APRILI 6
mwaka 1994,Rais wa Rwanda, Juvenal Habyariana, na mwenzake wa BurundI,Ntaryamirwa Cyprian,
wakiwa ndani ya ndege aina ya Falcon-50, wakatunguliwa kwa kombora na Waasi wa
Kitutsi,RPF.
Huu ndiy
mwanzo wa mauaji ya Halaiki ya Rwanda,nakichocheo cha vita Burundi na hata
Mashariki mwa Congo,JK Kongo.
Migogoro ya
Watu-tsi na Wahutu,inayotiwa mafuta na Mabwana wa Vita(WAR-LORDS)Paul Kagame na
Yoweri Kaguta Museveni,sasa cheche zake hutishia hata amani ya Tanzania.
Wakimbizi
maelfu wanakimbilia hapa Tanzania,kufuatia vita baina ya Wahutu na Watu-tsi wa
Rwanda,Burundi na hata walewaliotimkia Jamhuri ya Kongo,kwa sababu na muda
tofauti.
Tuwatazame wanaojiita
Waasi wa Congo,M-23,CNDP na FDRL wanaosababisha Jenerali Kagame aanze
kututukana huku.
FDRL(Democratic
Forces for The Liberation of Rwanda) ni kikundi cha wanamgambo wa Kihutu ambao
ni adui wakubwa wa KAGAME na nduguze Watu-tsi.
Kama jina
lao lilivyo,baada ya mauaji ya halaiki, wakatimkia Congo ambako hata leo
wanaota kumtimua Kagame mamlakani.
Hawa,ni
Wahutu(raia wa Rwanda0 wanaompinga Kagame.
Sasa,Rais
Jakaya Kikwete akiwa Addis Ababa, akamshauri Kagame ambaye naye alihudhuria
moja ya mikutano ya AU kukaa meza ya mazungumzo na hao Waasi wa Kihutu wa FDRL
ili kuleta amani na utangamano Maziwa Makuu,likawa kosa kubwa kwa Kagame na kuanza
kurushamakombora ya kama alivyozoea.
Kingalipo
kikundi kingine cha wanamgambo wa Majimaj(Mai mai) ambacho pia kimejichimbia
misitu ya CONGO ,kinapeleka mauti huko Jamhuri ya Congo,kinaitwa ADC.
Ndani ya
Congo kuna jamaa zake Kagame na rafikiye,Museveni yaani M-23.
Jina hili
hutokana na tarehehe 23 Machi mwaka 2009,siku ambayo serikali ya Congo ilifikia
makubaliano ya Amani na kundi la Waasi wa CNDP,wakajumuishwa katika majeshi ya
serikali.
Naam, hawa
ndiyo M-23 Movement ambao ni kikundi cha Waasi kama 5,500 hivi waliojichimbia
Kivu ya Kaskazini na kuuza kifo kwa raia wa Kongo,na hapa kwetu wamesababisha
kilio kwa kupoteza wanaeshi wetu.
Wametokana
na misuguano isiyoisha baina ya serikali ya DRC na hawa wanaojiita Waasi kwenye
mipaka ya Uganda,Rwanda na Burundi.
Hawa M-23
wametokana na CNDP(Congress for the National Defence) kilichoanzishwa na ‘jamaa’
za akina KAGAME na Museveni,mmoja anaitwa Jenerali Nkundabatware,Desemba 2006
huko Kivu.
Januari,2009
CNDP Kilikosa umuhimu,kikaparaganyika,hadi eti Nkunda akakamatwa na majeshi ya
Rwanda,ambayo sote tunajua yalimpa chakula,nguo,fedha,silaha n.k
Sehemu ya
kundi hilo Iliongozwa General Bosco Ntaganda, ambacho kiliingia mkataba wa
amani na serikali ya Congo Machi 23, mwaka 2009.
Wapiganaji
hawa walipounganishwa na jeshi la Congo,CNDP kikawa chama cha siasa,wanachama
wao wakaachiwahuru magerezani.Rais wa kundi hilo akiitwa Askofu Jean-Marie
RUNIGA Lugerero!
Utaona ‘maaskofu’
wa siku hizi wakiongoza vikundi vya wanamgambo na kuua raia! Jihadhari sana na
wanaojiita Maaskofu,Manabii na Mitume wa siku hizi!!
Rais wa
kundi la M-23 akiitwa ‘General’Makenga Sultan-wote hawa mabwana wa vita
walikuwa CNDP.
Hawa hawakuwahi
kuaminiwa na serikali ya mjini Kinshasa,hata baada ya makubaliano,Rais Joseph
Kabila wa Kabange aliamuru Jenerali Nkunda akamatwe Aprili 11 mwaka 2012.
Hawa ni
Watu-tsi,ambao ni adui wakubwa wa kile kikundi cha Wahutu cha Democratic Forces
for the LIBERATION OF Rwanda(FDRL).Hawa wote wanaendesha harakati zao za
kigaidi ndani ardhi ya Congo,ndiyo maana kuna shida kila kukicha.
Bila shaka,
msomaji unapata picha kwamba, kuna vikundi vya Wahutu(FDRL) waliokimbia Rwanda
wakati wa genocide, walitimkia Cogon a huko wanaendesha harakati za kumpinga
Kagame.
Hawa Watutsi
walimsaidia Papaa Kabila(baba0kumwondosha Mobutu madarakani, na baada ya vita
hivyo,walijumuishwa katika majeshi ya serikali.
Hawa
Watu-tsi, wanapokea msaada kutoka Rwanda na Uganda, eti sasa mazungumzo ya
kuleta amani Congo hufanyika mjini Kampala chini ya usimamizi wa Kaguta Museveni!
Kichekesho kikubwa.
Majeshi ya
serikali ya mjini Kinshasa(FARDC) yamekuwa hayawezi kuwatimia hawa jamaa za
Kagame na Museveni huko Mashariki mwa Kongo,kwa sababu ambazo sasa tayari
umeziona kufuatia mfululizo wa makala haya.
Wakati
mwingine, majenerali wa FARDC walijidai kujisalimisha kwa Waasi,wakawapa zana
za vita na chakula katika kinachoitwa ‘mapigano makali’ ambamo Waasi wanawateka
askari wa serikali!
Wanafanya
usanii huo huku majeshi ya Umoja wa Mataifa(MONUSCO) yakiangalia hata ujambazi
unaofanywa kwa raia wa Congo.
Hawa MONUSCO
wakati mwingine kazi yao ni kupora madini na kuuza Ughaibuni,na wala siyo
kulinda raia wa Congo kama walivyotumwa na Umoja wa Mataifa,
Baada ya
majeshi ya Tanzania kujumuishwa katika jeshi la MONUSCO, sasa kampeni ya
kuwaswaga hao M-23 inaleta tija,wanapigwa ilivyo,ndiyo maana wanasisitiza
mazungumzo kuendelea Kampala,ili ikiwezekana warejeshwe jeshini
Kinshasa,viongozi wao wapewe mishahara na serikali ili wadumu kufanya ujambazi!
Watanzania
tunasema kwa uchungu mkubwa kwa sababu tumekwishamwaga damu ya askari wetu huko
Kongo, tayari M-23 ni adui yetu wa dhati,ndiyo maana Kagame anachuki ya wazi
kwetu.Ingekuwa heri Umoja wa Mataifa ungeongeza jeshi ili hawa waasi watwangwe
vilivyo,wanapoingia Rwanda kupewa chakula,nguo na bunduki,Rwanda wapewe kibano!
Kuna njia
tele za kuipa kibano serikali ya Kagame ikiwa ni pamoja na Vikwazo vya
kiuchumi, ama kunyimwa msaada wa kijeshi na kuuziwa silaha na mafuta.
Kuishinikiza
serikali ya Kinshasa kuzungumza na Waasi,wakati kukiwa na wakimbizi 200,000 au
zaidi wanaokimbia mapigano huko Goma,kuna leta ukakasi.
Kagame
akiambiwa kufanya mazungumzo na FDRL anakasirika;wakati hao M-23 wakitwangwa
vikali na maiti zao kubanikwa na majeshi ya serikali, kelele zinapigwa za
mazungumzo mjini Kampala!
Mazungumzo
hayo yalianza Desemba 9,mwaka 2012.
M-23
ilianzishwa rasmi Aprili 4,mwaka 2012 wakateka Goma kirahisi sana,kabla ya
Makomandoo wa Tanzania kuwachakaza vikali hao Waasi na kuwatimua Goma chini ya
mwamvuli wa MONUSCO.
Hawa jamaa
za Kagame sasa wamejificha Rwanda! Inasemwa wako mpakani,huku makombora
yanapodaiwa kutua Rwanda ili kuwasindikiza huko,ama wanafanya mchezo wa
kuchongea kwamba MONUSCO wameivamia Rwanda!
Rais Kikwete
anapotaka Rwanda inayoongozwa na serikali ya RPF(ya Watu-tsi) kukaa meza moja
na Waasi wa Kihutu,FRDL waliokimbilia Kongo ili kuongeza vurugu huko maana yake
nini?
· Kwamba,ni mazungumzo ya amani
wanayotaka Kagame na Museveni na jamaa zao wa M-23 waongee na serikali ya mjini
Kinshasa.Ni sawa na namna ambavyo Kagame angezungumza na FDRL ili kuleta amani
Maziwa Makuu.
· Hata RPF(Rwandan Patriotic Front)
walipokuwa Waasi wa Rwanda walianza kuzunguza na Habyarimana.
· Mazungumzo ya mani(Peace talk and
cease fire agreement)mwisho huweza kuzaa mikataba ya amani(peace accord) na
kuleta amani na utangamano kati ya nchi za migogoro.
Sasa tujiulize Kagame anapojidai kutuliza uhasama kati ya Watu-tsi na
Wahutumbaada ya genocide mwaka 1994, anaposhauriwa na Kikwete kuzungumza na
FDRL anakasirika nini?
Ili kuleta usalama Mashariki mwa Kongo Waasi wa M-23,CNDP,Maimai n.k
wanapozungumza na serikali ya Kabila mjini Kampala, si busara pia Kagame
kuzungumza na Wahutu wa FDRL mezani sasa ili kualiza vita Ukanda wa Maziwa
Makuu?
Mbona hata Waundi wamekuwa wakipatanishwa na akina Nyerere,Mandela,Bill
Clinton,Mwinyi n.k
Hawa walitia saini makubaliano ya
amani mjini Arusha mwaka 2000 chini ya Mandela na Clinton.
Ndiyo maana,wanamgambo wa Kitu-tsi walioko Kongo tunasema wametumumiwewa
kuangamiza Wahutu waliokimbiliahuko! Wahutu nao ni binadamu,wahurumiwe.
Rais Kikwete anajua mambo haya, alipomwambia Kagame kuzungumza na FDRL
ligusa kizinga cha moto wa visasi,moto ukalipuka.
Wapo watu wanasema:
“Kikwete,kama siyo kuropoka,imemhusu nini kuingilia Rwanda dhidi ya Waasi
wa FDRL?”
Swali la kijinga kwelikweli!
Hawa waasi ama Wakimbizi wa Rwanda wanapokimbilia Kongo,hususan Wahutu
wanapoleta balaa la vita huko, ama wanapokimbilia kwetu,Kagame na Museveni
hawatakuja hata huku kwetu kuwasaka Wahutu ili kulipa kisasi?
Tumeeleza kisa cha mauaji ya Kanungu zama za Kibwetere.
Tumezungumza umuhimu wa Amani Maziwa Makuu.
Wanamgambo wa Intarahamwe-adui za Kagame-ni wakimbizi wa vita kama
wakimbizi wengine.
Sheria gani inasema wawindwe na kuuliwa tena katika ardhi ya Kongo?
Kwa nini wasizungumze kama Kongo wanavyozungumza?
Mbona tunazuia genocide(1994) ili kufanya genocide nyingine dhidi ya
Wahutu wa FDRL?
R
No comments:
Post a Comment