenye kemikali za sumu.
Mji
wa Musoma,umesemwa na LVEMP II kwamba baadhi ya wakazi wake hufanya
kilimo katika Bonde la Kitaji lenye ardhi oevu,ama chepechepe.
Bonde hilo la Kitaji, zamani likitumika kama dampo la kutupia taka ngumu na Halmashauri ya MANISPAA ya Musoma.
Kemikali
za mbolea za viwandani na sumu za kuulia wadudu pamoja na taka ngumu
zilizokuwa zikimwagwa Kitaji,ni chanzo cha uharibifu mkubwa wa Mzingira
katika Ziwa Victoria huko Mjini Musoma.
Kutokana
na kemikali za sumu kutoka mashambani jirani na chanzo hiki cha maji,
na kutokana na kumwaga taka ngumu,ujenzi holela ndani ya mita 60
,ukataji holela wa miti kando ya mito kufuatia upanuzi wa mashamba, maji
ya Ziwa Victoria yameharibiwa maradufu hadi samaki wamepungua na
kusababisha njaa na ukosefu wa ajira mjini Musoma.
Samaki
wametindika hadi bei yake imepanda maradufu.Samaki ni chanzo kikuu cha
chakula aina ya Protini kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa Victoria, sasa
kufuatia hali hiyo ya uchafuzi mkubwa wa mazingira,eneo la Kanda ya Ziwa
linakabiliwa na hatari na majanga ya kiafya na umasikini wa kutisha.
Jijini Mwanza wakulima wa mboga na matunda hulima kando ya Ziwa na kutiririsha kemikali ndani ya maji ya ziwa.
Mamlaka
ya Bandari(TPA) NAO HULALAMIKIWA kwa kutokuwa na mfumo wa maji taka ili
kuzuia mafuta machafu yanayotoka melini na katika mitambo,kumwagikia
ziwani.
Kuna
waosha magari na wenye viwanda ambao wamekuwa wakitiririsha maji ya
kemikali ziwani,na hata katika mashamba ya wananchi na kuwasababishia
hasara kubwa. Maelfu ya ekari yanaharibiwa na kemikali zitokazo
viwandani na migodini,na wakati mwingine mifugo wanaokula nyasi na
kunywa maji yaliyoathiriwa na kemikali hufa.
Kanda
ya Ziwa kuna viwanda vingi na watu wasiokuwa na Mfumo wa kusafisha
maji(Sewage System) matokeo yake kemikali nyingi huwamwagwa ziwani na
katika mito.
Lake
Victoria Environmental Management Project(LVEMP Phase II) wanasema
uchafuzi wa kimazingira unaofanywa kando ya mito na ziwa Victoria
huhatarisha maisha ya mamilioni ya watu,mifugo,wanyamapori na mimea.
Matokea ya uharibifu huu ni hatari ya kiafya,umasikini uliokithiri kwa wananchi na vifo.
Baadhi ya mito inayochafuliwa sana sanjari na ziwa Victoria ni Mto Mara,Kagera,Grumeti,Mbalageti,Simiyu, na Mto Mori.
Baadhi
ya migodi Kanda ya Ziwa humwaga kemikali kama Zebaki ambayo
hutiririshwa hadi ziwani. Zebaki hutumiwa hata na wachimbaji wadogo wa
madini kusafishia dhahabu migodini.
Zebaki inapofika ziwani hudhuru samaki na wanyama hadi walaji wa samaki wako hatarini kuugua saratani.
Upanuzi
wa mashamba huko Simiyu na Bariadi umesemwa kwamba ni chanzo cha
ukataji holela wa miti kandoni mwa mito, pia ni chanzo cha mmomonyoko
mkubwa wa ardhi.
Wakulima wengi hulima hadi ndani ya eneo la mita 60 kutoka chanzo cha maji,kitu ambacho huharibu mazingira na ikolojia.
Kufuatia uharibifu wa mazingira katika mito na Ziwa Victoria,sasa kuna majanga yasiyosemeka.
Wakati
Wazungu wakihaha kutafuta hifadhi katika Sayari ya Mars, Kanda ya Ziwa
kuna uchafuzi wa mazingira na vyanzo vya maji,kuna ukataji wa miti kwa
ajili ya mkaa nk
Matokeo yake eneo zima hilo mvua zitakoma kunyesha kabisa,na hata zaweza kunyesha mvua za sumu(acid rains) zinazoweza kuleta athari kubwa kwa mimea na viumbe hai.
Ni
kutokana na hali hiyo ya uchafuzi wa vyanzo ya maji(water pollution) na
uchafuzi wa hewa(air pollution) Wazungu wanafanya mipango kamambe
kuihama Dunia inayochafuliwa ili wakatorokee Anga za juu,hususan Sayari
ya Mars
0713 324074
No comments:
Post a Comment