*Kulikuwa na Mkono
wa Freemasons katika Ajali ya Titanic
KILA palipo
na utajiri:Mafuta(Dhahabu Nyeusi), Almasi, Dhahabu zenyewe, pembe za ndovu na
faru,gesi n.k) aghalabu pana vita kali.
Katibu Mkuu
wa Pili wa Umoja wa Mataifa,Dk. Darg Hammarskjold wa Sweden, alifanya kazi
tangu Aprili 10 mwaka 1953 hadi Septemba 18 mwaka 1961 akafa.
Alikufa kwa
ajali ya ndege nchini Congo(JK Kongo) wakati wa maasi ya Shaba na Katanga. Nani
anachochea maasi Kongo? Hadi leo ni nusu karne, vita vinapamba moto Congo.
Shirika la
Ujasusi la Marekani(CIA) na washirika wake, walichochea vita na maasi huko
Shaba na Katanga(majimbo tajiri ya rasilimali) wakamkamata Mwanamapinduzi, Patrice
Emery Lumumba, na kumuulia mbali.
Lumumba,
alikuwa na visheni ya kijamaa, kutaka rasilimali za Congo ziwe kwa manufaa ya
Wakongo, rasilimali za Waafrika ziwe kwa ajili ya Waafrika wenyewe. Akawakosea
hawa majahili.
Wakawachochea akina Moise Tshombe, Joseph
Kasavubu,Joseph Desire Mobutu na vibaraka wengine, Lumumba akauliwa kinyama
Januari 17, mwaka 1961.
Dk. Darg Hammarskjold akasafiri kwa ndege
kutoka New York hadi Congo ili kusuluhisha vita, Septemba 18 mwaka 1961 akafa
eti kwa ajali ya ndege.
Nataka
nikwambie msomaji. Ajali za ndege zimewamaliza wanamapinduzi:Samora Moises
Machel, Kanali Dk.John Garang de Mabior, Juvenal Habiarimana na Cyprian
Ntarwamira,orodha ni ndefu.
Lumumba
alipokufa, akina Moise Tshombe na Mobutu wakatawala Congo ambayo waliita Zaire.
Congo ina
makabila zaidi ya 200, ni nchi yenye almasi,dhahabu,mbao za thamani,
fedha,uranium n.kWakaiba madini wee. Mobutu alipokufa huko Rabat,Morocco
Septemba, 1997, alikuwa kaficha Ulaya
Dola za Maremani milioni sita,utajiri sawa na deni la nje la Congo wakati huo.
Mobutu eti
alibadili jina na kuitwa Kuku wa Zabanga Mobutu Sese Seko, akaibadili Congo
kuwa Zaire,tukadhani mzalendo-kumbe kibaraka wa Wazungu aliyejificha katika
ngozi ya chui!
Penye rasilimali za thamani kama
mafuta,dhahabu,almasi, gesi,uranium n.k kuna vita,kuna vurugu. Penye bahari
kuu,milango bahari na mifereji kama Panama,Suez n.k kuna mivutano na vurugu za
mabeberu, ndiyo Libya,Misri,Nigeria,PANAMA nitaeleza mbele ya safari.
Bosnia Herzegovina, mwaka 1995 walikufa watu
200,000.Rwanda mwaka 1994 walikufa 800,000.Lakini, kwakuwa hakukuwa na
almasi,mafuta na dhahabu na pembe za faru na ndovu,hawakwenda mapema.
Walimsukumia
mzigo Boutros Boutros Ghali wa Misri,kwamba alishindwa kuchukua hatua alipokuwa
Katibu Mkuu wa UN. Wazungu na mwavuli wao wa NATO hawakwenda huko;kulikuwa na
kitu gani cha kurejesha gharama zao? Hata Hague hawakwenda huko.
Kwenye mafuta: Agosti mwaka 1990 Saddam
Hussein alipoivamia Kuwait,kwa sababu zile zile kama za Sudan Kusini na Sudan
leo za kuibiana mafuta, tayari UN wakaamrisha NATO na kuigilia kijeshi mzozo
huo.
Novemba 19900 hadi Januari 1991 tayari madege
ya vita ya Wazungu yalishanyesha mvua kubwa ya mabomu Irak, Saddam
akajisalimisha Aprili 1991.
Baadaye mwaka 2003, akapinduliwa na Bush
mtoto, maana ‘Bush Baba’ aliacha kiporo-Saddam alinyongwa kwa kamba nene
shingoni, 2006.
Mfereji wa
Panama(Panama Canal) ulisababisha Rais Manuel Noriega kupinduliwa na kutiwa
mbaroni na CIA utadhani kibaka,walisema alijihusisha na biashara haramu ya
mihadarati! Huwezi kushindana nao,ukapona!!
Ilikuwa Januari 1980 Noriega alipopinduliwa na
kufungwa pingu,kasha kufunguliwa kesi ya mihadarati.Marekani wakitaka kitu
Fulani,rais akijidai kujua anatiwa mbaroni, inatangazwa kwamba anauza madawa ya
kulevya, sasa utasemaje?
Salvador
Allende wa Chile, zlizingirwa na
CIA,akakubali kujipiga risasi na SMG yake aliyokuwa amepewa na rafikiye, Fidel
Alejandro Castro Ruz wa Cuba, wakamweka rafiki yao, nitaeleza kisa hiki siku
nyingine.
Kifo cha Laurent Desire Kabila,Januari 16 mwaka
2001 huko Kongo kina mkono wa hawa jamaa, Mafreemasons,Kabila alijidai mjanja,
wakatumia Body guard wake kumfyatua, hadi sasa Kongo hakuna amani,kuna akina
Bosco Ntaganda, sijui Thomas Lubanga na akina Jen. Nkunda ambao ukitazama
wanafungamana na Rwanda na Uganda hivi,kuna mahali mali ya Congo inavushwa.
Naam, Guns for natural resources! Kongo ni
nchi tajiri,maize ya kijani hayataki kuondoka. Mashirika ya Umoja wa Mataifa,
eti ya kulinda Amani(UN Peacekeeping Missions) wanapofika nchi yenye vita vya
rasilimali,hawalindi amani, wanakalia mahali kwenye dhahabu,almasi au mafuta na
gesi-basi wanapora!
Ziwe pembe
za ndovu au za faru, wanapora na kusafirisha njia za panya hadi kwao. UNAMSIL
huko Sierra Leone(Milima ya Simba) mwaka 99-2002 ndiyo biashara waliyofanya
huko,wakipora almasi za damu,mbao n.k
Congo,kuna MONUC ambao wakati Fulani wanakutwa
wakipora madini, wanaacha raia kushambuliwa na waasi nao kukimbilia Rwanda
huku, wao wanapora na kujitajirisha…(This is Africa)!
Huko Irak,
UNIKOM lazima wawe wanamiliki visima vya mafuta,wanaomba mabomu yaendelee,ili
muda wa kukaa huko uendelee,usishangae mabomu mengine wanalipua wao!
Huko Sahara Magharibi, MINURSO wapo wanataza
cha kupora ili watajirike! Unataka Utajiri? Uko Afrika, badala ya sisi wenyewe
kutumia rasilimali zetu kwa akili, tunagonganishwa vichwa kama makondoo
tu,kisingizio,utawala bora, demokrasia,rushwa,ufisadi…hatuwezi kuondoa haya
mpaka bunduki?
Wakimbizi, nalo ni ‘deal’ kwa mashirika kama
UNHCR,UNICEF,FAO,WFP hata ILO n.k. watauza hata mahema hhuko Dar na Mwanza
halafu wajenga mahekalu makubwa,ukiuliza unaambiwa, “jamaa yuko na UN Mission”
labda Juba hivi au Congo.
Vita
vina leta utajiri kwa watu wa Ulaya, wananeemeka sana, wanaomba maasi
yaendelee.
Nataka
kusema kwamba, amani hakuna. Mungu alishaacha kulinda amani. Tazama Ufunuo
7:1-3, Isaya 24:17-20 na Danieli 2: 43-45 uone kwamba kuna kila sababu kusema
ni SIKU ZA MWISHO.
Tujadili
kidogo kiporo chetu cha meli kubwa ya Titanic ILIYOZAMA huko Bahari ya
Atlantic.
Titanic, iliitwa “The Unsikable” kwa
sababu ilithibitishwa kutozama kwa namna
yoyote.
Basi,ilizama kwa sababu ya Ibilisi na maajenti
wake Freemasons.
Saa nne na dakika 20. Ni usiku wa manane wa
Aprili 15, mwaka 1912. Hukuwepo na mimi sikuwepo, wakati huo-imepita miaka 100
kamili. Titanic ilianza kupotelea katika mawimbi makali ya Atlantic.
Ilikuwa meli ya fahari sana kupita zote wakati
huo,iligonga Mlima wa Barafu,ikaanza kupoteza mwelekeo wake.
Jumla ya watu 1,503 hatimaye walikufa katika
ajali ile ya kihistoria, na kulikuwa na majeruhi wengi.
Ajali mbaya
zaidi ya meli duniani ni ya Feburuari 26,mwaka 1916 meli ya Provence ya
Kifaransa ilizama Mediterranean na kuuaa 3,100. Kwanini haikumbukwi? Hii nayo
‘cha mtoto’.Uchina waliwahi kufa watu 6,000 katika ajali ya meli mwaka
1948,lakini watu hawaambiwi haya,isipokuwa Titanic tu.
Meli hii Titanic Unsikable,ilikuwa na uzito wa
tani 46,500, ilianza kuzama polepole katika muda usiopungua saa tatu hivi.
Iliundwa imara sana,lakini ‘Unsikable’ ilizama na kukomesha kiburi cha watu cha
utajiri.
Ilikuwa na
kimo cha futi 883. Jioni, Aprili 14 mwaka huo 1912 meli hiyo ikiwa safarini
baharini Atlantic ilikuwa ikipasua mawimbi shwari kabisa.
Ilikuwa
ikienda jijini New York, Marekani na ilitokea Southampton,Uingereza. Meli hii
iliambiwa kwamba baharini kulikuwa na mabonge ya barafu, hawakusikia. Ni hapa
tunapoambiwa,Nahodha wa meli alipewa maelekezo kuwazamisha watu Fulani
waliokuwemo melini,kwa sababu ambazo wao Freemasons walizijua.
Kama maili 20 hivi nyuma ya Titanic kulikuwa
na meli nyingine ikija-CALIFORIAN- ikazima injini zake,ikichelea kugonga milima
ya barafu na kuvunjika kasha kuzama.
Titanic waliziba masikio. Ni kawaida kwa
Aprili na Mei baharini kuwa na milima ama mabonge ya barafu makubwa na marefu
mno.
Mchanam saa
5:40 tayari Titanic ilikwishapinduka na ijini zake zilikwishaipeleka harijojo.
Kulikuwa na meli nyingine(The White Star Line)
ya kuratibu safari za Titanic ilikuwa ikikatisha bahari ya Atlantic,haikufua
dafu ili kuzuia Titanic isizame,maana ilikuwa kwa maelekezo ya Freemasons.
Angalia, abiria waliambiwa meli ilikuwa
inazama,wakakataa kuingia katika boti za uokozi.Waliendelea kucheza muziki
mtamu na kukamata ‘Kilaji’ tu, wengine walifunga ndoa humo-walipuuza onyo.
Niliwahi
kuona Filamu moja kwamba kulikuwa na maharusi mle,mmoja akafa mwingine
akanusurika, Titanic ilikuwa na starehe zote ndani, ndiyo maana watu
walioambiwa wajiokoe wakakataa. Hawakuamini “Unsinkable” ingezama hata siku
moja.
Wanaume
walikataa kupanda boti za uokozi wakasema wanawake na watoto kama waliogopa
basi wapande hizo boti, “Haitazama!’ walisisitiza.
Walisalia
ndani ya meli hii hadi ilipozama kabisa vilindini,mashua zikajaa watu wengi,wao
wakakosa nafasi hatimaye.
Meli ya Uingereza, Carpathia,ilisikia mlio wa
kuomba msaada ikarudi na kupita eneo lile la ajali.Iliokoa watu 712 tu
waliokuwa katika zile mashua za TITANIC ILIYOKWISHAZAMA.
Eneo la ajali hii ni karibu na Pwani ya New
Foundland. Hii Titanic-white star-nyota nyeupe ilikuwa ya Uingereza,na ilizama
kwa maelekezo ya Freemasons,kulikuwa na MATAJIRI ambao ilikuwa hapana budi wafe
kama Freemasons walivyotaka,nahodha alipewa agizo. Sijui unaelewa?
Meli hii inaacha simulizi, naomba mtafute
habari zake, msinisumbue kwa maswali.Titanic inafananishwa na kuzama kwa dunia
hii,watu wanaambiwa ajali inakuja,hawasikii ya wahubiri.
Tazama
Lukaa 21:35 utaona zama za Gharika ya Nuhu. Duniani kuna vita siku hizi Luka
21:9,10 na ni vita kuu ya dunia inayoongelewa hapa hadi Luka 21:11
Isaya 24:19-20 husema dunia inavunjika. Dunia
ina uzito wa tani 6,580,000,000,000,000,000,000!!
Hizi ni
trilioni bilioni 6.6 hivi kipenyo chake nikama maili 7,926 Ikweta na 7,900 Ncha
ya Kusini na Kaskazini. Biblia inasema dunia hii itaanguka imezidiwa
uzito,uzito wa dhambi na mauaji ya kinyama na uhalifu na watu kupenda utajiri
wa damu kama hao wanaoniomba niwaelekeze ofisi za Ibilisi!
Hawa nao
wataanguka katika hii The worst disaster of the 21st millennia. Tutapataje
kupona? Tubuni dhambi, na UN wamtegemee Mungu.
0786 324 074
No comments:
Post a Comment