Historia ndiyo
Darubini kali iliyomwibua mmoja wa Wanafalsafa wakubwa Ugiriki, ambaye anaweza
kutwambia nini maana ya Ukweli?
Aristotle wa
Athens aliyeishi kati ya mwaka 384 hadi 322 BC. Alipata kusema:
“Truth is
agreement with FACTS and REALITY” ,Tafsiri yangu ni kwamba,Ukweli ni mwafaka
baina ya habari ya kilichotukia na usahihi ama uhalisia wa mambo.
Kulingana na
Aristotle, ukweli huweza kuongopa ikiwa UKWELI nusu-nusu unapowaongoza watu
kwenye UONGO.
Aristotle alisema hivi:
“To say what is that is not or of
what is not that is-is FALSE, while to say what of what is that it is, and what
is not that is not-is TRUE!!
Tafsiri yangu
isiyo rasmi ni kwamba Aristotle alisema kusema jambo kwa namna isivyokuwa namna
kitu kilivyokuwa hakika,ni UONGO;wakati kusema kitu kilivyo hakika na ukasema
kwamba hakiko hivyo wakati hakiko hivyo huo ni Ukweli.
Aristotle,
hutwambia kuhusu UONGO WA UKWELI(The lie of Truth) ambao mfano wake ni kama
kudondosha tone la ukweli katika pipa la Uongo.Ukweli hauchanganywi na uongo
ukabaki ukweli.Sumu kidogo ya panya haichanganywi na unga au mkate,kikabaki
kuwa chakula bali sumu!
Chakula
jumlisha sumu ni sumu,basi.
Naam, ‘a
little truth drop in the bucket’ matokeo yake ni jamii kuamini uongo na
kuufanyia kazi, ndivyo ilivyo hata hapa Tanzania.Jamii hufanyia kazi
umbeya,uongo na upumbavu tu!
Watu wengi
hata hapa Tanzania hudanganywa kwa ukweli kidogo ndani ya uongo mwingi,na
tayari wameathiriwa na sumu ya uongo na umbeya,mishipa yao ya fahamu
imedhoofishwa na majungu na uvumi.
Nilishaandika
kwamba, Daktari akisema ‘Unaumwa Ukimwi’ ni FACTS-ni ukweli dhahiri. Lakini
mpigadebe akisema kwakuwa una kikohozi na kichomi na umekonda-ni ‘Opinion’ ni
maoni tu-maoni siyo ukweli halisi,ni kukisia na umbeya tu.Angalia sasa nchi hii
walivyo hawatofautishi Opinion na Facts!
Ukweli
haufahamiki kwa kusemwa na watu wengi ama kwa njia ya sanduku la kura!
Mwandishi,Derek
J.Morris aliandika katika Jarida la MINISTRY la Juni mwaka huu 2013, kama
ifuatavyo:
“TRUTH is not determined by opinion
poll or popular vote!”
Ukweli
hauamuliwi kwa wingi wa kura za maoni za watu wengi vijiweni! UKWELI huweza
kusemwa na mtu mmoja mwenye taaluma kama daktari kusema ‘una ukimwi’ ndugu zako
na jamaa wote wakashikilia umerogwa!
Ukweli
hauamuliwi kwa sauti kubwa na maandamano ya vibaka na wanasiasa wakasema ndiyo
NGUVU YA UMMA!
Aristotle amesema
watu wengi huchelea kusema ukweli wasije wakachukiwa na umma mkubwa, ‘PEOPLES
POWER’.
Watu wengi
siyo wa kuamini,na mawazo yao siyo ya kufanyia kazi mara zote,wapo wafuata mkumbo
tu,mashabiki na mabingwa wa kuigiza kila jambo na kuangamiza jambii kama
tunavyoona leo madawa ya kulevya,bangi na ndoa za jinsia moja!
Bendera
kufuata upepo tu! Kizazi hiki kimepotoka mno,kwa kuiga ya Magharibi ya watu
wengi, sasa wachache hawana cha kusema,wataalam kama madaktari,
wahandisi,maprofesa n.k ushauri wao ulishakataliwa na public opinion.
Siku hizi ‘wengi
wape’ japo wapumbavu sana!
Watu wengi,
aghalabu mbumbumbu mzungu wa reli fuata mkumbo, propaganda za siasa huishia
kuipotosha jamii na kizazi hiki kwamba ndiyo haki za Binadamu.Haki za
Mashoga,haki za wasagaji,haki za watoto kutochapwa viboko n.k
Watu
wachache wenye haki aghalabu hawana ubavu wa kutetea ukweli usiochanganywa na
uongo,umbeya,hisia tu na majungu.
Wakristo
wameonywa sana kuwa waangalifu katika kuamua kati ya UKWELI(Right) na
uongo(Wrong) kwa kufuata kura za maoni za wajinga wengi(Opinion poll) ama kura
za watu wengi wanaopenda uhalifu na uovu(popular vote).
Kuna watu
hawataki hata sheria ziwepo ili waingie mitaani na kupora mali za wenzao kwa
kisingizio, Maisha ni Magumu!
Wachache
wenye hekima wanajua matokeo ya kukosekana kwa sheria,lakini wapumbavu wengi
watalaani kuwepo sheria,mahakama,polisi,mgambo,mahakimu n.k hawa wote ni vibaka
akilini.
Ukweli na
uongo,sharti kuamuliwa kwa muktadha wa mafundisho sahihi ya Neno la Mungu(Biblia
n.k)Kwa mfano Zaburi 119:105 HUSEMA Neno la Mungu ni Taa iongozayo miguu ya
wenye haki.
Watu
wanasema Mungu alishakufa,hayupo na neon lake ni batili,sasa hawa wanakwenda
njia gani halafu uwafuate gizani?
Watu
wanapotaka kwenda upande wa kweli wa Historia,wanapaswa kugeukia hekima ya
Mungu tu basi. Hekima ya Mungu ni Ukweli,haki,amani,upendo n.k
Biblia,kwa
mfano husema njia ni nyembamba sana iendayo kwenye ukweli nao wanaoona ukweli
ni wachache tu.Wengi huenda kwenye uongo,maana njia ya uongo ni pana hata
mbumbumbu huiona.
Njia ya haki
huonwa na wenye hekima,ni nyembamba hutazamwa kwa hadubini kali.
Ni kwa
sababu hii,watu shupavu wanaotetea ukweli(rejea tafsiri ya ukweli) hawapendwi
na wengi;huishia kutengwa,kusulubiwa.
Kusema
kwamba kitu hiki hakiko hivyo wakati kweli hakiko hivyo ni hatari,unafanywa
kama Nabii Yeremia,Martin Luther King Jr,Martin Luther wa Ujerumani,Socrates,Yohana
Mbatizaji,orodha ndefu.
Katika
kitabu cha Luka Mtakatifu 3:11-14 Yohana Mbatizaji anapokemea rushwa,ufisadi
miongoni mwa maofisa wa serikali fisadi, anapokataza masikini kuporwa wake na
mali zao, anaishiwa kunyongwa kijinga.
Nani
atatetea kichwa ili akatwe kichwa?
Marko
Mtakatifu 6: 17 na 18 hutwambia kwamba ni mtu labda mmoja tu anayekubali ukweli
usemwe potelea mbali apoteze maisha yake,kuliko kuacha wajinga wengi waseme
uongo na kuufurahia.
Public
Opinion, mara nyingi hukinzana na ukweli na uhalisia wa mambo-husema minyoo huletwa
na wachawi,na wala siyo uchafu na kula bila kunawa ama kunywa maji yasiyo
chemshwa!
Ukisema
ukweli utaitwa msaliti! Kuna mifano tele katika Biblia,niiache wengine
wananiambia hataki kusoma biblia.Biblia ni kitabu,hawapendi kusoma ila kucheza
na kucheka-cheka tu.
Nimesema
kwamba ukweli huonwa na wachache tu na husimamiwa na watu shupavu wawili ama
watatu tu-wengine bendera kufuata upepo unakoelekea, watu wengi wanafiki tu.
Wanaosema
ukweli huitwa waongo na waongo huitwa wakweli.Mara nyingi waongo huenda kinyume
cha Historia-The wrong side of History.
Historia
inamsema Socrates(469-400 BC) ALIVYOULIWA na utawala wa Athens kwa kukataa
umbeya kwamba kuna miungu 391 inatawala juu ya Mlima Olympus!
Walimpa sumu
ainywe kwa kutetea kwamba kuna Mungu mmoja na huishi mbinguni tu. Yesu aligoma
kufuata dini ya ukandamizi ya Kiyahudi, Martin Luther aligomea mafundisho ya Kipapa,
Martin Luther King Jr. ambaye juzi Ndoto yake( (I have a Dream)ilisherehekewa
miaka 50 na akina Obama, aliuliwa Aprili 1968 kwa kusisitiza ukweli kuhusu
ubaguzi wa rangi Marekani, aliuliwa na Pentagon kwa kutetea ukweli.
Wapo akina
Mandela wamesota rumande miaka 27, wapo wengine walifukuzwa kazi n.k
Katika
mfululizo wa makala haya nitatilia shaka kila kinachoitwa UKWELI ili kutufanya
kuchunguza mambo kwa akili tunduizi(critical mind) kuacha mikumbo na umbeya wa
siasa za kipumbavu zinzoleta ugomvi katika jamii hii.
Tutajadili ‘fuata
mkumbo’ iliyoleta shida hapa Tanzania, katika Nyanja tofauti siyo siasa tumhata
dini zinazoshadidiwa na watu.
Nitakuwa
nikitumia nukuu za wanafalsafa,wasomi,wataalam lengo ni kukiokoa kizazi hiki na
kuiga na kufuata mkumbo wa kila kinachosemwa ili tuepuke propaganda,matangazo
ya uongo redioni kwenye tv na maamuzi ya wengi katika kura za maoni(Opinion
polls)
Nitatilia
shaka hata katiba mpya itakayoamuliwa na wengi,lakini vipofu wakaacha maoni ya
wachache ama mmoja mwenye hekima,mtu wa haki mnyoofu n.k
0786 324 074
No comments:
Post a Comment