Thursday, August 1, 2013

marekani

Turejee nyuma, wakati wa vita vya kumpindua Mtawala wa Nchi ya Mito miwili ya Tigris na Eufrates,Saddam Hussein.
Marekani, aslani haikusubiri ruhusa ya Umoja wa Mataifa(UN);Saddam alipinduliwa,Sanamu lake likang’olewa kuonesha enzi yake ilikwishakoma, baada ya miaka mitatu gerezani, akanyongwa huko Camp Justice,mjini Baghdad.
George Herbert Walker Bush(88),Agosti mwaka 1990 alijaribu kumng’oa Saddam Hussein huko Irak,kipindi alipoivamia Kuwait. Unajua sababu za Saddam kuivamia Kuwait? Waliiba mafuta.Bush huyu (Baba) alipata ushindi mwembamba katika medani ya vita.
Bush baba alisaidiwa sana na vikosi vya Umoja wa Mataifa(UN),vikosi vya Umoja wa Kujihami Ulaya Magharibi(NATO) na Muungano wa Kiarabu, Arab League.
Kuwait ilikombolewa toka mikononi mwa Saddam, Bush baba akapata hadhi katika historia ya nchi hiyo babe sana duniani siku hizi. Uchumi ulikwenda vibaya mno,ukaja kurekebishwa na Bill Clinton baada ya kushinda Uchaguzi mkuu mwaka 1992.
 Bush Baba, aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi la Marekani(CIA)na alisaidia sana kuparaganyika kwa iliyokuwa Dola ya Kisovieti ya Urusi(USSR) zama za Mikhail Gorbachev.
Kuparaganyika kwa USSR,ilikuwa kupisha njia kwa Mataifa ya Magharibi na Umoja wa Kujihami wa Ulaya Magharibi(NATO) kupanua himaya yake hadi Mashariki, na ilikuwa ishara ya kumalizika kwa VITA BARIDI,kasha UKUTA WA BERLIN ukavunjwa,mwaka 1994.
Kitendo cha George Bush(mtoto)kumnyonga Saddam,ilikuwa kurejesha heshima ya nyumba yao katika Taifa hilo babe sana duniani. Marekani ilivumbuliwa na Christopher Columbus,OKTOBA 12, MWAKA 1492, na ikaja kutangaza uhuru wake Julai 4,mwaka 1776. Juzi walisherehekea miaka 236 ya uhuru.
Sasa, tuchambue Ufunuo 18:11-18. Marekani ilipata uhuru na ikawa nchi kimbilio kwa waliosetwa na tawala katili sana.
Lakini, ilikuja kuwa nchi katili; na ikaanza kufanya mapenzi ya JOKA ambaye ni Ibilisi mwenyewe,pale ilipopindua marais wa mataifa mengine kwa jeuri. Hawa ni pamoja na Jenerali Manuel Noriega wa Panama na Salvador Allende wa Chile, wakamweka kibaraka wao Dikteta, Pinochet.
 Licha ya kupindua serikali za Panama na Chile kama nilivyokwishaandika katika makala zilizotangulia, Shirika lao la CIA lilishirikiana sana na manyang’au kama Dikteta Mobutu  wa Zaire kuua wanamapinduzi wa Afrika, akina Patrice Emely Lumumba.
CIA ilishirikiana na Makaburu wa Afrika ya Kusini kuwawinda wanamapinduzi wa Afrika ya Kusini,ili Botswana, Namibia,,Angola,Msumbiji na hata Afrika ya Kusini waafrika wasijitawale wenyewe.
 Ndani ya Angola,Chama cha MPLA na FNLA vilipambana wakati FNLA wakipewa msaada na CIA hadi uhuru ulipopatikana kutoka Ureno mwaka 1975. Jonas Malheiro Savimbi alikuwa kibaraka wa Marekani,ili kuvuruga maendeleo ya nchi, hadi walipomumwaga juzi juzi  akaachwa kupigwa risasi na majeshi ya serikali. Jambo hili alishalisema Kamara Kusupa.
MMarekani iwe chini ya Barack Obama ama Mgombea wa Republican,Mitt Romney, ina akili ile ile, ya kunena kama Shetani(Ufunuo 13: 11) yaani ubabe wake na kulazimisha watu kile wanachotaka wao.
Angalia, kwamba CIA waliwasaidia Makaburu wa Afrika ya Kusini kuwaua wanafunzi 250 katika kitongoji cha SOWETO(South West Township) mwaka 1976,mjini Pretoria.
Turejee Irak, ambayo baada ya Saddam hamkani si shwari. Nchi imegawanyika sasa ni baina ya dini na dini;msikiti kwa msikiti,ukoo baina ya ukoo wanapambana.
Watu wa Madhehebu ya SUNNI mwaka 2007 walikuwa milioni 3.8 baada ya Saddam ambaye pia alikuwa Sunni kunyongwa. Hawa wako Magharibi.
Wakurdi, ambao Saddam alidaiwa kuua walikuwa milioni 4.4 nao wanaishi Kaskazini  Mashariki mwa Ninawi,ule mji mkubwa aliokwenda kuhubiri Nabii Yona akamezwa na Nyangumi!
 Washia, nao ni milioni 8.4 wanaishi Babeli hadi Kusini Mashariki mwa nchi. Mjini Baghdad na Kati kati mwa nchi kuna watu wa dini mchanganyiko wapatao milioni 9.2.
Najaf na maeneo ya utajiri wa mafuta ni maeneo ya Washia ambao wamewekewa chuki na SUNNI,huku Bush,Obama na hata Mitt Romney(Mgombea wa Republican) wanaweza kuhangaika kurejesha amani,bila mafanikio…ni vita hadi kiama!
Dola lenye nguvu kandoni mwa Mto Frati,lilikuwa limevunjika ili kutoa nafasi kwa madola ya Mashariki kuungana na NATO na European Common Market, ama EU ili kuungana na Marekani kuandaa serikali moja ya Dunia.Huku ndiko kukauka kwa Mto Frati.
 Angalia nchi zilizo Mashariki mwa Mto Frati:Pamoja na nchi zilizokuwa katika Muungano wa Kisovieti(USSR), na Afghanistan,Pakistan,China,India,Korea Kaskazini na Kusini na Japan leo zinalazimishwa ama zinaungana na Marekani kwa hiari katika biashara na katika mambo mengi.
Kabla ya VITA BARIDI kwisha, hali ilikuwa tofauti. Jumatatu, Januari Mosi mwaka 2007, Romania na Burgaria zilijiunga na NATO(Northern Atlantic Treaty Organization); ilikuwa SIKU MOJA tu,baada ya Saddam  kuzikwa. Unabii unatimia bila kukosa.
 Bado Iran na Korea Kaskazini, na Syria itavurugwa kama nitakavyoonesha punde.
Kwa mujibu wa mwqandishi wa Iran anayeishi jijini Paris, Amir Taheri, Yule gaidi wa kale, Carlos The Jackal, alisema Marekani ni “Shaytan” yaani Shetani ama Joka(rejea Ufunuo 13:11) yaani Shetani amejivika mwili wa Marekani ili kuuhadaa Ulimwengu.
 Imesemwa kwamba waumini wa dini ya Kiislam wanapaswa kuichukia Marekani kama Shetani anavyochukiwa pasipo kuulizwa!
 Nirejee kidogo katika Historia ya Carlos ingawa nimeijadili kwa utulivu mwingi katika makala zilizotangulia.
Alizaliwa Oktoba 12,mwaka 1949. Katika kitabu kiitwacho Revolutionary Islam Editions Du Rocher,2003 yeye anadai ni Muislam huko gerezani,Ufaransa.
Babaye alikuwa mwanasheria milionea wa Venezuela,nchi ya Hugo Chavez. Carlos alimkubali sana Osama bin  Laden, na alisoma Patrice Lumumba University,huko Moscow. Hiki ni Chuo Kikuu kilichoanzishwa na Shirika la Ujasusi la Urusi,KGB,ili kuwafundisha wanaharakati wan chi za Dunia ya Tatu,
 Amefanya harakati nyingi mahali pengi kwa miaka 20 hivi, Urusi ilipoparaganyika, akaanza kujificha-ficha, hadi Makachero wa Ufaransa wakaja kumkamata mjini Khartoum, Agosti 14,mwaka 1994.
Alisafirishwa chini ya ulinzi mkali hadi Paris ambako amefungwa maisha. Nataka ujue kwamba 1994 Ukuta wa Berlin uliangushwa na kuondoa Kambi mbili za watu kuashiria kwisha kwa VITA BARIDI,na Marekani kuanza kutawala Dunia,huku Carlos akakamatwa, ambaye pia alipinga mno maslahi ya Magharibi. Umeona?
 Carlos aliwahi kutabiri mambo ambayo yametokea kwa usahihi kabisa. Ametabiri Irak kujengwa upya na Marekani, ametabiri SYRIA kuvunjika vipande vipande, na sasa tunaona vita vikali baina ya majeshi ya kigeni yanayounga mkono waasi na serikali inayoungwa mkono na Urusi na China.
 Ametabiri Lebanon kuanguka na kikundi cha HEZBOLLAH kuharibiwa.Ametabiri Kossovo kuwa huru na kwamba SUDAN(sasa Kusini na Kaskazini) itafanyiwa usanii ili kusukwa upya,hili limetimia,Sudan ni mbili siku hizi.
Ametabiri Ufaransa nayo kusambaratika na kuwa vinchi vidogo-vidogo.Mwisho wa siku Carlos anadhani ni Iran na Korea Kaskazini tu zitakazompinga Marekani.Anasema vita vya kumpinga Marekani vitakuwa virefu sana, na Marekani watashinda sana, anawataka Waislam kufanya JIHAD dhidi ya Marekani kuwa Nguzo Kuu ya Uislam,swala,kufunga,Hija huko Mecca N.K
Alimpenda Sana Rais wa Algeria, Azizi Bouteflika na kumwita,”Kaka yangu mpenzi” na Osama alimwita, “Sheikh” na anaogopa Algeria nayo kumezwa na ubeberu wa Magharibi
Hata hivyo, Carlos hakujua Algeria ilishaungana na Marekani na NATO pamoja na mataifa mengine ya Kiarabu,na Israeli katika urafiki unaoitwa, Partnership for Peace.
Leo, wapo wanaharakati wanaoitwa magaidi walioanzisha JIHAD dhidi ya Marekani na washirika wake.
 Hata hivyo, unabii wa Biblia na hata Carlos tumemwona akitabiri ushindi kwa Marekani,kwani unabii wa Biblia aslani hausemi uongo.
 Tijadili kidogo dhana ya kujitoa mhanga kupambana na Marekani na mabeberu wenzake.
Ni kweli Marekani wanafanya uchafu na unyama duniani. Hata hivyo kwa Wakristo,kupambana na adui kwa kumuua ni dhambi,maana Yesu alikataa chuki na uadui,sembuse kujitoa mhanga?
 Tazama Mathayo 5:43-48 na hata ule ujumbe wa Yesu kwa Petro kurejesha kisu halani mwake.
0786 324 074

MISRI HAMKANI SI SHWARI TENA

KUNA masuala machache tunayofanana na Misri.
Msri na mataifa ya Waafrika Weusi,tunasafiri katika barabara moja kurejea katika utumwa wa kidini,kiuchumi,kitamaduni na kisiasa.
Bahati mbaya sana!
Wakati mataifa ya rasilimali nyingi yanarejea katika utumwa,wananchi wake wana kiu ya mabadiliko ya serikali zao,mabadiliko ya siasa na kijamii pasipo kujua mabadiko haya yana athari gani kwao?
Watu wengi katika Afrika wana kiu ya maisha bora pasipo kujua atayaleta shetani ama mfadhili wa aina gani! Ufadhili. Kila kitu ufadhili,hakuna ujamaa na kujitegemea tena.
Matokeo yake Afrika inakwenda kasi kurejea utumwani,inarejea katika mapinduzi baada ya mapinduzi,yawe ya raia dhidi ya serikali, ya wanajeshi dhidi ya serikali za kiraia, ama jeshi na raia kwa upande mmoja dhidi serikali za kiraia kama ilivyotokea Misri.
Naam, hii huitwa struggle for freedom, harakati ambazo sasa ni za uhuru ndani ya nchi huru,uhuru dhidi ya uhuru bandia ili kurejea katika ukoloni.
Uhuru wa kwanza(1950-1970) ulidhaniwa ungeboresha uchumi,siasa na jamii ikashindikana,leo tunasema ilikuwa uhuru wa kuondoa Wakolobi Wazungu ili waingie wakoloni Weusi!
Serikali za vyama vya uhuru zilipambana na ukoloni mamboleo ukashindwa kufikia malengo.Rasilimali za nchi hazikugawanywa vizuri.Kada ya watawala walijipa kipaumbele,wakasaua tabaka la watwana,walalahoi.
Tutaondokaje katika shida hii,vijana sasa wakipata ufadhili toka nje,wanataka kununua bunduki ili kupambana kwa lengo la kujikomboa!
Bunduki na fedha kutoka Magharibi,ili kujikomboa dhidi ya Mkoloni Mweusi! Hakuna anayejali matokeo ya Wazungu kufadhili vita na fujo Afrika,atakuja nani kutawala?
Swali,tukipigana vita kali kuondosha serikali za vyama vya uhuru kwa msaada wa Mzungu,tutamlipa nini kama siyo rasilimali hizo anazochukua sasa kupitia uwekezaji?
Ni kweli mafisadi na wakoloni weusi hutorosha mali kwenda Ulaya na Marekani,sawa. Tukiwaondoa kwa vita kama Tunisia,Misri,Libya n.k tunawalipa nini wafadhili wetu? Au tunadhani wanatupenda sana?
Tufikiri vizuri,njia bora ya uhuru wa kweli.Ndiyo tunaona vyama vya siasa vinatamani kuanzisha majeshi eti kujilinda. Ukweli ni kuanzisha majeshi ili kupambana kukamata dola na rasilimali.
Ukichunguza kwa makini unaona sote tunakumbatia utegemezi wa Metropolitan Power kufanikisha malengo ya kwenda au kusalia Ikulu,kwa lengo la kufaidi rasilimali na madaraka!
Vyama halisi vya kumkomboa Mwafrika sasa havipo.tuambizane ukweli,kuna vyama vya malengo tofauti ya kushika dola na wala siyo kuleta ukombozi wa kweli wa Bara hili na watu wake kutoka kwa wakoloni mamboleo.
Mataifa haya yanayojidai sasa wafadhili na wawekezaji hayajasahau nia yao ya kuitawala Afrika na kujichotea rasilimali na rasilimali watu.
Ubinafsishaji ni sera za IMF na Benki ya Dunia(WB) zilizoanzishwa baada ya Vita kuu ya Pili ya Dunia.
Sasa,ni vita ya sisi kwa sisi,kila mtu na staili yake ya kumpelekea Mzungu rasilimali na madini,mafuta,gesi,wanyamapori,mazao ya kilimo n.k
Umwagaji wa damu unatumiwa sasa ili kuuza bunduki na kubadilishana kwa madini ama nishati na nguvu kazi ya chee.
Watu wanaomba vita viendelee Afrika ili hata hao wanaotaka kuanzisha majeshi katika vyama wagawane maeneo ya rasilimali na kuuza Ulaya na Marekani,kama wanavyofanya Waasi wa Uganda na Rwanda huko Congo(DRC).
Ni vita kama vya RUF dhidi ya serikali ya Sierra Leone miaka ya 1990-2000 ili kuchota almasi kwa damu ya raia.
Nataka kuseka kwamba ‘social revolution’ siyo kuunda jeshi ama kuchukua silaha na kuuana! Njia sahihi ni kulinda maslahi ya taifa nay a kila mwananchi kwa njia za haki bila kunyang’anya maisha ya watu ama umwagaji damu.
Hili la kwanza,Pili National Interests siyo kupambana jino kwa jino kama Chad,Misri,Libya.Mali n.k
Hizi dola kubwa,Urusi,Uchina,Marekani,Uingereza,Ufaransa n.k wakati Fulani hukubaliana kutugombanisha ili waendelee kuchota rasilimali na kufanya biashara ya bunduki kwa kubadilishana na mafuta,pembe za ndovu,dhahabu, almasi n.k
Kama hujui hili,jiulize silaha kwa waasi wa Congo hutoka wapi? Nani hulipa mishahara ya Waasi misituni? Nani huwapelekea maji na mafuta?
Kama hujui,ni kwamba Waasi hukamata eneo lenye manufaa ya biashara haramu ya magendo.Mataifa makubwa lao moja-kutuchonganisha.
Ni hapa ninapoona haja ya Waafrika kuwa na vyama vya siasa kwa lengo la kushindana kwa sera nzuri na kamwe siyo kugombania madaraka ya kushika dola ili kugawana rasilimali.
Hiki ndicho chanzo cha mapinduzi mapya katika Afrika.
Misaada ya Ulaya, “The Myth of Aid” katika vyama hivi vya siasa ndiyo nguvu yao ya kuleta vita na kuanzisha majeshi mapya ili kuwafunza vijana vita,ili kufikia malengo ya kushika dola,na kamwe si kumkomboa Mwafrika!
Hakuna ajenda ya kuondoa rasilimali zetu mikononi mwa wageni ili kujikomboa, ni kupambana kwa namna yoyote-hata kwa gharama za damu za wananchi-ili kushika ama kusalia madarakani ili kujineemesha!
Hakuna jipya katika vyama vyenu hivi vya siasa.Ajenda za ukombozi za kweli za akina Nyerere,Mandela na wenzake hakuna siku hizi.
Adui yetu Mkoloni,pande zote zimemgeuza Mfadhili na mshauri katika medani ya vita vya umwagaji damu.Akitoka Mwingereza kumfadhili Amin kuua watu anakuja Mrusi na kambi yake!
Hakuna jipya.Mursi na Adly Mansour wote wana wafadhili wao,kama si Warusi ni Waingereza na Wamarekani na wote lengo lao ni rasilimali na cheap labour kwa wananchi wetu.
Ni kufuatia hali hii Afrika bado haiko huru na inakwenda njia isiyo sahihi,watu wanaposhangilia,vyama siyo masihi.
Bungeni,vyama vya siasa na NGOs kumejaa mafisadi wanapaza sauti kusema serikali ni mafisadi.
Utashangaa kuona vyama vya waandishi wa habari mikoa na NGO za wajanja wanaojidai vyama vya wanahabari,wajidai kukemea ufisadi, huku wenye viti wanapowaita nyumba ndogo zao na ndugu zao kugawana posho za Pres conference!
Watu wanapandia katika ulaji kwa migongo ya wanahabari,wanunua magari na kuwanunulia nyumbandogo magari ya fahari huku wakiimba, “Mafisadi!”
Kawimbo ‘Mafisadi’ huibwa na watu wanaonuka mithili ya kwapa la shetani!
Hii ndiyo tabu! Hatujui adui yetu ni nani? Shetani naye anamtukana Shetani! Mwisho tutamalizana tusipojisahihisha ili kujua adui yetu ni nani? Ni rushwa,ni ufisadi na kila fisadi katika jamii,na siyo waliomo serikalini tu,wengine tunao hata humu kweye habari.
Akitoka fisadi anaandaa mkewe naye kurithi NGO na serikali ziko hivyo.Museveni-Janet-Muhoozi Trinity Power.
Hawa madikteta wako kila mahali siyo serikalini tu, bahati mbaya sana hawajui kuwa hawajui kwamba ni mafisadi na waporaji wa haki za wenzao.Wanadhani mafisadi na madikteta ni wa serikalini tu,hata vyama vya siasa ni mali za watu Fulani,mkikosana wanakutimua!
Wanachama hawana nguvu wala sauti.Hakuna full democratic liberties.Mtoto,mjukuu,shangazi, ndiyo huruhusiwa kukamata mamlaka.Kuongoza vyama.
Akina Nasser,Obote,Nyerere,Nkrumah walijaribu kujenga usawa wakashindwa,waliondoka wakaingia akina Amin Dada katika kila Nyanja ya maisha. Kinachoendelea ni uongo wa propaganda,na hakuna hatua kuelekea uhuru wa Mwafrika! Upendeleo na unyama. Hakuna jipya.
Ni kumalizana,kukanyagana,kuandamana kila asubuhi. Utumwa ni utumwa,hauna rangi!
Itaendelea
0786 324 074
 
AMIN DADA

KANALI Muammar al-Gaddafi, alimpa msaada wa mkijeshi na kifedha Nduli Iddi Amin Dada wa Uganda.
Mwaka 1974,Wafaransa walitengeneza ‘Documentary’ iitwayo, ‘General Iddi Amin Dada’ iliyoonesha Amin alipokuwa akipanga mipango mahsus ya kuivamia Israeli.
Eti, angetumia skari wa miavuli,mabomu na watu wanaojitoa mhanga.Wakati huo alipewa silaha na Muungano wa Kisovieti(USSR);wakati Ujerumani Mashariki(Berlin) walimsaidia Amin kuimarisha GSU na kile kikosi cha kifo, The State Research Bureau(SRB)kilichosulubu wapinzani.
Wamarekani walisitisha msaada kwa Amin, ambaye alianza kugeukia ulimwengu wa Kiarabu.
Amin aliwaruhusu Wapalestina kuwashikilia mateka 83 wa Kiisraeli na baadhi ya wafanyakazi wa ndege, Air France Air Bus.
Operesheni ya kuwakomboa mateka wa Israeli, Operation Thunderbolt, ilifanyika usiku wa Julai 3,kuamkia Julai 4 mwaka 1976.
Makomandoo wa Israeli waliteka Entebbe ili kumfungia kazi Amin aliyekuwa amelala usingizi mjini Kampala,kilomita 27 kutoka hapo Entebbe.
Mateka watatu waliuliwa katika Operesheni hiyo na wengine 10 walijeruhiwa.Wateka nyara saba walifagiliwa kwa risasi za makomandoo wa Kiisraeli waliojipenyeza katika jengo walimokuwa mateka,wakaongea Kiyahudi.
“Wote laleni chini”,Yule ambaye alisita kutekeleza amri hata kama alikuwa Muisraeli alifagiliwa kwa risasi haraka sana!
Askari 45 wa Amin walipigwa risasi na makomandoo hao katika Operesheni ya dakika 90 tu(The 90 minutes at Entebbe).
Komandoo mmoja wa Israeli,Jonathan ‘Yonnie’ Netanyahu aliuliwa na askari wa Amin.Huyu Yonnie ni kakaye mkubwa Waziri Mkuu wa sasa wa Israel,Benyamini Netanyahu.
Mama mmoja, Dora Bloch(75) aliyekuwa amekwamwa chakula kooni, alilazwa katika Hospitali ya Mulago siku hiyo makomando walipofika Entebbe usiku.
Amin kwa hasira, alimfuata asubuhi hapo hospitalini akamuua mama huyo kinyama ili kulipa kisasi.Alimuua pia Muingereza mwenye asili ya Kiyahudi ambaye alikuwepo pia hapo Mulago,mjini Kampala.
Serikali ya Uingereza ilifunga uhusiano wa kibalozi mjini Kampala.
Silaha za Amin zilitoka Urusi kupitia Bandari ya Mombasa, baadaye Kenya wakaanza kumwekea mizengwe, na uhusiano wa kibalozi baina ya Kenya na Uganda ukawa mashakani.
Mwaka 1976 alitamka kwamba eneo la kati la Kenya na hata kilomita 32 ndani ya Nairobi lilikuwa eneo la Uganda zama za ukoloni wa Kiingereza.
Juzi,tulisherehekea siku ya mashujaa,na kuwaenzi askari wetu takriban 620 waliopoteza maisha katika vita vya Kagera vilivyomchakaza Amin hadi akatimkia Saudi Arabia.
Amin aliivamia nchi yetu Novemba 1978, na ilipofika Aprili 11 mwaka 1979 Kampala ilikwishatekwa na majeshi ya Tanzania.
Sherehe za Kumbukumbu ya vita hivi zilihudhuriwa na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania, Jakaya Kikwete, ambaye ameonya kwamba bado tuna nguvu nyingi za kumchakaza adui yeyote atakayejitia uchokozi kama Nduli,Joka Kuu Amin.
Askari 100,000 wa Jeshi la Tanzania(TPDF) waliungana na vikosi vya Waganda waliompinga Amin, baada ya kukaa kikao chao mjini Moshi(The Moshi Conference) wakaunda kikosi,The Uganda National Liberation Army ,na kumfungia kazi Amin.
Vita vilianza rasmi Oktoba 30 mwaka 1978 ili kumwondoa Kyaka alikokuwa amevamia na kufanya unyama mkubwa huko Kagera.
Awali, jeshi la Tanzania lilikuwa na skari kama 40,000 tu;wakaongezwa wanamgambo,polisi, JKT n.k hadi kufikia askari 100,000.
Yoweri Museveni, sasa Rais wa Uganda,wakati huo aliongoza kikosi maalum cha FRONASA,na Tito Okello na David Oyite Ojok,waliongoza kikosi kingine.
Kulikuwa na vikosi vingine kama Save Uganda Movement; hiki kikiongozwa na p’Ojok,William Amaria na Ateker Ejalu.
Sisi Tanzania wakati huo tukivurumisha makombora ya Katyusha ama BM ya Kirusi ambayo yalipopigwa KAMPALA walihaha wakasema walipigwa na Mwalimu Nyerere mwenyewe kutokea viwanja wa Sabasaba,Dar.
Gaddafi ambaye sasa maiti yake inaota kaburini, baada ya kufanyiziwa na Wamarekani alituma askari 2,500 ili kumsaidia Amin Nduli Joka kuu.
Waarabu hawa walichapwa katika mstari wa mbele wa mapambano, wakatekwa nyara wengi tu.Gaddafi alimpa Amin silaha kama vifaru,T-54 na T-55,BTR APCs,BM-21,Grand MRLs,artillery,MiG-21 na TU-22 Bomber.
Turejee kidogo Entebbe,usiku wa kuamkia Julai 4,mwaka 1976.
Muda kitambo baada ya makomandoo 100 washirika wa Mossad,kumtia adabu Amin,Marekani walituma ndege Uganda,naam Entebbe, ili kuwasaidia majeruhi wa Operesheni ile kamambe.
 Unajua, maofisa 53 wa Ubalozi wa Marekani walishikiliwa na wanamgambo wa Kiislam mjini Tehran,huko Iran.
Wateka nyara wa Kipalestina waliuliwa katika tukio hilo la Entebbe, na kabla ya kukumbwa na mauti walisikika wakitaka Israeli iwaachie huru Wapalestina 40 walioshikiliwa nchini Israeli.
Hadi sasa akina Mahmoud Abbas na Benyamin Netanyahu, wanazungumza hay o hayo hata baada ya kifo cha Yasser Arafat.
 Naam vita vya kisasi vya miongo mingi.
Hadi sasa Israeli  inapambana na wanamgambo wa Kipalestina, na wakati mwingine ndege zimetekwa ama zimejaribiwa kulipuliwa angani-VITA VYA KISASI.
 
Kamanda wa Operesheni ya Entebbe, Muki Besta, alikiri kwamba Operesheni ya Entebbe ilifanikiwa kufuatia ukusanyaji wa data nyingi na muhimu wa Mossad.
Vita vilivyokuja kupiganwa hadi Rntebbe Julai 3,mwaka 1976 ili kuwakomboa mateka 103 wa Israeli,tumewaona makomandoo 100 walioandaliwa vema na Mossad wakimkomesha Mwarabu na rafiki yao Amin Dada.
Naam, vita vya dakika 90 tu, The 90 minutes at  Entebbe.
Kwa Israeli, Waziri Mkuu anayekuliana na Waarabu ili kuleta amani anauliwa kama Yizak Rabin aliyepigwa risasi Novemba 4 mwaka 1995.
Itaendelea
0786 324 074
 
MAREKANI NA UBEBERU

Hizi ni zama za kugombea rasilimali chache zilizobaki hapa duniani,baada ya watu kuzidi kuongezeka sana,hususan Afrika,kufuatia UKIMWI kushindwa kuwafyeka Weusi wote kabisa.
Kuna madai kwamba Virusi vya Ukimwi vilitengenezwa katika Maabara za Kijeshi huko Marekani,chini ya usimamizi wa akina Henry Alfred Kissinger.Hili liliweke kiporo,tutalijadili baadaye.
Katika sehemu ya mwanzo wa mfululizo wa makala hizi,tuliona Marekani inayojidai sana kuhimiza haki za binadamu, usawa wa kijinsia,haki za wanawake n.k ikiwa haijawahi kuongozwa na Mwanamke miaka takriban 240 tangu uhuru.
Tukawaona akina Yingluck Shinawatra wa Thai, wakiongoza, akina Christina Kirchner huko Argentina, Ellen Johnson Sirlief na Joyce Banda hapa Afrika, akina Dilma Rousef huko Brazil, akina Christina Lagarde wanaoongoza Fuko la Fedha(IMF) ,Asha Rose Migiro amekuwa Naibu Katibu Mkuu UN,Michelle Bechelet amekuwa Rais Chile tangu Januari, 2006.
Wapo akina Angela Merkel, na Margaret Thatcher huko Ulaya, lakini Marekani mwanamke hajawahi kuchaguliwa kuwa Rais,na sasa wapo marais 44.
Demokrasia, husemwa kuanzia Ugiriki,lakini hata Wagiriki hawakuruhusu mwanamke kupiga kura wala kupigiwa kura, sembuse kuongoza?.
Leo, demokrasia hiyo ya Kigiriki huonekana kuwa na viraka vikubwa sana kwa kuwanyima akina mama kuwa viongozi,na hata kuwakataza  kupiga kura.
Ndivyo walivyofanya Taliban huko Afghanistan, wakaonekana wa ajabu sana! Kumbe, kuna namna nyingine ya ukandamizaji hata Ulaya na Marekani, lakini nani awaambie?
Wao huiona Afrika,Asia na Amerika Kusini kwamba ndiko kwenye mbinyo wa demokrasia,kumbe nyani haoni kundule!
Si bahati mbaya, ni kusudi kuikamata dunia na kuiburuza watakavyo.
Katika Ujnabii wa Biblia,katika Ufunuo wa Yohana 16:12 kumetabiriwa ‘Roho Tatu za Vyura’ ambazo ni ‘Utatu Mtakatifu’ bandia hapa duniani, zikitoka kinywani mwa Shetani na kuwalazimisha Wakuu(Marais,Mawaziri Wakuu,Wafalme n.k) kuandaa vita dhidi ya Mungu Mwenyezi.
Chura ni alama ya uchafu katika Misri ya kale, ambayo sasa tunaona jeshi likipindua demokrasia, kwa risasi za moto mkali kushinda hata zama za Saddam,Gaddafi na madikteta wenzao.
Chura alikuwa nembo ya mungu mke,Heget, aliyeaminiwa kuwa chimbuko la uhai kwa watoto wanaozaliwa-vijana.
Huu Utatu Mtakatifu(Evil Trio) wenye sura ya vyura wa Misri, unavaa umizimu,uasi wa kidini, na ile hali ya vijana kuona DHAMBI(Uasi wa sheria ya Mungu) kama si kitu kikubwa!
Watoto wa siku hizi wenye haki za Kimarekani za kutokanywa wafanyapo makosa(Haki za Watoto), haki bandia za akina mama n.k huleta uhuru dhidi ya Mungu.
Mungu angejulikana mji anaokaa vijana wangeandamana hadi mlangoni,ili kumdai ajiuzulu na afungwe jela kwa kuweka sheria(kandamizi?) za kuwanyima uhuru wa kufanya wapendavyo!
Obama na David Cameron(umri wao sawa na wangu) wanajiona vijana sana wa siku hizi, hata hawaoni ushoga na usagaji kuwa ni tatizo, bali tatizo ni watu kunyimwa haki,uhuru na demokrasia!
Mila za Afrika zinaheshimu sana ndoa ya watu wa jinsia tofauti(Heterosexual couples), wanaamini Adamu na Hawa waliumbwa na Mungu mwaka 4004 BC kwa sababu na maakusudi muhimu ya kuanzisha familia.
Roho Tatu za vyura zinapinga kwa dhati ndoa kuwa ya mume na mke tu, bali hata ya mume na mume au mke kwa mke,mradi wamekubaliana-huu ni     Uhuru kamilifu!
Akina Obama,David Cameron,Blair na wenzao, wamewapongeza sana wanaume waliofunga ndoa na waume wenzao kwa uhuru wao wa kikatiba,na hata wamelazimisha Afrika ibadili katiba ili kuruhusu ushoga na usagaji kama inajitakia mema kwa mataifa haya.
Naam, kama Afrika inataka uchumi wake ukue na kuwe na amani na usalama kisiasa,kijamii na kiuchumi.na kiroho bila shaka.
Siku hizi watoto huzaliwa kwenye chupa za maabara(test tube babies) na mwanaume aweza kubadili jinsi kwa operesheni akawa mwanamke,akaolewa akazaa!
Hii huitwa transgender, na kuna sayansi ya human cloning, sasa Mungu naye wa nini sheria zake?
Leo, Afrika wazee ni wachache,vijana wanaotazama mitandao ya twitter na face book ndiyo wengi,ikipigwa kura ya kumkataa Mungu,inafanikiwa na inazidi kufanikiwa sana.
Akina Thomas Batie waliozaliwa Hawaii mwaka 1974 wakiwa wanawake,wakiitwa Tracy Logondino, walishabadilika na kuwa baba,sasa unasemaje?Demokrasia.
Kibaya zaidi, demokrasia ya Ulaya na Marekani hulazimishwa kufuatwa na ulimwengu wote.
Ukitaka kubadili jinsi unachomwa sindano zenye hormone(testosterone injections) kama ni msichana unapata sauti nzito,nywele fupi,unawekewa uume kwa operesheni,basi unakuwa dume jike!
Unaondolewa matiti kwa operesheni(Mastectomy), ukitaka uke au uume unaondolewa basi –ndiyo uhuru huu.
Hapa Afrika,kuna NGOs nyingi za kutetea mambo haya,serikali inapopinga inaonekana ya Kiimla,isiyojali  Haki za watu na vijana wanaanza kuandamana na kupinga serikali,kama huko Misri,Libya,Tunisia,Yemen n.k
Na viongozi wanaopinga sera za Ulaya wanapinduliwa na kuswekwa rumande kwamba mafisadi, wananyimwa misaada,uchumi unakuwa mbaya sana,vijana wana ‘riot’ nguvu iitwayo ya Umma inafanya kazi!
‘Nguvu ya Umma’ aghalabu ni Nguvu ya Utatu Mtakatifu(Evil Trio);nguvu hiyo husukumwa na umizimu wa kutisha-spiritualism.
Uhuru wa ngono,picha za uchi, wanawake kujiuza,ukahaba wa kutisha,ushenzi ndiyo uhuru unaopendwa mno na vijana,na uhalifu;hawa wangependa magereza yasiwepo,hata kodi hawataki kulipa,ila waishi maisha ya raha bila kujua pesa zitatoka wapi?
Nimejadili ukoloni mpya-neo colonialism-kupitia kutekwa nyara rasilimali zetu ili sisi tupatiwe msaada na IMF na WB,G-8,G-20 nk
Kwa akili hizi za kukosekana uzalendo,zama za utandawizi,hakuna mzalendo atakayezaliwa Afrika, bali kufanyika weusi wa Magharibi(Westernization) , na watu vijana wametimka vijijini kujaa mijini(Urbanization) ili iwe rahisi kuwateka kwa kampeni za wanasiasa na NGOs za Ulaya na Marekani!
Hamkani si shwari katika nchi za Kiarabu(Unrest in Arab Countries) huashiria Yemen,Misri,Libya,Syria,Irak, Oman,Mauritania,Saudia,Jordan,Tunisia n.k asiwepo wa kupinga utandawazi kwa kisingizio cha dini n.k
Nchi ambazo hakuna migogoro kama Qatar,Kuwait,UAE,Lebanon na Bahrain ujue viongozi wake wameafiki kimya kimya ajenda za wakubwa wa dunia,na raia hawana ubishi.
Rasilimali na kila kitu kinakwenda Ulaya bila taabu, inapotokea shida vita huanza na vijana hutumika kupinga serikali na kuanzisha ghasia na machafuko nchi nzima.
Marekani siku hizi huhimiza sana uhuru na demokrasia, FREEDOM of worship, freedom of speech, rule of law, equal rights for all-ndiyo ushoga na usagaji!
Sasa ikianzishwa dini ya kusali vijana na wasichana wakiwa uchi wewe ujidai kuikataa na kuwatia mbaroni uone. Tuendako hakutakuwa na ndoa tena,bali ni ngono holela tu na kuzaa vitoto visivyo na baba na mama zao walishakwenda danguro kujiuza,basi shetani analetea NGOs fedha za kulea yatima,zinaliwa, serikali ikisema inapingwa!
Sitetei mafisadi na wauza unga wa serikalini, bali nazungumza NGOs zinazojidai kutetea wanahabari kwa mfano,zinaombwa fedha nyingi Ulaya,vinaanzishwa vijiwe vya siasa kuipinga serikali maana inabinya demokrasia(ushoga,usagaji,uchafu),waandhi wa habari wametumika kuwabeba hawa migongoni mwao,siku hizi wana fedha,wana magari ya fahari kwa wizi na utapeli,ili mradi serikali ipingwe,Wazungu walete hela.
Dunia inaandaliwa kwa vita iitwayo Armageddon (tazama Zaburi sura ya 2).
“Anti Christ” and His Western Allies, wanajiandaa kwa vita dhidi ya haki halisi na ukweli,nchi zote na watu wote hawana budi kukubali.
Siasa ni Ulaya na Marekani,uchumi wa Kimarekani, rasilimali ziende Marekani, maisha na lugha,mila na desturi vya Ulaya na Marekani, na viongozi wawe wale wanaopendwa naUlaya na Marekani!
Nchi zetu zimebinafsishwa Marekani na Ulaya,na akina mama hawataki uafrika tena, mara ‘makalio ya Kichina’ mawigi ya Magharibi,wanakula Kimagharibi siku hizi Mwafrika halisi kama Mandela hayupo!
“Middle East” the focal point of the World damu yao itatiririka kama mto ili kuwavua akili za Kikomunisti(Ukomunisti ni ile hali ya rasilimali zote kumilikiwa na jamii,nchi na serikali ina dhibiti uchumi), na akina sisi tulielekea Usoshalisti(mfumo ambao uliipa nafasi jamii nzima kuwa wabia ama wamiliki wa rasilimali na njia kuu za uchumi kama usafiri n.k).
Akili zetu zinaondolewa kutoka ukomunisti na usoshalisti,ili tuishi kutazama kila kitu kutoka Ulaya,Marekani,tukiwadhania wajomba na ndugu, sisi tulishasahau kujitegemea-ni michongo tu,rushwa,ufisadi na ‘kupiga hela’ bila kujua zinatoka wapi?
Halafu kelele na kushabikia kila ujinga kutoka kwa  wanasiasa,Ulaya,Marekani n.k mradi kimesemwa,na hakuna tafakuri tunduizi!
Kufuatia hali hii,nchi inabaki haina kitu,mali inakwenda,viongozi nao wanakuwa watumwa wa sera za Ulaya,raia wanavaa mawigi na kutamani wawe Wachina au Wazungu!
Majina kama ya akina Mandela sasa yanapigwa marufuku,unazaa motto unamwita jina la Mzungu,makalio ya Kichina,nywele za Kizungu, kuongea lugha isiyoeleweka,nguo za Masela wa Kimarekani,wabwia unga,Malaya!
 Taifa gani tunajenga? Akili gani hii, yak u compromise na Mzungu(hata Mzungu wa unga) hata hatuna chetu?
Akitokea kiongozi wa kuwapinga Wazungu, anapingwa sana kwa maaandamano ya umma huku tukisema ni nguvu ya umma, anakamatwa na kuwekwa kizuizini,watu wanashangilia,misaada inamwagwa-tunacheka!
Vema tukaanza kufanya mapinduzi yakifikra ili tutambue wapi tunakwenda? Tuna viongozi sampuli gani? Raia wa akili gani hawa, jamii gani hii tunajenga sasa?
Halafu tutajua kuipinga Marekani na ubeberu wake wa kutaka kutupora tangu rasilimali hadi tamaduni,mila na kila tulichonacho!
0713 324 074

Monday, July 22, 2013

MISRI NA DEMOKRASIA YA AFRIKA