Rais Jakaya Kikwete aliongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano wa chakula mjini Rome , mji mkuu wa Italia mwaka 2009.
Rome , jiji lililojengwa miaka 754 kabla ya Kristo, ndilo makao makuu
ya Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa(FAO).
Viongozi hawa wa dunia, sasa wanahangaika kumwokoa mwanadamu katika maangamizi, siku baada ya kesho.
Pamoja na mambo mengine, ilisemwa katika mkutano huo kwamba, watu
bilioni moja miongoni mwa bilioni 7 wanaoishi duniani siku hizi,
wanakabiliwa na njaa kubwa.
Usalama wa chakula unakosekana.
Njaa, imeletwa na sababu nyingi.
Kubwa
ni kwamba, ukame ama kiangazi kikali huchukua muda mrefu siku hizi,
hadi mazao mashambani hunyauka, mifugo hufa na uchumi huwa mbaya kwa
kila mkazi wa dunia hii.
Hii ni kusema, chakula hakitakuwepo kabisa siku baada ya kesho, kama
uharibifu mkubwa wa mazingira unaofanywa sasa hautadhibitiwa.
Nataka
kujadili madhara ya uchafuzi wa hewa(Air Pollution) katika anga la
dunia hii tuishiyo, unaofanywa na mataifa makubwa yenye viwanda.
Marekani ni miongoni mwa mataifa hayo.
Kila
mwaka, Marekani na mataifa mengine takriban 40 yenye viwanda vingi,
hurusha angani moshi, vumbi, joto, mvuke na kemikali za sumu, nyingi.
Hizi sumu hufanya hali ya hewa kuwa isiyo na manufaa kwa maisha ya
mwanadamu.
Mpaka hapa, nimeandika kwamba, kuna sababu kubwa mbili za kutokea kwa majanga ya asili duniani:
Ongezeko
kubwa la watu ambao sasa wamefika bilioni 7 na uchafuzi wa hewa angani,
majini na nchi kavu. Tunataka kuona nyuma ya pazia lililofunika siku
baada ya kesho.
Kuongezeka kwa ukungu hewani, angani, wakati mataifa yanapodhamiria
kuigeuza dunia na mataifa kuwa yenye Nguvu ya Nyuklia(Nuclear Power),
ili kupata nishati ama nguvu ya umeme-viwanda vya Nyuklia vinatoa
mvuke mwingi angani unaoleta ukungu.
Magorofa makubwa na marefu sana katika majiji makubwa ya dunia, yanaelea siku hizi katika anga lililogubikwa ukungu mzito.
New
York, Ottawa, Canada, Tokyo nchini Japan na majiji mengine mengi
duniani, hufunikwa na ‘blanketi’ zito la ukungu, moshi, masizi ya
viwanda, moshi wa magari, migodi, magari moshi, ndege kama Concord na
mitambo mingine.
Miezi michache iliyopita, nilinunua mkanda wa DVD wenye filamu
tano(5Blockbuster Movies) iliyokuwa na sinema hizo tano kali sana zenye
kuonesha matokeo ya kuharibu mazingira ya anga la dunia.
‘THE DAY AFTER TOMORROW’ ni filamu inayoonesha dunia inavyokwenda kuwa
‘siku baada ya kesho’ ikiwa viwanda vya mabwanyenye wa Ulaya na
Marekani, na Mahariki ya Mbali, havitatakoma kumwaga sumu zake katika
anga la dunia na kusababisha Ongezeko la Joto duniani(Global Warming)
linalosababisha haya majanga ninayosema.
Naam, majanga yanayotishia uhai wa mwanadamu kama vimbunga, chamchela,
tufani, matetemeko ya ardhi, mawimbi makali yanayozoa maji baharini na
kuigharikisha nchi kavu, kama ile tufani ya Katrina huko Marekani.
Katika filamu hiyo kali sana , ‘The Day After Tomorrow’ kumeonyeshwa
mafuriko makubwa yakiigharikisha nchi kavu, majengo marefu ya miji ya
Marekani, shughuli za watu zikakoma, magari ya fahari yakasombwa na
mafuriko, magereza yakabomoka, wafungwa wakatoka na mafaili ya kesi za
majambazi na wahalifu wengine yakasombwa na mafuriko- katika kiama hiki
hakuna serikali, hakuna jaji, hakimu, wala sheria na ustaarabu, ni
machafuko.
Kwa sababu mwandishi wa safu hii siyo mwanasayansi, amini usiamini,
nimeona katika filamu hiyo kwamba mwisho wa majanga hayo kama matetemeko
ya ardhi kama tsunami na vimbunga vikali kama Mitch, ni dunia kuanza
kufunikwa na maji kisha barafu tupu.
Kila mtu atafute mwakozi wake, kwa sababu majanga ya kiasili yaletwayo
na Ongezeko la Joto Duniani linalosababisha mvua kubwa kama El-Nino,
tumelishuhudia Same, Kilimanjaro, ardhi anapoanza kuwafunika watu.
Kufuatia Ongezeko la Joto Duniani, siku hizi mabonge ya barafu katika
Ncha za Kaskazini na Kusini(North Pole&South P ole) yameanza
kuyeyuka na kujaza maji baharini kwa kimo cha futi 100, 200 kwenda 250.
Maji
haya yanapovuka mipaka ya bahari na kuingia nchi kavu, kunako starehe
na shughuli za kiuchumi za binadamu, ndiyo dira halisi ya siku baada ya
kesho.
Na hii ndiyo ‘Pata-Potea’ ya maisha ama uhai duniani.
Miaka
hii ya 2000 imetabiriwa(na wanasayansi) kwamba kutakuwa na tani milioni
404 za taka sumu hewani ambazo huzidisha joto duniani.
Kuna
tani milioni 76 za sulphur dioxide, tani milioni 207 za carbon
monoxide, tani milioni 53 za hydrocarbons, tani milioni 30 za nitrogen
oxides, na tani milioni 28 za vipande vya vumbi, moshi hata wa wavuta
sigara na bangi ambao sasa ni wengi sana duniani!Kuna uchomaji mwingi wa
misitu siku hizi.
Kuna vumbi na masizi pote angani. Inasemwa kwamba, binadamu ndiye
mnyama wa kwanza kwa uharibifu wa mazingira, yawe ya mito , maziwa
mbahari, nchi kavu n.k Binadamu hujiharibia maisha yake mwenyewe ili
asiweze kunusurika hiyo siku baada ya kesho.
Matokeo yake, ni majanga niliyotaja; ukame unaoleta kitisho cha njaa
hadi wakuu wa dunia wamekutana mjini Rome , Italia, ili kujadili namna
ya kuondokana na njaa hiyo kubwa sana inayokuja.
Wakuu wa dunia walipokutana mjini Rome na kujadili kitisho cha njaa ni kitu kikubwa sana kuliko unavyofikiria.
Hata Papa Benedict XVI alihudhuria mkutano huo.Papa huyu alishastaafu siku hizi.Lakini alisema kuhusu kinachoujia ulimwengu.
Bila shaka, aliwakumbusha wakuu hao wa dunia, kwamba njaa hiyo kubwa
ilitabiriwa na Yesu katika kitabu cha Injili ya Mathayo, sura ya 24.
Njaa ni dalili za ‘Mwisho wa Dunia’ ama ‘The D-Day ‘ unaofungamana na
kuja kwa Yesu mara ya pili.
Bila
shaka, siku ya kiama hii itakuja kabla ya dunia kuanza kuganda kwa
barafu itakayofunika miji yote kama inavyooneshwa katika hiyo filamu ya
‘The Day After Tomorrow’.
Kufuatia
Ongezeko la Joto na milima ya mabonge ya barafu kuanza kuyeyuka huko
North Pole na South Pole, maji yatagharikisha visiwa, mengine yatasombwa
na mawimbi makali na makubwa sana yaliyoletwa na vimbunga na tufani
kama Katrina, kwenda kugharikisha makazi ya watu mijini na mashambani.
Mambo haya yanatabiriwa katika hiyo Filamu ya ‘The Day After Tomorrow’.
Labda
ni gharika nyingine kama ile ya Nuhu, iliyotokea miaka 2000 Kabla ya
Kristo. Wewe msomaji utajificha wapi, siku hiyo baada ya kesho?
Pia, katika DVD hiyo yenye filamu tano ‘kiboko’(5Blockbuster Movies),
kuna moja inaitwa, Independent Day na nyingine inaitwa, ‘The Perfect
Storm’.
Hii
Perfect Storm inaonesha bahari ya Atlantic ikichemka kwa mawimbi makali
hadi futi 100 juu ya uso wa bahari, kufuatia kimbunga kinachoitwa
Grace.
Ilikuwa Oktoba mwaka 1991.
Sijaelewa ni kwa nini vimbunga vingi vinabatizwa majina ya akina mama!
Mimi
siyo mwanaharakati wa haki za wanawake; wao wapo wanaweza kujitetea
kwanini majanga ya asili yabatizwe kwa wingi majina yao .
Naam, nazungumzia siku baada ya kesho(The Day After Tomorrow) ili
kuwaonyesha wasomaji madhara ya uharibifu wa mazingira ya sayari
tunayoishi.
Matajiri
wameanza kutafiti kama kuna maisha katika sayari ya Mars na mwezini;
labda wana mpango wa kuhamia huko, hii sayari inapoangamizwa kwa sumu za
hewani na ukataji wa miti inayopunguza sumu hizo.
Pia kuna filamu kali sana iitwayo, TITANIC. Ni tukio la kihistoria
linalosimuliwa na akina Leonardo DiCaprio(huyu alicheza pia filamu ya
BLOOD DIAMOND) na Kate Winslet, wanaofahamika kwa majina ya Jack na
Rose.
Walikuwa katika penzi changa la tashtiti, ambao baada ya kuzama kwa
Titanic walikutwa baadaye katika vilindi vya maji ya Atlantic wakiwa
wamekumbatiana.
Meli ya fahari sana , “The Unsinkable” R.M.S TITANIC ya White Star Line.
Watu
1,500 waume, wake na watoto walikufa katika ajali ya meli hiyo
inayosimuliwa sana katika hadithi za dini za mapenzi na filamu nyingi
kama , “The sinking of unsinkable” kwamba vilivyoshindikana kuzama
hatimaye vilizama. Hiyo ilikuwa Aprili mwaka 1912.
Sababu za kuzama kwa Titanic zinatajwa kama ni kuparamia miamba ya barafu(icebergs) usiku katika hiyo bahari ya Atlantic .
Hizo
‘icebergs’ zimeanza kuyeyushwa na ongezeko la joto duniani kunakoletwa
na viwanda vya Marekani na wenzake, na yumkini maji yatajaa sana
Atlantic na kuanza kugharikisha nchi kavu.
Filamu ya mwisho katika DVD hiyo ni ‘TWISTER’ inayoonesha tufani ama
kimbunga kikali huko Kanda ya Ziwa wanaita, ‘Omusoke’ kikipepeusha kila
kitu nchi kavu, huku wanafunzi wa Chuo Kikuu wakihangaika kufanya
utafiti ili kubaini nguvu yake.
Kwa hakika, ukitazama filamu hizo tano katika hiyo DVD(5Blockbuster
Movies) utabaini mwisho wa historia ya mwanadamu katika sayari hii.
Sababu
za maangamizi ni kiburi chake cha kuharibu mazingira yake au h ii
nyumba yake, dunia, kama nilivyosema mwanzoni mwa makala hii.
DVD hiyo imetwaliwa katika Adventure Movies Collection inayoonesha
‘emisoke’ na vimbunga, matetemeko na majanga mengine kama mafuriko.
Katika “The Day After Tomorrow; where will you Be?
Tunaona
matetemeko ya ardhi, vimbunga, chamchela, tufani, mafuriko, emisoke n.k
inavyoisogeza dunia katika zama za kufunikwa na barafu(ICE AGE),
kwa sababu ongezeko la joto duniani limekausha miti, mito, nyasi,
maziwa kisha likayeyusha barafu nyingi huko baharini, maji yakaondoka
baharini na kugharikisha nchi kavu, kwa hiyo maji hayo yakaanza kuganda
na kuwa barafu-ice age!!
Labda, maprofesa kama huyo Profesa Adrian Hall(Ouaid) na ma-'pale
climatologist' (wanasayansi wasomao mabadiliko ya tabia ya nchi)
watafanikiwa kuiokoa dunia katika maangamizi hiyo siku baada ya kesho.
Tungoje tuone
www.congemrambatoday.blogspot.com
0713-324 074
No comments:
Post a Comment