TUREJEE kidogo katika somo la Kuzama kwa Meli ya Titanic.
Kwamba, ilizama kwa maelekezo ya Freemasons. Nahodha wa Meli
ya Titanic, E.J.Smith, alielekezwa kuizamisha meli ili kuwaulia mbali matajiri
waliokuwemo.
Mhariri wa Makala wa Gazeti hili, Markus Mpangala,Mei 22
mwaka huu akawataja matajiri hawa walioangamia katika ajali hiyo kwamba ni John
Jacob Astor,Archibald W.Butt,Charles M. Hayes,na mkewe na binzi zao,
W.T.Stead,Benjamin Guggenheim, F.D.Millett na G.D.Widher.
Wengine walioangamia ni Isidor Strauss, na mkewe,J.B Thayer,J,Bruce
Ismay,Henry B. Harris na mkewe na Washington A.Roebling.
Sina haja ya kulumbana na mtu kwamba Freemasons ambao
kimsingi ni mawakala wa Ibilisi hawasababishi ama wanasababisha kutokea kwa
majanga. Sote tunajua kuna nguvu mbili zinazoshindana duniani, nguvu ya wema na
ile ya kufanya mabaya. Freemasons ni mawakala wa Ibilisi wenye kazi maalum ya
kuhadaa watu,wakidhani wanafanya mema.
Hata hivyo, Alex
Mayoge wa Moshi,Kilimanjaro aliniandikia SMS kusema kwamba TITANIC ILIZAMA ili
kuwaua matajiri hao ili Freemasons wapore fedha zao kwenda kugharimia VITA VYA
KWANZA VYA DUNIA.
Titanic ilizama Aprili 1912 na ni miaka miwili baadaye,mwaka
1914 vita kuu ya kwanza ya Dunia ikaanza kwaka 1914.
Vita vila lengo Fulani,
na aghalafu vita wanavyoanzisha Freemasons ni vya kupora rasilimali ama kuweka
mamlaka yao mahali wanapopingwa,nguvu za ushawishi zinaposhindikana.
Vita vya Pili vilianza 1939 vikakoma 1954. Tulishajadili
jambo hili kwa kina,na anayetaka aangalie Blog yangu kuhusu vita hivi na
matokeo yake.
Malengo ya maharamia hawa yangalipo duniani,ndiyo maana kuna
vita leo Congo na maeneo mengine kama Sierra Leone, tuliona Revolutionary
United Front wakipewa silaha kuharibu serikali ya mjini Freetown,ili wapore
ALMASI ZA DAMU.
Mwisho wa siku Fodday Sankoh alikamatwa na kupelekwa The
Hague ambako eti alifariki ama kunyamazishwa, leo niandikapo hapa Taylor
anahukumiwa kifungo cha miaka mingi huko jijini London,Uingereza?
Soma tamthilia hii kama kichekesho tu(Satire) cha
Taylor huko Mahakamani Hague, dhidi ya wakubwa.
CHARLES TAYLOR 64 + 80
ASKARI:
Koooortiiiii?
(Mahakama ya Umoja wa
Mataifa,ICC,inaanza kikao chake, ‘session’ mjini The Hague, Uholanzi.
Washitakiwa, maofisa wa
Mahakama wanaingia,na watu wote ndani ya mahakama hiyo wanasimama wakati
wa majaji kuingia kortini, ambamo Taylor anashitakiwa kwa makosa 11 ya uhalifu
wa kivita huko Sierra Leone tangu 1991 hadi 2002, akiwasaidia United
Revolutionary Front).
KARANI:
Charles Ghankay Taylor
dhidi ya Haki za Binadamu?
TAYLOR: Timamu,
Mheshimiwa Jaji, Lussick. Hata hivyo nashangaa,katika kesi hii washitakiwa
wenzangu, akina mabwana George W.Bush na Tony Blair wameachwa. Haidhuru!
Nimamaizi Mheshimiwa Jaji, mahakama hii ya ICC hapa Hague ina makengeza!
JAJI LUSSICK:
Mwendesha Mashitaka una hoja?
MWENDESHA MASHITAKA: Mshitakiwa aliwafadhili
Waasi wa RUF walipoua watu huko Sierra Leone, akawatumikisha watoto maelfu
jeshini kwa muda wa miaka 11; naye ana makosa 11.
JAJI LUSSICK: Mshitakiwa, Charles
Taylor,Rais wa zamani wa Liberia, unapaswa kuieleza mahakama hii tukufu, una
maanisha nini kusema mahakama ina makengeza? Mahakama ina macho?
(kicheko cha kwikwi
toka kwa wasikilizaji)
TAYLOR: Mheshimiwa, sina maana kwamba
mahakama ni kipofu; ila ina makengeza! Haina macho, mahakama ina ‘double
standards’ yaani upendeleo, haiwaoni Wazungu tuliosaidiana nao kuwafadhili
United Revolutionary Front(RUF) ili wapore ALMASI ZA DAMU ili ‘deal’ hii itupe
utajiri? Sasa mheshimiwa, kazi tumefanya wote na akina Bush na Blair, eti ‘zengwe’
nasukumiwa mimi peke yangu. Hiyo noma Mheshimiwa!
JAJI LUSSICK: Okay! Okay! Nimekupata Mr. Taylor,
ohh..samahani, Mr. X-President! Hata hivyo hujakana shitaka lolote kati ya haya
11 unayokabiliwa nayo?
TAYLOR: Nikanushe nini
Mheshimiwa wakati mlikwishaamua kunitosa?
JAJI LUSSICK: Tumuulize Mwendesha Mashitaka
Mkuu,Louis Mareno-Ocampo. Kwanini Taylor? Why Taylor, and why not Wazungu in
this TRIAL?
OCAMPO:
Mheshimiwa Jaji,Lussick,
Rais Mstaafu wa Liberia, Bwana Caharles Taylor alishatakiwa na wenzake kama
Fodday Sankoh,kiongozi wa RUF.
TAYLOR: Mheshimiwa, nataka Ocampo aieleze hii
mahakama ya Fisi ambako mimi Mbuzi leo nasulubiwa kinyama! ‘Poppy’ Sankoh ni
mshitakiwa namba ngapi katika kesi hii?
OCAMPO:
Sankoh hayupo hapa mahakamani. Kama mahakama inakumbuka, alifariki akiwa
rumande hapa mjini Hague.Waasi wengine wakikamatwa upelelezi ukikamilika nao
tutawashitaki, hakuna ‘impunity’ kwa mkosaji yeyote.
TAYLOR: Mheshimiwa, inakuingia kichwani kwamba mimi peke
yangu ningeweza kufadhili RUF kuua watu,kubaka,kukata raia viungo na kupeleka
watoto 200,000 vitani,kama siyo msaada wa Bush,Blair na ‘Wadosi’ wengine wa
huku ‘majuu’ mheshimiwa, kama siyo kunionea?
JAJI:
Swali
jingine?
TAYLOR:
Mimi peke yangu
ningewezaje kumpa Poppy Sankoh ‘shavu’ kwa miaka thenashara, hadi akombe ALMASI
ZA DAMU Sierra Leone? Eti wanasema mjini Johannesburg nilimhonga yule kimwana,
Naomi Campbell bonge la almasi ghafi. Hizo almasi nilizipataje na nilikuwa
namuuzia nani, Mzungu au Mwafrika,Mweupe au mfupi, mnene au kimbaumbau? Ebo!
Noma mheshimiwa!!
(kicheko cha kwikwi
kutoka kwa wasikilizaji mahakamani)
BRENDA HOLLIS: Taylor na Sankoh
walishirikiana kufanya uhalifu Sierra Leone,KWA MTUTU WA BUNDUKI, walipora
almasi za damu na kuziuza kwa wateja wao Ulaya na Marekani
TAYLOR:
Tena huyu Brenda
Hollis,Mwendesha Mashitaka ni mpuuzi kabisa, afadhali Ocampo, tuliua watu kwa
bunduki? Umesikia Liberia kulikuwa na kiwanda cha bunduki kama AK 47?
OCAMPO: (anasimama) Mheshimiwa Jaji, ALMASI ZA
DAMU zilisafirishwa kwa magendo hadi Afrika Kusini hadi Ulaya na Marekani
ambako walibadilishana na Wazungu kwa almasi kwa bunduki yaani Guns for
Diamonds mheshimiwa!
TAYLOR: Basi poa, Mheshimiwa Jaji, sasa
wanataka mimi nikanushe nini kama hata wao wanajua Mzungu alifanya vikao vya
G-8 vya kinafiki huko Antwerp, kukataza biashara ya almasi za damu,kumbe naye
alizimaindi?
JAJI:
kama sijakosea, swali la mshitakiwa ni kwamba, kwa nini upande wa
mashitaka haujawaleta mahakamani walionunua almasi za damu toka Sierra
Leone,badala yake wamewaleta wauzaji peke yao?
TAYLOR: Hewaa! Jaji,kumbe hukusoma mwembeni na kupata
digrii za ‘madensa’ ila umebukua sheria! Umenipata! Huyu Ocampo kwao ni Buenos
Aires, Argentina, sasa ni kibaraka wa Mzungu wa Ulaya hajui EU walipora almasi
za damu licha ya sheria kupiga marufuku biashara hiyo, halafu anatukamata
Waafrika tu! Wapi Wazungu hapa bwana? Hiyo siyo ‘Fair Play’ ni Unfair kabisa,
Noma msikaji!!
(minong’ono na
miguno inasikika mahakamani)
OCAMPO: Waheshimiwa Jopo la Majaji,
mshitakiwa athibitishe kauli yake kama ICC inawashitaki Waafrika tu,na aslani
hakuna Mzungu hata mmoja! Hiki siyo chombo cha Umoja wa Mataifa(UN) na nchi 54
za Afrika hazijaridhia Mahakama hii tukufu?
TAYLOR:
Hawa mabwana wanatutuma kazi,tunatesa raia,tunakwiba
rasilimali na fursa zao nyingi,ili Punda afe Mzigo ufike! Halafu baadaye
wakitosheka wanaanza kutuchonganisha na raia na maandamano kama walivyofanya
Libya,Misri kwa Mubarak,Tunisia kwa Ben Ali n.k Je huu ni uungwana Mheshimiwa?
Tunapora nchi zetu kwa ufisadi na kuleta mzigo halafu kisha wanatusaliti! Huu
siyo uungwana mheshimiwa!
JAJI: Hujaitajia
mahakama Waafrika wangapi wamekamatwa peke yao na kushitakiwa The Hague?
TAYLOR: Mimi
ningali Rais halali wa Liberia, huyo Hellen Johnson Sielief, wamemleta wao ili
atawale kisha mimi waninyonge! Wanasema hakuna ‘Impunity’ wakati Blair,Bush
wanavamia na kuua hakuna mashitaka! Mnataka nife kama Gaddafi na Saddam?
JAJI: Enhe, wewe
na wengine kina nani? Wataje mlioshirikiana kuua raia mkapora utajiri wa Afrika
na kuuficha Ulaya na Marekani.
TAYLOR: Simple,
Fodday Sankoh, Laurent Nkundabatware, Jean-Pierre Bemba, Laurent Gbagbo, hawa
‘Ocampo Six’ mmewaacha mkachagua ‘Ocampo Four’, halafu mnamtaka Omar Hassan Al
Bashir, Tomas Lubanga,Joseph Kony,Paschal Ntaganda.
JAJI:
Umemaliza?
TAYLOR: Mobutu,
Savimbi,mbona hamsemi mliwasaidia hawa kupora utajiri wa Afrika na kuuhamishia
Ulaya na Marekani sasa Afrika ni The Shame of poverty in Plentiful?
OCAMPO:
Mheshimiwa,huyu jamaa sijui hamnazo, au kachapa kilaji! Amesahau Slobodan
Milosevic wa Serbia naye alishakamatwa mwaka 2000? Atasemaje kwamba
tunawakamata Waafrika tu?
TAYLOR: Mimi siyo
mlevi,ninakupa ‘facts’ usianze chuki zenu hapa. Mimi ni Rais halali Liberia
wananchi wananipenda, Marekani wamenitumia nikapora almasi za damu na
kuwapelekea,sasa wanasema mimi
muuaji. Guns for
Diamond ningefanyaje miaka 11 bila kushirikiana nao? Wazungu, acheni kufikiri
Mwafrika zoba, hamnazo?
(kicheko mahakamani,
zinasikika kelele za mashabiki wake nje ya mahakama wakishangilia)
JAJI: Order! Hapa tuko mahakamani,hatupo baa!
Utulivu tafadhali! Enhe, Taylor endelea kuuliza swali kama unalo; lakini wewe
siyo among the wealthiest in the world?
TAYLOR:
Umbeya tu mheshimiwa. Hawa wanatuchonganisha na wananchi wetu halafu wanasanua
deal kwa mitandao yao kama weakleaks, wanachochea maandamano kwa facebook na
twitter
OCAMPO: Kwani Wazungu
hawakamatwi?
TAYLOR: Baada ya Adolf
Hittler baada ya Vita ya Pili ya dunia nani aliyehukumiwa Hague,kama siyo mimi
mnataka kunionea eti nifungwe miaka 80,sasa nina 64, ndiyo nini kama siyo
kuniziba mdomo nisiseme mlivyopora ALMASI ZA DAMU huko Kono, Sierra Leone? Eti
mnataka kunifunga Uingereza!!
JAJI: Hoja
yako ni ipi hapa?
TAYLOR:
Ukiacha wale NAZIS, hawa jamaa ni matapeli hawajamkamata Mzungu,
wanatukamata sisi Waafrika tu, wana ‘double standards’ mheshimiwa Jaji na mambo
haya hapa siyo kesi ni siasa tupu-This massive inequality can be traced back to
cold war politics!!Sikubaliani na ukoloni wa ICC,WALA hakuna human rights wala
transparency international wala nini!!
JAJI: Wakili wa
mshitakiwa una swali?
WAKILI: Taylor, kina
nani wengine wanaonewa na ICC?
Taylor: Hata
mashirika ya wakimbizi na mengine ya Umoja wa Mataifa Congo,Dafur, Sierra Leone
n.k wizi mtupu, dunia haina amani ni utapeli tu,vita wachochee wao,tushitakiwe
sisi akina Taylor, Mobutu Sseseseko,Jonas Savimbi, Bosco Ntaganda,Thomas
Lubanga,Jonas Kony,orodha ni ndefu mheshimiwa! Hawa wote husaidiwa na Wazungu
kuharibu amani,uchumi na usalama wa Afrika,halafu hugeuka chameleon?
(anainamisha kichwa
kuonesha ameridhika, anaketi)
JAJI: Badala
ya kukanusha mashitaka unalalamika sana kwamba umeonewa,kwamba ICC
inawaonea Waafrika tu. Mahakama imeona una hatia ya mashitaka yote thenashara!
Upande wa Mashitaka una hoja?
BREBDA HOLLIS:
Huyu jamaa afungwe miaka 80, ukijumlishe umri wake wa miaka
64 maana yake ni kwamba afie ‘nondo’ ama mangenge ili liwe fundisho kwa
‘masera’ wenzake wanaoua raia!
JAJI:
Hukumu KAMILI Mei 30 mwaka huu 2012.
ASKARI:
Kooooortiii!!
Mei 30, magazeti ya Tanzania yanaandika, “Taylor
anyeshewa mvua ya miaka 80 jela!” mara, ‘Taylor kunyea mtondoo!”
TAMATI
0786 324 074 ama
www.congesmrambatoday.com
No comments:
Post a Comment