Monday, October 8, 2012

DALA DALA(3)



                              
Marekani, magazeti kama, Wall Street Journal, USA Today, Los Angeles Times, New York Daily Times, New York Times, Washington Post, New York Times, Tribune, Newsday n.k yanaongoza mauzo.
Huku kwetu Tanzania, jamii haipendi kusoma vitabu na magazeti yenye kuelimisha juu ya uchumi,ujasiliamali, elimu ama taaluma Fulani,kama kilimo bora n.k
Watu hupenda tetesi,picha zenye ladha mbaya(Bad taste),habari za kuvunjia watu heshima, zilizokolezwa na kuongezewa chumvi(exaggerated) ,uchochezi na mambo ya hihi-hivi tu,yasiyo na kichwa wala miguu,hushabikiwa sana.
Tovuti, blogs, face book, twitter zenye picha za kingono-ngono(pornography) hutembelewa na watuy wengi. Kamera za simu za mikononi siku hizi humfanya kila mtu kupiga picha bila hata kufuata taaluma, na kuzichapisha kwenye blogs,facebook n.k
Dhima, “Role” ya vyombo vya habari, “Kutaarifu/kuhabarisha,kuelimisha,kurekebisha jamii,kuburudisha,kukemea(to inform, to educate, to reform, to entertain, to incite) ilishatupwa na vyombo hivi siku nyingi.
Juma lililopita,tukagusia kuheshimu haki za watu,faragha zao(privacy),pasipo kisingizio kwamba eti wanahabari wana uhuru na kwamba kila kitu ni habari,hata kama mtu analalia jamvi. Jamii haina haja kujua kwamba mtu Fulani anaringa,lakini hulala penye jamvi!
Pana sheria zinazokataza vyombo vya habari kuchafua heshima za watu. “Libel” ni kosa linaloweza kuwa, ‘civil’ au ‘criminal offense’ .Kosa la madai au Jinai. Wanahabari wanategemewa kutangaza habari za kujenga na ziwe za kweli, sahihi na za kutegemewa na jamii,pasipo kuwa na upendeleo-habari zisiwe biased, ziwe ‘credible’ na ‘accurate’. Wanahabari hushauriwa kuchungulia katika pande zote za habari -checks and balances.
Tunataka jamii ipate habari ili iamue ifanye nini, na jamii ione mantiki na kuamua aidha kukubaliana au kutokubaliana.
Siku zetu hizi, DALADALA ya vyombo vya habari-MEDIA- inatumia haki ya kikatiba ya watu kujieleza- Freedom of expression, kuhukumu watu kwamba ni wezi,mafisadi na majambazi, na wengine kwamba ni miungu na malaika na mitume!
Vyombo vya habari vinalazimisha hata watu wote wafanye nini! Vimekuwa mgambo, mahakama,polisi, waendesha mashitaka,mahakimu na magereza kwa pamoja!!
Nakiri, vyombo vya habari ni muhimu sana katika taifa lolote, vina wajibu mtukufu kuifanya serikali ijitazame,ione makosa yake ili kujirekebisha,na watawaliwa wanapaswa kuhabarishwa ili waamue wao wenyewe nini cha kufanya.
Hata hivyo,vyombo vya habari vina jukumu mahsusi kuikosoa jamii ili ifuate sheria,taratibu siyo kuishia kuikosoa serikali tu na kuiacha jamii kuangamia kwenye majanga anuwai kama uchangudoa,ujinga,ukimwi,ugaidi n.k
Ukosoaji wa wanahari usiilenge tu serikali kutumia vibaya madaraka,’Abuses of power’ bali pia vyombo vyetu vitafute kuona yalipo maslahi ya taifa zima,na maslahi ya walio wengi.
 Tazama kauli hii:
“The Press is too quick to criticize authority, and does not support national interests”
Vyombo vya habari leo huishia kulalama na kuikosoa serikali, wakati vimesahau wajibu wa kuunga mkono maslahi ya taifa.Yako mengi, hata nchi inapoingia vitani, wanahabari hawapaswi kuunga mkono adui n.k
Kila mtu anajua sasa hatuna MAADILI,ndiyo maana maslahi ya taifa yanatupwa,na maslahi binafsi yanakumbatiwa na kila mtu,mimi hata wewe tukiwemo.
Nipewahi kuandika kwamba Maadili ni SHERIA ambayo kwa Kigiriki huitwa, “Nomos”, ama    ‘Torah’ kwa Kiebrania. Mana yake ni ‘Directions” maelekezo,mwongozo, “Guidance” utaratibu wa kufuata, ‘instructions’, ili watu wote waufuate kwa nia ya kuepuka makosa ama jambo Fulani muhali-baya.
Ni kutokana na Sheria, ‘Torah’ ama ‘Nomos’ tunapata uadilifu. Ikiwa watu watatii sheria na kuwa wanyoofu,tutakuwa na uadilifu. Kumbe, uadilifu hujenga unyoofu. Sheria za unyoofu(Moral Laws) ndiyo hasa maadili yanayolalamikiwa siku hizi kwamba yamepotea sana.
Ukweli ni kwamba, ‘Moral Laws’ ni AMRI 10 ZA MUNGU  ambazo ni kiwango bora cha maadili.
“God’s legal standard for morality” kiasi hata vyombo vya habari hatuwezi kuzishika hizo amri 10 za Mungu, kwa sababu wengine hawaamini kama kweli yupo, au ana itawala dunia hii. Labda alishakufa n.k!
Waandishi wa habari wengine licha ya kutokubali kwamba Mungu yupo, wengine hawampendi,na hakuna juhudi za kuwahimiza kuzitii sheria zake zinazojenga maadili katika taifa lolote. Kwa sababu hiyo, hata vipindi vya dini havipendwi na vimepuuzwa sana.
Nataka kusema kwamba uhuru wa habari ni mzuri sana. Hata hivyo, uhuru wa kusema chochote na mwandishi yeyote, au kunakilicho chote kutoka kwa mtu yeyote kwamba ndiyo haki  za binadamu kwa mujibu wa katiba ya nchi(Freedom of expression), ndiyo mwanzo hata wa kutangaza habari za Ibilisi, za uchochezi, maneno mabaya,picha mbaya za kutisha(bad taste);tunapotosha hata watoto wadogo na kuwafunza uchafu,kwa kisingizio cha demokrasia.
Tumeona kwamba, Shetani alimtumia Nyoka kama “MEDIUM”Chombo chake cha mawasiliano kupeleka uchochezi kwa Adamu na Hawa ili wachukie SHERIA/MAADILI’TARATIBU/MWONGOZO/KANUNI kwamba ni vitu visivyotekelezeka; na kwamba mambo hayo yote hapo juu ni ukatili,udikteta na ubinafsi wa Mungu! Mwanzo 3:1-5.
Je, sisi vyombo vya habari na wanahabari katika nchi hii,siku hizi tunatumia demokrasia na uhuru  aliodai Ibilisi dhidi ya sheria za Mungu KUFANYA NINI?
Au ndiyo sababu tunapotosha watu makusudi?
Sisi Media, tumeamua kuwa njia ya Ibilisi kufundisha ajenda yake, ili kuwapotosha watoto,kuwafundisha maneno mabaya,ngono, matusi,kuvaa nguo za uchi,nyimbo za uchi,picha za ngono,uchafu mwingi usiosemeka!
Tazama televisheni nyingi uone michezo ya kuigiza ya uchi uchi,muziki wa ovyo wa wabwia unga na wavuta bangi, maneno machafu ya kingono,ulevi, uvuta bangi, umalaya, halafu tunapiga kelele za kijinga:
“Taifa linaangamia kwa kukosa maadili! Mafisadii!”
Nini chimbuko la mafisadi na walevi, wabwia unga, kama si vyombo vya habari kuwahusudu sana wavuta bangi,Malaya,machangudoa na majambazi na wauaji wa Marekani na Ulaya?
Mauaji ya kinyama watoto wameyaona kwenye televisheni,kwenye sinema, uchangudoa watoto wametazama kwenye twitter,facebook,blogs n.k maadamu siku hizi tumewanunuliwa vijisimu vingi vya China, vinawaharibu wawapo hata vitandani vyumbani mwao. Adui namaba moja wa Maadili ni vyombo vya habari!
Kimsingi,vyombo vya habari visipotumika vizuri,ni DALADALA inayopeleka kizazi hiki Jehanum ya moto; vyombo vya habari vinamsaidia SHETANI KUTANGAZA uhalifu kuliko vinavyotumika kuelimisha watu na kuwaondoa kwenye giza.
Kuna vipindi vingapi vya dini? Nani anafuatilia vipindi vya dini kwenye televisheni? Muda wa habari ukifika watu wana tune kwenye michezo,muziki na kwenye comedy!
Matangaza ya pombe,sigara huwavutia hata watoto kupeperusha moshi angani kama treni, na kusema maneno machafu ya mastaa wa Ulaya au wa hapa Bongo! Nguo za nusu uchi,mapenzi,ngono,filamu za mauaji,za ngono,michezo ya kiwenda wazimu,ukatili,uvuta bangi n.k ndiyo vipindi vinavyopendwa sana!
Vyombo vya habari-MEDIA-vinapeleka habari namna hii kwa watazamaji,wasikilizaji na wasomaji, wau wanaita, Mass Audience. Nakwamba vyombo vya habari ni kama kisu,kikitumika vibaya kitakata nyanya,vitunguu na nyama mekoni nawe utakula chakula bora na kitamu sana. Kikitumika vibaya hiki kisu utaua watu!
Shetani, ametumia MEDIA au kimoja MEDIUM tangu Edeni. Nyoka alitumika kama chombo cha habari kuwasilisha uchochezi kwa Hawa.
Sasa, angalia kama vyombo hivi vya habari vinatekeleza hiyo dhima, “Role” ya vyombo vya habari: To inform, to educate, to reform, to entertain, to incite and to set an agenda!
 Kuhabarisha,kufundisha, kurekebisha jamii,kuburudisha,kuonya na kuweka jukwaa la mjadala wa manufaa kwa jamii.
Je, msomaji, wewe redio yako,televisheni yako na magazeti yako yanakusaidia kwa haya na watoto wako wanafaidika?
Sisi wanahabari tujiulize,tunahabarisha nini? Tunawapa watu jukwaa la kusema nini kama siyo utumbo?
 Sikiliza hata vituo vya redio, utasikia Kiswahili cha ovyo sana, “Masaa masita!!” badala ya saa sita, “Hiko” badala ya Hiki kijiko au hichi kijiti!
Eti lisaa limoja! Kuna lisaa  limoja jamani? Kuna saa moja,basi, Uchafu gani huu? Sikiliza nyimbo zao sasa, wasela wanaimba huku wakishika sehemu zao za siri utadhani wanawashwa upupu! Eti ‘hiko kikombe!’
Eti burudani, utasikia mtangazaji anawachochea manazi wa Yanga au Simba kumdunda mwamuzi kwamba hayuko ‘Fair’ kabisa!
Hivi wewe mtangazaji au mchochezi? Unataka manazi wafanye nini kama unasema goli lilikuwa si halali mwamuzi kaiua timu yenu? ‘sisi moja-wao bila!!
Watangazaji hao wa siku hizi.Muziki wa matusi ya nguoni, taarabu za kusimangana na kuoneshana viuno, hata kwa watoto under age. Katika Biblia, katika Amosi 6:5 Mungu anasema, “Niondoleeni nyimbo zenu za upuuzi” wanaimba Nakupenda tangu asubuhi hadi usiku wa manane, hakua kingine!
Siku hizi,nyimbo kama “Kabwe rudi nyumbani ushirikiane nasi kulijenga taifa” hakuna, hakuna uzalendo wowote,ni ngono tu na viroba!
Hakuna vitabu,hakuna maktaba.Kila mtaa kuna baa,saloni na stoo bubu,hakuna maktaba wala watu kujisomea. Vitabu tunavyopenda ni vyenye mapaja manene ya akina mama na uchawi. Hakuna maarifa, magazeti ya ngonongono ndiyo yanayopendwa.
Sasa, tunasema vyombo vya habari Media ni mhimili wa Nne wa Dola.
Mwanahistoria wa Kiingereza,Thomas Babington Macaulay ndiye aliyeita Media kwamba ni “The Fourth Estate” kwa sababu, ni mithili ya mbwa mlinzi kwa jamii. Vyombo vya habari vina jukumu mahsusi kama mbwa mlinzi –Watchdog Role.
Mihimili mingine ya Dola ni Mahakama,Serikali na Bunge.Sasa vyombo vya habari vinafuata,lakini vinaongoza kuchafua maadili ya watu na vinachangia sana kuwaambia watu kutofauata sheria.Wewe unamnunulia mwanao toy  la bunduki, si unataka awe jambazi?
SHERIA hufunua Mungu na tabia njema aliyo nayo na utakatifu na usafi wake.Sheria ni nakala ya upendo wa Mungu,ni kiwango cha maadili bora,maadili yametupwa kwa sababu vyombo vya habari ni Daladala iliyowasomba wengi na kuwatupa shimoni.
Siku hizi kuna ‘Yellow Journalism’ ambamo kuna ‘cooked stories’ mtu ana kaa anatunga story na kuwagutua watu anaongeza chumvi habari, sensationalism, basi vijana wanaamua kubeba rungu na kufanya vurugu,hapo mwandishi anapata Lead story! ‘Kiama chatokea Mwanza,Arusha au Dar!!’
Watazame baadhi ya wahariri wa vyombo hivi, chungulia maisha yao nje ya ofisi,yanatia kinyaa,Siyo waadilifu.Wao na wakuu wao wa vyombo vya habari,wameshiriki sana kupora malipo ya waandshi wao wa mikoani, ambao sasa ni omba omba,wanaoingilia hata harusi za watu-trespassing- na kudai posho!!
Wakuu wa tasnia ya habari baadhi yao ni wa ajabu mno, wanakula mgongoni mwa wanahanari! Kuna maadili wapi na yapi kwenye tasnia ya habari,kama mwandishi anaomba nauli kila siku,ili kujinusuru maana hajalipwa malipo yake miaka mitatuMwandishi wa safu hii(wa kwanza kulia) akiwa na wenzake walipokuwa wakiendesha kipindi katika studio za televisheni ya Barmedas Jijini Mwanza
 Hapa ndiyo mwanzo wa kutegemea vijizawadi-Payola-kutoka kwa vyanzo vya habari zake ili apate kujikimu! Hapo unategemea habari gani,kama siyo watu kilishwa uongo na uchochezi,na blahblah tu.
Amini usiamini,vyombo vya habari ni DALADALA inayopeleka watu SHIMONI -shimo la Tewa, aliloimba Samba Mapangala.
0713 324 074










Monday, October 1, 2012

DALADALA (2)



ARISTOTLE(384-322 BC) wa Ugiriki, aliwahi kusema hivi:

“To say of what is that is not; or of what is not that it is-is FALSE. While, to say what of what is that it is and of what is not that is not, is TRUE!!
 ARISTOTLE
Aristotle, alikuwa akisema hivi: “Kusema namna jambo lisivyokuwa ni Uongo, wakati mtu anaposema jambo lilivyo ama namna kitu kisivyokuwa,wakati kweli hakiko hivyo, huu ni UKWELI.
Ukweli, unaweza kuongopa pindi nusu ukweli unapochanganywa na uongo. Ukweli ni nini basi?
Kulingana na wanafalsafa UKWELI ni mwafaka baina ya mambo halisi au matukio halisi na ule uhalisia wa mambo( Truth is agreement with facts and reality).
Hata hivyo, kulingana na Injili ya Yohana Mtakatifu, Neno la Mungu ndiyo KWELI yenye uwezo wa kuwapa watu UHURU.
UKWELI, ni ulinganifu baina ya kilichotendeka, ama kilichopo na uhalisia wa mambo(agreement with facts and reality).
Nikaeleza katika sehemu ya kwanza ya makala haya,DALADALA, kwamba neno, “KAMUNYE” maana yake ni DALADALA, ambacho ndicho kichwa cha makala yangu hii.
Dada yangu mmoja, raia wa Uganda,Mwalimu wa sekondari Jijini Mwanza, ameniambia, “KAMUNYE” ni ndege TAI ambaye nimepata kuandika wasifu wake katika makala zilizotangulia.
Daladala za jijini Kampala zimepata jina hilo, KAMUNYE kufuatia sifa za ndege huyu tai; kuruka mbali na juu zaidi kuliko ndege mwingine, na uwezo wa kuona mawindo kutokea umbali mrefu
Wakati mwingine tai hufananishwa na uwezo wa Mungu wa kuona na kujua mambo ya kila mahali ulimwenguni, OMNISCIENCE.
Twapaswa kuona mbali kama Kamunye, wakati tunapofanya bidii kutafakari baina ya ukweli na uongo.
Hata hivyo, zipo DALADALA nyingi katika nyanja tofauti za maisha yaliyochanganyika, baina ya raha na karaka,furaha na huzuni,tumaini na kukata tamaa na amani na kinyume chake.
Maishani,kuna mema na mabaya, faida na hasara, kufuatia chaguzi zetu za kuamua kukwea DALADALA tofauti tofauti.
Leo,tujadili kuhusu UHURU wa uchaguzi- FREEDOM OF CHOICE.Dictionary(kamusi0 ya Kiingereza husema neno, Freedom,(Uhuru)kama ifuatavyo:
“Freedom is the state of being free; right or privilege of unlimited access”.
Tafsiri yangu: “Uhuru ni hali ya kuwa huria; ni haki au fursa ya kufika popote au kufanya chochote pasipo kizuizi”.
Kwa sababu hiyo, “Unlimited Access” iliyopiganiwa mwanzoni kabisa wa kuumbwa kwa Dunia,ni pale Ibilisi(Shetani) alipomwambia Hawa katika Bustani ya Edeni kwamba, Binadamu akipewa kujua,kufanya mambo yote-basi atakuwa kama Bwana Mungu(Tazama Mwanzo 3:5).
Mungu, ana “Unlimited Access” lakini kwa kuwa yeye ana nguvu zisizo kawaida ya wanadamu(OMNIPOTENT), hawezi kufanya mabaya. Mungu anayajua mabaya.lakini hana cha kumlazimisha kufanya mabaya-binadamu hawezi kujua baya na akaepuka kulifanya!
Tangu zama za Adamu na Hawa,kama mwaka wa 4004 BC) kumekuwa na harakati nyingi za wanadamu kusaka “Accessibility” Haki ya kupata au kuingia popote na kutenda chochote.
Katika sehemu iliyotangulia ya makala haya, DALADALA,tukajadili kidogo, “DALADALA” waliyokwea viongozi wa dini.Tukawaona wachungaji wanaume wakiwabatiza wanawake wakiwa uchi wa mnyama huko Uganda!
Walikuwa wakiwabatiza mahali penye maji mengi huko mtoni, ambamo waliwatosa au kuwazamisha majini, “Baptizo,” Kigiriki maana yake kuzamisha ambamo jina Baptism,lilitoholewa.
Naam, Uganda,ndiko mahali Kibwetere aliwachoma moto waumini wake 530 huko Kanungu; aliwapandisha “Daladala” ya kuendea peponi na kuzimuni kwa pamoja!
Leo, tutupie macho Daladala waliyokwea WANAHABARI.Naam, MEDIA!
Neno, MEDIA linamaanisha wingi wa neno MEDIUM ambamo limetokea neno,MASS M EDIA.
Nitasema ukweli mkali hata kama nitafanya KOSA LA UKWELI(The Crimes of Truth) kama Socrates,kama Martin Luther, Mahatma Gandhi n.k potelea mbali nichukiwe na wapenda kinyume cha ukweli. Naam, ukweli mchungu.
“Medium” maana yake ni chombo cha kuzungumzia,kupitia kuwasiliana,hata baina ya waliohai na wafu na mizimu, majini,misambwa n.k
Hata Ibilisi alimtumia Nyoka kama “Medium” ili kuwasiliana na Hawa, kwa nia ya kumpotosha ili aasi maadili ya Mungu(Tazama Mwanzo 3:1-24)
Medium ni chombo cha mawasiliano(vingi huitwa Media) baina ya watu walio hai kwa waliohai au wafu kwa waliohai. Tunaposema wafu kuwasiliana na waliohai tuna maana, umizimu, Spiritualism.
Kwa bahati mbaya sana, watu huamini kila kinachozungumzwa,kuonekana na kusomwa na vyombo vya habari-media.
Hawajui, hata Ibilisi ana “Access” anazungumza kupitia vyombo vya habari pasipo kuzuiliwa na chochote kama tulivyoona mantiki ya 'accessibility”.
Misingi hiyo huitwa, Uhuru,Demokrasia na eti Haki za Binadamu,haki za kusema, Freedom of Expression!
Watu hawa hawajui, Vyombo vya Habari ni DALADALA ya kuendea pazuri au pabaya, na pengine pazuri na pabaya kwa pamoja!
Kuna watu hawatofautishi maoni, habari 'hard news' makala,tahariri n.k. Hawatofautishi maoni ya mtu anapohojiwa na habari iliyothibitishwa, “balanced story”.
Hawajui katika vyombo vya habari kuna 'Facts” mambo halisi yanayozungumzwa na ushahidi upo na “Fiction” hadithi za kutunga ili kuburudisha.Pengine habari hujaa porojo tu,propaganda,uchochezi na umbea.
Wanaokwea Daladala ya vyombo vya habari, wao huitwa, “audience”ambao wengi wao hawana habari kuwa Ibilisi naye ana ruhusa, “access” ya kutoa uchochezi wake, “SEDITION”, badala ya “TRUTH” ukweli wa mambo-tumeona makosa ya ukweli-The Crimes of Truth.
Kulingana na taaluma ya habari, “SEDITION” is a speech or action encouraging rebellion against the government”
Maneno au vitendo vya kuongoza watu kuasi mamlaka ya serikali. Hivi ndivyo isemavyo sheria hata ya Uingereza na Marekani. Kumbuka kuna sheria mbaya(Bad LAWS)na usiniambie kuzivunja wakati zipo bado hazijaondolewa!
Naam, kuna LIBEL-Taarifa zinazotangazwa katika vyombo vya habari kwa nia ya kuharibu/kuchafua heshima ya watu na kuwaharibia utu wao.
Kuna uhuru wa vyombo vya habari 'Medium” kimoja ama Media,vingi.Taaluma ya habari na weledi, Profession and Professionalism,husisitiza nia ya ku 'Ku- balance between freedom of the press with the rights of individuals to privacy and their good names”.
"Professional Attitude” ya mwandishi wa habari mwenye weledi,ni KUJENGA jamii bora. Siyo kubomoa.Siyo kuchochea na kuchafua watoto,hasa wasichana na wavulana.
Siku hizi vyombo vya habari hujenga au hubomoa? Majibu unayo wewe mwenyewe.Uandishi wa kitaaluma na weledi ni kuweka uwiano/ulinganifu/mizania kati ya uhuru wa vyombo vya habari na Haki za kila mtu,pamoja na kutoingilia uhuru wawatu na kuwaharibia majina yao mazuri katika jamii.
Uhuru wa habari huishia mahali haki za Binadamu zinapoanzia. Habari,maneno,picha za atu,vitu n.k lazima vifuate misingi ya usawa na haki.”Fairness” na usahihi,”Accuracy” na habari lazima kutokuegemea upande kwa nia ya kupedelea na ndiyo habari yenye 'Objectivity”.
Sasa tujiulize: Twasoma nini na kusikiliza na kutazama kitu gani? Vyombo vya habari vinajenga jamii au kuibomoa?
Vyombo vingi vinavyopendwa sana hubeba blah blah nyingi,vicheko na maneno ya matusi yasiyo haiba(hasa ya watangazaji wa kike ambao hujidai kuongelea puani) huku wakisimanga wenzao wazi wazi walionyang'anyana mibuzi huko mitaani!
Vyombo vya habari hususan baadhi ya redio, hutumika kuumbua, kutusi,kutukana,kupeleka mivuto ya ovyo na kupiga vijinyimbo dhaifu vya matusi na ngono tu,hakuna messege.
Lugha wanayotumia mbovu saka, “Hiko” badala ya 'hicho' masaa masita, badala ya saa sita n.k mradi ni kichefuchefu,kikwifukwifu,utumbo mtupu!
Vyombo vyenye blah blah hizi hubeba purchasing power kubwa,husikilizwa na wengi na kupigiwa mfano!!
Redio zenye kuelimisha,kuburudisha,kuonya,kukosoa,kuweka ajenda n.k zimeachwa na vijana-vipindi vya elimu havipendwi,ni miziki ya ovyo ya ngono tangu asubuhi hadi asubuhi, hadi wameacha vijana kufanya kazi- idleness,
ili kusikiliza vijiredio na simu za mkononi.
Picha za ngono zinaonyehwa magazetini na televisheni. Picha za ngono- pornography, hupendwa sana siku hizi kunako facebook,twitter,blogs n.k
Katika vyombo hivi kuna matangazo ya biashara,ya POMBE,SIGARA n.k hata inaonekana itakuwa ngumu sana kwa kizazi hiki kumpata mtu ambaye ni “Teetotaler”-havuti wala hanywi pombe!
Itaendelea
0713 324 074




Friday, September 28, 2012

DALA DALA




 ASKOFU SENTAMU WA UGANDA

  TUKIIDURUSU Historia, tunawaona wanamapinduzi wengi waliowahi kuteswa,kuumizwa na kuuliwa kwa sababu ya kuushikilia ukweli.
Naam, Mahatma Gandhi,Socrates, Nelson Mandela alifungwa miaka 27 akaja kuachwa huru Feburuali 11 mwaka 1990, Martin Luther wa Ujerumani, Martin Luther King Junior wa Marekani, orodha ni ndefu kupindukia.
Wapo mashujaa wengi waliojitoa mhanga maisha yao ili kuusema ukweli,wakaishia kuuliwa mithili ya wasaliti na maadui. Aghalabu, hatuuelewi ukweli kirahisi. Ukweli umesitirika sirini.
‘Kuelewa’ kwa lugha ya Kigiriki ni “Ginesko” yaani kufahamu,kupata maarifa, yaani kupata maarifa ya kweli,ili kujua ama kufahamu.
 Kufahamu kweli ni kitu kimoja; na kuufahamu ukweli na kuupenda ili kuutumia katika maisha ya kila siku,kila wakati ni kitu kingine cha muhimu sana.
Hata hivyo, mashujaa wengi wa ukweli wameadhibiwa mithili ya wahalifu. Kusema na kuishi kulingana na ukweli ni kufanya makosa ya ukweli-Crimes of Truth.
Mwaka jana, nilikuwa nikijaribu kusoma Gazeti la Uganda liitwalo, “KAMUNYE” maana yake, DALADALA. Hizi Daladala ambazo huku kwetu tunaita Vifodi(Arusha), Mwanza wanaita Express n.k
Gazeti hilo, Daladala ama Kamunye,la Ijumaa,Julai 29 mwaka 2011,liliandika habari ya dini inayobatiza wanawake wakiwa uchi wa mnyama huko Uganda.
Gazeti hilo,huandika kwa lugha ya Kiganda, kichwa kikubwa cha habari cha kushangaza: “KIKA!”niliambiwa, “Kika!” ni neon ambalo halina tofauti kubwa na lile la Wajitta waishio tarafa ya Nyanja,huko Musoma vijijini, “Echika!” yaani kituko kikubwa mno,maajabu makubwa n.k
Halafu, liaandika kwa lugha ya Kiganda, “Eddiini eyambula abakazi okubabatiza esonze!” Vichwa vidogo vya habari hiyo  (sub headings) vilisema,”Abasajja basudde amaka okugyesogga!”
 Nikaambiwa na mtu aliyekuwa mhariri wa Jarida letu la Kanda ya Ziwa, The Lake Zone Today, Mukoche Sando Michael, raia wa Tanzania mwenye asili ya Uganda,kwamba gazeti hilo Daladala liliandika habari ya mchungaji mwanaume huko Uganda kuwabatiza wanawake warembo sana wanapokuwa uchi wa mnyama.
Mchungaji anayebatiza wanawake hawa wanapokuwa uchi huko mtoni,kichakani ni mwanaume rijali.Sasa, ukitaka uchukiwe, ama pengine uuawe. Nenda kawaonye wanawake wanaokwenda kubatizwa mtoni na wanaume wawapo uchi wa mnyama!
 Naam, nakusudia kuandika juu ya makosa ya ukweli-  The Crimes of Truth. Nakusudia kuandika juu ya watu wasiopenda ukweli wasije wakakosa chumo la udhalimu.Hapa duniani zipo dini nyingi za kihuni. Dini za uchi, ambazo watu husali wakiwa uchi wa mnyama,nyakati za usiku wa manane,taa zinapokuwa zimezimwa kabisa!!
Hata maskofu na wachungaji wa dini hizi hudai wanafundisha KWELI ya neon la Mungu, kwamba dini ni kama DALADALA ya kuwapeleka abiria mahali sahihi waendapo. Kwamba, duniani hapawezi kuwepo na DALADALA moja, dini moja,mlango mmoja na njia moja ya kuendea kwa Mungu n.k.
 Naam, DALADALA.Demokrasia ina ‘tamu-chungu’ zake,na ndiyo maana kuna CCM.Chadema, CUF, ADC n.k Kuna Mungu,miungu, Ibilisi, majini,misambwa, ‘tree spirits’ miungu ya voodoo n.k
Biblia, katika Injili ya Yohana 8:32 husema, KWELI ya NENO LA MUNGU ambayo mtu akiifahamu basi huwekwa HURU. Kwa Kiingereza, Yohana 8:32 husema hivi:
“The truth will set you free” ikiwa na maana kuwa KWELI YA NENO LA MUNGU itakufanya uwe huru.Uhuru ni kinyume cha utumwa,mbinyo,vizuizi ama kitu cha kulemea moyo na akili,kama vile mazoea mabaya, ‘Addictions’ n.k
Hata hivyo, kulingana na Kamunye(DALADALA) kuna mungu bandia siku hizi anayewafanya wachungaji wanaume kuwa HURU kuwabatiza hata mama zao na dada zao wanapokuwa uchi wa mnyama huko mtoni. Ubatizo huu ni ule wa kuzamisha, “Baptizo” majini,mtoni,baharini ama ziwani penye maji mengi. Na wanawake hubatizwa wakiwa uchi wa mnyama.
Yohana 8:32 huleta mjadala mkali sana juu ya ukweli uwawekao watu huru kweli kweli. Uhuru upi? Wa kubatizwa wewe mwanamama ukiwa uchi wa mnyama na mchungaji au kasisi mwanaume rijali? Uhuru upi?
Wa kuachana na tabia mbaya na mazoea ya hatari yanayolemea watu kama ulevi,uvutaji sigara,uchawi,uadui,uchafu,ufisadi,unyama,uzinzi,uasherati n.k?
Naam,UHURU katika muktadha tofauti. Uhuru katika miungu tofauti na DALADALA tofauto tofauti za kusafiria kwenda malengo tofauti huku ukweli unapofichwa kwamba kuna njia tofauti zenye lengo moja! DALADALA!
Tujadili kidogo kuhusu manabii,mitume wa siku hizi, wachungaji,masheikh,maimam na makasisi na maskofu kukosa ufahamu wa neon la kweli la Mungu wa KWELI hadi wameupindua ukweli kichwa chini-miguu juu,sasa mwanaume anawabatiza akina mama warembo wakiwa uchi wa mnyama, ili kuwapeleka mbinguni kwa DALADALA aina hiyo!
Maaskofu wanaolewa na wanaume wenzao.
Britain's Queen Elizabeth speaks with Rowan Williams, The Archbishop of Canterbury during a reception at the Houses of Parliament in London March 20, 2012. REUTERS/Toby Melville
Rowan Williams(62)
Juzi, nikisafiri kwa Daladala moja, kutoka Buzuruga hadi Kirumba jijini Mwanza, Kondakta akaanza kulalamika kufuatia habari iliyokuwa ikitangazwa saa saba mchana na Radio  Sauti ya Ujerumani(DW)kwamba uchanguzi wa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiingereza, Anglican, utaweza kulimega kabisa kanisa hilo,kufuatia kuunga mkono ushoga.
Wagombea katika nafasi hiyo inayoachwa wazi na Rowan Williams kufuatia kupindukia umri wa miaka 70 ni Richard Chartres(65), Christopher Cocksworth(53) na Mganda John SENTAMU(63),na JUSTIN WELBY
.Mmoja wao jina lake Wazirio Mkuu wa Uingereza, David Cameron analiwasilishwa kwa Malkia Elizabeth ili litangazwe kuwa ni Askofu Mkuu wa  Canterbury, Haya yamefanyika Jumatano na Alhamisi iliyopita.Tuyaache,yana wenyewe.
Askofu wa Canterbury, Rowan Williams anaachia ngazi, sasa uchaguzi mwingine ulikuwa ukifanyika wa askofu atakayechukua mikoba yake.Sasa huyu ‘Konda’ alikuwa akilalamika kusikia kuna askofu Shoga wa kanisa hili, ni mwanaume aliyeolewa na mwanaume mwingine-hii nayo ni Daladala nyingine!

Askofu V.Gene Robinson(kulia) akiwa na “Buzi” lake
http://ts1.mm.bing.net/images/thumbnail.aspx?q=4638316305122384&id=3221e7e58c16d89766ed39d09df26b13 
 V.GENE ROBINSON
Mwandishi,Chief Red Jacket,katika karne ya 19 alisema utata wa kumwabudu mungu aliyemwita, “THE GREAT SPIRIT” utawachanganya watu wengi. Bahati mbaya sana, Waafrika wengi tunapenda kuchaguliwa mungu wa kuabudu na hawa Wazungu.
Watu wa kwanza kumwabudu Mungu wa kweli ni Waisraeli, akina Ibrahim naye alitokea Ur ambako ni Irak, na siyo Uingereza au Marekani.
Nataka kusema kwamba Mzungu alishaleta ‘Moto Mgeni’ katika ibada ya kweli kama walivyofanya Korah,Dathan na Abiram wakamezwa na tetemeko la ardhi sambamba na wenzao 250 waliowashabikia.
 Kwa kifupi, DALADALA ni makala itakayojadili kilichomo NYUMA YA PAZIA(Behind the scenes) ili tuone uchafu uliomo katika dini hizi siku hizi,na zote ni DALADALA zinazojidai kuwasafirisha watu hadi kwa Mungu,labda kwa mungu,miungu au Great spirit.
Tutajadili faida na hasara za uhuru. Katika Daladala tutajadili uhuru na faida na hasara za kuchagua jambo lolote kama vile Mike Ezra,raia wa Uganda wakati Fulani kutaka kuinunua Klabu ya Leeds ya Premiership huko Uingereza kwa Pauni milioni 60 ambazo ni Dola za Marekani milioni 96. Ni uamuzi tu unaofuatia uhuru wa uchaguzi.
 Itaendelea
0713 324 074