Thursday, April 7, 2011

OBAMA HANA TOFAUTI NA OSAMA

Obama hana tofauti na Osama!


NIMEPATA KUSOMA mzaha katika gazeti moja litolewa ng’ambo, kwamba Obama na Osama ni mtu Yule Yule kasoro herufi mbili, “b” na “s” katikati ya majina yao!

Kulingana na lesoni ya Waadventista wa Sabato(Sabbath School Bible  Study Guide) ya Oktoba hadi Desemba, 2010 ukurasa wa 72 majina ni muhimu tangu nyakati za Biblia. Jina linamwonesha mtu tabia yake,urithi wake toka kwa wazazi wake.Mtu hufanana na jina lake.

 Wakati mwingine, jina hutafsiri kile wazazi walichotazamia au kile kilichowakabili wakati motto anazaliwa. Bila shaka umepata kusikia majina ya akina Semeni, Siwajibu, Masumbuko,Chuki,Mashaka,Majuto, Nyamayao n.k!
 Majina haya,huzungumza mazingira mtoto alimozaliwa na majaliwa yake. Majina kama Abram,Yakobo,Danieli n.k pia yalitabiri tabia ya watu hawa ya uchaji Mungu, utegemezi kwa Mungu kama Hakimu na Mwamuzi.
Yakobo, tafsiri yake ni ‘Mdanganyifu’ aliyemdanganya babaye, Isaka wakampora kakaye, Esau haki ya mzaliwa wa kwanza.

Kulingana na somo,’What’s in a Name?’ katika lesoni hiyo ya Wasabato, jina Osama,kwetu ni mtu katili; Yule gaidi hatari sana aliyesababisha majengo pacha ya World Trade Center(WTC)mjini New York kuteketea kwa mabomu Septemba 11, mwaka 2001 na zaidi ya watu 5,500 wakapoteza maisha.
Osama, katika kizazi hiki ni muuaji hata kama baadhi ya watu wanamwoma mwanaharakati, sahahidi mwaminifu, martyr!

Ni kwa sababu sababu hii tu,mtu akisema(Rais Barack Hussein)Obama anafanana na Gaidi la Kimataifa,linalosakwa sana,Osama(Bin Laden)aliyelipua pia Makao Makuu ya Wizara ya Ulinzi ya M arekani mjini Washington, “The Pentagon” nasi tunamwona leo Obama kwamba ni muuaji na katili kama Osama.
Kwamba, Obama na Osama ni mtu Yule Yule kasoro herufi ‘b’ na ‘s’ basi lingekuwa jina moja! 
Namfananisha Rais Obama wa Marekani na gazidi linalosakwa sana duniani, kwa kuhusika na ajali ya Septemba 11, hadi leo WTC haikujengwa, uwanja umeachwa kama Mnara wa Kumbukumbu ya kiama kile,na mahali hapa panaitwa, Ground Zero.

Katika mraba huu,niliwahi kuandika kwamba Waafrika hawakuwa na sababu ya kumsahangilia sana Obama, kwa kufanikiwa kukalia kiti kile cha ngozi nyeusi hapo “Oval Office” katika Ikulu ya White House,Marekani.
Kwamba, ingawa Obama,babu yake Mzee Obama alikuwa “Boy” wa Wazungu mjini Nairobi,Kenya akamzaa Hussein Obama aliyekwenda kusoma Marekani akakutana na mama Mzungu akampa ujauzito na akamzaa Barack Hussein Obama, bado Obama siyo Mwafrika.

Obama, ni Mmarekani anayetekeleza sera za Marekani za kibeberu; na lazima awe mtii kwa kiapo chake cha kulinda,kuhifadhi na kutekeleza sera za Marekani kwa maslahi ya Wamarekani,na aslani Obama hawezi kuwajua, na kuwajali Waafrika!

Naam, Obama siyo Mwafrika; ni Mmarekani. Kipaumblele chake siyo Kogelo,Kisumu, Nairobi, Afrika Mashariki,Afrika. Obama anatekeleza maslahi ya Marekani na viwanda vya Wamarekani, anajali mustakabali wa Marekani zaidi,hata kama kwa kufanya hivyo Afrika italipuka katika miali mikali ya moto.
Nadhani, sasa Afrika inameza machungu ya kumshangilia sana Obama Novemba 2008 hadi Januari 20,mwaka 2009.Obama   ana macho yanayoitazama Marekani, kamwe siyo Afrika.

Kwa sababu ya maslahi matukufu ya Marekani, Obama sharti apate kigugumizi katika mgogoro wa Cote d’ Ivoire .
Kwa sababu,Obama kwa maslahi ya Marekani,hawezi kukurupukia wimbo wa ‘Demokrasia’ ama Haki za Binadamu,kusema kwamba Alassane Ouattara,Muislam wa Kaskazini mwa nchi, aliyetangazwa mshindi wa kiti cha Urais na Tume Huru ya Uchaguzi(CEI),ati aungwe mkono kijeshi na Marekani na Washirika wake,au na Majeshi ya Umoja wa Kujihami Ulaya Magharibi,NATO(Northern Atlantic Treat Organization),dhidi ya Mkristo na kibaraka wao,Laurent Koudou Gbagbo.

Ouattara, ambaye Januari Mosi mwaka huu alitimiza umri wa miaka 70,licha ya kusoma Pennsylvania na kufanya kazi IMF,hataaminiwa na sera za Marekani za Nje, za kusaka mno maslahi pamoja na mafuta,gesi na mali ghafi kwa ajili ya viwanda vyao.

Marekani, walikenua meno hadi gego la mwisho,pale Laurent Gbagbo alipomtimua Dikteta Jenerali Robert Guei, alipotaka kung’ang’ania madarakani mwaka 2000,kwa nguvu ya umma, Peoples Power! Hii Nguvu ya Umma, haikuanzia Chadema, ilianzia Serbia pale alipotimliwa Dikteta Slobodan Milosevic, ikatua Cote d’ Ivories  kwa Jen Guei,mwaka 2000.

Jen.Robert Guei, alikuwa kaingia madarakani kwa mapinduzi wakati akiwa Mnadhimu wa Jeshi(Chief of staff).
Kiongozi wa Chama cha Kisoshalist, Gbagbo,ni Mkristo wa nyumbani kwao Guei, alikuwa mpinzani wa serikali kwa miaka 30. Bila shaka utajua uswahiba wa Marekani na wapinzani, amepata kufungwa jela.
 Mei mwaka huu, Gbagbo atakuwa anasherehekea ‘Birth Day’ ya 66 akiwa bado Ikulu ya mjini Abidjan,bila wasiwasi. Alianza kutawala Oktoba 26, mwaka 2000 baada ya ‘Wamachinga’ wa mjini Abidjan kuingia mabarabarani wakiwa na rungu, mawe,panga,mawe, matofali n.k wakachoma moto magari na majumba,jeshi likashindwa kuwafagia kwa risasi,kama ilivyotokea Tunisia,Misri na siku hizi Libya.

 Wafaransa hawa hawa wanaotaka kumwondoa madarakani Kanali Muammar al-Qaddafi, ndiyo waliomsaidia Guei kutorokea Benin,nchi ikaingia katika vita vya kidini,baina ya Ukristo na Uislam.
Polisi wa Kifaransa, The Gendarmes, walivamia nyumba ya Ouattara hadi alipotimkia ubalozi wa Ujerumani. Afadhali hata Mjerumani!

Umoja wa Mataifa na Washington wao waliomba uchaguzi urejewe,Ufaransa wakashinikiza Bunge kushika madaraka,au iundwe serikali ya Umoja wa Kitaifa(Government of The National Unity).
Mchezo uliopo Cote d’ Ivoire,ni ule ule uliokuwepo mwaka 2000 baina ya Gbagbo na Jen.Robert Guei, ama kati ya Mugabe na Morgan Richard Tsivangirai na kati ya Kibaki na Raila Odinga.

Na tabia na msimamo wa Ufaransa na Washirika wake,Marekani hauwezi kubadilika pale yalipo maslahi ya makampuni yake ndipo yalipo maslahi ya viongozi. Sera za NATO dhidi ya Abidjan na mji Mkuu wa Yamoussoukro, ni zile zile tu za kuchochea vurugu na vita ili wapate nafasi ya kupora mafuta,kokoa,mbao n.k
Na hata siwezi kuishangaa Marekani kuchochea machafuko Algeria, Yemen,Misri,Libya  n.k kwa sababu kuna mafuta!

George Soros,Mwenyekiti na Muasisi wa taasisi ya Open Society, kaandika Dibaji katika kitabu kiitwacho, ESCAPING THE RESOURCE CURSE, kilichoandikwa na Macartan Humphreys, J.D Sachs na Joseph Stglitz(Columbia University Press, New York 2007).
Kwamba, nchi tajiri za rasilimali hunyemelewa na vita,machafuko,migogoro na umasikini wa wananchi kwa sababu ya ufisadi na uchochezi toka nje.

Hawa ‘Mabwana Wakubwa’ hawawezi kukuacha hivi hivi bila kukuingilia kama una madini,una gesi, mafuta,uranium ama bahari muhimu na mito n.k
Kila penye madini,gesi,mafuta na Uranium kuna shida. Korea,HongKong, Singapote na Taiwan-Asian Tigers-zilisahauliwa kuburuzwa miaka ile ya 60 zikaendelea kiuchumi. Hazina rasilimali nyingi,lakini uchumi unapaa na hakuna maandamano.

Kwenye rasilimali, hususan Afrika,kuna vita. Angola huko Cabinda kuna mafuta na kuna vita, Congo(DRC) katika majimbo ya Shaba na Katanga kuna shaba na almasi na kuna vita. Sudan ya Kusini kuna mafuta na ndiyo chimbuko la vita.
Angalia, Yemen, Indonesia(West Papua),Myanmar(Hill Tribes) na Papua New Guinea(Boungainville) kuna shaba,dhahabu,mafuta na gesi na kuna matatizo.
Morocco huko SAHARA MAGHARIBI kuna vita, Nigeria huko Biafra na Niger Delta,kuna vita vya kugombea mafuta!

Nakupa shauri msomaji. Ukifika WHITE House,kamuulize Rais Obama,ana mpango gani wa kuhakikisha mafuta, gesi,dhahabu,shaba,almasi n.k zinawanufaisha raia wazawa wan chi husika,kuliko kuwanufaisha mafisadi wa serikalini na makampuni ya Kimarekani,Kifaransa na Kiingereza?
Ukigusa mikataba ya hila ya makampuni ya Wazungu,kwamba ni kama ile ya Carl Peters na Mangungo wa Msovero, basi utaona Obama anakuwa sawa sawa tu na Osama!
 Na ukipata kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa, kamuulize Rais Obama, ni mtazamo gani wan chi yake kuhusu Mashariki ya Kati(Mideast situation)?

Kamuulize Obama,Kwanini Marekani inazidi kuua watu kwa majanga ya asili kwa kukataa kusaini mikataba ya Kupunguza Joto Duniani kwa moshi wa viwanda vyake,kama ule Mkataba wa Kyoto,Japan?
Marekani huchangia kwa takriban asilima 50 ya gesi za sumu angani na ndiyo chimbuko la majanga ya asili-Natural calamities!

Kamuulize Obama, ule msamiati wa ‘Ocampo Six’ kufuatia Luis Moreno Ocampo kutaka                                                 Uhuru Kenyatta, Joshua arap Sang,William Rutto,Francis Muthaura, Hussein Ali, Henry Kosgei washitakiwe kwa uhalifu wa kivita, wakati Blair na Bush wakila good time,ndiyo nini? Hapa hakuna ‘Impunity’? ama ‘double standards’?

Ukifika Washington, kamuulize Obama,kwanini kuchochea vita Misri na Yemen na kumshambulia Kanali Muammar al Qaddafi huki Tripoli na Benghazi kwamba ame ‘Overstay’ wakati hawajatwambia unyama wa makampuni ya kuchimba na kusafirisha mafuta na gesi,na kutiririsha kemikali za sumu na kuua watu na wanyama migodini, Tanzania, ndiyo nini?

Kaulize,kampuni la Unocal la California lilifanya unyama gani huko Myanmar wakati linajenga bomba la urefu wa kilomita 62 huko Yadana, hawakuua raia na kuwatumikisha bila malipo? Namna gani migodi ya dhahabu hapa Tanzania kuwanyanyasa wananchi na kuua mifugo yao kwa kemikali za sumu bila kulipa fidia?

Kamuulize David Cameron wa Uingereza,kwanini Shell na Chevron wanapochimba mafuta Nigeria na kuharibu mazingira, wananchi wakihoji wao huwalipa polisi pesa ili wawapige risasi? Ndiyo Haki gani za Binadamu?
Kwanini Shell walimchochea Sani Abacha hadi akamuua Ken Saro-Wiwa na wenzake wananne mwaka 1995?
Kwanini Shell la Uingereza na Chevron la Marekani wanashirikiana na polisi huko Nigeria kuua waandamanaji wanaopinga wizi na uharibifu wa mashamba yao kwa mabaki ya mafuta yanayoachwa kuingia katika mashamba ya viazi na kuharibu uzalishaji,pasipo fidia yoyote?

Uingereza hao hao na Marekani na Ufaransa, wanamshambulia Kanali Muammar al-Qaddafi huko Libya kwamba anawashambulia waandamanaji!

Hizi ndizo ;double standards’ na mkuki kwa nguruwe hivi. Demokrasia inaimbwa kuhitajika Libya,Yemen na Misri, wakati mahali wanapokandamiza raia kwa kampuni zao kudhulumu na kuharibu mazingira, huko hawasemi!

 Kama kuua raia wanaoandamana ni kosa,kwanini Hosni Mubarak na Qaddafi waitwe wauaji na wachukuliwe hatua za kupinduliwa, wakati Shell,Chevron,Total n.k hayo makampuni ya Kimarekani,Kiingereza na Kifaransa,hayajakamatwa na kufungwa jela huko The Hague?

Qaddafi, ati ni muuaji wa waandamanaji, na Wamarekani,Wafaransa na Waingereza wakiua watu ni ‘Liberators’!

 Kuna mengi maovu yanayofanywa na Marekani na washirika wao chini ya mwavuli wa NATO, na Rais Obama hana ubavu wa kuyakemea, kwa sera za Marekani za Nje, za kuua na kupora!
 Tena Osama aliua tu hakupora rasilimali. Marekani chini ya Obama,wanaua na kupora rasilimali.

Kwa sababu hiyo, Obama na Osama ni wale wale tu(wauaji) kasoro ni “b” na “s” katika majina yao!
 Matendo ya Osama na Obama siku hizi  yanashabihiana sana, kasoro ni hizo 'b' na 's' tu!

0786/0754-324 074



No comments:

Post a Comment