ASKARI: Koooortiiiii?
(Mahakama ya Umoja wa Mataifa,ICC,inaanza kikao chake,
‘session’ mjini The Hague, Uholanzi.Washitakiwa, maofisa wa Mahakama
wanaingia,na watu wote ndani ya mahakama
hiyo wanasimama wakati wa majaji kuingia kortini, ambamo Taylor anashitakiwa
kwa makosa 11 ya uhalifu wa kivita huko Sierra Leone tangu 1991 hadi 2002,
akiwasaidia United Revolutionary Front).
KARANI: Charles Ghankay Taylor dhidi ya Haki za Binadamu?
TAYLOR:
Timamu, Mheshimiwa Jaji, Lussick. Hata hivyo nashangaa,katika kesi hii
washitakiwa wenzangu, akina mabwana George W.Bush na Tony Blair wameachwa.
Haidhuru! Nimamaizi Mheshimiwa Jaji, mahakama hii ya ICC hapa Hague ina
makengeza!
JAJI LUSSICK:
Mwendesha Mashitaka una hoja?
MWENDESHA MASHITAKA: Mshitakiwa aliwafadhili Waasi wa RUF
walipoua watu huko Sierra Leone, akawatumikisha watoto maelfu jeshini kwa muda
wa miaka 11; naye ana makosa 11.
JAJI LUSSICK: Mshitakiwa, Charles Taylor,Rais wa zamani wa
Liberia, unapaswa kuieleza mahakama hii tukufu, una maanisha nini kusema
mahakama ina makengeza? Mahakama ina macho?
(kicheko cha kwikwi toka kwa wasikilizaji)
TAYLOR:
Mheshimiwa, sina maana kwamba mahakama ni kipofu; ila ina makengeza!
Haina macho, mahakama ina ‘double standards’ yaani upendeleo, haiwaoni Wazungu
tuliosaidiana nao kuwafadhili United Revolutionary Front(RUF) ili wapore ALMASI
ZA DAMU ili ‘deal’ hii itupe utajiri? Sasa mheshimiwa, kazi tumefanya wote na
akina Bush na Blair, eti zengwe nasukumiwa mimi peke yangu. Hiyo noma
Mheshimiwa!
JAJI LUSSICK: Okay! Okay! Nimekupata Mr. Taylor,
ohh..samahani, Mr. X-President! Hata hivyo hujakana shitaka lolote kati ya haya
11 unayokabiliwa nayo?
TAYLOR:
Nikanushe nini Mheshimiwa wakati mlikwishaamua kunitosa?
JAJI LUSSICK: Tumuulize Mwendesha Mashitaka Mkuu,Louis
Mareno-Ocampo. Kwanini Taylor? Why Taylor, and why not Wazungu in this TRIAL?
OCAMPO: Mheshimiwa Jaji,Lussick, Rais Mstaafu wa Liberia, Bwana
Caharles Taylor alishatakiwa na wenzake kama Fodday Sankoh,kiongozi wa RUF.
TAYLOR: Mheshimiwa, nataka
Ocampo aieleze hii mahakama ya Fisi ambako mimi Mbuzi leo nasulubiwa kinyama! ‘Poppy’
Sankoh ni mshitakiwa namba ngapi katika kesi hii?
OCAMPO:
Sankoh hayupo hapa mahakamani. Kama mahakama inakumbuka, alifariki akiwa rumande
hapa mjini Hague.Waasi wengine wakikamatwa upelelezi ukikamilika nao
tutawashitaki, hakuna ‘impunity’ kwa mkosaji yeyote.
TAYLOR: Mheshimiwa, inakuingia kichwani kwamba mimi peke yangu
ningeweza kufadhili RUF kuua watu,kubaka,kukata raia viungo na kupeleka watoto
200,000 vitani,kama siyo msaada wa Bush,Blair na ‘Wadosi’ wengine wa huku ‘majuu’
mheshimiwa, kama siyo kunionea?
JAJI:
Swali jingine?
TAYLOR: Mimi peke yangu ningewezaje kumpa Poppy Sankoh ‘shavu’ kwa
miaka thenashara, hadi akombe ALMASI ZA DAMU Sierra Leone? Eti wanasema mjini
Johannesburg nilimhonga yule kimwana, Naomi Campbell bonge la almasi ghafi.
Hizo almasi nilizipataje na nilikuwa namuuzia nani, Mzungu au Mwafrika,Mweupe
au mfupi, mnene au kimbaumbau? Ebo! Noma mheshimiwa!!
(kicheko cha kwikwi kutoka kwa wasikilizaji
mahakamani)
BRENDA HOLLIS:
Taylor na Sankoh walishirikiana kufanya uhalifu Sierra Leone,KWA MTUTU
WA BUNDUKI, walipora almasi za damu na kuziuza kwa wateja wao Ulaya na Marekani
TAYLOR: Tena huyu Brenda Hollis,Mwendesha
Mashitaka ni mpuuzi kabisa, afadhali Ocampo, tuliua watu kwa bunduki? Umesikia
Liberia kulikuwa na kiwanda cha bunduki kama AK 47?
OCAMPO: (anasimama)
Mheshimiwa Jaji, ALMASI ZA DAMU zilisafirishwa kwa magendo hadi Afrika Kusini
hadi Ulaya na Marekani ambako walibadilishana na Wazungu kwa almasi kwa bunduki
yaani Guns for Diamonds mheshimiwa!
TAYLOR: Basi poa, Mheshimiwa
Jaji, sasa wanataka mimi nikanushe nini kama hata wao wanajua Mzungu alifanya
vikao vya G-8 vya kinafiki huko Antwerp, kukataza biashara ya almasi za
damu,kumbe naye alizimaindi?
JAJI: kama sijakosea, swali la mshitakiwa ni kwamba,
kwa nini upande wa mashitaka haujawaleta mahakamani walionunua almasi za damu
toka Sierra Leone,badala yake wamewaleta wauzaji peke yao?
TAYLOR: Hewaa! Jaji,kumbe hukusoma mwembeni na kupata digrii za ‘madensa’
ila umebukua sheria! Umenipata! Huyu Ocampo kwao ni Buenos Aires, Argentina,
sasa ni kibaraka wa Mzungu wa Ulaya hajui EU walipora almasi za damu licha ya
sheria kupiga marufuku biashara hiyo, halafu anatukamata Waafrika tu! Wapi
Wazungu hapa bwana? Hiyo siyo ‘Fair Play’ ni Unfair kabisa, Noma msikaji!!
(minong’ono
na miguno inasikika mahakamani)
OCAMPO:
Waheshimiwa Jopo la Majaji,
mshitakiwa athibitishe kauli yake kama ICC inawashitaki Waafrika tu,na aslani
hakuna Mzungu hata mmoja! Hiki siyo chombo cha Umoja wa Mataifa(UN) na nchi 54
za Afrika hazijaridhia Mahakama hii
tukufu?
TAYLOR: Hawa mabwana wanatutuma kazi,tunatesa
raia,tunakwiba rasilimali na fursa zao nyingi,ili Punda afe Mzigo ufike! Halafu
baadaye wakitosheka wanaanza kutuchonganisha na raia na maandamano kama
walivyofanya Libya,Misri kwa Mubarak,Tunisia kwa Ben Ali n.k Je huu ni uungwana
Mheshimiwa? Tunapora nchi zetu kwa ufisadi na kuleta mzigo halafu kisha
wanatusaliti! Huu siyo uungwana mheshimiwa!
JAJI: Hujaitajia
mahakama Waafrika wangapi wamekamatwa peke yao na kushitakiwa The Hague?
TAYLOR: Mimi ningali Rais halali wa Liberia, huyo
Hellen Johnson Sielief, wamemleta wao ili atawale kisha mimi waninyonge!
Wanasema hakuna ‘Impunity’ wakati Blair,Bush wanavamia na kuua hakuna mashitaka!
Mnataka nife kama Gaddafi na Saddam?
JAJI: Enhe, wewe na wengine kina nani? Wataje
mlioshirikiana kuua raia mkapora utajiri wa Afrika na kuuficha Ulaya na
Marekani.
TAYLOR: Simple, Fodday Sankoh, Laurent
Nkundabatware, Jean-Pierre Bemba, Laurent Gbagbo, hawa ‘Ocampo Six’ mmewaacha
mkachagua ‘Ocampo Four’, halafu mnamtaka Omar Hassan Al Bashir, Tomas
Lubanga,Joseph Kony,Paschal Ntaganda.
JAJI: Umemaliza?
TAYLOR: Mobutu,
Savimbi,mbona hamsemi mliwasaidia hawa kupora utajiri wa Afrika na kuuhamishia
Ulaya na Marekani sasa Afrika ni The Shame of poverty in Plentiful?
OCAMPO: Mheshimiwa,huyu jamaa sijui hamnazo, au
kachapa kilaji! Amesahau Slobodan Milosevic wa Serbia naye alishakamatwa mwaka
2000? Atasemaje kwamba tunawakamata Waafrika tu?
TAYLOR: Mimi
siyo mlevi,ninakupa ‘facts’ usianze chuki zenu hapa. Mimi ni Rais halali
Liberia wananchi wananipenda, Marekani wamenitumia nikapora almasi za damu na
kuwapelekea,sasa wanasema mimi
muuaji. Guns for Diamond ningefanyaje miaka 11
bila kushirikiana nao? Wazungu, acheni kufikiri Mwafrika zoba, hamnazo?
(kicheko mahakamani, zinasikika kelele za
mashabiki wake nje ya mahakama wakishangilia)
JAJI: Order! Hapa tuko mahakamani,hatupo baa! Utulivu
tafadhali! Enhe, Taylor endelea kuuliza swali kama unalo; lakini wewe siyo
among the wealthiest in the world?
TAYLOR: Umbeya tu mheshimiwa. Hawa wanatuchonganisha
na wananchi wetu halafu wanasanua deal kwa mitandao yao kama weakleaks,
wanachochea maandamano kwa facebook na twitter
OCAMPO: Kwani
Wazungu hawakamatwi?
TAYLOR: Baada
ya Adolf Hittler baada ya Vita ya Pili ya dunia nani aliyehukumiwa Hague,kama
siyo mimi mnataka kunionea eti nifungwe miaka 80,sasa nina 64, ndiyo nini kama
siyo kuniziba mdomo nisiseme mlivyopora ALMASI ZA DAMU huko Kono, Sierra Leone?
Eti mnataka kunifunga Uingereza!!
JAJI: Hoja
yako ni ipi hapa?
TAYLOR: Ukiacha
wale NAZIS, hawa jamaa ni matapeli hawajamkamata Mzungu, wanatukamata sisi
Waafrika tu, wana ‘double standards’ mheshimiwa Jaji na mambo haya hapa siyo
kesi ni siasa tupu-This massive inequality can be traced back to cold war
politics!!Sikubaliani na ukoloni wa ICC,WALA hakuna human rights wala
transparency international wala nini!!
JAJI: Wakili wa mshitakiwa una swali?
WAKILI: Taylor,
kina nani wengine wanaonewa na ICC?
Taylor: Hata mashirika ya wakimbizi na mengine ya
Umoja wa Mataifa Congo,Dafur, Sierra Leone n.k wizi mtupu, dunia haina amani ni
utapeli tu,vita wachochee wao,tushitakiwe sisi akina Taylor, Mobutu
Sseseseko,Jonas Savimbi, Bosco Ntaganda,Thomas Lubanga,Jonas Kony,orodha ni
ndefu mheshimiwa! Hawa wote husaidiwa na Wazungu kuharibu amani,uchumi na
usalama wa Afrika,halafu hugeuka chameleon?
(anainamisha kichwa kuonesha ameridhika,
anaketi)
JAJI: Badala
ya kukanusha mashitaka unalalamika sana
kwamba umeonewa,kwamba ICC inawaonea Waafrika tu. Mahakama imeona una hatia ya
mashitaka yote thenashara! Upande wa Mashitaka una hoja?
BREBDA
HOLLIS: Huyu jamaa afungwe miaka 80, ukijumlishe umri
wake wa miaka 64 maana yake ni kwamba afie ‘nondo’ ama mangenge ili liwe
fundisho kwa ‘masera’ wenzake wanaoua raia!
JAJI: Hukumu KAMILI Mei 30 mwaka huu 2012.
ASKARI: Kooooortiii!!
TAMATI
No comments:
Post a Comment