Monday, September 23, 2013

MAGAIDI WA BLACK SEPTEMBER

POLISI WA UJERUMANI walifika katika kijiji cha Olimpiki saa 11 Alfajiri.
Wale magaidi wa Kiarabu-Black September-walipoona polisi wamewasili katika mabweni ya Waisraeli, mahali walipowashikilia mateka wao, wakamtumia Kamanda wa Kikosi cha Polisi ujumbe kwa Kiingereza.
“Kuwaachilia huru wafungwa 200  Wapelestina waliokuwa wakishikiliwa katika jela la Israeli! Kama mamlaka  haitatekeleza madai haya mara moja, katika muda wa saa 3 Asubuhi, mateka(Wanariasha wa Israeli watauawa!” Ujumbe ule ulisema.
Ujumbe ule ukafafanua kuwa kila baada ya nusu saa wangekuwa wakichinjwa wawili-wawili!
Hata hivyo, muda wa nusu saa uliowkwa na hao magaidi kuwa wa mwisho(dead line)ili kutekeleza madai yao ulisogezwa mbele.
Baadaye, wateka nyara wa Kipalestina wakaongeza madai mengine kwamba,ilikuwa lazima wakubaliwe wao na mateka wao(Waisraeli) waondoke kwenda katika nchi yoyote ya Kiarabu, ambayo wangeichagua wao.
Elewa mateka wa Kiisraeli walikuwa ndani ya bweni, wakiwa wamefungwa mikono na miguu tena wakiwa wamefungiwa kitandani, wasiweze kufanya chochote, tena chini ya ulinzi wa SMG na AK-47.
Polisi wangejitia hata kuvunja mlango wa bweni lile(ulifungwa) mateka wale wangeweza kulipuliwa hata na maguruneti, pengine wangelipuliwa kwa risasi za rashasha,maiti zao zikakutwa zimetobolewa mithili ya chandarua1
 Umbali wa zaidi kidogo ya mita 220 kutoka jingo walimokuwa mateka wale wa Israeli,Mkuu wa Polisi wa mjini Munich, Manfred Schreiber, aliwaita Makomandoo 600,wakiwa na magari ya deraya.
Walitaka kuzingira bweni lile,na walikuwa na ambulance tayari kuchukua zile maiti za Yule Muisraeli aliyepigwa risasi, Moshe WEINBERG.
Schreiber, alikwenda na makomandoo wake kulihusuru lile jengo walimokuwa wale mateka wakiwa wameshikiliwa chini ya ulinzi mkali wa wateka nyara wa Kipalestina-wee uwasikie tu.
Alikutana na wale wanaume wa kazi-Black September- wakiwa wamevalia kofia nyeupe za tennis huku nyusoni wakiwa wametilia miwani myeusi ya jua, SUN GLASSSES.
Kiongozi wa Magaidi hao wa Kipalestina alikuwa mtu mwenye msimamo mkali. Schreiber aalipomtazama usoni, akaona alikuwa hatanii.Alikusudia kumtia chini ya ulinzi, akagwaya.
“Do you want to take me?”
Kiongozi wa magaidi wa Black September akamsaili Mkuu huyo wa polisi wa Mjini Munich.
Akafanya kama ananyoosha mkono wake ili labda utiwe pingu,kumbe ulikuwa na guruneti mkononi!
Kuanzia hapo simu zikaanza kupigwa mfululizo baina ya Munich, Bonn na Jerusalem.
Waziri Mkuu wa Israeli, Bibi Golda Meir na Mawaziri wake wakakaa kufikiri namna ya kufanya ili kuwaokoa mateka hao huko Munich.Mwisho, walikasirika na kuwaambia Wajerumani kwamba waliwajibika kwa uzembe wao,kwa hiyo iliwapasa kuokoa maisha ya wanamichezo hao ambao wamefanyiwa unyama katika ardhi yao!
Wakati haya yakitokea, kama umbali wa mita 400 tu kutoka hapo,michezo ya Olimpiki ilikuwa ikiendelea kama kawaida.
Wakati huo,Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani, Dietrich Gensncher, (nilimsikia katika taarifa za habari nikiwa mtoto, nikisoma darasa la pili)alianza mazungumzo ya kutafuta mwafaka(negotiations) kati ya wateka nyara wa Kipalestina na serikali ya Israeli na Ujerumani Magharibi zama hizo-Siku hizi Ujerumani ni moja baada ya Ukuta wa Berlin kuvunjwa mwaka 1991.
Gensncher, aliahidi magaidi wa Kipalestina kupewa KITITA CHA NOTI, kama wangekubali kuwaachia mateka wale.
Walizungumza ana kwa ana na Waziri huyo huku akiwahadaa, “Serikali ya Israeli bado inajadiliana ni mateka wangapi wa Palestina waachiliwe huru; bado kutoa jawabu” Waziri Gensncher alisema.
Black September, wakasogeza mbele tena ule muda walioweka-deadline-ya kuwaulia mbali wale mateka, kutoka Adhuhuri hadi saa 7 za mchana. Wakasogeza tena mbele deadline hadi saa tisa alasiri, hadi saa 11 jioni,ili serikali ya Israeli ikubali mateka wa Kipalestina Waachiliwe huru huko Jerusalem.
Kama msomaji unakumbuka kisa cha Iddi Amin Dada kilichosimuliwa katika gazeti hili, utakumbuka hata pale Entebbe, wakati magaidi wa Kipalestina wanawashikilia abiria wa Air France Air Bus, walitoa madai haya haya ya kutaka Israeli kuwaachia huru wanamgambo wa Kipaletina walioshikiliwa labda Tel Aviv au pengine popote katika ardhi ya Mayahudi.
Walisogeza mbele muda hadi mara sita.
Waziri Gensncher akaomba kwanza akawaone kwa maho hao mateka.Wakamchukua hadi bwenini,akawaona tisa wamefungwa watatu watatu mikono na miguu kwenye kitanda.
“Nimewaambia”,Gensncher akasema, “Kama wakikubali,basi ninyi muondoke na hawa mateka hadi nje ya Ujerumani”, wakati huo zilikuwa Ujerumani mbili,Berlin na Bonn.
Serikali ya Ujerumani ikifikiri cha kufanya ili kuwanusuru Waisraeli mikononi mwa mauti. Kama ingekurupuka,wale wateka nyara wangewaulia mbali hao mateka,halafu lawama zingekuwa pale pale,kwamba kwa uzembe wao raia wa mataifa ya kigeni waliokwenda kushiriki mashindano ya Olimpiki ya Munich, mwaka 1972 walitekwa nyara na kuuawa kinyama.
Kama ingekuwa hapa Tanzania, ungesikia kila mwanasiasa akiilaumu serikali kwa uzembe, pengine hata hapo mitaani kwenu,mngesema polisi wazembe lazima hata walipewa rushwa!
Basi,serikali ya Ujerumani ikawaleta polisi wenye shabaha, sharp shooters, wakiwa wavevalia fulana za kuzuia risasi kupenya-Bullet Proof juu ya jezi za kimichezo walizovalia.
Kamera kali sana zenye zoom zikawamulika hao makomandoo, hadi kule mateka wa Israeli walikokuwa wanashikiliwa.
Walichelea kuwafyatulia risasi wale magaidi wasije kufanya kosa moja halafu Black September wakawageukia wale adui zao na kuwalipua. Hapa kulikuwa na hesebu kali za nyoka na panya wanapokutana katika tundu dogo.
TV na Radio zikaanza kutangaza mkasa ule wa magaidi wa Kiarabu kuwateka nyara wanariadha wa Israeli hapo Munich.
Waisraeli 100 vijana wadogo wakaimba wimbo wao wa Taifa-HATIKVAH-kuwaambia Waisraeli waliotekwa nyara hapo Munich,
“Mjue hapo mlipo kwamba hamko peke yenu,tupo pamoja nanyi!”
Helkopta za polisi zikaanza kupaa angani katika vichwa vya wanamichezo wa Olimpiki.
                 
Naam, hadi wakati huo serikali ya Israeli nay a Ujerumani zilikuwa kiti moto.
Kansela Willy Brandt, BAADA YA KIKAO NA Baraza lake la Mawaziri mjini Bonn,alienda Munich ili kutafuta suluhisho la magaidi wale katika nchi yake.
Naandika kisa hiki kilichotokea mwaka 1972 leo wakati kunapokuwa na kisa kama hiki huko Jamhuri ya Kenya,baada ya magaidi labda al-Shabaab kuvamia Westgate.
Mawazo aliyo nayo Rais Uhuru Kenyatta,ni kama alivyokuwa Kansela Willy Brandt, wakati Waisraeli walipokuwa wametekwa nyara na magaidi wa Kipalestina katika bweni huko katika kijiji cha Olimpiki mjini Munich.
Nimekuambia,wakati huo Waziri Mkuu wa Israeli alikuwa mwanamama,Golda Meir, ambaye sasa alilihutubia Bunge kusema,  “Ilikuwa vema timu yetu kususia michezo ya Olimpiki iliyokuwa ikiendelea hapo Munich”.
Rais Richard Milhouse Nixon(alijiuzulu mwaka uliofuata kwa kashfa ile ya Watergate) alituma pole nyingi sana mjini Jerusalem; akaamuru Balozi za Marekani zote katika nchi za Kiarabu kushinikiza mateka wale kuachiwa huru.
Msomaji, nataka nikwambie kwamba,Rais wa Marekani ni mithili ya samba hapa duniani.
Anaponguruma ili kushinikiza jambo la muhali,dunia hukimbizana mithili ya vi-swala…Marais wa Kiarabu tumbo likawa joto!
Barozi za Kiarabu mjini Bonn-Arab League- waliwabembeleza wale wapalestina,pasipo mafanikio.
Kansela Willy Brandt wa Ujerumani,akampigia simu Rais Anwar al Sadat wa Misri, akamuunganisha na Waziri Mkuu,Aziz Sidky, aliyesema, “Hatutaki kuhusishwa na jambo hilo”.
Brandt, aliamuru wateka nyara kuondoka na mateka wao Waisraeli,wasije wakawapiga risasi bure ikifika asubuhi. Kumbuka sasa ilikuwa usiku hiyo Septemba 5,mwaka huo 1972.
Black September walisema watawaua hao mateka wa Israeli popote,kama serikali yao itajitia kichwa ngumu kutowaachilia huru mateka wa Kiarabu huko mjini Jerusalem.
Kwa msomaji anayesoma kisa hiki hapa, atapata picha kwamba,mashambulio ya kigaidi hata ya West gate, yanaweza kuandamana na madai kama haya ama wakati mwingine kikadaiwa kikombozi cha mamilioni ya fedha!
Ugaidi siyo ujambazi kama huu wa kawaida,lazima watu kuelewa.Ugaidi una sura ya kulipa visasi juu ya vuguvugu Fulani la siasa za kiulimwengu.
Kufuatia hali hiyo,Kansela wa Ujerumani ,Willy Brandt alitokwa kijacho chembamba!
“Haiwezekani kuona jambo kama hilo likitokea katika nchi yetu”,Willy Brandt alijiambia kimoyomoyo, “Tutawajibika kwa ajili ya maisha ya mateka hao Waisraeli”, alisema
Wateka nyara wakapigasimu toka humo ndani ya lile bweni kwenda mataifa ya Kiarabu.Walipiga Tunisia,hapakuwa na jibu la kuwasaidia, hata simu yenyewe haikupokelewa.
Si unajua Rais wa Marekani,Nixon alishapiga simu huko sasa nchi za Kiarabu kuonekana ziliwasaidia hao magaidi ingekuwa issue ya kupigwa hata na Drones!
Kumbuka, Marekani imetishia Balozi zote za nchi za Kiarabu kutokuwapokea magaidi hao wala kuwapa msaada.
Hata hivyo,sasa mashindano ya Olimpiki yangekuwa hatarini.Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani Magharibi, Hans Dietrich Gensncher, alimwambia Willy Brandt,
“Tusiwaache hapa Munich,isije kuwa noma bure,tuwaruhusu waondoke!” alisema.
Kufuatia hali hiyo, magaidi wale na mateka wao walichukuliwa hadi uwanja wa ndege wa jirani na Munich ambako wangekwea Lufthansa 727 Jet,hadi wanakotaka? Subiri uone kasheshe kama ya al-Shabbaab, West gate.
Baada ya saa 4 usiku(saa 18 baada ya kuwateka nyara Waisraeli) magaidi wanane wa Kipalestina wakawaongoza mateka wao mikono ikiwa imefungwa nyuma mgongoni, wakatoka nje ya bweni lile,wakatembea chini ya ulinzi,wakaingia ndani ya basi la rangi ya kijivu.
Walipelekwa hadi katika helkopta ambayo wangeitumia kuondoka hapo Munich,
‘Chopper ’mbili ziliwachukua hao magaidi  tisa na mateka wao wanane,Walipaa angani dakika kama 13 hivi hadi Furstenfeldbruck,kituo cha jeshi la Anga ambacho kilikuwa umbali wa kama maili 16 nje ya Munich.
Chopper ya tatu ilishapaa mapema kabla ya hizo mbili kutua;nayo iliwachukua maofisa wa Kijerumani na mashushushu wa Kiisraeli(Mosad), na kwa vyovyote huko kungekuwa na balaa kubwa!
Kumbe, uwanja huo wa ndege ulikwishazingirwa na askari 500 wenye silaha mkononi.
Walengashabaha(sharp shooters) walijiandaa kupokea amri ya kuwafagilia mbali wale magaidi wa Kiarabu.Walitarajia magaidi wanane wauliwe ili mateka 9 wa Istraeli waokolewe.Picha ni kama hiyo ya Westgate kati ya Al Shabbab na polisi wa Nairobi na washirikwa wa usalama.
Chopper ilipotua tu, wale magaidi walitegemea wawili kati yao wangeilinda ile 727,wawili wangechupa nje ya hiyo Boeing,nikisema 727 ni hiyo ndege iliyowaleta hapo.
Ingawa waliambiwa wasithubutu kuwageuza hata Wajerumani kuwa mateka,hao magaidi waliamuru hizo Chopper kuondoka hara sana hapo uwanjani.
Kumbe,Makomandoo wa Ujerumani watatu walikuwa kwenye mnara wa kuongozea ndege,ni kama yadi 38 hivi kutoka kwenye hizo chopper,wawili walikuwa ardhini.
Haikuchukua muda,vita vikali sana vikaanza.Waarabu wakawafyatulia risasi hao Wajerumani.
Mkuu wao tayari akarukia chini ya mvungu wa helkopta akaanza kumwaga risasi.Kwa saa nzima wakabadilishana risasi,vita vikapamba moto.
Baadaye,magaidi watano na kiongozi wao walilala mauti baada ya kupigwa risasi.Walikwishawaua wale mateka Waisraeli wote tisa,kwa sababu walikuwa bado wakiwa wamefungwa mikono nyuma mgongoni ndani ya zile chopper mbili wakati vita vinapamba moto.
Wale wanne waliungulia ndani ya chopper baada ya kulipuliwa na guruneti la wale magaidi wa Kipalestina,watano walipigwa kwa SMG NA AK -47 za magaidi.
Kufuatia vita hivi,polisi waliwatia mbaroni magaidi watatu;kati yao wawili wakiwa wamejeruhiwa vi-baya.
Itaendelea
0713 324 074
www.congesmrambatoday.blogspot.com

Tuesday, September 17, 2013

Wazungu wanahama dunia

  Rais Jakaya Kikwete aliongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano wa chakula mjini Rome , mji mkuu wa Italia mwaka 2009.
   Rome , jiji lililojengwa miaka 754 kabla ya Kristo, ndilo makao makuu ya Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa(FAO).
  Viongozi hawa wa dunia, sasa wanahangaika kumwokoa mwanadamu katika maangamizi, siku baada ya kesho.
  Pamoja na mambo mengine, ilisemwa katika mkutano huo kwamba, watu bilioni moja miongoni mwa bilioni 7 wanaoishi duniani siku hizi, wanakabiliwa na njaa kubwa.
 Usalama wa chakula unakosekana.
   Njaa, imeletwa na sababu nyingi.
 Kubwa ni kwamba, ukame ama kiangazi kikali huchukua muda mrefu siku hizi, hadi mazao mashambani hunyauka, mifugo hufa na uchumi huwa mbaya kwa kila mkazi wa dunia hii.
  Hii ni kusema, chakula hakitakuwepo kabisa siku baada ya kesho, kama uharibifu mkubwa wa mazingira unaofanywa sasa hautadhibitiwa.
 Nataka kujadili madhara ya uchafuzi wa hewa(Air Pollution) katika anga la dunia hii tuishiyo, unaofanywa na mataifa makubwa yenye viwanda. Marekani ni miongoni mwa mataifa hayo.
 Kila mwaka, Marekani na mataifa mengine takriban 40 yenye viwanda vingi, hurusha angani moshi, vumbi, joto, mvuke na kemikali za sumu, nyingi. Hizi sumu hufanya hali ya hewa kuwa isiyo na manufaa kwa maisha ya mwanadamu.
  Mpaka hapa, nimeandika kwamba, kuna sababu kubwa mbili za kutokea kwa majanga ya asili duniani:
Ongezeko kubwa la watu ambao sasa wamefika bilioni 7 na uchafuzi wa hewa angani, majini na nchi kavu. Tunataka kuona nyuma ya pazia lililofunika siku baada ya kesho.
   Kuongezeka kwa ukungu hewani, angani, wakati mataifa yanapodhamiria kuigeuza dunia na mataifa kuwa yenye Nguvu ya Nyuklia(Nuclear Power), ili kupata nishati ama nguvu   ya umeme-viwanda vya Nyuklia vinatoa mvuke mwingi angani unaoleta ukungu.
    Magorofa makubwa na marefu sana katika majiji makubwa ya dunia, yanaelea siku hizi katika anga lililogubikwa ukungu mzito.
 New York, Ottawa, Canada, Tokyo nchini Japan na  majiji mengine mengi duniani, hufunikwa na ‘blanketi’ zito la ukungu, moshi, masizi ya viwanda, moshi wa magari, migodi, magari moshi, ndege kama Concord na mitambo mingine.
   Miezi michache iliyopita, nilinunua mkanda wa DVD wenye filamu tano(5Blockbuster Movies) iliyokuwa na sinema hizo tano kali sana zenye kuonesha matokeo ya kuharibu mazingira ya anga la dunia.
  ‘THE DAY AFTER TOMORROW’ ni filamu inayoonesha dunia inavyokwenda kuwa ‘siku baada ya kesho’ ikiwa viwanda vya mabwanyenye wa Ulaya na Marekani, na Mahariki ya Mbali, havitatakoma kumwaga sumu zake   katika anga la dunia na kusababisha Ongezeko la Joto duniani(Global Warming) linalosababisha haya majanga ninayosema.
   Naam, majanga yanayotishia uhai wa mwanadamu kama vimbunga, chamchela, tufani, matetemeko ya ardhi, mawimbi makali yanayozoa maji baharini na kuigharikisha nchi kavu, kama ile tufani ya Katrina huko Marekani.
   Katika filamu hiyo kali sana , ‘The Day After Tomorrow’ kumeonyeshwa mafuriko makubwa yakiigharikisha nchi kavu, majengo marefu ya miji ya Marekani, shughuli za watu zikakoma, magari ya fahari yakasombwa na mafuriko, magereza yakabomoka, wafungwa wakatoka na mafaili ya kesi za majambazi na wahalifu wengine yakasombwa na mafuriko- katika kiama hiki hakuna serikali, hakuna jaji, hakimu, wala sheria na ustaarabu, ni machafuko.
   Kwa sababu mwandishi wa safu hii siyo mwanasayansi, amini usiamini, nimeona katika filamu hiyo kwamba mwisho wa majanga hayo kama matetemeko ya ardhi kama tsunami na vimbunga vikali kama Mitch, ni dunia kuanza kufunikwa na maji kisha barafu tupu.
   Kila mtu atafute mwakozi wake, kwa sababu majanga ya kiasili yaletwayo na Ongezeko la Joto Duniani linalosababisha mvua kubwa kama El-Nino, tumelishuhudia Same, Kilimanjaro, ardhi anapoanza kuwafunika watu.
  Kufuatia Ongezeko la Joto Duniani, siku hizi mabonge ya barafu katika Ncha za Kaskazini na Kusini(North Pole&South P ole) yameanza kuyeyuka na kujaza maji baharini kwa kimo cha futi 100, 200 kwenda 250.
 Maji haya yanapovuka mipaka ya bahari na kuingia nchi kavu, kunako starehe na shughuli za kiuchumi za binadamu, ndiyo dira halisi ya siku baada ya kesho.
   Na hii ndiyo ‘Pata-Potea’ ya maisha ama uhai duniani.
 Miaka hii ya 2000 imetabiriwa(na wanasayansi) kwamba kutakuwa na tani milioni 404 za taka sumu hewani ambazo huzidisha joto duniani.
 Kuna tani milioni 76 za sulphur dioxide, tani milioni 207 za carbon monoxide, tani milioni 53 za hydrocarbons, tani milioni 30 za nitrogen oxides, na tani milioni 28 za vipande vya vumbi, moshi hata wa wavuta sigara na bangi ambao sasa ni wengi sana duniani!Kuna uchomaji mwingi wa misitu siku hizi.
  Kuna vumbi na masizi pote angani. Inasemwa kwamba, binadamu ndiye mnyama wa kwanza kwa uharibifu wa mazingira, yawe ya mito , maziwa mbahari, nchi kavu n.k Binadamu hujiharibia maisha yake mwenyewe ili asiweze kunusurika hiyo siku baada ya kesho.
  Matokeo yake, ni majanga niliyotaja; ukame unaoleta kitisho cha njaa hadi wakuu wa dunia wamekutana mjini Rome , Italia, ili kujadili namna ya kuondokana na njaa hiyo kubwa sana inayokuja.
  Wakuu wa dunia walipokutana mjini Rome na kujadili kitisho cha njaa ni kitu kikubwa sana kuliko unavyofikiria.
Hata Papa Benedict XVI alihudhuria mkutano huo.Papa huyu alishastaafu siku hizi.Lakini alisema kuhusu kinachoujia ulimwengu.
  Bila shaka, aliwakumbusha wakuu hao wa dunia, kwamba njaa hiyo kubwa ilitabiriwa na Yesu katika kitabu cha Injili ya Mathayo, sura ya 24. Njaa ni dalili za ‘Mwisho wa Dunia’ ama ‘The D-Day ‘ unaofungamana na kuja kwa Yesu mara ya pili.
 Bila shaka, siku ya kiama hii itakuja kabla ya dunia kuanza kuganda kwa barafu itakayofunika miji yote kama inavyooneshwa katika hiyo filamu ya ‘The Day After Tomorrow’.
 Kufuatia Ongezeko la Joto na milima ya mabonge ya barafu kuanza kuyeyuka huko North Pole na South Pole, maji yatagharikisha visiwa, mengine yatasombwa na mawimbi makali na makubwa sana yaliyoletwa na vimbunga na tufani kama Katrina, kwenda kugharikisha makazi ya watu mijini na mashambani.
 Mambo haya yanatabiriwa katika hiyo Filamu ya ‘The Day After Tomorrow’.
 Labda ni gharika nyingine kama ile ya Nuhu, iliyotokea miaka 2000 Kabla ya Kristo. Wewe msomaji utajificha wapi, siku hiyo baada ya kesho?
  Pia, katika DVD hiyo yenye filamu tano ‘kiboko’(5Blockbuster Movies), kuna moja inaitwa, Independent Day na nyingine inaitwa, ‘The Perfect Storm’.
 Hii  Perfect Storm inaonesha bahari ya Atlantic ikichemka kwa mawimbi makali hadi futi 100 juu ya uso wa bahari, kufuatia kimbunga kinachoitwa Grace.
  Ilikuwa Oktoba mwaka 1991.
  Sijaelewa ni kwa nini vimbunga vingi vinabatizwa majina ya akina mama!
Mimi siyo mwanaharakati wa haki za wanawake; wao wapo wanaweza kujitetea kwanini majanga ya asili yabatizwe kwa wingi majina yao .
  Naam, nazungumzia siku baada ya kesho(The Day After Tomorrow) ili kuwaonyesha wasomaji madhara ya uharibifu wa mazingira ya sayari tunayoishi.
Matajiri wameanza kutafiti kama kuna maisha katika sayari ya Mars na mwezini; labda wana mpango wa kuhamia huko, hii sayari inapoangamizwa kwa sumu za hewani na ukataji wa miti inayopunguza sumu hizo.
   Pia kuna filamu kali sana iitwayo, TITANIC. Ni tukio la kihistoria linalosimuliwa na akina Leonardo DiCaprio(huyu alicheza pia filamu ya BLOOD DIAMOND) na Kate Winslet, wanaofahamika kwa majina ya Jack na Rose.
  Walikuwa katika penzi changa la tashtiti, ambao baada ya kuzama kwa Titanic walikutwa baadaye katika vilindi vya maji ya Atlantic wakiwa wamekumbatiana.
Meli ya fahari sana , “The Unsinkable” R.M.S TITANIC ya White Star Line.
 Watu 1,500 waume, wake na watoto walikufa katika ajali ya meli hiyo inayosimuliwa sana katika hadithi za dini za mapenzi na filamu nyingi kama , “The sinking of unsinkable” kwamba vilivyoshindikana kuzama hatimaye  vilizama. Hiyo ilikuwa Aprili mwaka 1912.
   Sababu za kuzama kwa Titanic zinatajwa kama ni kuparamia miamba ya barafu(icebergs) usiku katika hiyo bahari ya Atlantic .
 Hizo ‘icebergs’ zimeanza kuyeyushwa na ongezeko la joto duniani kunakoletwa na viwanda vya Marekani na wenzake, na yumkini maji yatajaa sana Atlantic na kuanza kugharikisha nchi kavu.
  Filamu ya mwisho katika DVD hiyo ni ‘TWISTER’ inayoonesha tufani ama kimbunga kikali huko Kanda ya Ziwa wanaita, ‘Omusoke’ kikipepeusha kila kitu nchi kavu, huku wanafunzi wa Chuo Kikuu wakihangaika kufanya utafiti ili kubaini nguvu yake.
   Kwa hakika, ukitazama filamu hizo tano katika hiyo DVD(5Blockbuster Movies) utabaini mwisho wa historia ya mwanadamu katika sayari hii.
Sababu za maangamizi ni kiburi chake cha kuharibu mazingira yake au h ii nyumba yake, dunia, kama nilivyosema mwanzoni mwa makala hii.
  DVD hiyo imetwaliwa katika Adventure Movies Collection inayoonesha ‘emisoke’ na vimbunga, matetemeko na majanga mengine kama mafuriko.
Katika “The Day After Tomorrow; where will you    Be?
Tunaona matetemeko ya ardhi, vimbunga, chamchela, tufani, mafuriko, emisoke n.k inavyoisogeza dunia katika zama za kufunikwa na barafu(ICE AGE),
  kwa sababu ongezeko la joto duniani limekausha miti, mito, nyasi, maziwa kisha likayeyusha barafu nyingi huko baharini, maji yakaondoka baharini na kugharikisha nchi kavu, kwa hiyo maji hayo yakaanza kuganda na kuwa barafu-ice age!!
  Labda, maprofesa kama huyo Profesa Adrian Hall(Ouaid) na  ma-'pale climatologist' (wanasayansi wasomao mabadiliko ya tabia ya nchi) watafanikiwa kuiokoa dunia katika maangamizi hiyo siku baada ya kesho.
 Tungoje tuone
www.congemrambatoday.blogspot.com
      0713-324 074
 
wazungu wanajiandaa kuhamia mars

Wazungu wanapojiandaa kuhamia Sayari ya Mars, Mwanza,Bukoba na Musoma watahamia kuzimu!

UHARIBIFU MKUBWA wa Mzingira hapa Duniani, ni  moja ya kichocheo ama chanzo cha safari za wanasayansi katika Anga za Juu.
Tangu mwaka 1969 akina Neil Armstrong walipofanya safari katika mwezi, wanasayansi wa Mataifa makubwa wamesafiri kwenda anga za juu ili kutafuta nishati, na hata makazi huko.
Watu wenye fedha wanatafuta viwanja vya kuishi huko Mars, wengine wametafuta sehemu ya kuzika wafu wao huko!
Inakisiwa hii Dunia imeharibiwa sana kwa sumu,uharibifu wa maji na anga kiasi kwamba uhai katika dunia hii hautakuwepo miaka 40 tu ijayo!
Uharibifu wa mazingira hapa duniani, unapoongeza kitisho cha uhai katika sayari ya Dunia,matajiri wa Ulaya na Marekani, wanapanga kuitoroka Dunia, ili wakaishi katika anga za Juu,mfano katika sayari ya Mars ambako kuna kila dalili ya maji na uhai.
Viwanja vimepimwa huko, watu wenye fedha kutoka nchi mbalimbali zenye vita,migogoro,uchumi mbaya,misuko-suko yenye kutokana na uharibifu mkubwa wa kimazingira n.k wanapanga kuitoroka Dunia yenye njaa,vita na majanga ya kimazingira.
Zaidi ya watu 200,000 hapa Duniani wametuma maombi kutaka kuhamia Mars,kufuatia hofu ya majanga ya kimazingira,maradhi mabaya,njaa n.k
Hawa wanatoka takriban nchi 140 hapa Duniani wamo pia Marais wa Mataifa makubwa. Hawa wanaona wakitorokea sayari ya Mars wanaweza kuepuka kifo kinachoinyemelea sayari hii inayochafuliwa kwa mionzi ya sumu, uchafuzi wa anga,hewa, uchafuzi wa maji ya maziwa,mito na bahari n.k
Kanda ya Ziwa, haijafahamu kwamba, wakati Marais kama Barack Obama wanahaha kutafuta makazi katika Anga za Juu kama katika sayari ya Mars, huku ndiyo kwanza majumba kama mahoteli makubwa hujengwa ndani ya eneo la mita 60 za Ziwa Victoria,mito inayomwaga maji katika ziwa hili na kilimo kinafanywa mita chache toka ziwa na mito.
Imeelezwa kwamba miji ya Bunda,Mwanza, Musoma na Bukoba,kuna viwanda,mahoteli na wananchi wanajenga ndani ya eneo la mita 60 ambalo haliruhusu shughuli za binadamu kutoka vyanzo vya maji kama mito,maziwa,bahari n.k
Mahoteli yamejengwa ziwani na mengine yako mitoni, shughuli za kiuchumi zinaendeshwa kama kawaida kinyume cha sheria za Mazingira huku Kanda ya Ziwa.
Hivi karibuni, Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira(NEMC) limekusudia kubomoa sehemu ya Hoteli ya Royal Sunset Beach,iliyopo katika fukwe za Luchelele, Nyegezi jijini Mwanza,kufuatia ujenzi wa hoteli hiyo kukiuka sheria za kimazingira.
Royal Sunset Beach, inamilikiwa na Mkurugunzi wa Jiji la Dar es salaam,Wilson Mbonea Kabwe, imejengwa ndani ya mita 60 kutoka ndani ya maji ya Ziwa Victoria.
Kabla ya kuhamishiwa Dar es salaam,mmiliki wa Hoteli hiyo, Royal Sunset Beach, alikuwa Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza.
Kulingana na Mwanasheria wa Baraza la Taifa la Mazingira(NEMC),Manchare Suguta, kujenga ndani ya eneo la mita 60 kutoka vyanzo vya maji,ni kinyume cha sheria ya Usimamizi wa Mazingira,kifungu nambari 57.
Licha ya Mmiliki wa Hoteli hiyo kutozwa faini ya shilingi milioni 10, wadau wa Mazingira hapa Kanda ya Ziwa Victoria wanasema, Ziwa hilo ambalo ni chanzo kikuu cha uchumi, maji ya kunywa na chakula, huharibiwa kwa kiango cha kutisha.
Wakazi wa Miji ya Musoma,Bunda, Magu,Mwanza na Bukoba, wasio na mfumo wa kusafisha maji taka na taka ngumu zenyewe, wanamwaga taka zao katika Ziwa hili ama katika mito inayomwaga maji Ziwa hili.
Kulingana na Mradi wa Ulinzi wa Mazingira ya Ziwa Victoria, The Lake Victoria Environmental Management Project(LVEMP) sehemu ya Pili, wanasema watu na hata viwanda vya miji ya Mwanza,Bukoba,Musoma,Bunda,Magu n.k na wengine wa Maswa,Bariadi na Simiyu wanalima mazao katika ndani ya eneo la mita 60 kutoka maji ya mito na Ziwa hili.
Kilimo cha kando kando ya ziwa na Mito inayomwaga maji katika   ziwa Victoria,licha ya kusababisha mmomonyoko wa ardhi,husababisha utiririshwaji wa kemikali zinazotokana na mbolea na dawa za kuulia wadudu,na kusababisha hatari kwa maisha ya viumbe kama samaki, wanyama,mimea,ndege na hata binadamu wanaotegemea maji ya ziwa hilo kwa kunywa na kuoga.
LVEMP Phase II wanasema, viwanda vya kutengeneza mafuta (ya pamba) ya kula huko Bunda,mkoani Mara havikuwa na mfumo wa kuhifadhi taka kwa muda mrefu.
Viwanda hivyo,vimekuwa vikitiririsha kemikali na mabaki ya mafuta hayo ziwa Victoria ambalo liko kilomita chache kutoka Bunda, katika kijiji cha Guta.
Kulingana na wataalam wa Mazingira, kemikali za viwanda,majumbani na maduka zisipodhibitiwa,huweza kusombwa na maji ya mvua hadi katika vyanzo vya maji hata umbali wa kilomita 100.
Kutoka Bunda hadi Guta.ni umbali wa takriban kilomita 10 tu; na hali hiyo ya kutiririsha kemikali na mabaki ya mafuta ya pamba huko Bunda,huhatarisha maisha ya watu,wanyama na viumbe wanaotegemea Ziwa Victoria kwa maisha ya kila siku.
Kuna migodi inayotiririsha kemikali za hatari kama zebaki hadi katika Mito inayomwaga maji yake katika ziwa hili muhimu kwa uhai wa takriban watu milioni 30 katika Ukanda wa Mziwa Makuu.
Mifugo Mkoani Mara ilisharipotiwa kufa kwa kunywa maji ya kemikali za migodi,walkati   wananchi walishaathiriwa na kemikali hizo hadi kulazwa hospitalini na wengine kupoteza maisha.
Athari hizi za kimazingira ndizo hufanya sasa matajiri mataifa makubwa kuhaha kutaka kutorokea katika sayari nyingine kama Mars,ili kuepuka madhara ya kimazingira katika sayari ya Dunia.
Miji kama Mwanza, wakazi wake huendesha kilimo kandoni mwa Ziwa Victoria,hulima bustani kama mbogamboga na matunda ambayo huhitaji mbolea za viwandani na viuwatilifu vyenye kemikali za sumu.
Mji wa Musoma,umesemwa na LVEMP II kwamba baadhi ya wakazi wake hufanya kilimo katika Bonde la Kitaji lenye ardhi oevu,ama chepechepe.
Bonde hilo la Kitaji, zamani likitumika kama dampo la kutupia taka ngumu na Halmashauri ya MANISPAA ya Musoma.
Kemikali za mbolea za viwandani na sumu za kuulia wadudu pamoja na taka ngumu zilizokuwa zikimwagwa Kitaji,ni chanzo cha uharibifu mkubwa wa Mzingira katika Ziwa Victoria huko Mjini Musoma.
Kutokana na kemikali za sumu kutoka mashambani jirani na chanzo hiki cha maji, na kutokana na kumwaga taka ngumu,ujenzi holela ndani ya mita 60 ,ukataji holela wa miti kando ya mito kufuatia upanuzi wa mashamba, maji ya Ziwa Victoria yameharibiwa maradufu hadi samaki wamepungua na kusababisha njaa na ukosefu wa ajira mjini Musoma.
Samaki wametindika hadi bei yake imepanda maradufu.Samaki ni chanzo kikuu cha chakula aina ya Protini kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa Victoria, sasa kufuatia hali hiyo ya uchafuzi mkubwa wa mazingira,eneo la Kanda ya Ziwa linakabiliwa na hatari na majanga ya kiafya na umasikini wa kutisha.
Jijini Mwanza wakulima wa mboga na matunda hulima kando ya Ziwa na kutiririsha kemikali ndani ya maji ya ziwa.
Mamlaka ya Bandari(TPA) NAO HULALAMIKIWA kwa kutokuwa na mfumo wa maji taka ili kuzuia mafuta machafu yanayotoka melini na katika mitambo,kumwagikia ziwani.
Kuna waosha magari na wenye viwanda ambao wamekuwa wakitiririsha maji ya kemikali ziwani,na hata katika mashamba ya wananchi na kuwasababishia hasara kubwa. Maelfu ya ekari yanaharibiwa na kemikali zitokazo viwandani na migodini,na wakati mwingine mifugo wanaokula nyasi na kunywa maji yaliyoathiriwa na kemikali hufa.
Kanda ya Ziwa kuna viwanda vingi na watu wasiokuwa na Mfumo wa kusafisha maji(Sewage System) matokeo yake kemikali nyingi huwamwagwa ziwani na katika mito.
Lake Victoria Environmental Management Project(LVEMP Phase II) wanasema uchafuzi wa kimazingira unaofanywa kando ya mito na ziwa Victoria huhatarisha maisha ya mamilioni ya watu,mifugo,wanyamapori na mimea.
Matokea ya uharibifu huu ni hatari ya kiafya,umasikini uliokithiri kwa wananchi na vifo.
Baadhi ya mito inayochafuliwa sana sanjari na ziwa Victoria ni Mto Mara,Kagera,Grumeti,Mbalageti,Simiyu, na Mto Mori.
Baadhi ya migodi Kanda ya Ziwa humwaga kemikali kama Zebaki ambayo hutiririshwa hadi ziwani. Zebaki hutumiwa hata na wachimbaji wadogo wa madini kusafishia dhahabu migodini.
Zebaki inapofika ziwani hudhuru samaki na wanyama hadi walaji wa samaki wako hatarini kuugua saratani.
Upanuzi wa mashamba huko Simiyu na Bariadi umesemwa kwamba ni chanzo cha ukataji holela wa miti kandoni mwa mito, pia ni chanzo cha mmomonyoko mkubwa wa ardhi.
Wakulima wengi hulima hadi ndani ya eneo la mita 60 kutoka chanzo cha maji,kitu ambacho huharibu mazingira na ikolojia.
Kufuatia uharibifu wa mazingira katika mito na Ziwa Victoria,sasa kuna majanga yasiyosemeka.
Wakati Wazungu wakihaha kutafuta hifadhi katika Sayari ya Mars, Kanda ya Ziwa kuna uchafuzi wa mazingira na vyanzo vya maji,kuna ukataji wa miti kwa ajili ya mkaa nk
Matokeo yake eneo zima hilo mvua zitakoma kunyesha kabisa,na hata     zaweza kunyesha mvua za sumu(acid rains) zinazoweza kuleta athari kubwa kwa mimea na viumbe hai.
Ni kutokana na hali hiyo ya uchafuzi wa vyanzo ya maji(water pollution) na uchafuzi wa hewa(air pollution) Wazungu wanafanya mipango kamambe kuihama Dunia inayochafuliwa ili wakatorokee Anga za juu,hususan Sayari ya Mars
0713 324074