Wednesday, February 13, 2013

PAPA BENEDICT XVI AMETEMWA NA SYSTEM VATICAN



FEBURUARI 11, mwaka huu wa 2013,Papa Benedict XV1 ametangaza kuachia ngazi ya Upapa(Papacy).
Papa,ni Askofu Mkuu wa Vatican, ambaye huchaguliwa na Makadinari aghalabu Papa mwingine anapofariki dunia,au kuachia madaraka.
Papa Benedict XVI alitishia kuachia ngazi mwaka jana; na tayari katangaza rasmi azma yake ya kuondoka katika kiti cha enzi cha Ukuu wa Kanisa Katoliki na Ukuu wan chi ya Vatican, Feburuali 28 mwaka huu.
Sababu, eti ni afya mbaya, wakati tulishaona PAPA JOHN PAUL II aliugua ugonjwa wa kutetemeka,akashindwa kuongea,lakini wakasubiri hadi alipofariki dunia mwaka 2005.
 Mwaka 753 BC mji uliojengwa Ulaya ni Rome. Na Vatican inazungukwa na Rome, ni mji wenye ukubwa wa ekari 108.7 tu ndani ya Rome.
Hata London haukuwepo, Uingereza ilikuwa kijiji kidogo mwaka 1000 AD. Hata mwaka 500 BC Rome lilikuwa jiji tena “SUPER POWER” Duniani, ulijengwa na Romulus.
 Katika mji huu ndiko yaliko mamlaka ya kidini,Vatican.
Unaposema Vatican unasema kanisa la Mungu. Vatican imekuwa nchi Feburuari 11, mwaka 1929 zama za Benito Mussolini.
Habari zinazovuja(hata BBC walitangaza mwaka jana) kwamba kuna njama za mapinduzi baridi na mchakato wa kumsimika Papa mpya badala ya Benedict XVI.
Rome ni mahali ambapo wameishi ma-Baba Watakatifu(Popes) wa Katoliki wapatao 302.
Mji huu ulikuwa makao makuu ya dola ya Rumi, hata zama za Yesu,mitume na zama za Biblia Takatifu yaani kati ya mwaka BC 1500 na 96 AD.
Profesa  Joseph Ratzinger,Mtaalamu wa theolojia(Profesa wa Theolojia katika Chuo Kikuu cha Munich,Ujerumani) alishiriki katika makongamano ya kutaka mageuzi katika kanisa Katoloki.
Kanisa Katoliki lilipinga Ukomunisti kwa nguvu zama za Vita vya Pili vya Dunia, ambavyo Joseph Ratzinger alishiriki kikamilifu.
Alianza kuaminiwa katika kanisa hili mwaka 1960; amekuwa Askofu Mkuu wa Munich,Kadinari na Mkuu wa Idara  wa Vatican,na Mrakibu wa Jumuiya ya Ulinzi wa Imani; akijua chochote kinachotakiwa kuangaliwa na Kanisa Katoloki.
Kashfa zinazilikumba kanisa: Ulawiti wa watoto wa kiume, yeye alikuwa ‘The Defense of Faith’.
Kuna misimamo ya mapadre kutaka kuoa.kanisa dada la Anglican limeruhusu ndoa za mashoga na wasagaji wakati kukiwa na mbinyo mkali katika kanisa hili. Yeye siku zote amekuwa akipinga,na juzi akaregeza msimamo katika matumizi ya kondomu.
Kuna wimbi la kanisa katika kufuata tamaduni za sikukuu za kipagani.Mfano:Krismasi ni Desemba 25 ambayo ni sikukuu ya kipagani ya SOLLNVICTUS MITHRAS-ni ibada ya jua.
Siku ya mungu jua asiyeshindwa,ilianza karne mbili kabla ya Kristo.Yesu hakuzaliwa tarehe 25 Desemba,isipokuwa ni siku ya kipagani ya kubambkwa.Kanisa linakiri wazi kwamba iliwekwa ili kuwafanya waumini waondoe upagani akilini mwao na kumfikiria mtoto Yesu,badala ya upagani wa mungu jua!
Profesa Ratzinger,naam Joseph Ratzinger,mtafiti wa Theolojia alianza kupingana na ukweli wa Biblia na kusisitiza kuwa Yesu alizaliwa Desemba 25; na akasisitiza siku hii ikumbukwe kama siku ya kuzaliwa Yesu,badala ya sikukuu ya mapagani.
Joseph Ratzinger ametawala Vatican kama Papa Benedict XVI wakati wa mpito ambao siri nyingi za Vatican zikivujishwa katika vyombo vya habari.
Ratzinger (85) alipochaguliwa kuwa Papa, alishadharauliwa,na ilidhaniwa kwamba mkusanyiko wa watu St.Peter’s Square ungepungua na mvuto wa upapa ungetindika.
Hakuheshimika kama mtangulizi wake,Papa Yohane Paulo II, NA Profesa Ratzinger amekuwa akiwachanganya Wakatoliki kwa mambo magumu, ‘difficult things’ wakati fulani Septemba huko Regensburg aliwachefua Waislam kuhusu imani na machafuko yanayoletwa na ugaidi.
Jumamosi usiku, Aprili Pili mwaka 2005,Profesa Ratzinger alichaguliwa kuwa Papa mara baada ya kifo cha Papa Yohanne Paulo II.
Yohanne Paulo II yeye alichaguliwa kuwa Papa Oktoba mwaka 1978,mara baada ya kifo cha Yohane Paulo I.
Alinusurika kuuawa, aliugua ugonjwa wa kutetemeka sana,mbona hakuwahi kujiuzulu?
Kwa miaka 455 kabla ya Papa Paulo II mapapa wote walikuwa Waitaliani,Papa Paulo II alikuwa kutoka Poland,Ulaya.Mwaka 1415 Papa Gregory alijiuzulu,bila shaka kwa sababu ya mbinyo mkali,na papa mwingine alipinduliwa na kufungwa jela alikofia gerezani, wakati wa maasi ya Wafaransa.
 Kuna mapapa takriban 302. Kulingana na Kanisa Katoloki,papa wa kwanza ni Petro(32-67 AD) HADI alipouliwa na Kaisari Nero. Kaisari Nero alichoma moto jiji la Rome akawasingizia Wakristo akina Petro,na ndipo alipofunguliwa kesi ya uhaini na kuhukumiwa kukatwa kichwa.
Mwaka 58 AD Paulo na Batholomayo waliuliwa kwa staili hiyo hiyo na kwa makosa ya kubambikwa,sasa utajiuliza upapa wa Petro ulianza lini?
 Nataka kusema kwamba, Papa Benedict XVI amekumbana na ‘vya kumkuta’kutokana na misimamo yake mikali,na sasa makadinari wasiopungua 118 watamchagua papa mwingine,kura zitakapopigwa na moshi mweupe kupaa angani,kabla ya mwezi Machi kwisha.
Makadinari wanaomchagua Papa huwa umri wao ni chini ya miaka 80;wengine wanasema ni fursa kwa Afrika sasa kupata upapa wanadhani ni uchaguzi wa Marekani,ambako Obama kawa Rais.
Hawajui kuna misimamo ya kanisa na mila na tamaduni anuwai. Na hawajui Papa ni kiongozi wan chi ya Vatican inayozungukwa na Italia.
Ulaya kuna makadinari takriban 50 watakaomchagua Papa,Afrika wapo 12 hivi.Asia wapo takriban 10 na amerika Kusini hususan Brazili wapo makadinari maarufu sana.
Kadinari wa Nigeria,Francio Arinze ndiye anayepigiwa debe kuwa Papa. Papa Gregory(1406-15) ndiye aliyejiuzulu kwa mashinikizo na wala siyo afya mbaya kama anavyosemwa Papa huyu wa siku hizi,Ratzinger.
Kuna ‘Presha’ hadi Vatican,kuna fujo na hata ufisadi na njama za mapinduzi na mauaji ya kinyama.

Rome, ni mahali Kanisa la Mt.Petro lilipojengwa juu ya Kanisa la Petro; linaitwa, St.Peter’s Basilica
 Limejengwa KATIKA ENEO LA EKARI SITA.
Hili kanisa, St. Peter’s Basilica, lina urefu wa futi 700 na upana ni futi 450 na linaweza kuchukua watu 80,000 kwa wakati mmoja.
Rome ni jiji lililopo nyuzi sawa na New York kwa nyuzi za Latitude; ni jiji lenye Coliseum, ambamo yalifugwa masimba yaliyorarua Wakristo maelfu.
Rome,uko futi 40 hadi 270 juu ya usawa wa Bahari
Jiji lenye kelele nyingi kuliko mji wowote duniani,lipo kando ya Bahari ya Mediterranean.
 Zama za Papa Pius XII alibebwa kwenye kiti cha enzi kiitwacho, Sedia Gastatoria ambacho ni kiti cha enzi cha dhahabu chenye rangi nyekundu.Papa huketi hapa mara anapochaguliwa na Moshi  Mweupe, hutoa BARAKA Duniani- Urbi et Orbi.
Rome umejengwa juu ya milima saba: CAPITALINE, PALATINE, AVENTINE, QUIRINAL, VIMINAL, ESQUILINE, na CAELIAN.
Vatican City(The Holy See) mwaka 2004 ulikuwa na watu 870;wengi Waitaliano na wapo Waswisi.
Wanaongea Kiitaliano, Kilatini, na wote ni Wakatoliki-Vatican ni nchi ya dini moja. Fedha wanayotumia ni Lira ya Vatican na ile ya Italia ambazo thamani yake ni sawa.
Lira tatu hivi thamani yake ni sawa na dola moja ya Marekani. Vatican inazungukwa na Italy-eneo lake ni ekari 108.7 na mtawala wake ni Papa.(Papal State).
Katika kitabu kiichwacho THE WORLD ALMANAC toleo la 2002,ukurasa wa 863 kuna maelezo kuhusu Vatican.
Kwamba,Feburuari 11 mwaka 1929 ulitiwa saini mkataba kati ya Kadinari Gasparri na Waziri Mkuu,Benito Mussolini; mkataba wa uhuru wa Vatican na ukatoliki kupewa “Special Status” ndani ya Italia.
Mkataba huu unaitwa, Lateran Agreement (Article 7). Feburuari 10 mwaka 1798 Papa alitiwa mbaroni na akafungwa jela.
Nataka kusema kwamba, ‘donda la mauti’ la Ufunuo 13 lilipona baada ya miaka 131 kamili.
Marekani, hawakuwahi kuitambua mamlaka haya ya VATICAN,SABABU zinafahamika, wakati wa vita kati ya Wakatoliki na wanamatengenezo(Christian Reformation) wa Ulaya walitimkia Marekani ili kukwepa vita vya miaka 1260 yaani kutoka 538 hadi 1798 AD.
Mtu anaweza kusoma vitabu vingi akajua haya, hasa kile kiitwacho, Africa Learns about Europe, The Great Controversy n.k
Marekani ilikuja kutambua mamlaka ya Vatican mwaka 1984,ilikuwa baada ya kuondoa uhusiano wa Kidiplomasia katika mwaka 1867.
Marekani walipata uhuru Julai mwaka 1776,kwa muda wote hawakuitambua Vatican hadi mwaka huo wa 1984.
 Vatican na Israeli walitiliana saini makubaliano ya uhusiano wa kibalozi Desemba 30 mwaka 1993. Msomaji mmoja aliniuliza uhusiano wa Israeli na Vatican, na anapaswa kujua kwamba Israeli maana yake ni dini ya Kiyahudi, ‘Judaism’ na Ukatoliki wa Vatican kuanza kuhusiana, maana yake ni kuondoa kizingiti kati ya Uzayoni na Ukatoliki.Sasa bado Waislam?


.

 Papa ni miongoni mwa viongozi wanaolindwa sana hapa duniani.
Analindwa na askari wa Kiswisi.-SWISS GUARD.
 Baba Mtakatifu ana maadui pia,lazima alindwe. Papa Pius VI alitiwa mbaroni na Jenerali Berthier wa Ufaransa,Feburuari 11 mwaka 1798.
 Papa John Paul II alipigwa risasi. Novemba 27 mwaka 1970 Papa Paulo VI alishambuliwa kwa kisu(hakuumia) katika Uwanja wa Ndege wa Manila, Ufilipino.
 Mwaka 1981 Papa Paulo II na watu wengine wawili waliokuwa jirani naye walipigwa risasi. Ilikuwa Mei 23, mwaka huo wa 1981 Mahmet Ali Agca, akafumua risasi akamjeruhi Papa. Huyu jamaa Mahmet Ali Agca, ni  Mturuki, ambaye alitekeleza tendo hilo la kigaidi wakati Papa akihutubia St. Peter’s Square ,Rome.
Huyu Papa alikufa mwaka 2005 kwa ugonjwa wa kutetemeka.
Mei 12 mwaka 1982  Papa John PauloII ALINYATIWA na muuaji mwenye kisu,walinzi wake wakamnyang’anya kisu huyo jamaa huko Fatima,Ureno.
Papa ni Askofu wa Rome; ni Mwakilishi wa Yesu-THE VICAR OF JESUS CHRIST-NI Mrithi wa Mtume Petro, ni Mkuu wa Mitume wote,ni Mkuu wa Kanisa lote la Kikristo Duniani. Papa ni Mamlaka.
Bila shaka, Profes Ratzinger, amesigana msimamo na maslahi ya Vatican na kuamua kubwaga manyanga,na wala siyo suala la afya mbaya.
Ni kama ‘ametemwa’ na system huko Vatican, Papa siyo kama Lowassa ama Rais Mstaafu Mwinyi waliojiuzulu.
Upapa (Papacy) bi taasisi kubwa hapa duniani,na papa anawasaidizi wajuzi na wengi kiasi kwamba kazi za upapa haziwezi kulala kama wengi wanavyodhani.
Upapa ni taasisi ya mambo mengi ambayo watu wengi hawajui,na papa hawezi kujiuzulu hivi tu.Papa Benedict,katemwa na system ya Vatican,amini usiamini.
www.congesmrambatoday,blogspot.com 














1 comment:

  1. wakristo na wasio wakristo ili tuweze kufanya maamuzi ya kumjua MUNGU wa mbinguni ni lazima tukubali kujifunza na kusoma vitabu vinavyomhusu MUNGU bila kujari Itikadi ya dini fulani .
    lakini vilevile sio tu wazazi ni wakristo au waislamu na wewe mtoto uwe katika itikadi hiyo ya wazazi kumbukuka hata wazazi ni binadamu kama wewe wanaweza kukosea hivyo kubali kuwa rafiki wa kujifunza neno la mungu bila kujali ITIKADI YA DINI YAKO AU YA WAZAZI WAKO.

    ReplyDelete