Thursday, April 25, 2013

USHIRIKI WA WANAUME KATIKA AFYA YA UZAZI




Na Clara Matimo, Mwanza
KAMPENI ya kupunguza Maambukizi ya Ukimwi kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto, “Prevention of Mother to Child Transmission”(PMTCT), na Ushiriki wa Wanaume katika Uzazi wa Mpango,unakwamishwa  na  tabia ya mfumo dume ulioota mizizi Kanda ya Ziwa, imefahamika.
Mratibu Msaidizi wa Afya ya Uzazi na Mtoto Jijini Mwanza, Sarah Mahumbuga, amesema kwa miaka miwili ya 2011 na 2012, akina baba wachache walifika Kliniki na katika vituo vya Afya,ili kupima afya zao na kushiriki Uzazi wa Mpango.
Amesema,Shirika la Engender Health kupitia Mradi wa CHAMPION(Men Involvement), linalotoa huduma katika baadhi ya mikoa hapa nchini, Mkoa wa Mwanza ukiwemo,  wilaya za Ilemela na Nyamagana zinahusishwa na mradi huo.
Hospitali ya Nyamagana na Kliniki ya Makongoro  huhusishwa na mradi huo kwa nia ya kuwahamasisha  akina baba kushiriki Afya ya Uzazi na Maambukizi ya Ukimwi.
Sarah Mahumbuga amesema, katika kipindi cha mwaka 2011,wanaume walioshiriki kupima afya zao na Uzazi wa Mpango ni 3,370 sawa na asilimia 18  tu ya lengo lililokusudiwa, katika Jiji la Mwanza.

Mhudumu wa Afya wa Kliniki ya Makongoro akimhudumia mama mjamzito Aprili 25,mwaka huu
Mahumbuga afafanua kwamba, mwaka 2012  akina baba walioshiriki katika zoezi hilo muhimu ni 8,541 sawa na asilimia 43.
“Mwaka 2010 wanawake waliohudhuria Kliniki kwa mara ya kwanza walikuwa 18,952. Idadi ya waliopima virusi vya Ukimwi ni 12,057 sawa na silimia 63 ya akina mama wote waliohudhuria Kliniki kwa mara ya kwanza, na kati ya hao wanawake 756 sawa na asilimia 6.2 walikutwa na maambukizi ya Ukimwi”,Mahumbuga amesema.
Akilinganisha na akina baba waliopima virusi vya Ukimwi mwaka huo 2010 amesema walijitokeza akina baba 328 tu ambao ni sawa na asilimia 6.
Akaongeza kuwa mwaka 2011 wanawake waliofika kliniki kwa mara ya kwanza walikuwa 18,726; na kati yao waliopima Virusi vya Ukimwi ni 7,947 sawa na asilimia 42. Kati yao waliokutwa wakiwa na maambukizi ya virusi hivyo vya Ukimwi ni 506 idadi ambayo ni sawa na asilimia 6.3.
Mratibu huyo Msaidizi wa Afya ya Uzazi na Mtoto Jijini Mwanza, anasema katika mwaka huo 2011 wanaume waliofika Kliniki na wake zao na wakapima afya ni 374 sawa na asilimi 6.9.
Katika mwaka 2012,Mratibu huyo amebainisha kuwa wanawake waliohudhuria kliniki kwa mara ya mwanzo walikuwa 19,946; na kati yao waliopima afya zao ni 11,299 sawa na asilimia 57.Waliokutwa na maambukizi ya Ukimwi ni 523 sawa na asilimia 4.6.
Mratibu huyo amesema wanaume waliohudhuria kliniki mwaka 2012 walikuwa 596 ambao ni asilimia 2.1 tu
 Baba akiwa    akishiriki zoezi la upimaji katika Kliniki ya Makongoro,Mwanza
“Kama wanawake wanaohudhuria kliniki wangekuwa wanafika na wenzi wao na kupima, akina baba wangetambua umuhimu wa kushiriki zoezi hilo la kuokoa maambukizi kutoka kwa wazazi kwenda kwa mtoto”, amefafanua.
Akizungumzia changamoto zinazokabili Kampeni hiyo ya Afya ya Uzazi na Mtoto,   katika utendaji wa kazi wa kila siku, ameseka kuna uhaba wa vitendanishi( HIV TEST KITS) , akatoa mfano kwamba kwa mwaka huu 2013 Jiji la Mwanza limepata kit 69 tu wakati vipo vituo 24 vinavyotoa huduma hiyo.     Kit moja ina vifaa 100 vya kupima ukimwi.
“Kufuatia hali hiyo, mwaka 2011 wanawake waliofika kliniki mara ya kwanza walikuwa 18,726,lakini waliopima walikuwa 7,947; hali hiyo husababisha waliobaki kukosa huduma kufuatia vifaa hivyo vya kupimia Ukimwi kuwa vichache”, alisisitiza.
Amewataka wanaume kujitokeza kwa wingi bila woga katika zoezi hilo ambalo lazima lihusishe baba,mama na mtoto.
“Wanaume wote wanapaswa kufika kliniki pindi wake zao wanapopata ujauzito; kwa sababu kuna faida nyingi; kujua mama ana tatizo gani wakati wa ujauzito,dalili za hatari; na ikitokea shida baba ajue cha kufanya ili kumsaidia mama mja mzito kujifungua salama”,
Hatari za akina baba kutoshiriki zoezi la upimaji wa afya ya uzazi  humfanya mama mjamzito kuathiriwa kisaikolojia,hususan anapopimwa na kubainika kuwa ameambukizwa.
“Wakipimwa pamoja wakagundua tatizo ina kuwa rahisi wote kwa pamoja kujua namna ya kumkinga mtoto aliyeko tumboni asipate maambukizi; na pia hujua namna ifaayo kutumia dawa za kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto”, Mratibu huyo amesisitiza.
 Imeelezwa pia kwamba,wanaume wengi wa Tanzania hawapendi kupima Ukimwi ukilinganisha na wageni wanaofika nchini, ambao Mratibu huyo wa Afya ya Uzazi na Mtoto amesema hawajifichi;lakini wanaume wa hapa nchini hawapendi kujitokeza kuzungumzia hali zao za kiafya kwa wataalam wa afya.
Mganga Mkuu wa Jiji la Mwanza, Dk.Kimaro Daniel amesema kuna wanaume wengi waliojitokeza kupima afya zao Mwanza ukilinganisha na wanaume wa wilaya za Sengerema na Ukerewe.
Akitoa taarifa kwa Naibu  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Seif Rashid,Siku ya Utepe Mweupe,Machi 15 mwaka huu,Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo amesema mkoa huu una jumla ya wakazi 2,571,402 kulingana na SENSA YA WATU NA MAKAZI ya 2012,ongezeko ambalo ni sawa na asilimia 2.7.
Ndikilo amesema Mkoa wa Mwanza una watoto wenye umri chini ya mwaka mmoja 106,360 na wenye umri wa chini ya miaka mitano 488,851; wakati akina mama wenye umri wa kuzaa ni 926,179.
Akizungumzia idadi ya hospitali na vituo vya afya vinavyotoa huduma ya Afya ya Uzazi na Mtoto,Dk.Ndikilo amesema kuna vituo 353; na kati ya hivi vipo katika hospitali 14(mbili za rufaa);hospitali za wilaya,za binafsi na za mashirikika ya dini.
Kati ya vituo hivyo 353,vituo 326 sawa na asilimia 92 hutoa huduma ya afya ya mama na mtoto;wakati vituo 239 sawa na asilimia 73.3 hutoa huduma ya kuzuia maambukizi ya Ukimwi toka kwa mama kwenda kwa mtoto.
          Mhudumu wa Afya akiwapa huduma  mama wajawazito
Miongoni mwa akina mama 926,179 wenye umri wa kuzaa, akina mama 121,530 walipata ujauzito na kati yao  82,214 walipata huduma ya uzazi wakati wa kujifungua sawa na asilimia 67.6
Mkuu wa Mkoa amesema kiwango cha maambukizi ya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kimeshuka kutoka asilimia 5.2 mwaka 2011 hadi asilimia 4.2 mwaka jana.
Amesema pia kwamba vifo vya akina mama vinavyotokana na uzazi vimepungua kutoka  217 kati ya 100,000 hadi 95 kati ya 100,000 mwaka jana.
Mkuu wa Mkoa amesema mkoani Mwanza sasa vifo vya watoto walio chini ya mwaka mmoja ni 11 kati ya watoto 1,000 waliozaliwa hai.Kiwango hiki ni cha asilimia 14.
Kulingana na Mratibu wa Taifa wa Afya na Mama na Mtoto katika Wizara ya Afya, Dk. Koheleth Winani,akina mama wa Tanzania wangali wanakabiliwa na hatari ya maradhi yanayoweza kuzuilika.
Kiwango cha akina mama  wajawazito wanaofariki nchini 454 kati ya 100,000.Na watoto wanaokufa ni 26 kwa kila watoto 1000 wakati wanapozaliwa.
Kufuatia halihiyo, Mkurugenzi wa Afya wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani(USAID),Alisa Cameron alisema siku ya uzinduzi wa Kampeni ya Uzazi salama Jijini Mwanza kwamba Kampeni ya ‘Wazazi Nipendeni’ inayotangazwa na vyombo vya habari nchini iwafanye akina baba kuacha mfumo dume na kushiriki ipasavyo katika zoezi la uzazi wa Mpango na kupima virusi vya Ukimwi,ili kuokoa maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa  mtoto.
“WAZAZI NIPENDENI” inalenga kuwezesha akina mama wajawazito na wenzi wao kuchukua hatua thabiti za uzazi salama, na kuzua maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto(PMTCT).
Sekamponge  Makuki (24)mkazi wa jijini  Mwanza ambaye  ni mjamzito,anasema yeye anafaraja sana kwa kipindi hiki cha ujauzito kwa kuwa yeye na mumewe walipanga kupata mtoto,na pia wote wanahudhuria klinik jambo linalowafanya kupata elimu ya pamoja kutoka kwa wataalamu wa afya,na pia mumewe anafundishwa jinsi ya kuishi nae kwa kipindi cha ujauzito.
“Tangu tulipofunga ndoa na mume wangu,tumekuwa tukishirikiana nae katika masuala yote ya afya ya uzazi,hivyo na huu ujauzito nilionao tulipanga kwamba tazae,hata kabla ya kupata ujauzito tulipima afya zetu na baada ya ujauzito tulipima pia kwa pamoja,namshukuru MUNGU hatukupatikana na maambukizi ya ukimwi  anasema na kuongeza kuwa 
“lakini kwa kuwa tunashirikiana hata kama majibu yangekuwa mabaya tungeyapokea kwa pamoja,ni vizuri akisikia mwenywe  majibu kutoka kwa mtaalamu wa afya kuliko kumwambia mimi’’”anaeleza Makuki.


     Mhudumu wa Afya aki wahudumia watoto katika Kliniki ya Makongoro

Mwanaume anayeshiriki katiaka suala zima la Uzazi wa Mpango katika kliniki ya makongoro iliyopo jijini Mwanza,Abel Luzibila (30)mkazi wa Bwiru jijini Mwanza anasema amekuwa akienda kliniki na mke wake tangu mwanzo wa ujauzito ili kufahamu maendeleo ya afya ya mke wake, kama wataalamu wa afya watabaini tatizo lolote kutoka kwa mke wake wajue watajipanga vipi kiuchumi katika kulitatua.
Luzibila, amesema kwamba mara ya kwanza alipofika Kliniki na mkewe ambaye ni mjamzito, alisema alivutiwa na somo la namna  inavyopasa kumsaidia mama mjamzito.
“Kwa mfano,leo(Aprili 25 mwaka,2013) tumejifunza somo la unyonyeshaji;tumefundishwa lishe bora wakati mama anaponyonyesha na sitabishia Bajeti inayotukabili kwa sababu tayari nimeshiriki mafunzo hayo na najua umuhimu  na athari za kukosa lishe bora”, Luzibila amesema.
Ofisa Mawasiliano wa Mradi  wa CHAMPION unaoshughulikia Ushiriki chanya wa Wanaume katika Mkakati wa kitaifa wa kupambana na Maambukizi ya  Virusi vya Ukimwi na Ukimwi (Engender Health),Muganyizi Mutta, anasema akina baba wanaposhiriki kikamilifu katika Uzazi wa Mpango watawezeshwa kupanga idadi ya watoto wanaowataka.
Mutta pia amesema baba na mama wakishiriki kwa pamoja katika zoezi hilo watapata njia za uzazi wa Mpango zinazofaa, na kuwa na familia zilizo bora.
“Shirika la Engender Health,kupitia Mradi wa CHAMPION(Men Involvement) limetenga Dola za Kimarekani milioni 16 kwa ajili ya kuhamasisha akina baba kushiriki kikamilifu katika mkakati huu kitaifa wa kupambana na virusi vya Ukimwi kutoka ,mradi ni wa miaka  mitano unaomalizika Septemba mwaka huu”, Mutta amesema




Monday, April 22, 2013

waadilifu waliuliwa hapa zama za Rumi,wengine watauliwa Ufunuo 13:1-10http://www.isangocdn.com/rsrc/cms/hero-large/3ce273c1-863d-4711-a81a-5434697414e2/Rome%20Colosseum%20Tours%20Hero%20(960x145).jpg

WALIOWAUA J.F KENNEDY,ABRAHAM LINCOLN NA WENZAO WANAFANYA VURUGU TANZANIA(3)




KATI YA MWAKA 54 na 68 AD, wafuasi wa Yesu Kristo,hususan wale mitume walijipatia wafuasi wengi sana katika ile milki ya Rumi ya kale.
Zama hizo, Makaisari wa Rumi waliabudiwa na raia wao;kwa sababu Kaisari alijidhania yeye ni Mungu!
Ukristo ulipoibuka ukawaambia watu kumwabudu Mungu wa Mbinguni pekee,ukatishia ibada hiyo ya wafalme wa Kirumi(emperors).
Kaisari Nero aliazimu kuwafyeka Wakristo, alifanya njama akauchoma moto mji wa Rome(sasa Italia),akawasingizia Wakristo kwa sababu waliwafundisha watu kuwadharao hao wafalme na kumheshimu Mungu wa mbinguni-ilionekana kama kukosa uzalendo na kutoheshimu maofisa wa serikali na serikali yenyewe.
Mtume Petro, aliuliwa na Kaisari Nero mwaka 67 AD na akazikwa mahali ambapo siku hizi kuna kanisa kubwa la St.Peters Basilica, jijini Rome.
Wengine walitimuliwa jijini humo wakakimbilia mahali pengine Ulaya,        Mitume Paulo,Barnaba,Yohana na wengine walifanyiwa ukatili na kuteswa kwa kesi za kubambikiwa.
Tabia hizi zingalipo hata sasa kwa wale wanaopenda kuabudiwa kusingizia wafuasi  halisi wa Mungu ili waonekane wakosaji wanaostahili kutupwa ama kuuliwa. Hili si jambo la ajabu.
Sababu za Makaisari wa Rumi kudai kuabudiwa ni kwamba kulikuwa na mahekalu na watu wakawa wanawaabudu asubuhi kabla ya kwenda kwenye shughuli zao, waliitwa “Theos” neon la Kigiriki maana yake mungu na ‘Savior’ ni kuonesha heshima.
Hata makaisari hawa walipokufa kukajengwa masanamu yao yaliyoendelea kuabudiwa na raia wa dunia nzima waliyotawala. Julius Caesar sanamu lake liliwekwa kati ya masanamu mengine ya miungu katika mahekalu anuwai.
Kaisari Augusto(27-14 BC)akaitwa ‘Sebastos’ maana yake mungu,Gaius Caligula(37-41AD) alitaka dunia nzima imwabudu,hata sanamu lake likapelekwa ndani ya hekali mjini Jerusalem, ili kuabudiwa,vurugu zikaanza kwa sababu Wayahudi wakati huo walipinga sana kuabudu sanamu.
Nataka msomaji atambue aina ya watu wanaoanzisha migogoro ya kidini,lakini huwasukumia lawama watu wasiohusika.
Vurugu,vita na mauaji ya kinyama siku hizi huchochewa sana na dini hiyo hiyo inayoshurutisha watu wa dunia nzima kuabudu Wafalme wa kale,matajiri ambao hujificha ndani ya imani ya Freemasons,wakijidai watu wa Bwana Mungu,kumbe siyo.
Kupinga aina ya dini hiyo ni kujipatia mauti kwa sababu utaonekana wewe huna uzalendo(Patriotism).Watu wakuu kama Adolf Hitler hujidai kuwa na nguvu za kimungu ndani yao(Divinity) wanachoamuru hutaka dunia nzima kufuata,na wanaopinga kusingiziwa na kubambikwa makosa.
Sasa,unaweza kutambua hata ni kwa nini Saddam Hussein,Osama,Gaddafi na wengine wengi walivyouliwa kwa visingizio kuwa ni watu hatari wanaomiliki Mass Destruction Weapons,Saddam alinyongwa Desemba 30 mwaka 2006 ili wapinzani waone.
Kila kiongozi wa dunia wan chi anapaswa kutii, “To pay divine honors to the emperor and thereby inviting the penalty of ostracism, exile, torture, imprisonment and death”.
Unaweza kuona Charles Taylor wa Liberia akitoroshwa jela gerezani mjini Boston,huko kulipolipuka mabomu juzi, akapelekwa kwa Gaddafi,Libya ili akafunzwe medani ya kijeshi.
Alitumwa baadaye kwenda kupindua serikali ya mjini Monrovia, akaanza kuwasaidia waasi wa Revulutionary United Front(RUF) wakaanza kuiba almasi za Sierra Leone na kuziuza Ulaya na Marekani kwa hawa mabedui.
Muda ulipopita,wakamweka jela wakamsingizia kesi na kumgunga miaka 50 mmjini London ili asije kutoa siri. Njia ni ile ile ya kuziba watu midomo wasije kutoa siri.
Taylor, aliwahi kusema hivi,     “When your Master is also your enemy, you are perished” Aliyekutuma kazi anapokugeuka na kuwa adui yako basi unaangamia!
Alitumwa kazi, wakamgeuka na kumwangamiza. Hakuonesha heshima kwa wakubwa wa dunia hii waliorithi heshima ya emperors wa Rumi.
Kuna wakubwa wa dunia hii wanaodai kuabudiwa na kuheshimiwa na ndiyo walioanza kuisumbua Tanzania,kwa sababu hata Rais wan chi anapatakiwa kuonesha heshima kwao,  “To pay patriotism and royalty to emperors or Lords of this World”
Unabambikiwa makosa nawe huwezi kujitetea unahukumiwa kama Mitume Paulo, Petro,Baranaba na wenzao, wanasema Kaisari yuko juu kuliko Kristo,Mtume yeyote n/k
Hawa Freemasons ndiyo huleta fujo hapa duniani,mitafaruku kama ile ya Waislam/Wakristo kuchinja au kutochinja n.k
Mgogoro wa kuchinja uliwahi kutokea mwanzoni mwa Ukristo,sababu zilionekana kama za msingi za kupinga ibada ya sanamu.
Baraza la Yerusalem liliketi kukataa Wakristo kula nyama zilizochinjwa na waliohisiwa makuhani wa miungu(Matendo ya Mitume 15:29).
Mtume Paulo, alipuuza maamuzi ya Baraza lile la kuwataka Wakristo kuacha kula nyama hizo zilizouzwa madukani(mabucha),akasema,kula hakuhusiani na ibada ya sanamu wala ibada ya miungu(1Wakorintho 8).
Kula nyama inayohisiwa ilitolewa kafara kwa miungu ama kuchinjwa baada ya kufanyiwa ibada Fulani,Paulo anasema hata sasa kuwa hakumpunguzii mlaji uaminifu kwa Mungu wa kweli(1Wakorintho 8:8-13).
Baraza la Yerusalem lilikaa mwaka 49 AD kupinga Wakristo kula nyama zilizochinjwa na makuhani wa miungu kabla ya kuuzwa sokoni.Paulo akaandika waraka kwa Wakorintho kupuuza ugomvi ule wa kula au kotokula nyama,kuchinja au kutochinja mwaka 55 AD.
“Eating things sacrificed to idols” maana yake ni mtu kula kwa makusudi kuwa nyama zile zilizotolewa sadaka kwa miungu, hiyo miungu ikupe neema wewe mlaji!
Kama huna mpango na mambo yale yanakuhusu nini? Kula au usile.poa tu!Wachinje wasichinje,poa tu!
Freemasons hufundisha  watu kufanya ubaya,kuua na kulipa visasi, wakijiddai kuwa roho  haiwezi kuchafua mwili wa mtu hata akapata hukumu.
Hii ni ‘Modern Gnosticism’ ambayo ni uasi kwa makanisa na misikiti kuhalalisha uasi,fitina,chuki na mapigano wakidhani ni kutetea imani.
Tukumbuke Kaisari Nero aliuchoma mji wa thamani kubwa ili kupata gharama ya kuwashitaki Paulo na wenzake ili waualiwe. Njama/Uongo ndivyo hutumika sasa kama Nero alivyochoma jiji la Rome mwaka 64 AD na kubambika makosa kwa watu waaminifu.
Haya majanga ya sasa ya watu kuchoma makanisa/Misikiti huchochewa na genge hilo ambalo lina pesa nyingi na hupeleka mambo haya kwa nchi wanazotaka kuvuruga.
Hakuna Mkristo safi atakayenufaika na vita dhidi ya Waislam, na hakuna Muislam atakayekuwa mwaminifu kwa Allah akichoma makanisa. Hii ni roho ya wale jamaa wanaotawala dunia.
 Nijadili kidogo upuuzi unaoenezwa kwamba Rais Jakaya Kikwete ndiye muasisi wa udini hapa Tanzania.
Jambo hili la kijinga na kipuuzi sana,huenezwa kwa makusudi kwa watu wajinga wasiotafakari. Mimi nawakumbusha mwaka 2005.
Maaskofu,Wachungaji na makasisi ndiyo waliompigia sana debe Kikwete awe rais kwamba alikuwa ‘Chaguo la Mungu!’
Ilishangaza kuona maaskofu wakiwa wamevaa TSHIRT NA KOFIA ZA CCM huku wakimpigia debe Kikwete madhabahuni kwamba ni ‘Chaguo la Mungu!”
Augustine Lyatonga Mrema,ndiye shahidi wa historia.Aliwapinga sana hawa maaskofu kusema Kikwete ni chaguo la Mungu,akasema  “Hawa maaskofu wanadai Kikwete ni chaguo la Mungu,walikaa kikao na Mungu lini akawaambia  Kikwete ni chaguo lake?”
Mrema, aliwasuta maaskofu hawa katika viwanja vya Furahisha,Mwanza wakati akifanya kampeni za Chama chake, TLP mwaka 2005.
Mrema, alisema hawa maaskofu walikuwa waongo,Mungu hakuwatuma walikuwa manabii wa uongo!
 Sasa,unawezam kuuona hawa ‘Manabii wa Uongo’ wa Mrema,wakigeuka mara moja na kuonesha kwamba huyo Mungu aliyemchagua Kikwete mwaka 2005,sasa ni kigeugeu, ameshamchagua mwingine,na sasa Kikwete hafai ni ‘mdini’ na mkabila!
Siku hizi wanahamasisha watu kugomea kula nyama zilizochinjwa na Waislam,na husema kwa kinywa kipana kwamba Kikwete hafai,siyo chaguo la mungu wao!!
Ilikuwa Januari 20,mwaka 2005,Prof.Ibrahim Lipumba akizungumza na waandishi wa habari,Kirumba Mwanza, alisema, “Kikwete hakuwa na ‘Presidential Material’ akapuuzwa na maaskofu,tena wakamwona yeye Lipumba kwamba anakumbatia udini na chama chake cha CUF, leo Lipumba kawa safi,mwenye ‘Uislam’ ni Kikwete! Tuachane na ujinga huu jamani!
Mbona hawa hawakumsikiliza Lipumba mwaka 2005 walipokuwa wamevaa Tshirt za Kikwete na kofia?
Nadhani, Kikwete alipoingia madarakani,alopoamua kuwa ‘Fair’ kuachana na mpango wa siri wa maaskofu, akawakosea,sasa wanamwandama na mambo ya kijinga!
Sina tabia ya kujikomba kwa mtu! Lipumgba ni shahidi, alisema “Kikwete ni rafiki yangu;ni ndugu yangu,lakini hana Presidential Material”.
Maaskofu walimpuuza Lipumba,wakmbeba Kikwete makanisani mwao,hawakuona Uislam wowote kwake, ati leo wanasema Kikwete anasambaza udini..naam Uislam! Upuuzi mkubwa!
Mrema, alisema hakuna Mungu aliyewatuma hawa kumpigia debe Kikwete mwaka 2005,ni tamaa zao za vyeo na madaraka, walipotupwa wakaanza hila na chokochoko,sasa tumejua udini huanzishwa na maaskofu,wachungaji,makasisi na masheikh,na wala siyo Kikwete na wenzake!
Mungu wa maaskofu angekuwa ‘Omniscient’ kama Mungu ninayemjua, asingemchagua Kikwete mwaka 2005 akajakumkata sasa,ni ujinga mtupu na hila kama za akina Kaisari Nero!
Maaskofu wa mungu ‘kigeugeu’ asiye na macho, ndiye anayetaka kuiangamiza Tanzania kwa vurugu za kidini na siasa uchwara.
Nchi imejaa matusi na ugomvi.Vyombo vya habari vinavyojiita ‘The Fourth     Estate” Mhimili wa  nne wa Dola, leo umeingiliwa na hao hao akina Kaisari Nero, hadi sasa tunashuhudia wahusika wakitoana macho,wasipate kuona ukweli wa mambo!
 Mungu inusuru Tanzania
Itaendelea
0713 324 074





Friday, April 19, 2013

WALIOWAUA J.F KENNEDY NA ABRAHAM LINCOLN WANAFANYA USHENZI TZ(2)




Desemba  26, mwaka 2004, sahani inayobeba sakafu ya Bahari ya Hindi ikapasuka na kusababisha ebneo la kilomita 975(maili 600) kuwa shimo kubwa chini ya ardhi!
Bahari ya Hindi ikakosa pa kutuama, juu hadi chini na kutoka upande mmoja kwenda wa pili.Matokeo yalikuwa ni tetemeko kubwa la ardhi lenye ukubwa wa 9.0 katika kipimo cha Richter,ambalo halikuwahi kutokea miaka 40 iliyopita katika Bahari ya Hindi,jirani na Pwani ya Magharibi ya Indonesia na Kisiwa cha Sumatra.
Tetemeko hilo kubwa la ardhi,lilisababisha tani trilioni moja za maji ya bahari kugongana na kusababisha mawimbi makali ya maji yaliyotimka mbio mithili ya ndege!
Miamba ilikuwa imefumuka chini ya ardhi ya sakafu inayobeba hiyo bahari ya Hindi;sasa maji yaliharakisha mahali pa kukaa,yakasababisha mawimbi makali ya kutisha.
Hili ndilo janga la tsunami,lililoua watu zaidi ya 150,000 na kuwafanya wengine mamilioni kukosa makazi katika nchi 11 duniani. Unakumbuka  tsunami?
Bila shaka,utakuwa hujasahau kwamba janga lile lilisombwa kwa yale mawimbi makali,baada ya maji kusukwa sukwa,kutoka Indonesia na Visiwa vya Sumatra hadi hapa Afrika ya Mashariki.
Dar es salaam,Mombasa,Somalia pia kulitokea vifo na upotevu wa mali.Nataka kusema kwamba,balaa moja linaloanzishwa na Ibilisi katika pembe moja ya dunia, mawimbi yake(athari) husafiri kwa kasi na kuenea katika dunia yote.
Tsunami,iliyotokea Desemba 26,mwaka 2004 na kuua maelfu ya watu katika nchi 11 duniani,ni dalili kwamba Watanzania hawako salama na kila ‘ushenzi’ unaotendeka mahali pengine duniani.
Ukisikia Marekani, demokrasia  maana yake ni hata kichaa ama mvuta bangi kuwa na uhuru wa kumiliki bunduki,na akijisikia anakwenda kulipua watu ‘kidemokrasia’; na ukisikia Rais Barack Obama amekwama kutaka sheria ibadilishwe,umiliki wa silaha ufanyike kwa makini,watu wamempinga!
Ujue Tanzania ‘Katiba Mpya’ nayo itakuja na uhuru huo wa mtu kumiliki ‘Revolver’ na  ukimnyang’anya mshushu wake baa, anakulipua wewe,mkeo,watoto ,nyanya n.k
Ndiko demokrasia ya uhalifu inakotupeleka,na hushadidiwa na majununi walio wengi siku hizi!
Umesikia Marekani inagugumia kwa milipuko ya mabomu na watu wengi wamekufa wengine kuumia-haya ndiyo matokeo ya kiwenda wazimu ya kila mtu kuwa huru kununua bunduki  na vilipuzi(explosives)dukani, hata mvuta bangi na wazimu,mradi anazo pesa!
Mauaji na milipuko ni vitu vya kawaida kwa watu wanaojidai kuwa na uhuru,na wendawazimu wana uhuru hata wa kuua!
Kiama cha World Trade Centre(WTC) cha Septemba 11,mwaka 2001 walisingiziwa magaidi wa al-Qaeda, na twajua Septemba 16 mwaka 1920 mitaa tajiri ya Wall Street,ilishawahi kulipuliwa kwa mabomu watu 30 wakapoteza maisha.
Feburuali 26 mwaka 1993 majengo ya WTC yaliwahi kulipuliwa(kabla ya Osama) kwa bomu watu sita wakapoteza maisha.
Sababu za majanga na mauaji ya kuangamiza namna hiyo ni ushenzi unaoitwa demokrasia na ujuaji,kila mwehu anaruhusiwa kumiliki bunduki ama mabomu!!
Matokeo yake,Marekani, Rais James J. Garfield alipigwa risasi na Charles Guiteau,jijini Washington akafa Septemba 19,mwaka 1881.
Katika sehemu ya kwanza,nikaandika kwamba Rais Anwar Sadat wa Misri naye alifumuliwa risasi na Komandoo,akati akikagua gwaride la heshima mjini Cairo.Ilikuwa Oktoba 6, mwaka 1981.
Askari 7 waliuliwa 28 wakajeruhiwa;aliyemuua Sadat akafumuliwa risasi ya kichwa ili kuficha siri.
Ninakuonesha vigogo waliowahi kuuawa kwa risasi katika nchi zilizoendelea ambako watu wananunua bunduki kama nyanya sokoni.
Waliowahi kujeruhiwa kwaa bunduki ni wengi: Theodore Roosevelt alikua Rais wa Marekani, alijeruhiwa Oktoba 14 mwaka 1912.Adolf Hitler(Julai 20 mwaka 1944),Harry Truman pia rais wa Marekani(Nov,mwaka 1950),Papa Paul II(Mei 12,mwaka 1982),Rais Gerald Ford pia wa Marekani(Sept. 5,mwaka 1975),Ronald Reagan pia rais(Machi 30, mwaka 1981,hata Margaret Thatcher,  “Iron Lady” aliyezikwa juzi mjini London alinusurika kulipuliwa kwa bomu lililotegwa na magaidi wa Irish Republican Army(IRA) huko hotelini Grand ,Brighton ,England.
Watu wengine wane walikufa wakiwemo wabunge, akina Pinochet,Mubarak anayeshikiliwa kizuizini huko Misri, akina Castro,Nyerere-orodha ni ndfu, walishanusurika njama za mauaji.
Naam, hii ndiyo dunia tunayolilia kwamba iwe na demokrasia na kila mpumbavu awe huru kusema upumbavu wake na kusikilizwa hata na watoto. Usishangae leo Tanzania waliodhaniwa wenye hekima kufuatia kuvaa suti,ni wakola na kauli zao ni chafu zilizojaa uchochezi hata kwa watoto!
Haya hayakuanza hapa,tumeyakurupukia tukidhani ‘uhuru’ wa kusema “Freedom of Exspression” na bahati mbaya sana hatuwezi kupambanua ujinga na werevu.
Watu wanadai uhuru wa kuua,kutukana,kuiba,kuumiza watu hasa wanyonge n.k
Novemba 4,mwaka 1995(siyo mwaka 1997 kama nilivyosema katika makala iliyotangulia)Yitzak Rabin,Waziri Mkuu wa Israeli aliuliwa na Yigal Amir,mjini Tel Aviv.
Sababu ilikuwa Rabin akitaka uhuru wa dini mjini Jerusalem, hawa jamaa wa Mossad wakamwasha risasi, wako akina Cyprien Ntaryamira na Juvenal Habyarimana,Olof Palme orodha ni ndefu.
Chuki,uhasama,kugombea madaraka(supremacy struggle),kugombea utajiri,mradi sasa mwenye nguvu ndiye atasalia(survival of the fittest) sisi dhaifu tutakuwa mbolea!
M asikini ni nadra kupona katika mbio hizi za kugombea maisha(struggle for existence), matokeo yake tunajua vita vitaanzia Bungeni,serikalini,mahakamani,katika vyombo vya habari vinavyojidai kuzodoa wengine,hatimaye  mitaa inaenea damu mbichi!
                               DUNIA UWANJA WA FUJO ZA KIJINGA!
Dunia ni sayari ya tano kutoka kwa ukubwa nay a tatu kutoka kwenye jua.Uzito wake ni tani 6,580,000,000,000,000,000,000!!
Dunia ina kipenyo cha maili 7,926 Ikweta na maili 7,900 tu kutoka ncha ya Kusini hadi Kaskazini. Humo ndani ni UWANJA WA FUJO za kijinga,kufuatia choyo,ubinafsi mwingi(Yakobo 3:16,17).Wajinga wengi wanaharakisha kila mtu awe tajiri, awe na heshima na cheo(1Timotheo 6:10).
                WANASIASA UCHWARA?
Nimewahi kuimba wimbo wa Mwanamuziki Roger Whittaker, kwamba:
“Politicians are like a bunch of bananas. They hang together, they all are yellow and there is not a straight one”
Wanasiasa wote hufananishwa na ndizi katika chane. Ndizi zote hushikana mahali pamoja, zinakula kwa mama mmoja, zina rangi moja ya njano zinapopevuka,na hakuna hata ndizi moja iliyonyooka!
Naam,ndizi  zote zimepinda! Na wanasiasa wamepinda,hakuna mnyoofu! Pole wajinga wanaowaamini wanasiasa wenye maneno mengi.
Waziri Mkuu wa Uingereza, Winston Churchill (1940-45) aliwahi kusema kwamba, “No sentence should be more than nine words” Kwamba maneno katika vifungu vya maneno yawe mafupi yasiyozidi  kenda katika kila sentensi moja.
Churchill, alikuwa Mwandi wa habari mahiri sana, na alijifunza kanuni ya uandishi ‘Word economy’ lengo likiwa watu wame na maneno mafupi vitendo vyema vizungumze.
Bahati mbaya,kila Mtanzania siku hizi husema sana hata povu kutoka mdomoni,kila mahali kuna Bunge lake-Freedom of Expression!!
                           KUCHINJA/KUTOCHINJA
Shida hii ilianza katika Karne ya kwanza A.D,shida ya Wakristo kutaka kuchinja nyama zao,kwa sababu Wachinjaji hugeuza kuchinja ibada(ya miungu); kwamba kula nyama iliyotolewa kafara kwa miungu ni ibada ya sanamu?
Baraza la Yerusalem lilipiga marufuku Wakristo kula nyama zilizotolewa kafara kwa sanamu na wale wachinjaji ambao walikuwa makuhani wa miungu?
Tazama Matendo ya Mitume 15:29 utaona Mtume Paulo akipuuza ugomvi ule wa watu kususia kula nyama, kununua nyama buchani. Tazama 1Wakorintho 8:8-13 utaona Paulo anasema hata kama wachinjaji walifanya ibada huko ya miungu,wewe mlaji kama hujali inakuathiri vipi?
Wakristo wasijidai kukataa kula nyama zilizotolewa kafara kwa miungu,wakati wanaabudu miungu tele,na hawajatengana na dhambi,wanatenda dhambi huku wakisema  Roho haichafuliwi na matendo ya mwili!
Eti angalia roho yangu acha kuangalia matendo ya mwili! Uzinzi,uchafu,ubakaji,ufisadi,uongo,ujambazi,ushenzi wa kila namna! Lakini kula nyama zilizochinjwa na Waislam,dhambi!! Dhambi ni uasi wa sheria ya Mungu,unaitunzaje kama wewe unabaka watoto chekechea na kupora wake za waumini ndani ya joho la Ukristo?
1Wakorintho sura 8 Paulo anaonya tabia hii ya kinafiki,na kuwataka Wakristo kuishi kwa amani na waabudu sanamu.
Nataka kuwaambia Watanzania kwamba yapo mambo ya uchochezi toka mbali sana,yanaingizwa hapa nchini na kukurupukiwa na watu hawa ili kuvuruga amani. Haya yametokea mbali sana kwa Ibilisi,lengo kuleta vita vya kidini,ili kuwe na maangamizi makubwa zaidi.
Tsunami ilikuja kasi huku Pwani ya Tanzania,na fujo zitakuja nyingi wapumbavu watazipokea na kuongeza mawimbi katika bahari,na mwisho hayo mawimbi huwa makubwa mno na hugharikisha watu.
Itaendelea
0713 324 074