Desemba 26, mwaka 2004, sahani inayobeba sakafu ya Bahari ya Hindi
ikapasuka na kusababisha ebneo la kilomita 975(maili 600) kuwa shimo kubwa
chini ya ardhi!
Bahari ya
Hindi ikakosa pa kutuama, juu hadi chini na kutoka upande mmoja kwenda wa pili.Matokeo
yalikuwa ni tetemeko kubwa la ardhi lenye ukubwa wa 9.0 katika kipimo cha Richter,ambalo
halikuwahi kutokea miaka 40 iliyopita katika Bahari ya Hindi,jirani na Pwani ya
Magharibi ya Indonesia na Kisiwa cha Sumatra.
Tetemeko
hilo kubwa la ardhi,lilisababisha tani trilioni moja za maji ya bahari
kugongana na kusababisha mawimbi makali ya maji yaliyotimka mbio mithili ya
ndege!
Miamba
ilikuwa imefumuka chini ya ardhi ya sakafu inayobeba hiyo bahari ya Hindi;sasa
maji yaliharakisha mahali pa kukaa,yakasababisha mawimbi makali ya kutisha.
Hili ndilo
janga la tsunami,lililoua watu zaidi ya 150,000 na kuwafanya wengine mamilioni
kukosa makazi katika nchi 11 duniani. Unakumbuka tsunami?
Bila
shaka,utakuwa hujasahau kwamba janga lile lilisombwa kwa yale mawimbi
makali,baada ya maji kusukwa sukwa,kutoka Indonesia na Visiwa vya Sumatra hadi
hapa Afrika ya Mashariki.
Dar es
salaam,Mombasa,Somalia pia kulitokea vifo na upotevu wa mali.Nataka kusema
kwamba,balaa moja linaloanzishwa na Ibilisi katika pembe moja ya dunia, mawimbi
yake(athari) husafiri kwa kasi na kuenea katika dunia yote.
Tsunami,iliyotokea
Desemba 26,mwaka 2004 na kuua maelfu ya watu katika nchi 11 duniani,ni dalili
kwamba Watanzania hawako salama na kila ‘ushenzi’ unaotendeka mahali pengine
duniani.
Ukisikia
Marekani, demokrasia maana yake ni hata
kichaa ama mvuta bangi kuwa na uhuru wa kumiliki bunduki,na akijisikia
anakwenda kulipua watu ‘kidemokrasia’; na ukisikia Rais Barack Obama amekwama
kutaka sheria ibadilishwe,umiliki wa silaha ufanyike kwa makini,watu
wamempinga!
Ujue
Tanzania ‘Katiba Mpya’ nayo itakuja na uhuru huo wa mtu kumiliki ‘Revolver’ na ukimnyang’anya mshushu wake baa, anakulipua
wewe,mkeo,watoto ,nyanya n.k
Ndiko
demokrasia ya uhalifu inakotupeleka,na hushadidiwa na majununi walio wengi siku
hizi!
Umesikia
Marekani inagugumia kwa milipuko ya mabomu na watu wengi wamekufa wengine
kuumia-haya ndiyo matokeo ya kiwenda wazimu ya kila mtu kuwa huru kununua
bunduki na vilipuzi(explosives)dukani,
hata mvuta bangi na wazimu,mradi anazo pesa!
Mauaji na
milipuko ni vitu vya kawaida kwa watu wanaojidai kuwa na uhuru,na wendawazimu
wana uhuru hata wa kuua!
Kiama cha World
Trade Centre(WTC) cha Septemba 11,mwaka 2001 walisingiziwa magaidi wa al-Qaeda,
na twajua Septemba 16 mwaka 1920 mitaa tajiri ya Wall Street,ilishawahi
kulipuliwa kwa mabomu watu 30 wakapoteza maisha.
Feburuali 26
mwaka 1993 majengo ya WTC yaliwahi kulipuliwa(kabla ya Osama) kwa bomu watu
sita wakapoteza maisha.
Sababu za majanga
na mauaji ya kuangamiza namna hiyo ni ushenzi unaoitwa demokrasia na
ujuaji,kila mwehu anaruhusiwa kumiliki bunduki ama mabomu!!
Matokeo
yake,Marekani, Rais James J. Garfield alipigwa risasi na Charles Guiteau,jijini
Washington akafa Septemba 19,mwaka 1881.
Katika
sehemu ya kwanza,nikaandika kwamba Rais Anwar Sadat wa Misri naye alifumuliwa
risasi na Komandoo,akati akikagua gwaride la heshima mjini Cairo.Ilikuwa Oktoba
6, mwaka 1981.
Askari 7
waliuliwa 28 wakajeruhiwa;aliyemuua Sadat akafumuliwa risasi ya kichwa ili
kuficha siri.
Ninakuonesha
vigogo waliowahi kuuawa kwa risasi katika nchi zilizoendelea ambako watu
wananunua bunduki kama nyanya sokoni.
Waliowahi
kujeruhiwa kwaa bunduki ni wengi: Theodore Roosevelt alikua Rais wa Marekani,
alijeruhiwa Oktoba 14 mwaka 1912.Adolf Hitler(Julai 20 mwaka 1944),Harry Truman
pia rais wa Marekani(Nov,mwaka 1950),Papa Paul II(Mei 12,mwaka 1982),Rais
Gerald Ford pia wa Marekani(Sept. 5,mwaka 1975),Ronald Reagan pia rais(Machi
30, mwaka 1981,hata Margaret Thatcher, “Iron
Lady” aliyezikwa juzi mjini London alinusurika kulipuliwa kwa bomu lililotegwa
na magaidi wa Irish Republican Army(IRA) huko hotelini Grand ,Brighton ,England.
Watu wengine
wane walikufa wakiwemo wabunge, akina Pinochet,Mubarak anayeshikiliwa kizuizini
huko Misri, akina Castro,Nyerere-orodha ni ndfu, walishanusurika njama za
mauaji.
Naam, hii
ndiyo dunia tunayolilia kwamba iwe na demokrasia na kila mpumbavu awe huru
kusema upumbavu wake na kusikilizwa hata na watoto. Usishangae leo Tanzania
waliodhaniwa wenye hekima kufuatia kuvaa suti,ni wakola na kauli zao ni chafu
zilizojaa uchochezi hata kwa watoto!
Haya
hayakuanza hapa,tumeyakurupukia tukidhani ‘uhuru’ wa kusema “Freedom of
Exspression” na bahati mbaya sana hatuwezi kupambanua ujinga na werevu.
Watu wanadai
uhuru wa kuua,kutukana,kuiba,kuumiza watu hasa wanyonge n.k
Novemba
4,mwaka 1995(siyo mwaka 1997 kama nilivyosema katika makala iliyotangulia)Yitzak
Rabin,Waziri Mkuu wa Israeli aliuliwa na Yigal Amir,mjini Tel Aviv.
Sababu
ilikuwa Rabin akitaka uhuru wa dini mjini Jerusalem, hawa jamaa wa Mossad
wakamwasha risasi, wako akina Cyprien Ntaryamira na Juvenal Habyarimana,Olof
Palme orodha ni ndefu.
Chuki,uhasama,kugombea
madaraka(supremacy struggle),kugombea utajiri,mradi sasa mwenye nguvu ndiye
atasalia(survival of the fittest) sisi dhaifu tutakuwa mbolea!
M asikini ni
nadra kupona katika mbio hizi za kugombea maisha(struggle for existence),
matokeo yake tunajua vita vitaanzia Bungeni,serikalini,mahakamani,katika vyombo
vya habari vinavyojidai kuzodoa wengine,hatimaye mitaa inaenea damu mbichi!
DUNIA UWANJA WA
FUJO ZA KIJINGA!
Dunia ni
sayari ya tano kutoka kwa ukubwa nay a tatu kutoka kwenye jua.Uzito wake ni
tani 6,580,000,000,000,000,000,000!!
Dunia ina
kipenyo cha maili 7,926 Ikweta na maili 7,900 tu kutoka ncha ya Kusini hadi
Kaskazini. Humo ndani ni UWANJA WA FUJO za kijinga,kufuatia choyo,ubinafsi
mwingi(Yakobo 3:16,17).Wajinga wengi wanaharakisha kila mtu awe tajiri, awe na
heshima na cheo(1Timotheo 6:10).
WANASIASA UCHWARA?
Nimewahi
kuimba wimbo wa Mwanamuziki Roger Whittaker, kwamba:
“Politicians are like a bunch of
bananas. They hang together, they all are yellow and there is not a straight
one”
Wanasiasa
wote hufananishwa na ndizi katika chane. Ndizi zote hushikana mahali pamoja,
zinakula kwa mama mmoja, zina rangi moja ya njano zinapopevuka,na hakuna hata
ndizi moja iliyonyooka!
Naam,ndizi zote zimepinda! Na wanasiasa wamepinda,hakuna
mnyoofu! Pole wajinga wanaowaamini wanasiasa wenye maneno mengi.
Waziri Mkuu
wa Uingereza, Winston Churchill (1940-45) aliwahi kusema kwamba, “No sentence should be more than nine words”
Kwamba maneno katika vifungu vya maneno yawe mafupi yasiyozidi kenda katika kila sentensi moja.
Churchill,
alikuwa Mwandi wa habari mahiri sana, na alijifunza kanuni ya uandishi ‘Word
economy’ lengo likiwa watu wame na maneno mafupi vitendo vyema vizungumze.
Bahati
mbaya,kila Mtanzania siku hizi husema sana hata povu kutoka mdomoni,kila mahali
kuna Bunge lake-Freedom of Expression!!
KUCHINJA/KUTOCHINJA
Shida hii
ilianza katika Karne ya kwanza A.D,shida ya Wakristo kutaka kuchinja nyama
zao,kwa sababu Wachinjaji hugeuza kuchinja ibada(ya miungu); kwamba kula nyama
iliyotolewa kafara kwa miungu ni ibada ya sanamu?
Baraza la
Yerusalem lilipiga marufuku Wakristo kula nyama zilizotolewa kafara kwa sanamu
na wale wachinjaji ambao walikuwa makuhani wa miungu?
Tazama Matendo
ya Mitume 15:29 utaona Mtume Paulo akipuuza ugomvi ule wa watu kususia kula
nyama, kununua nyama buchani. Tazama 1Wakorintho 8:8-13 utaona Paulo anasema
hata kama wachinjaji walifanya ibada huko ya miungu,wewe mlaji kama hujali
inakuathiri vipi?
Wakristo
wasijidai kukataa kula nyama zilizotolewa kafara kwa miungu,wakati wanaabudu
miungu tele,na hawajatengana na dhambi,wanatenda dhambi huku wakisema Roho haichafuliwi na matendo ya mwili!
Eti angalia
roho yangu acha kuangalia matendo ya mwili!
Uzinzi,uchafu,ubakaji,ufisadi,uongo,ujambazi,ushenzi wa kila namna! Lakini kula
nyama zilizochinjwa na Waislam,dhambi!! Dhambi ni uasi wa sheria ya
Mungu,unaitunzaje kama wewe unabaka watoto chekechea na kupora wake za waumini
ndani ya joho la Ukristo?
1Wakorintho
sura 8 Paulo anaonya tabia hii ya kinafiki,na kuwataka Wakristo kuishi kwa
amani na waabudu sanamu.
Nataka
kuwaambia Watanzania kwamba yapo mambo ya uchochezi toka mbali sana,yanaingizwa
hapa nchini na kukurupukiwa na watu hawa ili kuvuruga amani. Haya yametokea
mbali sana kwa Ibilisi,lengo kuleta vita vya kidini,ili kuwe na maangamizi
makubwa zaidi.
Tsunami
ilikuja kasi huku Pwani ya Tanzania,na fujo zitakuja nyingi wapumbavu
watazipokea na kuongeza mawimbi katika bahari,na mwisho hayo mawimbi huwa
makubwa mno na hugharikisha watu.
Itaendelea
0713 324 074
No comments:
Post a Comment