NIMEPATA KUSOMA mzaha katika gazeti moja litolewa ng’ambo,
kwamba Obama na Osama ni mtu yule yule kasoro herufi mbili, “b” na “s” katikati
ya majina yao!
Kulingana na lesoni ya Waadventista wa Sabato(Sabbath School
Bible Study Guide) ya Oktoba hadi
Desemba, 2010 ukurasa wa 72 majina ni muhimu tangu nyakati za Biblia. Jina
linamwonesha mtu tabia yake,urithi wake toka kwa wazazi wake.Mtu hufanana na jina lake.
Wakati mwingine, jina
hutafsiri kile wazazi walichotazamia au kile kilichowakabili wakati mtoto
anazaliwa.
Bila shaka umepata kusikia majina ya akina Semeni, Siwajibu,
Masumbuko,Chuki,Mashaka,Majuto, Nyamayao n.k!
Majina
haya,huzungumza mazingira mtoto alimozaliwa na majaliwa yake. Majina kama Abram,Yakobo,Danieli
n.k pia yalitabiri tabia ya watu hawa ya uchaji Mungu, utegemezi kwa Mungu kama
Hakimu na Mwamuzi.
Yakobo, tafsiri yake ni ‘Mdanganyifu’ aliyemdanganya babaye,
Isaka wakampora kakaye, Esau haki ya mzaliwa wa kwanza.
Kulingana na somo,’What’s in a Name?’ katika lesoni hiyo ya
Wasabato, jina Osama,kwetu ni mtu katili; Yule gaidi hatari sana aliyesababisha
majengo pacha ya World Trade Center(WTC)mjini New York kuteketea kwa mabomu
Septemba 11, mwaka 2001 na zaidi ya watu 5,500 wakapoteza maisha.
Osama, katika kizazi hiki ni muuaji hata kama baadhi ya
watu wanamwoma mwanaharakati, sahahidi mwaminifu, martyr!
Ni kwa sababu sababu hii tu,mtu akisema(Rais Barack
Hussein)Obama anafanana na Gaidi la Kimataifa,linalosakwa sana,Osama(Bin
Laden)aliyelipua pia Makao Makuu ya Wizara ya Ulinzi ya M arekani mjini
Washington, “The Pentagon” nasi tunamwona leo Obama kwamba ni muuaji na katili
kama Osama.
Kwamba, Obama na Osama ni mtu Yule Yule kasoro herufi ‘b’ na
‘s’ basi lingekuwa jina moja!
Namfananisha Rais Obama wa Marekani na gazidi
linalosakwa sana duniani, kwa kuhusika na ajali ya Septemba 11, hadi leo WTC
haikujengwa, uwanja umeachwa kama Mnara wa Kumbukumbu ya kiama kile,na mahali
hapa panaitwa, Ground Zero.
Katika safu hii napenda kuandika
kwamba Waafrika hawana sababu ya kumsahangilia sana Obama, kwa
kufanikiwa kukalia kiti kile cha
ngozi nyeusi hapo “Oval Office” katika Ikulu ya White House,Marekani,
kwa mara nyingine baada ya kumshinda Mitt Romney wa Republican kwa
ushindi wa kishindo wa kura 302 za electoral college,dhidi ya 206 za
Romney mchovu!
Kwamba, ingawa Obama,babu yake Mzee Obama alikuwa “Boy” wa
Wazungu mjini Nairobi,Kenya akamzaa Hussein Obama aliyekwenda kusoma Marekani
akakutana na mama Mzungu akampa ujauzito na akamzaa Barack Hussein Obama, bado
Obama siyo Mwafrika.
Nawashangaa sana Waafrika wanaomshangilia sana Obama,hadi mishipa inawatutumka vichwani! Obama siyo Mkenya wala Mghana!
Obama, ni Mmarekani anayetekeleza sera za Marekani za
kibeberu; na lazima awe mtii kwa kiapo chake cha kulinda,kuhifadhi na
kutekeleza sera za Marekani kwa maslahi ya Wamarekani,na aslani Obama hawezi
kuwajua, na kuwajali Waafrika!
Naam, Obama siyo
Mwafrika; ni Mmarekani. Kipaumblele chake siyo Kogelo,Kisumu, Nairobi, Afrika
Mashariki,Afrika. Obama anatekeleza maslahi ya Marekani na viwanda vya
Wamarekani, anajali mustakabali wa Marekani zaidi,hata kama kwa kufanya hivyo
Afrika italipuka katika miali mikali ya moto.
Nadhani, sasa Afrika inameza machungu
ya kumshangilia sana
Obama Novemba 2008 hadi Januari 20,mwaka 2009.Wanarejea kosa hilo hilo
la kumshangilia,wakidhani mhula wake wa Pili, White House, ataitazama
Afrika ili kuwatupia msaada!
Obama ana macho yanayoitazama Marekani, kamwe siyo
Afrika.Waafrika msitarajie kitu kwa Obama,jengeni nchi zenu!
Kwa sababu ya maslahi matukufu ya Marekani, Obama sharti
apate kigugumizi katika mgogoro wa Cote d’ Ivoire, au umasikini wa Waafrika na njaa Ethiopia au vita Somali. .
Kwa sababu,Obama kwa maslahi ya
Marekani,hawezi kukurupukia
wimbo wa ‘Demokrasia’ ama Haki za Binadamu,kusema kwamba Alassane
Ouattara,Muislam wa Kaskazini mwa nchi, aliyetangazwa mshindi wa kiti
cha Urais
na Tume Huru ya Uchaguzi(CEI),ati aungwe mkono kijeshi na Marekani na
Washirika
wake,au na Majeshi ya Umoja wa Kujihami Ulaya Magharibi.Marekani ni wale
wale wanaoweza kuwaunga mkono hata waasi na madikteta kama Meles
Zenawi,mradi anatimiza maslahi yao matukufu.
Gbagbo
yuko Hague, kujibu mashitaka ya uhalifu na mauaji yaliyotokea...lakini
Gbagbo alikuwa rafiki yao wamemtupa baada ya maslahi kuanguka upande.
Ouattara, ambaye Januari Mosi mwaka juzi alitimiza umri wa
miaka 70,licha ya kusoma Pennsylvania na kufanya kazi IMF,hataaminiwa na sera
za Marekani za Nje, za kusaka mno maslahi pamoja na mafuta,gesi na mali ghafi
kwa ajili ya viwanda vyao eti kwa sababu ni mtawala wa kizazi kipya Afrika.
Marekani, walikenua meno hadi gego la mwisho,pale Laurent
Gbagbo alipomtimua Dikteta Jenerali Robert Guei, alipotaka kung’ang’ania
madarakani mwaka 2000,kwa nguvu ya umma, Peoples Power!
Hii Nguvu ya Umma,
haikuanzia Chadema, ilianzia Serbia pale alipotimliwa Dikteta Slobodan
Milosevic, ikatua Cote d’ Ivories kwa
Jen Guei,mwaka 2000.
Jen.Robert Guei, alikuwa kaingia madarakani kwa mapinduzi
wakati akiwa Mnadhimu wa Jeshi(Chief of staff).
Kiongozi wa Chama cha Kisoshalist, Gbagbo,ni Mkristo wa
nyumbani kwao Guei, alikuwa mpinzani wa serikali kwa miaka 30. Bila shaka
utajua uswahiba wa Marekani na wapinzani, amepata kufungwa jela.
Mei mwaka juzi, Gbagbo
alisherehekea ‘Birth Day’ ya 66 akiwa bado Ikulu ya mjini Abidjan,bila
wasiwasi.
Hatimaye alitiwa mbaroni kwa msaada wa Wafaransa.
Alianza kutawala Oktoba 26, mwaka 2000 baada ya ‘Wamachinga’ wa mjini
Abidjan kuingia mabarabarani wakiwa na rungu, mawe,panga,mawe, matofali n.k
wakachoma moto magari na majumba,jeshi likashindwa kuwafagia kwa risasi,kama
ilivyotokea Tunisia,Misri na siku hizi Libya.
Wafaransa hawa hawa
waliomwondoa madarakani Kanali Muammar al-Qaddafi, ndiyo waliomsaidia
Guei kutorokea Benin,nchi ikaingia katika vita vya kidini,baina ya Ukristo na
Uislam.
Polisi wa Kifaransa, The Gendarmes, walivamia nyumba ya
Ouattara hadi alipotimkia ubalozi wa Ujerumani. Afadhali hata Mjerumani!
Umoja wa Mataifa na Washington wao waliomba uchaguzi
urejewe,Ufaransa wakashinikiza Bunge kushika madaraka,au iundwe serikali ya
Umoja wa Kitaifa(Government of The National Unity).
Mchezo uliopo Cote d’ Ivoire,ni ule ule uliokuwepo mwaka
2000 baina ya Gbagbo na Jen.Robert Guei, ama kati ya Mugabe na Morgan Richard
Tsivangirai na kati ya Kibaki na Raila Odinga.
Na tabia na msimamo
wa Ufaransa na Washirika wake,Marekani hauwezi kubadilika pale yalipo maslahi
ya makampuni yake ndipo yalipo maslahi ya viongozi. Sera za NATO dhidi ya
Abidjan na mji Mkuu wa Yamoussoukro, ni zile zile tu za kuchochea vurugu na
vita ili wapate nafasi ya kupora mafuta,kokoa,mbao n.k
Na hata siwezi kuishangaa Marekani kuchochea machafuko
Algeria, Yemen,Misri,Libya n.k kwa
sababu kuna mafuta!
George Soros,Mwenyekiti
na Muasisi wa taasisi ya Open Society, kaandika Dibaji katika kitabu kiitwacho,
ESCAPING THE RESOURCE CURSE, kilichoandikwa na Macartan Humphreys, J.D Sachs na
Joseph Stglitz(Columbia University Press, New York 2007).
Kwamba, nchi tajiri za rasilimali hunyemelewa na
vita,machafuko,migogoro na umasikini wa wananchi kwa sababu ya ufisadi na
uchochezi toka nje.
Hawa ‘Mabwana Wakubwa’ hawawezi kukuacha hivi hivi bila
kukuingilia kama una madini,una gesi, mafuta,uranium ama bahari muhimu na mito
n.k
Kila penye madini,gesi,mafuta na Uranium kuna shida.
Korea,HongKong, Singapote na Taiwan-Asian Tigers-zilisahauliwa kuburuzwa miaka
ile ya 60 zikaendelea kiuchumi.
Hazina rasilimali nyingi,lakini uchumi unapaa
na hakuna maandamano.
Kwenye rasilimali,
hususan Afrika,kuna vita. Angola huko Cabinda kuna mafuta na kuna vita,
Congo(DRC) katika majimbo ya Shaba na Katanga kuna shaba na almasi na kuna
vita. Sudan ya Kusini kuna mafuta na ndiyo chimbuko la vita.
Angalia, Yemen, Indonesia(West Papua),Myanmar(Hill Tribes)
na Papua New Guinea(Boungainville) kuna shaba,dhahabu,mafuta na gesi na kuna
matatizo.
Morocco huko SAHARA MAGHARIBI kuna vita, Nigeria huko Biafra
na Niger Delta,kuna vita vya kugombea mafuta!
Nakupa shauri msomaji. Ukifika WHITE House,kamuulize Rais
Obama,ana mpango gani wa kuhakikisha mafuta, gesi,dhahabu,shaba,almasi n.k
zinawanufaisha raia wazawa wan chi husika,kuliko kuwanufaisha mafisadi wa
serikalini na makampuni ya Kimarekani,Kifaransa na Kiingereza?
Ukigusa mikataba ya hila ya makampuni ya Wazungu,kwamba ni
kama ile ya Carl Peters na Mangungo wa Msovero, basi utaona Obama anakuwa sawa
sawa tu na Osama!
Na ukipata
kuhudhuria
Mkutano wa Kimataifa, kamuulize Rais Obama, ni mtazamo gani wan chi yake
kuhusu
Mashariki ya Kati(Mideast situation)? Au Afrika? Halafu mnamshangilia
Obama kuwa Rais kwa mhula wa Pili huko Marekani,utadhani atawaletea
unga!
Kamuulize Obama,Kwanini Marekani inazidi kuua watu kwa
majanga ya asili kwa kukataa kusaini mikataba ya Kupunguza Joto Duniani kwa
moshi wa viwanda vyake,kama ule Mkataba wa Kyoto,Japan?
Juzi,kulikuwa
na Mkutano Afrika ya Kusini,lakini mataifa haya makubwa yagomea
mikataba kama huo wa Kyoto, ambao mwaka kesho utakuwa umemaliza muda
wake bila mafanikio.
Marekani huchangia kwa takriban asilima 50 ya gesi za sumu
angani na ndiyo chimbuko la majanga ya asili-Natural calamities!
Kamuulize Obama, ule msamiati wa ‘Ocampo Six’ kufuatia Luis
Moreno Ocampo kutaka
Uhuru Kenyatta, Joshua arap Sang,William Rutto,Francis Muthaura, Hussein
Ali, Henry Kosgei washitakiwe kwa uhalifu wa kivita, wakati Blair na Bush
wakila good time,ndiyo nini? Hapa hakuna ‘Impunity’? ama ‘double standards’?
Ocampo sasa kaachia ngazi na kuwachia Bensouda wa Gambia.
Ukifika Washington,
kamuulize Obama,kwanini kuchochea vita Misri na Yemen na kumshambulia Kanali
Muammar al Qaddafi huko Tripoli na Benghazi kwamba ame ‘Overstay’ wakati
hawajatwambia unyama wa makampuni ya kuchimba na kusafirisha mafuta na gesi,na
kutiririsha kemikali za sumu na kuua watu na wanyama migodini, Tanzania, ndiyo
nini?
Kaulize,kampuni la Unocal la California lilifanya unyama
gani huko Myanmar wakati linajenga bomba la urefu wa kilomita 62 huko Yadana,
hawakuua raia na kuwatumikisha bila malipo? Namna gani migodi ya dhahabu hapa
Tanzania kuwanyanyasa wananchi na kuua mifugo yao kwa kemikali za sumu bila
kulipa fidia?
Kamuulize David Cameron wa Uingereza,kwanini Shell na
Chevron wanapochimba mafuta Nigeria na kuharibu mazingira, wananchi wakihoji
wao huwalipa polisi pesa ili wawapige risasi?
Ndiyo Haki gani za Binadamu?
Kwanini Shell walimchochea Sani Abacha hadi akamuua Ken
Saro-Wiwa na wenzake wananne mwaka 1995?
Afrika
inaadhimisha miaka 17 kamili ya kifo cha Saro-Wiwa.Saro Wiwa aliuliwa
na Abacha na makampuni ya mafuta ya Uingereza,Uholanzi na Marekani.
Kwanini Shell la Uingereza na Chevron la Marekani
wanashirikiana na polisi huko Nigeria kuua waandamanaji wanaopinga wizi na
uharibifu wa mashamba yao kwa mabaki ya mafuta yanayoachwa kuingia katika
mashamba ya viazi na kuharibu uzalishaji,pasipo fidia yoyote?
Uingereza hao
hao na
Marekani na Ufaransa, wanamshambulia Kanali Muammar al-Qaddafi huko
Libya
kwamba anawashambulia waandamanaji! Wamempindua Gaddafi kisha
kumuua,lakini hakuna wa kusema juu ya unyama unaoendeshwa na mataifa
haya babe sana duniani.
Hizi ndizo ;double standards’ na mkuki kwa nguruwe hivi.
Demokrasia inaimbwa kuhitajika Libya,Yemen na Misri, wakati mahali
wanapokandamiza raia kwa kampuni zao kudhulumu na kuharibu mazingira, huko
hawasemi!
Kama kuua raia
wanaoandamana ni kosa,kwanini Hosni Mubarak na Qaddafi waitwe wauaji na
wachukuliwe hatua za kupinduliwa, wakati Shell,Chevron,Total n.k hayo makampuni
ya Kimarekani,Kiingereza na Kifaransa,hayajakamatwa na kufungwa jela huko The
Hague?
Qaddafi, ati ni muuaji wa waandamanaji, na
Wamarekani,Wafaransa na Waingereza wakiua watu ni ‘Liberators’!
Kuna mengi maovu
yanayofanywa na Marekani na washirika wao chini ya mwavuli wa NATO, na Rais
Obama hana ubavu wa kuyakemea, kwa sera za Marekani za Nje, za kuua na kupora!
Tena Osama aliua tu
hakupora rasilimali. Marekani chini ya Obama,wanaua na kupora rasilimali.
Kwa sababu hiyo, Obama na Osama ni wale wale tu(wauaji)
kasoro ni “b” na “s” katika majina yao!
Matendo ya Osama na Obama siku hizi
yanashabihiana sana, kasoro ni hizo 'b' na 's' tu!
Nawasikitikia
waafrika wanaomshangilia sana Obama kwa ushindi Marekani,watalia
machozi kabla ya mwakakesho kufika,mimi nitawacheka sana!!
0786/0754-324 074
No comments:
Post a Comment