Thursday, May 31, 2012

Mwanamke wa Ufunuo 17 ni Kanisa la Rumi



    TUWEKE kumbukumbu zetu makini zaidi.
 Feburuari 26 mwaka 2009,William Shao aliandika katika Gazeti la Rai,kwamba mwanamke anayefanana na Yule wa Ufunuo wa Yohana 17:3-11, amejemgewa sanamu mbele ya Jengo la Bunge la Umoja wa Ulaya, huko Brussels,Ubelgiji.
Shao, alienda mbali zaidi kusema, hata jingo lenyewe la Bunge la Ulaya(EU) mjini Brussels, halina tofauti sana taswira yake na Mnara wa Babeli.

Shao, anasema sanamu ya mwanmke aliyeketi juu ya mnyama mbele ya ofisi za Bunge la Ulaya, haikuwekwa kwa bahati mbaya; inatafsiri jambo fulani muhimu wewe kuelewa.                     

 Ulaya, ilikuwa himaya ya Dola ya Rumi; na Mwanamke huyo wa mjini Brussels anayeitwa, “Europa Goddes” ni mungu mke wa Ulaya.
 Naam, mungu jike wa Ulaya ndiye mtawala wa Ulaya na makoloni yake duniani, na mji anaoketi huitwa kwa Jina la Siri, “Babeli” Ufunuo 17:5!!
Umeona picha ya mnara wa Babeli? Ni kama alivyosema mwandishi William Shao,kwamba inafanana sana na jingo la Bunge huko la Ulaya huko mjini Brussels, Ubelgiji.
‘Uropa Goddes’-mungu jike wa Ulaya,hufananishwa na jiji la kale sana Babeli ambayo ni Irak ya siku hizi.
 Kulingana na Biblia, mwanamke katika Unabii ni kundi la waabuduo-kanisa, waumini. Kuna wanawake wawili katika Ufunuo wa Yohana, Ufunuo 12 na 17; moja huwakilisha kundi nyoofu katika maadili ya kidini na, mwanamke wa Ufunuo 17 ni kundi kengeufu linalojichanganya na waabudu sanamu, anasa za dunia na uchafu wa kiroho.
Katika Hosea 2:10,Yeremia 3:14 na 2Korintho 11:2 uhusiano baina ya Mungu Mwenyezi na Kanisa lake hufananishwa na uhusiano wa ndoa,kati ya mume na mke.
Katika Ufunuo 21:2 mji wa Yerusalem umefananishwa na ‘Bibi Harusi’ yaani mwanamke safi. Kanisa la Mungu linapoungana na dunia na anasa na kuabudu sanamu, hufananishwa na UZINZI(Tazama Yakobo 4:4).
Naam, Yakobo anawaita watu wa Mungu waliomwacha na kuungana na Dunia ya dhambi kwamba ni Wazinzi, waasherati, makahaba!
 Ni hapa, tunapomaizi kwamba mwanamke wa Ufunuo 17:3 ambaye ni “mungu-jike wa Ulaya” ni Kanisa la Mungu lililoungana na Dunia na mivuto yake na anasa zake na kumwacha Mungu.
Anasa,ulevi,falsafa,ibada ya sanamu na miungu,ushoga,ulawiti hata wa watoto chekechea n.k
Mavazi ya ‘Mwanamke’ huyo ni rangi nyekundu na zambarau, ambayo yalivaliwa na makuhani wa miungu huko Babeli ya kale.
 Hawa ni kundi tajiri wenye madini,vito vya thamani na urembo ambalo linamvuto mkubwa kwa Wafalme wa Dunia. Kanisa hilo linasemwa kutawala miongoni mwa wafalme wa dunia(Marais, Mawaziri Wakuu,Wafalme n.k) yaani hubebwa na watawala wa Umoja wa Ulaya huko mjini Brussels(Tazama Ufunuo wa Yohana 17:4-6).
Muungano haramu wa Kanisa la Mungu na viongozi wa dunia(uzinzi) ndiyo kuungana kufanya yaliyo kinyume na Amri 10 za Mungu. Kuungana na upagani, kuabudu sanamu na miungu kama jua, sayari,nyota na mwezi.
Mwanamke wa mjini Brussels anao watoto wake nao ni ‘Makahaba’ yaani wazinzi wa kiroho.
Sasa, tutazame kwa makini; kama mji wa Brussels mwaka 96 AD wakati Mtume Yohana anaandika kitabu cha Ufunuo,ulikuwepo? Hasha!!
 Nchi nzima ya Ubelgiji ina watu wasiozidi milioni 12. Brussels siku hizi una wakazi milioni 1.5 tu.
Tuutafute mji wa kale sana Ulaya, ambao Yohana aliuita jina la mafumbo Babeli. Umejengwa juu ya milima saba(ufunuo 17:9).
 Mwaka 753 BC mji uliojengwa Ulaya ni Rome. Hata London haukuwepo, Uingereza ilikuwa kijiji kidogo mwaka 1000 AD. Hata mwaka 500 BC Rome lilikuwa jiji tena “SUPER POWER” Duniani, ulijengwa na Romulus.
 Katika mji huu ndiko yaliko mamlaka ya kidini,Vatican. Unaposema Vatican unasema kanisa la Mungu. Vatican imekuwa nchi Feburuari 11, mwaka 1929 zama za Benito Mussolini.
Habari zinazovuja(hata BBC wametangaza Jumatano iliyopita) kwamba kuna njama za mapinduzi baridi na mchakato wa kumsimika Papa mpya badala ya Benedict XVI.
Rome ni mahali ambapo wameishi ma-Baba Watakatifu(Popes) wa Katoliki wapatao 302. Mji huu ulikuwa makao makuu ya dola ya Rumi, hata zama za Yesu,mitume na zama za Biblia Takatifu yaani kati ya mwaka BC 1500 ZAMA ZA MUSA Hadi 96 AD alipofariki Yohana wa Patmo.
 Nataka msomaji atambue kwamba, waandishi wa Biblia waliposema Babeli,baada ya kuanguka kwa mji wa Babeli, walimaanisha MJI WA ROME(Isaya 21:9).
Fahari yake na ulikuwa mji mkuu wa biashara duniani. Kanisa Katoliki linadai Petro aliyefika mjini Rome mwaka 42 AD na akauliwa na Kaisari Nero Mkatili, mwaka AD 67,ndiye Papa wa Kwanza kwa Kanisa hilo.
 Tuwatazame mapapa. Huchaguliwa na Makadinari kama 131 hivi. Papa Benedict XVI yeye alichaguliwa na Makadinali 117, ambao hawakuwa na umri wa miaka 80. Papa ni Mwakilishi wa Yesu,mrithi wa Mtume Petro,Mkuu wa Mitume wote duniani,Papa ni Mamlaka na nguvu-Tazama Danieli 7:25.
 Rome, ni mahali Kanisa la Mt.Petro lilipojengwa juu ya Kanisa la Petro; linaitwa, St.Peter’s Basilica. Limejengwa KATIKA ENEO LA EKARI SITA.
Hili kanisa, St. Peter’s Basilica, lina urefu wa futi 700 na upana ni futi 450 na linaweza kuchukua watu 80,000 kwa wakati mmoja.
Rome ni jiji lililopo nyuzi sawa na New York kwa nyuzi za Latitude; ni jiji lenye Coliseum, ambamo yalifugwa masimba yaliyorarua Wakristo maelfu.
Rome,uko futi 40 hadi 270 juu ya usawa wa Bahari. Jiji lenye kelele nyingi kuliko mji wowote duniani,lipo kando ya Bahari ya Mediterranean.
 Zama za Papa Pius XII alibebwa kwenye kiti cha enzi kiitwacho, Sedia Gastatoria ambacho ni kiti cha enzi cha dhahabu chenye rangi nyekundu.Papa huketi hapa mara anapochaguliwa na Moshi  Mweupe, hutoa BARAKA Duniani- Urbi et Orbi.
Rome umejengwa juu ya milima saba: CAPITALINE, PALATINE, AVENTINE, QUIRINAL, VIMINAL, ESQUILINE, na CAELIAN.
Hapa, ndipo liketipo kanisa lile la Mungu ambalo sasa linataka kugeuka kuwa kama Yule mama wa mjini Brussels.
Mwanamke huyu ni kanisa. Kanisa linapoungana na dunia na kuacha usafi wa kiroho huitwa, ‘BABELI’ ya siri iliyoanguka na Mungu huwaita watu wake watoke humo(Ufunuo 18:2-4).
Kuanguka ni kuacha usafi wa kiroho,kumwacha Mungu na kuungana na uchafu kama unajisi,siasa za kugombea tawala za dunia,ufisadi,mapinduzi,ulawiti,ushoga n.k
Jiji lenye utajiri wa dhahabu na vito vya thamani lenye kuwakosesha watu kwa mafundisho yenye kuridhia dhambi(uasi wa sheria ya Mungu) kama jambo dogo tu-Uhuru na demokrasia,haki za binadamu n.k
Wapo wanaofuata kila jambo na ni ‘watoto’ wa Yule mama wa mjini Brussels. Tafakarini.
0786 324 074

No comments:

Post a Comment