KANALI
Muammar al-Gaddafi, alimpa msaada wa mkijeshi na kifedha Nduli Iddi Amin Dada
wa Uganda.
Mwaka
1974,Wafaransa walitengeneza ‘Documentary’ iitwayo, ‘General Iddi Amin Dada’
iliyoonesha Amin alipokuwa akipanga mipango mahsus ya kuivamia Israeli.
Eti,
angetumia skari wa miavuli,mabomu na watu wanaojitoa mhanga.Wakati huo alipewa
silaha na Muungano wa Kisovieti(USSR);wakati Ujerumani Mashariki(Berlin)
walimsaidia Amin kuimarisha GSU na kile kikosi cha kifo, The State Research
Bureau(SRB)kilichosulubu wapinzani.
Wamarekani
walisitisha msaada kwa Amin, ambaye alianza kugeukia ulimwengu wa Kiarabu.
Amin
aliwaruhusu Wapalestina kuwashikilia mateka 83 wa Kiisraeli na baadhi ya
wafanyakazi wa ndege, Air France Air Bus.
Operesheni
ya kuwakomboa mateka wa Israeli, Operation Thunderbolt, ilifanyika usiku wa
Julai 3,kuamkia Julai 4 mwaka 1976.
Makomandoo
wa Israeli waliteka Entebbe ili kumfungia kazi Amin aliyekuwa amelala usingizi
mjini Kampala,kilomita 27 kutoka hapo Entebbe.
Mateka
watatu waliuliwa katika Operesheni hiyo na wengine 10 walijeruhiwa.Wateka nyara
saba walifagiliwa kwa risasi za makomandoo wa Kiisraeli waliojipenyeza katika
jengo walimokuwa mateka,wakaongea Kiyahudi.
“Wote laleni
chini”,Yule ambaye alisita kutekeleza amri hata kama alikuwa Muisraeli
alifagiliwa kwa risasi haraka sana!
Askari 45 wa
Amin walipigwa risasi na makomandoo hao katika Operesheni ya dakika 90 tu(The
90 minutes at Entebbe).
Komandoo
mmoja wa Israeli,Jonathan ‘Yonnie’ Netanyahu aliuliwa na askari wa Amin.Huyu
Yonnie ni kakaye mkubwa Waziri Mkuu wa sasa wa Israel,Benyamini Netanyahu.
Mama mmoja,
Dora Bloch(75) aliyekuwa amekwamwa chakula kooni, alilazwa katika Hospitali ya
Mulago siku hiyo makomando walipofika Entebbe usiku.
Amin kwa
hasira, alimfuata asubuhi hapo hospitalini akamuua mama huyo kinyama ili kulipa
kisasi.Alimuua pia Muingereza mwenye asili ya Kiyahudi ambaye alikuwepo pia
hapo Mulago,mjini Kampala.
Serikali ya
Uingereza ilifunga uhusiano wa kibalozi mjini Kampala.
Silaha za
Amin zilitoka Urusi kupitia Bandari ya Mombasa, baadaye Kenya wakaanza kumwekea
mizengwe, na uhusiano wa kibalozi baina ya Kenya na Uganda ukawa mashakani.
Mwaka 1976
alitamka kwamba eneo la kati la Kenya na hata kilomita 32 ndani ya Nairobi
lilikuwa eneo la Uganda zama za ukoloni wa Kiingereza.
Juzi,tulisherehekea
siku ya mashujaa,na kuwaenzi askari wetu takriban 620 waliopoteza maisha katika
vita vya Kagera vilivyomchakaza Amin hadi akatimkia Saudi Arabia.
Amin
aliivamia nchi yetu Novemba 1978, na ilipofika Aprili 11 mwaka 1979 Kampala
ilikwishatekwa na majeshi ya Tanzania.
Sherehe za
Kumbukumbu ya vita hivi zilihudhuriwa na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya
Tanzania, Jakaya Kikwete, ambaye ameonya kwamba bado tuna nguvu nyingi za
kumchakaza adui yeyote atakayejitia uchokozi kama Nduli,Joka Kuu Amin.
Askari
100,000 wa Jeshi la Tanzania(TPDF) waliungana na vikosi vya Waganda waliompinga
Amin, baada ya kukaa kikao chao mjini Moshi(The Moshi Conference) wakaunda kikosi,The
Uganda National Liberation Army ,na kumfungia kazi Amin.
Vita
vilianza rasmi Oktoba 30 mwaka 1978 ili kumwondoa Kyaka alikokuwa amevamia na
kufanya unyama mkubwa huko Kagera.
Awali, jeshi
la Tanzania lilikuwa na skari kama 40,000 tu;wakaongezwa wanamgambo,polisi, JKT
n.k hadi kufikia askari 100,000.
Yoweri
Museveni, sasa Rais wa Uganda,wakati huo aliongoza kikosi maalum cha FRONASA,na
Tito Okello na David Oyite Ojok,waliongoza kikosi kingine.
Kulikuwa na
vikosi vingine kama Save Uganda Movement; hiki kikiongozwa na p’Ojok,William
Amaria na Ateker Ejalu.
Sisi
Tanzania wakati huo tukivurumisha makombora ya Katyusha ama BM ya Kirusi ambayo
yalipopigwa KAMPALA walihaha wakasema walipigwa na Mwalimu Nyerere mwenyewe
kutokea viwanja wa Sabasaba,Dar.
Gaddafi
ambaye sasa maiti yake inaota kaburini, baada ya kufanyiziwa na Wamarekani
alituma askari 2,500 ili kumsaidia Amin Nduli Joka kuu.
Waarabu hawa
walichapwa katika mstari wa mbele wa mapambano, wakatekwa nyara wengi
tu.Gaddafi alimpa Amin silaha kama vifaru,T-54 na T-55,BTR APCs,BM-21,Grand
MRLs,artillery,MiG-21 na TU-22 Bomber.
Turejee kidogo
Entebbe,usiku wa kuamkia Julai 4,mwaka 1976.
Muda kitambo baada ya
makomandoo 100 washirika wa Mossad,kumtia adabu Amin,Marekani walituma ndege
Uganda,naam Entebbe, ili kuwasaidia majeruhi wa Operesheni ile kamambe.
Unajua, maofisa 53
wa Ubalozi wa Marekani walishikiliwa na wanamgambo wa Kiislam mjini Tehran,huko
Iran.
Wateka nyara wa
Kipalestina waliuliwa katika tukio hilo la Entebbe, na kabla ya kukumbwa na
mauti walisikika wakitaka Israeli iwaachie huru Wapalestina 40 walioshikiliwa
nchini Israeli.
Hadi sasa akina Mahmoud
Abbas na Benyamin Netanyahu, wanazungumza hay o hayo hata baada ya kifo cha
Yasser Arafat.
Naam vita vya
kisasi vya miongo mingi.
Hadi sasa Israeli inapambana na wanamgambo wa Kipalestina, na
wakati mwingine ndege zimetekwa ama zimejaribiwa kulipuliwa angani-VITA VYA
KISASI.
Kamanda wa Operesheni ya
Entebbe, Muki Besta, alikiri kwamba Operesheni ya Entebbe ilifanikiwa kufuatia
ukusanyaji wa data nyingi na muhimu wa Mossad.
Vita vilivyokuja
kupiganwa hadi Rntebbe Julai 3,mwaka 1976 ili kuwakomboa mateka 103 wa
Israeli,tumewaona makomandoo 100 walioandaliwa vema na Mossad wakimkomesha
Mwarabu na rafiki yao Amin Dada.
Naam, vita vya dakika 90
tu, The 90 minutes at Entebbe.
Kwa Israeli, Waziri Mkuu
anayekuliana na Waarabu ili kuleta amani anauliwa kama Yizak Rabin aliyepigwa
risasi Novemba 4 mwaka 1995.
Itaendelea
0786 324 074
No comments:
Post a Comment