Thursday, February 7, 2013

musoma

Polisi wanapowasaka wauaji wa Musoma kwa bunduki,virungu na pingu,wanaharakati wafungue darasa la uwajibibikaji  na Haki za Binadamu
 
TOLEO nambari 852 la gazeti hili la Rai(Januari 21-27 mwaka huu), niliandika katika Mraba huu kwamba, iko haja ya wanaharakati wa Haki za Binadamu kwenda Musoma, kufundisha Haki za Binadamu.
   Niliandika kwamba, ukitembea Musoma na kusikiliza maoni ya baadhi ya watu, hutakosa kurejesha fikra zako katika zama za mauaji ya kuangamiza(genocide)huko Rwanda , mwaka 1994.
   Katika makala yenye kichwa, “Musoma vijijini uzee ni baraka au laana?” nilifananisha uwezo wa kufikiri wa baadhi ya wakazi wa huko na wauaji wa Jimbo la Darfur( Sudan ) ama huko Chad , Congo Mashariki, Somali n.k
    Nilisema hapa mrabani, kwamba maeneo niliyotaja yamesababisha vikao vingi mjini Geneva , Uswisi, kujadili namna ya kuwaokoa watu katika maangamizi.
  Geneva , ni makao makuu ya Mashirika ya kutetea wakimbizi nay ale yanayoshughulikia Haki za Binadamu. Geneva ni kitovu cha kamati ya kimataifa ya Shirika la Msalaba Mwekundu(ICRC).
     Msalaba Mwekundu kazi yao ni kulinda na kuokoa maisha ya watu. Kwamba, Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoridhia Tangazo la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu, lililotolewa Desemba 10, mwaka 1948.
    Kwamba, mikataba ya Haki za Binadamu na ile ya Geneva (The Geneva Conventions), kama ule wa mwaka 1949; hukataza mauaji.
 Hata mateka wa vita wanalindwa na mikataba hii wasiuliwe kasha wapewe matibabu na huduma za kiafya hata wawapo na majeraha ya risasi, wanapokuwa mikononi mwa adui zao vitani.
  Kinyume cha harakati zza mashirika ya Haki za Binadamu na Msalaba Mwekundu, katika kulinda na kuokoa maisha ya watu, Musoma kuja ‘Janjaweed’ mithili ya wale wanamgambo wa Kiarabu wa huko Sudan , wanaofyeka watu kwa majambia makali sana . Musoma kuna kila dalili za watu kuanza kulipizana visasi.
   Sababu za watu kuwa na majambia au mapanga, ni visasi kufuatia tuhuma za kijinga-jinga, kama uchawi, ulozi, usihiri, wizi wa mifugo na hata chuki za kikabila. Ukitazama kwa maikini, utaona mfumo wa kutoa haki Musoma, mkoani Mara, unaugua kiharusi.
  Katika makala yangu katika mraba huu, Januari 21 mwaka huu, nilitaraji serikali ingechukua hatua haraka kupeleleza na kuyasaka makundi ya wauaji wenye mapanga(Jajaweed) ambao hukodishwa na watu kwenda kutekeleza mauaji ya kinyama; naam mauaji ya kisasi.
  Walemavu wa ngozi(albino) pia huuawa na hawa hawa Janjaweed, wanapotumwa na wenye fedha, kutaka kufanya matambiko yao anuwai.
 Mauaji ya kishenzi kama hayo ya Buhare, nje kidogo ya Manispaa ya Musoma, siku chache zilizopita, bila shaka yamefanywa na Janjaweed.
   Nataka nikwamnie msomaji. Zamani kidogo, walilipwa fedha wauaji wenye pindi na mishale ya sumu. Kwenda kuua mtu yeyote aliyetuhumiwa kuwa mchawi ama mwizi kwa minajiri ya kulipa kisasi, mradi kulikuwa na aliyetangaza ‘zabuni’ hiyo kwa ujira wa pesa.
 Musoma, kuna ‘Janjaweed’ wanaoendesha maisha yao kwa kuua. Musoma kuna vikundi vya siri vya wauaji wa kukodishwa.Wamefuzu medani za kuua na hata kuangamiza kizazi na koo(genocide) kwa mapanga makali na pinde zenye mishale ya sumu kali.
   Akina mama na kina baba vikongwe wanaotuhumiwa kwa uchawi, wameuliwa wengi bila serikali kuchukua hatua. Ulegevu wa serikali-polisi na mahakama- umewapa Janjaweed kupenya mkondo wa sheria.
 Nataka kusema kwamba, polisi mkoani Mara ni wazembe; tena wazembe kuliko. Nachelea kusema ni wala rushwa, wanaoharibu upelelezi wa kesi za namna hii, wanapokuwa wamepewa chochote kitu, ama kama wamelipwa ng’ombe, kondoo, kuku, bata kama siyo fedha taslim.
 Amini usiamini, vyombo vya kutoa haki(polisi na mahakama) mkoani Mara havitendi kazi yake sawa sawa. Kwa sababu, wezi na wahalifu wengine hata wa mauaji, hukamatwa leo, kasha wakaachwa huru kesho asubuhi.
 Kisingizio, ni kukosekana kwa ushahidi ama kushinda rufaa. Rufaa za Musoma husikilizwa wapi usiku wa manane, kama siyo upenuni mwa vilabu vya pombe za kienyeji, ama baa?
 Mahakama gani hukaa usiku, siku za siku kuu na mapumziko?
     Musoma, mhalifu akifungwa jela na mahakama ya Mwanzo Ijumaa jioni, keshoye Jumamosi ama keshokutwa  Jumapili, anarejea nyumbani, kwamba kashinda rufaa!
   Hayo ndiyo ya Musoma, sasa  wana ula wa chuya! Wahalifu wanapoachiwa huru hurejea vijijini kwenda kutishia raia wema waliowasema polisi au kutoa ushahidi mahakamani.
   Musoma, ukatoe ushahidi mahakamani, mhalifu afungwe  jela siku mbili, na kurejea nyumbani baada ya juma moja; hujipendi?! Utakatwa koromeo mchana kweupe.
Raia wema na waadilifu wamekatishwa tamaa na utendaji wa vyombo vya dola.
  Siku hizi watuhumiwa huuawa na wananchi wenye hasira kali. Hufuatwa hata makwao na kuuliwa kinyama, wao, wake na ndugu na jamaa zao, nyumba huchomwa moto hata mchana kweupe.
 Hakuna kuwapeleka watuhumiwa polisi au mahakamani, kwa madai kwamba watarejea kesho! Mahakama zinaugua kiharusi;polisi wana mafua!
    Kuna mahakama 15 tu za Mwanzo mkoani Mara. Mkoa mzima wa Mwanza una mahakama za Mwanzo 20.Mahakimu ni wachache, tunaambiwa kuna upungufu wa mahakimu wa mahakama za Mwanzo 500 nchi nzima!
 Hizi mahakama ambazo ndizo huwahudumia wananchi wengi wa vijijini, zina mahakimu wachache sana . Hawana vitendea kazi, kesi zimefurika.
   Hakimu mmoja husafiri kutoka mahakama moja kwenda nyingine; na huko kuna msongamano wa kesi nyingi tena za miaka mingi.
 Nataka kusema kwamba, ni nadra kupata haki vijijini kupitia mahakama za Mwanzo. Hata mahakama za wilaya ndizo huwaachia wezi na wahalifu kwa rufaa zilizosikilizwa baa au klabuni, siku zisizo za kazi.
  Mfumo wa utoaji haki mkoani Mara, una walakini.
Kama hauugui kifaduro, una kiharusi kikali.Hakimu mmoja husafiri kutoka mahakama moja kwenda nyingine, anaposhindwa, watendaji wa vijiji na kata ndiyo wanaowasomea mashitaka washitakiwa.
   Hawa, hawana hata ‘ABC’ ya sheria. Matokeo yake, dhamana huandamana na kitita cha noti. Bila fedha hakuna dhamana hata kama ni haki ya mshitakiwa kikatiba na kisheria.
   Vituo vya polisi vya vijijini mkoani Mara, vimegeuka kuwa mahakama, kwa sababu polisi hutoa hukumu;hutoza faini vituoni.
Wauza gongo na bangi, wezi wa bata, kuku,ng’ombe n.k huachiliwa vituo vya polisi mradi wawe na pesa za hongo na rushwa!
   Kama hujawahi kuona mtu akikaa mahabusu mwaka mzima, nenda katika mahabusu za Musoma vijijini, ufanye kosa dogo kasha usiwape rushwa polisi, watendaji wa kata na vijiji.
   Hiki ni kichocheo cha watu kuchukua sheria mkononi, ama kukodisha ‘Janjaweed’ ili wakawalipie visasi, kwa kuwa polisi na mahakama walishashindwa kuwafunga jela wauaji, wezi, majambazi, kwa kuwa wana pesa za rushwa.
  Huko Musoma, ile dhana ya Robert Darwin ya “Survival of The Fittest”(ya mwenye nguvu kuua wanyonge bila kufanywa kitu) hutenda kazi. Huna kitu Musoma huna haki polisi, ofisini kwa Mtendaji wa kijiji, wa kata hata mahakamani!
  Musoma vijijini, kama huna fedha za kujaza mafuta katika pikipiki ama gari la polisi, hakuna mtuhumiwa wako kukamatwa. Hata akikamatwa na kufikishwa kituoni, huna fedha za kumlisha chakula au kumlipia nauli kwenda rumande mjini Musoma, hawezi kupelekwa!
  Mkoani Mara, ndipo hakimu mmoja wa mahakama ya mwazo hukabiliwa na kesi nyingi, kwa sababu tarafa nzima huwa na mahakama moja ama mbili. Tarafa inakuwa na takriban watu 600,000.
Kuna kesi ngapi? Kesi nyingi hazitolewi maamuzi kwa wakati; na wanasheria wanamsemo kwamba, “Justice delayed is Justice denied”(haki iliyocheleweshwa ni haki iliyopotea).
 Kwa hiyo, Musoma hakuna haki? Kwa sababu haki hucheleweshwa, haki imepotea. Katika mazingira haya, wananchi wamekata tamaa, wanaamua kuwalipa ujira ‘Janjaweed’ ili wakawalipie kisasi dhidi ya wahalifu,watuhumiwa wao ama wabaya wao hata kama ni tuhuma za kijinga kama za kishirikina.
  Mfumo wa kutoa haki unaugua kiharusi mkoani Mara.Wizi wa mifugo unaendelea kwa sababu ukiwa na fedha utakamatwa leo, kesho utaachwa huru, au utafungwa leo na mahakama ya chini na kushinda rufaa usiku wa manane!
   Wapo watu, wanaposikia Musoma kuna mauaji ya kutisha, wanadhani kuna watu wakatili sana . Hapana! Haya ni mauaji ya visasi kwa sababu mfumo wa sheria umeshindwa.
  Si kila raia mwema huuliwa, ila ukituhumiwa.Mauaji ya kinyama huandamana na visasi kwa sababu mfumo wa sheria unaugua kiharusi kikali.
  Mauaji ya juzi huko Buhare, Musoma, ambako watu 17 wa ukoo mzima walifyekwa mapanga na kuchinjwa mithili ya njiwa, ni matokeo ya kulipizana visasi, kwa sababu vyombo vya dola(polisi, mahakama, mageteza na watendaji) walishashindwa kufanya kazi yao barabara.
 Nazungumzia uwajibikaji wa vyombo vya dola, na umuhimu wa viongozi wa vyama na serikali kuhimiza watu kuishi kwa kufuata sheria za nchi-uadilifu.
   Mauaji ya kulipa visasi; naam kulipa baya kwa baya(tit-for-tat) hudhihirisha kwamba mfumo wa kutoa haki Musoma unaugua kiharusi cha ubongo na kiwili wili.
 Mahali haki inapopatikana mahakamani, watu huridhika, amani hushamiri, maendeleo huja na kuna demokrasia. Tabia ya kuchukua sheria mkononi(Mob justice) iliyoenea Musoma, ni kielelezo kwamba raia hawataki tena kupeleka kesi zao mahakamani ama polisi, kwa sababu wanadhani hakuna haki.
 Siku hizi watuhumiwa huuawa hata mbele ya polisi.Polisi wanapoaachia huru watuhumiwa, waelewe wanasababisha mauaji ya visasi namna hii.
 Niliandika mrabani hapa Januari 21 mwaka huu kwamba, Musoma ndiko wanakofanya mikutano ya hadhara kutafuta namna ya kuwadhibiti wachawi kwa kuwakata mapanga!
 Ujinga umejaa vichwani mwa viongozi wa vijiji, vitongoji, kata n.k hadi sheria na haki za binadamu ni kitenda wili.
 Haki za binadamu ni lugha ya kawaida ya ubinadamu.Haki ingalipo Musoma lakini hutindika.
   Nataka kusema kwamba, Musoma hakuna ubinadamu, kwa sababu watu huongea lugha ya kuua kwa kulipa visasi-ni kuwaondolea watuhumiwa haki ya kuishi, hata kabla ya mahakama(chombo pekee cha kutoa haki nchini)kutoa hukumu.
 Narejea wito wangu kuwataka wanaharakati wa haki za binadamu kwenda Musoma mkoani Mara, kufundisha haki za binadamu, haki za raia, itifaki ya Geneva , uwajibikaji serikalini na vyombo vya dola, ili kukinusuru kizazi hicho na maangamizi!
  Narejea kauli yangu kusema kwamba, unahitajika mkakati mzito wa kuwanusuru watu hawa katika kitisho cha uvuli wa mauti ya kuchunjana kama ng’ombe kwa mapanga utadhani Bosnia , Darfur , Rwanda ya mwaka 1994, Somalia au Congo na Chad !!
   0715-324 074  
 
AFRIKA KIZIMBANI (14)
 
 CHARLES GHANKAY Taylor (62), Rais wa zamani wa Liberia aliyekuwa akikabiliwa na mashitaka  11 ya uhalifu wa kivita huko Sierra Leone,  na baadaye kufungwa miaka 50 jela,anatufundisha somo mahsusi.
 Kwamba,katika mahakama ya uhalifu wa kivita(ICC) mjini Hague, Uholanzi, Taylor amesemwa na mashahidi wa upande wa mashitaka kwamba alipokuwa Afrika Kusini wakati fulani, akatumia almasi alizokwiba  bega kwa bega na waasi wa RUF  huko Sierra Leone, kumhonga kidosho,mwanamitindo wa Kiingereza, Naomi Campbell.
 Unaona utajiri wa Afrika unavyotumika?
 Naam, Filamu iitwayo, ‘Blood diamond’ ya Jennifer Connelly, inatueleza kwamba, Charles Taylor, Marehemu Fodday ‘Poppay’ Sankoh na waasi wa Revolutionary United Front(RUF) waliiba almasi,wakabadilishana kwa silaha na Wazungu wa Ulaya na Afrika ya Kusini.
  Kumbuka msomaji, kulikuwa na mikataba ya Umoja wa Mataifa(UN) ya kutofanya biashara ya almasi za damu kutoka Sierra Leone.
 Hata hivyo, almasi hizi zilinunuliwa kwa magendo na kuingizwa Afrika ya Kusini, Zimbambwe kisha Ulaya na Mrekani.
 Kitendo hicho kilichochea sana vita hivi, wakati nia ya Mzungu ilikuwa kunufaika na utajiri wa Mafrika,potelea mbali Mwafrika huyu afe; aaangamie kwa risasi-The Shame of Poverty in Plentiful.
 Je, hujawahi kusikia kwamba hata Congo(DRC) vikosi vya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa(UN),wakati mwingine husahau jukumu la kulinda amani,na badala yake huanza kuiba madini,huku wakiacha kuwaokoa watu wanaouawa na wanawake kubakwa?
 Tangu kifo cha Laurent Desire Kabila katika Ikulu ya mjini Kinshasa, Januari 16,mwaka 2001,ukichungulia ndani ya uasi na uporaji wa rasilimali za ‘Bakongo’ kuna Mzungu.
 Hata ufisadi mithili ya ule wa kampuni ya Kiingereza, British Aerospace(BAE Systems) kutuuzia rada kanyaboya hapa,kwa Dola za Marekani milioni 40, kuna Mzungu anayeshiriki kutuumiza sisi tunapokosa shule, hospitali,maji, barabara na kwa ujumla maisha bora.
  Fedha za wizi: Hufichwa Jersey, Uingereza, Uswisi na katika mabenki ya Ulaya na Marekani, na hawasemi wizi huu.
 Joseph Mobutu aliiba dola za Marelani milioni sita akazificha Ulaya, hawakusema mpaka akatimkia uhamishoni, Morocco, kisha amefariki, wakazirejesha kwa familia yake.
 Mifano iko tele ya wizi. Uingereza iliwahi kutiliana saini mkataba na Misri mwaka 1929 eti sisi tusitumia maji ya Ziwa Nyanza linaoliwa Victoria kwa heshima ya Malkia wa Uingereza.
  Mkataba huu wa 1929 uliorejewa mwaka 1957 lengo lake lilikuwa kutuzuia kutumia maji ya Ziwa hili kwa miradi ya  kilimo cha umwagiliaji ili kujiokoa na kitisho cha njaa , kinachotukabili kila mwaka.
  Sasa tafakari: Kuna Ongezeko la Joto Duniani linalochangia mabadiliko ya  Tabianchi(Global Warming&Climate Change)ambalo chimbuko lake hasa ni Marekani,Ulaya,Uchina, Japan, Mashariki ya Kati n.k-nchi za viwanda.
  Wanamwaga sumu nyingi angani, sisi Afrika tunachangia ongezeko la joto kwa asilimia tatu tu,lakinimadhara makubwa, majanga ya asili tunapata sisi kuliko wao.
 Mifugo imekufa kwa ukame, mazao yamenyauka shambani, kwa kukosa mvua-hata zikinyesha ni mafuriko yanayozoa mazao,kubomoa nyumba na udongo kuporomoka kama huko Same.
  Umasikini wetu unachangiwa na harakati za Mzungu kutafuta utajiri.
 Sasa angalia, Uingereza kutiliana saini na Misri mkataba kwamba tusitumie maji ya Ziwa hilo kumwagilia mashamba yetu mwaka 1929 na 1957.
  Mwaka 1929 na 57 Tanzania,Kenya na Uganda tulikuwa bado kupata uhuru. Uingereza; hili ziwa Nyanza lilikuwa lao lini mpaka wawagawie Misri?
Mzungu anaona mali ya Mwafrika ni ya kugawa kama nyama mezani!
  Wakati mikataba hiyo inatupiga marufuku kumwagilia mashamba maji ya Ziwa Nyanza, ama kuyatumia maji hayo kama chanzo cha umeme(hydroelectric schemes), kama huko Owen Falls,Jinja,Uganda na miradi kama huo wa kupeleka maji Kahama, Shinyanga, hawa Misri wanamwagilia mashamba makubwa ya kama ekari 600,000 jangwani.
  Uhalali huo Uingereza iliutoa wapi?
   Kutoka mwaka 1929 hadi sasa-takriban karne nzima, Uingereza na Misri wametulipa Pauni bilioni ngapi kama gawio katika biashara hii, ili sisi tuache kumwagilia mashamba,tusivue samaki n.k tuwaachie wao maji yote?
 Kwanza,kuliita ziwa hili eti Victoria, ni kesi; ni wizi wa mchana,ni utapeli. Hizi ziwa linaitwa Nyanza, Inyanja, Nyanja, Lweru n.k kulingana na makabila yanayolizunguka.
 Huyo Victoria amekujaje hapa?
 Ziwa Nyanza lilianza lini kuwa mjukuu wa Malkia Victoria, hata alibandike jina la ukoo? Anayo hakimiliki? Waache ujanja.
  Mto Nile(mungu wa Wamisri, “Ra”) unaanzia mto Kagera,hukatisha ziwani humo na kutokea Owen Falls, ambako huanza safari ya kilomita takriban 7,000 hadi huko Bahari ya Mediterranean.
 Nchi za Bonde la Nile ni Uganda, Tanzania, Kenya, Congo,Rwanda,Burundi, Ethiopia,Eritrea na Sudan ,lakini nchi iliyowahi kusema maji ni mali yake!
  Sasa, Uingereza ilikuwa Mungu kumuuzia maji ya Ziwa letu “Faraoh” wa Misri mwaka 1929 na 1957?
  Bila maji haya,hakuna Misri-River Nile is the matter of life and death.
Maji ni yetu,mali yao (basi uwe) ni mto bila maji yatokayo nyumbani kwetu!
Hapo mpo? Bila sisi,hakuna Nile, hakuna Hosni Mubarak waka Wamisri; wajirekebishe!! Ebo! wanatukatazaje kumwagilia mpunga huko Shinyanga na Kahama ili kujinusuru na njaa, na kula mafuvu ya mbwa, wakati wao wanategemea mashamba yaliyomwagiliwa na maji ya mvua inayonyesha huku kwetu Aprili na  Mei na kufika kwao Julai na Agosti?
 Misri ji jangwa,hakina mvua. Sisi tunaambiwa tukome kumwagilia viazi huko Majita, Nassa na Bukoba eti maji yatiririke kwa usalama hadi Bwawa la Aswan, Bonde la Toska n.k
  Eti watu milioni 100 tunaozunguka Ziwa hili kubwa Afrika,tufe njaa,wao watu takriban 75 walime,wavune wapate kuishi.Wao watu,sisi tumbili?
 Misri, imekuwepo tangu mwaka 3,2000 BC ina kila kitu,ina mafuta,madini,samaki, mbona haijatugawia sehemu ya maji ya Suez Canal, tuvue samaki?
 Waache uchokozi kwa mikataba feki ya mwaka 1929 na 57 sisi hatukuwahi kuitwa kusaini mikataba hii ya kitapeli.
  Afrika inajua njama za Mzungu kutaka kupora rasilimali zetu. Ndiyo maana, siku za karibuni, tulimsikia aliyekuwa Mwenyekiti wa AU, Kanali Muammar AL- Qaddafi wa Libya, kabla ya mauti kumkumba, akitaka Waafrika tuungane na kuwa taifa moja, UNITED STATES OF AFRICA.
 Tatizo, naye Gaddafi kaona umuhimu wa Waarabu wa Kaskazini na Weusi wa Kusini mwa Jangwa la Sahara(Pan Afrcanism) baada ya kuwindwa na Wamarekani kwa madege ya kivita huko Benghazi na Tripoli Aprili 14 mwaka 1986.
 Shushushu wa Libya, Abdel Basseti Ali al- Meghri,akahukumiwa kifo Januari 31 mwaka 2001 kwa ugaidi.
 Gaddafi, alikuwa na ugomvi na Wazungu,Wamarekani, kwa sababu wanasema Desemba 21 mwaka 1988 ndege ya Marekani Pan American Airways(Pan Am) aina ya Boeing 747 ililipuliwa na kombora na magaidi wa Gaddafi huko katika anga ya Lockerbie, Scotland.
Huu ulikuwa uongo mkubwa,na waliokamatwa na kuhukumiwa kifo waliachwa huru,ikasemwa walionewa!
  Watu 270 walikufa,wakafa pia 11 waliokuwa ardhini-Gaddafi kakubali yaishe,akalipa fidia.
  Gaddafi  akataka kuwapendeza  na kuacha kuisema Marekani ama Ulaya vibaya. Waburgaria waliwachoma watoto mjini Cairo kwa sindano zenye UKIMWI,wakaachiwa,wakarejea mjini Sofia,Burgaria kama mashujaa. Nani wa kukemea wazungu?
 Mandela? Gaddafi?
Labda, ‘R.G’ Mugabe .Hata Dodoma tuna Uranium,lakini nani wa kuanzisha mradi wa nyuklia ili tupate umeme?
  Najadili sababu za Afrika kuwa bara tajiri lakini watu wake masikini-The shame of plenty in the midst of poverty!
  Waafrika bilioni moja katika ya  wakazi bilioni 6.9 wa dunia ndifo fukara zaidi wakati kuna kila kitu?
 Uchaguzi huru na haki kama huu wa kwetu ndiyo unailetea Afrika matatizo makubwa.
 Transparency International(TI) linasema Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara ndiko kitovu cha ufisadi,wizi ndiko kuna nchi masikini zaidi, Highly or Heavily Indebted Poor Countries(HIPC) na sote tunafanya chaguzi za kidemokrasia!
 Huku twafa njaa,lakini akina Charles Taylor wanahonga almasi zetu kwa vimwana wa Uingereza, akina Naomi Campbell!!! Baadaye wanatiwa mbaroni na kufungwa ili kuwaziba midomo.
   0786 324 074
  
HAKI IKO KWA MUNGU TU

BIBLIA, na Wanaharakati wa Haki za Binadamu,hukubaliana kimsingi kwamba, “Haki za Binadamu zilianza wakati Binadamu alipoanza kuishi Duniani”.
Huu ni ukweli kamilifu; pale Mwanzo 2:16 na 17 Mungu anapomwambia Adamu kwamba alipewa ‘Uhuru’ wa kuchagua kumtii Mungu au kukataa(Freedom of Choice) alimpa HAKI ZA BINADAMU-Uhuru.
Hata hivyo, uhuru unawajibu,ukikosea umekwisha,ili haki za binadamu zidumu kuwepo ni sharti kuchagua vizuri kuitii sharia ya unyoofu ,The Moral law.
Dhana kwamba kila mtu anazo haki za binadamu ambazo tunasema ni haki za kimsingi,kwa kuwa kila mtu alizaliwa huru, ni ukweli halisi.
Haki za binadamu haziondolewi;hazipokonywi na  mtu na hakuna wa kuzipora-lakini zimeporwa sana hata na wanaojidai kuzihimiza siku hizi.Mtu anajidai kutangaza Haki za Binadamu,huku ni mwizi,fisadi,mbakaji!
Marekani na washirika wake wa Ulaya wanapojidai kuzitetea sana haki hizi za binadamu,wamezipora sana kwa kuua maelfu ya watu duniani pale wanapopigana vita vingi ili kutafuta maslahi yao.
Angalia vita vya Vietnam miaka ya 68-70;vita vya Irak,Afghanistan,Libya na mahali pengi hapa duniani ambako Shirika lao la Ujasusi, Central Intelligence Agency, wamechochea mno machafuko.
Mikataba na matangazo mengi ya Haki za Binadamu, imewapa watu kwa mkono wa kulia na kuziondoa kwa mkono wa pili wa kushoto.
Magna Carter ya Uingereza(1215),Bill of Rights ya Uingereza(1689),Tamko la Uhuru wa Marekani(1776),Tamko la Ufaransa la Haki za Mtu na Raia(French Declaration of Rights of man and Citizen) la 1789 n.k
Haya mengi,na linguine la Umoja wa Mataifa la Desemba 10,mwaka 1948,hakuna kinachosemwa kwa ukamilifu juu ya Haki zote za Binadamu na ukamilifu wake-ni udanganyifu mkubwa.
Maandamano yangalipo ya kudai haki Uingereza na Marekani,unyanyapaa na ubaguzi wa rangi ndiyo kwanza huendeshwa kila kona ya dunia,Waitalia walimnyanyapaa Zenedine Zidane,na hata sasa wanaongea ubaguzi wa rangi waziwazi.
Eti,misingi ya Haki za binadamu ni USAWA bila ubaguzi! Ubaguzi upo unalelewa Buckingham Palace, No 10 Downing Street na Oval Office, New York!
Vita vya kwanza vya Dunia(1914-18) na vya Pili(1939-45) vililetwa na mataifa makubwa.Waliua watu wengi sana kwa mamilioni,wengine walikosa makazi,wakawa wakimbizi,ili maslahi ya watu hawa yapatikane.
Hiroshima na Nagasaki.
Vita vya Kwanza vya Dunia, vilianza mwaka 1914 na vikaisha 1918.
Sababu hasa za vita hivi ni Mtawala wa Ujerumani, WILHELM  II,alitaka kuleta changamoto kwa maendeleo ya viwanda vya Uingereza,siyo vya Afrika,sawa?
 Katika Vita hivi vya Kwanza vya Dunia, walikufa jumla ya wanajeshi 8,418,000.
Askari wa Marekani waliouliwa vitani ni 126,000 na kiasi cha raia waliokufa katika vita hivyo ni 1,300,000.
Katika Vita vya Pili vya Dunia(1939-1945), walikufa askari 16,933,000; askari wa Kimarekani waliokufa ni 292,000 wakati raia waliouliwa ni 34,305,000.
 Vita hivi vilikoma wakati Marekani ilipolipua mabomu ya Atomiki katika miji ya Hiroshima na Nagasaki, Agosti 6 na 9 mwaka 1945.
Agosti 14, Japan ilitia saini ya kuacha vita na Septemba 2, mwaka huo wa 1945 vita hivi vilikwisha rasmi,vikiacha makovu ambayo hata sasa yangalipo. Hizi ni Haki za Binadamu sampuli gani wewe?
Huku ndiko tuendako,tunarejea katika vita, wakati mikataba ya amani inapovunjika,wakati uharibifu mkubwa wa mazingira unaposababisha karibu sana Mapigo saba ya Mwisho.
Kuharibika kwa utando wa Ozone angani,uharibifu wa vyanzo vya maji na ukataji miti ni janga lingine la hatari.
Tumchambue kidogo Adolf Hitler na chama chake cha NAZI dhidi ya Mayahudi wakati wa vita ya Pili ya Dunia, waliuawa Mayahudi wengi hata Umoja wa Mataifa ukaanzisha, “The Universal Declaration of Human Rights” mwaka 1948.
Mayahudi milioni sita waliuliwa kinyama.Tazama Filamu iitwayo, ESCAPING FROM SOBIBOR-Sobibor ni Poland,ambako Wayahudi waliuliwa na kuteswa kinyama ili kuangamizwa kabisa duniani.
Wauaji, eti walifikishwa mahakama ya Norenberg,iliyoanzishwa ajili ya kuwashitaki wahalifu wa vita,na uhalifu wa binadamu(crimes against humanity and war crimes).
Walipatikana na hatia ya kifungo jela.Kuna mahakama za aina hii nyingi kunapotokea mauaji ya kimbari kama Rwanda,ambako kuna mahakama ya Arusha,UNICTR.
Ipo ya Sierra Leone na ile ya Hague Uholanzi. Je haki hutendeka? Mbona wapo akina Felician Kibuga wamejificha Kenya,hawajawahi kukamatwa ili washitakiwe? Mahakamani kuna haki? Hakuna makengeza,  ‘double standards’?
Hata hivyo, Universal Declaration of Human Rights(UDHR), International Bill of Rights, International Covenant on Economic, Social and Cultural RightsI9CESCR),International Covenant on Civil and Political Rights(ICCPR) na mengine mengi husema kuwe na uhuru na haki,lakini hakuna haki hapa duniani.
Hakuna hata haki ya kuishi kwa masikini na makabwela kwa mfumo huu wa ubepari.
Nani anatengeneza bunduki na madege ya kijeshi? Nani hutengeneza misaili? Mizinga haiuzwi kwa waasi kama M23 huko Kongo? Kwa nini?
Marekani na Ulaya hawatengenezi silaha za maangamamizi hata leo baada ya vita baridi(Cold War) kumalizika?
Usidanganyike!Abu Ghraib,Guantanamo Bay na jela za wakubwa hawa huko Ulaya,huwakamata washukukiwa na kuwatesa,kuwafunga bila kuwafikisha mahakamani wakajitetee, haki gani sasa za binadamu?
Hakuna ‘Fair Trial’ ukikamatwa labda wa tuhuma za ugaidi. Hakuna haki hata katika mahakama za Tanzania,Ulaya na Marekani,tajiri hutazamwa zaidi na wakubwa hutetewa zaidi.
Mahakama ya Hague,Uholanzi ina makengengeza, haijawakamata Bush na Blair kwa kupeleka vita Irak kinyume na MATAKWA ya Umoja wa Mataifa.Wamekamatwa akina Charles Taylor tu, akina Uhuru Kenyatta watatiwa hatiani,lakini siyo wakubwa wa dunia.
Duniani mwenye haki ni mwenye nguvu,mamlaka,mali. Eti ‘retroactive punishment’ imezuiliwa kwa wote? Mbona Gaddafi na Osama waliuliwa kwa risasi bila kufikishwa mahakamani wakajitetee?
Sheria humtambua kila mtu hapa duniani? Huu ndiyo umbumbumbu wetu kushabikia Marekani na Ulaya kwamba kuna Haki za Binadamu!
Nimeeleza kasha cha Conjesta Ulikaye,Wazungu wa Uingereza waliombaka na kumuua na DPP(sasa Jaji)Geofrey Shaidi.Hata uhuru wa dini(Freedom of thoughts, Conscience and Religion)hakuna,subiri National Sunday Law,itatangazwa na Marekani,sasa watu wana uhuru gani wa kuabudu kama kuna New World Order?
Tumuulize Rais wetu Jakaya Kikwete,kama duniani(siyo Tanzania tu)kuna haki za watu wanyonge kabisa, ‘minority rights’? Hii mikataba sijui ya haki za raia na siasa ilishavunjwa na mataifa beberu na makampuni yao yanatumikisha watu kitumwa huko Myanmar!
Saro-Wiwa ameuliwa kwa nguvu za Royal/Dutch Shell,Chevron,Total na mengine huko Nigeria.Mrahaba wa haki za madini,nishati na mali asili zetu huporwa kwa kiburi cha mabwenyenye wa Marekani,viongozi wetu hupewa “Option” ama kuchukua r ushwa,au wakijidai wapotezwe!
Lumumba yuko wapi? Murtala Mohammed yuko wapi? Kabila?
Mnajidai kuandamana nini,waandamanaji huko Niger Delta waliuliwa na nani kama siyo makampuni ya Marekani na Uingereza? Uchochezi tu.
Eti haki za kuandamana! Mtavurugana kama Libya,kama Misri,kama Tunisia n.kWakubwa huongoza kuhalifu usawa na amani duniani,hakuna usawa wala usawia(universality) haki za watu wa mataifa madogo zilishaondolewa(alienable rights),sababu sisi waafrika,masikini?
Tukitaka haki ziwepo duniani,tukatae theories za akina Charles Robert Darwin(1809-1882) kwamba binadamu mwanzo alikuwa nyani,na kwamba dunia imetokea kwa bahati, ‘Big Bang’ ama evolution,uibukaji.
Kwenye uibukaji na maisha ya bahati hakuna usawa na haki,bali mwenye nguvu ndiye atastawi katika vita vya kugombea maisha-struggle for existence!
Katika dhana kwamba dunia imeibuka,na vilivyomo vimetokea kwa maguvu yake(survival of the fittest) hakuna haki na usawa wa binadamu, kuna sangara kuwala dagaa na furu,kuna simba kuwatafuna palahala na nyumbu.magugu kuyasonga mazao tunayolima ili tupate chakula n.k Haki itoke wapi sasa mahali ambapo hakuna sharia ya ulinganifu(universality) ama sharia ya unyoofu, moral conduct?
The Fundamental Code of Ethics ni Amri 10 za Mungu ambazo kila mtu hazitaki.Sasa unyoofu, “Morality’ hutoka wapi ili watu wasiwe wezi na mafisadi,bila Mungu?
Mkubwa atamjalije mdogo mahali ambapo watu hawataki amari ya kuwaheshimu watu,kuwajali na kuwapenda adui?Soma Mathayo 5:43-48. Matokeo yake, ‘Darwinism’ ni dhana ya mwenye nguvu ndiye atakayenusurika katika maisha haya ya kunyang’anyana chakula,maji na rasilimali.
Kwa kuwa hakuna kanuni za kupendana, basi watakaobaki duniani ni wenye nguvu(survival of the fittest) sisi tutakuwa mbolea ya kuneemesha mataifa makubwa,na wakubwa wenye uchumi mzuri-aliye na kidogo atanyang’anywa.
Kila mtu siku hizi hutamani awe na nguvu za utajiri,mamlaka na vyeo,wanaopiga kelele hawana jipya,wamepigwa kipepsi tu,lakini hata wao wakipata nafasi ni mafisadi wakubwa!
Kwa sababu hiyo,pasipo na Mungu akilini mwetu,hapana Haki za Binadamu,usawa,haki katika sharia na mgawo wa rasilimali n.k
Duniani hakuna sharia za unyoofu(morality) sasa haki itakujaje pasipo na sharia za unyoofu?Jambazi atakuwaje na upendo na huruma kazini kwake? Mwizi atakuwaje na huruma? Ingekuwa hivi basi wezi wangeshakoma kuiba.
Hakuna huruma,hakuna upendo kwa sababu pasipo Mungu na pasipo kutii sharia yake ya unyoofu na upendo,hakuna haki,kuna unyang’au.
Haki za Mashoga, Lesbian, Gay, Bisexual and Transgender(LGBT) ndizo haki hizi!Siku zote hakuna haki ila mwenye nguvu ndiye mshindi katika vita vya kupora rasilimali survival of the fittest, vita vya kugombea maisha, struggle foe existence,na vita vya kugombea mamlaka, struggle for supremacy.
Angalia wanasiasa wanavyowapambanisha ili wapate mamlaka! Kuna covenants sijui declarations za haki za binadamu,lakini hakuna haki!
Hakuna standard of rightness, kuna unyama watu wanakwenda upogo sababu hawaikubali sharia ya haki na unyoofu,moral principals, kuna uchoyo tu watu wote ni wanyama.
Sasa mnyama yupi atampa binadamu haki zake?Haki zimeporwa vitani, haki za wanyama kama zile za SHAMBA LA WANYAMA(animal farm) la George Orwell, zilishapokonywa na nguruwe wenye mamlaka!

Monday, February 4, 2013

afrika kizimbani-13

JAMII ya Kitanzania ilipewa changamoto chungu kupitia filamu ya Darwin’s Nightmare, ili ijirekebishe.
Mbali na kutiwa chumvi hapa na pale, filamu hiyo ni darasa tosha kwa uzembe, uchafu, umbumbumbu, kulindana na kukumbatia ulegevu, kunakofanywa na jamii yetu leo.
Naam,kuacha kuwategemea Wazungu,Mataifa makubwa kwa misaada na kuwachia kuchuma rasilimali zetu.
   Kwa mtu aliyewahi kuiona filamu hiyo, maarufu kama ‘Mapanki’ ataona changamoto anuai ambazo kama zitafanyiwa kazi kwa uzalendo na jamii ya Kitanzania (si serikali peke yake), athari hazitakuwepo.
  Kwanza kabisa,    Vyombbo vya usalama vya nchi yetu vinatia mashaka kama kweli vilikuwa vikifanya kazi yake sawasawa kipindi  mtengenezaji wa Darwin’s Nightmare, Hubert Sauper  alikuwepo nchini kutengeneza filamu hiyo.
     Aibu  ambayo ni changamoto ya kwanza inayotakiwa kuchukuliwa hatua kali na vyombo vyetu, ni jinsi mtu mgeni kama Sauper, alivyomudu kupiga picha chumba cha kuongozea ndege cha Mwanza, bila wahusika kujua anachofanya!
Mzungu akifika nchini hakaguliwi kama Mweusi,hiki nini kama siyo utumwa?
   Nasema bila wahusika kujua, kwa sababu mwanzoni tu mwa filamu hiyo uwanja wa ndege wa Mwanza unaonekana katika filamu hiyo: Mfanyakazi wa uwanja wa ndege anaacha kuongoza ndege, na kwenda kupiga nzi au tuseme wadudu waliokuwa wakirandaranda katika kioo cha dirisha la ofisi hiyo, kiasi cha kutia kinyaa!
   Mfanyakazi huyo mwanamume, anainuka kitini pake na kuwapiga wadudu hao kwa hasira kwa kutumia kitu kama gazeti!
   Katika hali inayosononesha sana,kishindo cha kumpiga nyuki  au tuseme mdudu yule (bila shaka mchafu sana) kinatikisa ofisi nzima ile hadi kioo cha dirisha kinakaribia kuvunjika!
Kwa mzalendo yeyote wa nchi hii aliyepata bahati ya kuiona filamu hiyo, hataacha kujiuliza: 
 
“Mainzi hadi Uwanja wa ndege?”
     Uwanja wa ndege ni usoni mwa nchi yoyote.
Wageni wanapofika katika nchi yoyote, iwe kwa mara ya kwanza au kadhaa, wanachoshuhudia uwanja wa ndege ndicho kinachowapa picha kwamba nchi wanayoingia sasa ni ya aina gani?
  Ya baridi , ama joto sana?
nchi Ya watu wacheshi, wakorofi, waungwana, wenye maringo, wazembe, wachafu wasiojijali; au hata maridadi sana.
    Lakini kinachoonekana katika filamu ile mwanzoni tu ni wadudu wanaorandaranda chumba kile cha kuongozea ndege; ambamo haiingii akilini kuwa wakati Sauper ama wasaidizi wake wanapiga picha wahusika hawakujua kuwa kitendo kile cha kizembe kingeidhalilisha nchi yetu?
   Tena tujiulize: Hubert Sauper, aliwahi kutiwa mbaroni na uongozi wa kijiji kimoja mkoani Kagera mwaka 2004. Baadaye aliachwa kwa amri ya vigogo serikalini.
Hata watu walioshirikiana naye walitiwa mbaroni kwa tuhuma za kupiga picha kambi za uvuvi, bila vibali!
   Ilielezwa kuwa kitendo hicho kilichoitwa cha kijasusi na viongozi hao kiliwafanya Sauper na wenzake kunyang’anywa vifaa vyao, zikiwemo kamera ambazo zilikuwa na picha tunazoema leo kuwa zimetudhalilisha!
   Ajabu ni kwamba licha ya baadhi ya vyombo vya habari kutangaza kuwa watu hao ‘walitekwa nyara’ waliachwa huru; na zana zao walikabidhiwa, wasipate usumbufu wowote!
   Naam, walikuwa na vibali vyote vya kazi; vilivyotolewa na Idara yetu ya Habari, Maelezo; na kwamba walikuwa na baraka zote za kufanya kazi hiyo ambayo leo imeleta kizaazaa na kiza kinene!
 
  Inadaiwa na Sauper mwenyewe na baadhi ya viongozi wa serikali kwamba mtu huyu “mwiba mchungu” kwa serikali, alikuwa akiwahonga baadhi ya maofisa wa serikakali, ili aende maeneo fulani fulani, ambako alifanikiwa kupiga picha mbaya ambazo kwa yakini zinatudhalilisha sana.
     Kama mgeni anaweza kuingia katika nchi  hii leo (miaka takriban 17 baada ya Vita Baridi) akafanya upelelezi wake kwa nguvu ya kuhonga, ni aibu na changamoto kwa kila Mtanzania kwamba nchi yetu inakwenda wapi? Uzalendo upo kwa kiwango gani dhalili katika nchi hii?
   Kila nchi, hata iwe dhalili kiasi gani; ina vyombo vyake vingi tu vya usalama. Kuna ulinzi na upelelezi wa namna nyingi tu.
Wapo wapelelezi wa siri ambao katika filamu nyingi wanaonyeshwa wakitimiza majukumu yao.
Katika vitabu vingi vya hadithi, tunawasoma wakitimiza wajibu wao kwa taifa lao.
   Kazi yao ya msingi ni kukusanya na kufafanua taarifa wanazokusanya hata za mataifa ya nje, kutazama uwezekano wa kuwepo vita na hata harakati na tamaduni mbalimbali za nchi nyingine; hususan zisizo rafiki.
  Tumewahi kujifunza kazi za mashirika makubwa ya kijasusi kama vile KGB (Komitet Gosudarstvennoy  Bezopasnosti) la Urusi ya zamani, ambalo sasa ni KFB.
Yapo mengine kama FBI na CIA ya Marekani, MI-5  na MI-6 ya Uingereza na mengine ambayo hufanya upelelezi wa ndani na nje; kwa lengo zuri la kuhakikisha usalama na ustawi wa nchi zao na watu wao.
    Linapokuja suala tete la Hubert Sauper na filamu yake ya mapanki, umma wa Watanzania unapata maswali mengi:
Kwamba vyombo vyetu vya usalama ( Intelligence Agencies) vilikuwa wapi kumnasa Sauper?
    Magazeti yaliandika habari za kutekwa kwake na wavuvi visiwani. Kwa nini aliachwa huru kwa amri toka juu, halafu miaka michache tu baadaye nchi inaombolezea picha zilizopigwa machoni mwa vyombo hivi?
   Changamoto nyingine kutokana na filamu hii ni ukosefu wa ajira kwa vijana wetu.
Mtu aitwaye Raphael ameonekana katika vipande vigi vya filanu hiyo. Amejitambulisha kama Mlinzi, bila shaka wa Chuo cha Utafiti wa samaki.
  Anasema katika fiamu hiyo: “ Ukipata kazi hata mbaya, unafanya. Kwani hivi sasa ukitafuta kazi (nzuri) hakuna”.Ajira hakuna.
Hapa anaonekana akiwa na upinde na mishale yake.
 Asilimia 80 ya Watanzania hawana ajira za moja kwa moja.
 Wanajitafutia vibarua wanavyofanya kwa malipo kidogo sana kutoka kwa hawa wawekezaji.Wanapunjwa ama kudhalilishwa tu.
   Wengi wa wakazi wa Kanda ya Ziwa ni wakulima na pia wavuvi.
Katika mikoa hiyo samaki ni chakula, fedha, tena ni ajira.Siku hizi samaki hakuna, wanakwenda Nairobi na Ulaya, hata ziwani hakuna samaki,wamekwisha.
    Hivyo kinachoonyeshwa katika filamu hiyo ni kuhoji kama samaki wanaitosheleza jamii hiyo kwa chakula; ama kama wengi wamenufaika kutokana na sekta hiyo; na pia kama wanazo fedha za kutosha kupata mahitaji yao kupitia samaki.
   Kama samaki bado wananufaisha watu wachache, tena wageni, basi ndiyo maana kuna kelele hizi za baadhi ya dada zetu kujiuza kwa marubani wa madege ya Kirusi yanayokuja kuchukua minofu ya samaki kwa ujira wa dola 10!
    Hapa kuna msichana aliyeitwa Eliza, anayesemwa kuwa ‘chakula’ cha marubani wengi (a girl friend of many pilots); pamoja na bishara hii haramu, haachi kuisifia Tanzania kwamba jina lake ni tamu sana!
      Kwamba, kama jamii hii ingekuwa imenufaika sana kiuchumi kufuatia biashara ya sangara, basi hata watoto wa mitaani walioachwa kuzagaa bila msaada, wangetafutiwa ufumbuzi. Omba-omba walioanzisha kwaya ili kujitafutia chakula kutoka kwa wapita njia, labda baada ya kutelekezwa na jamii (siyo serikali pekee) wangetazamwa na jamii hii, ili wasigeuke ajenda ya kitaifa; na si katika Darwin peke yake.
    Umasikini na ujinga wa watu wetu unawafanya wanywe gongo katika makambi ya uvuvi.
Kiongozi wa kambi aliyetambulishwa kama Mkono,anawaongoza wenzake waliohojiwa na Sauper kueleza namna wasivyonufaishwa na kazi ya uvuvi…wanaonekana wakiwa bado katika nishai ya ulevi wa gongo; tena wakiwa wachafu wenye tongotongo usoni…wanatia kinyaa.
    Kwa Mgeni ambaye hajafika Tanzania, akiwaona hao jamaa zake Mkono, bila shaka atajua samaki wale watamu sangara huvuliwa na wanywa gongo wale wasioweza hata kunawa tongotongo!
 Ni aibu, tena kinyaa!Umalaya,uchangudoa,watoto wa mitaani n.k wakati tuna rasilimali?
  Vema Watanzania tukajiuliza: Kuna vijiwe vingapi vya gongo, ambako Watanzania wenzetu huamkia hata kabla ya kupiga mswaki na kuanza kulewa chakari?
 Kuna vijiwe vingapi vya vijana wetu, wasiojua hata kufagia uwanja nyumbani, ila kula-kulala?
Tuna rasilimali nyingi,lakini watu masikini-Poverty in the midst of plentful!
  Tena vipo vijiwe vingapi vya vijana wasio na ajira, lakini huamkia kuvuta bangi, madawa ya kulevya,ulevi n.k? Mwanza kuna vijiwe vya siasa tangu asubuhi hadi jioni,nenda KEMONDO,jirani na mitaa ya Uhuru na Bantu!
Tuna ardhi,mito,maziwa na mabonde yenye rutuba lakini tungali wenye njaa na machangudoa,wakabaji,vibaka na majambazi.
    Halafu, watoto hurejea nyumbani nyakati za chakula (huitwa watoto wa mama, kula kulala!) ambao aghalabu huiba mali za nyumbani ili watimize kiu yao ya ulevi wa madawa haramu, gongo, uasherati, uchafu na ujinga, bila kuzingatia litakalotokea maishani. Hawafundishwi kujitegemea,bali kutegemea misaada ya wafadhili.
    Kuhusu madhara ya utandawazi, wakati nchi za Ulaya zikinufaika sana na rasilimali zetu kama sangara, sisi Watanzania tunaonekana kuchechemea vilivyo katika vita hiyo ya kugombea maisha ili kujinusuru na kifo.
    Wakati madege makubwa ya Kirusi, Ullyushin, yakipaa kwa kasi na shehena ya minofu yetu kwenda Ulaya, anaonekana Mtanzania mmoja jirani na Uwanja wa ndege wa Mwanza, akiwa anaendesha baiskeli yake kwa kasi, utadhani alikuwa akiifukuza!
    Bila shaka Sauper, alitaka kuuonyesha ulimwengu kwamba, wakati wenzetu wakipora rasilimali zetu kwa ndege, sisi tungali tukitumia usafiri wa baiskeli! Tutafika saa ngapi katika zama wa sayansi na teknolojia?
Tutamiliki lini zana bora, kupitia mauzo ya rasilimali zetu nje?
 Lini tutakwenda mwendo kasi kama Wazungu, katika mbio za maendeleo katika Ulimwengu wa Uatadawazi na teknolojia?
    Kila siku, marubani waliohojiwa walisema kati ya tani 500 hadi 600 za samaki husombwa na ndege kwenga Ulaya.
 Kwamba dege moja tu lilikuwa na uwezo wa kubeba tani 55. Hali hiyo huwafanya marubani hao kuwa kazini kila kukicha.
    Aliyekuwa mtoto wa mitaani, Jonathan Nathaniel ambaye ni mchora picha, anaonekana katika filanu hiyo akijitambulisha kama raia wa dunia (Citizen of the World) kufuatia jamii ya kitanzania kutochukua hatua madhubuti za kuondosha tatizo la watoto hao!
 Naam, kutowatekeleza.
    Hii ni kuonyesha kuwa baadhi ya watoto wa mitaani wamepoteza mapenzi na uzalendo wao kwa Tanzania!
 Badala yake walijitambulisha kwa Sauper kama raia wa Dunia, na wala si wa Tanzania.Watoto wa mitaani hawaoni faida kuitwa Watanzania,ila raia wa duniani.
  Kuna mashirika mangapi hapa yanayojidai kuwafadhili omba-omba na watoto wa mitaani, lakini bado wapo na jamii inaona tu bila kuchukua hatua? Wapo watu wangapi hata Mwanza kwenyewe, ambao huporwa simu za mononi na mali zingine na watoto hao?
 Je, tumekubali wawe majambazi, bila kuchukua hatua tangu leo kuhakikisha kuwa hawapo mitaani, badala yake wanawezeshwa kufanya kazi halali?
  Tena, wapo watu wangapi wanaojineemesha kwa asasi za watoto wa mitaani, wakati wao wakipata adha zinazofichuliwa na filamu hiyo tunayosema inatudhalilisha?
 Kumbe inatufunua uovu wetu pia.
    Wanaonekana wakivuta petroli ili walewe. Wanavuta gundi, wanavuta  sigara na hata bangi.
Jomathan anapohojiwa anasema wanafanya hivyo ili kujisahaulisha na madhila wanayopata mitaani! Jua kali, mvua, baridi kali na kukosa faragha…watoto hulala vibarazani na dada, kaka ,mama na baba zao wanaojamiana mithili ya ng’ombe, pasi na faragha!
 Huyo, Jonathan aliyemsaidia Sauper kutengeneza filamu hiyo, bado ni "Chokoraa" aishie hata leo mitaani jijini Mwanza, licha ya kulipwa shilingi 300,000 na huyu Hubert Sauper.
 Hiki ni kitisho kwa taifa lolote linalotaka kujenga maadili mema kuwaacha watoto wa mitaani kuzagaa ili kuwa chanzo cha mapato kwa Wazungu na aibu kwetu wenyewe.
      Kwamba wakisha lewa hulala popote bila kuogopa.
 Na kwamba kutokana na hali hiyo ya kulewa, na kutojijua (wengine huonekana katika filamu hiyo, wakiwa wamelala usingizi mitaani nyakati za usiku)   hata wale wa kiume hulawitiwa bila habari wala hadhari…Je, Tanzania tumeshindwa kukabiliana na watoto wa mitaani?
      Kuna dhana inayosemwa na marubani wa Kirusi kuwa Watanzania hawataki kufanya kazi! (These black people do not work)!
Picha inayoonekana kupitia Darwin’s Nightmare ni kwamba Watanzania walio wengi ni wavivu wanaopenda raha, lakini hawataki kazi
 Bila shaka hapa, kinachozungumzwa ni kuhusu vijiwe viwe vya kahawa, karata, ‘deal’ za mjini ,majungu, siasa au hata uongo, vinavyofanywa nyakati za kazi!
     Katika hali hii tutawanusuru watoto wetu kutopigania sufuria la wali waliopewa na mpita njia?
   Jamii ijitazame…kuna vijiwe vingapi vya" Binzala-nzala" au ‘kula kulala, hasa mijini, ambao huamkia bao, karata na ubishi wa kijinga nyakati za kazi?
  Mwisho, rubani mmoja anapohojiwa juu ya zawadi za Krisimasi, anasema anawapelekea watoto wa Ulaya  zabibu toka Afrika, wakati watoto wa Afrika wanaletewa zawadi ya bunduki toka Ulaya, ili waendelee kuuana !
    Haya ni baadhi ya matusi mazito tunayopata toka kwa Wazungu, ambayo kila mmoja wetu kwa nafasi yake anapaswa kuchukua hatua tangu sasa ili kuhakikisha kilichosemwa kama kipo tukiondoe ili kujitakasa.
   Leo Waafrika tunauana bila kusameheana.
Viongozi wetu wanapoingia madarakani, hawataki tena kutenda haki, bali kuiba mpaka wanapoondolewa kwa mtutu wa bunduki, zilizoletwa na haohao majahili, Wazungu! Hii ni aibu!
    Kwa upande mwingine matusi hayo yaliyomo katika Darwin’s Nightmare ni changamoto kwetu kuacha uchafu, ujinga ,  uzezeta wa kukubali kuibiwa kila kilicho chetu kwa ujira kidogo.
   Ifike hatua tuwe wazalendo wa kweli wa nchi yetu na Bara letu, na siyo uzalendo wa matumbo yetu.
 Hii ni changamoto kwa viongozi wetu wanaodanganya umma ili wasalie madarakani, ambako huiba na kujinufaisha huku raia wakibaki fukara, hadi waanzishe vita na mauaji kupindiua serikali..aibu!
Tangu leo Afrika ione uchungu kwa haya yaliyosemwa na Hubert Sauper, badala ya kumtafuta ili kumshitaki, tukae chini na kuvimeza ‘vidonge’ alivyo tupa…Baniani mbaya, kiatu chake dawa!
Afrika inaibiwa sana!
  Mwandishi hupatikana kwa simu 0754 324 074 au 0786 324 074
   
AFRIKA KIZMBANI 14