Thursday, November 8, 2012

Mnamshangilia Obama,lakini siyo Mwafrika ng'oo!

NIMEPATA KUSOMA mzaha katika gazeti moja litolewa ng’ambo, kwamba Obama na Osama ni mtu yule yule kasoro herufi mbili, “b” na “s” katikati ya majina yao!

Kulingana na lesoni ya Waadventista wa Sabato(Sabbath School Bible  Study Guide) ya Oktoba hadi Desemba, 2010 ukurasa wa 72 majina ni muhimu tangu nyakati za Biblia. Jina linamwonesha mtu tabia yake,urithi wake toka kwa wazazi wake.Mtu hufanana na jina lake.
 Wakati mwingine, jina hutafsiri kile wazazi walichotazamia au kile kilichowakabili wakati mtoto  anazaliwa.
Bila shaka umepata kusikia majina ya akina Semeni, Siwajibu, Masumbuko,Chuki,Mashaka,Majuto, Nyamayao n.k!
 Majina haya,huzungumza mazingira mtoto alimozaliwa na majaliwa yake. Majina kama Abram,Yakobo,Danieli n.k pia yalitabiri tabia ya watu hawa ya uchaji Mungu, utegemezi kwa Mungu kama Hakimu na Mwamuzi.
Yakobo, tafsiri yake ni ‘Mdanganyifu’ aliyemdanganya babaye, Isaka wakampora kakaye, Esau haki ya mzaliwa wa kwanza.
Kulingana na somo,’What’s in a Name?’ katika lesoni hiyo ya Wasabato, jina Osama,kwetu ni mtu katili; Yule gaidi hatari sana aliyesababisha majengo pacha ya World Trade Center(WTC)mjini New York kuteketea kwa mabomu Septemba 11, mwaka 2001 na zaidi ya watu 5,500 wakapoteza maisha.
Osama, katika kizazi hiki ni muuaji hata kama baadhi ya watu wanamwoma mwanaharakati, sahahidi mwaminifu, martyr!
Ni kwa sababu sababu hii tu,mtu akisema(Rais Barack Hussein)Obama anafanana na Gaidi la Kimataifa,linalosakwa sana,Osama(Bin Laden)aliyelipua pia Makao Makuu ya Wizara ya Ulinzi ya M arekani mjini Washington, “The Pentagon” nasi tunamwona leo Obama kwamba ni muuaji na katili kama Osama.
Kwamba, Obama na Osama ni mtu Yule Yule kasoro herufi ‘b’ na ‘s’ basi lingekuwa jina moja!
Namfananisha Rais Obama wa Marekani na gazidi linalosakwa sana duniani, kwa kuhusika na ajali ya Septemba 11, hadi leo WTC haikujengwa, uwanja umeachwa kama Mnara wa Kumbukumbu ya kiama kile,na mahali hapa panaitwa, Ground Zero.
Katika safu hii napenda kuandika  kwamba Waafrika hawana   sababu ya kumsahangilia sana Obama, kwa kufanikiwa kukalia kiti kile cha ngozi nyeusi hapo “Oval Office” katika Ikulu ya White House,Marekani, kwa mara nyingine baada ya kumshinda Mitt Romney wa Republican kwa ushindi wa kishindo wa kura 302 za electoral college,dhidi ya 206 za Romney mchovu!
Kwamba, ingawa Obama,babu yake Mzee Obama alikuwa “Boy” wa Wazungu mjini Nairobi,Kenya akamzaa Hussein Obama aliyekwenda kusoma Marekani akakutana na mama Mzungu akampa ujauzito na akamzaa Barack Hussein Obama, bado Obama siyo Mwafrika.
Nawashangaa sana Waafrika wanaomshangilia sana Obama,hadi mishipa inawatutumka vichwani! Obama siyo Mkenya wala Mghana!
Obama, ni Mmarekani anayetekeleza sera za Marekani za kibeberu; na lazima awe mtii kwa kiapo chake cha kulinda,kuhifadhi na kutekeleza sera za Marekani kwa maslahi ya Wamarekani,na aslani Obama hawezi kuwajua, na kuwajali Waafrika!
 Naam, Obama siyo Mwafrika; ni Mmarekani. Kipaumblele chake siyo Kogelo,Kisumu, Nairobi, Afrika Mashariki,Afrika. Obama anatekeleza maslahi ya Marekani na viwanda vya Wamarekani, anajali mustakabali wa Marekani zaidi,hata kama kwa kufanya hivyo Afrika italipuka katika miali mikali ya moto.
Nadhani, sasa Afrika inameza machungu ya kumshangilia sana Obama Novemba 2008 hadi Januari 20,mwaka 2009.Wanarejea kosa hilo hilo la kumshangilia,wakidhani mhula wake wa Pili, White House, ataitazama Afrika ili kuwatupia  msaada!
Obama   ana macho yanayoitazama Marekani, kamwe siyo Afrika.Waafrika msitarajie kitu kwa Obama,jengeni nchi zenu!
Kwa sababu ya maslahi matukufu ya Marekani, Obama sharti apate kigugumizi katika mgogoro wa Cote d’ Ivoire, au umasikini wa Waafrika na njaa Ethiopia au vita Somali. .
Kwa sababu,Obama kwa maslahi ya Marekani,hawezi kukurupukia wimbo wa ‘Demokrasia’ ama Haki za Binadamu,kusema kwamba Alassane Ouattara,Muislam wa Kaskazini mwa nchi, aliyetangazwa mshindi wa kiti cha Urais na Tume Huru ya Uchaguzi(CEI),ati aungwe mkono kijeshi na Marekani na Washirika wake,au na Majeshi ya Umoja wa Kujihami Ulaya Magharibi.Marekani ni wale wale wanaoweza kuwaunga mkono hata waasi na madikteta kama Meles Zenawi,mradi anatimiza maslahi yao matukufu.
Gbagbo yuko Hague, kujibu mashitaka ya uhalifu na mauaji yaliyotokea...lakini Gbagbo alikuwa rafiki yao wamemtupa baada ya maslahi kuanguka upande.
Ouattara, ambaye Januari Mosi mwaka juzi alitimiza umri wa miaka 70,licha ya kusoma Pennsylvania na kufanya kazi IMF,hataaminiwa na sera za Marekani za Nje, za kusaka mno maslahi pamoja na mafuta,gesi na mali ghafi kwa ajili ya viwanda vyao eti kwa sababu ni mtawala wa kizazi kipya Afrika.
Marekani, walikenua meno hadi gego la mwisho,pale Laurent Gbagbo alipomtimua Dikteta Jenerali Robert Guei, alipotaka kung’ang’ania madarakani mwaka 2000,kwa nguvu ya umma, Peoples Power!
Hii Nguvu ya Umma, haikuanzia Chadema, ilianzia Serbia pale alipotimliwa Dikteta Slobodan Milosevic, ikatua Cote d’ Ivories  kwa Jen Guei,mwaka 2000.
Jen.Robert Guei, alikuwa kaingia madarakani kwa mapinduzi wakati akiwa Mnadhimu wa Jeshi(Chief of staff).
Kiongozi wa Chama cha Kisoshalist, Gbagbo,ni Mkristo wa nyumbani kwao Guei, alikuwa mpinzani wa serikali kwa miaka 30. Bila shaka utajua uswahiba wa Marekani na wapinzani, amepata kufungwa jela.
 Mei mwaka juzi, Gbagbo alisherehekea  ‘Birth Day’ ya 66 akiwa bado Ikulu ya mjini Abidjan,bila wasiwasi.
Hatimaye alitiwa mbaroni kwa msaada wa Wafaransa.
Alianza kutawala Oktoba 26, mwaka 2000 baada ya ‘Wamachinga’ wa mjini Abidjan kuingia mabarabarani wakiwa na rungu, mawe,panga,mawe, matofali n.k wakachoma moto magari na majumba,jeshi likashindwa kuwafagia kwa risasi,kama ilivyotokea Tunisia,Misri na siku hizi Libya.
 Wafaransa hawa hawa waliomwondoa madarakani Kanali Muammar al-Qaddafi, ndiyo waliomsaidia Guei kutorokea Benin,nchi ikaingia katika vita vya kidini,baina ya Ukristo na Uislam.
Polisi wa Kifaransa, The Gendarmes, walivamia nyumba ya Ouattara hadi alipotimkia ubalozi wa Ujerumani. Afadhali hata Mjerumani!
Umoja wa Mataifa na Washington wao waliomba uchaguzi urejewe,Ufaransa wakashinikiza Bunge kushika madaraka,au iundwe serikali ya Umoja wa Kitaifa(Government of The National Unity).
Mchezo uliopo Cote d’ Ivoire,ni ule ule uliokuwepo mwaka 2000 baina ya Gbagbo na Jen.Robert Guei, ama kati ya Mugabe na Morgan Richard Tsivangirai na kati ya Kibaki na Raila Odinga.
 Na tabia na msimamo wa Ufaransa na Washirika wake,Marekani hauwezi kubadilika pale yalipo maslahi ya makampuni yake ndipo yalipo maslahi ya viongozi. Sera za NATO dhidi ya Abidjan na mji Mkuu wa Yamoussoukro, ni zile zile tu za kuchochea vurugu na vita ili wapate nafasi ya kupora mafuta,kokoa,mbao n.k
Na hata siwezi kuishangaa Marekani kuchochea machafuko Algeria, Yemen,Misri,Libya  n.k kwa sababu kuna mafuta!
 George Soros,Mwenyekiti na Muasisi wa taasisi ya Open Society, kaandika Dibaji katika kitabu kiitwacho, ESCAPING THE RESOURCE CURSE, kilichoandikwa na Macartan Humphreys, J.D Sachs na Joseph Stglitz(Columbia University Press, New York 2007).
Kwamba, nchi tajiri za rasilimali hunyemelewa na vita,machafuko,migogoro na umasikini wa wananchi kwa sababu ya ufisadi na uchochezi toka nje.
Hawa ‘Mabwana Wakubwa’ hawawezi kukuacha hivi hivi bila kukuingilia kama una madini,una gesi, mafuta,uranium ama bahari muhimu na mito n.k
Kila penye madini,gesi,mafuta na Uranium kuna shida. Korea,HongKong, Singapote na Taiwan-Asian Tigers-zilisahauliwa kuburuzwa miaka ile ya 60 zikaendelea kiuchumi.
Hazina rasilimali nyingi,lakini uchumi unapaa na hakuna maandamano.
 Kwenye rasilimali, hususan Afrika,kuna vita. Angola huko Cabinda kuna mafuta na kuna vita, Congo(DRC) katika majimbo ya Shaba na Katanga kuna shaba na almasi na kuna vita. Sudan ya Kusini kuna mafuta na ndiyo chimbuko la vita.
Angalia, Yemen, Indonesia(West Papua),Myanmar(Hill Tribes) na Papua New Guinea(Boungainville) kuna shaba,dhahabu,mafuta na gesi na kuna matatizo.
Morocco huko SAHARA MAGHARIBI kuna vita, Nigeria huko Biafra na Niger Delta,kuna vita vya kugombea mafuta!
Nakupa shauri msomaji. Ukifika WHITE House,kamuulize Rais Obama,ana mpango gani wa kuhakikisha mafuta, gesi,dhahabu,shaba,almasi n.k zinawanufaisha raia wazawa wan chi husika,kuliko kuwanufaisha mafisadi wa serikalini na makampuni ya Kimarekani,Kifaransa na Kiingereza?
Ukigusa mikataba ya hila ya makampuni ya Wazungu,kwamba ni kama ile ya Carl Peters na Mangungo wa Msovero, basi utaona Obama anakuwa sawa sawa tu na Osama!
 Na ukipata kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa, kamuulize Rais Obama, ni mtazamo gani wan chi yake kuhusu Mashariki ya Kati(Mideast situation)? Au Afrika? Halafu mnamshangilia Obama kuwa Rais kwa mhula wa Pili huko Marekani,utadhani atawaletea unga!
Kamuulize Obama,Kwanini Marekani inazidi kuua watu kwa majanga ya asili kwa kukataa kusaini mikataba ya Kupunguza Joto Duniani kwa moshi wa viwanda vyake,kama ule Mkataba wa Kyoto,Japan?
Juzi,kulikuwa na Mkutano Afrika ya Kusini,lakini mataifa haya makubwa yagomea mikataba kama huo wa Kyoto, ambao mwaka kesho utakuwa umemaliza muda wake bila mafanikio.
Marekani huchangia kwa takriban asilima 50 ya gesi za sumu angani na ndiyo chimbuko la majanga ya asili-Natural calamities!
Kamuulize Obama, ule msamiati wa ‘Ocampo Six’ kufuatia Luis Moreno Ocampo kutaka                                                  Uhuru Kenyatta, Joshua arap Sang,William Rutto,Francis Muthaura, Hussein Ali, Henry Kosgei washitakiwe kwa uhalifu wa kivita, wakati Blair na Bush wakila good time,ndiyo nini? Hapa hakuna ‘Impunity’? ama ‘double standards’?
 Ocampo sasa kaachia ngazi na kuwachia Bensouda wa Gambia.
 Ukifika Washington, kamuulize Obama,kwanini kuchochea vita Misri na Yemen na kumshambulia Kanali Muammar al Qaddafi huko Tripoli na Benghazi kwamba ame ‘Overstay’ wakati hawajatwambia unyama wa makampuni ya kuchimba na kusafirisha mafuta na gesi,na kutiririsha kemikali za sumu na kuua watu na wanyama migodini, Tanzania, ndiyo nini?
Kaulize,kampuni la Unocal la California lilifanya unyama gani huko Myanmar wakati linajenga bomba la urefu wa kilomita 62 huko Yadana, hawakuua raia na kuwatumikisha bila malipo? Namna gani migodi ya dhahabu hapa Tanzania kuwanyanyasa wananchi na kuua mifugo yao kwa kemikali za sumu bila kulipa fidia?
Kamuulize David Cameron wa Uingereza,kwanini Shell na Chevron wanapochimba mafuta Nigeria na kuharibu mazingira, wananchi wakihoji wao huwalipa polisi pesa ili wawapige risasi?
Ndiyo Haki gani za Binadamu?
Kwanini Shell walimchochea Sani Abacha hadi akamuua Ken Saro-Wiwa na wenzake wananne mwaka 1995?
Afrika inaadhimisha miaka 17 kamili ya kifo cha Saro-Wiwa.Saro Wiwa aliuliwa na Abacha na makampuni ya mafuta ya Uingereza,Uholanzi na Marekani.
Kwanini Shell la Uingereza na Chevron la Marekani wanashirikiana na polisi huko Nigeria kuua waandamanaji wanaopinga wizi na uharibifu wa mashamba yao kwa mabaki ya mafuta yanayoachwa kuingia katika mashamba ya viazi na kuharibu uzalishaji,pasipo fidia yoyote?
 Uingereza hao hao na Marekani na Ufaransa, wanamshambulia Kanali Muammar al-Qaddafi huko Libya kwamba anawashambulia waandamanaji! Wamempindua Gaddafi kisha kumuua,lakini hakuna wa kusema juu ya unyama unaoendeshwa na mataifa haya babe sana duniani.
Hizi ndizo ;double standards’ na mkuki kwa nguruwe hivi.
Demokrasia inaimbwa kuhitajika Libya,Yemen na Misri, wakati mahali wanapokandamiza raia kwa kampuni zao kudhulumu na kuharibu mazingira, huko hawasemi!
 Kama kuua raia wanaoandamana ni kosa,kwanini Hosni Mubarak na Qaddafi waitwe wauaji na wachukuliwe hatua za kupinduliwa, wakati Shell,Chevron,Total n.k hayo makampuni ya Kimarekani,Kiingereza na Kifaransa,hayajakamatwa na kufungwa jela huko The Hague?
Qaddafi, ati ni muuaji wa waandamanaji, na Wamarekani,Wafaransa na Waingereza wakiua watu ni ‘Liberators’!
 Kuna mengi maovu yanayofanywa na Marekani na washirika wao chini ya mwavuli wa NATO, na Rais Obama hana ubavu wa kuyakemea, kwa sera za Marekani za Nje, za kuua na kupora!
 Tena Osama aliua tu hakupora rasilimali. Marekani chini ya Obama,wanaua na kupora rasilimali.
Kwa sababu hiyo, Obama na Osama ni wale wale tu(wauaji) kasoro ni “b” na “s” katika majina yao!
 Matendo ya Osama na Obama siku hizi  yanashabihiana sana, kasoro ni hizo 'b' na 's' tu!
Nawasikitikia waafrika wanaomshangilia sana Obama kwa ushindi Marekani,watalia machozi kabla ya mwakakesho kufika,mimi nitawacheka sana!!
 0786/0754-324 074
 
Monday, November 5, 2012

UNALIJUA JIJI LA MWANZA?

                                      TAHADHARI!!
 *Mwanza kuendelea kubugia  kinyesi na kemikali za sumu wasipodhibitiwa kwa sheria kali
 
WAZIRI WA ARDHI,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Kajumlo Tibaijuka, aliwahi kusema kwamba, Mwanza ni miongoni mwa miji iliyojengwa pasipokuzingatia sheria za makazi na ulinzi wa mazingira.
Jiji hili lilijengwa na Mjerumani, Emin Pasha,mwaka 1892,ili kuwa kituo cha ununuzi wa mazao ya biashara kama pamba,katika ukanda wa ziwa.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Daniel Ole Njoolay, Machi 5,mwaka 2004 wakati akizindua Mradi wa   Majitaka jijini Mwanza,alisema Jiji hili linaongoza kuwa na watu wengi wanaoishi katika eneo  eneo dogo(high population density),kiasi cha kuchafua mazingira,hususan vyanzo vya maji.
Jiji la Mwanza sasa hukadiriwa kuwa na wakazi takriban milioni moja, ambao kwa siku hunywa maji safi kiasi cha mita za ujazo 70,000.Wakazi wa Mwanza,kwa siku huzalisha maji taka,zaidi kinyesi,kiasi cha lita milioni 38.Asilimia  90 ya maji taka hurejea Ziwa Victoria bila kutibiwa.
Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Majisafi na Taka Mwanza(MWAUWASA),Robert Masunya,katika mahojiano na safu hii juzi, anasema wakazi wa Mwanza kwa siku hunywa maji yenye ujazo wa lita milioni 70.
Hii ni sawa na kusema,kwa siku wakazi wa Jiji hili,ambao wao wenyewe huita,” The Rock City” hunywa kiasi cha mapipa 350,000 ya maji safi ya MWAUWASA. Maji taka wanayozalisha(kinyesi,uchafu na kemikali za sumu) ni sawa na mapipa 200,000 ambayo humwagwa ziwani kila siku.
Afisa Uhusiano wa MWAUWASA,Robert Nasunya, ameiambia safi hii kwamba,ifikapo mwaka 2020,uwezo wao ni kuzalisha maji safi na salama yenye viwango vya ubora wa kimataifa kufikia mita za ujazo 108,000 ambazo ni sawa na lita milioni 108, ama mapipa 549,000 kila siku.
MWAUWASA wana matangi matano yenye uwezo wa kuhifadhi maji yenye ujazo wa mita 27,000,sawa na lita milioni 27.
 Kutokana na ujenzi holela usiozingatia sheria za makazi,MWAUWASA wanapozalisha maji mengi hata kiwango kisichotumika(Idle Capacity),yapo maeneo ambayo hayapati maji ya bomba yaliyotibiwa na kusafishwa.
Maeneo hayo hayafikiwi na maji ya bomba; mengi yako katika miinuko mikali,vilimani,kwa sababu maji ya bomba hutiririka kwa ‘gravity’,hayapandi mlima mpaka yasukumwe kwa mashine kama pampu.
Maeneo ya vilimani(Mwanza huzungukwa na vilima,miamba na mawe)yasiyopata maji ni pamoja na Kabuhoro, Ibanda,na Mji Mwema.Mengine ni Sangabuye,Kayenze na Bugogwa.
Afisa Uhusiano wa MWAUWASA,Masunya anasema, wakati wakazi wa Mwanza wanakunywa maji safi lita 70 milioni kwa siku moja, na wakati uwezo wa MWAUWASA ni kuzalisha lita milioni 108 kwa siku moja, lita 30 milioni hubaki-hushindwa kuwafikia watu.
Masunya anasema, wakazi hawa wa Mwanza huzalisha lita milioni 40 za taka zikiwemo kemikali za majumbani, hospitalini,viwandani,madukani na hata kinyesi cha binadamu na mifugo.
Serikali na Jumuiya ya Ulaya(EU) wamejenga mfumo wa kusukuma maji taka kutoka lita 35 hadi lita 170 kwa sekunde.Maji haya taka husukumwa hadi katika mabwawa 10 yaliyoko Butuja,Ilemela ambako hutibiwa kabla ya kurejeshwa Ziwani Victoria.
Mradi huu ulifadhhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Ujerumani(KfW) na ukakamilika Oktoba mwaka 2010.Una uwezo wa kukusanya majitaka ya kiwango cha  asilimia 15 tu ya wakazi wa Jiji linalokuwa kila siku. Ukiamka asubuhi,unakuta vijumba vimeota milimani,pasi na ruhusa ya Mipango miji!
Asilimia 9 ya wakazi wa  Jiji hili la miamba,ndiyo waliounganisha maji yao katika mfumo huu wa maji taka,nao hawazidi wateja 2,000. Hawa ndiyo kinyesi chao na kemikali zao husafishwa na kurejeshwa ziwani.
Nimezungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA,Anthony Sanga, Alhamisi iliyopita, akasema mfumo wa MWAUWASA wa kutibu maji taka,hufanya kazi chini ya kiwango,kwa sababu wakazi wa jiji wameshindwa kuunganisha makaro yao ya maji machafu kwenye mfumo huo wa kutibu maji taka.
Sanga, ananiambia kwamba sasa wameanzisha mpango wa kuwakopesha wananchi ili waunganishe maji taka yao kwenye mfumo wa maji taka.Wanachotakiwa kufanya ni kulipa sh.5,000/ tu,halafu watakatwa pole pole baada ya kuingia mkataba.
Mfumo huu wa maji taka ulijengwa na Sirling International ya Italia. Na kulingana na MWAUWASA,Mwanza kuna vyanzo vya maji safi katika eneo la Capri Point,Chakula Barafu na Luchelele, ambavyo vyote hutoa maji Ziwa Victoria linalochafuliwa kwa kinyesi kisichorejezwa(recycled) kwa kutibiwa Butuja.
Kuna mpango wa kuongeza chanzo kingine cha maji chenye uwezo wa kuzalisha mita za ujazo 50,000 kwa siku ili kuondoa shida ya maji Kabuhoro,Ibanda na maeneo mengine wanakolazimika kunywa maji ya ziwani yasiyotibiwa na kupimwa kitaalam,ili kudhibiti uchafu na kiwango cha kemikali.
Kemikali zinaweza kuleta madhara ya afya kwa binadamu na wanyama.Ziwa Victoria liko kandoni mwa migodi ya dhahabu ambayo hutumia zebaki(mercury)kusafishia dhahabu,na kasha mvua zinaponyesha husomba zebaki hiyo hadi ziwani na kuua samaki,wanyama,binadamu kasha kuharibu mazingira.
Hata hivyo,licha ya MWAUWASA kuzalisha maji kwa kiwango cha ziada,Mwanza ni jiji ambalo wakazi wake hunywa maji ya chupa ya Uhai kutoka Dar es salaam, Kilimanjaro, wakati mwingine wanakunywa Rwenzori,kutoka Milima ya Rwenzori huko Uganda!
Yaani, bei ya lita moja ya maji ya kunywa Mwanza haina tofauti kubwa na bei ya lita ya petrol kutoka Arabuni,wakazi Ziwa tunalo hapa,lakini maji yamechafuliwa kwa kinyesi! Fika Mwaloni Kirumba,utajionea kinyesi majini,Ziwani…hii ndiyo Mwanza!
Sasa,Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA,Anthony Sanga, ananiambia labda sheria zitumike sasa kuwabana watu wanaotiririsha maji taka Ziwani, wanaokataa kuunganisha majitaka yao katika mfumo wa MWAUWASA,ili yakatibiwe Butuja.
Wakati wa mvua,watu hutapisha vyoo vyao na hufungulia makaro ya maji taka ambayo huingia ziwani. Kutiririsha kinyesi mitaroni Mwanza ni kitu cha kawaida. Halafu eti Mwanza ndilo jiji safi kuliko yote Tanzania!!
Zaidi ya asilimia 90 ya wakazi wa Mwanza,ambao huishi vilimani katika makazi yasiyopimwa,hhutiririsha kinyesi na kemikali ziwani. Maji ya ziwa yanapotumiwa pasipo kuchemshwa ni hatari.
Novemba, 22 mwaka 2005,aliyekuwa Mkemia Mkuu wa Serikali,  Dk.Ernest  Mashimba, alisema jijini Mwanza kuwa Sheria namba 3 ya mwaka 2003 ya Udhibiti wa Kemikali Viwandani na Majumbani,haizingatiwi na wakazi wa jiji hili.
Hayati,Dk. Mashimba alisema,Mwanza ni miongoni mwa maeneo ambayo kuna uvuvi haramu kwa kutumia kemikali za sumu.Wakati wavuvi wanapovua kwa kutumia sumu,humwaga kemikali hizo ziwani na kuhatarisha maisha ya viumbe.
Makopo ya sumu Mwanza hutupwa mitaroni na kuachwa kuingia ziwa Victoria,wakati sheria hii inawataka kuzika makopo hayo au kuyarejesha viwandani,yaharibiwe.
Kulingana na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa(WHO)asilimia kubwa ya watu wanaodhuriwa na sumu ni kama hawa wakazi wa Mwanza,ambao huacha hata sumu za kuulia wadudu kuingia ziwani.
Maradhi yanayoongoza kuwaua watu wengi Mwanza ni minyoo,kichocho,kuhara damu,safura,homa za matumbo na hata kipindupindu-hii ni kutokana na kunywa kinyesi hiki wanachorudisha ziwani; kuliko na chanzo chao cha maji.
Mwanza,watu hubugia kinyesi chao kwa hiari!!
Ili kunusuru hali hii,Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Anthony Sanga, anasema sheria zitumike kuwafanya wakazi wa Mwanza kuunganisha maji taka yao na mfumo rasmi wa maji taka wa MWAUWASA.
0713 324 074
 
BURIANI KAMANDA BARLOW 4

INSPEKTA JENERALI WA POLISI(IJP) Said  A.Mwema, akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza,Oktoba 25 mwa huu, akasema wajibu wa raia na polisi kwa taifa letu.
Aliwakariri wanafalsafa juu ya wajibu wa kila mtu kuweka mbele  maslahi ya Taifa.Alizungumza wajibu wa Jeshi la polisi kushirikiana na wananchi katika kulinda Amani ya nchi yetu.
Tuijadili kidogo kauli ya Mwema kuhusu Rais wa 35 wa Marekani,John Fitzgerald maarufu sana kama “Mr. J.F” Kennedy(Democratic) ambaye aliishi kati ya Mei 29 mwaka 1917-Novemba 22,mwaka 1963.Alifariki kwa kupigwa risasi katika msafara wake huko Dallas,hiyo Novemba 22 mwaka 1963.
Uzalendo wa wajibu wa kwanza wa kila raia(hata polisi,JWTZ,Uhamiaji,Usalama wa Taifa n.k).Hata hivyo, wananchi tunamshauri IJP Mwema,atazame ikiwa polisi wake,wakiwemo wenye vitambi, wanao uzalendo kwa taifa,ama kama wanaweka mbele maslahi ya Taifa,au maslahi binafsi ambayo ndiyo uzalendo wa matumbo yao wenyewe.
Ni wazi, Tanzania kuna kitisho cha amani ,kwa sababu maadili yamepotea,na uzalendo wan chi na maslahi ya Taifa kama alivyosema Mwema,akimkariri JF Kennedy na Abrahm Lincoln,leo vinatupiliwa mbali.
Turejee Mwanza,katika matukio ya uhalifu yaliyowahi kufanyika Mwanza,polisi wa IGP Mwema wakiwepo,wakashindwa kuwatia mbaroni wahusika.
Aliyekuwa Mbunge wa Mwanza Mjini(baadaye majimbo haya yaliitwa Ilemela na Nyamagana),Marehemu Ali Shomari, alimwagiwa tindikali na mtu ambaye hatimaye “aliyeyuka” mikononi mwa dola.
Pia,mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato(TRA)alimwagiwa tindikali(corrosive acid) iliyomuunguza vibaya,akalazwa hospitalini.Mwanza ni mahali ukicheza unamwagiwa tindikali.Polisi wa Mwema,wapo wanabarizi upepo!
Hata siku za karibuni,baada ya mauaji ya Kamanda Barlow,yupo mwanasheria aliyepigwa risasi pajani na kulazwa hoi hospitalini Bugando.
Matendo haya na mengine mengi,huripotiwa polisi. Tatizo,umma huwa haujui na haujulishwi hatma ya mambo haya, na mustakabali wa kesi hizo huwa haujulikani.
Tunazungumza juu ya uzalendo na wajibu wa raia kuona FAHARI kwa nchi yetu Tanzania. Mke wa Rais Obama(naamini anashinda mhula wa pili)Michelle Obama, aliwahi kusema hivi:
“For the first time in my adult life time, I am really proud of my country”  akimaanisha kuionea fahari nchi yake katika maisha yake ya sasa ya utu uzima.
Naam, kama kila raia wa Tanzania atatekeleza wajibu wake,huu uzembe,kukosa uzalendo na mauaji ya kinyama sampuli hii,vitaondoka.
Tuitembee Mwanza kidogo. Mei 20 mwaka 2010, aliyekuwa Meya wa Jiji la Mwanza, ambalo sasa linakuwa Manispaambili, Leonard Bihondo(64) alitiwa mbaroni na polisi kwa tuhuma za kuhusika katika mauaji ya aliyekuwa Katibu Kata wa CCM,Isamilo,Bahati Stephano.
Bihondo, alikamatwa uwanja wa ndege wa Mwanza, akitokea Dar es salaam,ambako alihudhuria mkutano wa ALAT,alituhumiwa kushirikiana na Jumanne Oscar(30),Abdul Ausi na Baltazar Shushi, ambao wote pia walitiwa mbaroni,na kesi yao ingali inasubiri kusikilizwa.
Oktoba 15,kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Lucas Omahe Garani, alijipenyeza katika ‘msitu’ wa walinzi wakiwemo polisi, Green guard na Usalama wa taifa, akavamia jukwaa ambako    Rais Jakaya Kikwete alikuwa,wakati huo akiwa mgombea wa CCM.
Ilikuwa Jumamosi, Alasiri,safu hii ilikuwepo uwanjuani hapo ikifuatilia kwa makini. Huyu Omahe Garani, alinyatia jukwaa akamfumania Kikwete na kuanza kumnyuka mieleka ili ambwage chini!
Kilichomfanya Kikwete asianguke chini,ni medani ya kijeshi,Kikwete alimudu kujitetea,baadaye Green Guard na polisi wakamtia mbaroni Garani na mwenzake Mzaki JAMAL,wakasokomezwa ndani ya karandinga la polisi,baada ya kukong’otwa sana na virungu vya Green Guard na polisi.
Walipelekwa gerezani Butimba. Matimbiko yaliyofanywa ili kumtawaza Kikwete kuwa ‘Chifu’ wa Wasukuma, eti yaliwaalika Omahe Garani(Mkurya wa Mara) na Mzaki Jamal(Muha wa Kigoma!)sijui walitaka kufanya nini! Wee Mwanza uione hivyo tu.
Kamanda wa polisi mkoani Mwanza,zama hizo,Zelothe Stephen, alisema polisi hawakupaswa kulaumiwa kwa tukio hilo,kwa kuwa hawakuhusishwa katika tukio hilo la kumtawaza Kikwete kuwa Chifu wa Wasukuma.
Chama cha Mapinduzi, kililaumiwa kwa kukumbatia sana imani za kishirikiana, hadi mgombea wake wa Urais akafanyiwa huduma ya tambiko bila vikosi vya usalama kuhusishwa.
Lucas Omahe GARANI na mwenzake Mzaki Jamal walifikishwa mahakama ya Hakimu Mkazi, Ilvin Mgetta,kwa makosa ya kula njama na kumfanyia fujo Kikwete,jukwaani.
Waendesha mashitaka, Wilson Frank na Muna Paschal waliiambia mahakama kuwa washitakiwa walitenda kosa hilo katika mkutano wa kampeni,Oktoba 15 mwaka 2005.
Kwa kifupi, washitakiwa walipatikana na hatia wakafungwa jumla ya miaka 10 kufuatia tukio hilo la kumfanyia fujo Kikwete ambaye alishinda uchaguzi baadaye na kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
 Nakutembeza katika mitaa ya Mwanza,uone maajabu.Twende pamoja msomaji!
Desemba 4, mwaka 2009 saa 10  jioni.Edwin Miyaye(4) anatekwa nyara na Sospeter Nyanda(17) ambaye alikuwa mwanafunzi wa kidato cha tatu katika sekondari ya Mnarani.Mwingine aliyeshirikiana na Sospeter kumteka mtoto huyu ni Daudi Madaraka(16) mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi,Bwiru. Mwanza kuna vituko!
Michael Joseph naye mwanafunzi wa shule ya msingi Bwiru naye alimteka mtoto huyo,walishirikiana na Getrude Rutabura(39).
Walimpomteka Edwin wakampigia simu babaye,Miyaye.Wakamwambia awalipe shilingi Milioni tano;la sivyo wangemuaa Edwin!Sospeter Nyanda, alijua namba ya simu ya Baba Edwin, alikuwa na nasaba naye.
Miyaye, alichelewa kuwapa wateka nyara hao sh. 5,000,000/= Alikwenda polisi ili wamsaidie kuokoa maisha ya mtoto, baada ya saa kupita, watekaji nyara wale walimfunga Edwin mawe makubwa shingoni na kiunoni,wakamtosa ndani ya vilindi vya maji ya Ziwa Victoria!!
Polisi waliwatia mbaroni Sospeter na wenzake kwa tuhuma za mauaji. Baada ya mahojiano na polisi(na virungu vya haja) walikubali kwenda kuonesha mahali walipomtosa Edwin.Micheal Joseph aliyekuwa mwanafunzi wa shule ya msingi Bwiru ati alitoroka,hakukamatwa.
Edwin(4) alitoswa vilindini kwa sababu babaye,Miyaye alikosa sh.5,000,000 za kikombozi.Desemba 5,mwaka 20059 ndiyo siku maiti ya Edwin ilipoopolewa majini,Ziwa Victoria,ili kufanyiwa Postmortem na Daktari.Alikuwa kwa kuwa babaye alishindwa kulipa kikombozi-ransom!
Ilikuwa huzuni na majonzi. Edwin aliopolewa mbele za kamera za televisheni ya Star ya Jijini Mwanza.Maiti ya Edwin ilikuwa uchi wa mnyama! Naam,hii ndiyo Mwanza!
Desemba 6,mwaka huohuo wa 2009 Yohana Musa(25) muuza ndizi wa soko la Kirumba akiwa na mwenzake,Abuu walimteka nyara msichana,Judith John(29),Mhaya wa Bukoba,walimchinja mithili ya mbuzi.
Yohana na Judith walikuwa katika uhusiano wa kimahaba, sasa Judith akataka kumpiga chenga Yohana,ili achukuliwe na ‘mabuzi’ mengine yenye fedha. Unajua Krismasi ilikuwa ikijongea, na watu hutaka sana pesa wakati huo.
Sasa, Yohana akaazimu kulipa kisasi, yeye na wenzake wakazungumza na Abdallah Lucheme(70) aliyekuwa mganga wa kienyeji.Wakakubaliana kumchinja Judith na kumnyofoa viungo nyeti,kama shavu la kulia na nyeti zake ili wakafanyie matambiko ya pesa-ndagu!
Judith, alichinjwa majira ya saa sita usiku huko Songambele,Kirumba, walimchinja chumbani, wakatenganisha kichwa na kiwiliwili,chumbani kwa Yohana.
Kile kiwiliwili cha Judith kikafutikwa ndani ta gunia,wakakitelekeza kwenye pagala jirani na Mtaa wa Kiyungi.
Polisi walimtia mbaroni Yohana Musa(25) akiwa chumbani kwake akiuchapa usingizi.Walimtia pingu na baada ya dakika 40 hivi, akawaambia makachero wa polisi ni wapi kilipokuwa kichwa cha Judith.
Mganga wa kienyeji,Abdallah Lucheme(70) alitajwa na Yohana,akatiwa mbaroni na kufungwa pingu,akawapeleka korongoni ambamo kichwa cha Judith kilifichwa ndani ya mfuko mweusi wa Rambo, kichwa kilikuwa kimenyofolewa shavu la kulia. Jamani!
Walimchinja Judith baada ya kumfutika matambara kinywani,ili asiweze kupiga kelele humo chumbani kwa Yohana. Desemba 9,mwaka huo wa 2009 mwaka wa mauaji ya kishenzi-mwili wa Judith ukazikwa makaburini,Kitangiri.
Hii ndiyo Mwanza ambayo miaka mitatu baadaye,imechukua maisha ya Liberatus Lymo Barlow.
Hadi sasa watuhumiwa watano wa mauaji ya Kamanda Barlow wamepandishwa kizimbani, waliopandishwa kizimbani ni Muganyizi Michael Peter(36) Mhaya ambaye ni dereva,mkazi wa Nyakabungo,Mwanza,ambaye ndiye hasa anasadikiwa kumpiga risasi Barlow kwa bunduki, Shotgun-Greener.
Chacha Wekena Mwita(50)Mkurya ambaye ni mfanyabiashara wa Gongo la Mboto,Dar-Magige Mwita a.k.a ‘Tatoo’ yaani mzee ana umri wa miaka 48 naye ni Mkurya,mkulima eti wa mjini Bugarika,jijini Mwanza.
 Mwingine aliyepandishwa kizimbani  ni Bugazi Edward Buseta(22)Mhaya mfanyabiashara wa Tandika, Dar es salaam na Boke mwana wa Marwa Mwita(42) Mkurya na mfanyabiashara wa Mombasa-Ukonga,Dar.
Mbele ya Hakimu Mkazi,Angelo Lumisha, wakili wa serikali Castus Ndagambo, amesema washitakiwa wanakabiliwa na kesi ya mauaji kinyume na sheria ya nchi kipengele cha 196 na 197 katika Penal Code Na 16.
Ndagambo, ameiambia mahakama kuwa washitakiwa hao watano kwa pamoja walimuua Kamanda Liberatus Lymo Barlow, Oktoba 13,mwaka huu  majira ya usiku huko Kitangiri,katika eneo la MINAZI MITATU,Wilaya ya Ilemela.
Washitakiwa wote watano kwa pamoja hawakutakiwa kusema lolote kufuatia mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo ya mauaji.
Gwaride la utambulisho, IDENTIFICATION Parade lilifanywa, Dorothy,Yule mwanamama aliyekuwa na Barlow usiku wa mauti, akawatambua wote watano.
Walirejeshwa Butimba nyuma ya nondo hadi kesi yao hiyo JINAO NAMBA 30 ya mwaka 2012 itakapotajwa tena Novemba 15 mwaka huu.
Tukutane katika sehemu ya mwisho wa mkasa huu wa kusisimua

0713 324 o74

www