TAHADHARI!!
*Mwanza kuendelea kubugia
kinyesi na kemikali za sumu
wasipodhibitiwa kwa sheria kali
WAZIRI WA
ARDHI,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Kajumlo Tibaijuka, aliwahi
kusema kwamba, Mwanza ni miongoni mwa miji iliyojengwa pasipokuzingatia sheria
za makazi na ulinzi wa mazingira.
Jiji hili
lilijengwa na Mjerumani, Emin Pasha,mwaka 1892,ili kuwa kituo cha ununuzi wa
mazao ya biashara kama pamba,katika ukanda wa ziwa.
Aliyekuwa
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Daniel Ole Njoolay, Machi 5,mwaka 2004 wakati akizindua
Mradi wa Majitaka jijini Mwanza,alisema
Jiji hili linaongoza kuwa na watu wengi wanaoishi katika eneo eneo dogo(high population density),kiasi cha
kuchafua mazingira,hususan vyanzo vya maji.
Jiji la
Mwanza sasa hukadiriwa kuwa na wakazi takriban milioni moja, ambao kwa siku
hunywa maji safi kiasi cha mita za ujazo 70,000.Wakazi wa Mwanza,kwa siku
huzalisha maji taka,zaidi kinyesi,kiasi cha lita milioni 38.Asilimia 90 ya maji taka hurejea Ziwa Victoria bila
kutibiwa.
Afisa
Uhusiano wa Mamlaka ya Majisafi na Taka Mwanza(MWAUWASA),Robert Masunya,katika
mahojiano na safu hii juzi, anasema wakazi wa Mwanza kwa siku hunywa maji yenye
ujazo wa lita milioni 70.
Hii ni sawa
na kusema,kwa siku wakazi wa Jiji hili,ambao wao wenyewe huita,” The Rock City”
hunywa kiasi cha mapipa 350,000 ya maji safi ya MWAUWASA. Maji taka
wanayozalisha(kinyesi,uchafu na kemikali za sumu) ni sawa na mapipa 200,000 ambayo
humwagwa ziwani kila siku.
Afisa
Uhusiano wa MWAUWASA,Robert Nasunya, ameiambia safi hii kwamba,ifikapo mwaka
2020,uwezo wao ni kuzalisha maji safi na salama yenye viwango vya ubora wa
kimataifa kufikia mita za ujazo 108,000 ambazo ni sawa na lita milioni 108, ama
mapipa 549,000 kila siku.
MWAUWASA
wana matangi matano yenye uwezo wa kuhifadhi maji yenye ujazo wa mita
27,000,sawa na lita milioni 27.
Kutokana na ujenzi holela usiozingatia sheria
za makazi,MWAUWASA wanapozalisha maji mengi hata kiwango kisichotumika(Idle
Capacity),yapo maeneo ambayo hayapati maji ya bomba yaliyotibiwa na kusafishwa.
Maeneo hayo
hayafikiwi na maji ya bomba; mengi yako katika miinuko mikali,vilimani,kwa
sababu maji ya bomba hutiririka kwa ‘gravity’,hayapandi mlima mpaka yasukumwe
kwa mashine kama pampu.
Maeneo ya
vilimani(Mwanza huzungukwa na vilima,miamba na mawe)yasiyopata maji ni pamoja
na Kabuhoro, Ibanda,na Mji Mwema.Mengine ni Sangabuye,Kayenze na Bugogwa.
Afisa
Uhusiano wa MWAUWASA,Masunya anasema, wakati wakazi wa Mwanza wanakunywa maji
safi lita 70 milioni kwa siku moja, na wakati uwezo wa MWAUWASA ni kuzalisha
lita milioni 108 kwa siku moja, lita 30 milioni hubaki-hushindwa kuwafikia
watu.
Masunya
anasema, wakazi hawa wa Mwanza huzalisha lita milioni 40 za taka zikiwemo
kemikali za majumbani, hospitalini,viwandani,madukani na hata kinyesi cha
binadamu na mifugo.
Serikali na
Jumuiya ya Ulaya(EU) wamejenga mfumo wa kusukuma maji taka kutoka lita 35 hadi
lita 170 kwa sekunde.Maji haya taka husukumwa hadi katika mabwawa 10 yaliyoko
Butuja,Ilemela ambako hutibiwa kabla ya kurejeshwa Ziwani Victoria.
Mradi huu
ulifadhhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Ujerumani(KfW) na ukakamilika Oktoba
mwaka 2010.Una uwezo wa kukusanya majitaka ya kiwango cha asilimia 15 tu ya wakazi wa Jiji linalokuwa
kila siku. Ukiamka asubuhi,unakuta vijumba vimeota milimani,pasi na ruhusa ya
Mipango miji!
Asilimia 9
ya wakazi wa Jiji hili la miamba,ndiyo
waliounganisha maji yao katika mfumo huu wa maji taka,nao hawazidi wateja
2,000. Hawa ndiyo kinyesi chao na kemikali zao husafishwa na kurejeshwa ziwani.
Nimezungumza
na Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA,Anthony Sanga, Alhamisi iliyopita, akasema
mfumo wa MWAUWASA wa kutibu maji taka,hufanya kazi chini ya kiwango,kwa sababu
wakazi wa jiji wameshindwa kuunganisha makaro yao ya maji machafu kwenye mfumo
huo wa kutibu maji taka.
Sanga,
ananiambia kwamba sasa wameanzisha mpango wa kuwakopesha wananchi ili
waunganishe maji taka yao kwenye mfumo wa maji taka.Wanachotakiwa kufanya ni
kulipa sh.5,000/ tu,halafu watakatwa pole pole baada ya kuingia mkataba.
Mfumo huu wa
maji taka ulijengwa na Sirling International ya Italia. Na kulingana na
MWAUWASA,Mwanza kuna vyanzo vya maji safi katika eneo la Capri Point,Chakula
Barafu na Luchelele, ambavyo vyote hutoa maji Ziwa Victoria linalochafuliwa kwa
kinyesi kisichorejezwa(recycled) kwa kutibiwa Butuja.
Kuna mpango
wa kuongeza chanzo kingine cha maji chenye uwezo wa kuzalisha mita za ujazo
50,000 kwa siku ili kuondoa shida ya maji Kabuhoro,Ibanda na maeneo mengine wanakolazimika
kunywa maji ya ziwani yasiyotibiwa na kupimwa kitaalam,ili kudhibiti uchafu na
kiwango cha kemikali.
Kemikali
zinaweza kuleta madhara ya afya kwa binadamu na wanyama.Ziwa Victoria liko
kandoni mwa migodi ya dhahabu ambayo hutumia zebaki(mercury)kusafishia
dhahabu,na kasha mvua zinaponyesha husomba zebaki hiyo hadi ziwani na kuua
samaki,wanyama,binadamu kasha kuharibu mazingira.
Hata
hivyo,licha ya MWAUWASA kuzalisha maji kwa kiwango cha ziada,Mwanza ni jiji
ambalo wakazi wake hunywa maji ya chupa ya Uhai kutoka Dar es salaam,
Kilimanjaro, wakati mwingine wanakunywa Rwenzori,kutoka Milima ya Rwenzori huko
Uganda!
Yaani, bei
ya lita moja ya maji ya kunywa Mwanza haina tofauti kubwa na bei ya lita ya petrol
kutoka Arabuni,wakazi Ziwa tunalo hapa,lakini maji yamechafuliwa kwa kinyesi!
Fika Mwaloni Kirumba,utajionea kinyesi majini,Ziwani…hii ndiyo Mwanza!
Sasa,Mkurugenzi
Mtendaji wa MWAUWASA,Anthony Sanga, ananiambia labda sheria zitumike sasa
kuwabana watu wanaotiririsha maji taka Ziwani, wanaokataa kuunganisha majitaka
yao katika mfumo wa MWAUWASA,ili yakatibiwe Butuja.
Wakati wa
mvua,watu hutapisha vyoo vyao na hufungulia makaro ya maji taka ambayo huingia
ziwani. Kutiririsha kinyesi mitaroni Mwanza ni kitu cha kawaida. Halafu eti
Mwanza ndilo jiji safi kuliko yote Tanzania!!
Zaidi ya
asilimia 90 ya wakazi wa Mwanza,ambao huishi vilimani katika makazi
yasiyopimwa,hhutiririsha kinyesi na kemikali ziwani. Maji ya ziwa yanapotumiwa
pasipo kuchemshwa ni hatari.
Novemba, 22
mwaka 2005,aliyekuwa Mkemia Mkuu wa Serikali, Dk.Ernest Mashimba, alisema jijini Mwanza kuwa Sheria
namba 3 ya mwaka 2003 ya Udhibiti wa Kemikali Viwandani na
Majumbani,haizingatiwi na wakazi wa jiji hili.
Hayati,Dk. Mashimba
alisema,Mwanza ni miongoni mwa maeneo ambayo kuna uvuvi haramu kwa kutumia
kemikali za sumu.Wakati wavuvi wanapovua kwa kutumia sumu,humwaga kemikali hizo
ziwani na kuhatarisha maisha ya viumbe.
Makopo ya
sumu Mwanza hutupwa mitaroni na kuachwa kuingia ziwa Victoria,wakati sheria hii
inawataka kuzika makopo hayo au kuyarejesha viwandani,yaharibiwe.
Kulingana na
Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa(WHO)asilimia kubwa ya watu wanaodhuriwa na
sumu ni kama hawa wakazi wa Mwanza,ambao huacha hata sumu za kuulia wadudu
kuingia ziwani.
Maradhi
yanayoongoza kuwaua watu wengi Mwanza ni minyoo,kichocho,kuhara damu,safura,homa
za matumbo na hata kipindupindu-hii ni kutokana na kunywa kinyesi hiki
wanachorudisha ziwani; kuliko na chanzo chao cha maji.
Mwanza,watu
hubugia kinyesi chao kwa hiari!!
Ili kunusuru
hali hii,Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Anthony Sanga, anasema sheria
zitumike kuwafanya wakazi wa Mwanza kuunganisha maji taka yao na mfumo rasmi wa
maji taka wa MWAUWASA.
0713 324 074
No comments:
Post a Comment