Monday, April 18, 2011

Umoja wa Mataifa(United Nations)wa Marekani?! *UN ni ng’ombe wa maziwa wa Marekani *umefungwa kamba shingoni MAKALA yangu iitwayo, “Safari ya Dunia kutoka uhuru kurejea utumwani” iliyochapishwa katika gazeti la Tazama -Tanzania, imezua maswali lukuki na kiu ya wasomaji. Kufuatia hali hiyo, naamua kuyajibu maswali hayo kwa kunukuu vyanzo anuwai vya habari,kikiwemo kijarida kitolewacho kila baada ya majuma mawili na Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agostino(SAUT) jijini Mwanza, Malimbe Campus. Kijarida hiki,kinaitwa CURRENT AFFAIRS, na unaweza kukipata pia kupitia website:www.saut.ac.tz/Current Affairs. Kichwa cha makala yangu hii,”Umoja wa Mataifa wa Marekani” hufanana na kichwa cha makala ya Amani Nkurlu,mmoja wa wahariri wasaidizi wa Current Affairs,katika toleo la Aprili 8-25 mwaka huu wa 2011. Amani Nkurlu,aliandika katika ukurasa wa nne, kwamba The United Nations of America” huku akieleza malengo ya kuanzishwa Umoja huo wa Mataifa Oktoba 24, mwaka 1945 kwamba ilikuwa ni kuondoa utumwa na vita duniani,ili kustawisha Haki za Binadamu,Amani na kuleta maendeleo kwa wakazi wa dunia. Kinyume chake, Umoja wa Mataifa(UN) ukiwa mithili ya ng’ombe aliyefungwa kamba shingoni na Marekani, unaburuzwa kwenda kuua mamia ya maelfu ya watu Afghanistan, Irak, sasa Libya,Yemen, baadaye Uturuki, Iran n.k Umoja huu(UN) uko mbioni kupeka vita vya maangamizi Iran, Yemen,Uturuki na katika nchi nyingine zilizoko jirani na Mfereji wa Suez na Bahari ya Mediterranean, ambazo huzalisha kwa wingi mafuta takriban asilimia nane za mahitaji ya dunia. Nimeandika pia makala iitwayo, “Safari ya miaka 59 ya Afrika,kutoka Uhuru kurejea Utumwani” iliyochapwa katika gazeti hili,nikieleza ubeberu na mpango wa mabepari wa Marekani na washirika wake,na mashirika yao ya kijasusi, kama Central Intelligence Agency(CIA) na lile la kibaraka wao, Israeli(Mossad)kuvuruga amani katika eneo lenye mafuta mengi,huko Mashariki ya Kati. Awali, walitumia Shirika la Makaburu wa Afrika Kusini(BOSS) kuhujumu harakati za uhuru,wakawaua wanamapinduzi wa Afrika,kama Samora Moises Machel,na wengine ndani ya Afrika Kusini, wakawafunga jela Nelson Rolihlahla “Madiba” Mandela n.k Kwanza, niwapongeze wajumbe wa Bodi ya uhariri na waandishi wa Current Affairs:Theresia Christian,Gregory Gondwe, Amani Nkurlu na wenzao, kwa kuuona ubeberu na ubepari kasha ukoloni mamboleo, ukipindua mamlaka za nchi zenye rasilimali nyingi kama mafuta. Visingizio vyao eti ni kuleta amani na demokrasia katika nchi hizo, na kasha Haki za Binadamu! Marekani, Uingereza na Ufaransa,wamempindua kibaraka wao Hosni Mubarak,kwa sababu ya Mfereji wa Suez uliojengwa na Ufaransa na Uingereza mwaka 1859-1869.Walianza kuupigania,Misri ikautaifisha Julai 28 mwaka 1956. Una urefu wa maili 103 unatumiwa na mameli kuziunganisha Bahari ya Shamu(Red Sea) na Bahari ya Kati-Mediterranean. Misri pia kuna mafuta mengi na madini mengine,na ina ushawishi katika nchi nyingi za Kiarabu zenye utajiri wa mafuta. Huko Libya, kosa la kwanza la Kanali Muammar al-Gaddafi,lilikuwa kutaifisha visima vya mafuta mara baada ya kuingia madarakani mwaka 1969, kwa maslahi ya wananchi wa Libya, na aslani si kwa maslahi ya makampuni ya Ulaya na Marekani. Utaifishaji, katika macho ya wakiloni hawa,mabeberu ni kosa kubwa na hatari kwa maslahi yao-wao na Mashirika yao kama International Monetary Fund(IMF) na Benki ya Dunia(WB) wanataka dunia nzima itekeleze amri yao iitwayo UBINAFSISHAJI!! Hapa kwetu,tumebinafsisha hata makampuni na mabenki yaliyojiendesha kwa faida kubwa na kuwapa ajira wananchi,kwa sababu tunawaogopa hawa mabwenyenye na taasisi zao za Breton Woods. Marekani na washirika wake, wanauburuza Umoja huu wa Mataifa(United Nations of America?), wanawafadhili waasi nchili Libya kwa silaha nzito na fedha,ili wapigane vita vyao walivyoanzisha tangu mwaka 1986 vya kumpindua Kanali Muammar al-Gaddafi. Kwa sababu, Gaddafi alikuwa na kiburi cha kutowafungulia mlango makampuni ya Marekani na Ulaya, na alithubutu kuhujumu ndege ya Pan American Airways(PAN AM) huko Lockerbie, Scotland mwaka 1988. Akasalimu amri nusu nusu kwa kulipa fidia ya mamilioni ya Dola za mafuta, ili sasa wamwondoe katika ramani ya Mhimili wa Uovu(The Axis of Evil),kumbe wapi bwana!Wanae tu. Hapa kwetu wanatuingilia hata jikoni, eti kwa sababu wametufunika kwa chandarua cha kukinga Malaria! Gaddafi, alitaka Afrika iunde taifa kubwa-The United States of Africa! Hii ndiyo ilikuwa njozi ya akina Kwame Nkurumah, Gamal Abdel Nasser, Julius Nyerere, Patrice Emery Lumumba, Ahmad Sekou Toure na wenzao, wakaishia kuwekewa vikwazo vya uchumi na kuuawa. Na Gaddafi anarejea kosa la wenzake,kutaka mafuta ya Afrika,madini na gesi view kwa maslahi ya Waafrika tu. Kama Umoja wa Mataifa(UN) ulianzishwa ili kulinda amani baada ya Vita vikuu vya Kwanza na Vya Pili,kuhifadhi Haki za Binadamu na kuleta maendeleo kwa watu: Kwanini Umoja huu(UN) uwe wa Marekani na washirika wake,Uingereza na Ufaransa,na wajiamulie wao kwenda Afghanistan kupindua serikali na kuweka watu wao,kasha wakaenda Irak na kumkamata Saddam na kumchinja kwa kitanzi huku wakiua mamia kwa maelfu? Irak, wameua watu zaidi ya 700,000 sasa na wanatesa raia wanaowapinga kwa vifungo jela huko Guantanamo Bay na Abu-Ghraib. Wanawafunga jela watuhumiwa hata kabla ya kuwafikisha mahakamani. Je,huku si kuhujumu Haki za Binadamu wanazodai zinakiukwa Misri, Yemen,Tunisia,Uturuki,Iran,Korea Kaskazini na nchi adui zao? Umoja wa Mataifa unaburuzwa kupelekwa Iran,ili wakampindue Mujahiddin Mahmoud Ahmadnejad,kwamba anarutubisha madini ya Uranium kwa ajili ya silaha za nyuklia. Wametoa amri ndege za Gaddafi zisiruke angani Libya kuwapika waasi(rafiki zao na vibaraka wao) kwa amri ya “No Fly Zone”! Sasa msomaji, badala ya amri hii, “No Fly Zone” kutolewa na Katibu Mkuu wa UN, Bwana Ban-Ki Moon huko 1st Avenue, New York,inatolewa na akina Obama, Hillary Clinton na Robert Gates, huko White House, mjini Washington!! Kumbe, ndiyo maana tunasema UN ni Umoja wa Mataifa wa Marekani! Na hii siyo mara ya kwanza kwa mabepari kuchochea vita duniani,mahali kulipo na alamasi,dhahabu,mafuta,gesi,uranium na mifereji kama Panama na Suez na bahari kama Mediterranean n.k Katibu Mkuu wa Pili wa Umoja wa Mataifa,huu wa Marekani(The United Nations of America)Mswedeni, Darg Hjalmar Agne Carl Hammarskjold, aliyefanya kazi tangu Aprili 10 mwaka 1953-Septemba18 mwaka 1961, alikufa kwa ajali ya ndege Congo,leo DRC. Nani alichochea vita Congo? Kwa nini? Ni Marekani na washirika wake na majasusi wa CIA walileta uasi na vurugu huko Shaba na Katanga,wakamkamata mwanamapinduzi, Patrice Lumumba na kumuua. Lumumba, alikuwa na sera za kijamaa,za kutaka madini ya Congo na rasilimali zingine kuwa mali ya raia wa Congo—ooh, akawakosea hawa. Wakawachochea akina Moise Tshombe,Joseph Kasavubu na vibaraka wao wengine kama Joseph Desire Mobutu Sesesseko, wakamuua Lumumba. Sasa, Katibu Mkuu wa UN wakati huo Dk. Darg Hammarskjold akasafiri kwa ndege kwenda Congo kutafuta amani, Septemba 18 mwaka 1961 akafa kwa ajali ya ndege. Hadi leo, Umoja huu wa Mataifa wa Marekani(United Nations of America)HAUJATULIZA VITA Congo. Badaye, walimweka kibaraka wao Mobutu, wakaiba madini wee, Mobutu alipora Dola za Marekani milioni sita akaficha Ulaya-fedha hizi ni nyingi sawa la deni la nje la nchi nzima. Salim Ahmed Salim, alijaribu kugombea Ukatibu M kuu wa UN. Marekani walimkataa kwa sababu alikuwa anatoka nchi ya kijamaa,na hasa ujamaa wa akina Nyerere! Umoja wa Mataifa wenye nia ya kuboresha maslahi ya watu duniani,ukatae ujamaa? Aliwekwa Boutros Boutros-Ghali wa Misri kuwa Katibu Mkuu wa sita,Januari Mosi mwaka 1992. Nataka nikwambie msomaji. Huyu Boutros Boutros Ghali, alikataliwa na Marekani asigombee mhula wa pili,kwa kisingizio kwamba alishindwa kuzuia mauaji ya Kimbari-genocide-huko Rwanda, kasha hakuzuia vita Angola! Nani alichochea vita Angola? Siyo Marekani na washirika wake na majasusi wa CIA waliomfadhili Jonas Malheiro Savimbi,ili kukwamisha juhudi za akina Agostino Neto? Nani alihujumu MPLA? Ndiyo, walimtoa kafara Boutros Ghali, kwa sababu alishindwa kubeba maslahi ya Marekani, akataka kuleta uarabu-arabu huko. Alikuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa UN kutumikia mhula mmoja tu, wakati huko Cabinda, Angola tunajua kuna mafuta mengi na Marekani wananchochea maasi, Naam, Umoja wa Mataifa(UN) ni ng’ombe wa maziwa wa Marekani! Kisha,twajua Umoja wa Kujihami wa Ulaya Magaharibi(Northern Atlantic Treaty Organization) ULIANZISHWA NA Rais Franklin Roosevelt wa Marekani na Waziri Mkuu Winston Churchill wa Uingereza mwaka 1941 ili kujihami dhidi ya Urusi na washirika wake wa Warsaw Pact. Sasa, NATO kuishambulia Libya, maana yake Gaddafi aliwashambulia NATO lini? Marekani inayochangia UN kwa zaidi ya asilimia 30 ilimweka Kofi Annan,wa saba wakamburuza hadi mwenyewe amekiri kuhenyeshwa. UN ni ng’ombe wa Marekani wa maziwa na kafungwa kamba shingoni.Wanakotaka kwenda Marekani, na UN inakwenda. Rwanda walikufa watu 800,000 bila msaada wa UN kwa sababu hakukuwa na mafuta. Bosnia na Herzegovina mwaka 1995 walikufa 200,000,Irak wameuliwa watu 700,000, Afghanistan wamekufa mamia kwa maelfu, UN wapo tu hadi ofisi zake zikalipuliwa kwa bomu. Hawana kazi! Hakuna wanachokataa juu ya Misri,Libya,Yemen, Uturuki n.k Huu Umoja wa Mataifa umeshindwa kuleta amani duniani,unaleta kiza na wakimbizi kuliko wakati wa Vita vya Kwanza na Vya Pili vya Dunia. Hata Ivory Coast, UN hawatafanya kitu, Laurent Gbagbo kakamatwa Aprili 11, mkewe Simone akabakwa na wafuasi wa Ouattara Dramane, watu wanaweza kuuana kikabila na kidini,lakini utaona UN inatazama mafuta, kakao na mbao zaidi kuliko kulinda watu! Vita vya kwanza vya Dunia(1914-1918) vilisababisha wanajeshi 8,418,000 na raia 1,3000 kupoteaa maisha. Vita vya Pili vya Dunia(1939-45)viliua wanajeshi 16,933,000 na raia 34,305,000 wakiwemo babu zetu. Vita ambavyo Marekani Vietnam(1962-70)Vikaua watu 500,000,Korea wamekufa wau milioni nzima mwaka 1950-53. Kasome kitabu kiitwacho CONFICT ON THE TWENTIETH CENTURY cha David Wood(Institute for Strategic Studies),London. Nataka msomaji wangu ujue kwamba Umoja wa Mataifa(UN) unaoburuzwa na Marekani na washirika wake kwa tabia hizi, kamwe hawaleti amani na maendeleo-ni vita,njaa na wakimbizi,na maradhi na mauti. Hakuna uhuru,kama raia wanaamuliwa nani awatawale na Marekani,tena kwa muda gani. Umoja huu una umri wa miaka 66, una Makatibu Wakuu nane: Trygve Lie wa Norway,Hammarskjold wa Sweden, Dk U-Thant wa Burma, Kurt Waldheim wa Austria, Javier Perez de Cueller wa Peru,Boutros Ghali wa Misri, Kofi Annan wa Ghana na Ban Ki Moon wa Korea Kusini nchi rafiki yao. Hawezi kutokea Katibu Mkuu wa UN Uchina, Urusi,Tanzania ama Korea Kaskazini!Wakitaka kuvamia Yemen,Uturuki au Iran kwamba kuna nyuklia, hawa watakataa. Kinachotakiwa na Marekani na washirika wao,ni kuwapigia goti tu, na ukiwapinga ni kupigwa vita vikali kwa visingizio vya demokrasia na haki za binadamu ambazo wao wamezivunja mno. Ndiyo maana, Biblia katika Ufunuo wa Yohana 13:11-18, inawasema Marekani kama Mnyama kama mwanakondoo aliyekuwa na demokrasia na Uhuru wa dini, sasa ni Ibilisi anayewalazimisha watu wote kumsujudia shetani na Freemasons, wanaokataa wanauawa na kuwekewe vikwazo vya kiuchumi-economic sanctions! www.congesmrambatoday.blogspot.com 0786/0754-324 074 Go to Previous message | Go to Next message | Back to Messages | Full Headers Reply Reply All Forward Forward Mail Search WelcomeInboxNewFoldersMail Options


  Umoja wa Mataifa(United Nations)wa Marekani?!
                 *UN ni  ng’ombe wa maziwa wa Marekani
                 *umefungwa kamba shingoni

MAKALA yangu iitwayo, “Safari ya Dunia kutoka uhuru kurejea utumwani” iliyochapishwa katika gazeti  la Tazama -Tanzania, imezua maswali lukuki na kiu ya wasomaji.
   Kufuatia hali hiyo, naamua kuyajibu maswali hayo kwa kunukuu vyanzo anuwai vya habari,kikiwemo kijarida kitolewacho kila baada ya majuma mawili na Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agostino(SAUT) jijini Mwanza, Malimbe Campus.
  Kijarida hiki,kinaitwa CURRENT AFFAIRS, na unaweza kukipata pia kupitia website:www.saut.ac.tz/Current Affairs.
Kichwa cha makala yangu hii,”Umoja wa Mataifa wa Marekani” hufanana na kichwa cha makala ya Amani Nkurlu,mmoja wa wahariri wasaidizi wa Current Affairs,katika toleo la Aprili 8-25 mwaka huu wa 2011.
   Amani Nkurlu,aliandika katika ukurasa wa nne, kwamba The United Nations of America” huku akieleza malengo ya kuanzishwa Umoja huo wa Mataifa Oktoba 24, mwaka 1945 kwamba ilikuwa ni kuondoa utumwa na vita duniani,ili kustawisha Haki za Binadamu,Amani na kuleta maendeleo kwa wakazi wa dunia.
  Kinyume chake, Umoja wa Mataifa(UN) ukiwa mithili ya ng’ombe aliyefungwa kamba shingoni na Marekani, unaburuzwa kwenda kuua mamia ya maelfu ya watu Afghanistan, Irak, sasa Libya,Yemen, baadaye Uturuki, Iran n.k
 Umoja huu(UN) uko mbioni kupeka vita vya maangamizi Iran, Yemen,Uturuki na katika nchi nyingine zilizoko jirani na Mfereji wa Suez na Bahari ya Mediterranean, ambazo huzalisha kwa wingi mafuta takriban asilimia nane za mahitaji ya dunia.
   Nimeandika pia makala iitwayo, “Safari ya miaka 59 ya Afrika,kutoka Uhuru kurejea Utumwani” iliyochapwa katika gazeti hili,nikieleza ubeberu na mpango wa mabepari wa Marekani na washirika wake,na mashirika yao ya kijasusi, kama Central Intelligence Agency(CIA) na lile la kibaraka wao, Israeli(Mossad)kuvuruga amani katika eneo lenye mafuta mengi,huko Mashariki ya Kati.
   Awali, walitumia Shirika la Makaburu wa Afrika Kusini(BOSS) kuhujumu harakati za uhuru,wakawaua wanamapinduzi wa Afrika,kama Samora Moises Machel,na wengine ndani ya Afrika Kusini, wakawafunga jela Nelson Rolihlahla “Madiba” Mandela n.k
   Kwanza, niwapongeze wajumbe wa Bodi ya uhariri na waandishi wa Current Affairs:Theresia Christian,Gregory Gondwe, Amani Nkurlu na wenzao, kwa kuuona ubeberu na ubepari kasha ukoloni mamboleo, ukipindua mamlaka za nchi zenye rasilimali nyingi kama mafuta.
 Visingizio vyao eti ni kuleta amani na demokrasia katika nchi hizo, na kasha Haki za Binadamu!
 Marekani, Uingereza na Ufaransa,wamempindua kibaraka wao Hosni Mubarak,kwa sababu ya Mfereji wa Suez uliojengwa na Ufaransa na Uingereza mwaka 1859-1869.Walianza kuupigania,Misri ikautaifisha Julai 28 mwaka 1956.
 Una urefu wa maili 103 unatumiwa na mameli kuziunganisha Bahari ya Shamu(Red Sea) na Bahari ya Kati-Mediterranean.
  Misri pia kuna mafuta mengi na madini mengine,na ina ushawishi katika nchi nyingi za Kiarabu zenye utajiri wa mafuta.
Huko Libya, kosa la kwanza la Kanali Muammar al-Gaddafi,lilikuwa kutaifisha visima vya mafuta mara baada ya kuingia madarakani mwaka 1969, kwa maslahi ya wananchi wa Libya, na aslani si kwa maslahi ya makampuni ya Ulaya na Marekani.
   Utaifishaji, katika macho ya wakiloni hawa,mabeberu ni kosa kubwa na hatari kwa maslahi yao-wao na Mashirika yao kama  International Monetary Fund(IMF) na Benki ya Dunia(WB) wanataka dunia nzima itekeleze amri yao iitwayo UBINAFSISHAJI!!
 Hapa kwetu,tumebinafsisha hata makampuni na mabenki yaliyojiendesha kwa faida kubwa na kuwapa ajira wananchi,kwa sababu tunawaogopa hawa mabwenyenye na taasisi zao za Breton Woods.
  Marekani na washirika wake, wanauburuza Umoja huu wa Mataifa(United Nations of America?), wanawafadhili waasi nchili Libya kwa silaha nzito na fedha,ili wapigane vita vyao walivyoanzisha tangu mwaka 1986 vya kumpindua Kanali Muammar al-Gaddafi.
 Kwa sababu, Gaddafi alikuwa na kiburi cha kutowafungulia mlango makampuni ya Marekani na Ulaya, na alithubutu kuhujumu ndege ya Pan American Airways(PAN AM) huko Lockerbie, Scotland mwaka 1988.
 Akasalimu amri nusu nusu kwa kulipa fidia ya mamilioni ya Dola za mafuta, ili sasa wamwondoe katika ramani ya Mhimili wa Uovu(The Axis of Evil),kumbe wapi bwana!Wanae tu.
  Hapa kwetu wanatuingilia hata jikoni, eti kwa sababu wametufunika kwa chandarua cha kukinga Malaria! Gaddafi, alitaka Afrika iunde taifa kubwa-The United States of Africa!
 Hii ndiyo ilikuwa njozi ya akina Kwame Nkurumah, Gamal Abdel Nasser, Julius Nyerere, Patrice Emery Lumumba, Ahmad Sekou Toure na wenzao, wakaishia kuwekewa vikwazo vya uchumi na kuuawa.
 Na Gaddafi anarejea kosa la wenzake,kutaka mafuta ya Afrika,madini na gesi view kwa maslahi ya Waafrika tu.
 Kama Umoja wa Mataifa(UN) ulianzishwa ili kulinda amani baada ya Vita  vikuu vya Kwanza na Vya Pili,kuhifadhi Haki za Binadamu na kuleta maendeleo kwa watu:
  Kwanini Umoja huu(UN) uwe wa Marekani na washirika wake,Uingereza na Ufaransa,na wajiamulie wao kwenda Afghanistan kupindua serikali na kuweka watu wao,kasha wakaenda Irak na kumkamata Saddam na kumchinja kwa kitanzi huku wakiua mamia kwa maelfu?
  Irak, wameua watu zaidi ya 700,000 sasa na wanatesa raia wanaowapinga kwa vifungo jela huko Guantanamo Bay na Abu-Ghraib.
 Wanawafunga jela watuhumiwa hata kabla ya kuwafikisha mahakamani. Je,huku si kuhujumu Haki za Binadamu wanazodai zinakiukwa Misri, Yemen,Tunisia,Uturuki,Iran,Korea Kaskazini na nchi adui zao?
 Umoja wa Mataifa unaburuzwa kupelekwa Iran,ili wakampindue Mujahiddin Mahmoud Ahmadnejad,kwamba anarutubisha madini ya Uranium kwa ajili ya silaha za nyuklia.
  Wametoa amri ndege za Gaddafi zisiruke angani Libya kuwapika waasi(rafiki zao na vibaraka wao) kwa amri ya “No Fly Zone”!
 Sasa msomaji, badala ya amri hii, “No Fly Zone” kutolewa na Katibu Mkuu wa UN, Bwana Ban-Ki Moon huko 1st Avenue, New York,inatolewa na akina Obama, Hillary Clinton na Robert Gates, huko White House, mjini Washington!!
 Kumbe, ndiyo maana tunasema UN ni Umoja wa Mataifa wa Marekani!
 Na hii siyo mara ya kwanza kwa mabepari kuchochea vita duniani,mahali kulipo na alamasi,dhahabu,mafuta,gesi,uranium na mifereji kama Panama na Suez na bahari kama Mediterranean n.k
 Katibu Mkuu wa Pili wa Umoja wa Mataifa,huu wa Marekani(The United Nations of America)Mswedeni, Darg Hjalmar Agne Carl Hammarskjold, aliyefanya kazi tangu Aprili 10 mwaka 1953-Septemba18 mwaka 1961, alikufa kwa ajali ya ndege Congo,leo DRC.
  Nani alichochea vita Congo? Kwa nini? Ni Marekani na washirika wake na majasusi wa CIA walileta uasi na vurugu huko Shaba na Katanga,wakamkamata mwanamapinduzi, Patrice Lumumba na kumuua.
 Lumumba, alikuwa na sera za kijamaa,za kutaka madini ya Congo na rasilimali zingine kuwa mali ya raia wa Congo—ooh, akawakosea hawa.
 Wakawachochea akina Moise Tshombe,Joseph Kasavubu na vibaraka wao wengine kama Joseph Desire Mobutu Sesesseko, wakamuua Lumumba.
 Sasa, Katibu Mkuu wa UN wakati huo Dk. Darg Hammarskjold akasafiri kwa ndege kwenda Congo kutafuta amani, Septemba 18 mwaka 1961 akafa kwa ajali ya ndege.
 Hadi leo, Umoja huu wa Mataifa wa Marekani(United Nations of America)HAUJATULIZA VITA Congo.
 Badaye, walimweka kibaraka wao Mobutu, wakaiba madini wee, Mobutu alipora Dola za Marekani milioni sita akaficha Ulaya-fedha hizi ni nyingi sawa la deni la nje la nchi nzima.
   Salim Ahmed Salim, alijaribu kugombea Ukatibu M kuu wa UN. Marekani walimkataa kwa sababu alikuwa anatoka nchi ya kijamaa,na hasa ujamaa wa akina Nyerere!
  Umoja wa Mataifa wenye nia ya kuboresha maslahi ya watu duniani,ukatae ujamaa?
Aliwekwa Boutros Boutros-Ghali wa Misri kuwa Katibu Mkuu wa sita,Januari Mosi mwaka 1992.
 Nataka nikwambie msomaji. Huyu Boutros Boutros Ghali, alikataliwa na Marekani asigombee mhula wa pili,kwa kisingizio kwamba alishindwa kuzuia mauaji ya Kimbari-genocide-huko Rwanda, kasha hakuzuia vita Angola!
 Nani alichochea vita Angola? Siyo Marekani na washirika wake na majasusi wa CIA waliomfadhili Jonas Malheiro Savimbi,ili kukwamisha juhudi za akina Agostino Neto?
 Nani alihujumu MPLA? Ndiyo, walimtoa kafara Boutros Ghali, kwa sababu alishindwa kubeba maslahi ya Marekani, akataka kuleta uarabu-arabu huko.
  Alikuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa UN kutumikia mhula mmoja tu, wakati huko Cabinda, Angola tunajua kuna mafuta mengi na Marekani wananchochea maasi,
 Naam, Umoja wa Mataifa(UN) ni ng’ombe wa maziwa wa Marekani!
Kisha,twajua Umoja wa Kujihami wa Ulaya Magaharibi(Northern Atlantic Treaty Organization) ULIANZISHWA NA Rais Franklin Roosevelt wa Marekani na Waziri Mkuu Winston Churchill wa Uingereza mwaka 1941 ili kujihami dhidi ya Urusi na washirika wake wa Warsaw Pact.
 Sasa, NATO kuishambulia Libya, maana yake Gaddafi aliwashambulia NATO lini? Marekani inayochangia UN kwa zaidi ya asilimia 30 ilimweka Kofi Annan,wa saba wakamburuza hadi mwenyewe amekiri kuhenyeshwa.
 UN ni ng’ombe wa Marekani wa maziwa na kafungwa kamba shingoni.Wanakotaka kwenda Marekani, na UN inakwenda.
 Rwanda walikufa watu 800,000 bila msaada wa UN kwa sababu hakukuwa na mafuta. Bosnia na Herzegovina mwaka 1995 walikufa 200,000,Irak wameuliwa watu 700,000, Afghanistan wamekufa mamia kwa maelfu, UN wapo tu hadi ofisi zake zikalipuliwa kwa bomu.
 Hawana kazi! Hakuna wanachokataa juu ya Misri,Libya,Yemen, Uturuki n.k Huu Umoja wa Mataifa umeshindwa kuleta amani duniani,unaleta kiza na wakimbizi kuliko wakati wa Vita vya Kwanza na Vya Pili vya Dunia.
  Hata Ivory Coast, UN hawatafanya kitu, Laurent Gbagbo kakamatwa Aprili 11, mkewe Simone akabakwa na wafuasi wa Ouattara Dramane, watu wanaweza kuuana kikabila na kidini,lakini utaona UN inatazama mafuta, kakao na mbao zaidi kuliko kulinda watu!
 Vita vya kwanza vya Dunia(1914-1918) vilisababisha wanajeshi 8,418,000 na raia 1,3000 kupoteaa maisha.
 Vita vya Pili vya Dunia(1939-45)viliua wanajeshi 16,933,000 na raia 34,305,000 wakiwemo babu zetu. Vita ambavyo Marekani Vietnam(1962-70)Vikaua watu 500,000,Korea wamekufa wau milioni nzima mwaka 1950-53. Kasome kitabu kiitwacho CONFICT ON THE TWENTIETH CENTURY cha David Wood(Institute for Strategic Studies),London.
 Nataka msomaji wangu ujue kwamba Umoja wa Mataifa(UN) unaoburuzwa na Marekani na washirika wake kwa tabia hizi, kamwe hawaleti amani na maendeleo-ni vita,njaa na wakimbizi,na maradhi na mauti.
 Hakuna uhuru,kama raia wanaamuliwa nani awatawale na Marekani,tena kwa muda gani. Umoja huu una umri wa miaka 66, una Makatibu Wakuu nane: Trygve Lie wa Norway,Hammarskjold wa Sweden, Dk U-Thant wa Burma, Kurt Waldheim wa Austria, Javier Perez de Cueller wa Peru,Boutros Ghali wa Misri, Kofi Annan wa Ghana na Ban Ki Moon wa Korea Kusini nchi rafiki yao.
 Hawezi kutokea Katibu Mkuu wa UN Uchina, Urusi,Tanzania ama Korea Kaskazini!Wakitaka kuvamia Yemen,Uturuki au Iran kwamba kuna nyuklia, hawa watakataa.
 Kinachotakiwa na Marekani na washirika wao,ni kuwapigia goti tu, na ukiwapinga ni kupigwa vita vikali kwa visingizio vya demokrasia na haki za binadamu ambazo wao wamezivunja mno.
  Ndiyo maana, Biblia katika Ufunuo wa Yohana 13:11-18, inawasema Marekani kama Mnyama kama mwanakondoo aliyekuwa na demokrasia na Uhuru wa dini, sasa ni Ibilisi anayewalazimisha watu wote kumsujudia shetani na Freemasons, wanaokataa wanauawa na kuwekewe vikwazo vya kiuchumi-economic sanctions!
 
      0786/0754-324 074
 



No comments:

Post a Comment