KUNA masuala
machache tunayofanana na Misri.
Msri na mataifa ya Waafrika Weusi,tunasafiri
katika barabara moja kurejea katika utumwa wa kidini,kiuchumi,kitamaduni na
kisiasa.
Bahati mbaya
sana!
Wakati
mataifa ya rasilimali nyingi yanarejea katika utumwa,wananchi wake wana kiu ya
mabadiliko ya serikali zao,mabadiliko ya siasa na kijamii pasipo kujua mabadiko
haya yana athari gani kwao?
Watu wengi
katika Afrika wana kiu ya maisha bora pasipo kujua atayaleta shetani ama
mfadhili wa aina gani! Ufadhili. Kila kitu ufadhili,hakuna ujamaa na
kujitegemea tena.
Matokeo yake
Afrika inakwenda kasi kurejea utumwani,inarejea katika mapinduzi baada ya
mapinduzi,yawe ya raia dhidi ya serikali, ya wanajeshi dhidi ya serikali za
kiraia, ama jeshi na raia kwa upande mmoja dhidi serikali za kiraia kama
ilivyotokea Misri.
Naam, hii
huitwa struggle for freedom, harakati ambazo sasa ni za uhuru ndani ya nchi
huru,uhuru dhidi ya uhuru bandia ili kurejea katika ukoloni.
Uhuru wa
kwanza(1950-1970) ulidhaniwa ungeboresha uchumi,siasa na jamii
ikashindikana,leo tunasema ilikuwa uhuru wa kuondoa Wakolobi Wazungu ili
waingie wakoloni Weusi!
Serikali za
vyama vya uhuru zilipambana na ukoloni mamboleo ukashindwa kufikia
malengo.Rasilimali za nchi hazikugawanywa vizuri.Kada ya watawala walijipa
kipaumbele,wakasaua tabaka la watwana,walalahoi.
Tutaondokaje
katika shida hii,vijana sasa wakipata ufadhili toka nje,wanataka kununua
bunduki ili kupambana kwa lengo la kujikomboa!
Bunduki na
fedha kutoka Magharibi,ili kujikomboa dhidi ya Mkoloni Mweusi! Hakuna anayejali
matokeo ya Wazungu kufadhili vita na fujo Afrika,atakuja nani kutawala?
Swali,tukipigana
vita kali kuondosha serikali za vyama vya uhuru kwa msaada wa Mzungu,tutamlipa
nini kama siyo rasilimali hizo anazochukua sasa kupitia uwekezaji?
Ni kweli
mafisadi na wakoloni weusi hutorosha mali kwenda Ulaya na Marekani,sawa.
Tukiwaondoa kwa vita kama Tunisia,Misri,Libya n.k tunawalipa nini wafadhili
wetu? Au tunadhani wanatupenda sana?
Tufikiri
vizuri,njia bora ya uhuru wa kweli.Ndiyo tunaona vyama vya siasa vinatamani
kuanzisha majeshi eti kujilinda. Ukweli ni kuanzisha majeshi ili kupambana
kukamata dola na rasilimali.
Ukichunguza
kwa makini unaona sote tunakumbatia utegemezi wa Metropolitan Power kufanikisha
malengo ya kwenda au kusalia Ikulu,kwa lengo la kufaidi rasilimali na madaraka!
Vyama halisi
vya kumkomboa Mwafrika sasa havipo.tuambizane ukweli,kuna vyama vya malengo
tofauti ya kushika dola na wala siyo kuleta ukombozi wa kweli wa Bara hili na
watu wake kutoka kwa wakoloni mamboleo.
Mataifa haya
yanayojidai sasa wafadhili na wawekezaji hayajasahau nia yao ya kuitawala
Afrika na kujichotea rasilimali na rasilimali watu.
Ubinafsishaji
ni sera za IMF na Benki ya Dunia(WB) zilizoanzishwa baada ya Vita kuu ya Pili
ya Dunia.
Sasa,ni vita
ya sisi kwa sisi,kila mtu na staili yake ya kumpelekea Mzungu rasilimali na
madini,mafuta,gesi,wanyamapori,mazao ya kilimo n.k
Umwagaji wa
damu unatumiwa sasa ili kuuza bunduki na kubadilishana kwa madini ama nishati
na nguvu kazi ya chee.
Watu
wanaomba vita viendelee Afrika ili hata hao wanaotaka kuanzisha majeshi katika
vyama wagawane maeneo ya rasilimali na kuuza Ulaya na Marekani,kama
wanavyofanya Waasi wa Uganda na Rwanda huko Congo(DRC).
Ni vita kama
vya RUF dhidi ya serikali ya Sierra Leone miaka ya 1990-2000 ili kuchota almasi
kwa damu ya raia.
Nataka
kuseka kwamba ‘social revolution’ siyo kuunda jeshi ama kuchukua silaha na
kuuana! Njia sahihi ni kulinda maslahi ya taifa nay a kila mwananchi kwa njia
za haki bila kunyang’anya maisha ya watu ama umwagaji damu.
Hili la
kwanza,Pili National Interests siyo kupambana jino kwa jino kama
Chad,Misri,Libya.Mali n.k
Hizi dola
kubwa,Urusi,Uchina,Marekani,Uingereza,Ufaransa n.k wakati Fulani hukubaliana
kutugombanisha ili waendelee kuchota rasilimali na kufanya biashara ya bunduki
kwa kubadilishana na mafuta,pembe za ndovu,dhahabu, almasi n.k
Kama hujui
hili,jiulize silaha kwa waasi wa Congo hutoka wapi? Nani hulipa mishahara ya
Waasi misituni? Nani huwapelekea maji na mafuta?
Kama
hujui,ni kwamba Waasi hukamata eneo lenye manufaa ya biashara haramu ya
magendo.Mataifa makubwa lao moja-kutuchonganisha.
Ni hapa
ninapoona haja ya Waafrika kuwa na vyama vya siasa kwa lengo la kushindana kwa
sera nzuri na kamwe siyo kugombania madaraka ya kushika dola ili kugawana
rasilimali.
Hiki ndicho
chanzo cha mapinduzi mapya katika Afrika.
Misaada ya
Ulaya, “The Myth of Aid” katika vyama hivi vya siasa ndiyo nguvu yao ya kuleta
vita na kuanzisha majeshi mapya ili kuwafunza vijana vita,ili kufikia malengo
ya kushika dola,na kamwe si kumkomboa Mwafrika!
Hakuna
ajenda ya kuondoa rasilimali zetu mikononi mwa wageni ili kujikomboa, ni
kupambana kwa namna yoyote-hata kwa gharama za damu za wananchi-ili kushika ama
kusalia madarakani ili kujineemesha!
Hakuna jipya
katika vyama vyenu hivi vya siasa.Ajenda za ukombozi za kweli za akina
Nyerere,Mandela na wenzake hakuna siku hizi.
Adui yetu
Mkoloni,pande zote zimemgeuza Mfadhili na mshauri katika medani ya vita vya
umwagaji damu.Akitoka Mwingereza kumfadhili Amin kuua watu anakuja Mrusi na
kambi yake!
Hakuna jipya.Mursi
na Adly Mansour wote wana wafadhili wao,kama si Warusi ni Waingereza na
Wamarekani na wote lengo lao ni rasilimali na cheap labour kwa wananchi wetu.
Ni kufuatia
hali hii Afrika bado haiko huru na inakwenda njia isiyo sahihi,watu wanaposhangilia,vyama
siyo masihi.
Bungeni,vyama
vya siasa na NGOs kumejaa mafisadi wanapaza sauti kusema serikali ni mafisadi.
Utashangaa
kuona vyama vya waandishi wa habari mikoa na NGO za wajanja wanaojidai vyama
vya wanahabari,wajidai kukemea ufisadi, huku wenye viti wanapowaita nyumba
ndogo zao na ndugu zao kugawana posho za Pres conference!
Watu
wanapandia katika ulaji kwa migongo ya wanahabari,wanunua magari na kuwanunulia
nyumbandogo magari ya fahari huku wakiimba, “Mafisadi!”
Kawimbo ‘Mafisadi’
huibwa na watu wanaonuka mithili ya kwapa la shetani!
Hii ndiyo
tabu! Hatujui adui yetu ni nani? Shetani naye anamtukana Shetani! Mwisho
tutamalizana tusipojisahihisha ili kujua adui yetu ni nani? Ni rushwa,ni
ufisadi na kila fisadi katika jamii,na siyo waliomo serikalini tu,wengine tunao
hata humu kweye habari.
Akitoka
fisadi anaandaa mkewe naye kurithi NGO na serikali ziko
hivyo.Museveni-Janet-Muhoozi Trinity Power.
Hawa
madikteta wako kila mahali siyo serikalini tu, bahati mbaya sana hawajui kuwa
hawajui kwamba ni mafisadi na waporaji wa haki za wenzao.Wanadhani mafisadi na
madikteta ni wa serikalini tu,hata vyama vya siasa ni mali za watu Fulani,mkikosana
wanakutimua!
Wanachama
hawana nguvu wala sauti.Hakuna full democratic liberties.Mtoto,mjukuu,shangazi,
ndiyo huruhusiwa kukamata mamlaka.Kuongoza vyama.
Akina
Nasser,Obote,Nyerere,Nkrumah walijaribu kujenga usawa wakashindwa,waliondoka
wakaingia akina Amin Dada katika kila Nyanja ya maisha. Kinachoendelea ni uongo
wa propaganda,na hakuna hatua kuelekea uhuru wa Mwafrika! Upendeleo na unyama. Hakuna jipya.
Ni
kumalizana,kukanyagana,kuandamana kila asubuhi. Utumwa ni utumwa,hauna rangi!
Itaendelea
0786 324 074
No comments:
Post a Comment