·
Al-Shabaab!
Al-Qaeda?
Tumechoka kuhesabu maiti
Na Conges Mramba
MATUKIO ya Ugaidi yaliyotokea jijini
London ,Uingereza, na kuua zaidi ya watu 50 mwaka 2005, yanaonyesha kuwa Tony
Blair na George Bush, wakati huo walikuwa wameshindwa kudhibiti ugaidi kwa
matumizi ya nguvu(Aggressive power); badala yake kilichotakiwa sasa ,ni njia za
kidiplomasia.
Diplomasia haikutumika wakati
huo,wala haikutumika wakati waSeptember 11 huko Marekani.
Dunia,ikiwemo Afrika,hususan Bara la
Afrika tenaMashariki huku,tumeumia maradufu kufuatia kipigo cha magaidi!
Tangu matukio ya Septemba 11,2001
yametokea matukio makubwa mengi sana ya ugaidi duniani; na nchi za Iraq
na Afghanistan ziliposhambuliwa na Majeshi
ya Uingereza na Marekani na kisha kupinduliwa, hakuna amani iliyopatikana.
Ulimwengu ulitegemea kwamba, baada
ya serikali za Wataleban na Saddam Hussein kupinduliwa Afghanstan na Iraq ,
sasa ulimwengu ungekuwa mahali salama, lakini badala yake sasa ni kiama cha
mabomu ulimwengu mzima.
Siyo ulimwengu ulioendelea kiulinzi,
na wala siyo nchi masikini kama hizi zetu, sote twagugumia machungu ya mabomu
mtindo mmoja!
Agosti 7,1998 mabomu yalipolipuliwa
katika ubalozi wa Marekani Nairobi na Dar es salaam, na kuua watu 224,ilisemwa
kuwa ni kwa sababu ya umasikini wetu, rushwa na miundo mbinu dhaifu ya ulinzi
dhidi ya magaidi.
Mwaka 2002,Machi 21, bomu
lililotegwa garini liliua watu tisa katika ubalozi wa Marekani mjini Lima ,
Peru .Ikasemwa hivyo, kwamba ni nchi dhaifu.
Oktoba 12,mwaka huo wa 2002, mabomu
yalilipuka katika klabu ya usiku mjini Bali , na kuua watu 202.
Wakati wa milipuko ya Septemba 11,
wakauawa zaidi ya watu 3,000 .hatua zilianza kuchukuliwa dhidi ya ugaidi.
Maana, ilionekana sasa magaidi hawakuwa wakitania.
Huu ni wakati WTC ilipogeuka Ground
Zero,na kifusi chake ni mnara wa kumbukumbu za magaidi,kifusi kimejaa ekari
moja!
Walishakamatwa magaidi kama akina
Riduan Isamadun, au Hambali, waliohisiwa kushiriki kiama hicho cha Septemba 11
. Alikamatwa pia Khalid Sheikh
Mohammed na wengine wengi.
Magaidi wengi walishakamatwa Iraq na
Afghanistan na kupelekwa Guantanamo Bay , lakini uovu unaendelea
tu.Ilichokipata Marekani, ni lawama za kukiuka haki za Binadamu.
Licha ya Osama Bin Laden, Mullah
Mohammed Omar na Abu Musab Al Zarqawi kusakwa sana , bado ugaidi ni kitisho
kikubwa kwa maendeleo ya watu Duniani.
Obama ameuawa na Carlos kafungwa
maisha,lakini ugaidi ungalipo.
Licha ya Tawala zilizodaiwa
kuwafadhili hawa majaili kupinduliwa, bado mabomu yanalipuka mahali popote
magaidi wanapoona panafaa yalipuke.
Agosti 19,2003 bomu lilipolipuka
katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa, mjini Baghdad , na kuua watu 22,
akiwemo mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, De Mello, ulimwengu
ulipata kitisho kikubwa, kwamba ulimwengu mzima uko hatarini.
Hata Umoja wa Mataifa?
Hata hivyo, mabomu ya 2005 ya London
, yaliyoua zaidi ya watu 50, na kuharibu miundombinu ya reli katika jiji hilo
maarufu sana duniani, ni hatari zaidi!!
Msiseme Nairobi,Dar au Kampala!
Mbona New York,Washington na London ni miji iliyolipuliwa?
Tatizo watu hawana kumbukumbu,wamekalia siasa
za kuchoma magogo na matairi barabarani!
London, ni jiji lenye ulinzi wa hali
ya juu.Taasisi za ulinzi, upelelezi au ujasusi zilizopo London ni maarufu mno
duniani, na huogopwa ulimwengu mzima.
Lakini jinsi mtandao katili wa
Al-Qaeda ulivyojipenyeza na kupiga mabomu njia za reli za chini kwa chini(tube)
na mabasi, ni kitisho zaidi; na mashambulizi haya yanatosha kutufanya tuamini
kuwa mkakati wa Bush na Blair,Cameron na Obama kupambana na ugaidi kwa kutumia
nguvu(Aggressive Power) umepitwa na wakati.
Dunia ikae mezani kutazama
magaidi(ama wawe wanaharakati,walipa visasi n.k) wanatakaje ili kutuliza
mizuka?
.Magaidi wamesakwa sana, wameuawa
sana, lakini wamaomgezeka na kuua watu wengi mahali popote bila kuogopa umahiri
wa ulinzi, au utajiri!Marekani, Uingereza, Kenya na Tanzania zote zimepigwa na
Al-Qaeda!!
Kama majahili hawa wameweza kufanya
unyama mkubwa London , New York na Washington, ni wapi wataogopa?
Walipopiga Nairobi, Dar es salaam ,
Bali na ofisi za Umoja wa Mataifa, Baghdad , ilionekana ni udhaifu wa ulinzi.
Ilipopigwa miji ya Washington na New
York (Septemba 11) ilisemwa kuwa watakomeshwa.
Tumeona Osama akisakwa, utawala wa
Taleban na Saddam ukiangushwa, na kumfanya Saddam kuwa mateka na mfungwa katika
mji wake Mkuu aliotumia kuitawala Iraq , Lakini mabomu yanaendelea.
Saddam,Osama,Gaddafi wameuliwa
lakini mabomu na risasi vimerindima duniani,sasa West Gate,NAIROBI!!
Irak,Libya,Misri,SYRIA nk hamkani si
shwari tena.
Mtazamo wangu ni kuwa iko haja ya
Umoja wa Mataifa kujua kwamba Blair na Bush siyo majemadari tena wa vita dhidi
ya ugaidi duniani; wameshindwa vibaya; kwa kuwa miji yao mikuu imepigwa na
maelfu ya watu kuuawa.Iko siku nao watapigwa na kuuawa!
Hawa Cameron,Obama,Bush na Blair, sasa hawana jipya
la kuuhadaa ulimwengu kwamba ugaidi utatokomezwa.
Vita dhidi ya ugaidi, War Against
Terrorism, ni danganya toto!
Ni wajibu wa Umoja wa Mataifa kukaa na
kutafuta mbinu sahihi za kuondoa kitisho hiki, badala ya kuwategemea hawa akina
Bush, Obama,Hollande na Blair, walioshindwa vibaya na kwa aibu.
Hivi ulimwengu ungekuwaje mabomu ya London yangeelekezwa Gleneagles, walikokuwa
wakifanya mkutano wakuu wan chi tajiri zenye viwanda, G-8?
Bush, aliyeongoza vita dhidi ya
Afghanistan na Iraq , alikuwepo, na wengine wengi walikuwepo Scotland , mabomu
yalipolipuka.
Nataka kusema kuwa, kufuatia mkutano
huo mkubwa, na ulioandamwa na waandamanaji, kulikuwa na ulinzi mkali eneo zima
la Ufalme wa Uingereza, Lakini mabomu yalilipuka na kuua watu 52.
Hii ni kuonyesha kuwa iko siku
magaidi watapiga ikulu zote duniani, na kuleta msiba mkubwa.
Kwanini isitafutwe njia nyingine ya
kupambana na ugaidi, badala ya kutumia ubabe wa akina Bush na Blair?
Obama,Cameron,Hollande?
Miongo michache iliyopita, Uingereza
ilikuwa katika kitisho cha mabomu ya vikundi kama Irish Republican Army(IRA),
ambao sasa hawafanyi tena hujuma, kwa sababu Ireland inao uhuru na Haki
zilizokuwa zikitafutwa.
Serikali ya Uingereza ilitambua
madai ya magaidi hao wa IRA, na amani ikawepo.
Kwa mantiki hii magaidi ni binadamu
wanaofanya vitendo vya kinyama, ili kupata haki zao.
Ugaidi siyo ujambazi unaoandamana na
tamaa tu
. Bali , ugaidi ni harakati za
kutafuta maslahi Fulani.Wakati Fulani wanaharakati kama Martin Luther King,
Kanali John Garang, Museveni, Marehemu Samora Machel na wengine, walionekana
kama magaidi, lakini leo tuna waona mashujaa wa watu wao.
Hii ni kusema kuwa hawa magaidi
wanayomadai yao , ambayo Umoja wa Mataifa lazima uyatazame, na kuyatafutia
ufumbuzi.
Kama Kanali Gaddafi, wakati Fulani
ikulu yake ilipigwa mabomu na Marekani, hadi mwanaye akauawa, na leo
inasemekana nchi yake imekoma kuunga mkono ugaidi, hata Osama angeweza
kubadilika, kupitia meza ya mazungumzo!
Gaddafi baadaye aliuliwa kwa sababu
eti za kuwaita waasi mende,panya!
Ulimwengu unataka amani, hivyo
zitafutwe njia elfu kukomesha ugaidi, kwani Bush na Blair Obama na Cameron
wameshindwa sana ; hata miji yao yote mikuu imepigwa hadi maelfu kuuawa
.Magaidi hawana nchi, hawana mipaka,
hivyo wamepata ushindi wa kishindo, yapaswa wakabiliwe kidiplomasia, ili
kuondoa kitisho.
Tumecoka kusesabu maiti na ndoo za
damu inayomwagika!
Hivi leo mtu aweza kusema Bush na
Blair,Obama,Cameron na Hollande wataweza kuifanya dunia mahali pa salama?
La hasha… wameshindwa tangu Iraq , Afghanistan
, Afrika, Asia na hata jirani na Ikulu zao.
Shime, Umoja wa Mataifa utafute njia
mbadala ya kupambana na ugaidi; la sivyo tutateketea kwa mabomu ya majahili
hawa
0713 324 074.
J
|
Wednesday, September 25, 2013
TUNAHESABU MAITI ZA MAGAIDI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment