BIBLIA, na
Wanaharakati wa Haki za Binadamu,hukubaliana kimsingi kwamba, “Haki za Binadamu
zilianza wakati Binadamu alipoanza kuishi Duniani”.
Huu ni
ukweli kamilifu; pale Mwanzo 2:16 na 17 Mungu anapomwambia Adamu kwamba alipewa
‘Uhuru’ wa kuchagua kumtii Mungu au kukataa(Freedom of Choice) alimpa HAKI ZA
BINADAMU-Uhuru.
Hata hivyo,
uhuru unawajibu,ukikosea umekwisha,ili haki za binadamu zidumu kuwepo ni sharti
kuchagua vizuri kuitii sharia ya unyoofu ,The Moral law.
Dhana kwamba
kila mtu anazo haki za binadamu ambazo tunasema ni haki za kimsingi,kwa kuwa
kila mtu alizaliwa huru, ni ukweli halisi.
Haki za
binadamu haziondolewi;hazipokonywi na
mtu na hakuna wa kuzipora-lakini zimeporwa sana hata na wanaojidai
kuzihimiza siku hizi.Mtu anajidai kutangaza Haki za Binadamu,huku ni
mwizi,fisadi,mbakaji!
Marekani na
washirika wake wa Ulaya wanapojidai kuzitetea sana haki hizi za
binadamu,wamezipora sana kwa kuua maelfu ya watu duniani pale wanapopigana vita
vingi ili kutafuta maslahi yao.
Angalia vita
vya Vietnam miaka ya 68-70;vita vya Irak,Afghanistan,Libya na mahali pengi hapa
duniani ambako Shirika lao la Ujasusi, Central Intelligence Agency, wamechochea
mno machafuko.
Mikataba na
matangazo mengi ya Haki za Binadamu, imewapa watu kwa mkono wa kulia na
kuziondoa kwa mkono wa pili wa kushoto.
Magna Carter
ya Uingereza(1215),Bill of Rights ya Uingereza(1689),Tamko la Uhuru wa
Marekani(1776),Tamko la Ufaransa la Haki za Mtu na Raia(French Declaration of
Rights of man and Citizen) la 1789 n.k
Haya
mengi,na linguine la Umoja wa Mataifa la Desemba 10,mwaka 1948,hakuna
kinachosemwa kwa ukamilifu juu ya Haki zote za Binadamu na ukamilifu wake-ni
udanganyifu mkubwa.
Maandamano
yangalipo ya kudai haki Uingereza na Marekani,unyanyapaa na ubaguzi wa rangi
ndiyo kwanza huendeshwa kila kona ya dunia,Waitalia walimnyanyapaa Zenedine
Zidane,na hata sasa wanaongea ubaguzi wa rangi waziwazi.
Eti,misingi
ya Haki za binadamu ni USAWA bila ubaguzi! Ubaguzi upo unalelewa Buckingham
Palace, No 10 Downing Street na Oval Office, New York!
Vita vya
kwanza vya Dunia(1914-18) na vya Pili(1939-45) vililetwa na mataifa
makubwa.Waliua watu wengi sana kwa mamilioni,wengine walikosa makazi,wakawa
wakimbizi,ili maslahi ya watu hawa yapatikane.
Hiroshima na
Nagasaki.
Vita vya
Kwanza vya Dunia, vilianza mwaka 1914 na vikaisha 1918.
Sababu hasa za vita hivi ni Mtawala wa Ujerumani, WILHELM II,alitaka kuleta changamoto kwa maendeleo ya viwanda vya Uingereza,siyo vya Afrika,sawa?
Katika Vita hivi vya Kwanza vya Dunia, walikufa jumla ya wanajeshi 8,418,000.
Askari wa Marekani waliouliwa vitani ni 126,000 na kiasi cha raia waliokufa katika vita hivyo ni 1,300,000.
Katika Vita vya Pili vya Dunia(1939-1945), walikufa askari 16,933,000; askari wa Kimarekani waliokufa ni 292,000 wakati raia waliouliwa ni 34,305,000.
Vita hivi vilikoma wakati Marekani ilipolipua mabomu ya Atomiki katika miji ya Hiroshima na Nagasaki, Agosti 6 na 9 mwaka 1945.
Sababu hasa za vita hivi ni Mtawala wa Ujerumani, WILHELM II,alitaka kuleta changamoto kwa maendeleo ya viwanda vya Uingereza,siyo vya Afrika,sawa?
Katika Vita hivi vya Kwanza vya Dunia, walikufa jumla ya wanajeshi 8,418,000.
Askari wa Marekani waliouliwa vitani ni 126,000 na kiasi cha raia waliokufa katika vita hivyo ni 1,300,000.
Katika Vita vya Pili vya Dunia(1939-1945), walikufa askari 16,933,000; askari wa Kimarekani waliokufa ni 292,000 wakati raia waliouliwa ni 34,305,000.
Vita hivi vilikoma wakati Marekani ilipolipua mabomu ya Atomiki katika miji ya Hiroshima na Nagasaki, Agosti 6 na 9 mwaka 1945.
Agosti 14,
Japan ilitia saini ya kuacha vita na Septemba 2, mwaka huo wa 1945 vita hivi
vilikwisha rasmi,vikiacha makovu ambayo hata sasa yangalipo. Hizi ni Haki za
Binadamu sampuli gani wewe?
Huku ndiko tuendako,tunarejea katika vita, wakati mikataba ya amani inapovunjika,wakati uharibifu mkubwa wa mazingira unaposababisha karibu sana Mapigo saba ya Mwisho.
Kuharibika kwa utando wa Ozone angani,uharibifu wa vyanzo vya maji na ukataji miti ni janga lingine la hatari.
Huku ndiko tuendako,tunarejea katika vita, wakati mikataba ya amani inapovunjika,wakati uharibifu mkubwa wa mazingira unaposababisha karibu sana Mapigo saba ya Mwisho.
Kuharibika kwa utando wa Ozone angani,uharibifu wa vyanzo vya maji na ukataji miti ni janga lingine la hatari.
Tumchambue kidogo Adolf Hitler na chama chake cha NAZI dhidi
ya Mayahudi wakati wa vita ya Pili ya Dunia, waliuawa Mayahudi wengi hata Umoja
wa Mataifa ukaanzisha, “The Universal Declaration of Human Rights” mwaka 1948.
Mayahudi milioni sita waliuliwa kinyama.Tazama Filamu
iitwayo, ESCAPING FROM SOBIBOR-Sobibor ni Poland,ambako Wayahudi waliuliwa na
kuteswa kinyama ili kuangamizwa kabisa duniani.
Wauaji, eti walifikishwa mahakama ya Norenberg,iliyoanzishwa
ajili ya kuwashitaki wahalifu wa vita,na uhalifu wa binadamu(crimes against
humanity and war crimes).
Walipatikana na hatia ya kifungo jela.Kuna mahakama za aina
hii nyingi kunapotokea mauaji ya kimbari kama Rwanda,ambako kuna mahakama ya
Arusha,UNICTR.
Ipo ya Sierra Leone na ile ya Hague Uholanzi. Je haki
hutendeka? Mbona wapo akina Felician Kibuga wamejificha Kenya,hawajawahi
kukamatwa ili washitakiwe? Mahakamani kuna haki? Hakuna makengeza, ‘double standards’?
Hata hivyo, Universal Declaration of Human Rights(UDHR),
International Bill of Rights, International Covenant on Economic, Social and
Cultural RightsI9CESCR),International Covenant on Civil and Political Rights(ICCPR)
na mengine mengi husema kuwe na uhuru na haki,lakini hakuna haki hapa duniani.
Hakuna hata haki ya kuishi kwa masikini na makabwela kwa
mfumo huu wa ubepari.
Nani anatengeneza bunduki na madege ya kijeshi? Nani
hutengeneza misaili? Mizinga haiuzwi kwa waasi kama M23 huko Kongo? Kwa nini?
Marekani na Ulaya hawatengenezi silaha za maangamamizi hata
leo baada ya vita baridi(Cold War) kumalizika?
Usidanganyike!Abu Ghraib,Guantanamo Bay na jela za wakubwa
hawa huko Ulaya,huwakamata washukukiwa na kuwatesa,kuwafunga bila kuwafikisha
mahakamani wakajitetee, haki gani sasa za binadamu?
Hakuna ‘Fair Trial’ ukikamatwa labda wa tuhuma za ugaidi.
Hakuna haki hata katika mahakama za Tanzania,Ulaya na Marekani,tajiri hutazamwa
zaidi na wakubwa hutetewa zaidi.
Mahakama ya Hague,Uholanzi ina makengengeza, haijawakamata
Bush na Blair kwa kupeleka vita Irak kinyume na MATAKWA ya Umoja wa Mataifa.Wamekamatwa
akina Charles Taylor tu, akina Uhuru Kenyatta watatiwa hatiani,lakini siyo
wakubwa wa dunia.
Duniani mwenye haki ni mwenye nguvu,mamlaka,mali. Eti ‘retroactive
punishment’ imezuiliwa kwa wote? Mbona Gaddafi na Osama waliuliwa kwa risasi
bila kufikishwa mahakamani wakajitetee?
Sheria humtambua kila mtu hapa duniani? Huu ndiyo umbumbumbu
wetu kushabikia Marekani na Ulaya kwamba kuna Haki za Binadamu!
Nimeeleza kasha cha Conjesta Ulikaye,Wazungu wa Uingereza
waliombaka na kumuua na DPP(sasa Jaji)Geofrey Shaidi.Hata uhuru wa dini(Freedom
of thoughts, Conscience and Religion)hakuna,subiri National Sunday
Law,itatangazwa na Marekani,sasa watu wana uhuru gani wa kuabudu kama kuna New
World Order?
Tumuulize Rais wetu Jakaya Kikwete,kama duniani(siyo
Tanzania tu)kuna haki za watu wanyonge kabisa, ‘minority rights’? Hii mikataba
sijui ya haki za raia na siasa ilishavunjwa na mataifa beberu na makampuni yao
yanatumikisha watu kitumwa huko Myanmar!
Saro-Wiwa ameuliwa kwa nguvu za Royal/Dutch
Shell,Chevron,Total na mengine huko Nigeria.Mrahaba wa haki za madini,nishati
na mali asili zetu huporwa kwa kiburi cha mabwenyenye wa Marekani,viongozi wetu
hupewa “Option” ama kuchukua r ushwa,au wakijidai wapotezwe!
Lumumba yuko wapi? Murtala Mohammed yuko wapi? Kabila?
Mnajidai kuandamana nini,waandamanaji huko Niger Delta
waliuliwa na nani kama siyo makampuni ya Marekani na Uingereza? Uchochezi tu.
Eti haki za kuandamana! Mtavurugana kama Libya,kama
Misri,kama Tunisia n.kWakubwa huongoza kuhalifu usawa na amani duniani,hakuna
usawa wala usawia(universality) haki za watu wa mataifa madogo
zilishaondolewa(alienable rights),sababu sisi waafrika,masikini?
Tukitaka haki ziwepo duniani,tukatae theories za akina
Charles Robert Darwin(1809-1882) kwamba binadamu mwanzo alikuwa nyani,na kwamba
dunia imetokea kwa bahati, ‘Big Bang’ ama evolution,uibukaji.
Kwenye uibukaji na maisha ya bahati hakuna usawa na
haki,bali mwenye nguvu ndiye atastawi katika vita vya kugombea maisha-struggle
for existence!
Katika dhana kwamba dunia imeibuka,na vilivyomo vimetokea
kwa maguvu yake(survival of the fittest) hakuna haki na usawa wa binadamu, kuna
sangara kuwala dagaa na furu,kuna simba kuwatafuna palahala na nyumbu.magugu
kuyasonga mazao tunayolima ili tupate chakula n.k Haki itoke wapi sasa mahali
ambapo hakuna sharia ya ulinganifu(universality) ama sharia ya unyoofu, moral
conduct?
The Fundamental Code of Ethics ni Amri 10 za Mungu ambazo
kila mtu hazitaki.Sasa unyoofu, “Morality’ hutoka wapi ili watu wasiwe wezi na
mafisadi,bila Mungu?
Mkubwa atamjalije mdogo mahali ambapo watu hawataki amari ya
kuwaheshimu watu,kuwajali na kuwapenda adui?Soma Mathayo 5:43-48. Matokeo yake,
‘Darwinism’ ni dhana ya mwenye nguvu ndiye atakayenusurika katika maisha haya
ya kunyang’anyana chakula,maji na rasilimali.
Kwa kuwa hakuna kanuni za kupendana, basi watakaobaki
duniani ni wenye nguvu(survival of the fittest) sisi tutakuwa mbolea ya
kuneemesha mataifa makubwa,na wakubwa wenye uchumi mzuri-aliye na kidogo atanyang’anywa.
Kila mtu siku hizi hutamani awe na nguvu za utajiri,mamlaka
na vyeo,wanaopiga kelele hawana jipya,wamepigwa kipepsi tu,lakini hata wao
wakipata nafasi ni mafisadi wakubwa!
Kwa sababu hiyo,pasipo na Mungu akilini mwetu,hapana Haki za
Binadamu,usawa,haki katika sharia na mgawo wa rasilimali n.k
Duniani hakuna sharia za unyoofu(morality) sasa haki
itakujaje pasipo na sharia za unyoofu?Jambazi atakuwaje na upendo na huruma
kazini kwake? Mwizi atakuwaje na huruma? Ingekuwa hivi basi wezi wangeshakoma
kuiba.
Hakuna huruma,hakuna upendo kwa sababu pasipo Mungu na
pasipo kutii sharia yake ya unyoofu na upendo,hakuna haki,kuna unyang’au.
Haki za Mashoga, Lesbian, Gay, Bisexual and Transgender(LGBT)
ndizo haki hizi!Siku zote hakuna haki ila mwenye nguvu ndiye mshindi katika
vita vya kupora rasilimali survival of the fittest, vita vya kugombea maisha,
struggle foe existence,na vita vya kugombea mamlaka, struggle for supremacy.
Angalia wanasiasa wanavyowapambanisha ili wapate mamlaka!
Kuna covenants sijui declarations za haki za binadamu,lakini hakuna haki!
Hakuna standard of rightness, kuna unyama watu wanakwenda
upogo sababu hawaikubali sharia ya haki na unyoofu,moral principals, kuna
uchoyo tu watu wote ni wanyama.
Sasa mnyama yupi atampa binadamu haki zake?Haki zimeporwa
vitani, haki za wanyama kama zile za SHAMBA LA WANYAMA(animal farm) la George
Orwell, zilishapokonywa na nguruwe wenye mamlaka!
No comments:
Post a Comment