Friday, May 25, 2012

MELI ZA ZIWA VICTORIA NI MAJENEZA YANAYOELEA?


                   

                    *Kununua tiketi  ya usafiri katika boti hizo, ni kununua tiketi ya kuzimu!
          
                 Na Conges Mramba, Mwanza
   NI SAA nane mchana, Alhamisi,Mei 24. Niko Mwaloni,Kirumba,Jijini Mwanza,katika moja ya Bandari bubu zilizomea kama uyoga, kandoni mwa Ziwa Victoria.
 Mbele yangu kuna boti iliyojengwa kwa mbao na mabati; imechakaa. Inapakia abiria na mizigo,tayari kung’oa nanga kuelekea katika moja ya visiwa vingi vidogo vidogo vya Ziwa Victoria.
   Nachungulia ndani ya boti hii, Mv. Maisha, nabaini kuna maboya machache yameputikwa ndani ya gunia kuu kuu.Sioni vifaa vya kuzimia moto(Fire Extinguishers), sioni kisanduku cha Msaada wa Kwanza(First Aid).
 Kama ada, makuli wanaendelea kupakia ndani ya Mv.Maisha mizigo; viroba vya sukari,chumvi,maboksi ya sabuni. Pia wanapakia magudulia ya mafuta ya taa na hata petrol! Wanachanganya abiria na mizigo? Abiria na petroli?
  Naam, hii ni boti iitwayo, Mv.Maisha inapakia abiria na mafuta ya taa na petrol, abiria wameketi botini kimya,hakuna anayeshangalia kitisho cha ajali ya moto, pindi petrol ikichokozwa kwa moto wa injini ya boti, ama moshi wa sigara!
  Abiria wanazidi kuingia na kuketi. Hawana muda kuhoji ikiwa boti hii ina maboya ya kutosha? Ina Bima? Ina vifaa vya kuzimia moto, au vile vya uokozi pindi ajali ikitokea?
   Alfred Wariana, ni Afisa Mfawidhi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini(SUMATRA), Mkoani Mwanza, ambaye anasema Ajali ya Meli ya Mv.Bukoba,Mei 21,mwaka 1996,iliizindua serikali katika usingizi wa pono,imetunga sheria za Usalama Majini!
  “Kufuatia Ajali ile. Sheria ya Kuongozea vyombo vya majini, The Merchant Shipping Act, imetungwa mwaka 2003,ikaanza kutumika mwaka 2004 ili kudhibiti Ajali”,Wariana anasema katika Mahojiano Maalum ofisini mwake.
   Kulingana na Wariana, Ofisa huyu  Mfawidhi wa SUMATRA, Mwanza kuna jumla ya Meli 47 ambazo zote zimesajiliwa, zina BIMA kwa sababu mtu hawezi kuendesha biashara ya huduma za Usafiri pasipo kuzingatia taratibu, sheria na kanuni.
  “Changamoto ya SUMATRA,Mwanza kuna boti zaidi ya 10,000 zinazosafirisha abiria na mizigo kwenda visiwani na Sengerema,Ukerewe na Geita. Huwezi kusema, asilimia mia zote hufuata sheria, na kuzingatia maelekezo.SUMATRA Mwanza, tuna wakaguzi watatu tu,lakini tunao mtandao(usiotosha) wa kuwadhibiti wasafirishaji wasiopenda kutii sheria pasipo shuruti. Kumbuka, Ziwa siyo barabarani ambako utaweza vizuizi njiani na kufanya ukaguzi ili kuwabaini wakosaji”, anafafanua Wariana.
  Polisi na Watendaji wa vijiji wapo katika maeneo ya vituo vya kibiashara,ambako boti hizi hutia nanga na kupeleka bidhaa,wanapaswa kuwatia mbaroni wasafirishaji wasiozingatia sheria za Usafirishaji wa Majini.
Kulingana na SUMATRA,Mwanza, ziko changamoto kuwafikia wamiliki wote wa vyombo vya majini,hususan vidogo vidogo,na kuvikagua kila mara.
 “Hata hivyo,mtandao wetu wapaswa kukagua na kuhakikisha kila chombo ni salama kabla ya kuanza safari,na kila chombo cha usafiri chapaswa kuwa na cheti cha kufaa-sea worthiness.
 Katika Ziwa Victoria,SUMATRA wana ofisi Mwanza, Bukoba na Musoma. Ziwa Victoria kuna visiwa takriban 60, Ukerewe pekee kuna visiwa 38 vingine hukaliwa na wavuvi tu.
  Mei 21, mwaka 1996,Meli iliyomilikiwa na lililokuwa Sherika la Reli(TRC) ilizama umbali wa mail inane(kilomita 12) za majini, jirani na Bandari ya Mwanza, uelekeo wa Bwiru.
 Mv. Bukoba, ilipinduka kasha kuzama,ikasababisha vifo vya zaidi ya watu 800.Wengine zaidi ya 100 walijeruhiwa,wakipoteza mali nyingi za mamilioni ya shilingi,hususan mikungu mingi ya ndizi.
 Kwa mujibu wa Ripoti ya Tume ya Jaji Robert Kissanga, iliyochunguza chanzo cha Ajali hiyo,usiku wa kuamkia siku ya ajali,Mv.Bukoba ilipakia abiria kati ya 750 na 800 pamoja na wafanyakazi 37 wa Meli hii.
  Kati ya hao, 114 waliokolewa wakiwa hai, wakati 391 waliopolewa wakiwa   wamefariki wakazikwa katika Makaburi ya Igoma,nje kidogo ya Jiji la Mwanza. Miili mingine ilichukuliwa na jamaa zao kwenda kuzikwa kwao. Jumla ya miili 332 haikupatikana.
      Kila mwaka, ifikapo Mei 21, serikali inayosema Haina Dini, huongozana na viongozi wa madhehebu ya dini na waganga kwenda eneo la ajali,kufanya ‘matambiko’ na kumwaga mchanga eneo  majini!
  Serikali iliwashitaki  katika Mahakama Kuu  aliyekuwa Nahodha wa Mv.Bukoba, Jumanne Rume-Mwiru, (ambaye sasa ni Marehemu),Mkaguzi wa Mamlaka ya Bandari(wakati huo THA),Gilbert Mokiwa, aliyekuwa Meneja wa Bandari ya Bukoba, Alphonce Sambo, na aliyekuwa Maneja wa Bandari ya Kemondo, Prosper Lugumila.
  Kesi hiyo Nambari 22 ya mwaka 1998, ilianza kusikilizwa Mei 14 mwaka 2001. Miongoni mwa waendesha mashitaka katika kesi hiyo ni Eliezer Feleshi, ambaye sasa ni Mkurugenzi wa Mashitaka nchini(DPP).
  Hukumu ya kesi hii ilitolewa Ijumaa, Novemba 29 mwaka 2002,majira ya saa sita mchana hadi saa 9 na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Juxton Mlay(amestaafu).
 Washitakiwa wote walishinda kesi hiyo,kufuatia Hukumu yenye kurasa 118 iliyosomwa kwa dakika 160 na Jaji Mlay,kusema Mv.Bukoba ilizama kwa sababu haikuwa na uwiano wa majini, na siyo uzembe wa washitakiwa.
 Serikali ikakata rufaa, hadi leo majaliwa na rufaa hiyo hayajulikani,na baadhi ya washitakiwa wamefariki dunia,bila kujua hatma ya kesi hiyo na stahili zao.
   Mv.Bukoba ilikuwa ‘Kaburi’ lenye kuelea Ziwa Victoria. Ilikwishapigwa marufuku,kwa kuwa haikuwa na viwango vya ubora-sea   worthiness.

Ilijengwa na Kampuni ya Kibelgiji,ikazinduliwa  Julai 27 mwaka 1979.Siku ya uzinduzi, ilibainika haikuwa thabiti,na ilikosa uwiano,ilitaka kumtosa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere ambaye alikuwa Rais wan chi wakati huo.
   Miaka michace iliyopita, meli nyingine ya MSC, Mv. Butiama, ilizimika injini zake jirani tu na Bandari ya Mwanza, lakini ikaelea kwa zaidi ya saa mbili,huku abiria wakihaha bila msaada. Ilikuja kufahamika kwamba, meli hiyo haikuwa na mawasiliano!
 Meli nyingine ya mizigo, Mv.Nyamageni,ilizama ziwa Victoria ikiwa na abiria zaidi ya 20 waliosafirishwa pamoja na masanduku ya soda kwenda visiwani.
 Feburuari mwaka huu,  Mv. Pacific iliyokuwa ikisafiri kati ya Mwanza na kisiwa cha Ghana ilizama, ilikuwa na abiria 17, mmoja alifariki wengine wakaokolewa.
 Kwa mujibu wa SUMATRA, Boti nyingine iliyokuwa na abiria 31 ilizama huko Musoma,mkoani Mara,abiria   wote wakaokolewa kwa kytumia zana za uokozi.
 Kwa mujibu wa Alfred Wariana, Ofisa Mwandamizi wa SUMATRA, katika ajali tatu za karibuni, kati ya watu 81 waliokuwemo katika boti hizo,ni mmoja tu aliyefariki dunia,na anasema hii huonesha kwamba sheria zimeanza kufuatwa.
  Kabla ya vyombo vya majini kuanza safari ni sharti kukaguliwa ili kuthibitishwa usalama wake.
Hata hivyo, Wariana anasema bado usafiri wa majini Ziwa Victoria ni salama zaidi kuliko barabarani.
“Usafiri wa barabarani hata wa ndege hapa Afrika ndiyo ‘Moving Coffins’ (majeneza yanayotembea),Barabarani kuna magari kuna pikipiki zinazochinja watu kila siku”, anasema Wariana.
http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/7/7b/Liemba1.jpg/238px-Liemba1.jpg moja ya meli za MSC ziwani Victoria
 
Akizungumza kuhusu ushindani wa kibiashara, Ofisa huyu wa SUMATRA amesema, kuimarishwa kwa miundombinu ya barabara, hususan kutoka   Mwanza hadi Musoma, Tarime na hata Kenya,kumesababisha abiria wengi kususia usafiri wa meli.
 Tangu barabara ya lami ya Mwanza hadi Musoma ikamilike mwaka 1985, hakuna tena abiria wanaosafiri kwa meli kwenda Musoma,Shirati au hata Kisumu,Kenya.
    Upungufu huu ni wa abiria wa meli ni wa takriban asilimia 50.
  Kaimu Meneja Masoko na Biashara wa Kampuni ya Meli(MSC)Kapt. Obedi Nkongoki, anasema mwaka jana Kampuni hii ilisafirisha jumla ya abiria 235,794 tu ambao ni chini ya uwezo wake. Mizigo iliyosafirishwa ni tani 54,212.
  Kulingana na Kapt. Nkongoki, MSC ina jumla ya meli 15 zinazosafirisha abiria na mizigo kati ya Mwanza na  Musoma,Bukoba,Kemondo,Jinja(Uganda),Kisumu(Kenya),Port Bell Uganda, na Ukerewe.
 Mv.Victoria ndiyo meli kongwe kuliko zote; ilijengwa mwaka 1960. Imekuwa ikifanyiwa matengenezo na ukarabati mkubwa na mdogo.
 Kaimu Meneja Mkuu wa Marine Services Company(MSC)Projest Kaija, anasema Mv..Victoria ina umri wa miaka 52, lakini imefanyiwa ukarabati mkubwa na mdogo mara nyingi. Mara ya mwisho ilifanyiwa ukarabati mkubwa(Major Rehabilitation) mwaka 2008 ambako ilikaa miezi sita katika Bandari ya Mwanza South Port bila kufanya huduma.
  Ina uwezo wa kuchukua abiria 1,200 na tani 200 za mizigo;lakini kufuatia abiria kupungua siku hizi inachukua abiria 500-800,chini ya uwezo wake. Inafanya safari zake kati ya Mwanza-Kemondo-Bukoba-Mwanza.
 Kwa mujibu wa Kaija, meli nyingine za MSC zinazofanya huduma Ziwa Victoria, ni Mv. Butiama,Serengeti,Clarias ambazo hubeba abiria na mizigo kati ya Mwanza,Bukoba na hata Nansio-Ukerewe.
 Meli za mizigo ni pamoja na Mv. Umoja, Mt. Nyangumi ambayo husafirisha mafuta kutoka Mwanza hadi Kisumu,Kenya na Jinja na Port Bell huko Uganda.
 Mv.Ukerewe, MI wimbi na Malindi husafirisha mizigo,wakati Tanganyika Sea Warrior ni  boti mpya ya kusafirisha watalii wapatao 15 kwa wakati mmoja.
 Mt(Motor Tug) HUVUTA MATISHARI.
  Ziwa Victoria lina eneo la kilomita za mraba 68,800. Ni ziwa la pili kubwa duniani lenye maji baridi na ni nyumba ya sangara ambao sasa wamekaribia kwisha. Ni ziwa kubwa kuliko yote Afrika, Tanzania inamiliki asilimia 49 ya ziwa hili, Kenya asilimia 6 na Uganda inamiliki asilimia 45.
  Kulingana na Wariana, Ofisa Mfawidhi wa SUMATRA,Mwanza, mabaharia wote wa meli wanapaswa kuwa na viwango na wawe wamehitimu katika Chuo cha Mabaharia, Dar es salaam Maritime Institute,(DMI) ambacho hutambuliwa kimataifa.
 “Hakuna meli inayoendeshwa na Nahodha asiye na sifa”, anasema Wariana wa SUMATRA.Vyo mbo vyote vinapaswa kuwa na BIMA na vifaa vya uokozi,lakini boti chache na mitumbwi midogo na majahazi husafirisha abiria pasipo mamlaka kubaini,na ni changamoto zilizopo, wanapaswa kufuata sheria”, anasema Wariana wa SUMATRA.
Vyombo hivi vispofuata sheria,kanuni na taratibu za usafirishaji salama majini, Wariana anasema ndiyo hufanya kununua tiketi za usafiri katika vyombo hivi kuwa tiketi za kuendea KUZIMU!
  “Kwa bahati, shughuli za uvuvi ziwa Victoria zimepungua sana katika visiwa hakuna tena watu wengi wanaoenda huku na huko,kwa sababu samaki wamepungua sana ziwani,na ajali za majini zimepungua”, anasema Alfred Wariana, Ofisa Mfawidhi wa SUMATRA,Mkoani Mwanza.


Tuesday, May 22, 2012

OBAMA NA ROHO TATU ZA VYURA



Juma lililopita tukaona kuanguka kwa Ukomunisti na kuinuka kwa Dola la Madola ya Ulaya na Marekani; na namna yalivyoanza kuwafyeka Wakomunisti Duniani.
Carlos, aliitwa ‘The Jackal’ na Gazeti la The Guardian la Uingereza, kufuatia  riwaya(novel) yaa Fredrick Forsyth.
Carlos, alisuswa na Chama cha Ukombozi cha Palestina(PFLP) baada ya wale magaidi wa BLACK SEPTEMBER kuvamia wanariadha wa Israeli katika kijiji cha Olimpiki huko Munich,Ujerumani Septemba 5, mwaka 1972.
Nitaeleza tukio hili kwa kina sana wakati michezo ya Olimpiki ya London itakapoanza mwezi Julai,mwaka huu-usipange kukosa TAZAMA upate darasa.
Ilikisiwa kwamba, Carlos aliwasaliti PFLP hadi wale magaidi wake wakauawa na makomando wa Kijerumani, hiyo Septemba,mwaka 1972.
Carlos,chakaramu mpenda vimwana warembo, mvuta sigara aliyekubuhu na mpenda starehe hususan, ‘kilaji’ alianza kuwa gaidi wa kukodishwa hadi alipotiwa mbaroni mjini Kharthoum,Sudan mwaka 1994.
Naam, chakaramu mpenda anasa(playboy) alishiriki Operesheni tele za kigaidi katika miaka ya 70 mna 80,tangu kuuliwa kwa hao wanariadha 11 wa Kiisraeli mjini Munich.
Hata ile ndege ya Ufaransa,Air France Air Bus, iliyotekwa na Wapalestina na kulazimishwa kutua Entebbe,mwaka 1976 zama za Dikteta Idi Amin Dada, Carlos alisuka mpango-nitaeleza kisa hiki kwa utulivu miezi michache ijayo.
Hata hivyo, Carlos anasema hajawahi kuua mtu kwa ajili ya pesa, “Nimeua watu kwa sababu ya ukombozi wa Palestina”, anasema.Ndivyo wafanyavyo al-Qaeda, na al-Shabaab, violence resistance!
 Wakati wa Mkutano wa Mawaziri wa Mafuta wa OPEC,mjini Vienna, Austria,walitekwa nyara watu 70,na Carlos alishiriki kufanya tendo hili na kuua wana usalama.Waliachiwa huru nchini Algeria, baada ya Carlos The Jackal kulipwa kikombozi cha Dola za Marekani Milioni moja ambazo sasa ni kama Bilioni 1.6 HIVI.
Fedha hizi,wanasema alilipwa na Muammar al Qaddafi, aliyekuwa akiunga mkono kitendo cha kuwateka nyara mawaziri wa OPEC huko Vienna.
 Nataka msomaji atambue uhusiano uliokuwepo kati ya Carlos, Osama, Saddam Hussein na wanaharakati wengine waliopinga ubeberu wa Kimagharibi kwa mabomu na mtutu wa silaha.
 Fedha hizi zikamgombanisha Carlos na magaidi wenzake wa Kipalestina.OPEC walishindwa kufanya mikutano kwa jumla ya miaka 25, hatimaye PFLP wakamkataa Carlos.
Akafanya makazi yake Syria(kunawaka moto wa mabomu hata leo),Lebanon(nako wako hatarini) na mahali pengine walikoungwa mkono kama Berlin Mashariki.
 Ile roho ya akina Carlos ingalipo Syria na mahali pengine,na ndiyo maana unasikia vuguvugu la vibaraka wa Marekani na Ulaya wakipingwa wasikamate utawala katika nchi hizo sasa.
 Tunajadili vuguvugu la vibaraka wa Magharibi kukamata sukani za utawala katika nchi za Ulimwengu wa Kiarabu, na kuinuka kwa ‘Roho Tatu’ za Freemasons,Illuminati na mawakala.
Wasomaji wataniuliza kama Carlos aliwahi kuoa? Naam, Magdalena Kopp,walizaa naye mtoto wa kike. Kopp alikamatwa na vilipuzi(explossives) huko Ufaransa, akafungwa jela.
 Carlos alikuwa mshirika wa Shirika la Ujasusi la Urusi(KGB) siku hizi linaitwa KFB, hivyo majasusi wa CIA na mashushushu wa Ulaya, hususan Ufaransa walimsaka sana,wakaja kumnasa Khartoum, Sudan mwaka 1994.
Kwa nini?
 Ni baada ya kuanguka kwa UKUTA WA BERLIN na kuparaganyika kwa Dola la Urusi,yaani kuanza mchakato wa ‘Kukaushwa kwa Mto Frati’ vita Baridi vikatoweka duniani, Carlos akakosa hifadhi, akatiwa mbaroni,kwa sababu dunia ilikuwa ikiungana, muungano haramu.
Carlos amehukumiwa kifungo cha maisha,Desemba mwaka 1997 katika gereza la Clairvaux, Ufaransa.
Hata hivyo, alibadili dini na kuwa Muislam,akamuoa kidosho mmoja Mwanasheria wake,Isabelle Coutant-Peyre,mwaka 2001.
 ‘Revolutionary Islam’ ni kitabu chake cha mambo yake ya Harakati zake za kigaidi. Anajitetea katika kitabu hicho,kusema alitumia risasi na mabomu kutafuta HAKI.Anamuunga mkono Osama Bin Laden, anasema alikuwa ‘Mrithi’ wake mahsusi.
 Carlos aliwahi kuandika waraka akiwa gerezani ukafika hata kwa Barack Obama.ANAILAUMU sana mahakama ya Haki za Binadamu kwa kunyimwa haki ya kuonana na wafungwa wenzake na anavyonyimwa matibabu.
 Rais Hugo Chavez wa taifa alikozaliwa, Venezuela, anamuenzi Carlos kama “Mwanamapinduzi Mpiganaji”.
Waliomuunga mkono Carlos: Saddam Hussein, Osama aliyeuliwa Mei Mosi mwaka jana,Fidel Alejandro Castro Ruz na Hugo Chavez. Mto Frati ulishaanza kukauka tangu mwaka 1994,na wafalme wa Dunia wanaanza kuunga mkono kila Marekani na washirika wake wanachosema, kukiwemo kubadili katiba na kukubali ushoga!
 Carlos akiwa gerezani anakotumikia kifungo cha amaisha, siku moja akapelekwa tena mahakamani kujibu mashitaka ya mauaji ya mawakala wa Usalama.
Alipelekwa mbele ya Jaji  Jean-Louis Bruguiere, ambako alishitakiwa kuua na kuharibu mali kwa milipuko huko Ufaransa kati ya mwaka 1982-83.
Unamfahamu Jaji Bruguiere? Nitakupa stori: Mwaka 2006 alitaka Rais wa Rwanda Jenerali Paul Kagame, akamatwe na kushitakiwa kwa makosa ya kulipua ndege iliyowabeba marais wawili wa Rwanda na Burundi, Juvenal Habyarimana na Cyprien Ntaryamirwa, Aprili 6 mwaka 1994 katika anga ya Mjini Kigali.
Wakati huo Kagame alikuwa Kamanda wa vikosi vya Waasi wa Rwandese Patriotic Front(RPF)kwamba aliwaamuru Waasi wa RPF kutungua ndege iliyowabeba marais hao waliokuwa wakijiandaa kutua wakitokea Dar,mkutanoni.
 Siku 100 za Mauaji ya Kimbari zilianza wakati huu na zikasababisha watu 800,000 kufa. Hili niliache.
Nijadili kidogo Illuminati na Freemasons wanavyopanga kupindua serikali za     dunia na hata viongozi wa makanisa yenye nguvu duniani.
Jumanne, Mei 8 mwaka huu, mwandishi Gideon M. alimkariri Peirs Comptons kupitia kitabu chake THE BROKEN CROSS  akisema kwamba Illuminati walikuwa na mpango kamambe wa kumpindua Papa Benedict XVI.
Nimemsikia Papa huyu akitangaza kutaka kuachia madaraka, nikajiuliza: Mapapa takriban wote hufia madarakani; iweje yeye astaafu,ikiwa ametawazwa Mei mwaka 2005?
 Kwamba Illuminati wanampango wa kumweka ‘mtu wao’ katika nafasi hiyo nyeti sana, kwamba kitabu hicho ukurasa wa saba na nane Peirs aliandika mpango wa kuunganisha dini zote duniani.
 Kwamba, Illuminati wana ajenda ya siri ya kuuteka Upapa na kumweka mtu wao katika ‘Kiti cha Enzi’ kinachoitwa, Sedia Gestatoria,kiti cha dhahabu chenye rangi nyekundu, ni kitu cha kuleta tashtiti.
 Mtu Fulani kutawazwa kushika mahali pa ‘Mrithi wa Mtume Petro’ maana yake siyo kuongoza Kanisa Katoliki tu,ni kuongoza Jumuiya za Kikristo,Kibudha,Waislam, Bahai’s,Orthodox,Protestants n.k
 Huyu Peirs ni kasisi wa Kanisa Katoliki na aliwahi kuwa Mhariri wa Gazeti la Universe la Kanisa hili huko Mjini Vatican.Siku hizi siri hata za ufisadi zinavuja kutoka Vatican, Hamkani si shwari Vatican.
 Kumweka wakala wa Freemasons katika kiti cha enzi Mtakatifu Petro,maana yake ni Freemasons kuongoza dini zote duniani,kuongoza imani.
 Petro,Mtume wa Bwana Yesu anaaminiwa na Wakatoliki kuwa ndiye hasa muasisi wa kanisa hilo.
Alifika Rome mwaka AD 42 akaja kuuliwa na Kaisari Nero mwaka 67 AD.Kanisa Katoliki wanasema Petro alianza Upapa mwaka 32-67 AD.
Kanisa la Mtakatifu Petro, St.Peter’s Basilica limejengwa juu ya kaburi la Petro. Papa ni Mrithi wa Petro,PAPA aliyemrithi Petro ni Linus(67-76 AD),ni Mkuu wa Vatican analindwa sana na Swiss Guard, ni Askofu wa Rome,ni mwakilishi (The Vicar of the son of God) wa Yesu duniani,ni Mkuu wa mitume wote katika zama zote,wakiwemo mitume wa siku hizi,yuko juu ya Judaism, Hinduism, Budhism,Islam n.k?
 Naam, tuzilinganishe habari hizi na mafungu ya Biblia Takatifu.
Papa anayetangazwa na moshi mweupe, ni miongoni mwa viongozi wa dini wanaoenziwa mno na mamlaka za dunia.
Tulijadili sanamu la mwanamke aketiye juu ya mnyama mwekundu sana mbele ya ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Ulaya(EU) huko mjini Brussels.
Angalia picha hiyo na ile ya Ufunuo 17:1-7. Mwanamke katika unabii wa Biblia huwakilisha kundi Fulani la waabuduo madhehebu Fulani. Katika Biblia kuna wanawake wawili: Ufunuo 12:1-6 na Ufunuo 17:1-18.
 Huyu mwanamke wa Ufunuo 17 anaitwa ‘kahaba’ ama mzinzi na amezaa watoto(wa kike) nao ni makahaba(Ufunuo 17:5).
Mwanamke huyu pia huwakilisha jiji kubwa duniani uitwao Babeli ya SIRI. Gideon M. AMEANDIKA kwamba kiti cha enzi cha Mji huu kinanyatiwa na Freemasons.
 Na mji huu uko juu ya vilima saba(Ufunuo 17:9) na wakati wa Nabii Yohana aliyeandika kitabu cha Ufunuo mwaka 96 AD ni mji uliokaliwa na watu wengi sana yanayofananishwa na maji mengi(Ufunuo17:15,18).
Siku hizi, miji yenye wakazi wengi ni Tokyo,wenye wakazi zaidi ya milioni 28,Mexico City,Mumbai, Sao Paulo, New York, Los Angeles,Lagos,Calcutta,Shanghai, Buenos Aires, Dhaka,Karachi, Jakarta na Osaka.
 Hata hivyo, miji yote hii katika karne ya Kwanza AD haikuwepo, na haikuwa na sifa za kuwa na wakazi wengi.
Katika karne ya kwanza, wakazi wa dunia hawakufika milioni 500.Mwaka 1AD Kulikuwa na watu milioni 200 tu duniani, siku hizi kuna bilioni saba.
 Itaendelea

0754 324 074


Tuesday, May 15, 2012

OBAMA AMETANGAZA UHURU DHIDI YA AMRI 10 ZA MUNGU!!



BARACK OBAMA, ni Rais wa Taifa kubwa kuliko yote Duniani(Marekani), ametangaza kuunga mkono Ndoa za Jinsia Moja,Mei 10 mwaka huu.
Tangu uhuru,Julai 6 mwaka 1776,hakuna Rais wa Marekani,miongoni mwa marais 43 waliomtangulia, aliyewahi kuunga mkono ushoga na usagaji.
Obama, ni Rais wa 44 wa nchi hii inayofananishwa na MWANAKONDOO mwenye pembe mbili(Tazama Ufunuo wa Yohana 13:11-18) katika Biblia.
Nchi iliyowatunza Wakristo na kuwapa upendo(lamblike beast) yenye kutenganisha masuala ya dini na siasa(separation  of powers), inaoneshwa katika unabii huu kuwa ilikuwa na pembe mbili(two horned).
Pembe,katika unabii ni mamlaka(Zaburi 18:2,Luka 1:69).Pembe mbili zinatafsiriwa vizuri katika sanamu liitwalo, THE STATUE OF LIBERTY; umewahi kuliona?


sanamu la uhuru,Mwenge na BIBLIA,sasa Rais Obama ametangaza uhuru dhidi ya AMRI 10 za Mungu, hususan zinazopinga ushoga!


Sanamu hili, tangu mwaka 1886 linaashiria Dunia nzima kwamba Marekani kuna uhuru wa kusema na uhuru wa kuabudu. Lilisanifiwa na kujengwa na Mfaransa, Frederic Auguste Bartholdi(1834-1904).   
Wafaransa waliwakabidhi Wamarekani sanamu hili la Uhuru ambalo lipo mbele ya lango la Bandari ya mjini New York. Sanamu hili ndilo huwakaribisha wakazi wote wa Dunia mjini New York ambao hufika nchini humo kwa meli.
 Kuna mwenge unaoshikiliwa na mkono mmoja wa sanamu hili, unamaanisha UHURU na demokrasia, na mkono wa pili unashikilia Biblia kuonesha uhuru wa dini,ama uhuru wa kuabudu,tofauti na ilivyokuwa Ulaya.
 Sanamu hilo lilikamilika kujengwa Mei 21, mwaka 1884. Uzito wake ni Pauni 450,000 au tani 225. Sanamu hilo ambalo ni makumbusho ya Taifa, mkono wake wa pili umeshika Biblia, kuonesha uhuru wa watu kuabudu,bila kulazimishwa.
Sanamu hili la uhuru linalotenganisha masuala ya dini nay a kiserikali,na linalohamasisha demokrasia na uhuru wa dini,kwa karne nyingi, limeashiria demokrasia na uhuru ukiwemo wa ibada katika nchi hii.
Hata hivyo, kwa Tangazo la Rais Obama kwamba yeye na mkewe,Michelle, na  bintize, Malia  na Sasha, na rafiki zao wa karibu,hawaoni ubaya wa ndoa za jinsia moja,na kwamba wanawaunga mkono mashoga na wasagaji, maana yake ni kama ifuatavyo:
Kwanza, Obama ni Rais wa Taifa kubwa duniani. Kauli yake ni kama Amri ya 10 ya Mungu Duniani! Mivuto yake katika dunia ni mikubwa sana kwa watu wengi.Sasa kutangaza kutoona ubaya wa ushoga na usagaji,maana yake ni kuutangazia Ulimwengu kwamba wanaopinga ushoga,ni wajinga na wapuuzi hivi.
Maana yake ni kwamba, ni kusisitiza nchi masikini duniani kubadili Katiba zao ili kuunga mkono ndoa za Jinsia moja, kwa kuwa hata Obama anaona hazina shida, ndiyo maana hata yeye mwenyewe alishawachagua mashoga takriban 200 katika nafasi za juu za utumishi wa umma serikalini mwake.
 Sasa, tunaingia rasmi katika Sodoma na Gomora. Marekani iliyokuwa nchi ya uhuru wa siasa na Dini, imeanza kunena kama JOKA-Ibilisi, Obama kutangaza kuunga mkono ushoga,maana yake ni kuutangazia Ulimwengu UHURU dhidi ya Sheria za Mungu muumbaji, na uhuru dhidi ya mbinyo wa AMRI 10 ZA MUNGU.
Katika Ufunuo 13:11 Biblia inatabiri kwamba,Marekani yenye uhuru,demokrasia na haki za binadamu katika katiba yake, sasa ingeutumia UHURU huo na demokrasia kuachana na Mungu na matakwa yake na kwenda katika njia ya Shetani(kunena kama Joka).
 Makamu wa Rais wa Obama, Joe Biden na Waziri Mkuu wa Uingereza,David Cameron  ni miongoni mwa watu wakuu duniani wanaounga mkono ushoga na usagaji.Wewe nani hadi upinge? Ukipinga, unapinduliwa, tena wanyimwa msaada,unawekewa vikwazo-economic sanctions!!
 Marekani,nchi ya Waprotestanti,Wakatoliki ni wachache. Marekani inaanza kunena kama JOKA ambaye ni Shetani. Nchi hii ya Wakristo wengi wanaoamini kwamba NDOA ni muungano kati ya watu wawili wa jinsia tofauti, ndoa iliyohasisiwa na Mungu mwenyezi katika Bustani ya EDENI, sasa imeanza kutangazwa kwamba ni muungano wa watu wawili,mradi wawe na umri kuanzia miaka 18.
 Dini ya Angican(Malkia Elizabeth ndiye Mkuu wake) ilishakubali ndoa hizi za mashoga, ingawa Kanisa hili hapa Afrika linapinga jambo hili na kusisitiza kuwa ndoa iwe muungano wa hiari kati ya mume na mke.
Askofu, V. Gene Robinson wa Jimbo la Hampshire huko Marekani ndiye askofu wa kwanza mume kuolewa na mwanaume mwenzake aitwaye Mark Andrew. Ni miaka michache tu iliyopita, na hawa walifunga ndoa kanisani tena mbele ya ndugu zao wa pande mbili.
 Majimbo takriban 10 ya Marekani yamekubali ndoa hizi, na majimbo mengine mashoga wanafunga ndoa kwa leseni. Haya mambo yamefika hadi Afrika ya Kusini,na Kenya nayo iko hatarini, hata Tanzania katiba yetu inaweza kuwekwa kipengele cha haki za  mashoga na wasagaji kuoana.
 Naam, huu ndiyo uhuru na demokrasia tunayotaka, ndiko tuendako,ukurasa mpya umefunguliwa na Obama na David Cameron, huu ni UHURU DHIDI YA MUNGU!
 Unaweza kujiuliza kwamba, Marekani inaheshimu sana demokrasia na uhuru wa watu? Mbona gereza la Guantanamo huko Cuba,linawatesa wafungwa na raia wanahukumiwa katika magereza ya kijeshi,hata kama ni magaidi?
Kuanzia hapa,tunamaizi kwamba Mungu ameanza kupingwa waziwazi na sheria zake zinazopingwa ushoga na usagaji zimewekewa kibanzi,ili zisitumike,ndiyo Marekani kunena kama JOKA.
                                                          (ii)
Nijadili kidogo kuanguka kwa ukuta wa Berlin mwaka 1994,kwamba kuliashiria kumalizika kwa VITA BARIDI,baada ya Vita vikuu vya Pili vya Dunia 1945.
 Kumalizika kwa vita Baridi,vilivyoanza baada ya vita vya pili kwisha, maana yake ni kuufagilia mbali UKOMUNISTI.Dola la Urusi la Kisovieti(USSR) liliparaganyika tangu mwaka 1991.
Ukuta wa Berlin ulioitenga dunia katika Mihimili miwili ya Magharibi na Mashariki ulishavunjwa na kuifanya dunia kuwa kama kijiji kimoja. Kuanguka kwa Ukuta wa Berlin na Kuparaganyika kwa Dola la Kisovieti la Urusi(USSR) ni kuonesha kwamba ubepari ulikuwa umeushinda ujamaa duniani.
 Tunaishi katika zama za MWENYE NGUVU MPISHE.Kuanguka kwa ukuta wa Berlin na UKOMUNISTI maana yake ni kwamba “Mto Frati” uliokuwa ukiitenda dunia ya zama za Waisraeli kati ya Mashariki na Magharibi, ulikuwa umeanza ‘kukaushwa’.
MMchakato wa kukaushwa maji ya Mto Frati(the dries up process of the River Euphrates) ulishaanza,ili njia itengenezwe wafalme watokao nji za Mashariki(UCHINA,INDIA,JAPAN n.k) wapiti na kwenda kuungana na madola ya Magharibi. Tumeona mataifa ya Kisovieti yakijiunga NATO na Umoja wa Ulaya EU.
 Tumeona, Uchina,Urusi, Japan,Korea Kusini,Pakistan,India n.k wakishirikiana na Mataifa ya NATO hata kutoa ardhi zao kwa majeshi ya NATO na mashirika ya kijasusi kama CIA na MOSSAD kutekeleza Operesheni anuwai za kijeshi.
Tumeona nchi za Kiarabu zikigeuza ardhi zao kuwa Base za kijeshi za Marekani na washirika wake, tunaona juhudi za mataifa ya Mashariki hata kujiunga umoja wa sarafu moja ya Euro-Euro Zone , tunaona juhudi za Mashariki kushiriki Soko la Pamoja Ulaya European Common Market n.k
 Ufunuo 16:12-16 huonesha wazi kwamba nchi za Kisovieti na zingine za Mashariki na mrengo wa kijamaa, zitaungana na Ulaya na Marekani, na zitaachana na imani zao na ibada zao na kwenda kuungana na roho za  mashetani, za Freemasons na Illuminati,ndiyo ROHO ZA VYURA na manabii wa Uongo(Ufunuo 16:13-16)
 Har-Magedon, ni vita dhidi ya Mungu na Amri 10. Mataifa yote ya Dunia yataungana ili kumpinga Mungu,yataungana na Ibilisi kwa misingi ya kusaka uhuru na demokrasia.Pepo wachafu wataungana na wanadamu ili kukataa mafundisho ya Mungu na maagizo yake,wanaanzia kwenye kanuni za ndoa na imani ya kweli.
 Dunia nzima itaungana kiuchumi,kisiasa, na wale waliokuwa na itikadi za Carl Marx(Marxists) wataondolewa kwa nguvu kubwa.
Hadithi ya Illich Ramirez Sanchez(Carlos The Jackal) inatuonesha namna hawa Wa-Marx walivyoshindwa na ubepari.
Carlos The Jackal(63) alizaliwa Caracas,Venezuela mwaka 1949. Babaye alikuwa mfuasi wa siasa za Karl Marx akawahusudu mno wanamapinduzi wa Amerika Kusini: Carlos Merighella, Camillo Torres na Che Guevara.
Carlos, ni mfano wa Osama bin Laden wa zama hizo, alipinga ubeberu wa Magharibi kwa njia ya nguvu za kigaidi,Mungu hataki kutumia njia hizo ili kuleta haki duniani.
 Alisoma katika Chuo cha kijeshi cha Mantanzas huko Havana,Cuba na akatokea kuwa Komandoo kutokana na walimu wa medani za kijeshi wa                   Urusi.
 Babaye hakumwamini Mungu na mamaye alikuwa Mkatoliki,wakaachana. Carlos alikwenda London, baadaye akapelekwa kkusoma katika Chuo Kikuu cha wanamapinduzi cha Patrice Lumumba,huko Moscow.
 Carlos, alikuwa ‘troublemarker’ dhidi ya maslahi ya mabeberu wa Magharibi. Akajiunga na Chama cha Popular Front for The Liberation of  Palestine(PFLP) Wakateka nyara watu na ndege za Magharibi ili kudai uhuru wa Palestina.
 Carlos, alijiunga na PFLP mwaka 1970 akapewa jina la Carlos kwa sababu ya asili yake ya Venezuela, Amerika ya Kusini.
 Aliitwa, The Jackal na gazeti la The Guardian la Uingereza kufuatia kisasiri(novel) cha Mwandishi Fredrick Forsyth.
Itaendelea
    0786 324 074
 
 
 

Thursday, May 10, 2012

unataka uatajiri?-8


                           *Kulikuwa na Mkono wa Freemasons katika Ajali ya Titanic
KILA palipo na utajiri:Mafuta(Dhahabu Nyeusi), Almasi, Dhahabu zenyewe, pembe za ndovu na faru,gesi n.k) aghalabu  pana vita kali.
Katibu Mkuu wa Pili wa Umoja wa Mataifa,Dk. Darg Hammarskjold wa Sweden, alifanya kazi tangu Aprili 10 mwaka 1953 hadi Septemba 18 mwaka 1961 akafa.
Alikufa kwa ajali ya ndege nchini Congo(JK Kongo) wakati wa maasi ya Shaba na Katanga. Nani anachochea maasi Kongo? Hadi leo ni nusu karne, vita vinapamba moto Congo.
Shirika la Ujasusi la Marekani(CIA) na washirika wake, walichochea vita na maasi huko Shaba na Katanga(majimbo tajiri ya rasilimali) wakamkamata Mwanamapinduzi, Patrice Emery Lumumba, na kumuulia mbali.
Lumumba, alikuwa na visheni ya kijamaa, kutaka rasilimali za Congo ziwe kwa manufaa ya Wakongo, rasilimali za Waafrika ziwe kwa ajili ya Waafrika wenyewe. Akawakosea hawa majahili.
 Wakawachochea akina Moise Tshombe, Joseph Kasavubu,Joseph Desire Mobutu na vibaraka wengine, Lumumba akauliwa kinyama Januari 17, mwaka 1961.
  Dk. Darg Hammarskjold akasafiri kwa ndege kutoka New York hadi Congo ili kusuluhisha vita, Septemba 18 mwaka 1961 akafa eti kwa ajali ya ndege.
Nataka nikwambie msomaji. Ajali za ndege zimewamaliza wanamapinduzi:Samora Moises Machel, Kanali Dk.John Garang de Mabior, Juvenal Habiarimana na Cyprian Ntarwamira,orodha ni ndefu.
Lumumba alipokufa, akina Moise Tshombe na Mobutu wakatawala Congo ambayo waliita Zaire.
Congo ina makabila zaidi ya 200, ni nchi yenye almasi,dhahabu,mbao za thamani, fedha,uranium n.kWakaiba madini wee. Mobutu alipokufa huko Rabat,Morocco Septemba,  1997, alikuwa kaficha Ulaya Dola za Maremani milioni sita,utajiri sawa na deni la nje la Congo wakati huo.
Mobutu eti alibadili jina na kuitwa Kuku wa Zabanga Mobutu Sese Seko, akaibadili Congo kuwa Zaire,tukadhani mzalendo-kumbe kibaraka wa Wazungu aliyejificha katika ngozi ya chui!
  Penye rasilimali za thamani kama mafuta,dhahabu,almasi, gesi,uranium n.k kuna vita,kuna vurugu. Penye bahari kuu,milango bahari na mifereji kama Panama,Suez n.k kuna mivutano na vurugu za mabeberu, ndiyo Libya,Misri,Nigeria,PANAMA nitaeleza mbele ya safari.
 Bosnia Herzegovina, mwaka 1995 walikufa watu 200,000.Rwanda mwaka 1994 walikufa 800,000.Lakini, kwakuwa hakukuwa na almasi,mafuta na dhahabu na pembe za faru na ndovu,hawakwenda mapema.
Walimsukumia mzigo Boutros Boutros Ghali wa Misri,kwamba alishindwa kuchukua hatua alipokuwa Katibu Mkuu wa UN. Wazungu na mwavuli wao wa NATO hawakwenda huko;kulikuwa na kitu gani cha kurejesha gharama zao? Hata Hague hawakwenda huko.
 Kwenye mafuta: Agosti mwaka 1990 Saddam Hussein alipoivamia Kuwait,kwa sababu zile zile kama za Sudan Kusini na Sudan leo za kuibiana mafuta, tayari UN wakaamrisha NATO na kuigilia kijeshi mzozo huo.
 Novemba 19900 hadi Januari 1991 tayari madege ya vita ya Wazungu yalishanyesha mvua kubwa ya mabomu Irak, Saddam akajisalimisha Aprili 1991.
 Baadaye mwaka 2003, akapinduliwa na Bush mtoto, maana ‘Bush Baba’ aliacha kiporo-Saddam alinyongwa kwa kamba nene shingoni, 2006.
Mfereji wa Panama(Panama Canal) ulisababisha Rais Manuel Noriega kupinduliwa na kutiwa mbaroni na CIA utadhani kibaka,walisema alijihusisha na biashara haramu ya mihadarati! Huwezi kushindana nao,ukapona!!
 Ilikuwa Januari 1980 Noriega alipopinduliwa na kufungwa pingu,kasha kufunguliwa kesi ya mihadarati.Marekani wakitaka kitu Fulani,rais akijidai kujua anatiwa mbaroni, inatangazwa kwamba anauza madawa ya kulevya, sasa utasemaje?
Salvador Allende  wa Chile, zlizingirwa na CIA,akakubali kujipiga risasi na SMG yake aliyokuwa amepewa na rafikiye, Fidel Alejandro Castro Ruz wa Cuba, wakamweka rafiki yao, nitaeleza kisa hiki siku nyingine.
  Kifo cha Laurent Desire Kabila,Januari 16 mwaka 2001 huko Kongo kina mkono wa hawa jamaa, Mafreemasons,Kabila alijidai mjanja, wakatumia Body guard wake kumfyatua, hadi sasa Kongo hakuna amani,kuna akina Bosco Ntaganda, sijui Thomas Lubanga na akina Jen. Nkunda ambao ukitazama wanafungamana na Rwanda na Uganda hivi,kuna mahali mali ya Congo inavushwa.
 Naam, Guns for natural resources! Kongo ni nchi tajiri,maize ya kijani hayataki kuondoka. Mashirika ya Umoja wa Mataifa, eti ya kulinda Amani(UN Peacekeeping Missions) wanapofika nchi yenye vita vya rasilimali,hawalindi amani, wanakalia mahali kwenye dhahabu,almasi au mafuta na gesi-basi wanapora!
Ziwe pembe za ndovu au za faru, wanapora na kusafirisha njia za panya hadi kwao. UNAMSIL huko Sierra Leone(Milima ya Simba) mwaka 99-2002 ndiyo biashara waliyofanya huko,wakipora almasi za damu,mbao n.k
 Congo,kuna MONUC ambao wakati Fulani wanakutwa wakipora madini, wanaacha raia kushambuliwa na waasi nao kukimbilia Rwanda huku, wao wanapora na kujitajirisha…(This is Africa)!
Huko Irak, UNIKOM lazima wawe wanamiliki visima vya mafuta,wanaomba mabomu yaendelee,ili muda wa kukaa huko uendelee,usishangae mabomu mengine wanalipua wao!
 Huko Sahara Magharibi, MINURSO wapo wanataza cha kupora ili watajirike! Unataka Utajiri? Uko Afrika, badala ya sisi wenyewe kutumia rasilimali zetu kwa akili, tunagonganishwa vichwa kama makondoo tu,kisingizio,utawala bora, demokrasia,rushwa,ufisadi…hatuwezi kuondoa haya mpaka bunduki?
  Wakimbizi, nalo ni ‘deal’ kwa mashirika kama UNHCR,UNICEF,FAO,WFP hata ILO n.k. watauza hata mahema hhuko Dar na Mwanza halafu wajenga mahekalu makubwa,ukiuliza unaambiwa, “jamaa yuko na UN Mission” labda Juba hivi au Congo.
 Vita     vina leta utajiri kwa watu wa Ulaya, wananeemeka sana, wanaomba maasi yaendelee.
Nataka kusema kwamba, amani hakuna. Mungu alishaacha kulinda amani. Tazama Ufunuo 7:1-3, Isaya 24:17-20 na Danieli 2: 43-45 uone kwamba kuna kila sababu kusema ni SIKU ZA MWISHO.
Tujadili kidogo kiporo chetu cha meli kubwa ya Titanic ILIYOZAMA huko Bahari ya Atlantic.
 Titanic, iliitwa “The Unsikable” kwa sababu  ilithibitishwa kutozama kwa namna yoyote.
 Basi,ilizama kwa sababu ya Ibilisi na maajenti wake Freemasons.
 Saa nne na dakika 20. Ni usiku wa manane wa Aprili 15, mwaka 1912. Hukuwepo na mimi sikuwepo, wakati huo-imepita miaka 100 kamili. Titanic ilianza kupotelea katika mawimbi makali ya Atlantic.
 Ilikuwa meli ya fahari sana kupita zote wakati huo,iligonga Mlima wa Barafu,ikaanza kupoteza mwelekeo wake.
 Jumla ya watu 1,503 hatimaye walikufa katika ajali ile ya kihistoria, na kulikuwa na majeruhi wengi.
Ajali mbaya zaidi ya meli duniani ni ya Feburuari 26,mwaka 1916 meli ya Provence ya Kifaransa ilizama Mediterranean na kuuaa 3,100. Kwanini haikumbukwi? Hii nayo ‘cha mtoto’.Uchina waliwahi kufa watu 6,000 katika ajali ya meli mwaka 1948,lakini watu hawaambiwi haya,isipokuwa Titanic tu.
 Meli hii Titanic Unsikable,ilikuwa na uzito wa tani 46,500, ilianza kuzama polepole katika muda usiopungua saa tatu hivi. Iliundwa imara sana,lakini ‘Unsikable’ ilizama na kukomesha kiburi cha watu cha utajiri.
Ilikuwa na kimo cha futi 883. Jioni, Aprili 14 mwaka huo 1912 meli hiyo ikiwa safarini baharini Atlantic ilikuwa ikipasua mawimbi shwari kabisa.
Ilikuwa ikienda jijini New York, Marekani na ilitokea Southampton,Uingereza. Meli hii iliambiwa kwamba baharini kulikuwa na mabonge ya barafu, hawakusikia. Ni hapa tunapoambiwa,Nahodha wa meli alipewa maelekezo kuwazamisha watu Fulani waliokuwemo melini,kwa sababu ambazo wao Freemasons walizijua.
 Kama maili 20 hivi nyuma ya Titanic kulikuwa na meli nyingine ikija-CALIFORIAN- ikazima injini zake,ikichelea kugonga milima ya barafu na kuvunjika kasha kuzama.
 Titanic waliziba masikio. Ni kawaida kwa Aprili na Mei baharini kuwa na milima ama mabonge ya barafu makubwa na marefu mno.
Mchanam saa 5:40 tayari Titanic ilikwishapinduka na ijini zake zilikwishaipeleka harijojo.
 Kulikuwa na meli nyingine(The White Star Line) ya kuratibu safari za Titanic ilikuwa ikikatisha bahari ya Atlantic,haikufua dafu ili kuzuia Titanic isizame,maana ilikuwa kwa maelekezo ya Freemasons.
 Angalia, abiria waliambiwa meli ilikuwa inazama,wakakataa kuingia katika boti za uokozi.Waliendelea kucheza muziki mtamu na kukamata ‘Kilaji’ tu, wengine walifunga ndoa humo-walipuuza onyo.
Niliwahi kuona Filamu moja kwamba kulikuwa na maharusi mle,mmoja akafa mwingine akanusurika, Titanic ilikuwa na starehe zote ndani, ndiyo maana watu walioambiwa wajiokoe wakakataa. Hawakuamini “Unsinkable” ingezama hata siku moja.
Wanaume walikataa kupanda boti za uokozi wakasema wanawake na watoto kama waliogopa basi wapande hizo boti, “Haitazama!’ walisisitiza.
Walisalia ndani ya meli hii hadi ilipozama kabisa vilindini,mashua zikajaa watu wengi,wao wakakosa nafasi hatimaye.
 Meli ya Uingereza, Carpathia,ilisikia mlio wa kuomba msaada ikarudi na kupita eneo lile la ajali.Iliokoa watu 712 tu waliokuwa katika zile mashua za TITANIC ILIYOKWISHAZAMA.
 Eneo la ajali hii ni karibu na Pwani ya New Foundland. Hii Titanic-white star-nyota nyeupe ilikuwa ya Uingereza,na ilizama kwa maelekezo ya Freemasons,kulikuwa na MATAJIRI ambao ilikuwa hapana budi wafe kama Freemasons walivyotaka,nahodha alipewa agizo. Sijui unaelewa?
 Meli hii inaacha simulizi, naomba mtafute habari zake, msinisumbue kwa maswali.Titanic inafananishwa na kuzama kwa dunia hii,watu wanaambiwa ajali inakuja,hawasikii ya wahubiri.
  Tazama Lukaa 21:35 utaona zama za Gharika ya Nuhu. Duniani kuna vita siku hizi Luka 21:9,10 na ni vita kuu ya dunia inayoongelewa hapa hadi Luka 21:11
 Isaya 24:19-20 husema dunia inavunjika. Dunia ina uzito wa tani 6,580,000,000,000,000,000,000!!
Hizi ni trilioni bilioni 6.6 hivi kipenyo chake nikama maili 7,926 Ikweta na 7,900 Ncha ya Kusini na Kaskazini. Biblia inasema dunia hii itaanguka imezidiwa uzito,uzito wa dhambi na mauaji ya kinyama na uhalifu na watu kupenda utajiri wa damu kama hao wanaoniomba niwaelekeze ofisi za Ibilisi!
  Hawa nao wataanguka katika hii The worst disaster of the 21st millennia. Tutapataje kupona? Tubuni dhambi, na UN wamtegemee Mungu.
0786 324 074